Arsenal - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 09 Feb 2025 15:21:48 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Arsenal - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Arteta adai kukatishwa tamaa https://www.greensports.co.tz/2025/02/04/arteta-adai-kukatishwa-tamaa/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/04/arteta-adai-kukatishwa-tamaa/#respond Tue, 04 Feb 2025 19:36:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12974 London, EnglandKocha wa Arsenal, Mikel Arteta amedai kukatishwa tamaa baada ya timu hiyo kutofanya usajili wowote katika dirisha dogo ingawa amepongeza nidhamu ya timu.Awali zilikuwapo habari kwamba Arsenal ingesajili mshambuliaji baada ya Gabriel Jesus kupata matatizo ya misuli mwishoni mwa mwezi uliopita wakati Bukayo Saka naye akiwa na tatizo linalofanana na hilo na wote wakishindwa […]

The post Arteta adai kukatishwa tamaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amedai kukatishwa tamaa baada ya timu hiyo kutofanya usajili wowote katika dirisha dogo ingawa amepongeza nidhamu ya timu.
Awali zilikuwapo habari kwamba Arsenal ingesajili mshambuliaji baada ya Gabriel Jesus kupata matatizo ya misuli mwishoni mwa mwezi uliopita wakati Bukayo Saka naye akiwa na tatizo linalofanana na hilo na wote wakishindwa kuiwakilisha timu hiyo.
Arteta alisema dhamira yao ilikuwa wazi kwamba baada ya dirisha la usajili kufunguliwa walitakiwa kuangalia fursa za kusajili ili kuimarisha kikosi kwa kusajili wachezaji ambao wangekuwa msaada kwa timu.
Arteta ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja kabla ya Arsenal kujitupa dimbani kuikabili Newcastle katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la EFL itakayopigwa kesho Jumatano.

“Kutokana na wachezaji kuwa majeruhi tulijipa matumaini, hatujayafikia, imetukatisha tamaa lakini hapo hapo tunafahamu kwamba tulitakiwa kusajili aina fulani ya wachezaji na tunatakiwa pia kuwa na nidhamu katika hilo, nafikiri la la nidhamu tuko sawa,” alisema Arteta.


Arteta alisema kuna mchezaji ambaye waliamini angewafanya wawe bora zaidi ingawa alifafanua kuwa katika masuala ya kifedha pia kuna mambo mengi ambayo ni lazima wayasimamie na ndiyo yaliyowafikisha walipofika na kuanzia hapo wanajaribu kuwa bora zaidi.
Arsenal ambayo mwishoni mwa wiki iliyopita iliibugiza Man City mabao 5-1, kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu England (EPL) ikiwa imezidiwa na vinara wa ligi hiyo, Liverpool kwa tofauti ya pointi sita.

The post Arteta adai kukatishwa tamaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/04/arteta-adai-kukatishwa-tamaa/feed/ 0
Arsenal matatani kwa kumzonga refa https://www.greensports.co.tz/2025/01/30/arsenal-matatani-kwa-kumzonga-refa/ https://www.greensports.co.tz/2025/01/30/arsenal-matatani-kwa-kumzonga-refa/#respond Thu, 30 Jan 2025 17:04:19 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12954 London, EnglandChama cha Soka England (FA) kimeikuta na hatia klabu ya Arsenal baada ya wachezaji wake kumzonga mwamuzi Michael Oliver wakipinga kadi nyekundu aliyompa, Myles Lewis katika mechi yao na Wolves.Oliver alimpa Lewis kadi nyekundu kipindi cha kwanza baada ya nyota huyo wa miaka 18 kumchezea rafu Matt Doherty na mwamuzi kutafsiri tukio hilo kuwa […]

The post Arsenal matatani kwa kumzonga refa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Chama cha Soka England (FA) kimeikuta na hatia klabu ya Arsenal baada ya wachezaji wake kumzonga mwamuzi Michael Oliver wakipinga kadi nyekundu aliyompa, Myles Lewis katika mechi yao na Wolves.
Oliver alimpa Lewis kadi nyekundu kipindi cha kwanza baada ya nyota huyo wa miaka 18 kumchezea rafu Matt Doherty na mwamuzi kutafsiri tukio hilo kuwa ni rafu mbaya.
Arsenal waliipinga kadi hiyo na hatimaye sasa imefutwa na hivyo mchezaji huyo kufutiwa adhabu ya kukosa mechi tatu aliyopaswa kuitumikia ingawa klabu hiyo imeponzwa na tuki la wachezaji wake kumzonga na kumbughudhi mwamuzi.
Arsenal ambayo ilitoka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi hiyo, baada ya kukutwa na hatia, klabu hiyo imepewa muda hadi Februari 3 iwe imejibu kwa FA kuhusu suala hilo.
Maofisa wa timu ya waamuzi wamedai kuwa Polisi wamekuwa katika uchunguzi wa tukio hilo yakiwamo madai ya vitisho na lugha zisizofaa alizokuwa akitamkiwa Oliver.
Kwa mujibu wa FA, klabu ya Arsenal imeingia matatani kwa kosa la kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake na kuhakikisha hawafanyi mambo yaliyo kinyume na taratibu za soka.
Wakati wa faulo hiyo, Dogerty alikuwa nje ya eneo la penalti wakati akijaribu kufanya shambulizi la kushtukiza katika dakika ya 43 na ndipo alipokwatuliwa na Lewis na mwamuzi kutoa kadi nyekundu hapo hapo.
Uamuzi wa kumpa kadi nyekundu Lewis ingawa ulipata baraka zote ikiwamo matumizi ya VAR lakini umeibua maoni tofauti kwa wachambuzi mbalimbali huku kocha wa Arsenal Mikel Arteta akikiri kukerwa na kadi hiyo.

The post Arsenal matatani kwa kumzonga refa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/01/30/arsenal-matatani-kwa-kumzonga-refa/feed/ 0
Ndoto za Arteta kubeba taji EPL zipo hai https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/ndoto-za-arteta-kubeba-taji-epl-zipo-hai/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/ndoto-za-arteta-kubeba-taji-epl-zipo-hai/#respond Sat, 18 May 2024 17:17:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11015 London, EnglandKocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema ndoto zake za kubeba taji la Ligi Kuu England (EPL) kesho Jumapili zipo hai wakati huu akijiandaa kwa mechi ya mwisho iliyobeba hatma ya timu yake katika taji hilo.Mabingwa watetezi, Man City wanashika usukani wa ligi hiyo wakiwazidi Arsenal walio nafasi ya pili kwa pointi mbili wakati Jumapili […]

The post Ndoto za Arteta kubeba taji EPL zipo hai first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema ndoto zake za kubeba taji la Ligi Kuu England (EPL) kesho Jumapili zipo hai wakati huu akijiandaa kwa mechi ya mwisho iliyobeba hatma ya timu yake katika taji hilo.
Mabingwa watetezi, Man City wanashika usukani wa ligi hiyo wakiwazidi Arsenal walio nafasi ya pili kwa pointi mbili wakati Jumapili timu hizo kila moja itacheza mechi yake ya mwisho ya kufunga msimu.
Arsenal ili itwae taji hilo italazimika kushinda mechi hiyo dhidi ya Everton wakati huo huo ikiombea mabingwa watetezi Man City wapoteze au walau watoke sare mechi yao dhidi ya West Ham.
“Tulitaka kuwa katika nafasi hii, tumeshinda yote hadi kufikia hapa katika siku nzuri mbele ya watu wetu hapo Jumapili tukiwa na matumaini katika fursa hii kubwa kwamba tutabeba taji mwisho wa mechi hii,” alisema Arteta.

“Tuna uwezekano wa kuifurahia siku hii nzuri ya Jumapili, siku ambayo ndoto zetu bado zipo hai na bado tunaamini inawezekana, haya ndiyo mambo ya soka,” alisema Arteta.


Arteta anaelewa Man City ndiyo iliyo juu katika mbio za kulisaka taji hilo lakini ameamua kuweka nguvu na umakini katika mechi na Everton akiamini lolote linaweza kutokea katika mechi ya Man City na West Ham.
Artete ambaye amewahi kuwa mchezaji Arsenal hakuwahi kulibeba taji la EPL wakati huo na sasa anaamini litakuwa jambo kubwa kufanya hivyo na hiyo ni moja ya ndoto zake.
Mara ya mwisho Arsenal kubeba taji la EPL ilikuwa msimu wa 2003-04 wakati Man City inawania kuweka rekodi ya kulibeba taji hilo kwa mara ya nne mfululizo.

The post Ndoto za Arteta kubeba taji EPL zipo hai first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/ndoto-za-arteta-kubeba-taji-epl-zipo-hai/feed/ 0
City yaiweka pagumu Arsenal https://www.greensports.co.tz/2024/04/26/man-city-yaiweka-pagumu-arsenal/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/26/man-city-yaiweka-pagumu-arsenal/#respond Fri, 26 Apr 2024 20:59:30 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10752 London, EnglandMan City imeiweka pagumu Arsenal katika mbio za kuliwania taji la Ligi Kuu England (EPL) baada ya kuichapa Brighton mabao 4-0 na kuchupa hadi nafasi ya pili ikiachwa na Arsenal kwa tofauti ya pointi moja.Arsenal inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 77 katika michezo 34 wakati Man City inayoshika nafasi ya pili hadi sasa […]

The post City yaiweka pagumu Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Man City imeiweka pagumu Arsenal katika mbio za kuliwania taji la Ligi Kuu England (EPL) baada ya kuichapa Brighton mabao 4-0 na kuchupa hadi nafasi ya pili ikiachwa na Arsenal kwa tofauti ya pointi moja.
Arsenal inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 77 katika michezo 34 wakati Man City inayoshika nafasi ya pili hadi sasa imecheza michezo 33 na imebakiza mechi tano kabla ya kuhitimisha mbio za EPL.
Kwa msimamo huo maana yake ni kwamba Mikel Arteta na Arsenal yake ili waweze kulibeba taji la EPL msimu huu si tu kwamba wanatakiwa washinde mechi zao zote zilizobaki bali pia waiombee Man City ipate matokeo mabaya.
Liverpool inayoshika nafasi ya tatu japo si sahihi kuitoa moja kwa moja katika mbio hizo lakini baada ya kupoteza mechi yake na Everton ni kama vile nayo imejiweka pagumu kwani ina pointi 74 katika mechi 34.
Kwa Liverpool nayo si tu kwamba inatakiwa ishinde mechi zake zote zilizobaki bali nayo pia inatakiwa kuiombea Arsenal iteleze na pia inatakiwa ifanye maombi kama hayo dhidi ya Man City.


Kwa jinsi hali ilivyo sasa, vita kubwa zaidi ni kwa Arsenal na Man City na kwa kuwa Man City ina faida ya mechi moja basi haitokuwa ajabu timu hiyo ikifanikiwa kulitetea vyema taji la ligi hiyo.
Man City ikiwa chini ya kocha Pep Guardiola katika mechi yake na Brighton iliyopigwa jana Alhamisi kwenye Uwanja wa Amex, mabao yaliyoipa timu hiyo pointi tatu yalifungwa na Kevin de Bruyne kwa kichwa katika dakika ya 17.
Man City waliongeza mabao mengine mawili yaliyofungwa na Phil Foden katika dakika za 26 na 34 kabla ya Alvarez kufunga ukurasa wa mabao kwa kupachika bao la nne katika dakika ya 62.

The post City yaiweka pagumu Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/26/man-city-yaiweka-pagumu-arsenal/feed/ 0
Jesus awaambia Bayern, Arsenal si watoto tena https://www.greensports.co.tz/2024/04/09/jesus-awaambia-bayern-arsenal-si-watoto/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/09/jesus-awaambia-bayern-arsenal-si-watoto/#respond Tue, 09 Apr 2024 08:25:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10561 London, EnglandKocha wa Bayern Munich, Thomas Tuchel amesema uzoefu wao mkubwa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya utakuwa faida kubwa katika mechi na Arsenal leo Jumanne ingawa nyota wa Arsenal, Gabriel Jesus ameionya timu hiyo akisema kwamba wao si watoto tena.Timu hizo zinaumana katika mechi ya robo fainali ya ligi hiyo huku Tuchel akisema wanajua namna […]

The post Jesus awaambia Bayern, Arsenal si watoto tena first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Bayern Munich, Thomas Tuchel amesema uzoefu wao mkubwa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya utakuwa faida kubwa katika mechi na Arsenal leo Jumanne ingawa nyota wa Arsenal, Gabriel Jesus ameionya timu hiyo akisema kwamba wao si watoto tena.
Timu hizo zinaumana katika mechi ya robo fainali ya ligi hiyo huku Tuchel akisema wanajua namna ya kuiumiza Arsenal ambayo mafanikio yao makubwa katika ligi hiyo mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2006 walipofikia hatua ya fainali.
“Tuna uzoefu zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa, ligi hii ni tofauti na Ligi Kuu England (EPL), tunataka kuitumia faida hiyo,” alisema Tuchel.
Tuchel (pichani chini) ambaye ataachana na timu hiyo baada ya msimu huu hata hivyo alisema ni sahihi kwa timu yake kukoselewa kwa kuwa imekosa matokeo bora ikiwamo kwenye Ligi Kuu Ujerumani yaani Bundesliga.
Wakati hali ikiwa hivyo kwa Bayern, Arsenal imekuwa na mwenendo mzuri na ni kati ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kulibeba taji la EPL msimu huu.
Kwa upande wake Jesus amewaonya Bayern akisema Arsenal si watoto tena na sasa wanawania kufikia hatua ya nusu fainali ambayo mara ya mwisho waliifikia mwaka 2006.
“Kama nitaona jambo naweza kuwaambia na kuwasaidia (wachezaji wenzangu) nitafanya hivyo lakini sidhani kama hapa bado kuna watoto kila mmoja ameshacheza hatua kubwa kwenye soka, Kombe la Dunia, ligi kuu na sasa ligi ya mabingwa, kwa hiyo nafikiri kila mmoja wetu yuko tayari kuisaidia Arsenal,” alisema Jesus.


Jesus alisema msimu uliopita walicheza soka la uhakika katika sehemu kubwa ya mwanzo ya msimu hadi Januari na baada ya hapo hali ikawa kidogo si nzuri, msimu huu imekuwa kinyume chake.
Bayern katika mechi ya leo itamtegemea Harry Kane kuongoza mashambulizi, mshambuliaji ambaye tayari ameonesha ubora wa kuzifumania nyavu katika msimu wake wa kwanza tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Tottenham.
Hadi sasa Kane ana mabao 38 katika mechi 37 na hivyo usajili wake ulioigharimu Bayern Dola 130 milioni umeonekana kulipa licha ya kiujumla timu hiyo kutokuwa na mwenendo mzuri.

“Kila mtu anajua ubora wa Harry Kane, kwangu mimi huyu ni mfungaji bora duniani, kwa hiyo ni jambo kubwa kucheza na timu yenye wachezaji wa aina hii lakini tunataka kumnyamazisha, na baada ya hapo tujaribu kushinda mechi,” alisema Jesus.


“Pia si Harry Kane pekee, lakini kuna wachezaji wengi kama Sane (Leroy) rafiki yangu wa zamani, Musiala (Jamal) Coman, Muller (Thomas) Gnabry, ni wengi, wana wachezaji wa hadhi ya juu,” alisema Jesus.
Mechi za leo Jumanne Ligi ya Mabingwa Ulaya
Arsenal v Bayern Munich
Real Madrid v Man City

The post Jesus awaambia Bayern, Arsenal si watoto tena first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/09/jesus-awaambia-bayern-arsenal-si-watoto/feed/ 0
Arsenal yashika usukani EPL https://www.greensports.co.tz/2024/03/10/arsenal-yashika-usukani-epl/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/10/arsenal-yashika-usukani-epl/#respond Sun, 10 Mar 2024 11:05:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10119 London, EnglandArsenal hatimaye imefanikiwa kushika usukani wa Ligi Kuu England (EPL) kwa mara ya kwanza tangu Desemba mwaka jana baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Brentford ingawa huenda ikakaa kileleni muda usiozidi saa 24.Ushindi huo wa Jumamosi hii jioni ulitokana na mabao ya Declan Rice dakika ya 19 na Kai Havert dakika ya […]

The post Arsenal yashika usukani EPL first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Arsenal hatimaye imefanikiwa kushika usukani wa Ligi Kuu England (EPL) kwa mara ya kwanza tangu Desemba mwaka jana baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Brentford ingawa huenda ikakaa kileleni muda usiozidi saa 24.
Ushindi huo wa Jumamosi hii jioni ulitokana na mabao ya Declan Rice dakika ya 19 na Kai Havert dakika ya 86 wakati bao pekee la Brentford lilipatikana dakika ya 45 mfungaji akiwa ni Yoane Wissa,
Matokeo hayo yameifanya Arsenal kufikisha pointi 64 katika mechi 28 ikifuatiwa na Liverpool inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 63 na Man City ya tatu yenye pointi 62,
Man City na Liverpool kila moja imecheza mechi 27 na Jumapili hii timu hizo zinaumana katika mechi ngumu ambayo matokeo yake yatakuwa sababu ya kuiengua Arsenal kileleni mwa msimamo huo.
Faraja pekee kwa Arsenal ni timu hizo kutoka sare ambayo itaifanya Liverpool kufikisha pointi 64 kama za Arsenal na hivyo kushindana kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa na Man City watafikisha pointi 63 na kuendelea kuwa nyuma ya Arsenal.
Tofauti na matokeo hayo ushindi wa aina yoyote katika mechi hiyo utaitoa Arsenal kileleni, Liverpool ikishinda itakuwa imefikisha pointi 66 wakati Man City ikishinda itakuwa imefikisha pointi 65.
Matokeo ya mechi za EPL Jumamosi hii…
Man Utd 2-0 Everton
Bournemouth 2-2 Sheff Utd
Crystal Palace 1-1 Luton
Wolves 2-1 Fulham
Arsenal 2-1 Brentford

The post Arsenal yashika usukani EPL first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/10/arsenal-yashika-usukani-epl/feed/ 0
Arteta akataa kuilaumu VAR https://www.greensports.co.tz/2023/12/29/arteta-akataa-kuilaumu-var/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/29/arteta-akataa-kuilaumu-var/#respond Fri, 29 Dec 2023 18:14:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9065 London, England Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amekataa kuitupia lawama teknolojia ya VAR baada ya timu yake kufungwa mabao 2-0 na West Ham badala yake amesema kwamba timu yake ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga. Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England (EPL) iliyopigwa jana Alhamisi, West Ham ilipata bao la kwanza dakika ya 13, bao […]

The post Arteta akataa kuilaumu VAR first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amekataa kuitupia lawama teknolojia ya VAR baada ya timu yake kufungwa mabao 2-0 na West Ham badala yake amesema kwamba timu yake ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga.

Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England (EPL) iliyopigwa jana Alhamisi, West Ham ilipata bao la kwanza dakika ya 13, bao lililozua mjadala na kulazimika kutumia teknolojia ya VAR kwa kilichoonekana kuwa mpira huo uliokolewa.

Bao hilo liliwakumbusha mashabiki bao pekee la ushindi la Newcastle katika mechi dhidi ya Arsenal iliyopigwa Septemba mwaka huu, bao ambalo nalo lilizua utata kiasi cha Arteta kulaumu matumizi ya VAR na kudai kuwa bao hilo ni aibu na fedheha katika EPL.
West Ham iliandika bao lake la pili dakika ya 55 lililofungwa na Konstantinos Mavropanos, matokeo ambayo yameinyima Arsenal nafasi ya kumaliza mechi 19 za mzunguko wa kwanza ikiwa kileleni. Akizungumzia bao la West Ham Arteta alisema ni aibu kwamba pamoja na uwapo wa teknolojia bado kunakuwa na mjadala wa kama bao liliingia au halikuingia lakini mwisho wa siku hawana la kufanya.
Arsenal ilipiga mashuti 30 kwenye lango la West Ham na kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa kwenye eneo la wapinzani wao lakini hayo yote hayakuweza kuwasaidia kupata ushindi.

“Kama hatukufunga bao katika mashuti 30 maana yake ni kwamba tunatakiwa kujaribu kupiga mashuti 50 au 60 ili kufunga goli, hilo ndilo jambo pekee la kufanya,” alisema Arteta.

Kwa upande wake kocha wa West Ham, David Moyes alielezea furaha yake baada ya ushindi huo na kusema kwamba hivi karibuni atakaa na mabosi wake kujadili mpango wa kusaini mkataba mpya wakati mkataba wake wa sasa unafikia mwisho baada ya msimu huu.

The post Arteta akataa kuilaumu VAR first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/29/arteta-akataa-kuilaumu-var/feed/ 0
Luiz wa Villa atakiwa Arsenal https://www.greensports.co.tz/2023/11/29/luiz-wa-villa-atakiwa-arsenal/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/29/luiz-wa-villa-atakiwa-arsenal/#respond Wed, 29 Nov 2023 06:59:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8668 London, EnglandArsenal inataka kufanya mabadiliko kidogo katika safu ya kiungo ikiwania kumsajili kiungo wa Aston Villa, Douglas Luiz katika dirisha dogo la Januari huku majaliwa ya Thomas Partey yakiwa njia panda.Hii si mara ya kwanza Arsenal kumtaka Luiz, jaribio la kwanza lilikuwa Septemba mwaka jana ambapo ofa ya Pauni milioni 25 iliyowasilishwa na timu hiyo, […]

The post Luiz wa Villa atakiwa Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Arsenal inataka kufanya mabadiliko kidogo katika safu ya kiungo ikiwania kumsajili kiungo wa Aston Villa, Douglas Luiz katika dirisha dogo la Januari huku majaliwa ya Thomas Partey yakiwa njia panda.
Hii si mara ya kwanza Arsenal kumtaka Luiz, jaribio la kwanza lilikuwa Septemba mwaka jana ambapo ofa ya Pauni milioni 25 iliyowasilishwa na timu hiyo, Villa waliikataa kabla ya mchezaji huyo kusaini mkataba mpya na Villa unaofikia ukomo mwaka 2026.
Kiwango cha Luiz hasa msimu huu kimeendelea kuishawishi Arsenal kuendelea na mipango ya kumsajili ikiamini mchezaji huyo anaweza kuwa msaada mkubwa kwa timu hiiyo katika michuano inayoshiriki.
Luiz, nyota Mbrazili, hadi sasa amecheza mechi zote 13 za Ligi Kuu England akiiwakilisha vyema Villa ambayo inashika nafasi ya nne katika ligi hiyo baada ya Jumapili kuichapa Tottenham mabao 2-1.
Arsenal haionekani kukata tamaa katika mbio za kumsaka mchezaji huyo lakini kilichopo ni kwamba italazimika kuboresha ofa yake ili kuishawishi Villa imuachie katikati ya msimu hasa kutokana na mafanikio ambayo timu hiyo imeanza kuyaona.
Tatizo linaloikabili Arsenal ni ufinyu wa bajeti licha ya kuhitaji kwa hali na mali huduma ya Luiz na ili kufanikisha hilo huenda ikalazimika kumpiga bei Partey ambaye hadi sasa ameanza mechi tatu tu za msimu huu akiandamwa na matatizo ya misuli.

The post Luiz wa Villa atakiwa Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/29/luiz-wa-villa-atakiwa-arsenal/feed/ 0
Arsenal yaua, Nketiah apiga hat trick https://www.greensports.co.tz/2023/10/29/arsenal-yaua-nketiah-apigia-hat-trick/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/29/arsenal-yaua-nketiah-apigia-hat-trick/#respond Sat, 28 Oct 2023 21:03:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8266 London, EnglandEddie Nketiah kwa mara ya kwanza ameifungia Arsenal mabao matatu (hat trick) wakati timu hiyo ikiichapa Sheffield United 5-0 katika mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Emirates.Ushindi huo ambao umemfanya Nketiah aondoke uwanjani na mpira wa mechi hiyo pia umeipaisha Arsenal hadi nafasi ya pili katika ligi nyuma ya […]

The post Arsenal yaua, Nketiah apiga hat trick first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Eddie Nketiah kwa mara ya kwanza ameifungia Arsenal mabao matatu (hat trick) wakati timu hiyo ikiichapa Sheffield United 5-0 katika mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Emirates.
Ushindi huo ambao umemfanya Nketiah aondoke uwanjani na mpira wa mechi hiyo pia umeipaisha Arsenal hadi nafasi ya pili katika ligi nyuma ya mahasimu wao wa London, Tottenham Hotspur ambao wanashika usukani.
Nketiah (pichani juu) ambaye alipata nafasi kikosi cha kwanza baada ya kuumia kwa Gabriel Jesus, aliitumia nafasi hiyo vizuri na kufungua ukurasa wa mabao katika dakika ya 28 akiitumia vizuri pasi ya Declan Rice.
Katika mechi hiyo ambayo Arsenal iliitawala vyema, Nketiah alifunga mabao mengine katika dakika za 50 na 58 wakati mabao mengine yalifungwa na Fabio Vieira (kwa penalti) dakika ya 88 na Tomiyasu aliyefunga la tano katika dakika za nyongeza.
Nketiah angeweza kutoka uwanjani na mabao manne kama asingemuachia Vieira apige mkwaju wa penalti iliyotolewa baada ya Vieira kuchezewa rafu na Oliver Norwood.
Kama mchezaji huyo angepiga penalti na kufunga bao la nne angekuwa mchezaji wa tatu wa Arsenal kufunga idadi hiyo ya mabao kwenye mechi ya ligi, wengine ni Thierry Henry na Andrey Arshavin.

“Ni maajabu haikuwa rahisi, mwezi uliopita nilimpoteza shangazi yangu, kwa hiyo nataka niyatoe mabao haya matatu kama heshima kwake, familia yake ilikuwa hapa ikiangalia kwa hiyo hakika ni tukio la kipekee,” alisema Nketiah baada ya mechi hiyo.


Akizungumzia tukio la penalti hiyo, Nketiah alisema kwamba awali akili ilimtuma kuuchukua mpira huo ili apige penalti, “Fabio aliuwahi na lilikuwa tukio zuri, ni suala la mchezaji kwenye timu moja, ni kupata nafasi na kuitumia.”
Matokeo ya mechi za Ligi Kuu England leo Jumamosi…
Chelsea 0-2 Brentford
Arsenal 5-0 Sheff Utd
Bournemouth 2-1 Burnley
Wolves 2-2 Newcastle

The post Arsenal yaua, Nketiah apiga hat trick first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/29/arsenal-yaua-nketiah-apigia-hat-trick/feed/ 0
Arteta akiri kuumia Saka pigo Arsenal https://www.greensports.co.tz/2023/10/04/arteta-akiri-kuumia-saka-pigo-arsenal/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/04/arteta-akiri-kuumia-saka-pigo-arsenal/#respond Wed, 04 Oct 2023 08:26:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7940 Lens, UfaransaKocha wa Arsenal, Mikel Arteta amekiri kuumia kwa Bukayo Saka (pichani) ni jambo lililoleta hofu ingawa hajutii kumpanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana Jumanne dhidi ya Lens, mechi ambayo Arsenal ililala kwa mabao 2-1.Saka aliumia katika mechi mbili za Ligi Kuu England lakini katika hali ambayo haikutarajiwa alipangwa katika mechi ya […]

The post Arteta akiri kuumia Saka pigo Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Lens, Ufaransa
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amekiri kuumia kwa Bukayo Saka (pichani) ni jambo lililoleta hofu ingawa hajutii kumpanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana Jumanne dhidi ya Lens, mechi ambayo Arsenal ililala kwa mabao 2-1.
Saka aliumia katika mechi mbili za Ligi Kuu England lakini katika hali ambayo haikutarajiwa alipangwa katika mechi ya jana kwenye dimba la Bollaert-Delelis na kucheza kwa dakika 34 kabla ya kutolewa akiwa na maumivu ya misuli.
Mchezaji huyo ndiye aliyepika bao la kwanza la Arsenal lililofungwa na Gabriel Jesus lakini Lens walisawazisha kupitia Adrien Thomasson kabla ya kuongeza la pili lililofungwa na Elye Wahi na kuwa kipigo cha kwanza kwa Arsenal tangu kuanza kwa msimu huu.
Saka ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya England anatarajia kufanyiwa vipimo ili kujua ukubwa wa majeraha aliyonayo lakini ana uwezekano mdogo wa kucheza mechi ya Jumapili ya Ligi Kuu England (EPL) dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Man City.
“Alijaribu kupiga mpira kwa nyuma katika kipindi cha kwanza na akajikuta katika hali tofuati, ni tatizo la misuli, alijisikia vibaya na tukalazimika kumtoa nje,” alisema Arteta.

“Hatuna tunachojua zaidi ya hilo lakini ni wazi lilikuwa tatizo kubwa la kumzuia kuendelea kucheza na hilo ni dhahiri kwamba linatupa hofu, sina ninachojua kuhusu mechi ijayo, sijui,” alisema Arteta.


Alipoulizwa kama anajuta kumpanga Saka katika mechi hiyo, Arteta alisema, “hapana, ni maumivu aliyoyapata siku nyingine na akawa vizuri kabisa, ni tukio la kupiga mpira kwa nyuma ambalo linaweza kusababisha aina hii ya maumivu, ngoja tujue ukubwa wa tatizo.”
“Maumivu yaliyopita yalikuwa ya kawaida, hakukosa mechi nyingi, tulimpumzisha katika mechi na Brentford, hivyo ndivyo ilivyokuwa,” alisema Arteta.

The post Arteta akiri kuumia Saka pigo Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/04/arteta-akiri-kuumia-saka-pigo-arsenal/feed/ 0