Geita Gold - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 15 Mar 2024 07:58:48 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Geita Gold - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Yanga yachanja mbuga ligi kuu https://www.greensports.co.tz/2024/03/15/yanga-yachanja-mbuga-ligi-kuu/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/15/yanga-yachanja-mbuga-ligi-kuu/#respond Fri, 15 Mar 2024 07:58:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10204 Na mwandishi wetuYanga imeendelea kuchanja mbuga katika Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Geita Gold bao 1-0 katika mechi iliyopigwa Alhamisi hii kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.Ushindi huo pia unaifanya Yanga kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 52 katika mechi 19 ikifuatiwa na Azam FC yenye […]

The post Yanga yachanja mbuga ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga imeendelea kuchanja mbuga katika Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Geita Gold bao 1-0 katika mechi iliyopigwa Alhamisi hii kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Ushindi huo pia unaifanya Yanga kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 52 katika mechi 19 ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 44 katika mechi 20.
Mahasimu wa Yanga, Simba wao wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 42 katika mechi 18 walizocheza hadi sasa.
Bao hilo pekee la ushindi kwa Yanga lilipatikana katika dakika ya 28 ya mchezo huo mfungaji akiwa ni Aziz Ki ambaye sasa anakuwa amefikisha mabao 13 katika ligi hiyo.
Baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Geita, Yanga sasa inajiandaa kwa kibarua kigumu dhidi ya Azam, mechi ambayo itapigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa Jumatatu hii, Coastal Union ikiwa nyumbani Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ilitoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu.
Kwa ushindi huo, Coastal sasa inakuwa imejikusanyia jumla ya pointi 30 katika michezo 21 ikiwa imejichimbia katika nafasi ya nne mbele ya Prisons yenye pointi 28 katika michezo 21.

The post Yanga yachanja mbuga ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/15/yanga-yachanja-mbuga-ligi-kuu/feed/ 0
Kocha Geita alaumu wachezaji https://www.greensports.co.tz/2023/11/08/kocha-geita-alaumu-wachezaji/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/08/kocha-geita-alaumu-wachezaji/#respond Wed, 08 Nov 2023 19:11:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8405 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Geita Gold, Hemed Morocco amesema hali ya kukosa ushindi mfululizo katika timu hiyo inatokana na kikosi chake kukosa wachezaji wenye ubora wa kupambana katika Ligi Kuu NBC.Morocco ameyasema hayo baada ya timu hiyo kukosa ushindi katika mechi zake nane mfululizo kati ya tisa ilizocheza mpaka sasa, hali iliyopelekea Mkurugenzi wa […]

The post Kocha Geita alaumu wachezaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Geita Gold, Hemed Morocco amesema hali ya kukosa ushindi mfululizo katika timu hiyo inatokana na kikosi chake kukosa wachezaji wenye ubora wa kupambana katika Ligi Kuu NBC.
Morocco ameyasema hayo baada ya timu hiyo kukosa ushindi katika mechi zake nane mfululizo kati ya tisa ilizocheza mpaka sasa, hali iliyopelekea Mkurugenzi wa Halmashauri ya Geita, Zahara Michuzi kumtaka kocha huyo kuonana naye kuwaeleza juu ya matokeo hayo mabaya ya timu hiyo.
Akizungumza na GreenSports leo Jumatano, Morocco alisema hajawahi kuwa na matokeo mabovu kiasi hicho lakini ubora mdogo wa wachezaji unachangia matokeo hayo na sasa akijipanga kuongeza idadi ya wachezaji wanne mpaka watano katika usajili wa dirisha dogo ili kuhakikisha wanakuwa bora mzunguko wa pili.

“Hii hali haijawahi kunitokea kabla lakini ni matokeo ya mpira ambayo nafikiri ni kutokana na kukosa wachezaji wenye ubora wa kupambana kwenye ligi ndio maana tuna mpango wa kuongeza wachezaji wanne mpaka watano kwa ajili kuongeza nguvu mzunguko wa pili,” alisema Morocco.


Alisema kwa mechi za kwanza wachezaji hao walionesha ubora mkubwa lakini wamekuwa wakishuka viwango kadri siku zinavyosonga na zaidi makosa ya mchezaji mmoja mmoja ndio yamekuwa yakiwagharimu.
Kocha huyo alipoulizwa kama alishakutana na Mkurugenzi Michuzi alisema hayuko tayari kuzungumzia suala hilo kwa kuwa ameamua kukaa kimya.
Geita ambayo imeshinda mechi moja, sare nne na kufungwa mara nne, inashika nafasi ya 15 kati ya timu 16 ikiwa na pointi saba.

The post Kocha Geita alaumu wachezaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/08/kocha-geita-alaumu-wachezaji/feed/ 0
Yanga yaipopoa Geita 3-0 https://www.greensports.co.tz/2023/10/07/yanga-yaipopoa-geita-3-0/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/07/yanga-yaipopoa-geita-3-0/#respond Sat, 07 Oct 2023 18:24:36 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8001 Na mwandishi wetuYanga leo Jumamosi imenyakua pointi tatu muhimu baada ya kuichapa Geita Gold mabao 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa kwenye Uwanja wa CCM, Kirumba mjini Mwanza.Bao la kwanza la Yanga lilipatikana dakika moja kabla ya timu hizo kwenda mapumziko mfungaji akiwa ni Pacome Zouazoua akiitumia pasi ya beki Yao Kouasi.Dakika moja […]

The post Yanga yaipopoa Geita 3-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga leo Jumamosi imenyakua pointi tatu muhimu baada ya kuichapa Geita Gold mabao 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa kwenye Uwanja wa CCM, Kirumba mjini Mwanza.
Bao la kwanza la Yanga lilipatikana dakika moja kabla ya timu hizo kwenda mapumziko mfungaji akiwa ni Pacome Zouazoua akiitumia pasi ya beki Yao Kouasi.
Dakika moja baadaye, Geita walishangazwa kwa kuchapwa bao la pili lililofungwa na Stephanie Aziz Ki ambaye aliinasa krosi ya Maxi Nzengeli na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko Yanga ikiwa mbele kwa mabao 2-0.
Kipindi cha pili Yanga waliendelea kuisakama Geita na hatimaye kuandika bao la tatu lililofungwa na Maxi katika dakika ya 67.
Kwa ushindi huo Yanga sasa imefikisha pointi 12 ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Azam ingawa huenda ikashuka zaidi kutegemea matokeo ya mechi ya Jumapili ya Simba dhidi ya Singida Fountain Gate. Simba pia ina pointi 12.
Katika mechi hiyo, Geita ilijikuta katika wakati mgumu mapema dakika ya 14 baada ya mshambuliaji wake tegemeo na nahodha wa timu hiyo, Elius Maguli kuumia wakati akiwania mpira wa juu na beki wa Yanga, Bakari Mwamnyeto.
Mechi ya leo pia iliathiriwa na mvua ambayo ilinyesha muda mfupi kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza kwa takriban dakika tatu kabla ya kukatika.

The post Yanga yaipopoa Geita 3-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/07/yanga-yaipopoa-geita-3-0/feed/ 0
‘Tuna uwezo kuifunga timu yoyote’ https://www.greensports.co.tz/2023/08/13/tuna-uwezo-kuifunga-timu-yoyote/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/13/tuna-uwezo-kuifunga-timu-yoyote/#respond Sun, 13 Aug 2023 00:56:19 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7355 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Geita Gold, Hemed Morocco (pichani) amesema wanaweza kuifunga timu yoyote kwani wana kikosi kizuri cha vijana wenye uzoefu kwa ajili ya kupambana kwenye Ligi Kuu NBC msimu ujao.Geita inatarajia kuondoka Jumapili hii kuelekea Mbarali, mkoani Mbeya kuifuata Ihefu kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kufungua pazi la ligi hiyo […]

The post ‘Tuna uwezo kuifunga timu yoyote’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Geita Gold, Hemed Morocco (pichani) amesema wanaweza kuifunga timu yoyote kwani wana kikosi kizuri cha vijana wenye uzoefu kwa ajili ya kupambana kwenye Ligi Kuu NBC msimu ujao.
Geita inatarajia kuondoka Jumapili hii kuelekea Mbarali, mkoani Mbeya kuifuata Ihefu kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kufungua pazi la ligi hiyo msimu 2023/2024 utakaochezwa Uwanja wa Highland Estate, Agosti 15, mwaka huu.
Akizungumzia maandalizi ya timu hiyo, Morocco alisema wamefurahia kambi ya maandalizi waliyoweka Morogoro kwani ilikuwa nzuri, wamepata muda wa kutosha kujiweka imara na sasa wako tayari kuanza harakati za kulipigania taji la ligi.
“Nimefurahia kambi yetu ya Morogoro. Wachezaji wako na afya njema na naamini wako vizuri kiakili na kimwili kuelekea katika mchezo wetu ujao dhidi ya Ihefu, naamini kwa kile nilichowaelekeza tutaanza vizuri Jumanne kwa kushinda bila kujali kuwa tunaanza ugenini,” alisema.
Morocco alisema kama ambavyo wengine wamesajili wachezaji wazuri hata wao pia wana kikosi kizuri kitakachowafikisha kwenye malengo waliyojiwekea.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Geita, Samwel Dida, jumla ya wachezaji 27 wataelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo huo na wengine watarudi Geita kujiandaa na mchezo ujao.

The post ‘Tuna uwezo kuifunga timu yoyote’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/13/tuna-uwezo-kuifunga-timu-yoyote/feed/ 0
Morocco amfurahia kipa Geita https://www.greensports.co.tz/2023/08/05/morocco-amfurahia-kipa-geita/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/05/morocco-amfurahia-kipa-geita/#respond Sat, 05 Aug 2023 14:10:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7243 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Geita Gold, Hemed Morocco (pichani) amesema kwa sasa lango lake liko salama kwa asilimia 100 baada ya kutua kwa kipa Eric Johora katika kikosi hicho akitokea Yanga SC.Morocco ameiambia GreenSports kuwa mbali na ubora aliokuwa nao kipa huyo aliyetambulishwa na timu hiyo lakini pia mafanikio na ujuzi alioupata akiwa Yanga […]

The post Morocco amfurahia kipa Geita first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Geita Gold, Hemed Morocco (pichani) amesema kwa sasa lango lake liko salama kwa asilimia 100 baada ya kutua kwa kipa Eric Johora katika kikosi hicho akitokea Yanga SC.
Morocco ameiambia GreenSports kuwa mbali na ubora aliokuwa nao kipa huyo aliyetambulishwa na timu hiyo lakini pia mafanikio na ujuzi alioupata akiwa Yanga ni jambo muhimu kwao.
“Ni kipa anayekuja kuongeza upinzani na kuliweka lango salama zaidi kutokana na ujuzi alionao, anatokea Yanga ambayo imekuwa ikishiriki michuano mingi na kufika mbali hivyo ujuzi wake pia ni jambo zuri zaidi kabla ya kugusa kipaji kikubwa alichonacho,” alisema Morocco.
Kocha huyo wa zamani wa Taifa Stars alieleza kutua kwa Johora sasa ni wazi wako hatua za mwisho kukamilisha usajili kuelekea msimu ujao, wakitarajia kuhitimisha kwa kuongeza beki mmoja pekee.
Wachezaji wengine waliosajiliwa na Geita mpaka sasa ni Carlos Protas, Tariq Seif, Samuel Onditi, Valentino Kusengama, Yusuf Dunia, Mwaite Gereza na Abeid Athuman.

The post Morocco amfurahia kipa Geita first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/05/morocco-amfurahia-kipa-geita/feed/ 0
Geita Gold kuweka kambi Moro https://www.greensports.co.tz/2023/07/18/geita-gold-kuweka-kambi-moro/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/18/geita-gold-kuweka-kambi-moro/#respond Tue, 18 Jul 2023 18:58:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6998 Na mwandishi wetuTimu ya Geita Gold inatarajiwa kuweka kambi ya wiki tatu mkoani Morogoro kujiandaa na maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu NBC utakaoanza Agosti 15, mwaka huu.Akizungumza na GreenSports, Ofisa Habari wa Geita, Samuel Dida alisema program za mazoezi zitaanza kesho Jumatano.Alisema wamechagua kambi ya Morogoro kutokana na hali ya hewa nzuri lakini […]

The post Geita Gold kuweka kambi Moro first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Geita Gold inatarajiwa kuweka kambi ya wiki tatu mkoani Morogoro kujiandaa na maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu NBC utakaoanza Agosti 15, mwaka huu.
Akizungumza na GreenSports, Ofisa Habari wa Geita, Samuel Dida alisema program za mazoezi zitaanza kesho Jumatano.
Alisema wamechagua kambi ya Morogoro kutokana na hali ya hewa nzuri lakini pia wanatarajia kucheza michezo kadhaa ya kirafiki kupitia mashindano maalum yatakayofanyika mkoani hapo.
“Tutakuwa na michezo ya kirafiki pale lakini pia kutakuwa na mashindano maalum ambayo tumealikwa, yatafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, na sisi ni miongoni mwa timu zitakazoshiriki,” alisema.
Kwa mujibu wa Dida, watakaa Morogoro mpaka Agosti 3, kisha wataelekea nchini Rwanda kucheza michezo ya kirafiki dhidi ya klabu ya Mukulu wanaoadhimisha miaka 60 ambapo watakaa kwa siku mbili kisha waterejea Geita.
Alisema kabla ya kuanza msimu watafanya uzinduzi wa jezi kisha tamasha fupi la kutambulisha wachezaji wapya na kuwapongeza vijana wao waliofika hatua ya fainali kwenye ligi ya vijana.

The post Geita Gold kuweka kambi Moro first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/18/geita-gold-kuweka-kambi-moro/feed/ 0
Maguli aongezewa mwaka Geita https://www.greensports.co.tz/2023/07/14/maguli-aongezewa-mwaka-geita/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/14/maguli-aongezewa-mwaka-geita/#respond Fri, 14 Jul 2023 15:23:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6973 Na mwandishi wetuTimu ya Geita Gold imetangaza kumuongeza mkataba wa mwaka mmoja mshambuliaji wake mahiri, Elias Maguli,(pichani) utakaomuweka mpaka mwisho wa msimu wa 2023-24.Maguli aliyetangazwa leo Ijumaa kuongeza mkataba huo ndiye mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kuelezwa juu ya kuendelea na timu hiyo msimu ujao baada ya jana Geita kutangaza kutema wachezaji tisa waliomaliza […]

The post Maguli aongezewa mwaka Geita first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Geita Gold imetangaza kumuongeza mkataba wa mwaka mmoja mshambuliaji wake mahiri, Elias Maguli,(pichani) utakaomuweka mpaka mwisho wa msimu wa 2023-24.
Maguli aliyetangazwa leo Ijumaa kuongeza mkataba huo ndiye mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kuelezwa juu ya kuendelea na timu hiyo msimu ujao baada ya jana Geita kutangaza kutema wachezaji tisa waliomaliza mikataba.
“Timu inaendelea kutengenezwa vizuri zaidi ingawa tayari kuna vitu tumeshavimaliza na tunasubiri muda sahihi ufike tuweke hadharani tuendelee na mengine kwa hiyo Maguli ni mpango wa timu ndiyo maana ameongeza mkataba, tupo naye,” alisema Ofisa Habari wa Geita, Samwel Dida.
Hata hivyo, Wachimba Dhahabu hao tayari wameeleza kumalizana na kocha wao mkuu mpya anayetajwa kutoka nchi za Afrika Mashariki, mabeki wa kati wawili kutoka Kenya na Rwanda, mshambuliaji kutoka Afrika Kusini na wachezaji wengine takriban sita wapya kutoka Tanzania.
Wachezaji walioachana na timu hiyo baada ya kumaliza mikataba ni Danny Lyanga, George Wawa, Mark Arakaza, Geofrey Manyasi, Jonathan Ulaya, Mussa Gadi, Shinobu Sakai, Jonathan Mwaibindi na Juma Luizio aliyeomba kuvunja mkataba.

The post Maguli aongezewa mwaka Geita first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/14/maguli-aongezewa-mwaka-geita/feed/ 0
Minziro ajiweka kando Geita Gold https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/minziro-ajiweka-kando-geita-gold/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/minziro-ajiweka-kando-geita-gold/#respond Tue, 06 Jun 2023 20:21:19 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6483 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Felix Minziro amejiweka kando na timu hiyo baada ya kile kilichoelezwa kuwa ni kushindwana kwa maslahi binafsi nje ya mkataba baina ya pande hizo.Minziro ameiambia GreenSports leo Jumanne kuwa amekaa kando kutokana na timu hiyo kumkatalia matakwa yake ya kumlipa kiasi cha pesa alichowatajia katika mechi mbili […]

The post Minziro ajiweka kando Geita Gold first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Felix Minziro amejiweka kando na timu hiyo baada ya kile kilichoelezwa kuwa ni kushindwana kwa maslahi binafsi nje ya mkataba baina ya pande hizo.
Minziro ameiambia GreenSports leo Jumanne kuwa amekaa kando kutokana na timu hiyo kumkatalia matakwa yake ya kumlipa kiasi cha pesa alichowatajia katika mechi mbili zilizosalia za Ligi Kuu NBC msimu huu.
“Mkataba wangu umeisha tangu Mei 28, niko nje ya mkataba nikijihudumia kwa kila kitu hivyo nikawaambia wanipe pesa kidogo kwa ajili ya kumaliza hizo mechi mbili na siwezi kuwatajia pesa kubwa sababu mimi niko na timu mwaka wa tatu sasa, lakini wakanijibu hawana kiasi hicho.

“Basi mimi nimeondoka zangu, niko Dar es Salaam naendelea na mambo mengine maana kwa tafsiri fupi unaweza kusema hawakutaka labda niendelee kwenye mechi hizi mbili na uzuri nimezungumza nao, tumemalizana vizuri,” alisema Minziro.


Alipotafutwa Ofisa Habari wa Geita, Samwel Dida alisema: “Hizi mechi mbili ziko nje ya mkataba wake, tukamwomba amalizie hizi dakika 180, akatupa utaratibu wake wa malipo, tuliona hatuwezi kumudu na yeye akawa na msimamo wake basi tukamalizana.”
Dida pia alisema mechi zao mbili zilizosalia ikiwemo ya leo dhidi ya Ihefu na ya Mei 9, mwaka huu dhidi ya Mtibwa Sugar, kikosi chao kitakuwa chini ya kocha wa timu ya vijana, Choke Abeid.
Dida aliongeza kuwa kulingana na hali iliyopo sasa baada ya kushindwana na Minziro, imekuwa ngumu kufahamu kama watakua na kocha huyo msimu ujao au la.

The post Minziro ajiweka kando Geita Gold first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/minziro-ajiweka-kando-geita-gold/feed/ 0
Wachezaji Geita waandaliwa tuzo https://www.greensports.co.tz/2023/05/30/wachezaji-geita-waandaliwa-tuzo/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/30/wachezaji-geita-waandaliwa-tuzo/#respond Tue, 30 May 2023 18:50:36 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6374 Na mwandishi wetuUongozi wa timu ya Geita Gold umeeleza kuwa upo kwenye mchakato wa kuandaa tuzo za msimu kwa ajili ya wachezaji wa timu hiyo kuanzia msimu ujao wa 2023-24.Ofisa Habari wa Geita, Samwel Dida ameiambia GreenSports leo Jumanne kuwa kwa sasa wapo kwenye majadiliano ya kina kuhakikisha wanalitekeleza kwa weledi mkubwa jambo hilo kwa […]

The post Wachezaji Geita waandaliwa tuzo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Uongozi wa timu ya Geita Gold umeeleza kuwa upo kwenye mchakato wa kuandaa tuzo za msimu kwa ajili ya wachezaji wa timu hiyo kuanzia msimu ujao wa 2023-24.
Ofisa Habari wa Geita, Samwel Dida ameiambia GreenSports leo Jumanne kuwa kwa sasa wapo kwenye majadiliano ya kina kuhakikisha wanalitekeleza kwa weledi mkubwa jambo hilo kwa ajili ya kuthamini mchango wa timu nzima kwa kila mchezaji.
Alisema tuzo hizo zitakuwa ni kwa ajili ya mchezaji bora wa kila mwezi katika miezi minane ya msimu mzima, mchezaji bora wa kila mechi na tuzo za idara mbalimbali ndani ya uwanja mwisho wa msimu.

“Timu imekuwa ikipambana mno, msimu uliopita tulimaliza kwenye nne bora na msimu huu tunapambana kumaliza tano bora. Kwa hiyo ni mwenendo mzuri na katika kulithamini hilo tupo kwenye mchakato wa kuwaandalia tuzo, tunahitaji wapate stahiki yao mwisho wa mapambano,” alisema Dida.


Geita iliyopanda kushiriki ligi kuu msimu wa 2021-22, msimu uliopita ilimaliza nafasi ya nne na kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza. Msimu huu zimesalia mechi mbili kumalizika kwa ligi, ikiwania kumaliza juu ya Namungo iliyo nafasi ya tano kwa pointi 39 wakati Geita ina pointi 37.

The post Wachezaji Geita waandaliwa tuzo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/30/wachezaji-geita-waandaliwa-tuzo/feed/ 0
Minziro: Sijui hatma yangu Geita Gold https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/minziro-sijui-hatma-yangu-geita-gold/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/minziro-sijui-hatma-yangu-geita-gold/#respond Fri, 26 May 2023 19:26:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6300 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Felix Minziro amesema bado hafahamu hatma yake ya kuendelea kuinoa timu hiyo kutokana na kufika ukingoni kwa mkataba wake.Kocha huyo ameiambia GreenSports leo Ijumaa kuwa mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu, ingawa amepata ofa za timu nyingine tayari lakini anasikiliza kwanza mazungumzo ya mabosi wake hao […]

The post Minziro: Sijui hatma yangu Geita Gold first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Felix Minziro amesema bado hafahamu hatma yake ya kuendelea kuinoa timu hiyo kutokana na kufika ukingoni kwa mkataba wake.
Kocha huyo ameiambia GreenSports leo Ijumaa kuwa mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu, ingawa amepata ofa za timu nyingine tayari lakini anasikiliza kwanza mazungumzo ya mabosi wake hao wa sasa.
Amesema ingawa anatarajia kukutana na uongozi wa timu hiyo hivi karibuni kufahamu kama anaendelea au la lakini kutokuwa na uhakika kwa sasa kunamkwamisha kuanza harakati za mapema za kufanya usajili wa wachezaji wa msimu ujao.
“Ni kweli namaliza mkataba mwisho wa msimu huu, zimesalia siku chache mno lakini bado hakuna mazungumzo na uongozi kuhusiana na hilo japokuwa natarajia kukutana nao kabla ya kucheza mechi mbili zilizosalia za ligi.

“Kama inavyoonekana kweli tunaelekea kipindi cha usajili, kuisuka vizuri zaidi timu kwa ajili ya msimu ujao lakini huwezi kufanya hivyo kwa sasa sababu bado haijafahamika itakuwaje siku za usoni kuhusu kuendelea kubaki Geita,” alisema Minziro.


Minziro beki wa zamani wa Yanga, amekuwa na Geita tangu alipoipandisha timu hiyo daraja kucheza ligi kuu msimu wa 2021-22 na kisha kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Hiyo ni baada ya kumaliza kwenye nne bora ya msimamo wa ligi kuu katika msimu wao wa kwanza. Msimu huu Geita ipo nafasi ya sita ikipambana kumaliza kwenye tano bora.

The post Minziro: Sijui hatma yangu Geita Gold first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/minziro-sijui-hatma-yangu-geita-gold/feed/ 0