Neymar - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 22 Oct 2024 07:18:27 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Neymar - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Neymar arejea uwanjani https://www.greensports.co.tz/2024/10/22/neymar-arejea-uwanjani/ https://www.greensports.co.tz/2024/10/22/neymar-arejea-uwanjani/#respond Tue, 22 Oct 2024 07:18:26 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12025 Riyadh, Saudi ArabiaMshambuliaji nyota wa Brazil aliyekuwa majeruhi kwa takriban mwaka mmoja, Neymar hatimaye amerejea uwanjani kwa mara ya kwanza na kuiwakilisha timu yake ya Al Hilal ya Saudi Arabia.Neymar alicheza mechi hiyo Jumatatu hii dhidi ya Al Ain, aliingia akitokea benchi katika dakika ya 77 na kuchukua nafasi ya Nasser Al Dawsari wakati huo […]

The post Neymar arejea uwanjani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabia
Mshambuliaji nyota wa Brazil aliyekuwa majeruhi kwa takriban mwaka mmoja, Neymar hatimaye amerejea uwanjani kwa mara ya kwanza na kuiwakilisha timu yake ya Al Hilal ya Saudi Arabia.
Neymar alicheza mechi hiyo Jumatatu hii dhidi ya Al Ain, aliingia akitokea benchi katika dakika ya 77 na kuchukua nafasi ya Nasser Al Dawsari wakati huo Al Hilal ikiwa inaongoza kwa mabao 5-3.
Mara baada ya kuingia Neymar nusura aisaidie timu yake kupata bao la sita baada ya kucheza pasi kadhaa na Aleksandar Mitrovic kabla ya kufumua shuti lililotoka kidogo nje ya lango.
Baada ya mechi hiyo iliyoisha kwa Al Hilal kutoka na ushindi wa mabao 5-4, Neymar alisema anajisikia furaha na wakati wote amekuwa na timu nzuri lakini zaidi ana furaha ya kurudi tena uwanjani.
Neymar nyota wa zamani wa PSG ya Ufaransa aliumia goti wakati akiiwakilisha Brazil dhidi ya Uruguay na kufanyiwa upasuaji Novemba mwaka jana na tangu hapo amekuwa nje ya uwanja kabla ya kurejea Jumatatu.
Aljiunga na Al Hilal Agosti mwaka jana akitokea PSG kwa ada ya Euro 90 milioni lakini aliichezea timu yake hiyo mpya mechi tano tu kabla ya kuumia na sasa amerejea na kupongezwa na timu yake ya zamani ya Santos ya kwao Brazil.
“Ni zaidi ya miezi 12 ya kuwa nje ya uwanja, akiwa na shauku kubwa ya kurudi ili kufanya kile anachokipenda zaidi,” ilieleza taarifa ya Santos kupitia mitandao ya kijamii.
Wakati wote akiwa majeruhi, Neymar mbali na kushindwa kuiwakilisha Al Hilal pia alishindwa kuiwakilisha Brazil kwenye fainali za Copa America zilizofanyika Marekani na Argentina kubeba kombe.
Kwa sasa inasubiriwa kuona kama mchezaji huyo ataweza kuiwakilisha Brazil kwenye mechi mbili za kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Venezuela na Uruguay zitakazopigwa Novemba mwaka huu.

The post Neymar arejea uwanjani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/10/22/neymar-arejea-uwanjani/feed/ 0
Kocha Al Hilal amsubiri Neymar https://www.greensports.co.tz/2024/05/23/kocha-al-hilal-amsubiri-neymar/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/23/kocha-al-hilal-amsubiri-neymar/#respond Thu, 23 May 2024 09:27:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11088 Riyadh, Saudi ArabiaKocha wa Al Hilal ya Saudi Arabia, Jorge Jesus amesema kwamba ana matumaini mshambuliaji wao, Neymar ambaye ni majeruhi atarudi mwezi Septemba na kuanza kuitumikia timu hiyo.Neymar, 32, amekuwa nje ya uwanja tangu afanyiwe upasuaji wa goti la mguu wa kushoto baada ya kuumia wakati akiiwakilisha timu yake ya taifa ya Brazil, Oktoba […]

The post Kocha Al Hilal amsubiri Neymar first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabia
Kocha wa Al Hilal ya Saudi Arabia, Jorge Jesus amesema kwamba ana matumaini mshambuliaji wao, Neymar ambaye ni majeruhi atarudi mwezi Septemba na kuanza kuitumikia timu hiyo.
Neymar, 32, amekuwa nje ya uwanja tangu afanyiwe upasuaji wa goti la mguu wa kushoto baada ya kuumia wakati akiiwakilisha timu yake ya taifa ya Brazil, Oktoba mwaka jana.
“Kwa maumivu kama ya Neymar muda ambao wanautoa hadi mchezaji kupona ni kati ya miezi 10 hadi 11, tunadhani Neymar hatopona mwanzoni mwa msimu mpya, tunadhani kati ya Septemba au Oktoba atakuwa fiti,” alisema Jorge.
Baada ya kujiunga na Al Hilal akitokea PSG Agosti mwaka huu, Neymar ameichezea timu hiyo mechi tano tu kwenye Ligi Kuu Saudi Arabia kabla ya kuumia na hivyo kushindwa kuutumikia vizuri mkataba wake wa miaka miwili na timu hiyo.
Neymar ambaye ndiye anayeongoza kwa kuifungia timu ya taifa ya Brazil mabao mengi (mabao 79) pia atakosa kuiwakilisha Brazil kwenye michuano ya Copa America ingawa huenda akaiwakilisha kwenye mechi za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026.
Wakati huo huo, Jorge naye amethibitisha kwamba yuko mbioni kuongeza mkataba na vinara hao wa Ligi Kuu Saudi Arabia akiwa anajivunia rekodi ya ushindi wa mechi 34 mfululizo akiwa na timu hiyo.

The post Kocha Al Hilal amsubiri Neymar first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/23/kocha-al-hilal-amsubiri-neymar/feed/ 0
Kocha Brazil abadili kauli kuhusu Neymar https://www.greensports.co.tz/2024/02/22/kocha-brazil-abadili-kauli-kuhusu-neymar/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/22/kocha-brazil-abadili-kauli-kuhusu-neymar/#respond Thu, 22 Feb 2024 08:03:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9849 Rio de Janeiro, BrazilKocha wa timu ya taifa ya Brazil, Dorival ambaye aliwahi kusema kwamba Brazil ianze kufikiria maisha bila ya Neymar, amebadili kauli hiyo na sasa anasema Neymar ataendelea kuwa mchezaji muhimu kwenye timu ya taifa.Neymar, 32 anayekipiga Al Hilal ya Saudi Arabia, aliumia goti la mguu wa kushoto wakati akiiwakilisha timu ya taifa […]

The post Kocha Brazil abadili kauli kuhusu Neymar first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rio de Janeiro, Brazil
Kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Dorival ambaye aliwahi kusema kwamba Brazil ianze kufikiria maisha bila ya Neymar, amebadili kauli hiyo na sasa anasema Neymar ataendelea kuwa mchezaji muhimu kwenye timu ya taifa.
Neymar, 32 anayekipiga Al Hilal ya Saudi Arabia, aliumia goti la mguu wa kushoto wakati akiiwakilisha timu ya taifa ya Brazil Oktoba mwaka jana na hadi sasa anaendelea na matibabu na ameonesha dalili za kupona na kurudi uwanjani.
Akimzungumzia mchezaji huyo, Dorival alinukuliwa mwezi uliopita akisema ingawa Neymar ni kati ya wachezaji bora watatu duniani lakini Brazil inalazimika kujifunza kucheza bila ya mchezaji huyo.
Kwa sasa Dorival si tena mwenye imani hiyo baada ya kunukuliwa hivi karibuni akisema kwamba Neymar ana nafasi katika mipango yake kwenye kikosi cha Brazil.
Dorival aliulizwa kuhusu kupona kwa Neymar naye akasema,”Ni kati ya mambo muhimu, Neymar ni mchezaji muhimu sana, hilo hata yeye analifahamu, ni kati ya wachezaji bora duniani.”

“Matumaini yetu ni kwamba atapona, atakuwa vizuri, bado ana nafasi (kwenye kikosi) kwa kila ambacho amekifanikisha katika timu ya taifa lakini anahitaji kujiamini, kutulia na kuwa vizuri na zaidi ya yote kuwa makini, atakuwa sehemu ya mpango wetu kama atakuwa fiti,” alisema Dorival.


Tangu aanze kuichezea timu ya taifa ya Brazil, Agosti 2010, Neymar hadi sasa ndiye kinara wa mabao wa timu akiwa na rekodi ya kuifungia jumla ya mabao 79 katika mechi 128

The post Kocha Brazil abadili kauli kuhusu Neymar first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/22/kocha-brazil-abadili-kauli-kuhusu-neymar/feed/ 0
Neymar nje Copa America https://www.greensports.co.tz/2023/12/20/neymar-nje-copa-america/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/20/neymar-nje-copa-america/#respond Wed, 20 Dec 2023 08:53:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8953 Rio de Janeiro, BrazilMshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar atazikosa fainali za michuano ya soka ya Copa America zitakazofanyika mwakani nchini Marekani kutokana na maumivu ya goti yanayomkabili.Daktari wa timu ya taifa ya Brazil, Rodrigo Lasmar amethibitisha hilo jana Jumanne ikiwa imepita miezi miwili tangu mchezaji huyo aumie katika mechi ya Brazil dhidi […]

The post Neymar nje Copa America first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rio de Janeiro, Brazil
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar atazikosa fainali za michuano ya soka ya Copa America zitakazofanyika mwakani nchini Marekani kutokana na maumivu ya goti yanayomkabili.
Daktari wa timu ya taifa ya Brazil, Rodrigo Lasmar amethibitisha hilo jana Jumanne ikiwa imepita miezi miwili tangu mchezaji huyo aumie katika mechi ya Brazil dhidi ya Uruguay ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026.
Neymar, nyota wa zamani wa Barcelona na PSG ambaye kwa sasa anaichezea Al Hilal ya Saudi Arabia, aliumia goti la mguu wa kushoto katika mechi hiyo na kufanyiwa upasuaji wiki mbili baadaye.
Fainali za Copa America zitaanza kutimia vumbi Juni 20 hadi Julai 14 na Dk Lasmar ametaka kusiwe na haraka ya kumuwahisha mchezaji huyo kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha tatizo kuwa kubwa zaidi hapo baadaye.
“Ni mapema mno, hakuna sababu ya kukwepa hatua za tiba kwa lengo la kutaka kupona haraka na kujiweka katika hali hatari zaidi, matarajio yetu ni kwamba atajiandaa kurudi uwanjani mwanzoni mwa msimu wa 2024 Ulaya ambao unaanza mwezi Agosti,” alisema Dk Lasmar.

“Tunahitaji kuwa na subira, kuzungumzia kurudi uwanjani kabla ya miezi tisa ni kutaka kuwahisha jambo, hizi ni taratibu za duniani kote kuhusu matatizo ya goti na upasuaji, ni muhimu kuheshimu muda wa kitabibu, muda ambao mwili unahitaji ili kuwa fiti,” alisema Dk Lasmar.


Dk Lasmar alisisitiza kwamba kama hatua husika zitafuatwa, baada ya kuwa katika kipindi kirefu cha kupona, matarajio ni kwamba Neymar anaweza akapona na kucheza kwa mara nyingine kwa kiwango cha juu.
Neymar kwa sasa ndiye mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil mwenye mabao mengi katika historia ya timu hiyo akiwa amefunga jumla ya mabao 79 katika mechi 129.
Katika fainali za Copa America, Brazil imepangwa Kundi D pamoja na timu za Paraguay, Colombia na timu mojawapo kati ya Costa Rica au Honduras ambazo zinasubiri kucheza Playoff ili kupata mshindi.

The post Neymar nje Copa America first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/20/neymar-nje-copa-america/feed/ 0
Neymar kufanyiwa upasuaji https://www.greensports.co.tz/2023/10/19/neymar-kufanyiwa-upasuaji/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/19/neymar-kufanyiwa-upasuaji/#respond Thu, 19 Oct 2023 09:56:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8167 Rio de Janeiro, BrazilMshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia, Neymar atalazimika kufanyiwa upasuaji baada ya kuumia misuli ya goti la mguu wa kushoto wakati akiiwakilisha Brazil.Neymar aliuamia juzi Jumanne katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Uruguay, mechi ambayo Brazil ililala kwa mabao 2-0 […]

The post Neymar kufanyiwa upasuaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rio de Janeiro, Brazil
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia, Neymar atalazimika kufanyiwa upasuaji baada ya kuumia misuli ya goti la mguu wa kushoto wakati akiiwakilisha Brazil.
Neymar aliuamia juzi Jumanne katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Uruguay, mechi ambayo Brazil ililala kwa mabao 2-0 na mchezaji huyo kutolewa uwanjani akiwa amebebwa kwenye machela.
Mara baada ya kuumia katika dakika ya 44, Neymar alilala chini na baadaye alinukuliwa kupitia mitandao ya kijamii akisema kwamba kimekuwa kipindi kigumu mno kwake. “Najua niko imara lakini safari hii nitaihitaji zaidi familia yangu pamoja na marafiki.”
Haijaweza kufahamika mara moja muda ambao Neymar atautumia hadi kupona ingawa katika hali ya kawaida kwa aina ya upasuaji atakaofanyiwa atahitaji kipindi cha kuanzia miezi minane hadi 10.
“Watu wa Brazil na dunia ya watu wa soka wanamhitaji Neymar akiwa mwenye afya na aliyepona kwa sababu soka inakuwa raha Neymar anapokuwa uwanjani,” alisema rais wa Shirikisho la Soka Brazil, Ednaldo Rodrigues katika taarifa yake.
Neymar, 31 kwa sasa anashika namba moja kwa kuifungia mabao mengi timu ya taifa ya Brazil, aliihama PSG ya Ufaransa mwishoni mwa msimu uliopita na kujiunga na Al-Hilal ingawa kwa miaka ya karibuni amekuwa akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara.

“Si jambo rahisi kupitia majeraha na upasuaji, jaribu kufikiri unarudia jambo hilo kwa mara nyingine baada ya miezi minne ya kuwa fiti,” alisema Neymar.


The post Neymar kufanyiwa upasuaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/19/neymar-kufanyiwa-upasuaji/feed/ 0
Neymar arushiwa mfuko wa bisi https://www.greensports.co.tz/2023/10/14/neymar-arushiwa-mfuko-wa-bisi/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/14/neymar-arushiwa-mfuko-wa-bisi/#respond Sat, 14 Oct 2023 13:54:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8098 Rio de Janeiro, BrazilKocha wa Brazil, Fernando Diniz amechukizwa na kitendo cha mashabiki wa timu hiyo kumpiga kichwani na mfuko wa bisi mshambuliaji wa timu hiyo, Neymar katika mechi dhidi ya Venezuela iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.Mfuko huo wa bisi au popcorn ulirushwa wakati Neymar akitoka katika dimba la Pantanal mara baada ya mechi […]

The post Neymar arushiwa mfuko wa bisi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rio de Janeiro, Brazil
Kocha wa Brazil, Fernando Diniz amechukizwa na kitendo cha mashabiki wa timu hiyo kumpiga kichwani na mfuko wa bisi mshambuliaji wa timu hiyo, Neymar katika mechi dhidi ya Venezuela iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.
Mfuko huo wa bisi au popcorn ulirushwa wakati Neymar akitoka katika dimba la Pantanal mara baada ya mechi hiyo ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 iliyochezwa juzi Alhamisi.
Neymar ambaye alicheza mechi hiyo dakika zote baada ya tukio hilo kocha wake alijaribu kumlinda na mchezaji huyo alionekana akiwatolea maneno makali mashabiki waliokuwa eneo ambalo mfuko huo wa bisi ulitokea.
“Hakika sikubaliani na hili, kumzomea na kumshutumu mchezaji sina tatizo lakini kurusha mfuko wa bisi hakumsaidii mtu, ni ukosefu wa heshima kwa wachezaji waliokuja hapa kucheza na kujitahidi kadri walivyoweza,” alisema Diniz.


Diniz pia alionesha kukerwa kwa namna ambavyo Brazil ilishindwa kupata ushindi na hivyo kujikuta ikizidiwa na Argentina walioifunga Paraguay bao 1-0 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa kuwa na pointi mbili zaidi ya Brazil baada ya kucheza mechi tatu.

“Tungeweza kupata bao la pili, la tatu na la nne, tulimalizia uchezaji wetu vibaya, na pia tusingeruhusu kufungwa goli na Venezuela, tungekuwa makini katika kukaba na kutowapa wapinzani nafasi ya kumalizia,” alisema Diniz.


Katika mechi hiyo, Neymar ndiye aliyetoa pasi ya kona iliyozaa bao la Brazil lililofungwa na beki wa Arsenal, Gabriel Magalhaes kabla Venezuela hawajasawazisha kupitia Eduard Bello jambo lililowakera mashabiki wa Brazil waliotaka kuona timu yao ikipata ushindi wa tatu mfululizo.
Brazil itajitupa tena uwajani Jumanne ijayo ugenini kwa kuumana na Uruguay, mechi ambayo itapigwa mjini Montevideo.

The post Neymar arushiwa mfuko wa bisi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/14/neymar-arushiwa-mfuko-wa-bisi/feed/ 0
Neymar avunja rekodi ya Pele Brazil https://www.greensports.co.tz/2023/09/09/neymar-avunja-rekodi-ya-pele-brazil/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/09/neymar-avunja-rekodi-ya-pele-brazil/#respond Sat, 09 Sep 2023 12:23:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7720 Rio de Janeiro, BrazilMshambuliaji wa Brazil, Neymar kwa sasa ndiye kinara wa wakati wote wa mabao wa timu ya taifa ya Brazil akiwa amempiku Pele kwa mabao mawili, Neymar sasa ana mabao 79.Neymar ameweka rekodi hiyo baada ya kufunga mabao mawili wakati Brazil ikiichapa Bolivia mabao 5-1 katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia […]

The post Neymar avunja rekodi ya Pele Brazil first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rio de Janeiro, Brazil
Mshambuliaji wa Brazil, Neymar kwa sasa ndiye kinara wa wakati wote wa mabao wa timu ya taifa ya Brazil akiwa amempiku Pele kwa mabao mawili, Neymar sasa ana mabao 79.
Neymar ameweka rekodi hiyo baada ya kufunga mabao mawili wakati Brazil ikiichapa Bolivia mabao 5-1 katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 iliyopigwa usiku wa kuamkia leo Jumamosi.
Neymar alifunga mabao hayo mawili katika kipindi cha pili na huo ukiwa ni mchezo wake wa 125 katika timu ya Brazil ingawa tayari ametahadharisha kwamba yeye si bora kumzidi Pele.
“Sikuwahi kufikiria kuifikia rekodi hii, lakini mimi si bora kuliko Pele au mchezaji mwingine yeyote wa timu ya taifa,” alisema Neymar mchezaji wa zamani wa Barcelona na PSG ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia.
Kwa kuvunja rekodi ya Pele Neymar amepewa tuzo maalum na shirikisho la soka la Brazil baada ya kuwa ndiye mwanasoka mwanaume anayeongoza kwa kuifungia Brazil mabao mengi kwa sasa.
Pele ambaye alifariki dunia Desemba mwaka jana akiwa na miaka 82, aliifungia Brazil mabao 77 katika mechi 92 kati ya mwaka 1957 hadi 1971 na hadi sasa anatajwa duniani kote kuwa mmoja wa wachezaji bora waliowahi kuuteka ulimwengu wa soka.

“Hongera kwako Neymar kwa kuipiku rekodi ya mfalme wa mabao wa Brazil, hata Pele naye pia anakupongeza kwa hili,” ilieleza taarifa ya shirikisho la soka Brazil.


Kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Fernando Diniz alisema: “Alikuja (Neymar) kufanya kile alichokifanya, alifunga mabao mawili na kuvunja rekodi.”

The post Neymar avunja rekodi ya Pele Brazil first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/09/neymar-avunja-rekodi-ya-pele-brazil/feed/ 0
Rais PSG amjibu Neymar https://www.greensports.co.tz/2023/09/08/rais-psg-amjibu-neymar/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/08/rais-psg-amjibu-neymar/#respond Fri, 08 Sep 2023 13:36:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7697 Paris, UfaransaRais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi (pichani) amewajibu aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo, Neymar na aliyekuwa mkurugenzi wa michezo, Leonardo akisema kwamba PSG kwa sasa ina umoja ambao haujawahi kutokea.Neymar hivi karibuni alisema kwamba alikuwa katika wakati mgumu akiwa PSG pamoja na mchezaji mwenzake, Lionel Messi ambao katika baadhi ya mechi walijikuta wakizomewa na baadhi […]

The post Rais PSG amjibu Neymar first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Paris, Ufaransa
Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi (pichani) amewajibu aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo, Neymar na aliyekuwa mkurugenzi wa michezo, Leonardo akisema kwamba PSG kwa sasa ina umoja ambao haujawahi kutokea.
Neymar hivi karibuni alisema kwamba alikuwa katika wakati mgumu akiwa PSG pamoja na mchezaji mwenzake, Lionel Messi ambao katika baadhi ya mechi walijikuta wakizomewa na baadhi ya mashabiki wa timu hiyo.
Leonardo naye aliwahi kunukuliwa akiushutumu uongozi wa PSG akisema kwamba Neymar, Messi na Kylian Mbappe walikosa kuungwa mkono na kuthaminiwa ili wawe katika mazingira mazuri ya kuipa timu hiyo ushindi.
Wakati Messi na Neymar wameihama timu hiyo, Mbappe ameendelea kubaki licha ya kuwapo utata kuhusu mkataba wake na Al-Khelaifi amempongeza mchezaji huyo ambaye pia ni nahodha wa timu ya Ufaransa pamoja na kuwajibu Neymar na Leonardo. “Kylian Mbappe ni mchezaji wa kipekee na mtu mzuri,” alisema Al-Khelaifi.

“Na timu ya PSG haijawahi kuwa katika umoja ndani na nje ya uwanja kama ilivyo sasa, hiki ni kitu ambacho tumekiona wikiendi hii katika mechi ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Lyon, tuna kocha mzuri (Luis Enrique) na mkurugenzi wa michezo, Luis Campos, na nina furaha kwa ari mpya iliyopo katika klabu,” alisema Al-Khelaifi.


Baada ya kuwakosa Messi aliyejiunga na Inter Miami FC ya Marekani na Neymar aliyetimkia Saudi Arabia, PSG ilianza Ligi 1 nchini Ufaransa kwa sare mbili kabla ya kuanza kuibuka na ushindi.
PSG ina kibarua kigumu kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa kundi moja na timu za Newcastle, AC Milan na Borussia Dortmund ingawa Al-Khelaifi anaamini watakuwa na mafanikio katika fainali hizo msimu huu.
“Mwaka huu tupo katika muelekeo mpya, hatuangalii kwa sana matokeo badala yake tunaangalia kiwango na aina ya uchezaji wetu, kama tutaendelea hivyo, matokeo yatatufuata,” alisema Al-Khelaifi.
Al-Khelaifi pia alisema kuna watu wamesahau kwamba katika misimu minne iliyopita PSG ilifikia fainali na nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

The post Rais PSG amjibu Neymar first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/08/rais-psg-amjibu-neymar/feed/ 0
Neymar akumbuka majanga ya PSG https://www.greensports.co.tz/2023/09/07/neymar-akumbuka-majanga-ya-psg/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/07/neymar-akumbuka-majanga-ya-psg/#respond Thu, 07 Sep 2023 15:37:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7682 Riyadh, Saudi ArabiaMshambuliaji wa Brazil, Neymar amesema kwamba alipitia kupindi kigumu yeye na mshambuliaji mwenzake Lionel Messi wakati wakiichezea klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa.Neymar na Messi wote waliihama PSG katika majira ya kiangazi msimu huu, Neymar akijiunga na klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia kwa ada ya Dola 98.6 milioni wakati messi […]

The post Neymar akumbuka majanga ya PSG first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabia
Mshambuliaji wa Brazil, Neymar amesema kwamba alipitia kupindi kigumu yeye na mshambuliaji mwenzake Lionel Messi wakati wakiichezea klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa.
Neymar na Messi wote waliihama PSG katika majira ya kiangazi msimu huu, Neymar akijiunga na klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia kwa ada ya Dola 98.6 milioni wakati messi alijiunga na Inter Miami ya Marekani akiwa mchezaji huru.
Kauli hiyo ya Neymar imekuja baada ya mchezaji huyo kuulizwa kuhusu Messi kubeba Kombe la Dunia na timu ya Argentina ambapo alisema alifurahi mwenzake alipobeba taji hilo la dunia lakini alikuwa na huzuni kwa kilichokuwa kikiendelea PSG.

“Nilikuwa mwenye furaha kwa jinsi mwaka wake ulivyokuwa lakini pia nilikuwa na huzuni kwa sababu alikuwa na upande mwingine, alikuwa mwenye furaha akiwa na Argentina akishinda mataji mengi na kwa PSG ilikuwa majanga kwake na kwangu,” alisema Neymar.


Messi na Neymar waliwahi kucheza pamoja Barcelona na kushinda mataji ya Ligi I Ufaransa lakini katika klabu hiyo walishindwa kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Messi ambaye naye alikuwa na wakati mgumu PSG aliwahi kunukuliwa akisema kwamba kwa misimu miwili aliyoichezea timu hiyo, kulikuwa na tatizo kati yake na baadhi ya mashabiki.
Neymar na Messi waliwahi kukutana na matukio ya kuzomewa na mashabiki wa PSG katika miaka yao miwili baada ya timu hiyo kutolewa kwenye fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

The post Neymar akumbuka majanga ya PSG first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/07/neymar-akumbuka-majanga-ya-psg/feed/ 0
Neymar akamilisha usajili Al Hilal https://www.greensports.co.tz/2023/08/15/neymar-akamilisha-usajili-al-hilal/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/15/neymar-akamilisha-usajili-al-hilal/#respond Tue, 15 Aug 2023 19:43:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7396 Riyadh, Saudi ArabiaMshambuliaji wa Brazil, Neymar amejiunga na klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia akitokea PSG ya Ufaransa kwa ada inayotajwa kufikia Pauni 77 milioni.Neymar katika siku za karibuni amekuwa akihusishwa na mipango ya kuihama PSG na Jumamosi aliachwa katika kikosi cha timu hiyo kilichoumana na Lorient katika mechi ya Ligi 1 na kutoka […]

The post Neymar akamilisha usajili Al Hilal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabia
Mshambuliaji wa Brazil, Neymar amejiunga na klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia akitokea PSG ya Ufaransa kwa ada inayotajwa kufikia Pauni 77 milioni.
Neymar katika siku za karibuni amekuwa akihusishwa na mipango ya kuihama PSG na Jumamosi aliachwa katika kikosi cha timu hiyo kilichoumana na Lorient katika mechi ya Ligi 1 na kutoka sare ya bao 1-1.
Inaaminika kwamba Neymar mwenye umri wa miaka 31, amechukua uamuzi wa kuachana na PSG baada ya kufahamu kwamba hakuwa katika mipango ya baadaye ya kocha mpya wa timu hiyo, Luis Enrique.
PSG pia inaaminika kuwa katika mkakati wa kuachana na wachezaji wenye majina makubwa na waliosajiliwa kwa bei mbaya, lengo likiwa ni kupunguza gharama kubwa za mishahara.
Hivi karibuni nyota mwingine wa bei mbaya aliyekuwa akiichezea PSG, Lionel Messi aliachana na timu hyo na kutimkia nchini Marekani akiendelea kucheza soka nchini humo.
“Nipo hapa Saudi Arabia, mimi ni wa Hilali,” alisema Neymar katika picha ya video iliyoonekana kwenye mitandao ya kijamii ya klabu hiyo.
Habari zaidi zinadai kwamba akiwa Saudi Arabia na klabu hiyo, Neymar atakuwa akilipwa kiasi cha Pauni 129.2 milioni kwa mwaka, fedha ambazo ni karibu mara sita ya kiasi alichokuwa akilipwa PSG.

“Wakati wote ni vigumu kuagana na mchezaji wa kipekee kama Neymar, mmoja wa wachezaji mahiri duniani, sitosahau siku aliyowasili PSG na kile alichochangia katika klabu na mradi wetu kwa miaka sita iliyopita,” alisema rais na mtendaji mkuu wa PSG, Nasser Al-Khelaifi.


Neymar ambaye amekuwa akiandamwa na maumivu ya enka mara kwa mara, hadi anaondoka PSG ameichezea timu hiyo mara 173 na kuisaidia kubeba mataji 13 yakiwamo matano ya Ligi 1 pamoja na kuiwezesha kufikia fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2020.

The post Neymar akamilisha usajili Al Hilal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/15/neymar-akamilisha-usajili-al-hilal/feed/ 0