mayele - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 04 Apr 2024 20:43:16 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg mayele - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mayele awatembelea Simba Misri https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/mayele-awatembelea-simba-misri/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/mayele-awatembelea-simba-misri/#respond Thu, 04 Apr 2024 20:43:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10519 Na mwandishi wetuMshambuliaji wa Pyramids FC, Fiston Mayele ametinga katika hoteli waliyofikia Simba nchini Misri kwa ajili ya mechi yao ya mkondo wa pili ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.Mayele aliyewahi kukipiga Yanga, aliwatembelea mahasimu wake hao wa zamani na kuonana na baadhi ya wachezaji na viongozi wa timu […]

The post Mayele awatembelea Simba Misri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Pyramids FC, Fiston Mayele ametinga katika hoteli waliyofikia Simba nchini Misri kwa ajili ya mechi yao ya mkondo wa pili ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.
Mayele aliyewahi kukipiga Yanga, aliwatembelea mahasimu wake hao wa zamani na kuonana na baadhi ya wachezaji na viongozi wa timu hiyo ambao alisalimiana nao na kubadilishana nao mawazo.
Katika video iliyowekwa leo Alhamisi na mtandao wa Simba, Mayele raia wa DR Congo alionekana akisalimiana na wachezaji wa Simba akiwemo Fabrice Ngoma ambaye alionekana akimtania kuwa anapaswa kujiunga na Wekundu hao.
Mfungaji huyo bora wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita alionekana mwenye furaha kuonana na ‘nduguze’ hao aliokuwa akishindana nao kwenye Ligi Kuu NBC huku akiwatakia kila la heri katika mechi yao hiyo itakayopigwa kesho Ijumaa, Uwanja wa Cairo, mjini Cairo.
Katika mchezo huo, Simba inahitaji ushindi ili kusonga hatua ya nusu fainali baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kwenye mechi ya awali iliyopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam wiki iliyopita.

The post Mayele awatembelea Simba Misri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/mayele-awatembelea-simba-misri/feed/ 0
Mayele ampa Aziz Ki tuzo ya mfungaji bora https://www.greensports.co.tz/2023/12/25/mayele-ampa-aziz-ki-tuzo-ya-mfungaji-bora/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/25/mayele-ampa-aziz-ki-tuzo-ya-mfungaji-bora/#respond Mon, 25 Dec 2023 09:41:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9017 Na mwandishi wetuMshambuliaji wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele amesema kuwa iwapo kiungo Stephan Aziz Ki ataendelea kuwa na ubora alionao sasa atanyakua kiatu cha ufungaji bora Ligi Kuu NBC msimu huu.Mayele alisema hayo baada ya Aziz Ki kufikisha mabao 10 kwenye orodha ya wafungaji wa ligi kuu akiwa ameshuka uwanjani mara 11 akiwa na […]

The post Mayele ampa Aziz Ki tuzo ya mfungaji bora first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele amesema kuwa iwapo kiungo Stephan Aziz Ki ataendelea kuwa na ubora alionao sasa atanyakua kiatu cha ufungaji bora Ligi Kuu NBC msimu huu.
Mayele alisema hayo baada ya Aziz Ki kufikisha mabao 10 kwenye orodha ya wafungaji wa ligi kuu akiwa ameshuka uwanjani mara 11 akiwa na wastani wa kufunga bao moja kwenye kila mchezo.
Mayele aliyekuwa Yanga msimu uliopita na sasa akikipiga Pyramids ya Misri, msimu uliopita alinyakua kiatu hicho baada ya kupachika mabao 17 akiwa sawa na Saido Ntibazonkiza wa Simba.
Mshambuliaji huyo raia wa DR Congo alisema hashtushwi na kinachofanywa na Aziz Ki kutokana na ubora alionao na wala hatashangaa akimuona akishinda tuzo ya mfungaji bora.

“Nimekuwa nikimuangalia nini anafanya, amekuwa na muendelezo mzuri tangu msimu ulipoanza kama ataendelea hivi basi kiatu cha ufungaji ataenda kukitwaa,” alisema Mayele.


Mayele alisema kuwa kinachombeba Aziz Ki ni hamu aliyonayo ya kufanya mambo makubwa kwa ajili ya timu pamoja na kujituma kwenye uwanja wa mazoezi.

The post Mayele ampa Aziz Ki tuzo ya mfungaji bora first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/25/mayele-ampa-aziz-ki-tuzo-ya-mfungaji-bora/feed/ 0
Mayele awatuliza Yanga https://www.greensports.co.tz/2023/08/16/mayele-awatuliza-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/16/mayele-awatuliza-yanga/#respond Wed, 16 Aug 2023 05:41:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7404 Na mwandishi wetuMshambuliaji wa Pyramids FC ya Misri, Fiston Mayele ameitaka Yanga SC kusahau machungu ya kupoteza mechi ya fainali ya Ngao ya Jamii badala yake wahamishie nguvu zote kwenye Ligi Kuu NBC.Mayele aliyewika akiwa Yanga kabla ya hivi karibuni kutimkia Pyramids, ameyasema hayo baada ya Yanga kupoteza mechi na mahasimu wao Simba SC kwa […]

The post Mayele awatuliza Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Pyramids FC ya Misri, Fiston Mayele ameitaka Yanga SC kusahau machungu ya kupoteza mechi ya fainali ya Ngao ya Jamii badala yake wahamishie nguvu zote kwenye Ligi Kuu NBC.
Mayele aliyewika akiwa Yanga kabla ya hivi karibuni kutimkia Pyramids, ameyasema hayo baada ya Yanga kupoteza mechi na mahasimu wao Simba SC kwa matuta 3-1 kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Jumapili iliyopita.
Mfungaji huyo bora wa Ligi Kuu NBC msimu uliopita, aliandika maneno hayo katika ukurasa wa mtandao wa Instagram wa kiungo wa Yanga, Khalid Aucho akionesha kuifariji timu nzima.
“Jana imepita, muangalie ligi sasa Inshallah,” aliandika Mayele huku Aucho akimjibu kwa kumuunga mkono akiandika: “Ndio kaka.”
Mayele raia wa DR Congo amekuwa pia akikumbukwa na mashabiki wa Yanga katika mechi mbili zilizopita za Ngao ya Jamii kutokana na uhaba wa upatikanaji mabao wa timu hiyo licha ya utengenezwaji wa nafasi nyingi za kufunga.
Kabla ya kufungwa juzi, Yanga ilikuwa imetwaa ndoo hiyo mara mbili mfululizo, mara zote ikiifunga Simba kwa bao 1-0 na mabao 2-1. Mabao hayo yote ya Yanga yalifungwa na Mayele.
Tangu kutua kwa Mayele, Yanga imekusanya makombe yote ya ndani iliyoshiriki kwa misimu miwili mfululizo kuanzia Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la FA (ASFC) huku msimu uliopita ikifika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza.
Katika michuano hiyo pia Mayele aliibuka mfungaji bora kwa kufunga mabao saba na kuweka rekodi kwa Yanga kutoa mfungaji bora kwa mara ya kwanza pia katika historia ya michuano hiyo.
Baada ya kupoteza mchezo huo wa juzi, chini ya kocha mpya, Muargetina, Miguel Gamondi aliyerithi mikoba ya Nasreddine Nabi, Yanga sasa ina kibarua cha kuhakikisha mwisho wa msimu huu inatetea makombe yake mawili yaliyosalia.

The post Mayele awatuliza Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/16/mayele-awatuliza-yanga/feed/ 0
Straika wa Burundi aipamba Yanga https://www.greensports.co.tz/2023/07/18/straika-wa-burundi-aipamba-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/18/straika-wa-burundi-aipamba-yanga/#respond Tue, 18 Jul 2023 19:06:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7003 Na mwandishi wetuStraika anayetajwa kuwaniwa na Yanga SC, Sudi Abdallah (pichani) ingawa amegoma kueleza alikofikia na Yanga lakini ameisifu timu hiyo kuwa hakuna mchezaji asiyetaka kuitumikia kwa sasa.Sudi raia wa Burundi aliyekuwa akiitumikia Kuching City ya Malaysia amekuwa akitajwa kuwa kwenye rada za Yanga kuja kuziba nafasi ya Fiston Mayele aliyeondoka Jangwani hivi karibuni.Akizungumza leo […]

The post Straika wa Burundi aipamba Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Straika anayetajwa kuwaniwa na Yanga SC, Sudi Abdallah (pichani) ingawa amegoma kueleza alikofikia na Yanga lakini ameisifu timu hiyo kuwa hakuna mchezaji asiyetaka kuitumikia kwa sasa.
Sudi raia wa Burundi aliyekuwa akiitumikia Kuching City ya Malaysia amekuwa akitajwa kuwa kwenye rada za Yanga kuja kuziba nafasi ya Fiston Mayele aliyeondoka Jangwani hivi karibuni.
Akizungumza leo Jumanne alipokuwa akihojiwa na kituo cha redio cha nchini humo, Sudi alisema hawezi kueleza chochote kama amewasiliana na Yanga au la kwa kuwa hilo si suala lake lakini akakiri ni timu ya kuvutia.
“Unajua Yanga ni timu kubwa na kila mchezaji anayetaka kufika mbali amekuwa akifiria hilo, japo zipo timu nyingine kubwa kushinda Yanga lakini unaweza kupita Yanga kutokana na vitu vingi.
“Kwanza kulingana na kiwango walichonacho katika ligi, hata kwenye michuano ya Afrika wamekuwa wakifanya vitu vikubwa kabla ya kutolewa na Waarabu (USM Alger katika fainali) kwa hiyo kila mchezaji anaweza kuvutiwa kuwa hapo,” alisema Abdallah.
Mshambuliaji huyo anayeelezwa kuwa yuko huru kwa sasa amewahi kukipiga Al-Naft ya Iraq, Al-Faisaly ya Saudi Arabia, AS Kigali ya Rwanda na Vital’O ya kwao Burundi.
Yanga imeripotiwa kuingia sokoni kutafuta mshambuliaji mpya baada ya kuondoka kwa nyota wao, Mayele anayetajwa kutimkia Pyramids ya Misri huku pia jina la mshambuliaji kinda Muivorycoast, Sankara Karamoko anayekipiga Asec Mimosas likitajwa katika timu hiyo.

The post Straika wa Burundi aipamba Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/18/straika-wa-burundi-aipamba-yanga/feed/ 0
Ntibazonkiza, Mayele wang’ara tuzo TFF https://www.greensports.co.tz/2023/06/13/ntibazonkiza-mayele-wangara-tuzo-tff/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/13/ntibazonkiza-mayele-wangara-tuzo-tff/#respond Tue, 13 Jun 2023 09:03:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6578 Na mwandishi wetuKitendawili cha mfungaji bora Ligi Kuu NBC kimeteguliwa kwa Fiston Mayele na Saido Ntibazonkiza wote kupewa tuzo hiyo baada ya kila mmoja kufunga mabao 17 na wote wameng’ara kwa kubeba tuzo nyingine mbili.Vinara wengine wa soka waliong’ara kwa ufungaji na kushinda tuzo ni Jentrix Shikangwa wa Simba Queens ambaye kama ilivyo kwa Mayele […]

The post Ntibazonkiza, Mayele wang’ara tuzo TFF first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kitendawili cha mfungaji bora Ligi Kuu NBC kimeteguliwa kwa Fiston Mayele na Saido Ntibazonkiza wote kupewa tuzo hiyo baada ya kila mmoja kufunga mabao 17 na wote wameng’ara kwa kubeba tuzo nyingine mbili.
Vinara wengine wa soka waliong’ara kwa ufungaji na kushinda tuzo ni Jentrix Shikangwa wa Simba Queens ambaye kama ilivyo kwa Mayele na Ntibazonkiza naye amemaliza Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) na mabao 17.
Naye mshambuliaji wa Ihefu, Andrew Simchimba yeye amebeba tuzo ya mfungaji bora wa michuano ya Kombe la FA (ASFC).
Hafla ya utoaji tuzo hizo ilifanyika Jumatatu hii usiku mjini Tanga ambapo awali zilikuwapo hisia miongoni mwa wadau wa soka kwamba TFF ingekuja na kigezo cha kumpa tuzo mfungaji bora mmoja kati ya Mayele au Ntibazonkiza.
Wachezaji hao mbali na kutwaa tuzo ya mfungaji bora, kila mmoja ana tuzo nyingine mbili, Mayele ana tuzo ya bao bora la msimu na ile ya mchezaji bora wa msimu wakati, Ntibazonkiza naye pia ana tuzo ya fair play na kiungo bora.

Fiston Mayele

Sambamba na tuzo hizo, Mayele na Ntibazonkiza pia wamo kwenye kikosi bora cha msimu wa 2022-23 ambao pia umehitimishwa Jumatatu hii kwa mechi ya fainali ya Kombe la FA kati ya Yanga na Azam, mechi iliyoisha kwa Yanga kuifunga Azam bao 1-0.
Ukiachana na wachezaji hao, kipa wa Yanga, Djigui Diarra yeye ametwaa tuzo mbili akiwa na tuzo ya kipa bora wa ASFC pamoja na ya Ligi Kuu NBC na yumo pia kwenye kikosi bora cha msimu.
Wachezaji wengine wa Yanga, beki Dickson Job amebeba tuzo ya beki bora wakati Bakari Mwamnyeto amebeba tuzo ya mchezaji bora wa ASFC na wote hao wameingia kwenye kikosi bora.
Katika kikosi bora cha msimu pia wamo Mohammed Hussein, Henoc Inonga, Mzamiru Yassin, Shomari Kapombe na Clatous Chama ambao wote ni wachezaji wa Simba wakati kocha wa Yanga, Nasredinne Nabi yeye ametwaa tuzo ya kocha bora.


Mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize ameshinda tuzo ya mchezaji bora kijana chini ya miaka 20 anayecheza ligi kuu wakati Lameck Lawi wa Coastal Union ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi katika ligi hiyo hiyo.
Kwa upande wa ligi ya Championship mchezaji bora wa ligi hiyo ni Edward Songo wa JKT Tanzania wakati meneja bora wa uwanja ni Omar Malule na tuzo ya gwiji wa zamani wa soka imekwenda kwa Leopold Mukebezi beki wa zamani wa timu ya Pan Africa na Taifa Stars.
Tuzo ya mwamuzi bora wa ligi hiyo imechukuliwa na Jonesia Rukyaa wakati ile ya mwamuzi msaidizi imebebwa na Frank Komba huku Jonesia Rukya, Zawadi Yusuph, Athuman Rajab na Ally Simba wakibeba tuzo ya seti bora ya waamuzi kwa namna walivyosimamia vizuri mechi ya Geita Gold na Dodoma Jiji na Isack Munisi amebeba tuzo ya kamishna bora.
Kwa upande wa WPL mbali na Jentrix (pichani juu) aliyetwaa tuzo ya mfungaji bora, Ally Ally wa JKT Queens ametwaa tuzo ya kocha bora wakati Donisia Minja akitwaa tuzo ya mchezaji bora, Winfrida Charles tuzo ya mchezaji bora chipukizi na Najat Abbas yeye amechukua tuzo ya kipa bora.
Katika WPL pia, tuzo ya mwamuzi bora imekwenda kwa Ester Adalbert wakati ile ya mwamuzi msaidizi imechukuliwa na Glory Tesha.

The post Ntibazonkiza, Mayele wang’ara tuzo TFF first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/13/ntibazonkiza-mayele-wangara-tuzo-tff/feed/ 0
Ntibazonkiza amnasa Mayele kwa mabao https://www.greensports.co.tz/2023/06/09/ntibazonkiza-amnasa-mayele-kwa-mabao/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/09/ntibazonkiza-amnasa-mayele-kwa-mabao/#respond Fri, 09 Jun 2023 15:19:03 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6534 Na mwandishi wetuMabao saba aliyofunga Saido Ntibazonkiza wa Simba katika mechi mbili za mwisho za Ligi Kuu NBC msimu huu yamemfanya afungane mabao ya kufunga na Fiston Mayele kila mmoja akiwa na mabao 17.Kwa kipindi kirefu Mayele amekuwa kinara wa mabao wa ligi hiyo akiwa na mabao 16 wakati Ntibazonkiza alikuwa na mabao 10 kabla […]

The post Ntibazonkiza amnasa Mayele kwa mabao first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Saido Ntibazonkiza

Na mwandishi wetu
Mabao saba aliyofunga Saido Ntibazonkiza wa Simba katika mechi mbili za mwisho za Ligi Kuu NBC msimu huu yamemfanya afungane mabao ya kufunga na Fiston Mayele kila mmoja akiwa na mabao 17.
Kwa kipindi kirefu Mayele amekuwa kinara wa mabao wa ligi hiyo akiwa na mabao 16 wakati Ntibazonkiza alikuwa na mabao 10 kabla mambo hayajabadilika katika mechi mbili za mwisho.
Katika mechi hizo, Ntibazonkiza alifunga mabao matano peke yake dhidi ya Polisi Tanzania katika ushindi wa 6-1 na leo Ijumaa amefunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Coastal Union.
Kwa matokeo ya mechi hizo za mwisho za ligi msimu wa 2022-23, wachezaji hao wanakuwa wamefungana kwa idadi ya mabao ya kufunga ingawa Ntibazonkiza anajivunia kwa kuwa na asisti nyingi, 12 dhidi ya nne za Mayele.
Katika vita ya kujinasua na janga la kucheza play-offs, mambo hayakuwa mazuri kwa timu za Mbeya City na KMC ambazo zitalazimika kucheza mechi hizo. KMC imeshika nafasi ya 13 licha ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mbeya City.
Ushindi wa KMC umeifanya timu hiyo ifikishe pointi 32 ambazo hazikuweza kuitoa katika nafasi ya 13 wakati Mbeya City iliyokuwa nafasi ya 13 inashuka hadi nafasi ya 14 na pointi zake 31.
Polisi Tanzania inabaki nafasi ya 15 na Ruvu Shoting inabaki ikiburuza mkia katika nafasi ya 16.
Matokeo ya mechi za mwisho Ligi Kuu NBC msimu wa 2022-23 zilizochezwa leo Ijumaa ni kama ifuatavyo…
Azam 8-0 Polisi Tanzania
Coastal 1-3 Simba
Mtibwa Sugar 3-1 Geita Gold
Prisons 0-2 Yanga
Ihefu 2-0 Kagera Sugar
Mbeya City 0-1 KMC
Ruvu Shooting 0-1 Dodoma Jiji
Namungo 1-1 Singida Big

The post Ntibazonkiza amnasa Mayele kwa mabao first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/09/ntibazonkiza-amnasa-mayele-kwa-mabao/feed/ 0
Vita ya Mayele, Ntibazonkiza yafika patamu https://www.greensports.co.tz/2023/06/09/vita-ya-mayele-nitabazonkiza-yafika-patamu/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/09/vita-ya-mayele-nitabazonkiza-yafika-patamu/#respond Fri, 09 Jun 2023 09:41:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6526 Na Hassan KinguHuo ndio ukweli, mechi za mwisho za Ligi Kuu NBC zinanogeshwa na vita ya Fiston Mayele na Saido Ntibazonkiza kwenye tuzo ya mfungaji bora, ukiacha vita kali ya kujinasua na janga la kushuka daraja.Mechi hizo zinapigwa leo Ijumaa saa tisa na nusu alasiri, tuzo ya kuwania kiatu cha mfungaji bora ghafla imegeuka kuwa […]

The post Vita ya Mayele, Ntibazonkiza yafika patamu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Hassan Kingu
Huo ndio ukweli, mechi za mwisho za Ligi Kuu NBC zinanogeshwa na vita ya Fiston Mayele na Saido Ntibazonkiza kwenye tuzo ya mfungaji bora, ukiacha vita kali ya kujinasua na janga la kushuka daraja.
Mechi hizo zinapigwa leo Ijumaa saa tisa na nusu alasiri, tuzo ya kuwania kiatu cha mfungaji bora ghafla imegeuka kuwa mpambano wa Mayele na Ntibazonkiza.
Ntibazonkiza amebadili upepo ghafla kwa mabao yake matano aliyofunga katika mechi dhidi ya Polisi Tanzania na hivyo kufikisha mabao 15 akizidiwa bao moja na Mayele.
Na ingawa Ntibazonkiza amenukuliwa na GreenSports akisema hashindani na Mayele lakini si kweli kwamba haitaki tuzo ya mfungaji bora, atapambana kuhakikisha anafunga ili kuibuka mfungaji bora na hiyo maana yake ni kwamba yupo vitani.
Katika hali ya kawaida wachezaji wenzake wa Simba pia watapenda kuona anaibuka mfungaji bora, penalti, mipira ya adhabu na mazingira yote ya kupata bao watampa yeye ili aibuke mfungaji bora na kumbwaga Mayele ambaye kila mtu aliamini msimu huu tuzo hiyo ni mali yake.
Leo Yanga inakamilisha mechi yake ya mwisho ya ligi dhidi ya Prisons wakati Simba itaivaa Coastal Union, kama tutazichukulia mechi hizi kwa kuangalia yaliyopita, mashabiki wa Simba wana kila sababu ya kujipa matumaini kwamba mchezaji wao Ntibazonkiza ataibuka mfungaji bora na wale wa Yanga wataingiwa na huzuni na wasiwasi kwamba Mayele ataikosa tuzo hiyo kwa mara ya pili.
Prisons wamekuwa wagumu kwa Yanga wakati Coastal wanajulikana ni vibonde wa Simba, haitokuwa ajabu Simba kuifunga Coastal hata mabao matano na Yanga haitokuwa ajabu kutoka sare na Prisons.
Mazingira hayo hata hivyo hayana jibu la moja kwa moja kwamba nani ataibuka kinara wa mabao msimu huu, lolote linaweza kutokea katika mechi hizo za kufunga msimu.

Saido Ntibazonkiza

Msimu uliopita wa 2021-22 Mayele alipoteza tuzo hiyo katika hatua za mwisho mbele ya George Mpole na msimu huu anatakiwa kujiandaa kisaikolojia kwa hali hiyo kwani kwa hatua iliyofikia anaweza akashangazwa tena msimu huu wa 2022-23.
Matarajio yote makubwa ya awali yakafutika na badala yake akaishia nafasi ya pili kama ilivyokuwa msimu uliopita, chanzo cha yote ni huyu mtu anayeitwa Ntibazonkiza ambaye alikuwa naye Yanga kabla ya kutimuliwa na sasa anaelekea kuzima ‘mitetemo’ ya Mayele katika hatua za mwisho.
Ntibazonkiza ambaye alijiunga na Simba akitokea Geita Gold katika dirisha dogo, mabao yake mengine aliyafunga akiwa na timu hiyo, ametokea kuwa moto tangu atue Simba, si kwa kufunga mabao tu bali pia amekuwa mpishi muhimu wa mabao ya timu hiyo.
Ukiachana na Mayele na Ntibazonkiza janga la kujinasua na hatari ya kushuka daraja nalo lina vita yake inayohusisha timu za Mbeya City, iliyo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 31, KMC ya 14 pointi 29, na Polisi Tanzania ya 15 pointi 25 na Ruvu Shooting ya 16 pointi 20.
Matokeo ya mechi za leo pia ndiyo yatakayoamua timu ipi itacheza play-off, zilizo katika hatari hiyo ni KMC, Coastal Union, Mbeya City na Mtibwa Sugar.
Mechi za leo Ijumaa za Ligi Kuu NBC ni kama ifuatavyo…
Prisons v Yanga
Simba v Coastal
Azam v Polisi Tanzania
Namungo v Singida Big
Ihefu v Kagera
Mbeya City v KMC
Mtibwa Sugar v Geita Gold
Ruvu Shooting v Dodoma Jiji

The post Vita ya Mayele, Ntibazonkiza yafika patamu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/09/vita-ya-mayele-nitabazonkiza-yafika-patamu/feed/ 0
Ntibazonkiza: Sishindani na Mayele https://www.greensports.co.tz/2023/06/07/ntibazonkiza-sishindani-na-mayele/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/07/ntibazonkiza-sishindani-na-mayele/#respond Wed, 07 Jun 2023 15:27:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6502 Na mwandishi wetuMshambuliaji wa Simba, Saido Ntibazonkiza amesema hana mpango wa kushindana na mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele kuwania kiatu cha ufungaji bora msimu huu kwa kuwa amewekeza nguvu kubwa kuisaidia timu kwanza.Ntibazonkiza alifunga mabao matano jana katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na […]

The post Ntibazonkiza: Sishindani na Mayele first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Simba, Saido Ntibazonkiza amesema hana mpango wa kushindana na mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele kuwania kiatu cha ufungaji bora msimu huu kwa kuwa amewekeza nguvu kubwa kuisaidia timu kwanza.
Ntibazonkiza alifunga mabao matano jana katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na hivyo kufikisha mabao 15 nyuma ya Mayele aliyefunga mara 16.
Ntibazonkiza hata hivyo alisema anashukuru kuisaidia timu yake kupata matokeo na kama itatokea atatwaa kiatu cha ufungaji bora basi itakuwa vizuri lakini kwa sasa anaitanguliza Simba kisha mambo mengine yatafuata.

“Kwa sasa ni timu kwanza kupata matokeo mazuri kisha vingine hivyo tutaangalia kitakachotokea kwa uwezo wa Mungu. Fiston ni mfungaji mzuri, mshambuliaji mzuri kila mtu anamjua kwa hiyo ikitokea nikifanikiwa kuchukua nitamshukuru Mungu lakini timu kwanza,” alisema Ntibazonkiza.


Kwa mabao matano aliyofunga juzi, Ntibazonkiza anakuwa mchezaji wa kwanza msimu huu kufunga mabao mengi katika mechi moja lakini pia akifunga ‘hat-trick’ya pili msimu huu, sawa na nahodha wa Simba, John Bocco.

The post Ntibazonkiza: Sishindani na Mayele first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/07/ntibazonkiza-sishindani-na-mayele/feed/ 0
Ntibazonkiza amtikisa Mayele https://www.greensports.co.tz/2023/06/07/ntibazonkiza-amtikisa-mayele/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/07/ntibazonkiza-amtikisa-mayele/#respond Wed, 07 Jun 2023 06:43:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6494 Na mwandishi wetuYanga imetoka sare ya mabao 3-3 na Mbeya City wakati Simba ikiilaza Polisi Tanzania 6-1, Saido Ntibanzokiza akifunga mabao matano kati ya sita ya Simba na kufikisha mabao 15 katika Ligi Kuu NBC akimtikisa Fiston Mayele anayeshika usukani akiwa na mabao 16.Katika mechi hizo za ligi hiyo zilizopigwa Jumanne hii, matokeo hayo yameibua […]

The post Ntibazonkiza amtikisa Mayele first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga imetoka sare ya mabao 3-3 na Mbeya City wakati Simba ikiilaza Polisi Tanzania 6-1, Saido Ntibanzokiza akifunga mabao matano kati ya sita ya Simba na kufikisha mabao 15 katika Ligi Kuu NBC akimtikisa Fiston Mayele anayeshika usukani akiwa na mabao 16.
Katika mechi hizo za ligi hiyo zilizopigwa Jumanne hii, matokeo hayo yameibua gumzo jipya la nani ataibuka mfungaji bora msimu huu wa 2022-23? Je Ntibazonkiza (pichani juu) atambwaga Mayele?
Katika mechi za kukamilisha ligi hiyo zitakazopigwa Juni 9, Simba itakuwa mwenyeji wa Coastal Union wakati Yanga itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons, mechi ambazo matokeo ya pointi yanaweza yasiwe na maana badala yake mbio za kuwania kiatu cha mfungaji bora zikateka hisia za mashabiki.
Kati ya mabao 15 aliyofikisha Ntibazonkiza hadi sasa, mengine aliyafunga wakati akiichezea Geita Gold wakati kwa Mayele yote ameyafunga akiwa na Yanga.

Kwa Mayele (pichani) iwapo ataangushwa na Ntibazonkiza, itakuwa mara ya pili mfululizo kukutana na hali inayofanana na hiyo, msimu uliopita alishindwa kutamba mbele ya George Mpole. Mayele alipigwa bao na Mpole katika mechi za mwisho na safari hii huenda akakutana tena na hali hiyo.
Zaidi ya hilo, Mayele atakuwa ameshindwa kutimiza ndoto yake aliponukuliwa akisema angependa kumaliza msimu huu akiwa mfungaji mwenye mabao mengi katika Kombe la Shirikisho Afrika na Ligi Kuu NBC.
Tayari amefanikisha hilo kwenye Kombe la Shirikisho baada ya kuongoza na mabao yake saba lakini kwenye Ligi Kuu NBC ametikiswa kidogo, Ntibazonkiza amemsogelea na haitoshangaza wakifungana kwa mabao au hata akapitwa.
Katika mechi ya Simba ukiacha mabao ya Ntibazonkiza, bao jingine la Simba lilifungwa na Israel Mwenda wakati bao pekee la Polisi likifungwa na Steven Mayala.
Yanga nao ambao tayari ni vinara wa Ligi Kuu NBC, matokeo ya mechi hiyo japo yamewaumiza mashabiki wake lakini yamezidi kuiweka pagumu Mbeya City ambayo ilitakiwa ishinde ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuepuka janga la kushuka daraja.
Wakati Polisi ikiwa tayari imeshuka daraja, Mbeya City yenye pointi 31 italazimika kupambana kufa na kupona ili ishinde mechi yake ya mwisho na KMC na hivyo kufikisha pointi 34.
Ugumu wa mechi hiyo unachangiwa na mazingira ya KMC yenye pointi 29 ambayo pia inahitaji ushindi ili ifikishe pointi 32. Je nani atashinda na kujinasua na janga la kushuka daraja? KMC kwa sasa inashika nafasi ya 14 wakati Mbeya City inashika nafasi ya 13.

The post Ntibazonkiza amtikisa Mayele first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/07/ntibazonkiza-amtikisa-mayele/feed/ 0
Mayele, Inonga waitwa DR Congo https://www.greensports.co.tz/2023/05/30/mayele-inonga-waitwa-dr-congo/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/30/mayele-inonga-waitwa-dr-congo/#respond Tue, 30 May 2023 19:44:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6382 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa timu ya taifa ya DR Congo, Sébastien Desabre ameita kikosi chake akiwajumuisha Fiston Mayele wa Yanga na Henock Inonga wa Simba kwa ajili ya kuivaa Gabon katika mechi ya kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2023.Mayele anaitwa kwa mara ya pili mfululizo kutokana na kiwango anachoendelea kukionesha kwenye michuano inayoshiriki Yanga […]

The post Mayele, Inonga waitwa DR Congo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya DR Congo, Sébastien Desabre ameita kikosi chake akiwajumuisha Fiston Mayele wa Yanga na Henock Inonga wa Simba kwa ajili ya kuivaa Gabon katika mechi ya kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2023.
Mayele anaitwa kwa mara ya pili mfululizo kutokana na kiwango anachoendelea kukionesha kwenye michuano inayoshiriki Yanga ikiwemo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambako mchezaji huyo anaongoza kwa mabao saba.


Na licha ya Simba kushindwa kutwaa taji lolote msimu huu lakini kiwango cha Inonga kimeendelea kung’ara na kumshawishi Desbare kumwita kwenye kikosi hicho chenye wachezaji 27.
Kabla ya kuivaa Gabon Juni 18, DR Congo itacheza na Uganda mechi ya kirafiki itakayopigwa Juni 14, mwaka huu mjini Douala, Cameroon.
Congo inahitaji ushindi dhidi ya Gabon ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya Kundi I ambako inaburuza mkia kwa pointi nne baada ya mechi nne ikiwa imeshinda mchezo mmoja, sare moja na kufungwa mara mbili.
Pia, Congo ikiwa ugenini Uwanja wa Franceville, mjini Franceville itahitaji ushindi kulipa kisasi kwa Gabon iliyoibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye mechi iliyopita iliyopigwa Uwanja wa Martyrs, Kinshasa, DR Congo.
Mara ya mwisho, Chui hao kushiriki michuano ya Afcon ilikuwa mwaka 2019 walipopangwa kundi moja na Misri, Zimbabwe na Uganda ambapo Desabre ndiye aliyekuwa kocha wao wakati huo.

The post Mayele, Inonga waitwa DR Congo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/30/mayele-inonga-waitwa-dr-congo/feed/ 0