Antonio Conte - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 27 Mar 2023 06:29:30 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Antonio Conte - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Conte ang’atuka Spurs https://www.greensports.co.tz/2023/03/27/conte-angatuka-spurs/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/27/conte-angatuka-spurs/#respond Mon, 27 Mar 2023 06:29:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5608 London, EnglandBaada ya kumshutumu mmiliki wa klabu ya Tottenham Hotspur na wachezaji wa timu hiyo akidai ni wabinafsi, hatimaye kocha Antonio Conte ametangaza kung’atuka kuinoa timu hiyo.Mara baada ya Conte kuchukua uamuzi huo binafsi jana Jumapili jioni, msaidizi wake, Cristian Stellini amekabidhiwa majukumu ya Conte na Ryan Mason ameteuliwa kuwa msaidizi wa Stellini.Wiki iliyopita, Conte […]

The post Conte ang’atuka Spurs first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Baada ya kumshutumu mmiliki wa klabu ya Tottenham Hotspur na wachezaji wa timu hiyo akidai ni wabinafsi, hatimaye kocha Antonio Conte ametangaza kung’atuka kuinoa timu hiyo.
Mara baada ya Conte kuchukua uamuzi huo binafsi jana Jumapili jioni, msaidizi wake, Cristian Stellini amekabidhiwa majukumu ya Conte na Ryan Mason ameteuliwa kuwa msaidizi wa Stellini.
Wiki iliyopita, Conte aliyekuwa kocha wa Spurs kwa miezi 16 iliyopita alimshutumu mwenyekiti na mmiliki wa klabu hiyo, Dany Levy akimshangaa kuimiliki klabu kwa muda mrefu bila mafanikio yoyote.
Kauli hiyo ya Conte ilitafsiriwa kwamba ni ama alijiandaa kwa lolote lakini kwa wengi iliaminika kwamba siku zake katika klabu hiyo zilikuwa zikihesabika.
Spurs kwa sasa inashika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu England (EPL) na matumaini ya kubeba taji lolote msimu huu yakizidi kuyeyuka baada ya kutolewa katika mshindano mengine jambo lililosababisha kuyumba kwa uhusiano kati ya Conte na mabosi wake.
Akizungumza mara baada ya Conte kutangaza kuondoka katika klabu hiyo, Levy alisema, “Tuna mechi 10 za ligi kuu zimebaki na tuna vita ya kupigania kusaka nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa.”

“Sote tunahitaji kuweka mambo yetu pamoja, kila mmoja anatakiwa kujiweka sawa kuhakikisha tunamaliza tukiwa juu kadri iwezekanavyo kwa ajili ya klabu yetu na mashabiki wetu,” alisema Levy.


The post Conte ang’atuka Spurs first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/27/conte-angatuka-spurs/feed/ 0
Conte: Wachezaji Spurs wabinafsi https://www.greensports.co.tz/2023/03/19/conte-wachezaji-spurs-wabinafsi/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/19/conte-wachezaji-spurs-wabinafsi/#respond Sun, 19 Mar 2023 11:37:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5538 London, EnglandKocha wa Tottenham, Antonio Conte amewatupia lawama wachezaji wake akidai ni wabinafsi na kumshutumu mmiliki wa klabu kwa kuimiliki kwa muda mrefu bila kushinda lolote.Conte ameshusha tuhuma hizo baada ya sare ya mabao 3-3 jana Jumamosi dhidi ya Southampton akidai klabu hiyo inaweza kumtimua kocha lakini mambo hayatobadilika huku akidai wachezaji hawataki kusaidiana“Hadithi ya […]

The post Conte: Wachezaji Spurs wabinafsi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Tottenham, Antonio Conte amewatupia lawama wachezaji wake akidai ni wabinafsi na kumshutumu mmiliki wa klabu kwa kuimiliki kwa muda mrefu bila kushinda lolote.
Conte ameshusha tuhuma hizo baada ya sare ya mabao 3-3 jana Jumamosi dhidi ya Southampton akidai klabu hiyo inaweza kumtimua kocha lakini mambo hayatobadilika huku akidai wachezaji hawataki kusaidiana
“Hadithi ya Tottenham ni hii ya miaka 20 ambapo kuna huyu mmiliki na hawajawahi kushinda chochote. Kwa nini?” Alihoji Conte.
Tottenham au Spurs ilikuwa ikiongoza kwa mabao mawili lakini katika dakika 15 ilijikuta ikifungwa mara mbili jambo ambalo ni kama liliamsha hasira za Conte katika mechi hiyo.
“Je tatizo ni kwa klabu tu au kwa kila kocha anayekuwa hapa? Nimewaona makocha ambao Tottenham inakuwa nao kwenye benchi, unajiweka katika hali hatarishi ya kumvuruga kocha na kulinda mazingira mengine kila wakati,” alisema Conte.

“Hadi wakati huu nimekuwa nikijaribu kuficha mambo lakini si kwa sasa tena kwa sababu hiyo narudia, hii hali niliyoiona leo (jana Jumamosi) sitaki kuiona tena kwa sababu hii haikubaliki na haikubaliki pia kwa mashabiki,” alisema Conte.


Tangu mwaka 2001 klabu hiyo ilipoanza kumilikiwa na Daniel Levy ambaye ndiye mwenyekiti, Tottenham imeshinda taji moja tu (Kombe la Ligi) ambalo walilibeba mwaka 2008.
Timu hiyo imekuwa na makocha tofauti 11 tangu wakati huo wakiwamo watatu waliokuwa katika kipindi cha mwaka 2019 alipoondoka Mauricio Pochettino ambaye aliifikisha timu hiyo katika fainali ya Ligi ya Mabingwa kabla ya kutimuliwa miezi sita baadaye.
Tottenham imetolewa katika mashindano karibu yote, kuanzia FA ilipotolewa na Sheffield United kabla ya kutolewa na AC Milan kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na sasa Conte anasema umefika wakati wa klabu na wachezaji kila mmoja abebe jukumu lake.
“Si tu kwa klabu, kocha na maofisa, wachezaji nao ni lazima wahusike katika hali hii kwa sababu ni wakati sasa wa kubadili hii hali kama Tottenham inataka mabadiliko,” alisema Conte.
“Kama wanataka kuendelea na hali hii wanaweza kumbadili kocha, watabadili makocha wengi lakini hii hali haiwezi kubadilika, niamini mimi,” alisema.


Alipoulizwa ni kwa nini hali hiyo ipo Tottenham, Conte alisema: “Ni kwa sababu hapa wamezowea hivyo, hawachezi kwa ajili ya kitu muhimu, hawataki kucheza kama wapo katika presha ya kutaka kitu, hawataki kucheza wakiwa katika hali ya kuhimizwa na kutakiwa wapambane kupata ushindi,” alisema.
“Tuna mechi 10 na kuna watu wanafikiri tunaweza kupambana, kupambania nini katika hulka za aina hii, misimamo hii, kujituma kwa aina hii, ni kwa ajili ya nini? Nafasi ya saba, nane, 10?” Alihoji Conte.

The post Conte: Wachezaji Spurs wabinafsi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/19/conte-wachezaji-spurs-wabinafsi/feed/ 0
Conte arejea kibaruani Spurs https://www.greensports.co.tz/2023/02/10/conte-arejea-kibaruani-spurs/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/10/conte-arejea-kibaruani-spurs/#respond Fri, 10 Feb 2023 07:43:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5078 London, EnglandKocha wa Tottenham Hotspur, Antonio Conte jana Alhamisi alirudi kazini na kuendelea na majukumu yake baada ya kufanyiwa upasuaji wa kibofu.Conte alifanyiwa upasuaji huo nyumbani kwao Iralia wiki iliyopita baada ya kuwa na maumivu kwenye tumbo na hivyo kuikosa mechi ya Jumapili iliyopita ambayo timu yake iliichapa Man City bao 1-0.Kocha huyo mwenye umri […]

The post Conte arejea kibaruani Spurs first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Tottenham Hotspur, Antonio Conte jana Alhamisi alirudi kazini na kuendelea na majukumu yake baada ya kufanyiwa upasuaji wa kibofu.
Conte alifanyiwa upasuaji huo nyumbani kwao Iralia wiki iliyopita baada ya kuwa na maumivu kwenye tumbo na hivyo kuikosa mechi ya Jumapili iliyopita ambayo timu yake iliichapa Man City bao 1-0.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 53, alirejea jijini London juzi Jumatano lakini hadi sasa haijaweza kufahamika mara moja kama atakuwa kwenye benchi kesho Jumamosi wakati Spurs itakapokuwa ugenini dhidi ya Leicester.

“Ni lazima ajitulize kwa muda, asijichoshe lakini tuna furaha kukutana naye kwa mara nyingine kwenye uwanja wa mazoezi, leo (jana) asubuhi alikuwa uwanjani pamoja nasi,” alisema kocha msaidizi, Cristian Stellini akimzungumzia Conte aliyetua Spurs mwaka 2021 akitokea Inter Milan.


“Alitumia muda mwingi akisalimiana kwa kukumbatiana na kila mtu, hakuzungumza chochote kuhusu atafanya nini baada ya hapo lakini kimsingi amerudi na tuna furaha,” aliongeza Stellini.
Stellini ambaye ndiye aliyeiongoza timu hiyo katika mechi dhidi ya City pia alimzungumzia kipa wao majeruhi aliyeumia goti, Hugo Lloris akisema kwamba atakosekana uwanjani kwa wiki tano hadi sasa.
Kocha huyo msaidizi pia alikataa kuzungumza chochote kuhusu mambo ya baadaye ya Conte katika klabu hiyo. Mkataba wa Conte unafikia tamati mwishoni mwa msimu huu ingawa ana nafasi ya kuongeza miezi mingine 12.
“Hatukuwahi kuzungumzia hilo la mkataba, katika soka huwezi kutulia kwa sababu tu una mkataba au hauna, ni lazima ufanye kazi kwa bidii, huwezi kubweteka, unaishi ukiwa na nguvu kwa kuwa unataka kushinda, kwa hiyo huna muda wa kuzungumzia mambo yako yajayo,” alisema.
“Haya ndiyo maisha yetu, hii ni soka, ni mchezo, unafikiria lengo lijalo unalotaka kulifanikisha, unachotaka kufanikisha ni hilo kwa hiyo hubweteki, uwe na mkataba au usiwe nao,” alifafanua.

The post Conte arejea kibaruani Spurs first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/10/conte-arejea-kibaruani-spurs/feed/ 0
Conte kufanyiwa upasuaji https://www.greensports.co.tz/2023/02/01/conte-kufanyiwa-upasuaji/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/01/conte-kufanyiwa-upasuaji/#respond Wed, 01 Feb 2023 12:27:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4948 London, EnglandKocha wa Tottenham Hotspur, Antonio Conte anatarajia kufanyiwa upasuaji wa kibofu. Klabu yake imethibitisha hilo hii leo Jumatano.Conte ambaye alijiunga na timu hiyo mwaka 2021 alikutwa na uvimbeuchungu karibu na kibofu na kujisikia vibaya zaidi ikiwa ni maumivu ya tumbo“Kila mmoja katika klabu anamtakia heri kocha apone haraka,” ilieleza taarifa ya klabu hiyo na […]

The post Conte kufanyiwa upasuaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Tottenham Hotspur, Antonio Conte anatarajia kufanyiwa upasuaji wa kibofu. Klabu yake imethibitisha hilo hii leo Jumatano.
Conte ambaye alijiunga na timu hiyo mwaka 2021 alikutwa na uvimbeuchungu karibu na kibofu na kujisikia vibaya zaidi ikiwa ni maumivu ya tumbo
“Kila mmoja katika klabu anamtakia heri kocha apone haraka,” ilieleza taarifa ya klabu hiyo na kufafanua kwamba kocha huyo atarudi baada ya kumaliza matibabu.
Mechi ijayo ya Spurs itakuwa Jumapili ijayo nyumbani dhidi ya Manchester City katika Ligi Kuu England, mechi ambayo ni muhimu kwa timu hiyo kushinda ili kuimarisha nia yake ya kubaki katika nne bora au top four.
Spurs kwa sasa inashika nafasi ya tano ikiwa na pointi 36, imezidiwa na vinara na mahasimu wao wa jiji la London, Arsenal kwa tofauti ya pointi 14.
Hivi karibuni Conte alinukuliwa akijivua lawama baada ya kuulizwa kuhusu matokeo yasiyoridhisha ya timu hiyo ambapo alisema asilaumiwe peke yake bali waulizwe watu wengine kwenye timu wakiwamo madaktari na maofisa wengine.

The post Conte kufanyiwa upasuaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/01/conte-kufanyiwa-upasuaji/feed/ 0
Conte ajivua lawama Spurs https://www.greensports.co.tz/2023/01/18/conte-ajivua-lawama-spurs/ https://www.greensports.co.tz/2023/01/18/conte-ajivua-lawama-spurs/#respond Wed, 18 Jan 2023 08:04:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4792 London, EnglandKocha wa Tottenham Hostpur, Antonio Conte amejivua lawama akisema si sahihi kulaumiwa peke yake kwa matokeo mabaya ya timu hiyo badala yake ametaka watu wengine katika klabu nao waangaliwe katika jambo hilo.Jumapili iliyopita timu hiyo ilichapwa mabao 2-0 na mahasimu wao wa London, Arsenal katika mechi ya Ligi Kuu England na kuifanya timu ipoteze […]

The post Conte ajivua lawama Spurs first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Tottenham Hostpur, Antonio Conte amejivua lawama akisema si sahihi kulaumiwa peke yake kwa matokeo mabaya ya timu hiyo badala yake ametaka watu wengine katika klabu nao waangaliwe katika jambo hilo.
Jumapili iliyopita timu hiyo ilichapwa mabao 2-0 na mahasimu wao wa London, Arsenal katika mechi ya Ligi Kuu England na kuifanya timu ipoteze jumla ya mechi tano kati ya tisa za ligi hali inayomuweka pagumu kocha huyo ambaye kesho Alhamisi ana mtihani mwingine mgumu dhidi ya Man City.
“Kwa England nadhani kumekuwa na hulka mbaya, ni kocha tu anayetakiwa kuzungumza na kujieleza,” alisema Conte.

“Sijawahi kuona madaktari wa timu wakija kujieleza, sijawahi kuona klabu au mkurugenzi wa michezo akija hapa kueleza mipango au dira ya klabu, nchini Italia kabla ya kila mechi kuna mtu kutoka katika klabu anayekwenda kuzungumzia mazingira ambayo anayaona kuwa sahihi kwa klabu,” alisema Conte.


“Nafikiri kwa upande wetu pia itakuwa bora, vinginevyo kunakuwa na sura moja tu ya kutoa ufafanuzi kuhusu hali ya klabu ambayo nadhani ingekuwa vizuri kama angetoka mtu katika klabu kuielezea,” alisema kocha huyo Mtaliano akitaka uongozi wa klabu uwepo kwenye mkutano na wanahabari.
Tottenham au Spurs kwa sasa mambo yake si mazuri kwenye Ligi Kuu England ikiwa katika nafasi ya tano ikiachwa na Newcastle inayoshika nafasi ya tatu kwa tofauti ya pointi tano kama ilivyo kwa Man United inayoshika nafasi ya nne.
Conte amejikuta akiwa ‘mhanga mkuu’ wa mwenendo usioridhisha wa Spurs na sasa ameamua kujivua lawama akitaka wabebeshwe lawama hizo na watu wengine kwenye klabu ambao ametaka wawe na nafasi ya kuizungumzia klabu si kila wiki bali japo mara moja kwa mwezi au kila baada ya siku 15.

The post Conte ajivua lawama Spurs first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/01/18/conte-ajivua-lawama-spurs/feed/ 0