Chelsea - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 24 Apr 2024 06:25:58 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Chelsea - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Chelsea laini yamtesa Pochettino https://www.greensports.co.tz/2024/04/24/chelsea-laini-yamtesa-pochettino/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/24/chelsea-laini-yamtesa-pochettino/#respond Wed, 24 Apr 2024 06:25:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10727 London, EnglandBaada ya kuchapwa mabao 5-0 na Arsenal kwenye Uwanja wa Emirates jana Jumanne, kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino amesema timu yake ni kama iliacha kucheza soka na ilikuwa laini.Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England (EPL), Chelsea ilikwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao 1-0 lakini kipindi cha pili ikajikuta ikichapwa mabao manne katika muda […]

The post Chelsea laini yamtesa Pochettino first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Baada ya kuchapwa mabao 5-0 na Arsenal kwenye Uwanja wa Emirates jana Jumanne, kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino amesema timu yake ni kama iliacha kucheza soka na ilikuwa laini.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England (EPL), Chelsea ilikwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao 1-0 lakini kipindi cha pili ikajikuta ikichapwa mabao manne katika muda usiozidi dakika 18.
Matokeo hayo mabaya kwa Chelsea yameweka rekodi ya kuwa kipigo kikubwa zaidi katika London Derby tangu mwaka 1986.
“Hakuna ugumu wowote wa kuelezea hali ilivyokuwa, kila mmoja aliona, hatukuwa tukipambana tangu mwanzo wa mchezo,” alisema Pochettino.
“Baada ya kufungwa goli la kwanza timu ilikuwa laini, ilinisikitisha tangu tulipoanza kwa sababu tulitakiwa kuwa na nguvu na kupambana vizuri, hatukuonesha ushindani, hatukuwa makini na mazingira ambayo ilikuwa rahisi kuyapatia suluhisho, na hiyo ndiyo sababu hasa iliyonikatisha tamaa,” alisema Pochettino
Katika mechi hiyo, Pochettino alifanya mabadiliko matatu katika safu ya ulinzi akimpumzisha Trevoh Chalobah na Thiago Silva wakati Malo Gusto alikuwa majeruhi baada ya kuumia katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Man City.
Pochettino alisema timu yake ilipambana vizuri katika mechi na Man City ambayo pia walipoteza lakini akashangaa kushindwa kufanya hivyo siku tatu baadaye na kuongeza kuwa huenda timu haikuwa ‘fresh’.

“Tulikuwa tukizungumza wakati wa mapumziko kuhusu kuanza kipindi cha pili katika namna tofauti lakini hatukufanya hivyo, tulipofungwa bao la tatu timu ni kama iliacha kucheza, hali ilikuwa ngumu,” alisema Pochettino.


Kocha huyo hata hivyo alikataa kuzungumzia wachezaji waliokosekana katika mechi hiyo kwa kile alichosema kwamba si haki kuzungumzia jambo hilo kwani tangu mwanzo wa msimu wamekuwa wakiwakosa wachezaji wengi karibu kila baada ya wiki.
Mabao ya Arsenal katika mechi hiyo yalifungwa na Trossard dakika ya nne wakati mengine yalifungwa na White dakika za 52 na 70 na Havertz dakika za 57 na 65.
Kwa ushindi huo Arsenal sasa inashika usukani EPL ikiwa imefikisha pointi 77 katika mechi 34 ikifuatiwa n Liverpool yenye pointi 74 katika mechi 33 wakati Chelsea imeshuka hadi nafasi ya tisa ikiwa na pointi 47 katika mechi 32.

The post Chelsea laini yamtesa Pochettino first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/24/chelsea-laini-yamtesa-pochettino/feed/ 0
Pochettino: Matajiri Chelsea wananisapoti https://www.greensports.co.tz/2024/02/28/pochettino-matajiri-chelsea-wananisapoti/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/28/pochettino-matajiri-chelsea-wananisapoti/#respond Wed, 28 Feb 2024 07:05:03 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9908 London, EnglandKocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino amesema anaungwa mkono na wamiliki wa klabu hiyo licha ya kuibuka presha baada ya kupoteza mechi ya fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Liverpool.Chelsea Jumapili iliyopita ililala mbele ya Liverpool kwenye mechi ya fainali kwa bao la dakika ya 118 lililofungwa na Virgil van Dijk na kumuwezesha kocha […]

The post Pochettino: Matajiri Chelsea wananisapoti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino amesema anaungwa mkono na wamiliki wa klabu hiyo licha ya kuibuka presha baada ya kupoteza mechi ya fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Liverpool.
Chelsea Jumapili iliyopita ililala mbele ya Liverpool kwenye mechi ya fainali kwa bao la dakika ya 118 lililofungwa na Virgil van Dijk na kumuwezesha kocha wa Liverpool Jurgen Klopp kubeba taji lake la nane na timu hiyo akiwa tayari ametangaza kujiondoa baada ya msimu huu.
Kitendo cha Chelsea kupoteza mechi mbele ya Liverpool iliyolazimika kuwatumia wachezaji makinda kutokana na janga la majeruhi, kimemuweka Pochettino pagumu na kujikuta akilaumiwa kwa kuongoza timu iliyofanya usajili wa mabilioni lakini haina kitu uwanjani.
Mabilionea wanaomiliki klabu ya Chelsea, Todd Boehly na Clearlake Capital tangu wainunue klabu hiyo Mei 2022 wanadaiwa kutumia Pauni 1 bilioni jambo ambalo ilitarajiwa lingekuwa na faida kwa kuipa ushindi timu hiyo.
“Ndio, ndio, ndio, wananipa sapoti na hata baada ya mechi Todd alinitumia ujumbe mzuri sana,” alisema Pochettino.

“Tunazungumza, niliwasalimia nilipowaona uwanjani na baada ya mechi usiku nilikutana nao na tulizungumza, tulipeana mawazo kuhusu mechi, tulizungumza kuhusu nafasi tulizopoteza ambazo zingetuwezesha kubeba taji kwa sababu nadhani tulicheza vizuri katika dakika 90 na nafikiri timu ilikuwa vizuri,” alisema Pochettino.


Chelsea Jumatano hii usiku itakuwa na mtihani mwingine dhidi ya Leeds United katika mechi ya raundi ya tano ya Kombe la FA itakayopigwa kwenye dimba la Stamford Bridge huku ikitarajiwa kumkosa nyota wake, Christopher Nkunku ambaye ni majeruhi.

The post Pochettino: Matajiri Chelsea wananisapoti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/28/pochettino-matajiri-chelsea-wananisapoti/feed/ 0
Chelsea laini yamkera Pochettino https://www.greensports.co.tz/2023/11/26/chelsea-laini-yamkera-pochettino/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/26/chelsea-laini-yamkera-pochettino/#respond Sun, 26 Nov 2023 17:59:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8640 London, EnglandKocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino (pichani) amekasirishwa kwa namna ambavyo timu yake imekuwa ‘laini’ na kukubali kichapo cha mabao 4-1 mbele ya Newcastle katika mechi iliyochezwa jana Jumamosi.Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England iliyopigwa kwenye dimba la St James, hadi mapumziko, Chelsea walikuwa tayari wamesawazisha bao moja walilofungwa kabla mambo hayajaharibika kipindi cha […]

The post Chelsea laini yamkera Pochettino first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino (pichani) amekasirishwa kwa namna ambavyo timu yake imekuwa ‘laini’ na kukubali kichapo cha mabao 4-1 mbele ya Newcastle katika mechi iliyochezwa jana Jumamosi.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England iliyopigwa kwenye dimba la St James, hadi mapumziko, Chelsea walikuwa tayari wamesawazisha bao moja walilofungwa kabla mambo hayajaharibika kipindi cha pili.
Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Chelsea ambayo ilijikuta ikibaki na wachezaji 10 uwanjani baada ya nahodha wa timu hiyo Reece James kutolewa nje.
Akizungumzia matokeo hayo, Pochettino ambaye alivutiwa na kiwango cha timu yake katika mechi na Tottenham, alisema matokeo ya Newcastle yamemkatisha tamaa kwa kile alichosema timu yake ilishindwa kupambana na kuwa laini.
“Hatukuonesha kwamba tulikuwa tunacheza katika mechi muhimu, tulitakiwa kuwaonesha kwamba mechi ingekuwa ngumu kwao, kwamba isingewezekana kucheza vizuri na kutushinda,” alisema Pochettino.
“Lakini ilikuwa rahisi mno kwa namna ambavyo tulikubali kufungwa, na kwa namna tulivyokuwa laini katika kila eneo la upambanaji,” alisema Pochettino.

“Na hilo ndilo lililonifanya niwe na hasira na kuvurugwa, tunazungumzia kuhusu timu yenye vijana na ni lazima tujifunze lakini nafikiri aina hii ya mechi inanifanya niwe mwenye hasira sana kwa sababu ni suala la kuonesha ubora na upambanaji,” alisema Pochettino.


Matokeo ya mechi za Jumamosi Ligi Kuu England…
Man City 1-1 Liverpool
Burnley 1-2 West Ham
Luton Town 2-1 Crystal Palace
Newcastle 4-1 Chelsea
Nottingham Forest 2-3 Brighton
Sheffield United 1-3 Bournemouth
Brentford 0-1 Arsenal

The post Chelsea laini yamkera Pochettino first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/26/chelsea-laini-yamkera-pochettino/feed/ 0
Liverpool yapigwa bao, Caicedo aelekea Chelsea https://www.greensports.co.tz/2023/08/13/liverpool-yapigwa-bao-caicedo-aelekea-chelsea/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/13/liverpool-yapigwa-bao-caicedo-aelekea-chelsea/#respond Sun, 13 Aug 2023 11:13:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7361 London, EnglandLiverpool huenda ikamkosa kiungo wa Brighton, Moises Caicedo (pichani) ambaye zipo habari kwamba Chelsea imempandia dau ikiwa tayari kutoa Pauni 115 milioni na haitoshangaza kiungo huyo akiachana na Liverpool.Hivi karibuni, Liverpool ilitangaza kukubali kumsajili kiungo huyo ambaye pia anaichezea timu ya Taifa ya Ecuador kwa ada ya Pauni 111 milioni, hiyo ni baada ya […]

The post Liverpool yapigwa bao, Caicedo aelekea Chelsea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Liverpool huenda ikamkosa kiungo wa Brighton, Moises Caicedo (pichani) ambaye zipo habari kwamba Chelsea imempandia dau ikiwa tayari kutoa Pauni 115 milioni na haitoshangaza kiungo huyo akiachana na Liverpool.
Hivi karibuni, Liverpool ilitangaza kukubali kumsajili kiungo huyo ambaye pia anaichezea timu ya Taifa ya Ecuador kwa ada ya Pauni 111 milioni, hiyo ni baada ya awali Chelsea kutangaza kumtaka mchezaji huyo.
Uamuzi wa Chelsea kuongeza nguvu na kumpandia dau kiungo huyo utaiweka Liverpool pagumu baada ya kuamini kuwa Caicedo angesaidia kuimarisha safu ya kiungo ya timu hiyo baada ya kuondoka kwa
Jordan Henderson na Fabinho waliotimkia Saudi Arabia.
Habari za ndani zinadai kwamba makubaliano ya awali baina ya Chelsea na Caicedo ni kwa mchezaji huyo kusaini mkataba utakaofikia mwisho Juni, 2031, ukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.
Liverpool pia huenda ikazidiwa ujanja na Chelsea katika kuisaka saini ya kiungo wa Ubelgiji, Romeo Lavia ambaye kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari anatarajia kuihama Southampton na kutua Chelsea kwa ada ya Pauni 55 milioni.
Liverpool mbali na Caicedo pia ilionesha nia ya kumtaka Romeo ilipokwama kumsajili kiungo Jude Bellingham kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani baada ya mchezaji huyo kujiunga na Real Madrid.
Mabosi wa Chelsea na Liverpool huenda wakakutana Stamford Bridge wakati timu zao zitakapoumana leo Jumapili katika mechi zao za kwanza za Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2023-24.
Huenda usajili wa Caicedo na Romeo ukawaweka katika wakati mgumu mabosi hao ambao wote watakaa jukwaa kuu katika viti vinavyokaliwa na watu maalum.

The post Liverpool yapigwa bao, Caicedo aelekea Chelsea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/13/liverpool-yapigwa-bao-caicedo-aelekea-chelsea/feed/ 0
Man United yamnasa Mason Mount https://www.greensports.co.tz/2023/06/30/man-united-yamnasa-mason-mount/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/30/man-united-yamnasa-mason-mount/#respond Thu, 29 Jun 2023 21:58:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6768 Manchester, EnglandKlabu ya Manchester United imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa Chelsea na timu ya Taifa ya England, Mason Mount kwa ada inayotajwa kufikia Pauni 60 milioni na mkataba wa miaka mitano.Man United imekuwa ikimuwinda mchezaji huyo katika siku za karibuni na sasa huo unakuwa usajili wa kwanza wa kocha Erik ten Hag katika kipindi […]

The post Man United yamnasa Mason Mount first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Klabu ya Manchester United imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa Chelsea na timu ya Taifa ya England, Mason Mount kwa ada inayotajwa kufikia Pauni 60 milioni na mkataba wa miaka mitano.
Man United imekuwa ikimuwinda mchezaji huyo katika siku za karibuni na sasa huo unakuwa usajili wa kwanza wa kocha Erik ten Hag katika kipindi hiki cha usajili cha majira ya kiangazi.
Ten Hag kwa sasa anahaha kukiimarisha kikosi chake ili kuhakikisha anafanya vizuri msimu ujao wa 2023-24 kwenye Ligi Kuu England (EPL) pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Msimu uliopita, Chelsea ilitumia Pauni 600 milioni na sasa klabu hiyo inahitajika kuuza baadhi ya wachezaji kabla ya Juni 30 ili kuondokana na hofu ya kubanwa na kanuni za matumizi ya fedha.
Chelsea haikuwa tayari kumuuza kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 lakini imewawia vigumu kusaini naye mkataba mpya hasa kwa kuwa mkataba wake wa sasa unafikia ukomo mwakani hivyo ingeweza kumuacha akaondoka bila ya wao kupata chochote.
Tayari Chelsea imeshawapiga bei Kai Havert katika klabu ya Arsenal na Mateo Kovacic aliyetua Man City wakati kipa Edouard Mendy, Kalidou Koulibaly na N’Golo Kante wameuzwa katika klabu za Al-Ahli na Al-Ittihad za Saudi Arabia.
Mount (pichani juu) ameifungia Chelsea mabao 33 katika mechi 195 za Chelsea tangu ajiunge na kikosi cha kwanza cha timu hiyo mwaka 2019, msimu huu umekuwa mgumu kwake kutokana na kuandamwa na majeraha lakini kwa ujumla Chelsea nayo haikuwa na msimu mzuri, imemaliza EPL ikiwa nafasi ya 12.
Mount alishiriki kikamilifu katika timu ya Chelsea iliyotwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2021 waikiibwaga Man City kwa bao 1-0 katika mechi ya fainali ambayo Mount alikuwamo kwenye kikosi cha kwanza.

The post Man United yamnasa Mason Mount first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/30/man-united-yamnasa-mason-mount/feed/ 0
Pochettino kocha mpya Chelsea https://www.greensports.co.tz/2023/05/14/pochettino-kocha-mpya-chelsea/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/14/pochettino-kocha-mpya-chelsea/#respond Sun, 14 May 2023 16:10:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6161 London, EnglandKlabu ya Chelsea hatimaye imefikia makubaliano na kocha wa zamani wa klabu za Tottenham Hotspur na PSG, Mauricio Pochettino ambaye sasa atakuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo.Pochettino (pichani) hivi karibuni amekuwa akitajwa kupewa jukumu la kuinoa Chelsea ambayo inanolewa na kocha wa muda Frank Lampard aliyekabidhiwa mikoba baada ya Graham Potter kutimuliwa.Kocha Pochettino […]

The post Pochettino kocha mpya Chelsea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Klabu ya Chelsea hatimaye imefikia makubaliano na kocha wa zamani wa klabu za Tottenham Hotspur na PSG, Mauricio Pochettino ambaye sasa atakuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo.
Pochettino (pichani) hivi karibuni amekuwa akitajwa kupewa jukumu la kuinoa Chelsea ambayo inanolewa na kocha wa muda Frank Lampard aliyekabidhiwa mikoba baada ya Graham Potter kutimuliwa.
Kocha Pochettino ambaye amekuwa bila ya kazi tangu majira ya kiangazi mwaka jana alipotimuliwa PSG, na nafasi yake kukabidhiwa Christophe Galtier, ataanza kazi rasmi mara baada ya msimu huu.
Pochettino mwenye umri wa miaka 51 ambaye pia amewahi kuinoa Southampton, anakuwa kocha wa sita wa Chelsea katika kipindi cha miaka mitano.
Chelsea imekuwa na msimu mbaya ikitolewa na Man City katika Kombe la FA na lile la Ligi na hivi karibuni imetolewa na Real Madrid katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kibaya zaidi ni kwamba kwa sasa inashika nafasi ya 11 kwenye Ligi Kuu England (EPL) ikiwa na rekodi ya kushinda mechi moja tu kati ya 11 zilizopita ikipoteza mechi nane na tayari imepoteza matumaini ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Machi mwaka huu baada ya Spurs kuachana na kocha Antonio Conte, Pochettino alikuwa akitajwa kurudi katika timu hiyo akikumbukwa kuiwezesha kufikia hatua ya fainali ya Kombe la Ligi mwaka 2015 na kuiwezesha kushika nafasi ya pili kwenye EPL msimu wa 2016-17.

The post Pochettino kocha mpya Chelsea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/14/pochettino-kocha-mpya-chelsea/feed/ 0
Lampard apata ushindi wa kwanza https://www.greensports.co.tz/2023/05/07/lampard-apata-ushindi-wa-kwanza/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/07/lampard-apata-ushindi-wa-kwanza/#respond Sun, 07 May 2023 13:09:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6045 London, EnglandHatimaye kocha wa muda wa Chelsea, Frank Lampard amepata ushindi wa kwanza na timu hiyo baada ya mechi sita wakiilaza, Bournemouth mabao 3-1 katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL) jana Jumamosi.Lampard, alikabidhiwa jukumu la kuinoa Chelsea mapema mwezi uliopita akichukua nafasi ya Graham Potter lakini amejikuta akiishuhudia timu hiyo ikichezea vichapo mfululizo zikiwamo […]

The post Lampard apata ushindi wa kwanza first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Hatimaye kocha wa muda wa Chelsea, Frank Lampard amepata ushindi wa kwanza na timu hiyo baada ya mechi sita wakiilaza, Bournemouth mabao 3-1 katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL) jana Jumamosi.
Lampard, alikabidhiwa jukumu la kuinoa Chelsea mapema mwezi uliopita akichukua nafasi ya Graham Potter lakini amejikuta akiishuhudia timu hiyo ikichezea vichapo mfululizo zikiwamo mechi nne za EPL na mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Conor Gallagher dakika ya tisa, Benoit Badiashile dakika ya 82 na Joao Felix dakika ya 86 wakati bao pekee la Bournemouth waliokuwa wenyeji likifungwa na Matias Vina dakika ya 21.
Katika mechi ya jana, Lampard aliamua kubadili kikosi akiwaacha benchi Pierre-Emerick Aubameyang na Raheem Sterling ambao walikuwamo katika kikosi kilichochapwa mabao 3-1 n Arsenal.
Matokeo hayo yanaiweka pagumu Bournemouth inayoandamwa na janga la kushuka daraja zikiwa zimebakia mechi tatu kabla ya ligi kumalizika huku Chelsea nayo ikiwa kwenye nafasi ya 11.
Na ingawa Bournemouth ina pointi tisa zaidi ukilinganisha na timu tatu zinazopambana mkiani lakini lolote linaweza kutokea hasa kwa kuwa baadhi ya timu zimebakiwa na mechi nne.
Matokeo mechi za EPL za Jumamosi ni kama ifuatavyo…
Bournemouth 1-3 Chelsea
Man City 2-1 Leeds
Tottenham 1-0 Crystal Palace
Wolves 1-0 Aston Villa
Liverpool 1-0 Brentford

The post Lampard apata ushindi wa kwanza first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/07/lampard-apata-ushindi-wa-kwanza/feed/ 0
Arsenal yarejea kileleni lakini… https://www.greensports.co.tz/2023/05/03/arsenal-yarejea-kileleni-lakini/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/03/arsenal-yarejea-kileleni-lakini/#respond Wed, 03 May 2023 12:43:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5992 London, EnglandArsenal jana Jumanne iliichapa Chelsea mabao 3-1 na kushika usukani wa Ligi Kuu England (EPL) ingawa huenda furaha yao ikafikia ukomo leo Jumatano usiku.Kwa ushindi huo Arsenal inaongoza ligi ikiwa na pointi 78 ikifuatiwa na Man City yenye pointi 76 ingawa City imecheza mechi 32 na Arsenal 34 na leo City inaumana na West […]

The post Arsenal yarejea kileleni lakini… first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Arsenal jana Jumanne iliichapa Chelsea mabao 3-1 na kushika usukani wa Ligi Kuu England (EPL) ingawa huenda furaha yao ikafikia ukomo leo Jumatano usiku.
Kwa ushindi huo Arsenal inaongoza ligi ikiwa na pointi 78 ikifuatiwa na Man City yenye pointi 76 ingawa City imecheza mechi 32 na Arsenal 34 na leo City inaumana na West Ham.
Ushindi wowote leo utaifanya City iiengue Arsenal kileleni na hivyo kuifanya timu hiyo iliyoshika usukani kwa muda mrefu kurejea katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Rekodi nzuri ya Arsenal ilianza kuharibika hivi karibuni baada ya kucheza mechi nne bila ushindi na hapo hapo ikaambulia kichapo mbele ya Man City ambao Jumapili waliwaengua Arsenal kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya ushindi walioupata kwa Fulham.
Mabao ya washindi katika mechi hiyo yalifungwa na Odegaard aliyefunga mawili na Gabriel Jesus aliyefunga bao moja wakati bao pekee la Chelsea lilifungwa na Madueke.
Kwa upande mwingine mambo yameendelea kuwa mabaya kwa Chelsea na kocha wao wa muda, Frank Lampard ambaye anaishuhudia timu hiyo ikipata kipigo cha sita mfululizo na hivyo kuzidisha habari kwamba kocha huyo hana nafasi au nafasi yake ndogo mno Chelsea.

The post Arsenal yarejea kileleni lakini… first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/03/arsenal-yarejea-kileleni-lakini/feed/ 0
Chelsea, Nagelsmann wateta https://www.greensports.co.tz/2023/04/17/chelsea-nagelsmann-wateta/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/17/chelsea-nagelsmann-wateta/#respond Mon, 17 Apr 2023 19:35:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5842 Munich, UjerumaniKlabu ya Chelsea inadaiwa kufanya mazungumzo na kocha wa zamani wa Bayern Munich, Julian Nagelsmann ili akabidhiwe mikoba ya kuinoa timu hiyo inayochechemea kwenye Ligi Kuu England.Kwa sasa timu hiyo inanolewa na kocha wa muda, Frank Lampard ambaye naye mambo hayaonekani kuwa mazuri huku mabosi wa timu hiyo wakianza kuwekeza nguvu kwa ajili ya […]

The post Chelsea, Nagelsmann wateta first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Klabu ya Chelsea inadaiwa kufanya mazungumzo na kocha wa zamani wa Bayern Munich, Julian Nagelsmann ili akabidhiwe mikoba ya kuinoa timu hiyo inayochechemea kwenye Ligi Kuu England.
Kwa sasa timu hiyo inanolewa na kocha wa muda, Frank Lampard ambaye naye mambo hayaonekani kuwa mazuri huku mabosi wa timu hiyo wakianza kuwekeza nguvu kwa ajili ya msimu ujao.
Katika hesabu za msimu ujao, moja ya kazi kubwa inayofanywa ni kumtafuta kocha atakayekabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo huku jina la Nagelsmann (pichani) likionekana kupewa nafasi kubwa.
Chelsea hivi karibuni ilimtimua kocha Graham Potter baada ya mambo kumuendea kombo. Potter alichukua jukumu la kuinoa timu hiyo kutoka kwa Thomas Tuchel ambaye naye alitimuliwa na kwa sasa anainoa Bayern Munich.
Iwapo Chelsea watafanikiwa kumchukua Nagelsmann, kocha huyo atakuwa kama amebadilishana timu na Tuchel ambaye kwa sasa anainoa Bayern timu iliyomtimua Nagelsmann hivi karibuni.
Kocha mwingine ambaye amekuwa akihusishwa na Chelsea, ni kocha wa zamani wa Barca, Luis Enrique ambaye amekuwa hana kazi tangu aachane na timu ya Taifa ya Hispania baada ya fainali za Kombe la Dunia za Qatar.

The post Chelsea, Nagelsmann wateta first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/17/chelsea-nagelsmann-wateta/feed/ 0
Lampard alaumu wachezaji Chelsea https://www.greensports.co.tz/2023/04/16/lampard-alaumu-wachezaji-chelsea/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/16/lampard-alaumu-wachezaji-chelsea/#respond Sun, 16 Apr 2023 12:25:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5834 London, EnglandKocha wa muda wa Chelsea, Frank Lampard amewalaumu wachezaji wake kwa kutokuwa wapambanaji na sasa ana kazi ya kuweka mambo sawa kabla ya mechi ya Jumanne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.Lampard alitoa kauli hiyo baada ya Chelsea ikiwa nyumbani kufungwa mabao 2-1 na Brighton na kubaki nafasi ya 11 kwenye […]

The post Lampard alaumu wachezaji Chelsea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa muda wa Chelsea, Frank Lampard amewalaumu wachezaji wake kwa kutokuwa wapambanaji na sasa ana kazi ya kuweka mambo sawa kabla ya mechi ya Jumanne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.
Lampard alitoa kauli hiyo baada ya Chelsea ikiwa nyumbani kufungwa mabao 2-1 na Brighton na kubaki nafasi ya 11 kwenye Ligi Kuu England huku ikipoteza matumaini ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

“Nimekatishwa tamaa katika kila eneo, timu nzuri ilishinda na ingeweza kushinda zaidi, walicheza kitimu, wanacheza kwa pamoja kwa muda mrefu, tuwape heshima yao,” alisema Lampard.


“Lakini kwa upande wetu haitoshi, mambo ya msingi katika soka, kupambana, kukimbia na mambo kama hayo tulikuwa na upungufu, ni lazima tutoke katika hilo kwa haraka sana,” alisema.
“Tuna mechi kubwa Jumanne, hatuhitaji kuwa nyuma, badala yake tuwe profesheno ni lazima tuelewe ni kwa nini leo (jana Jumamosi) tumefanya tulichofanya na hakikuwa kizuri kwa upande wetu,” aliongeza.
Chelsea imepoteza mechi zote tatu tangu Lampard akabidhiwe jukumu la kuinoa timu hiyo kutoka kwa Graham Potter lakini kocha huyo amedai kwamba kiwango cha timu hiyo katika mechi na Brighton ndicho kikilichomkatisha tamaa zaidi.

The post Lampard alaumu wachezaji Chelsea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/16/lampard-alaumu-wachezaji-chelsea/feed/ 0