PSG - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 03 Jun 2026 18:04:50 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg PSG - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 PSG yabeba tena taji Ulaya https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/psg-yabeba-tena-taji-ulaya/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/psg-yabeba-tena-taji-ulaya/#respond Sun, 31 May 2026 12:20:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14670 Budapest, HungaryParis St-Germain au PSG ya Ufaransa kwa mara ya pili mfululizo imedhihirisha ubora wake barani Ulaya kwa kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufuta matumaini ya Arsenal kubeba taji hilo.PSG wamebeba taji hilo kwa ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Arsenal baada ya sare ya bao 1-1 katika mechi iliyochezwa Jumamosi, Mei […]

The post PSG yabeba tena taji Ulaya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Budapest, Hungary
Paris St-Germain au PSG ya Ufaransa kwa mara ya pili mfululizo imedhihirisha ubora wake barani Ulaya kwa kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufuta matumaini ya Arsenal kubeba taji hilo.
PSG wamebeba taji hilo kwa ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Arsenal baada ya sare ya bao 1-1 katika mechi iliyochezwa Jumamosi, Mei 30, 2026 mjini Budapest, Hungary.
Miezi 12 iliyopita, ni PSG hao hao waliolibeba taji hilo kwa kuichapa Inter Milan mabao 5-0 katika mechi ya fainali iliyopigwa mjini Munich, Ujerumani.
Arsenal waliouanza vyema mchezo wakiwa na matumaini makubwa yaliyozaa bao la mapema dakika ya sita mfungaji akiwa ni Havertz kwa pasi ya Trossard, bao lililodumu kwa dakika 45 za awali.
PSG walipambana na kupata bao la kusawazisha lililofungwa na Dembele katika dakika ya 65 kwa mkwaju wa penalti na hatimaye timu kumaliza dakika 90 kwa sare pamoja na 30 za nyongeza kabla ya kuingia kwenye penalti na PSG kuibuka mashujaa.
Furaha isiyo kifani ilidhihirika kwa kocha wa PSG, Luis Enrique anayeingia katika rekodi ya watu watano waliobeba taji hilo mara tatu na ambaye alinukuliwa baada ya mechi akisema kwamba amechanganywa kwa furaha.
“Nina furaha, uchovu wa akili na kila kitu lakini hili ni tukio muhimu la msimu, sisi bado ni mabingwa, mara mbili mfululizo, ni jambo la kipekee,” alisema Enrique.
Mtu mwingine aliyedhihirisha furaha ya ushindi huo ni rais wa klabu ya PSG, Nasser Al-Khelaifi ambaye baada ya Enrique kuvalishwa medali yake, wawili hao walionekana wakicheza mbele ya mashabiki kufurahia taji hilo.
PSG chini ya Enrique ambaye pia alilibeba taji hilo mwaka 2015 akiwa mchezaji wa Barcelona, tangu akabidhiwe jukumu la kuinoa timu hiyo Julai 2023 amefanikiwa kuigeuza kuwa timu bora.
Baada ya kuachana na baadhi ya wachezaji mastaa kina Lionel Messi, Kylian Mbappe, Neymar Jr na wengineo, Enrique ni kama alianza kufanya kazi ya kuisuka upya PSG na akafanikiwa kuifanya iwe katika ubora.
Ubora wa timu hiyo ukiendelea hakuna atakayeshangaa iwapo wataisogelea rekodi ya Real Madrid ya kutwaa mataji matano ya Ulaya kwa miaka mitano mfululizo waliyoiweka kati ya mwaka 1956 hadi 1960.

The post PSG yabeba tena taji Ulaya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/psg-yabeba-tena-taji-ulaya/feed/ 0
Ni Arsenal, PSG fainali ligi ya mabingwa https://www.greensports.co.tz/2026/05/08/ni-arsenal-psg-fainali-ligi-ya-mabingwa/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/08/ni-arsenal-psg-fainali-ligi-ya-mabingwa/#respond Fri, 08 May 2026 19:15:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14617 Munich, UjerumaniMabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, PSG wamefuzu kwa mara ya pili mfululizo hatua ya fainali ya ligi hiyo baada ya kuibwaga Bayern Munich na sasa wanasubiri kuumana na Arsenal.PSG wakiwa ugenini Allianz Arena katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa Jumatano Mei, 6, 2026 walilazimisha sare ya bao 1-1 kwa wenyeji Bayern.Kwa matokeo […]

The post Ni Arsenal, PSG fainali ligi ya mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, PSG wamefuzu kwa mara ya pili mfululizo hatua ya fainali ya ligi hiyo baada ya kuibwaga Bayern Munich na sasa wanasubiri kuumana na Arsenal.
PSG wakiwa ugenini Allianz Arena katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa Jumatano Mei, 6, 2026 walilazimisha sare ya bao 1-1 kwa wenyeji Bayern.
Kwa matokeo hayo, PSG wamekata tiketi ya kucheza fainali kwa ushindi wa jumla ya mabao 6-5 baada ya kupata ushindi wa mabao 5-4 katika mechi ya kwanza baina ya timu hizo.
PSG, wababe kutoka Ufaransa sasa wanasubiri kuikabili Arsenal katika fainali itakayopigwa Mei 30, 2026 mjini Budapest, mechi itakayoamua kama PSG watatwaa taji mara ya pili mfululizo au Arsenal watafanya yao.
Kufuzu fainali kwa mara ya pili mfululizo ni tukio kubwa si kwa mashabiki, wachezaji na benchi la ufundi la PSG linaloongozwa na kocha Luis Enrique, bali hata rais wa klabu hiyo, Nasser Al-Khelaifi hakusita kuonesha furaha yake kwa mafanikio hayo.


“Ni jambo la kipekee, fainali mara ya pili, na sasa tutakwenda pale na kujaribu kuisaka nyota ya pili, niliwaambia wachezaji sisi ni mashujaa,” alisema Al-Khelaifi.
Wakati, PSG wakisaka taji mara ya pili mfululizo, Arsenal chini ya kocha Mikel Arteta wao wamezika unyonge wa muda mrefu kwa kufikia hatua ya fainali, mara ya mwisho kufikia hatua hiyo ilikuwa mwaka 2006.
Kilichobaki kwa Arteta ni kufungua ukurasa mpya kwa kulibeba taji hilo, ubora wa timu hiyo msimu huu unatoa kila ishara kwamba inawezekana kubeba taji hilo msimu huu ingawa jibu sahihi litapatikana Mei 30, 2026.

The post Ni Arsenal, PSG fainali ligi ya mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/08/ni-arsenal-psg-fainali-ligi-ya-mabingwa/feed/ 0
PSG yatakiwa kumlipa Mbappe https://www.greensports.co.tz/2025/12/17/psg-yatakiwa-kumlipa-mbappe/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/17/psg-yatakiwa-kumlipa-mbappe/#respond Wed, 17 Dec 2025 12:27:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14186 Paris, UfaransaMahakama ya Kazi nchini Ufaransa imeitaka klabu ya PSG kumlipa mshambuliaji wake wa zamani, Kylian Mbappe fidia ya Pauni 52 milioni ikiwa ni malimbikizo ya mishahara na marupurupu.Mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa anaichezea Real Madrid katika madai yake ya awali aliyoyafikisha katika mahakama hiyo ya mjini Paris alitaka alipwe Pauni 231 milioni huku PSG […]

The post PSG yatakiwa kumlipa Mbappe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Paris, Ufaransa
Mahakama ya Kazi nchini Ufaransa imeitaka klabu ya PSG kumlipa mshambuliaji wake wa zamani, Kylian Mbappe fidia ya Pauni 52 milioni ikiwa ni malimbikizo ya mishahara na marupurupu.
Mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa anaichezea Real Madrid katika madai yake ya awali aliyoyafikisha katika mahakama hiyo ya mjini Paris alitaka alipwe Pauni 231 milioni huku PSG nao wakifungua kesi kudai fidia ya Pauni 211 milioni.
Katika madai ya awali Mbappe alikuwa akiidai PSG fidia kwa kuchafuliwa jina katika mgogoro wa mkataba wake na klabu hiyo na namna ambavyo klabu haikumpa heshima lakini mahakama iliamua alipwe sehemu ya alichodai.
Inaaminika kuwa sehemu kubwa ya fedha ambazo mahakama imetaka mshambuliaji huyo alipwe ni za marupurupu na si mshahara ambapo awali mahakama ilizuia akaunti za PSG baada ya maombi ya mawakili wa Mbappe.

“Tumeridhishwa na uamuzi huu, hiki ndicho unachokitarajia pale ambapo mishahara hailipwi, uamuzi wa aina hii unaonesha ni kwa kiasi gani makubaliano yanapofikiwa ni lazima yatekelezwe,”ilieleza taarifa ya mawakili wa Mbappe.


Wakati timu ya mawakili wa Mbappe ikionekana kuridhishwa na uamuzi wa mahakama, upande wa PSG hakufuta uwezekano wa kuukatia rufaa uamuzi huo.
PSG imekuwa ikidai kulipwa Pauni zaidi ya 290 milioni ikiwa ni fidia katika mpango wa mwaka 2023 wa uhamisho wa Mbappe kwenda Saudi Arabia kujiunga na klabu ya Al Hilal, uhamisho ambao ulikwama.
Badala yake Mbappe alihamia Real Madrid akiwa mchezaji huru na sasa PSG wamepokea uamuzi wa Mahakama ya Kazi ya Paris na wanajipanga kufanyia kazi uamuzi huo wakitambua kwamba wana haki ya kukata rufaa.

The post PSG yatakiwa kumlipa Mbappe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/17/psg-yatakiwa-kumlipa-mbappe/feed/ 0
Ushindi wa PSG, wawili wauawa, magari yachomwa moto https://www.greensports.co.tz/2025/06/02/ushindi-wa-psg-wawili-wauawa-magari-yachomwa-moto/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/02/ushindi-wa-psg-wawili-wauawa-magari-yachomwa-moto/#respond Mon, 02 Jun 2025 18:54:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13544 Paris, UfaransaWatu wawili wamefariki dunia huku mamia wakishikiliwa na polisi nchini Ufaransa baada ya mashabiki wa klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) kusherehekea ushindi wa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.PSG walifanikiwa kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumamosi Mei 31, 2025 baada ya kuichapa Inter Milan ya Italia mabao 5-0.Taarifa ya polisi […]

The post Ushindi wa PSG, wawili wauawa, magari yachomwa moto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Paris, Ufaransa
Watu wawili wamefariki dunia huku mamia wakishikiliwa na polisi nchini Ufaransa baada ya mashabiki wa klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) kusherehekea ushindi wa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
PSG walifanikiwa kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumamosi Mei 31, 2025 baada ya kuichapa Inter Milan ya Italia mabao 5-0.
Taarifa ya polisi ilieleza kuwa kijana mmoja wa miaka 17 katika mji wa Dax alifariki Jumamosi usiku kwa kuchomwa na kitu kifuani wakati mashabiki wa PSG wakiwa katika shmrashamra za ushindi huo.
Mtu mwingine aliyeuawa ni kijana wa miaka 23 ambaye alikuwa akiendesha baiskeli ndogo katikati ya jiji la Paris ambaye kifo chake kilitokea baada ya kugongwa na gari.
Mashabiki wa PSG walionekana kuwehuka na ushindi huo wa kihistoria na baadhi yao kufikia hatua ya kuvunja vituo vya mabasi na kuchoma moto magari.
Klabu ya PSG ilitoa taarifa kulaani matukio hayo ya vurugu na kuongeza kuwa yanakwenda kinyume na maadili ya klabu hiyo na kwa namna yoyote ni vitendo ambavyo haviwakilishi sehemu kubwa ya mashabiki wao.
Kwa upande wake Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron alisema vurugu hizo hazikubaliki na hazina uhalali wowote na wote waliohusika wataadhibiwa.
Mashabiki wa PSG hata hivyo waliendelea na maandamano yao ya kusherehekea ushindi hadi siku iliyofuata yaani Jumapili ingawa idadi ya maofisa usalama iliongezeka katika mitaa waliyokuwa mashabiki hao.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ilieleza kuwa polisi 20 na maofisa saba ya kikosi cha zimamoto walijeruhiwa huku jumla ya magari 264 yakichomwa moto katika matukio yaliyotokea mapema Jumapili.

The post Ushindi wa PSG, wawili wauawa, magari yachomwa moto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/02/ushindi-wa-psg-wawili-wauawa-magari-yachomwa-moto/feed/ 0
PSG yabeba taji la kwanza ligi ya mabingwa https://www.greensports.co.tz/2025/06/02/psg-yabeba-taji-la-kwanza-ligi-ya-mabingwa/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/02/psg-yabeba-taji-la-kwanza-ligi-ya-mabingwa/#respond Mon, 02 Jun 2025 18:29:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13534 Munich, UjerumaniHatimaye klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) kwa mara ya kwanza imebeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya huku ikiweka rekodi ya kipekee kwa kuibugiza Inter Milan mabao 5-0.Ushindi huo uliopatikana Jumamosi hii Mei 31, 2025 kwenye dimba la Allianz Arena mjini Munich utabaki katika kumbukumbu ya kuwa ushindi mkubwa kupatikana katika mechi ya fainali […]

The post PSG yabeba taji la kwanza ligi ya mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Munich, Ujerumani
Hatimaye klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) kwa mara ya kwanza imebeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya huku ikiweka rekodi ya kipekee kwa kuibugiza Inter Milan mabao 5-0.
Ushindi huo uliopatikana Jumamosi hii Mei 31, 2025 kwenye dimba la Allianz Arena mjini Munich utabaki katika kumbukumbu ya kuwa ushindi mkubwa kupatikana katika mechi ya fainali ya michuano hiyo tangu mwaka 1956.
PSG, timu iliyopiganiwa kwa jeuri ya fedha kwa kusajili wachezaji wa bei mbaya kwa lengo la kusaka mafanikio hatimaye imeyapata mafanikio hayo ikimaliza msimu huu na mataji matatu yaani treble, mataji mengine ni lile la Ligi 1 na Coupe de France.
Alianza Achraf Hakimi kwa kufungua ukurasa wa mabao dakika ya 12 dhidi ya timu yake ya zamani na kufuatiwa na mabao mengine mawili kutoka kwa Desire Doue, mshambuliaji kinda mwenye umri wa miaka 19.
Mabao mengine mawili katika ushindi huo wa kihistoria yalifungwa na Khvicha Kvaratskhelia na Senny Mayulu aliyeingia akitokea benchi.
Ushindi wa PSG umekuja baada ya miaka takriban 10 baada ya bilionea wa Qatari kuinunua timu hiyo na kuanza kufanya usajili wa fujo kwa kuwabeba mastaa kibao kwa bei mbaya.
Katika orodha ya mastaa hao walikuwamo kina Neymar, Lionel Messi, Zlatan Ibrahimovic, Kylian Mbappe na wengineo lakini hawakuweza kuipa timu hiyo taji la hadhi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Miaka miwili iliyopita, PSG iliachana na utaratibu wa kusajili mastaa hao badala yake ikawekeza kwa wachezaji wa umri mdogo ambao hatimaye wamewapa taji ambalo wamekuwa wakilisaka kwa muda mrefu.
Kwa ushindi huo PSG inakuwa timu ya pili ya Ufaransa kubeba taji hilo lenye hadhi ya juu na utajiri kati ya mashindano ya klabu Ulaya na duniani, timu nyingine ni Marseille ambayo ilifanya hivyo mwaka 1993.
Kwa upande wa kocha wa timu hiyo, Luis Enrique hii inakuwa mara yake ya pili kubeba taji hilo baada ya kufanya hivyo akiwa na Barcelona mwaka 2015.
“Tumeweka historia, tumeandika majina yetu katika historia ya hii klabu, kwa muda mrefu hiki ndicho kitu ambacho klabu hii ilipaswa kukipata, tuna furaha, tumetengeneza familia kubwa,” alisema Hakimi.

The post PSG yabeba taji la kwanza ligi ya mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/02/psg-yabeba-taji-la-kwanza-ligi-ya-mabingwa/feed/ 0
Mbappe ajibebesha lawama PSG ikilala 1-0 https://www.greensports.co.tz/2024/05/08/mbappe-ajibebesha-lawama-psg-ikilala-1-0/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/08/mbappe-ajibebesha-lawama-psg-ikilala-1-0/#respond Wed, 08 May 2024 06:24:18 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10892 Paris, UfaransaMshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe amesema kushindwa kwa timu yake kufuzu hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kulala kwa bao 1-0 mbele ya Borussia Dortmund, sababu ni kupoteza nafasi zikiwamo alizopoteza yeye.PSG ikiwa nyumbani katika jiji la Paris, jana Jumanne ililala kwa bao 1-0 na hivyo kutolewa kwa jumla ya […]

The post Mbappe ajibebesha lawama PSG ikilala 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Paris, Ufaransa
Mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe amesema kushindwa kwa timu yake kufuzu hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kulala kwa bao 1-0 mbele ya Borussia Dortmund, sababu ni kupoteza nafasi zikiwamo alizopoteza yeye.
PSG ikiwa nyumbani katika jiji la Paris, jana Jumanne ililala kwa bao 1-0 na hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 2-0 baada ya kulala kwa bao 1-0 katika mechi ya nusu fainali ya kwanza.
Kwa matokeo hayo, Dortmund sasa inasubiri kucheza mechi ya fainali kwenye dimba la Wembley na mshindi wa mechi nyingine ya nusu fainali kati ya Real Madrid na Bayern Munich leo Jumatano.
Akizungumza baada ya matokeo hayo, Mbappe alisema kwamba katika mechi hiyo alijaribu kadri alivyoweza kuisaidia timu yake lakini hapo hapo alikiri kushindwa kufanya hivyo kiasi cha kutosha.
“Tunapozungumzia kuwa sahihi katika eneo la boksi, nafikiri mimi hapo ndiye mlengwa, mimi ni mtu ambaye ni lazima nifunge mabao na niwe makini, mambo yanapokuwa mazuri nabeba sifa zote na inapokuwa tofauti nabeba lawama, hilo si tatizo,” alisema Mbappe.
Akifafanua zaidi Mbappe alisema mtu wa kwanza ambaye ilikuwa lazima afunge ni yeye na kwamba kilichojitokeza ndivyo maisha yalivyo na sasa ni lazima yeye na wenzake waangalie mbele.
Mchezaji huyo ambaye anahusishwa na mipango ya kujiunga na Real Madrid alisema kwamba PSG si kwamba haikuwa na bahati bali haikuwa katika ubora kiasi cha kutosha.
PSG ambao walifanya mashambulizi kadhaa yakiwamo mashuti yaliyogonga mwamba, jambo ambalo Mbappe alisema linaonesha jinsi ambavyo hawakuwa vizuri na kwa upande wa Dortmund alisema hana uhakika kama timu hiyo ilikuwa bora zaidi yao.

“Sipendi kuzungumzia suala la kutokuwa na bahati, unapokuwa vizuri mashuti hayawezi kugonga mwamba, yanaingia nyavuni, leo (jana) hatukuwa vizuri sisi washambuliaji,” alisema Mbappe.


Bao lililoibeba Dortmund lilipatikana mapema kipindi cha pili mfungaji akiwa ni Mats Hummels na baada ya hapo timu hiyo ilifanya kazi nzuri kumdhibiti Mbappe ambaye huenda hiyo ikawa mechi yake ya mwisho ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na jezi ya PSG.

Mbappe hata hivyo alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu kujiunga na Real Madrid aliishia kukunja uso na kuondoka.
Naye kocha wa PSG, Luis Enrique aliwapongeza Dortmund kwa ushindi na kusema kwamba kilichoikuta timu yake kinasikitisha hasa kwa namna ambavyo walicheza vizuri na kufanya mashambulizi ya kutosha.
“Inasikitisha unapopoteza mchezo hasa kwa namna hii, tumegonga mwamba wa goli mara sita, tumepiga mashuti 31 lakini hatukuweza kufunga goli, inaonekana kama ni jambo gumu kuamini,” alisema Enrique.
Dortmund wakifanikiwa kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu watakuwa wanafanya hivyo kwa mara ya kwanza tangu kufanya hivyo mara ya mwisho mwaka 1997.

The post Mbappe ajibebesha lawama PSG ikilala 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/08/mbappe-ajibebesha-lawama-psg-ikilala-1-0/feed/ 0
Mbappe apewa jukumu la ulinzi PSG ikiivaa Dortmund https://www.greensports.co.tz/2024/05/07/mbappe-apewa-jukumu-la-ulinzi-psg/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/07/mbappe-apewa-jukumu-la-ulinzi-psg/#respond Tue, 07 May 2024 06:27:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10869 Paris, UfaransaKocha wa PSG, Luis Enrique amemtaka mshambuliaji wake Kylian Mbappé kufanya kazi ya ulinzi katika mechi ya nusu fainali ya pili dhidi ya Borussia Dortmund leo Jumanne ili kubadili matokeo baada ya kulala kwa bao 1-0 katika mechi ya kwanza.Enrique alikuwa akijibu swali aliloulizwa kuhusu nini anachoweza kufanya Mbappe ili kuipatia timu hiyo ushindi […]

The post Mbappe apewa jukumu la ulinzi PSG ikiivaa Dortmund first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Kylian Mbappe

Paris, Ufaransa
Kocha wa PSG, Luis Enrique amemtaka mshambuliaji wake Kylian Mbappé kufanya kazi ya ulinzi katika mechi ya nusu fainali ya pili dhidi ya Borussia Dortmund leo Jumanne ili kubadili matokeo baada ya kulala kwa bao 1-0 katika mechi ya kwanza.
Enrique alikuwa akijibu swali aliloulizwa kuhusu nini anachoweza kufanya Mbappe ili kuipatia timu hiyo ushindi ambapo kocha huyo alisema mshambuliaji huyo nyota anahitaji kutoa mchango wake katika eneo lote la uwanja.
“Sisi ni timu, tunawataka washambuliaji kusaidia kuhakikisha mipira inafika mara chache kwenye eneo letu la ulinzi, kwa pamoja kila mmoja ana wajibu wa kutoa mchango wake, hata mchezaji nyota duniani anatakiwa kusaidia katika ulinzi,” alisema Enrique.
Enrique hata hivyo alisema kwamba ana matumaini ya timu yake kutoka na ushindi katika mechi hiyo na hatimaye kucheza fainali ya michuano hiyo mikubwa ya ngazi ya klabu barani Ulaya.
Kocha huyo pia alisema kwamba kitendo cha kuwa nyuma katika mechi ya kwanza si jambo ambalo linamfanya aogope badala yake anaamini timu yake ipo vizuri kimtazamo na kifikra kwa ajili ya mechi hiyo.

“Nafikiri unahitaji utulivu wa kifikra ili kukabiliana na jambo lolote katika taaluma yako au maisha yako binafsi, wakati wote jiandae mambo yanaweza kwenda vibaya kama ni lazima iwe hivyo na uwe tayari kubadili hali hiyo,” alisema Enrique.


Kwa upande wake kocha wa Dortmund, Edin Terzic alisema timu yake inahitaji kuboresha kiwango ilichokionesha katika mechi ya kwanza ili iweze kufuzu na hatimaye kusonga mbele na kucheza mechi ya fainali.

The post Mbappe apewa jukumu la ulinzi PSG ikiivaa Dortmund first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/07/mbappe-apewa-jukumu-la-ulinzi-psg/feed/ 0
Enrique aamini PSG itaizamisha Barca https://www.greensports.co.tz/2024/04/16/enrique-aamini-psg-itaizamisha-barca/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/16/enrique-aamini-psg-itaizamisha-barca/#respond Tue, 16 Apr 2024 07:19:31 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10621 Paris, UfaransaKocha wa PSG, Luis Enrique amesema anaamini timu yake inaweza kupindua meza na kuibuka na ushindi katika mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona itakayopigwa leo Jumanne.Katikam mechi ya kwanza iliyopigwa mjini Paris, Barca iliibuka na ushindi wa mabao 3-2, matokeo ambayo pia yaliifanya PSG ibaki na rekodi ya […]

The post Enrique aamini PSG itaizamisha Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Paris, Ufaransa
Kocha wa PSG, Luis Enrique amesema anaamini timu yake inaweza kupindua meza na kuibuka na ushindi katika mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona itakayopigwa leo Jumanne.
Katikam mechi ya kwanza iliyopigwa mjini Paris, Barca iliibuka na ushindi wa mabao 3-2, matokeo ambayo pia yaliifanya PSG ibaki na rekodi ya kucheza mechi 27 za mashindano yote bila kupoteza hata moja.
Enrique alikuwa kocha wa Barça mwaka 2017 na kufanikiwa kupindua meza baada ya kufungwa mabao 4-0 na PSG lakini katika mechi ya pili waliichapa PSG 6-1 na sasa kocha huyo anataka jambo hilo lijirudie akiwa kocha PSG.
“PSG haijawahi kupindua meza baada ya kufungwa katika mechi ya kwanza, lakini Jumanne ndio siku ya kufanya hivyo,” alisema Enrique katika mkutano na waandishi wa habari.
“Baada ya kupoteza mechi muhimu, baada ya mechi hiyo mambo yanakuwa magumu, ni mtego fulani, kunakuwa na ugumu kujiweka sawa kisaikolojia lakini jambo zuri katika soka ni kwamba baada ya hapo unakuwa na mechi nyingine dhidi ya mpinzani yule yule,” alisema Enrique.
Kabla ya mechi ya kwanza baina ya timu hizo, Enrique anakumbukwa kwa kusema kwamba analijua vyema soka la Barca kumzidi kocha wa sasa wa timu hiyo, Xavi Hernandez na msimamo wake utaendelea kuwa hivyo ingawa hiyo haimaanishi kwamba haheshimu kazi ya Xavi.
Kwa upande wake, Xavi yeye alisema kwamba anamuweka Enrique kwa ubora sawa na makocha wa kiwango cha juu kina Pep Guardiola na Luis Aragones na kwake kati ya makocha bora waliowahi kumfundisha.
Xavi ambaye leo ana faida ya kuwa nyumbani, aliwahi kucheza soka na Enrique wakiwa Barça na baadaye katika msimu wa 2014-15, Enrique alikuwa kocha wa Barca, Xavi akiwa mchezaji.
Mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya leo Jumanne
Barca v PSG
B Dortmund v Atl Madrid
Mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya kesho Jumatano
Bayern Munich v Arsenal
Man City v Real Madrid

The post Enrique aamini PSG itaizamisha Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/16/enrique-aamini-psg-itaizamisha-barca/feed/ 0
Mbappe aipeleka PSG robo fainali Ulaya https://www.greensports.co.tz/2024/03/06/mbappe-aipeleka-psg-robo-fainali-ulaya/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/06/mbappe-aipeleka-psg-robo-fainali-ulaya/#respond Wed, 06 Mar 2024 06:03:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10051 Madrid, HispaniaKocha wa PSG, Luis Enrique huenda akalazimika kufikiria upya uamuzi wake wa kutaka timu hiyo ianze mapema kujipanga bila ya Kylian Mbappe baada ya mshambuliaji huyo kufunga mabao mawili na kuiwezesha PSG kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.Enrique alitangaza mpango huo na kuanza kuufanyia kazi katika mechi mbili za Ligi 1 dhidi […]

The post Mbappe aipeleka PSG robo fainali Ulaya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Kylian Mbappe

Madrid, Hispania
Kocha wa PSG, Luis Enrique huenda akalazimika kufikiria upya uamuzi wake wa kutaka timu hiyo ianze mapema kujipanga bila ya Kylian Mbappe baada ya mshambuliaji huyo kufunga mabao mawili na kuiwezesha PSG kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Enrique alitangaza mpango huo na kuanza kuufanyia kazi katika mechi mbili za Ligi 1 dhidi ya Rennes na dhidi ya Monaco, alimuweka benchi Mbappe baada ya kucheza kwa dakika kadhaa na mechi zote hizo ziliisha kwa sare.
Mabao mawili ya Mbappe aliyofunga jana Jumanne usiku dhidi ya Real Sociedad yameifanya PSG kutoka uwanjani na ushindi wa 2-1 na kufuzu robo fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-1, mabao hayo yanatosha kabisa kumfikirisha upya Enrique, bao pekee la Sociedad lilifungwa na Merino.
Si Enrique pekee, hata mabosi PSG nao wana kazi ya kutafakari kama ni sahihi kumuachia Mbappe aondoke licha ya ukweli kwamba mkataba wake unafikia ukomo mwishoni mwa msimu huu na habari zilizopo ni kwamba mazungumzo yake na Real Madrid yanakwenda vizuri.
Kutokana na juhudi hizo za Mbappe, PSG sasa wanasubiri hapo Machi 15 ili kumjua mpinzani wao katika mechi ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa ya klabu barani Ulaya..
Nayo Bayern Munich, timu ambayo imekuwa na msimu mbaya katika Ligi Kuu ya Ujerumani au Bundesliga, jana ilifanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuilaza Lazio mabao 3-0 na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1.
Katika mechi hiyo nyota ya nahodha wa England, Harry Kane iling’ara baada ya kutupia wavuni mabao mawili peke yake wakati bao la tatu likifungwa na Muller.
Matokeo ya mechi za jana Ligi ya Mabingwa Ulaya…
Bayern Munich 3-0 Lazio
Real Sociedad 1-2 PSG

The post Mbappe aipeleka PSG robo fainali Ulaya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/06/mbappe-aipeleka-psg-robo-fainali-ulaya/feed/ 0
Messi aitolea uvivu PSG https://www.greensports.co.tz/2023/09/23/messi-aitolea-uvivu-psg/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/23/messi-aitolea-uvivu-psg/#respond Sat, 23 Sep 2023 13:39:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7838 Miami, MaarekaniMshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi amesema alichukizwa kwa kutopewa heshima na klabu yake ya zamani wa PSG baada ya kubeba kombe la dunia wakati wachezaji wenzake wote wa Argentina walipewa heshima hiyo na klabu zao.Katika mechi ya fainali kati ya Argentina na Ufaransa, Messi alifunga mabao mawili na lingine la […]

The post Messi aitolea uvivu PSG first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Miami, Maarekani
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi amesema alichukizwa kwa kutopewa heshima na klabu yake ya zamani wa PSG baada ya kubeba kombe la dunia wakati wachezaji wenzake wote wa Argentina walipewa heshima hiyo na klabu zao.
Katika mechi ya fainali kati ya Argentina na Ufaransa, Messi alifunga mabao mawili na lingine la tatu kwenye mikwaju ya penalti na kuiwezesha Argentina kutoka na ushindi wa 4-2 na hatimaye kubeba Kombe la Dunia katika fainali zilizopigwa Qatar, Novemba na Desemba mwaka jana.
Akizungumzia hali ilivyokuwa baada ya ushindi huo aliporejea katika klabu yake Messi alisema, “mimi nilikuwa mchezaji pekee kati ya 25 ambaye sikupewa heshima na klabu.”
Messi katika hilo alifafanua, “inaeleweka, kwa sababu sisi (Argentina) wao (Ufaransa) hawakuweza kulitetea Kombe la Dunia.”
Katika usajili wa dirisha kubwa la kiangazi, mwezi Juni, Messi aliachana na PSG na alikuwa na wakati mgumu katika klabu hiyo na alikiri kwamba kulikuwa na tatizo kati yake na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo katika misimu miwili aliyoichezea.
Alipoulizwa kama hakupenda kujiunga na PSG, Messi alisema, “Ilitokea kama ilivyokuwa, halikuwa jambo ambalo nililitarajia lakini wakati wote huwa nasema, kuna mambo hutokea kwa sababu, hata kama sikuwa vizuri pale lakini ilitokea kwamba nilikuwa bingwa wa dunia wakati nikiwa pale.”
Akiizungumzia klabu yake ya sasa ya Inter Miami FC ya Marekeni, Messi alisema kwamba anafurahia soka lake katika klabu hiyo.

“Napenda ninachokifanya, nafurahia kucheza na kwa sasa nacheza katika namna tofauti, na hii ndio sababu iliyonifanya nichukua uamuzi wa kuja Miami na si kuendelea na soka kwingineko, unapata uzoefu tofauti,” alisema Messi.


Kuhusu uwezekano wa kustaafu soka, Messi mwenye umri wa miaka 36 sasa alisema kwamba hafikirii jambo hilo na hajaufuta uwezekano wa kurudi nyumbani Argentina na kuichezea klabu yake ya zamani ya utotoni ya Newell’s Old Boys kabla ya kustaafu soka hasa baada ya kuwa tayari amebeba taji la dunia.

The post Messi aitolea uvivu PSG first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/23/messi-aitolea-uvivu-psg/feed/ 0