Ligi Kuu NBC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 05 Jan 2026 18:03:07 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Ligi Kuu NBC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Usajili ligi kuu mwisho Januari 30 https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/usajili-ligi-kuu-mwisho-januari-30/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/usajili-ligi-kuu-mwisho-januari-30/#respond Sun, 04 Jan 2026 06:13:00 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14242 Na mwandishi wetuShirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangza kufunguliwa kwa pazia la usajili wa wachezaji kuanzia Januari Mosi 2026, zoezi ambalo litafungwa rasmi Januari 30, 2026.Taarifa ya TFF iliyopatikana Alhamisi, Januari Mosi, 2026 ilieleza kuwa usajili huo wa wachezaji utazihusu timu za Ligi Kuu NBC, NBC Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake kwa […]

The post Usajili ligi kuu mwisho Januari 30 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangza kufunguliwa kwa pazia la usajili wa wachezaji kuanzia Januari Mosi 2026, zoezi ambalo litafungwa rasmi Januari 30, 2026.
Taarifa ya TFF iliyopatikana Alhamisi, Januari Mosi, 2026 ilieleza kuwa usajili huo wa wachezaji utazihusu timu za Ligi Kuu NBC, NBC Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake kwa msimu wa 2025-26.
Katika taarifa hiyo iliyosainiwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Ndimbo, Klabu husika zimekumbushwa kufanya usajili kupitia mfumo wa usajili wa Fifa Connect.
TFF imezikumbusha klabu katika taarifa hiyo kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe husika na hivyo ni muhimu kuzingatia muda.
Wakati TFF ikitangaza taarifa hiyo tayari baadhi ya klabu hasa za Ligi Kuu NBC zimeanza kuhusishwa na wachezaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.
Mmoja wa wachezaji ambaye jina lake limeibuka katika siku za karibuni akihusishwa na timu ya Yanga ni Allan Okelo, nyota wa Uganda Cranes aliyekosa penalti katika mechi ya Afcon dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.

The post Usajili ligi kuu mwisho Januari 30 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/usajili-ligi-kuu-mwisho-januari-30/feed/ 0
Yanga yaendeleza dozi za 5-0 https://www.greensports.co.tz/2025/06/22/yanga-yaendeleza-dozi-za-5-0/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/22/yanga-yaendeleza-dozi-za-5-0/#respond Sun, 22 Jun 2025 20:10:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13646 Na mwandishi wetuVinara wa Ligi Kuu NBC, Yanga wameendelea kutoa dozi ya mabao matano baada ya leo Jumapili Juni 22, 2025 kutoka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Dodoma Jiji.Hii inakuwa mara ya pili mfululizo kwa Yanga kupata ushindi kama huo katika mechi ya ligi hiyo baada ya Jumatano iliyopita kuilaza Prisons mabao kama […]

The post Yanga yaendeleza dozi za 5-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Vinara wa Ligi Kuu NBC, Yanga wameendelea kutoa dozi ya mabao matano baada ya leo Jumapili Juni 22, 2025 kutoka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Dodoma Jiji.
Hii inakuwa mara ya pili mfululizo kwa Yanga kupata ushindi kama huo katika mechi ya ligi hiyo baada ya Jumatano iliyopita kuilaza Prisons mabao kama hayo.
Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi 79 na imebakiwa na mchezo mmoja ambao utapigwa Jumatano ijayo dhidi ya mahasimu wao Simba na wakishinda au kutoka sare watatawazwa mabingwa wa ligi hiyo msimu huu wa 2024-25.
Yanga ilianza kuandika bao la kwanza kupitia kwa Clatous Chama kwa pasi ya Clement Mzize, bao ambao lilidumu kwa dakika 45 za mwanzo na hivyo kutoonesha dalili zozote za timu hiyo kupata ushindi mkubwa.
Mambo yalianza kuwaendea kombo Dom Jiji kipindi cha pili baada ya Yanga kuandika bao la pili lililofungwa na Duke Abuya kwa pasi ya Chama, bao lililofungwa dakika tano baada ya mapumziko.
Kasi ya Yanga iliendelea na kufanikiwa kupata bao la tatu lililofungwa na Ibrahim Bacca akiutumia vizuri mpira uliopigwa na Maxi Nzengeli.
Dom Jiji walijikuta wakifungwa mabao mawili katika dakika za lala salama, moja beki wao Joash Onyango alijifunga wakati akiokoa mpira uliopigwa na Farid Musa wakati bao la tano lilifungwa na Nzengeli akimalizia pasi ya Jonathan Ikangalombo.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo, Simba nayo ilitoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar huku bao hilo pekee likifungwa na Steven Mukwala.
Kwa ushindi huo Simba wamefikisha pointi 78 wakiwa wamebakiwa na mchezo mmoja wao dhidi ya Yanga ambao umebeba hatma ya nani atakuwa kinara wa ligi hiyo msimu huu.
Matokeo ya mechi nyingine za ligi hiyo zilizochezwa leo ni kama ifuatavyo…
Namungo 5-0 Ken Gold
Coastal Union 1-1 Tabora United
Fountain Gate 2-3 Azam FC
Pamba FC 1-1 KMC
Singida BS 3-3 Prisons
Mashujaa 0-0 JKT Tanzania

The post Yanga yaendeleza dozi za 5-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/22/yanga-yaendeleza-dozi-za-5-0/feed/ 0
Yanga, Simba zagawa dozi ya 5-0 https://www.greensports.co.tz/2025/06/18/yanga-simba-zagawa-dozi-ya-5-0/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/18/yanga-simba-zagawa-dozi-ya-5-0/#respond Wed, 18 Jun 2025 19:45:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13629 Na waandishi wetuTimu za Yanga na Simba zimeendeleza moto kwenye Ligi Kuu NBC kwa kupata ushindi wa mabao 5-0 kila moja, Yanga ikiichapa Prisons na Simba ikitoa kipigo kama hicho kwa Ken Gold.Ushindi wa timu hizo umepatikana leo Jumatano Juni 18, 2025 zikiwa zimebaki siku takriban sita kabla ya timu hizo mahasimu wa soka Tanzania […]

The post Yanga, Simba zagawa dozi ya 5-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na waandishi wetu
Timu za Yanga na Simba zimeendeleza moto kwenye Ligi Kuu NBC kwa kupata ushindi wa mabao 5-0 kila moja, Yanga ikiichapa Prisons na Simba ikitoa kipigo kama hicho kwa Ken Gold.
Ushindi wa timu hizo umepatikana leo Jumatano Juni 18, 2025 zikiwa zimebaki siku takriban sita kabla ya timu hizo mahasimu wa soka Tanzania kukutana kwenye mechi nyingine ya ligi hiyo.
Matokeo ya mechi za leo yanazidi kuongeza ushindani katika kuwania taji la ligi hiyo msimu huu wa 2024-25 ambao unaelekea ukingoni huku Yanga ikishika usukani na pointi 76 katika mechi 28 na Simba ikiwa nafasi ya pili na pointi 75 katika mechi 28.
Simba ikiwa kwenye dimba la Ali Hassan mwinyi mjini Tabora ilianza kuziona nyavu za wapinzani wao dakika ya 20 kwa bao la Kibu Denis kabla ya Elly Mpanzu kuongeza la pili dakika mbili baadaye.
Nyota ya Kibu ambaye alikuwa mchezaji bora wa mechi hiyo, iliendelea kung’ara dakika ya 25 alipopachika bao la tatu na Jean Ahoua kufunga la nne na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko Simba ikiwa mbele kwa mabao 4-0.
Bao la tano na la mwisho kwa Simba lilipatikana dakika ya 76 mfungaji akiwa Jean Ahoua, bao ambalo linamfanya kiungo huyo kuzidi kung’ara katika orodha ya wafungaji wenye mabao mengi ya ligi akiwa amefikisha 16.
Kwa upande wa Yanga wakiwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya waliandika bao lao la kwanza kupitia kwa Mudathir Yahya kabla ya Clatous CHama kuandika la pili wakati mabao mengine matatu yalifungwa na Israel Mwenda na Pacome Zouzoua aliyefunga mawili.

Katika mechi nyingine za ligi hiyo zilizochezwa leo, matokeo ni kama ifuatavyo…
Azam FC 5-0 Tabora United
Coastal Union 1-0 Fountain Gate
Singida BS 2-1 Dodoma Jiji
Pamba 1-0 JKT Tanzania
Mashujaa 1-1 KMC
Namungo 0-0 Kagera Sugar

The post Yanga, Simba zagawa dozi ya 5-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/18/yanga-simba-zagawa-dozi-ya-5-0/feed/ 0
Miezi miwili bila Ligi Kuu NBC https://www.greensports.co.tz/2025/01/01/miezi-miwili-bila-ligi-kuu-nbc/ https://www.greensports.co.tz/2025/01/01/miezi-miwili-bila-ligi-kuu-nbc/#respond Wed, 01 Jan 2025 17:58:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12551 Na mwandishi wetuBurudani ya soka ya Ligi Kuu NBC itasimama kwa kipindi cha miezi miwili kuanzia Desemba 29 mwaka jana na kurejea Machi Mosi, 2025 kutokana na matukio kadhaa ya kimichezo.Taarifa ya idara ya mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) iliyopatikana Desemba 31 iliyataja matukio mawili yanayosababisha kusimamishwa kwa ligi hiyo.Matukio hayo ni […]

The post Miezi miwili bila Ligi Kuu NBC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Burudani ya soka ya Ligi Kuu NBC itasimama kwa kipindi cha miezi miwili kuanzia Desemba 29 mwaka jana na kurejea Machi Mosi, 2025 kutokana na matukio kadhaa ya kimichezo.
Taarifa ya idara ya mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) iliyopatikana Desemba 31 iliyataja matukio mawili yanayosababisha kusimamishwa kwa ligi hiyo.
Matukio hayo ni michuano ya Kombe la Mapinduzi itakayofanyika kisiwani Pemba pamoja na fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) ambazo Tanzania ni mmoja wa wenyeji.
TPLB ilifafanua kuwa licha ya changamoto hiyo lakini wamejipanga kuhakikisha msimu wa ligi hiyo wa 2024-25 unafikia tamati kwa mujibu wa kanuni za ligi na kutoathiri kipindi cha mapumziko na maandalizi ya msimu ujao wa 2025-26.
Bodi pia inaamini klabu zitakitumia vyema kipindi hiki cha mapumziko kwa kufanya maboresho na marekebisho katika vikosi vyao ili kuendana na ushindani mkubwa uliopo kwenye ligi hiyo.
Taarifa ya bodi ilimalizia kwa kuitakia kila la kheri timu ya taifa ya Tanzania katika maandalizi ya Chan pamoja na kuwatakia heri ya mwaka mpya wa 2025 wadau wote wa mpira wa miguu nchini.

The post Miezi miwili bila Ligi Kuu NBC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/01/01/miezi-miwili-bila-ligi-kuu-nbc/feed/ 0
Mechi ya Simba, Mtibwa yaahirishwa https://www.greensports.co.tz/2024/02/16/mechi-ya-simba-mtibwa-yaahirishwa/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/16/mechi-ya-simba-mtibwa-yaahirishwa/#respond Fri, 16 Feb 2024 19:11:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9763 Na mwandishi wetuBodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), imeuahirisha mchezo wa Ligi Kuu NBCkati ya Simba SC na Mtibwa Sugar uliopangwa kuchezwa Februari 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.Sababu iliyotajwa ya kuahirisha mchezo huo katika taarifa ya bodi iliyotolewa leo Ijumaa ni kutoa mafasi zaidi ya maandalizi na taratibu za safari kwa […]

The post Mechi ya Simba, Mtibwa yaahirishwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), imeuahirisha mchezo wa Ligi Kuu NBCkati ya Simba SC na Mtibwa Sugar uliopangwa kuchezwa Februari 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Sababu iliyotajwa ya kuahirisha mchezo huo katika taarifa ya bodi iliyotolewa leo Ijumaa ni kutoa mafasi zaidi ya maandalizi na taratibu za safari kwa Simba kuelekea mchezo wake wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika mechi ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika Simba inajiandaa kuumana na Asec Mimosas ya Ivory Coast, mchezo unaotarajiwa kupigwa Februari, 23 mwaka huu.
Mchezo huo ni muhimu kwa Simba ambayo inashika nafasi ya pili kwenye Kundi B ikiwa na pointi tano nyuma ya Asec Mimosas wanaoongoza wakiwa na pointi 10.
Timu ya Jwaneng Galaxy iko nafasi ya tatu kwa pointi nne na Wydad AC inaburuza mkia kwa pointi tatu baada ya kila timu kucheza mechi nne.
Simba watakuwa wageni wa mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Le Felicia mjini, Abidjan kuanzia saa 4.00 usiku huku kukiwa na kumbukumbu ya sare ya bao 1-1, timu hizo zilipokutana kwenye mchezo wa awali Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

The post Mechi ya Simba, Mtibwa yaahirishwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/16/mechi-ya-simba-mtibwa-yaahirishwa/feed/ 0
Pazia Ligi Kuu NBC kufunguliwa https://www.greensports.co.tz/2024/01/26/pazia-ligi-kuu-nbc-kufunguliwa/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/26/pazia-ligi-kuu-nbc-kufunguliwa/#respond Fri, 26 Jan 2024 20:34:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9463 Na mwandishi wetuImeelezwa kuwa Ligi Kuu NBC inatarajia kuendelea wakati wowote kuanzia sasa baada ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kutolewa kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon).Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Almasi Kasongo (pichani) akieleza kwamba hiyo inatokana na kanuni kuruhusu ligi kuendelea.“Kanuni inasema […]

The post Pazia Ligi Kuu NBC kufunguliwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Imeelezwa kuwa Ligi Kuu NBC inatarajia kuendelea wakati wowote kuanzia sasa baada ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kutolewa kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon).
Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Almasi Kasongo (pichani) akieleza kwamba hiyo inatokana na kanuni kuruhusu ligi kuendelea.
“Kanuni inasema klabu yenye wachezaji wasiopungua watatu kwenye timu ya taifa basi michezo ya klabu hiyo itasimama, kwa sasa timu imetolewa kwenye mashindano ya Afcon, ni wazi kila klabu iliyokuwa na mchezaji wake kwenye timu ya taifa atakuwa amerudi kwa ajili ya mwendelezo wa ligi,” alisema Kasongo.
Kasongo alisema kabla ya fainali za Afcon kuanza, alieleza kuhusu kusimama kwa ligi na itarejea pale ambapo timu itakaporejea rasmi kutoka kwenye michuano hiyo inayoendelea nchini Ivory Coast.
Kasongo alisema baada ya hilo kueleweka Bodi inatarajia kukaa kufanya majumuisho na baadaye watatangaza rasmi tarehe ya kurudi kwa ligi hiyo inayoshirikisha timu 16.
Hadi ligi inasimama baadhi ya timu zilibakiza mechi moja kumaliza mzunguko wa kwanza huku nyingine zikiwemo klabu za Simba na Yanga zikibakiwa na michezo minne mpaka mitano huku Azam FC ikiwa kileleni mwa msimamo ikikusanya pointi 31.

The post Pazia Ligi Kuu NBC kufunguliwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/26/pazia-ligi-kuu-nbc-kufunguliwa/feed/ 0
TFF, NBC wasaini mkataba wa bilioni 32 https://www.greensports.co.tz/2023/08/11/tff-nbc-wasaini-mkataba-wa-bilioni-32/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/11/tff-nbc-wasaini-mkataba-wa-bilioni-32/#respond Fri, 11 Aug 2023 18:47:49 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7343 Na mwandishi wetu, TangaBenki ya NBC imetangaza kuongeza mkataba wa udhamini kwenye Ligi Kuu NBC kwa muda wa miaka mitano kuanzia msimu huu wa 2023-24 wenye thamani ya jumla ya Shilingi bilioni 32.56.Mkataba huo ambao sasa utakuwa ukidhamini ligi tatu yaani Ligi Kuu NBC, Ligi ya Championship na Ligi ya Vijana chini ya miaka 20 […]

The post TFF, NBC wasaini mkataba wa bilioni 32 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu, Tanga
Benki ya NBC imetangaza kuongeza mkataba wa udhamini kwenye Ligi Kuu NBC kwa muda wa miaka mitano kuanzia msimu huu wa 2023-24 wenye thamani ya jumla ya Shilingi bilioni 32.56.
Mkataba huo ambao sasa utakuwa ukidhamini ligi tatu yaani Ligi Kuu NBC, Ligi ya Championship na Ligi ya Vijana chini ya miaka 20 baada ya ule wa awali wa miaka mitatu uliokuwa na thamani ya Sh bilioni 2.5.
Mkataba huo umesainiwa leo Ijumaa kati ya NBC na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jijini Tanga ambako michuano mipya ya Ngao ya Jamii inaendelea.
Baada ya makubaliano yaliyosainiwa na Rais wa TFF, Wallace Karia na Mkurugenzi wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, imetambulishwa rasmi kuwa Ligi ya Championship sasa itafahamika kwa jina la NBC Championship na Ligi ya Vijana U20 itaitwa NBC Youth League.
Sabi alisema kuwa wameendelea na udhamini huo kutokana na kupata baadhi ya faida ikiwemo uwezeshwaji wa ajira za moja kwa moja 7,000, ukuaji wa chapa ya benki ya NBC, ujumuishaji na uwezeshaji wa kifedha pamoja na kuchangia pato la taifa na kuchagiza shughuli za utalii.

The post TFF, NBC wasaini mkataba wa bilioni 32 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/11/tff-nbc-wasaini-mkataba-wa-bilioni-32/feed/ 0
Ligi Kuu NBC Agosti 16 https://www.greensports.co.tz/2023/08/08/ligi-kuu-nbc-agosti-16/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/08/ligi-kuu-nbc-agosti-16/#respond Tue, 08 Aug 2023 07:20:26 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7274 Na mwandishi wetuPazia la Ligi Kuu NBC msimu wa 2023-24 litafungiliwa Agosti 16 kwa mabingwa watetezi Yanga kurusha karata ya kwanza Agosti 23 dhidi ya KMC wakati Simba wataianza ligi Agosti 17 dhidi ya Mtibwa Sugar.Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Stephen Mguto, Agosti 16 ambayo ndiyo siku ya ufunguzi wa ligi hiyo […]

The post Ligi Kuu NBC Agosti 16 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Pazia la Ligi Kuu NBC msimu wa 2023-24 litafungiliwa Agosti 16 kwa mabingwa watetezi Yanga kurusha karata ya kwanza Agosti 23 dhidi ya KMC wakati Simba wataianza ligi Agosti 17 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Stephen Mguto, Agosti 16 ambayo ndiyo siku ya ufunguzi wa ligi hiyo zitapigwa mechi tatu; Ihefu itaumana na Geita Gold, Namungo dhidi ya JKT Tanzania na Dodoma Jiji dhidi ya Coastal Union.
Ukiacha mechi ya Simba na Mtibwa ya Agosti 17, siku hiyo pia kutakuwa na mechi kati ya Singida Fountain Gate itakayotoana jasho na Tanzania Prisons wakati Simba watarudi uwanjani kwa mara ya pili Agosti 20 kuoneshana kazi na Dodoma Jiji.
Siku tisa baada ya Simba kucheza mchezo wa pili yaani Agosti 29, mahasimu wao Yanga wataingia dimbani dhidi ya JKT Tanzania wakati siku moja kabla yaani Agosti 28, Azam watakuwa dimbani dhidi ya Tanzania Prisons.
Kati ya Oktoba 4 hadi 19, ligi itasimama kupisha michuano ya kimataifa kwa timu za Yanga, Simba, Azam na Singida Fountain Gate zitakazokuwa zikiumana kwenye Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.
Kwa upande wa Simba wanatarajia kukosekana kwa kipindi kirefu cha mwezi Oktoba kwa kuwa mbali na kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, timu hiyo pia itashiriki michuano mipya ya Africa Super Cup.
Baada ya mtihani huo, Simba itakuwa na kazi nyingine mapema Novemba 5 itakapokutana na hasimu wake wa jadi Yanga katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo kwenye Uwanja wa Mkapa Simba ikiwa mwenyeji.
Timu hizo mbili mahasimu, mechi hiyo inaweza kuwa ya pili kwa msimu huu kama ikitokea zikakutana kwenye mechi ya Ngao ya Jamii inayoshirikisha timu za Yanga, Simba, Azam na Singida Fountain Gate.
Kwa mujibu wa Mguto, ligi hiyo imepangwa kufikia tamati Mei 29, 2024 kwa mechi zote kuchezwa siku hiyo.

The post Ligi Kuu NBC Agosti 16 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/08/ligi-kuu-nbc-agosti-16/feed/ 0
Ligi Kuu NBC 2022-23 ilijaa rekodi mpya https://www.greensports.co.tz/2023/06/16/ligi-kuu-nbc-2022-23-ilijaa-rekodi-mpya/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/16/ligi-kuu-nbc-2022-23-ilijaa-rekodi-mpya/#respond Fri, 16 Jun 2023 07:11:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6618 Na Hassan KinguMsimu wa soka 2022-23 umemalizika rasmi Jumatatu iliyopita, ukihitimishwa kwa mechi ya fainali ya Kombe la FA (ASFC) kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC.Huo ni ubingwa wa tatu kwa Yanga msimu huu baada ya awali kutwaa ndoo ya Ligi Kuu NBC zikiwa zimesalia mechi mbili kumalizika ligi […]

The post Ligi Kuu NBC 2022-23 ilijaa rekodi mpya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Hassan Kingu
Msimu wa soka 2022-23 umemalizika rasmi Jumatatu iliyopita, ukihitimishwa kwa mechi ya fainali ya Kombe la FA (ASFC) kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC.
Huo ni ubingwa wa tatu kwa Yanga msimu huu baada ya awali kutwaa ndoo ya Ligi Kuu NBC zikiwa zimesalia mechi mbili kumalizika ligi lakini pia ikiwa imeshaweka kibindoni Ngao ya Jamii walioipata kwa kuifumua Simba mabao 2-1 katika mechi ya kuukaribisha msimu huu.
Yanga imekuwa na mafanikio makubwa msimu huu kwa kuweka alama nyingi sehemu mbalimbali walizotia mguu, ikiwemo kuweka rekodi kwa kuingia fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza.
Kwa Tanzania imekuwa mara ya pili baada ya kupita miaka 30 tangu Simba ilipofanya hivyo mwaka 1993 na kupoteza mbele ya Stella Abidjan ya Ivory Coast kwa kufungwa mabao 2-0.
Yanga yenyewe iliupoteza ubingwa huo baada ya kufungwa mabao 2-1 na USM Alger nyumbani kabla ya ushindi wa bao 1-0 ugenini lakini USMA ilitawazwa bingwa wa kombe hilo kwa mara ya kwanza kupitia kanuni ya bao la ugenini.
Mbali na hilo, msimu huu pia Yanga imeionesha Afrika makucha yake kwa kutoa mfungaji bora mwenye mabao mengi katika Kombe la Shirikisho, Fiston Mayele aliyefunga mabao saba, pia kwenye fainali ya michuano hiyo ikatoa kipa bora, Djigui Diarra ambaye alikuwa nyota wa mchezo.

Tanzania ya tano Afrika
Ukiachana na alama za Yanga, ni msimu huu pia ambapo Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Soka Duniani (IFFHS) likaitangaza Ligi Kuu ya Tanzania Bara kushika namba tano kwa ubora Afrika na 39 duniani.
Ligi namba moja ni Misri ikifuatiwa na Algeria, Morocco, Sudan wakati kidunia Brazil imeendelea kuwa ya kwanza na England ya pili. Tanzania imeweka rekodi ikitoka nafasi ya 62 kwa mwaka 2021 hadi nafasi ya 39 wakati IFFHS ikitangaza takwimu hizo mpya Januari, mwaka huu.

Hat-trick nyingi
Msimu huu ni miongoni mwa misimu ambayo imeshuhudiwa rekodi ya ‘hat-trick’ nane zikifungwa na wachezaji tofauti. Wachezaji wa Simba, John Bocco na Saido Ntibazonkiza kila mmoja amefunga ‘hat-trick’ mbili.
Wengine ni Ibrahim Mkoko wa Namungo, Jean Baleke (Simba) na Mayele na Stephane Aziz Ki wa Yanga ambao kila mmoja amefunga hat-trick moja.

Saido achangamsha ligi mwishoni
Kama inavyofahamika baada ya Yanga kutangaza ubingwa mapema, kilichobaki ilikuwa ni kuhitimisha msimu kwa mechi zilizosalia na kusubiri timu zitakazoshuka daraja lakini Saido akaibua upinzani mzito wa kuwania ufungaji bora zikiwa zimesalia mechi mbili kufungwa rasmi pazia la ligi.
Saido akiwa na mabao 10 nyuma ya Mayele aliyekuwa amefunga mara 16, akafunga mabao matano katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Polisi Tanzania na kufikisha mabao 15 na kuibua hisia za ushindani huo mpya kwa wadau na wapenzi wa soka nchini.
Kasi yake hiyo ikawafanya watu waifuatilie tena kwa karibu ligi ikiwa mwishoni ili kubaini nani ataibuka kinara wa mabao hasa ukizingatia uhasimu wa timu za nyota hao.
Hata hivyo, katika mechi za mwisho, Saido alifunga mabao mawili na Mayele akafunga bao moja na wote kulingana kwa mabao 17, hivyo wote wakapewa kiatu cha ufungaji bora kama ilivyokuwa miaka sita iliyopita kwa Simon Msuva (Yanga) na Abdulrahman Mussa (Ruvu) wote kupewa viatu kwa kufunga mabao 14.

Fei Toto aitingisha nchi
Kingine kitakachobaki kwenye kumbukumbu ya wengi ni kuvurugana kwa Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Yanga akidai amevunja mkataba na timu hiyo na yuko huru.
Jambo ambalo halikuwaingia Yanga akilini, wakamburuza mchezaji huyo kwenye kamati za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kuamuliwa mchezaji huyo kurejea Yanga, lakini Fei naye hakukubaliana na hilo na kuendelea kuvutana.
Suala hilo limechukua miezi sita kabla ya wiki mbili zilizopita Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuingilia kati na kuwaomba Yanga kumalizana na kijana huyo na siku tatu baadaye, Azam FC ilitangaza kumsajili Fei kutoka Yanga baada ya pande hizo tatu kumalizana.

Fei Toto

Manzoki kuibukia uchaguzi Simba
Kitendo cha Simba pia kumshusha mshambuliaji hatari wa Dalian Pro ya Ligi Kuu ya China, Cesar Manzoki raia wa DR Congo kwenye uchaguzi wao mkuu uliofanyika Januari mwaka huu kiliibua hisia mbalimbali.
Baadhi ya mashabiki na wanachama wa Simba walilipuka kwa hisia tofauti wakidai wanafanyiwa ‘utoto’ kuletewa mshambuliaji huyo wakati dirisha la usajili limefungwa na kuonekana kama alitumika kwenye kampeni za baadhi ya washiriki wa uchaguzi huo.
Wengine walifurahia ujio wake hasa baada ya nyota huyo kueleza kuwa timu anayoweza kuja kuitumikia ni Simba pekee na si wapinzani wa Wekundu hao, Yanga.
Kwa upande wa pili yaani Yanga, kauli hiyo hawakupendezwa nayo na kumfanya Manzoki kuzizima kwa wiki kadhaa nchini kupitia mijadala mbalimbali.

Sekeseke la SportPesa, Yanga
Mkataba wa Wadhamini Wakuu wa Yanga, SportPesa uliyumba baada ya timu hiyo kutangaza wadhamini wao wapya, Haier kuelekea michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
SportPesa walieleza kulilia haki yao ya kukaa kifuani na kwamba hawakuridhia wadhamini wapya kukaa kwenye nafasi yao hata kama kanuni za Kombe la Shirikisho Afrika ilieleza wazi kutotumika kwa nembo za wadhamini wa Kampuni za Michezo ya Kubashiri kwa timu shiriki.
Baada ya vuta nikuvute ya hapa na pale, mwisho walilimaliza suala hilo na kuendelea na safari yao ya pamoja licha ya kuwa tayari lilishaanza kuibua mihemko baina ya mashabiki wa Yanga na viongozi wa SportPesa.

Singida inabadilika kila wakati
Timu ya Singida Big Stars imekuwa na historia yake msimu huu. Kwanza imepanda daraja ikiwa na nyota wengi wanaohofiwa ligi kuu na kuonesha makali yake wakiwa na kocha mkongwe, Hans van Der Pluijm.
Licha ya ugeni wao, walionesha umwamba wao na kufanikiwa kumaliza ligi nafasi ya nne na kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza msimu ujao. Pia ilitinga nusu fainali ya Kombe la FA kabla ya kufungwa bao 1-0 na Yanga.
Singida pia imeingia kwenye rekodi ya kubadilishwa majina matatu ndani ya msimu mmoja. Wakati inapanda kutoka Championship ilikuwa ikiitwa DTB kabla ya kuitwa Singida BS zilipoanza mechi za ligi kuu.
Na kama ulivyosikia na kuona, tayari Singida imebadilishwa tena siku chache baada ya kukamilika kwa ligi na sasa inaitwa Singida Fountain Gate FC baada ya timu hiyo kuuzwa kwa Taasisi ya Fountain Gate.
Hayo ni machache kati ya mengi yaliyojiri msimu huu ambayo hayatasahaulika ikiwemo rekodi mbovu ya Polisi Tanzania ya kushuka daraja na kufungwa jumla ya mabao 14 katika mechi zao mbili za mwisho. Simba iliifunga mabao 6-1 na Azam ikaibonda mabao 8-0.
Yote kwa yote ulikuwa msimu wenye msisimko mkubwa, rekodi nyingi na mengi ya kujivunia kama nchi na soka lake ingawa yapo yanayobaki kama funzo na mengine ya kuyaendeleza kwa ajili ya kuendelea kuing’arisha Tanzania misimu ijayo.

The post Ligi Kuu NBC 2022-23 ilijaa rekodi mpya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/16/ligi-kuu-nbc-2022-23-ilijaa-rekodi-mpya/feed/ 0
Kikosi Bora Ligi Kuu NBC 2022-23 https://www.greensports.co.tz/2023/05/19/kikosi-bora-ligi-kuu-nbc-2022-23/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/19/kikosi-bora-ligi-kuu-nbc-2022-23/#respond Fri, 19 May 2023 19:03:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6219 Na Hassan KinguMsimu wa Ligi Kuu NBC 2022-23 umefikia ukingoni zikiwa zimesalia mechi mbili kwa kila timu kabla ya kufungwa rasmi pazia la ligi msimu huu.Miongoni mwa timu zilizofanikiwa kutimiza ndoto zake katika ligi hiyo ni Yanga ambao wameutetea ubingwa wao baada ya mechi 28 walipoifunga Dodoma Jiji mabao 4-2 na kufikisha pointi 74 ambazo […]

The post Kikosi Bora Ligi Kuu NBC 2022-23 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Hassan Kingu
Msimu wa Ligi Kuu NBC 2022-23 umefikia ukingoni zikiwa zimesalia mechi mbili kwa kila timu kabla ya kufungwa rasmi pazia la ligi msimu huu.
Miongoni mwa timu zilizofanikiwa kutimiza ndoto zake katika ligi hiyo ni Yanga ambao wameutetea ubingwa wao baada ya mechi 28 walipoifunga Dodoma Jiji mabao 4-2 na kufikisha pointi 74 ambazo hazitafikiwa na timu nyingine.
Singida Big Stars wanachuana na Azam kwenye vita ya kumaliza nafasi ya tatu kama ilivyo vita ya Namungo na Geita Gold ya kuwania kumaliza nafasi ya tano.
Ruvu Shooting tayari imeshuka daraja lakini kuna utata kuanzia nafasi ya nane hadi ya 15, wote wanapambana kutoungana na Ruvu au kutocheza mechi za mtoano kuwania kusalia kwenye ligi hiyo msimu ujao.
Hata hivyo, utamu na ugumu wa ligi hiyo umechangiwa na uzuri, ubora, viwango na ushindani unaooneshwa na wachezaji wa timu hizo 16 zinazoshiriki michuano hiyo maarufu kwa sasa Afrika.
Kama ilivyo ada, mwisho wa msimu hugawiwa tuzo za wachezaji binafsi waliofanya vizuri kwenye nyanja mbalimbali kwa kutambua mchango wao au namba za ubora wao ndani ya msimu mzima.
GreenSports imekuandalia orodha ya baadhi ya wachezaji waliofanya vizuri zaidi na kuunda kikosi bora cha msimu huu kulingana na ubora, ubunifu na uwezo waliounesha katika timu zao na kuzisaidia kufika hapo zilipo:
-1. Djigui Diarra (Yanga)
Ubora aliounesha akiwa na Yanga tangu msimu uliopita na kutunukiwa tuzo ya kipa bora wa msimu ndicho alichoendeleza kukifanya msimu huu pia kwa kuiweka Yanga katika mikono salama ya ulinzi.
Diarra ndiye anaongoza kwa ‘clean sheet’ akiwa nazo 16 mpaka sasa akifuatiwa na Aishi Manula wa Simba aliyefanya hivyo mara 12.
Kuonesha anazidi kuimarika kila msimu, Diarra tayari amevunja rekodi ya clean sheet 15 alizoweka msimu uliopita.
Kipa huyo raia wa Mali pia ni mahiri kwenye kupanga ukuta wake wa ulinzi, ukali wa kuwashtua mabeki wake wawe makini, ujuzi wa kuanzisha mashambulizi ni miongoni mwa silaha zake zinazompa ubora wa hali ya juu.
-2. Shomari Kapombe (Simba)
Kapombe maarufu kwa mashabiki wa Simba kama Baba Esther ameendelea kuimarika kila msimu na kuthibitisha kwa mara nyingine ukongwe alionao katika ligi hiyo kutokana na kazi safi ya beki wa kulia anayoifanya.
Mbali na shughuli za ulinzi anazozifanya kwa bidii kubwa lakini pia anahusika kutengeneza nafasi nyingi za mabao za timu hiyo akiwa na pasi sita za mwisho za mabao mpaka sasa.
-3. Mohamed Hussein (Simba)
Nahodha msaidizi wa Simba, ndiye beki pekee aliyefungana kileleni kwa pasi za mabao na Kapombe. Haishangazi kufanya hivyo kutokana na ubora alionao anapopanda kwenda kushambulia.
Kasi, ujanja, namna ya kuuchezea mpira mguuni ni moja ya silaha zake adimu anapokuwa kwenye majukumu yake ya kulilinda lango la Simba na pia kufanya mashambulizi kwa ufasaha ikiwa ni jukumu lake la pili la beki wa pembeni kulingana na mifumo ya sasa.


-4. Dickson Job (Yanga)
Umbo dogo alinalo beki huyu wa zamani wa Mtibwa Sugar, halimzuii kufanya majukumu ya kikatili kwa washambuliaji wenye uchu wa mabao na wenye miili mikubwa.
Akili kubwa aliyonayo na utulivu kwenye eneo la ulinzi vimemuongezea nafasi kubwa ya kuingia katika kikosi hiki huku akiwa na uwezo wa kuanzisha mashambulizi. Job ni kati ya silaha zilizofanya Yanga ifungwe mabao machache mpaka sasa, 15.

-5. Henock Inonga (Simba)
Utulivu wa hali ya juu, umakini anapokaba washambuliaji, ubora wa kucheza mipira ya vichwa, burudani ya chenga pamoja na pasi za uhakika, ndivyo vinavyompa ubora na kuimbwa na mashabiki wa Simba kila kukicha.
Hana umbo la upambanaji lakini ‘jihad’ na akili za mpira alizonazo dhidi ya wapinzani zimekuwa nguzo kubwa kwa Simba msimu huu na kufanya Wekundu hao kuungana na Yanga kuwa timu mbili pekee zilizofungwa mabao machache mpaka sasa.
-6. Khalid Aucho (Yanga)
Kiungo wa kati mwenye uwezo wa kukaba na kuchezesha timu kutoka Uganda ni chachu nyingine ya mafanikio ya Yanga msimu huu kwenye eneo hilo muhimu la kuunganisha mawasiliano ya timu.
Aucho au ‘The Tank’ amekuwa akilitumia vyema umbo lake kubwa alilonalo kuonesha ubabe kwa wapinzani, kupokonya mipira lakini pia silaha yake ya kutokaa na mpira muda mrefu, akipiga pasi za haraka vimekuwa vikimlinda mno na kumuweka kwenye ubora kila wakati.
-7. Saido Ntibazonkiza (Simba)
Kiungo mshambuliaji huyu aliyeanza kuonesha makali yake msimu huu akiwa na Geita Gold ameendelea kuonesha kazi yake hata baada ya kuhamia Simba kwenye dirisha dogo msimu huu.
Licha ya kasi na mashuti ya uhakika aliyonayo lakini Ntibazonkiza ndiye mchezaji pekee aliyechangia mabao mengi. Amefunga mabao 10 na ametoa pasi za mwisho 12 na kumfanya kuhusika kwenye jumla ya mabao 22.
-8. Mzamiru Yassin (Simba)
Unaweza kumwita ‘kiungo punda’ kwa shughuli nzito ya kukimbizana na mipira, kuipokonya, kuitawanya na wakati mwingine kupiga pasi za mwisho kwa washambuliaji.
Sio mzuri sana wa maamuzi ya pasi za mbali lakini ni mzuri mno wa kupiga pasi fupi na kusumbua maadui eneo la tatu ya mwisho ya lango la wapinzani.
Mzamiru pia anatajwa kama miongoni mwa viungo wenye kufanya kazi kwa hesabu kubwa kulingana na maelekezo ya kocha anayoyataka akitumika kama kiunganishi cha timu inapohitaji mkakati maalum kwa wapinzani.


-9. Fiston Mayele (Yanga)
Kinara wa mabao 16 katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu mpaka sasa. Anafunga kila aina ya mabao, anaimbwa kila kona kwa jihad ya kutaka kuzifumania nyavu katika kila mechi.
Ana kasi, mjanja wa kuhadaa mabeki, anapiga mashuti bila ya kusahau sifa yake ya ‘uchoyo’ ambayo imekuwa ni sababu nyuma ya mafanikio yake ya kufunga mabao mengi na kuwa tishio kwa msimu wa pili mfululizo kwenye ligi.
Mayele ni mchezaji wa pili kuhusika katika mabao mengi msimu huu baada ya Ntibazonkiza. Amehusika kwenye upatikanaji wa mabao 19.

-10. Bruno Gomez (Singida BS)
Kiungo Mbrazil mwenye ubunifu, ujanja, chenga na uwezo wa kufunga mabao ya mbali. Amethibitisha ubora wake akiwa na msimu wa kwanza Singida na kuwa moja ya chachu ya timu hiyo kufanya vizuri.
Mabao tisa aliyofunga na uwezo mkubwa anauonesha umemfanya atamkwe kwenye ofisi nyingi za viongozi wa timu kubwa za soka nchini, wengi wakivutiwa na huduma yake adhimu aliyoionesha mpaka sasa akiwa na uwezo wa kucheza nafasi zote za katikati ya uwanja.
-11. Clatous Chama (Simba)
Mbabe wa pasi za mwisho, akiwa anaongoza orodha hiyo kwa pasi 14 mpaka sasa. Ubora wake wa kuuchezea mpira, kuituliza timu vinamuweka kwenye viwango vya juu mno msimu huu.
Usisahau pia uwezo wake mkubwa wa kufunga mabao ya utulivu na ya kushangaza, faulo na kadhalika vimemfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wa juu. Kwa kifupi Chama ni miongoni mwa viungo washambuliaji wachache wa ligi hii wanaoonesha utofauti mkubwa na wengine.

Benchi la Ufundi
Nasreddine Nabi, Cedric Kaze na Juma Mgunda
Wachezaji wa akiba
Aishi Manula (Simba), Nicholaus Gyan (Singida BS), Joyce Lomalisa, Bakari Mwamnyeto, Stephane Aziz Ki (Yanga), Yusuf Kagoma (Singida BS), James Akaminko, Ayoub Lyanga (Azam), Jean Baleke (Simba) na Eric Kaijage (Kagera Sugar).

The post Kikosi Bora Ligi Kuu NBC 2022-23 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/19/kikosi-bora-ligi-kuu-nbc-2022-23/feed/ 0