Nabi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 24 Jun 2023 19:33:56 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Nabi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Gamondi amrithi Nabi Yanga https://www.greensports.co.tz/2023/06/24/gamondi-amrithi-nabi-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/24/gamondi-amrithi-nabi-yanga/#respond Sat, 24 Jun 2023 19:33:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6710 Na mwandishi wetuHatimaye Yanga imetegua kitendawili cha kocha mpya wa timu hiyo baada ya kumtangaza Miguel Angel Gamondi (pichani) kuwa kocha wao mkuu mpya akirithi mikoba ya Nasreddine Nabi.Uamuzi wa kumtangaza Gamondi ikiwa ni siku chache zimepita tangu kuachana na Nabi ambaye baada ya kumaliza mkataba wake hakuwa tayari kuongeza mkataba mwingine.Yanga imemtangaza Gamondi leo […]

The post Gamondi amrithi Nabi Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Hatimaye Yanga imetegua kitendawili cha kocha mpya wa timu hiyo baada ya kumtangaza Miguel Angel Gamondi (pichani) kuwa kocha wao mkuu mpya akirithi mikoba ya Nasreddine Nabi.
Uamuzi wa kumtangaza Gamondi ikiwa ni siku chache zimepita tangu kuachana na Nabi ambaye baada ya kumaliza mkataba wake hakuwa tayari kuongeza mkataba mwingine.
Yanga imemtangaza Gamondi leo Jumamosi ilipokuwa ikiendelea na mkutano wake mkuu unaofanyika kwenye Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe wakati akimtambulisha kocha huyo alisema wamemchukua wakifahamu ni kocha atakayewapeleka mbali kwenye michuano ya klabu Afrika kulingana na wasifu alionao na uzoefu wake soka la Afrika akifundisha kwenye timu mbalimbali.
Gamondi raia wa Argentina amewahi kuinoa timu ya taifa ya Burkina Faso, klabu za Esperance ya Tunisia, Asec Mimosas, USM Alger, Mamelodi Sundowns aliyoipa ubingwa wa Ligi Kuu Afrika Kusini msimu wa 2005-06.
Kocha huyo pia amewahi kuinoa klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco aliyoipeleka nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2020-21.
Duru mbalimbali za michezo zinafafanua kuwa kocha huyo anayeelezwa kupata elimu yake ya ukocha nchini Hispania, Ufaransa, England na Afrika ni mpenzi wa mfumo wa 4-2-3-1 akitumia viungo wengi katikati ya uwanja akipendelea zaidi soka la pasi na kuvutia.

The post Gamondi amrithi Nabi Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/24/gamondi-amrithi-nabi-yanga/feed/ 0
Nabi aalikwa Wiki ya Mwananchi https://www.greensports.co.tz/2023/06/20/nabi-aalikwa-wiki-ya-mwananchi/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/20/nabi-aalikwa-wiki-ya-mwananchi/#respond Tue, 20 Jun 2023 20:58:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6666 Na mwandishi wetuUongozi wa klabu ya Yanga, umemwalika kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi ambaye anatajwa kutimkia Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.Kwa sasa uongozi wa timu hiyo upo katika mchakato wa kusaka mbadala wa Nabi pamoja na kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye michuano […]

The post Nabi aalikwa Wiki ya Mwananchi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Uongozi wa klabu ya Yanga, umemwalika kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi ambaye anatajwa kutimkia Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
Kwa sasa uongozi wa timu hiyo upo katika mchakato wa kusaka mbadala wa Nabi pamoja na kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye michuano ya ndani na ile ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
Rais wa Yanga, Hersi Said alieleza kuwa wameamua kumpa Nabi mwaliko huo kutokana na utaratibu wao wa kuishi kwa upendo na watumishi wao pamoja na mafanikio aliyowapa katika kipindi chote cha misimu miwili na nusu alichokuwa Yanga.
“Huu ni mwaliko maalumu ambao umetoka kwa mfadhili wetu, Ghalib Said na hiyo ni kutokana na kuthamini mchango wake na mafanikio aliyoipa timu yetu na itakuwa fursa pekee kuagana na mashabiki na wanachama ambao walimpenda kutoka moyoni,” alisema Hersi.
Pia inaelezwa kuwa Nabi amekubali mwaliko huo na atahudhuria sherehe hiyo ambayo hutumika kutambulisha wachezaji na benchi la ufundi kuelekea msimu unaofuata.
Hersi alieleza kuwa wanajivunia mahusiano mazuri waliyokuwa nayo na kocha huyo ambaye kitendo chake cha kuifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kimeifanya timu hiyo kujulikana zaidi Afrika nzima.
Nabi bado yuko jijini Dar es Salaam na leo Jumanne majira ya saa sita za mchana alionekana katikati ya jiji barabara ya Azikiwe akiwa kwenye pikipiki.

The post Nabi aalikwa Wiki ya Mwananchi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/20/nabi-aalikwa-wiki-ya-mwananchi/feed/ 0
Nabi kuondoka na nani Yanga? https://www.greensports.co.tz/2023/06/18/nabi-kuondoka-na-nani-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/18/nabi-kuondoka-na-nani-yanga/#respond Sun, 18 Jun 2023 08:18:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6632 Na Hassan KinguKocha Nasreddine Nabi ameondoka Yanga, huko anakokwenda iwe Kaizer Chiefs au kwingineko moja ya swali atakaloulizwa ni mahitaji yake kuanzia wachezaji anamtaka nani pamoja na benchi la ufundi.Na ingawa zimekuwapo habari kwamba hatochukua mchezaji yeyote katika klabu ya Yanga, uongozi Yanga haupaswi kubweteka badala yake ujiandae kwa lolote.Upo uwezekano, tena mkubwa tu wa […]

The post Nabi kuondoka na nani Yanga? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Hassan Kingu
Kocha Nasreddine Nabi ameondoka Yanga, huko anakokwenda iwe Kaizer Chiefs au kwingineko moja ya swali atakaloulizwa ni mahitaji yake kuanzia wachezaji anamtaka nani pamoja na benchi la ufundi.
Na ingawa zimekuwapo habari kwamba hatochukua mchezaji yeyote katika klabu ya Yanga, uongozi Yanga haupaswi kubweteka badala yake ujiandae kwa lolote.
Upo uwezekano, tena mkubwa tu wa kuwapoteza baadhi ya mastaa wake au sehemu kubwa ya wasaidizi wake katika benchi la ufundi la Yanga wakalazimika kuondoka na kocha huyo huko aendako.
Katika benchi la ufundi mhanga wa kwanza anaweza kuwa Cedric Kaze, katika kipindi chote ambacho Nabi amedumu Yanga kuanzia Aprili 2021 hadi Juni 2023, Kaze amekuwa mmoja wa wasaidizi wake muhimu.
Hatujui umuhimu wa Kaze kwa Nabi, anayejua ni Nabi mwenyewe na ndio maana wamekuwa pamoja katika safari ya mafanikio ya Yanga hadi kufikia hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kubeba mataji kadhaa nchini,


Kwa hali hiyo tusishangae akaamua kufuatana naye huko anakokwenda, kwa maana nyingine Yanga wasijiaminishe kwa asilimia 100 kwamba Kaze hawezi kuondoka.
Hadithi ya Kaze inaweza kufanana ya Charles Boniface Mkwassa akiwa Yanga kama msaidizi wa Hans Pluijm, kocha huyo alipopata nafasi ya kuinoa timu moja ya Saudi Arabia aliondoka na Mkwasa na ingawa mambo hayakuwa mazuri lakini Pluijm alionesha ni kwa kiasi gani Mkwasa alikuwa mshauri mzuri kwake hivyo tusishangae jambo kama hilo kutokea kwa Kaze na Nabi.
Na kwa Yanga si Kaze peke yake bali Nabi anaweza kuondoka na watu wengine katika benchi la ufundi kuanzia wataalamu wa viungo na wengineo ambao ataona umuhimu wao kwake.

Djigui Diarra

Kwa upande wa wachezaji hapa ndipo kuna mengi, kila mchezaji anataka maslahi, anataka changamoto mpya, anataka fursa ya kuonekana katika ligi ambazo zitamfungulia njia ya kwenda kucheza soka barani Ulaya.
Na hapa bila kupepesa Yanga wasishangae wakipoteza wachezaji wao muhimu, kipa Djigui Diarra, huyu ni namba moja, amedhihirisha uwezo wake si tu katika ligi kwa kubeba tuzo ya kipa bora lakini hata kwenye michuano ya klabu Afrika.
Diarra amekuwa nyota wa mchezo katika mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya USM Alger na Yanga, amekuwa nguzo muhimu katika safari ya mafanikio ya Yanga katika misimu miwili.
Kilicho wazi ni kwamba hakuna timu au kocha ambaye hapendi kuwa na kipa wa aina ya Diarra. Yanga ijiandae kwa lolote.

Fiston Mayele
Huyu naye ni mchezaji mwingine aliyedhihirisha umahiri na ubora wake, Afrika inatambua ubora wake, ameibuka kinara wa mabao katika Ligi Kuu NBC lakini pia ndiye kinara wa mabao katika Kombe la Shirikisho Afrika.
Yote haya yanamfanya Fiston Mayele kuwa hazina muhimu ya Yanga kwa ajili ya msimu ujao lakini hapo hapo kuna ukweli kwamba zipo klabu nyingine zinazomtaka, haitoshangaza Nabi akaungana naye huko anapokwenda.
Kwa Mayele tayari zimekuwapo fununu kwa muda mrefu sasa kwamba anatakiwa Arabuni na hata Afrika Kusini hivyo haitokuwa ajabu akiondoka na kuacha maumivu Yanga kwani ubora wake ni jambo lililo dhahiri.

Yannick Bangala
Amekuwa na tatizo, kuna wakati hawi katika ubora wake lakini jambo hilo haliwezi kuondoa ukweli kwamba Yannick Bangala ni mmoja wa wachezaji muhimu ndani ya Yanga na ndio maana amekuwa mara kwa mara yumo kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.


Anayemjua vizuri mchezaji huyo ni Nabi, anajua umuhimu wake na anajua nini cha kufanya ili ayaone matunda ya ubora wa Bangala na kukabiliana na tatizo la kushuka ubora ambalo kuna wakati humtokea.
Na japo Bangala hapewi nafasi kubwa sana ya kuondoka Yanga lakini mabosi wa klabu hiyo wajiandae lolote linaweza kutokea kwani kama nilivyosema awali kwamba anayeujua vizuri ubora na udhaifu wa Bangala ni Nabi na anajua nini cha kufanya kwa mchezaji huyo.

Kennedy Musonda
Mfungaji wa bao lililoipa Yanga taji la FA (ASFC) naye ni mtu mwingine muhimu katika kikosi cha Yanga, amekuwa katika ubora ambao umeibeba klabu mara kadhaa, na ndio maana ni mmoja wa wachezaji muhimu katika kikosi cha kwanza cha Yanga.

Musonda ana kila kitu cha kumfanya amudu kucheza kwenye ligi yoyote ya soka barani Afrika na ndio maana yupo Tanzania akiwa mmoja wa wachezaji kutoka nje ya mipaka ya Tanzania.
Nabi anaujua umuhimu wa Musonda lakini Nabi ameondoka Yanga hivyo hiyo haitokuwa ajabu akiungana na mchezaji huyo huko aendako.

Mudathir, Sure Boy
Mafundi hawa wawili Salum Aboubakar ‘Sure Boy na Mudathir Yahya, wanahitaji pongezi, wote walikuwa Azam lakini tangu watue Yanga wameweza kuteka hisia za mashabiki si tu wa timu hiyo bali wadau wa soka kwa ujumla.
Kwanza wameweza kupenya katika kikosi cha kwanza chenye timu iliyosheheni mastaa kutoka sehemu mbalimbali Afrika, hili ni jambo linalohitaji pongezi, si wachezaji wengi wa Kibongo wenye uwezo huo.
Kitendo cha Nabi kuwa tayari kuwachukua wachezaji ambao walionekana kama kususwa na kutopewa umuhimu katika timu nyingine kinafikirisha, katika hali ya kawaida mtu anaweza kujiuliza unachukuaje mchezaji asiyehitajika anakotoka.
Kocha Nabi aliyajua tusiyoyajua wengi kwa Mudathir na Sure Boy na hilo limejionesha kwa namna ambavyo amekuwa akiwatumia katika kikosi chake, ni kati ya wachezaji ambao umuhimu wao Yanga ni jambo lililo wazi.
Jambo zuri kwa Sure Boy na Mudathir ni kwamba wakianza kipindi cha kwanza utaona umuhimu wao na hata wakiingia kutokea benchi utaliona jambo hilo. Nani atashangaa mmoja wao au wote wakiungana na Nabi huko aendako?

Fei Toto
Maumivu ambayo huenda yakawakuta Yanga kwa wachezaji wao kumfuata Nabi, Azam nao wajiandae, wanaweza wasiwe salama, Feisal Salum au Fei Toto ni mtu mwingine aliyekuwa muhimu mno katika kikosi cha Nabi Yanga.


Ile hadithi ya No Fei No Problem (Hakuna Fei hakuna tatizo) ni mazungumzo tu ya kujifariji, ukweli ni kwamba Fei Toto alikuwa mchezaji muhimu na aliyehitajika katika kikosi cha Yanga.
Alikuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza Yanga chini ya kocha Nabi, na ndio maana kutokana na ubora wake Yanga waliumia mno aliposusa Desemba mwaka jana na pengine baadhi yao bado wana hasira kwa kitendo hicho hata baada ya mchezaji huyo kuhamia rasmi Azam FC.
Nabi akipata fursa ya kumsajili Fei au akiwa na uhitaji wa mchezaji katika eneo analochezea Fei, mmoja wa wachezaji ambao atawaingiza katika hesabu za kuwasajili ni Fei, hatoona tabu kumchukua mchezaji huyo na kuungana naye kwa mara nyinngine.
Nimewataja wachezaji wachache lakini kimsingi klabu ya Yanga au hata Simba zijiandae kwa lolote, zinaweza kupoteza baadhi ya wachezaji wao muhimu kuungana na Nabi huko aendako kwani anaijua ligi ya Tanzania na anawajua mastaa wenye uwezo.
Takwimu zinazoibeba ligi ya Tanzania na kuitaja kuwa ni ligi bora namba tano Afrika zinamaansha kwamba katika ligi hiyo kuna wachezaji bora ambao pia wanahitajika kwingineko.

The post Nabi kuondoka na nani Yanga? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/18/nabi-kuondoka-na-nani-yanga/feed/ 0
Nabi asikitika kuondoka Yanga https://www.greensports.co.tz/2023/06/16/nabi-asikitika-kuondoka-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/16/nabi-asikitika-kuondoka-yanga/#respond Fri, 16 Jun 2023 13:48:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6630 Na mwandishi wetuAliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi ameeleza huzuni yake kuondoka katika klabu hiyo, akisema hakufanya maamuzi hayo kwa ajili ya fungu la pesa alilowekewa na klabu anayojiunga nayo.Juzi Jumatano, Yanga ilitangaza kuachana na Nabi raia wa Tunisia baada ya kocha huyo kutotaka kuongeza mkataba na kuhitaji changamoto mpya.Nabi ambaye anahusishwa kuhamia Kaizer […]

The post Nabi asikitika kuondoka Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Nasreddine Nabi

Na mwandishi wetu
Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi ameeleza huzuni yake kuondoka katika klabu hiyo, akisema hakufanya maamuzi hayo kwa ajili ya fungu la pesa alilowekewa na klabu anayojiunga nayo.
Juzi Jumatano, Yanga ilitangaza kuachana na Nabi raia wa Tunisia baada ya kocha huyo kutotaka kuongeza mkataba na kuhitaji changamoto mpya.
Nabi ambaye anahusishwa kuhamia Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ameandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, akieleza pia namna gani anamshukuru mfadhili wa Yanga, Ghalib Said, wachezaji, benchi la ufundi, mashabiki kwa ushirikiano waliompa tangu ametua Yanga.
“Ni jambo gumu zaidi nimelazimika kufanya katika miaka miwili iliyopita, lakini mambo yote mazuri lazima yafike mwisho. Tulipitia mihemko yote pamoja, huzuni, furaha, wakati mwingine hasira, lakini kwa neema ya Mungu tuliishi nyakati zisizosahaulika,” aliandika Nabi.
Kocha huyo ameshukuru pia kufanikisha mengi ambayo wengi hawakutarajia kutoka kwake wakati anatua Yanga miaka miwili na nusu iliyopita lakini kwa walipofikia, anawashukuru mno wachezaji wake ambao aliwachukulia kama watoto wake na kufanikisha mafanikio waliyoyapata mpaka sasa.
Pia, amewashukuru kamati ya utendaji, watendaji wenzake wa benchi la ufundi akibainisha bila wao hakuna ambacho kingewezekana huku akibainisha namna anavyowapenda mashabiki wa Yanga kwa nguvu na ujasiri waliompa wakati wote.
“Hatimaye, mashabiki, hakuna maneno yanayoweza kuelezea kiwango cha upendo nilichonacho kwenu na nguvu zote mlizonipa. Naumia moyoni kuachana nanyi, lakini ndivyo maisha ya ukocha yalivyo.

“Ningependa kuwaambia, haijawahi kuwa juu ya pesa, na kwamba muumini mzuri anajua kuwa pesa tunayopata katika maisha yetu tayari imepangwa kwa ajili yetu na kwamba kupata pesa hizo leo au kesho haitabadilika. Kwaheri familia yangu, nitawakumbuka sana. Nawapenda wote,” aliandika Nabi.


Nabi aliyetua Yanga akitokea Al Merrikh ya Sudan, anaondoka akiwa ameipa Yanga mataji mawili ya Ligi Kuu Bara, mataji mawili ya Kombe la FA, mataji mawili ya Ngao ya Jamii na kuifikisha Yanga kwa mara ya kwanza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.

The post Nabi asikitika kuondoka Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/16/nabi-asikitika-kuondoka-yanga/feed/ 0
Nabi aondoka Yanga https://www.greensports.co.tz/2023/06/15/nabi-aondoka-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/15/nabi-aondoka-yanga/#respond Thu, 15 Jun 2023 05:53:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6599 Na mwandishi wetuKocha Nasreddine Nabi hatimaye ameamua kuachana na klabu ya Yanga huku kukiwa na habari kwamba anaenda kujiunga na klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.Uamuzi huo wa Nabi unakuwa umefuta mjadala uliotawala siku za hivi karibuni miongoni mwa wadau wa soka kuhusu majaliwa ya kocha huyo kama angeongeza mkataba au angeamua kuondoka.Awali Jumtano […]

The post Nabi aondoka Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Nasreddine Nabi hatimaye ameamua kuachana na klabu ya Yanga huku kukiwa na habari kwamba anaenda kujiunga na klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
Uamuzi huo wa Nabi unakuwa umefuta mjadala uliotawala siku za hivi karibuni miongoni mwa wadau wa soka kuhusu majaliwa ya kocha huyo kama angeongeza mkataba au angeamua kuondoka.
Awali Jumtano hii, GreenSports ilimnukuu Makamu Rais wa Yanga, Arafat Haji akisema kwamba walitarajia kukutana na kocha huyo Alhamisi ili kujadili suala la kumuongezea mkataba.
Hata hivyo saa kadhaa baada ya kauli ya kiongozi huyo, uongozi wa Yanga kupitia Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo ulitoa taarifa rasmi ya kuagana na kocha huyo.
Taarifa hiyo ilidai kuwa uongozi wa Yanga umefikia makubaliano ya kuachana na Nabi baada ya kocha huyo mwenyewe kuomba kutoongeza mkataba na klabu hiyo.
Mkataba wa Nabi pamoja na sehemu kubwa ya jopo lake kwenye benchi la ufundi umefikia ukomo mwishoni mwa msimu huu na awali yalikuwapo matarajio makubwa kwa kocha huyo kuongeza mkataba.
Uongozi wa Yanga umemshukuru kocha huyo kwa kipindi chote ambacho amekuwa na timu hiyo ba kumtakia heri katika majukumu yake mapya ingawa haijaeleweka kuhusu wajumbe wengine wa benchi la ufundi waliokuwa wakisaidiana na kocha huyo.
Nabi ataendelea kukumbukwa katika klabu ya Yanga kwa kuiwezesha timu hiyo kubeba mataji mawili ya Ligi Kuu NBC, mawili ya Kombe la FA (ASFC) pamoja na mataji mawili ya Ngao ya Jamii.
Kocha huyo pia ataendelea kukumbukwa kwa kuweka rekodi ya kuifikisha kwa mara ya kwanza timu hiyo katika hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na ingawa hakujawa na taarifa rasmi za kocha huyo kwenda Kaizer Chiefs, duru za kimichezo katika siku za karibuni zimeripoti kuwa klabu hiyo imekuwa ikimuwinda Nabi kutokana na mafanikio ambayo ameyapata akiwa Yanga.

The post Nabi aondoka Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/15/nabi-aondoka-yanga/feed/ 0
Mikataba ya Nabi, Kaze kujadiliwa https://www.greensports.co.tz/2023/06/14/mikataba-ya-nabi-kaze-kujadiliwa/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/14/mikataba-ya-nabi-kaze-kujadiliwa/#respond Wed, 14 Jun 2023 15:00:19 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6594 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi na msaidizi wake Cedric Kaze kesho Alhamisi wanatarajia kukutana na uongozi wa timu hiyo kuendeleza mazungumzo ya kusaini mkataba mpya wa kukinoa kikosi hicho msimu ujao.Mikataba ya makocha hao na wengine wa benchi la ufundi imemalizika baada ya mchezo wa fainali wa Kombe la FA (ASFC) juzi […]

The post Mikataba ya Nabi, Kaze kujadiliwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi na msaidizi wake Cedric Kaze kesho Alhamisi wanatarajia kukutana na uongozi wa timu hiyo kuendeleza mazungumzo ya kusaini mkataba mpya wa kukinoa kikosi hicho msimu ujao.
Mikataba ya makocha hao na wengine wa benchi la ufundi imemalizika baada ya mchezo wa fainali wa Kombe la FA (ASFC) juzi mkoani Tanga ambapo Yanga ilibeba taji hilo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC.
Makamu Rais wa Yanga, Arafat Haji alieleza kuwa dhamira yao kubwa ni kuhakikisha wanawabakisha makocha hao kwa kuwaboreshea maslahi yao ili kuendeleza mafanikio ambayo wameyapata msimu huu.

“Tutakuwa viongozi wa ajabu kama tutawaacha makocha hawa waliotupa mafanikio kuondoka, tumeandaa ofa nono kwa ajili yao ikiwemo kuwapa mikataba mirefu ili tuendeleze mazuri waliyotupa msimu huu,” alisema Arafat.


Kiongozi huyo alieleza kuwa kabla ya msimu kuisha tayari walishaanza kuzungumza na makocha hao kuhusu kuongeza mkataba na mazungumzo yao yalifikia sehemu nzuri hivyo anaamini baada ya kikao cha kesho, mustakabali wa benchi la ufundi utajulikana.
Haji pia alisema kwamba katika kikao hicho wanatarajia kupokea ripoti nzima ya msimu uliopita pamoja na maboresho ya kikosi chao cha msimu unaokuja wa 2023/24.
Alifafanua kuwa dhamira yao ni kuhakikisha wanawabakisha kundini nyota wote pia walioisaidia timu yao kupata mafanikio waliyokuwa nayo na kusajili wachezaji wachache kwa ajili ya kuimarisha sehemu zilizokuwa na udhaifu.
Baadhi ya wachezaji ambao wanatajwa kusajiliwa na Yanga kwenye dirisha kubwa ni mshambuliaji Ranga Chivaviro kutoka Marumo Gallants ya Afrika Kusini na winga wa TP Mazembe ya DR Congo, Philipe Kinzumbi.

The post Mikataba ya Nabi, Kaze kujadiliwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/14/mikataba-ya-nabi-kaze-kujadiliwa/feed/ 0
Kiwango Yanga hakijamridhisha Nabi https://www.greensports.co.tz/2023/05/11/kiwango-yanga-hakijamridhisha-nabi/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/11/kiwango-yanga-hakijamridhisha-nabi/#respond Thu, 11 May 2023 13:09:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6117 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema licha ya timu yake kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini, hajaridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake katika mchezo huo.Mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ulichezwa jana Jumatano jioni kwenye […]

The post Kiwango Yanga hakijamridhisha Nabi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema licha ya timu yake kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini, hajaridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake katika mchezo huo.
Mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ulichezwa jana Jumatano jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Nabi alisema anasikitika kwa kuwa walitengeneza nafasi nyingi kipindi cha kwanza cha mchezo huo lakini walishindwa kuzitumia ipasavyo tofauti na alivyotarajia.

“Mechi ilikuwa ngumu, kipindi cha kwanza tulitengeneza nafasi nyingi hatukupata magoli. Ninachosikitika hatukutumia nafasi kama nilivyowafundisha wachezaji wangu kwenye mazoezi, walicheza tofauti kabisa,”alisema Nabi.


Kuhusu Marumo, Nabi alisema: “Siwezi kusema ni timu dhaifu, tofauti kidogo ipo kwenye safu yao ya ulinzi ila ni wazuri wana timu nzuri, timu yangu ndio iliyokuwa na matatizo kwa sababu wachezaji wangu hawakucheza vizuri.”
Alisema katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Mei 17, mwaka huu Afrika Kusini kila mchezaji anatakiwa kufahamu wajibu wake kwa kufanya kazi kama alivyoelekezwa kwani kazi bado haijaisha.
Kwa upande wa Kocha wa Marumo, Dylan Kerr alisema anasikitika kwa timu yake kushindwa kuzitumia nafasi nne walizotengeneza kipindi cha kwanza licha ya kumiliki mpira.
“Tulipata nafasi nne za kufunga, tulimiliki mpira lakini umaliziaji wetu haukuwa bora, tunapaswa kwenda kurekebisha makosa yetu na kujipanga kwa mchezo wa pili,” alisema.

The post Kiwango Yanga hakijamridhisha Nabi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/11/kiwango-yanga-hakijamridhisha-nabi/feed/ 0
Nabi: Tutaikabili Marumo kwa tahadhari https://www.greensports.co.tz/2023/05/09/nabi-tutaikabili-marumo-kwa-tahadhari/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/09/nabi-tutaikabili-marumo-kwa-tahadhari/#respond Tue, 09 May 2023 17:15:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6070 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kipo kamili, kina ari na watacheza kwa tahadhari mechi ya kesho Jumatano ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini.Nabi amezungumza hayo leo Jumanne jijini Dar es Salaam akisema pia wanaingia kwenye mechi hiyo wakifahamu ubora wa […]

The post Nabi: Tutaikabili Marumo kwa tahadhari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kipo kamili, kina ari na watacheza kwa tahadhari mechi ya kesho Jumatano ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini.
Nabi amezungumza hayo leo Jumanne jijini Dar es Salaam akisema pia wanaingia kwenye mechi hiyo wakifahamu ubora wa Marumo mpaka wanafika nusu fainali bila ya kutazama hali mbaya waliyonayo kwenye Ligi ya Afrika Kusini.
Alisema kuelekea mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.00 jioni, amewasoma wapinzani wao hivyo wanaingia na tahadhari zote katika mtanange huo.
“Wachezaji wote wana utimamu wa mechi ya kesho, maandalizi yamekwenda kama tulivyopanga, wachezaji wamejiandaa kikamilifu, tumeisoma timu pinzani, wachezaji wako tayari kupambana na wana ari ya kucheza na Marumo.

“Niwapongeze Marumo ni timu nzuri japo kwenye ligi yao hawafanyi vizuri lakini kwenye michuano hii wanafanya vizuri, kila mechi wamepata bao na wameitoa Pyramids, hivyo hiyo si timu ya kubeza, tutacheza kwa umakini mkubwa kulingana na wapinzani tunaokutana nao ukizingatia ni mechi za mikondo miwili, nyumbani na ugenini,” alisema Nabi.


Nabi raia wa Tunisia pia aliwashukuru mashabiki wa Yanga kwa ushirikiano waliowapa mpaka sasa, akiwataka kuongeza nguvu hiyo kesho kwa kushangilia na kuwapa nguvu wachezaji hata inapotokea Yanga haina mpira kwa wakati huo.
Naye Raymond Mdaka, kocha msadizi wa Marumo alisema hawawezi kuzungumzia maandalizi yao kwa undani kwa sababu ni sehemu yao ya kazi ya kila siku kutokana na mechi za michuano hiyo na za ligi walizonazo kila wakati ingawa wamewasoma Yanga kuelekea mechi hiyo.
“Tumekuwa tukifanya maandalizi kila baada ya mechi moja kuelekea nyingine, tunachojua timu zina utofauti na huwezi kubadili kucheza kila mechi iliyo mbele lakini kuna vitu tumeangalia kama ugumu wao, namna wanavyocheza hivyo hakukuwa na maandalizi makubwa japo tupo tayari kwa kila mchezo ulio mbele yetu,” alisema Mdaka.
Timu hizo zinashuka dimbani zikiwa na uwiano tofauti kwenye ligi zao ambapo Yanga ni kinara wa Ligi Kuu NBC kwa pointi 71 wakati Marumo ipo nafasi ya 14 kwa pointi 29.
Marumo ambayo imeifunga Pyramids ya Misri jumla ya mabao 2-1 kwenye robo fainali ya Kombe la Shirikisho, kwenye michezo yao mitano ya mwisho ya ligi wameshinda mmoja, wakidroo mitatu na kufungwa mmoja.
Yanga wao ambao wamefungwa mechi moja kwenye mechi tano za ligi zilizopita na kushinda nne, iliiondosha Rivers United ya Nigeria kwa jumla ya mabao 2-0 na kutinga nusu fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza kama ilivyo Marumo.

The post Nabi: Tutaikabili Marumo kwa tahadhari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/09/nabi-tutaikabili-marumo-kwa-tahadhari/feed/ 0
Nabi atoa angalizo Dar Derby https://www.greensports.co.tz/2023/04/13/nabi-atoa-angalizo-dar-derby/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/13/nabi-atoa-angalizo-dar-derby/#respond Thu, 13 Apr 2023 20:09:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5797 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ametoa angalizo kabla ya mechi yao na Simba akiwataka ka wachezaji wake kuwa makini zaidi kwenye mchezo huo kwani ndio ulioshikilia ubingwa wao msimu huu.Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu NBC kwa sasa wapo kwenye maandalizi ya mchezo huo maarufu Dar Derby au Kariakoo Derby unaosubiriwa kwa […]

The post Nabi atoa angalizo Dar Derby first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ametoa angalizo kabla ya mechi yao na Simba akiwataka ka wachezaji wake kuwa makini zaidi kwenye mchezo huo kwani ndio ulioshikilia ubingwa wao msimu huu.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu NBC kwa sasa wapo kwenye maandalizi ya mchezo huo maarufu Dar Derby au Kariakoo Derby unaosubiriwa kwa hamu utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Jumapili hii.
Yanga itakuwa wageni wa Simba ingawa rekodi zinaonesha kuwa katika siku za karibuni imekuwa ikipata matokeo mazuri mbele ya Simba ambayo nayo kwa sasa imeimarika kwa kiasi kikubwa.
Katika kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo, Nabi amefuta mapumziko na sasa wapo kambini kuendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo ambao umeshikilia hatima ya ubingwa wao kwa msimu huu.

“Ni mchezo mgumu wenye hadhi ya fainali sababu tukishinda tutakuwa na asilimia 85 ya kuwa mabingwa, nimewaeleza wachezaji wangu umuhimu wa ushindi na kuwataka kuzingatia kila tunachofanya mazoezini sababu hii ni mechi ya ubingwa,” alisema Nabi.


Kocha huyo ambaye amekipeleka kikosi cha Yanga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ameeleza kuwa anajua mchezo huo utakuwa mgumu na wenye ushindani mkali kutokana na ubora wa kikosi cha Simba lakini ni lazima wapambane kuthibitisha kuwa wao ni bora.
Alisema anajua Simba wataingia kwa lengo la kutafuta ushindi ili kupunguza pengo la pointi nane lililopo kwa sasa lakini zipo mbinu mbadala ambazo amewapa wachezaji wake kwa ajili ya kuzifanyia kazi na kumpa pointi zote tatu kwenye mchezo huo.
Timu hizo zitaingia dimbani, Yanga ikiwa kileleni kwa pointi 68 dhidi ya Simba wanaoshika nafasi ya pili kwa pointi 60 huku zikiwa zimesalia mechi tano kabla ya kufungwa rasmi kwa pazia la ligi msimu huu.

The post Nabi atoa angalizo Dar Derby first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/13/nabi-atoa-angalizo-dar-derby/feed/ 0
Metacha apania kumshawishi Nabi https://www.greensports.co.tz/2023/03/29/metacha-apania-kumshawishi-nabi/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/29/metacha-apania-kumshawishi-nabi/#respond Wed, 29 Mar 2023 20:08:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5629 Na mwandishi wetuKipa namba mbili wa Yanga, Metacha Mnata (pichani) amesema atatumia mchezo wa TP Mazembe kumshawishi kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi kumpanga kikosi cha kwanza.Kipa namba moja wa timu hiyo, Djigui Diarra ataukosa mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mazembe utakaopigwa Aprili 2, mwaka […]

The post Metacha apania kumshawishi Nabi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kipa namba mbili wa Yanga, Metacha Mnata (pichani) amesema atatumia mchezo wa TP Mazembe kumshawishi kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi kumpanga kikosi cha kwanza.
Kipa namba moja wa timu hiyo, Djigui Diarra ataukosa mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mazembe utakaopigwa Aprili 2, mwaka huu mjini Lubumbashi.
Kipa huyo ameeleza kuwa tangu arejee kwa mkopo katika kikosi hicho kwenye dirisha dogo msimu huu, amejifunza mengi kutoka kwa Diarra hivyo anaamini yupo tayari kuidakia timu yake katika mchezo huo wa Kombe la Shirikisho na kuonesha kiwango kikubwa.

“Najua kocha nini anataka nifanye lakini natambua timu yangu inahitaji nini katika mchezo huo kwa hiyo nipo tayari, ukizingatia uzoefu wa kucheza mechi hizi za kimataifa ninao na sina presha,” alisema Metacha.


Kipa huyo ameeleza kuwa si kitu rahisi kucheza na Mazembe wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani bila kuruhusu bao lakini kwake atapambana kwa kushirikiana na wachezaji wenzake ili asiruhusu bao.
Alisema endapo hilo litafanikiwa anaamini atafanikiwa kubadilisha mawazo ya kocha wake na ataanza kumtumia kwenye kikosi cha kwanza kama ilivyokuwa kabla hajatimka kwenye timu hiyo misimu miwili iliyopita na kutua Polisi Tanzania.
Metacha ambaye anacheza kwa mkopo wa miezi sita akitokea Singida Big Stars, amesema matumaini yake ni kuendelea kubaki kwenye kikosi cha miamba hiyo ya soka nchini kwa uongozi kumpa mkataba wa kudumu.

The post Metacha apania kumshawishi Nabi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/29/metacha-apania-kumshawishi-nabi/feed/ 0