Mwinyi Zahera - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 04 May 2024 19:11:51 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mwinyi Zahera - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mabao 4-1 hayamuumi Zahera https://www.greensports.co.tz/2024/05/04/kipigo-cha-4-1-hakijamuumiza-zahera/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/04/kipigo-cha-4-1-hakijamuumiza-zahera/#respond Sat, 04 May 2024 18:51:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10837 Na mwandishi wetuBaada ya kuchapwa mabao 4-1 na Azam FC jana Ijumaa, kocha mkuu wa Namungo FC, Mwinyi Zahera amesema haumii na matokeo hayo kwani yalisababishwa na makosa ya kibinadamu ya mchezaji mmoja mmoja.Namungo ilipokea kipigo hicho katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho CRDB (FA) uliopigwa kwenye Uwanja […]

The post Mabao 4-1 hayamuumi Zahera first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Baada ya kuchapwa mabao 4-1 na Azam FC jana Ijumaa, kocha mkuu wa Namungo FC, Mwinyi Zahera amesema haumii na matokeo hayo kwani yalisababishwa na makosa ya kibinadamu ya mchezaji mmoja mmoja.
Namungo ilipokea kipigo hicho katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho CRDB (FA) uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Zahera alisema timu yake ilikuwa ikicheza vizuri, inafunguka na inafika kwenye lango la wapinzani lakini makosa madogo ya kibinadamu ndio yamewagharimu na yeye hilo halimuumizi sababu timu haikushindwa kupitia mipango yake.
“Nafikiri mpaka dakika ya 20 walikuwa (Azam) wanaongoza mabao matatu, na magoli yenyewe ukiangalia si magoli ya kitimu, ni magoli ya kosa la kibinadamu la mtu mmoja mmoja, na makosa kama hayo yaliyotokea hakuna ambaye anapanga kwamba afanye hivyo kwenye mipango yake na hiyo ndio imetuumiza.
“Ila kingine hata kama tumefungwa lakini ukiangalia timu inacheza, inafunguka tunafika kwenye goli, kwa hiyo siwezi kulaumu wachezaji wangu sana sababu kosa ni la mtu mmoja mmoja, wakati kipa au mabeki wanataka kumtoka mtu wananyang’anywa unafungwa.

“Yale ni makosa ya mtu binafsi, hivyo hainiumizi sana kufungwa sababu kama tungefungwa nne kwa kuzidiwa zaidi kimpira mpaka unakosa cha kufanya hiyo kweli unaonekana huna unachokifanya,” alisema Zahera.

Kwa matokeo hayo, hatua inayofuata ya nusu fainali ya michuano hiyo, Azam itaumana na Coastal Union kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Mei 18 huku Yanga ikitifuana na Ihefu FC Mei 19, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

The post Mabao 4-1 hayamuumi Zahera first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/04/kipigo-cha-4-1-hakijamuumiza-zahera/feed/ 0
Zahera amtaka Mzize aondoke Yanga https://www.greensports.co.tz/2024/04/18/zahera-amtaka-mzize-aondoke-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/18/zahera-amtaka-mzize-aondoke-yanga/#respond Thu, 18 Apr 2024 19:44:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10667 Na mwandishi wetuKocha wa zamani wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema huu ni wakati sahihi wa mshambuliaji wa Clement Mzize kuihama Yanga na kutafuta changamoto kwingine ili kuimarisha kipaji na uwezo alionao.Zahera ameeleza hayo leo Alhamisi wakati kukiwa na fununu za mchezaji huyo ambaye makabrasha yake yanaonesha ana miaka 20, kuwaniwa na baadhi ya timu vigogo […]

The post Zahera amtaka Mzize aondoke Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha wa zamani wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema huu ni wakati sahihi wa mshambuliaji wa Clement Mzize kuihama Yanga na kutafuta changamoto kwingine ili kuimarisha kipaji na uwezo alionao.
Zahera ameeleza hayo leo Alhamisi wakati kukiwa na fununu za mchezaji huyo ambaye makabrasha yake yanaonesha ana miaka 20, kuwaniwa na baadhi ya timu vigogo ikiwemo Azam FC na Watford inayoshiriki Ligi ya Championship nchini England.
Zahera ambaye kwa sasa anainoa Namungo FC ameeleza: “Lazima (Mzize) aende nje ya nchi, maana hapa hawezi kuwa na muendelezo mazuri na kufanya zaidi ya sasa, sababu anazijua timu zote.
Zahera alifafanua kuwa anafahamu jinsi wanavyojifunza lakini kwa maendeleo yake lazima aende nje apate utofauti namna ya kucheza, ufundishwaji wake pia hata mbinu ni tofauti sana.

“Kwa nafasi yake anapaswa kusaidia timu kwenda mbali kama ilivyokuwa kwa Mayele (Fiston) ambaye alikuwa namba moja kwa ushambuliaji na asilimia 90 timu ilitegemea mabao yake na yeye sasa anapaswa kuwa hivyo kwa timu nyingine maana ameshakaa Yanga na bado hana uhakika wa nafasi lakini anafanya vizuri kulingana na umri wake,” alisema Zahera.


Mzize ambaye kwenye ushindi wa mwisho wa Yanga wa mabao 3-0 dhidi ya Singida FG alitoa asisti mbili, Zahera anaamini huu ni wakati wake wa kuwa mshambuliaji kiongozi wa timu kubwa.
Alisema kwamba jambo hilo litawezekana endapo Mzize atakubali kutafuta changamoto nyingine katika mataifa mengine yaliyoendelea zaidi kimiundombinu ya soka.
Mzize anayepata upinzani wa namba kutoka kwa Joseph Guede na Kennedy Musonda, licha ya kutofunga mabao mengi msimu huu lakini mpaka sasa ametoa pasi tano za mabao akizidiwa pasi tatu na kinara Kipre Junior wa Azam mwenye asisti nane.
Katika kikosi ch Yanga, Mzize anazidiwa na Stephane Aziz Ki na Kouassi Yao ambao kila mmoja ana asisti saba.

The post Zahera amtaka Mzize aondoke Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/18/zahera-amtaka-mzize-aondoke-yanga/feed/ 0
Zahera akiri Namungo kazi wanayo https://www.greensports.co.tz/2024/02/13/zahera-akiri-namungo-kazi-wanayo/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/13/zahera-akiri-namungo-kazi-wanayo/#respond Tue, 13 Feb 2024 06:06:31 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9701 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Namungo, Mwinyi Zahera amesema wana kazi ya kufanya ili kuhakikisha wanapanda kwenye nafasi za juu za msimamo wa Ligi Kuu NBC.Zahera ameeleza hayo Jumatatu hii baada ya sare yao ya bao 1-1 katika mechi yao na Tabora United iliyopigwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora akidai imevuruga mipango yake.“Malengo […]

The post Zahera akiri Namungo kazi wanayo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Namungo, Mwinyi Zahera amesema wana kazi ya kufanya ili kuhakikisha wanapanda kwenye nafasi za juu za msimamo wa Ligi Kuu NBC.
Zahera ameeleza hayo Jumatatu hii baada ya sare yao ya bao 1-1 katika mechi yao na Tabora United iliyopigwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora akidai imevuruga mipango yake.
“Malengo yetu yalikuwa pointi tatu lakini vijana wangu walizembea kidogo, wapinzani wakasawazisha, sio mbaya tunajipanga kuhakikisha tunashinda mechi zijazo ili kurudi kwenye lengo letu kuu ambalo ni kupanda nafasi za juu,” alisema Zahera.
Zahera alisema ulikuwa mchezo muhimu kwake lakini hana namna zaidi ya kukubaliana na matokeo na kurudi uwanja wa mazoezi ili kupanga mikakati mipya itakayowapa ushindi wa mechi zinazofuata.
Kwa matokeo hayo Namungo FC, sasa imefikisha pointi 18 ikiwa nafasi ya nane kwenye msimamo katika mechi 15 ilizocheza.

The post Zahera akiri Namungo kazi wanayo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/13/zahera-akiri-namungo-kazi-wanayo/feed/ 0
Zahera kuendeleza ushindi Namungo https://www.greensports.co.tz/2023/12/30/zahera-kuendeleza-ushindi-namungo/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/30/zahera-kuendeleza-ushindi-namungo/#respond Sat, 30 Dec 2023 19:53:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9078 Na mwandishi wetuKocha muu mpya wa Namungo, Mwinyi Zahera amesema kitendo cha kupewa nafasi kwenye timu hiyo inaonesha kuaminika na uongozi, hivyo ana kazi ya kuhakikisha timu inaendelea kufanya vizuri.Zahera ameyasema hayo leo Jumamosi baada ya jana kutangazwa rasmi na uongozi wa Namungo kuwa kocha mpya wa kikosi chao akichukua nafasi ya Denis Kitambi aliyetua […]

The post Zahera kuendeleza ushindi Namungo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha muu mpya wa Namungo, Mwinyi Zahera amesema kitendo cha kupewa nafasi kwenye timu hiyo inaonesha kuaminika na uongozi, hivyo ana kazi ya kuhakikisha timu inaendelea kufanya vizuri.
Zahera ameyasema hayo leo Jumamosi baada ya jana kutangazwa rasmi na uongozi wa Namungo kuwa kocha mpya wa kikosi chao akichukua nafasi ya Denis Kitambi aliyetua Geita Gold hivi karibuni.

“Uongozi umenipa nafasi ya kuinoa timu hii na kazi iliyonileta hapa ni kuhakikisha malengo ya timu yanafikiwa na yatafikiwa ikiwa tutafanya kazi pamoja kwa umoja na kila mtu akitimiza majukumu yake,” alisema Zahera.


Zahera amejiunga na Wauaji hao wa Kusini akitokea Coastal Union ambapo alikuwa kocha wa timu ya vijana baada ya kuondolewa kwenye kikosi cha timu kubwa.
Kocha huyo raia wa DR Congo anakuwa kocha wa tatu kufanya kazi Namungo msimu wa 2023/24 baada ya Cedric Kaze na Kitambi.
Pia Namungo inakuwa timu ya nne kwa Zahera kufundisha tangu alipotua Tanzania ambapo amepita Yanga msimu wa 2017/18, Polisi Tanzania 2022/23 na Coastal Union.
Namungo yenye pointi 17 kwa sasa iko nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC ikiwa imeshuka uwanjani mara 14, ikishinda michezo minne, sare tano na kufungwa mechi tano.

The post Zahera kuendeleza ushindi Namungo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/30/zahera-kuendeleza-ushindi-namungo/feed/ 0
Matokeo Coastal yamchefua Zahera https://www.greensports.co.tz/2023/10/14/matokeo-coastal-yamchefua-zahera/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/14/matokeo-coastal-yamchefua-zahera/#respond Sat, 14 Oct 2023 13:37:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8093 Na mwandishi wetuBaada ya kushindwa kupata ushindi kwenye michezo mitano ya Ligi Kuu NBC, Kocha Mkuu wa Coastal Union, Mwinyi Zahera ameeleza kukerwa na matokeo hayo.Coastal Union inaburuza mkia kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC wakiwa na pointi mbili baada ya mchezo mitano wakitoka sare mara mbili na kufungwa michezo mitatu.Wagosi wa Kaya hao wamepoteza […]

The post Matokeo Coastal yamchefua Zahera first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Baada ya kushindwa kupata ushindi kwenye michezo mitano ya Ligi Kuu NBC, Kocha Mkuu wa Coastal Union, Mwinyi Zahera ameeleza kukerwa na matokeo hayo.
Coastal Union inaburuza mkia kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC wakiwa na pointi mbili baada ya mchezo mitano wakitoka sare mara mbili na kufungwa michezo mitatu.
Wagosi wa Kaya hao wamepoteza dhidi ya Azam FC bao 1-0, Simba mabao 3-0, kabla ya kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Dodoma Jiji huku ikiambulia suluhu mbele ya Tabora United na sare ya 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Zahera alisema kuwa kama mwalimu hafurahishwi kabisa na kipindi anachopitia hivi sasa baada ya kushindwa kupata ushindi wowote na sasa anarejea kujipanga kwa ajili ya michezo ijayo kuhakikisha anabadili mwelekeo.

“Hakuna mwalimu anayependa kuona anashindwa kupata matokeo katika michezo mfululizo hivyo nimeyaona mapungufu ya kikosi changu naenda kuyafanyia kazi makosa yote yaliyojitokeza katika michezo iliyopita ili turudi kwenye ubora wetu,” alisema Zahera .


Alisema kuwa huu ni wakati wa kushikamana pamoja na kuangalia madhaifu yao kitaalamu zaidi kabla ya kushuka uwanjani tena kuzisaka pointi tatu zitakazorudisha morali yao.

The post Matokeo Coastal yamchefua Zahera first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/14/matokeo-coastal-yamchefua-zahera/feed/ 0
Zahera amtahadharisha Ajibu https://www.greensports.co.tz/2023/08/09/zahera-amtahadharisha-ajib/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/09/zahera-amtahadharisha-ajib/#respond Wed, 09 Aug 2023 19:44:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7316 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Coastal Union, Mwinyi Zahera amemtaka kiungo mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Ibrahim Ajibu (pichani) kuitumia nafasi aliyompa kwa uzito wa juu vinginevyo akishindwa hapo atakuwa amepotea kabisa kwenye soka.Ajibu ni miongoni mwa sura mpya zinazounda kikosi cha Coastal Union kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu NBC na michuano ya Kombe […]

The post Zahera amtahadharisha Ajibu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Coastal Union, Mwinyi Zahera amemtaka kiungo mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Ibrahim Ajibu (pichani) kuitumia nafasi aliyompa kwa uzito wa juu vinginevyo akishindwa hapo atakuwa amepotea kabisa kwenye soka.
Ajibu ni miongoni mwa sura mpya zinazounda kikosi cha Coastal Union kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu NBC na michuano ya Kombe la Azam (ASFC).
Zahera ameeleza kuwa yeye ni kati ya makocha wanaotambua uwezo na kipaji alichonacho Ajibu ndio sababu akaamua kumsajili kwenye timu hiyo akiamini atambadilisha na kurudi kwenye kiwango chake kama ilivyokuwa awali.

“Ajibu ni miongoni mwa wachezaji wachache wenye kipaji kikubwa cha kucheza mpira, nilifanya naye kazi pale Yanga, nikampa hadi unahodha anachotakiwa kufanya ni kucheza kwa kujitoa kuipigania timu yake, hii ni nafasi yake ya mwisho kwenye soka,” alisema Zahera.


Kocha huyo mwenye uraia wa nchi mbili za DRC Congo na Ufaransa alisema hata hapo Coastal ameamua kumpa unahodha anachoamini atamfua yeye pamoja na wachezaji wengine ili kumrudisha kwenye ubora wake.
Tangu atoke Yanga misimu mitatu iliyopita Ajibu amezichezea timu tatu tofauti ambazo ni Simba, Azam FC na Singida Fountain Gate na kote huko hakuonekana na mchango kwenye timu kiasi cha kutolewa kwa mkopo au kuvunjiwa mkataba.

The post Zahera amtahadharisha Ajibu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/09/zahera-amtahadharisha-ajib/feed/ 0
Zahera aigeuza fainali mechi ya Polisi, Mtibwa https://www.greensports.co.tz/2023/05/03/zahera-aigeuza-fainali-mechi-ya-polisi-mtibwa/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/03/zahera-aigeuza-fainali-mechi-ya-polisi-mtibwa/#respond Wed, 03 May 2023 16:45:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5999 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Mwinyi Zahera amesema mechi yao dhidi ya Mtibwa Sugar itakuwa kama fainali kwa kuwa ndio imebeba matumaini yao ya kubaki Ligi Kuu NBC.Maafande hao watakuwa nyumbani Uwanja wa Ushirika, Moshi Mei 15, mwaka huu kucheza na Mtibwa mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na timu zote […]

The post Zahera aigeuza fainali mechi ya Polisi, Mtibwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Mwinyi Zahera amesema mechi yao dhidi ya Mtibwa Sugar itakuwa kama fainali kwa kuwa ndio imebeba matumaini yao ya kubaki Ligi Kuu NBC.
Maafande hao watakuwa nyumbani Uwanja wa Ushirika, Moshi Mei 15, mwaka huu kucheza na Mtibwa mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na timu zote mbili kuwa katika nafasi mbaya kwenye msimamo wa ligi.
Zahera ameeleza kuwa ushindi walioupata kwenye mchezo uliopita dhidi ya Ihefu umeamsha ari ya kupambana kwenye kikosi chake hivyo anaamini kwa maandalizi waliyofanya hata mchezo ujao watachukua pointi tatu.

“Ni mchezo muhimu kwetu najua utakuwa mgumu lakini naamini tutapata ushindi ambao utasaidia kujiweka angalau kwenye ‘play off’ na siyo kushuka daraja moja kwa moja,” alisema Zahera.


Kocha huyo alisema kwa nama ushindani ulivyo kwa sasa uwezekano wa kujinasua moja kwa moja na janga la kushuka daraja ni mgumu kwa hiyo wanapambana kuangukia kwenye mechi za mtoano na baada ya hapo watajipanga kucheza mechi hizo za mtoano ili kusalia Ligi Kuu.
Polisi ambayo mechi iliyopita waliifunga Ihefu mabao 2-1, ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 22 wakati Mtibwa ipo nafasi ya 12 na pointi 29 huku zikiwa zimesalia mechi tatu kumaliza msimu.

The post Zahera aigeuza fainali mechi ya Polisi, Mtibwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/03/zahera-aigeuza-fainali-mechi-ya-polisi-mtibwa/feed/ 0
Zahera: Polisi haishuki daraja https://www.greensports.co.tz/2023/04/04/zahera-polisi-haishuki-daraja/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/04/zahera-polisi-haishuki-daraja/#respond Tue, 04 Apr 2023 19:11:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5687 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Mwinyi Zahera (pichani) amesema timu hiyo haishuki daraja na matumaini yao ya kuepuka kushuka daraja yanaanza Ijumaa hii kwa kuifunga Singida Big Stars.Polisi Tanzania itaikabili Singida kwenye Uwanja wa Liti, Singida ukiwa ni mchezo wa raundi ya 26 wa Ligi Kuu NBC.Zahera ameendelea kusisitiza kuwa timu yake haitoshuka […]

The post Zahera: Polisi haishuki daraja first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Mwinyi Zahera (pichani) amesema timu hiyo haishuki daraja na matumaini yao ya kuepuka kushuka daraja yanaanza Ijumaa hii kwa kuifunga Singida Big Stars.
Polisi Tanzania itaikabili Singida kwenye Uwanja wa Liti, Singida ukiwa ni mchezo wa raundi ya 26 wa Ligi Kuu NBC.
Zahera ameendelea kusisitiza kuwa timu yake haitoshuka daraja msimu huu licha ya kushika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoelekea ukingoni.

“Tumefanya maandalizi ya kutosha kipindi hiki ambacho ligi ilisimama kwa muda, tulicheza mechi tatu za kirafiki ambazo naamini zimetuimarisha na kurekebisha makosa yetu ndio maana hata mchezo wa keshokutwa dhidi ya Singida Big Stars naamini tunashinda,” alisema Zahera.


Kocha huyo ameeleza kuwa anajua watu wengi hawaamini maneno yake lakini mechi tano zilizobaki zinatosha kabisa kuiweka timu yake sehemu salama.
Alisema amekuwa akizungumza na wachezaji wake na kuwaeleza umuhimu wa mechi zilizobaki anaamini kila kitu kitakwenda vizuri na watu watakubaliana na yeye baada ya ligi kumalizika.
Polisi Tanzania ina pointi 19 katika michezo 25 iliyocheza hadi sasa na ili kuepuka kushuka daraja inalazimika kushinda michezo yote huku ikiziombea mabaya timu za Ruvu Shooting, Prisons na Coastal Union.

The post Zahera: Polisi haishuki daraja first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/04/zahera-polisi-haishuki-daraja/feed/ 0
Zahera awaza 5 bora Polisi Tanzania https://www.greensports.co.tz/2023/01/17/zahera-awaza-5-bora-polisi-tanzania/ https://www.greensports.co.tz/2023/01/17/zahera-awaza-5-bora-polisi-tanzania/#respond Tue, 17 Jan 2023 20:21:18 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4779 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Mwinyi Zahera amesema hesabu zake kwa sasa anawaza namna ya kumaliza ligi katika nafasi tano za juu na siyo kuiokoa timu kushuka daraja.Timu hiyo inashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi ikiwa imekusanya pointi 14 katika michezo 20 ambayo imecheza hadi sasa.Zahera ameelea kuwa usajili walioufanya kwenye […]

The post Zahera awaza 5 bora Polisi Tanzania first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Mwinyi Zahera amesema hesabu zake kwa sasa anawaza namna ya kumaliza ligi katika nafasi tano za juu na siyo kuiokoa timu kushuka daraja.
Timu hiyo inashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi ikiwa imekusanya pointi 14 katika michezo 20 ambayo imecheza hadi sasa.
Zahera ameelea kuwa usajili walioufanya kwenye dirisha dogo unampa jeuri ya kushinda mechi zilizosalia na kupanda hadi nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC iliyobakisha takriban mechi 10 kabla ya kufungwa rasmi pazia la msimu wa 2022-23.

“Najua watu wengi hawaamini lakini ukweli ni kwamba Polisi haitoshuka daraja, sababu tumesajili vizuri na tayari matokeo ya usajili wetu yameanza kuonekana katika mchezo uliopita ambao tuliifunga Namungo FC kwao Lindi,” alisema Zahera.


Kocha huyo aliyewahi kupita timu kadhaa nchini ikiwemo mabingwa watetezi Yanga, ameeleza kuwa anachojivunia katika usajili huo ni wachezaji wapya kuelewana kwa haraka na wachezaji waliokuwepo tangu mwanzo wa msimu na kushika haraka mifumo.
Alisema kwa namna alivyoijenga timu hiyo ana uhakika wa kushinda mechi sehemu yoyote ikiwemo viwanja vya ugenini ambavyo kwa kiasi fulani vimekuwa vigumu kupata ushindi.
Zahera amewataka viongozi wa timu hiyo kuondoa presha kwani timu yao kwa sasa ipo katika mikono salama na itaendelea kutamba kwenye ligi hiyo kwa misimu kadhaa ijayo.

The post Zahera awaza 5 bora Polisi Tanzania first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/01/17/zahera-awaza-5-bora-polisi-tanzania/feed/ 0