Ngumi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 10 May 2024 22:22:10 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Ngumi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Palasa ajivunia uongozi wake TPBRC https://www.greensports.co.tz/2024/05/11/palasa-ajivunia-uongozi-wake-tpbrc/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/11/palasa-ajivunia-uongozi-wake-tpbrc/#respond Fri, 10 May 2024 22:22:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10924 Na mwandishi wetuRais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), Chaurembo Palasa ambaye siku tatu zilizopita alisimamishwa kupisha uchunguzi dhidi ya uongozi wake amesema pamoja na yote lakini anajivunia kuona ngumi sasa zinapigwa kote nchini bila ya malalamiko.Palasa na viongozi wenzake wa TPBRC walisimamishwa na serikali kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo ingawa […]

The post Palasa ajivunia uongozi wake TPBRC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), Chaurembo Palasa ambaye siku tatu zilizopita alisimamishwa kupisha uchunguzi dhidi ya uongozi wake amesema pamoja na yote lakini anajivunia kuona ngumi sasa zinapigwa kote nchini bila ya malalamiko.
Palasa na viongozi wenzake wa TPBRC walisimamishwa na serikali kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo ingawa kiongozi huyo anaendelea anajivunia mafanikio na kupungua malalamiko tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Palasa amezungumza hayo leo Ijumaa alipokuwa akihojiwa na Green Sports juu ya tuhuma zinazomkabili ambapo alisema kwa sasa hana lolote la kuzungumza.
Badala yake alisema kwamba anasubiri kujibu hoja zinazomkabili mbele ya tume ya uchunguzi iliyoteuliwa juzi na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro.
“Bado sijahojiwa na kamati kwa hiyo siwezi kusema lolote, sababu hata nikisema sasa itakuwa haisaidii, nasubiri kwanza waniite nizungumze nao kisha nitakuwa na lolote la kusema kuhusiana na hilo,” alisema Palasa.
Palasa ambaye ni bondia wa zamani alisisitiza kuwa anafurahi kuona ngumi zinapigwa sehemu nyingi Tanzania bila malalamiko kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

“Huko awali kulikuwa na shida ya malipo lakini sasa watu wanapewa malipo yao, wanapata stahiki zao ndiyo maana hizo kelele hazipo, kilichobaki sasa ni mtu kulalamika inapotokea ameguswa kwenye masuala mengine binafsi lakini nafurahi kuona ngumi kama ngumi zinakwenda vizuri na hakuna malalamiko,” alisema Palasa.


Juzi Waziri Ndumbaro aliusimamisha uongozi TPBRC kupisha uchunguzi dhidi yao juu ya tuhuma zinazowakabili ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka, ukiukaji wa katiba ya kamisheni na mgongano wa maslahi.

The post Palasa ajivunia uongozi wake TPBRC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/11/palasa-ajivunia-uongozi-wake-tpbrc/feed/ 0
Serikali yausimamisha uongozi TPBRC https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/serikali-yausimamisha-uongozi-tpbrc/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/serikali-yausimamisha-uongozi-tpbrc/#respond Fri, 10 May 2024 07:29:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10899 Na mwandishi wetuUongozi wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) umesimamishwa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili ikiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka, ukiukaji wa Katiba ya Kamisheni hiyo na mgongano wa maslahi.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa (pichani), hatua hiyo imechukuliwa na […]

The post Serikali yausimamisha uongozi TPBRC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Uongozi wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) umesimamishwa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili ikiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka, ukiukaji wa Katiba ya Kamisheni hiyo na mgongano wa maslahi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa (pichani), hatua hiyo imechukuliwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Damas Ndumbaro baada ya kikao cha jana Jumatano kilichofanyika jijini Dodoma.
Imeelezwa zaidi kuwa kufuatia uamuzi huo, Waziri Ndumbaro ameunda kamati ya mpito ya kuongoza kamisheni hiyo ambayo itaongozwa na Mwenyekiti Emmanuel Salehe na viongozi wengine wakiwa ni Alex Galinoma (Makamu Mwenyekiti), Joseph Mpuya (Katibu Mkuu) na wajumbe ni Patrick Nyembela, Shaffi Dauda na Irene Mwasanga.
Ndumbaro pia ameunda kamati ya kufanya uchunguzi kwa kamisheni iliyosimamishwa kuhusu tuhuma hizo mbalimbali zilizoibuliwa na wanachama wao.
Kamati hiyo itafanya kazi kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia Mei 8 mwaka huu ikiongozwa na mwenyekiti Christopher Kamugisha akiwa na katibu Ingridy Kimario, wajumbe ni Mariam Aziz Faki na Sophia Alponary.
Ndumbaro pia amewataka wadau wa michezo kote nchini kufuata sheria, kanuni na miongozo iliyopo kwenye vyama na mashirikisho ya michezo ili azma ya serikali ya kukuza na kuendeleza

michezo nchini itimie.

The post Serikali yausimamisha uongozi TPBRC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/serikali-yausimamisha-uongozi-tpbrc/feed/ 0
Mwakinyo amfurahia mpinzani bora https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/mwakinyo-amfurahia-mpinzani-bora/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/mwakinyo-amfurahia-mpinzani-bora/#respond Wed, 01 May 2024 19:59:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10813 Na mwandishi wetuBondia Hassan Mwakinyo ‘Champez’ amesema anashukuru kupata nafasi ya kupigana na bondia bora Afrika, Patrick Alotey raia wa Ghana huku akiamini atafanya vyema na mpinzani wake atakwenda kusimulia kitakachomtokea siku hiyo.Mwakinyo amezungumza hayo leo Jumatano jijini Dares Salaam kuelekea pambano hilo ambalo atakuwa akitetea mkanda wake wa WBO, litakalopigwa Mei 31 mwaka huu, […]

The post Mwakinyo amfurahia mpinzani bora first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Bondia Hassan Mwakinyo ‘Champez’ amesema anashukuru kupata nafasi ya kupigana na bondia bora Afrika, Patrick Alotey raia wa Ghana huku akiamini atafanya vyema na mpinzani wake atakwenda kusimulia kitakachomtokea siku hiyo.
Mwakinyo amezungumza hayo leo Jumatano jijini Dares Salaam kuelekea pambano hilo ambalo atakuwa akitetea mkanda wake wa WBO, litakalopigwa Mei 31 mwaka huu, Masaki jijini Dar es Salaam.
“Kwanza niwashukuru makocha wangu, mashabiki wangu ambao wameendelea kunitumainia hata baada ya kupita kipindi kirefu, ila kumekuwa na maneno mengi ya kimichezo lakini nafikiri hili pambano la tarehe 31 kwangu mimi litakwenda kudhihirisha ukweli unazoungumzwa na watu wazuri na wabya juu yangu kwamba mimi ni nani.
“Kwangu mimi kupigana na bondia mwenye rekodi kubwa Afrika ni bahati kwenye maisha yangu, ‘boxer’ mwenye rekodi kubwa kidunia, hajawahi kupigwa na Mwafrika, lakini mimi nitakuwa Mtanzania, Mwafrika wa kwanza kuharibu rekodi ya bondia Alotey.

“Naomba tu listokee jambo la kinchi likasababisha pambano kuahirishwa lakini nina uhakika asilimia 100 atakwenda kusimulia kitakachomtokea,” alisema Mwakinyo.


Wakati huohuo, katika mkutano huo na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Kampuni ya Golden Boy Promotion, Shomari Kimbau alimtaka mwanamuziki, Rajabu Kahali kufuata taratibu rasmi za ngumi kama kweli anataka kupambana na Mwakinyo ulingoni.
Kimbau alisema kwamba anaamini Mwakinyo ana uwezo wa kumchapa Harmonize hata akiwa amefungwa mkono mmoja.
Kimbau amezungumza hayo baada ya hivi karibuni kuibuka malumbano na kejeli mitandaoni baina ya wawili hao kabla ya majuzi kusambaa video inayowaonesha Mwakinyo na Harmonize wakizuiwa ili wasipigane.
Tukio hilo lilitokea wawili hao walipokutana kwenye gym moja jijini Dar es Salaam na kuanza kurushiana maneno kila mmoja akimtambia mwenzake kwamba anaweza kupigana na mwenzake na kumpiga.

The post Mwakinyo amfurahia mpinzani bora first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/mwakinyo-amfurahia-mpinzani-bora/feed/ 0
Dullah Mbabe apigwa stop Uingereza https://www.greensports.co.tz/2024/04/16/dullah-mbabe-apigwa-stop-uingereza/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/16/dullah-mbabe-apigwa-stop-uingereza/#respond Tue, 16 Apr 2024 06:58:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10610 Na mwandishi wetuImeelezwa kuwa bodi ya kusimamia ngumi za kulipwa nchini Uingereza imemfungia bondia Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ wa Tanzania kutozichapa kwa muda nchini humo.Uamuzi wa bodi hiyo umekuja wiki mbili baada ya bondia huyo namba tatu nchini katika uzani wa super middle kupigwa kwa Knock Out (KO) ya raundi ya nne Machi 31, mwaka […]

The post Dullah Mbabe apigwa stop Uingereza first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Imeelezwa kuwa bodi ya kusimamia ngumi za kulipwa nchini Uingereza imemfungia bondia Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ wa Tanzania kutozichapa kwa muda nchini humo.
Uamuzi wa bodi hiyo umekuja wiki mbili baada ya bondia huyo namba tatu nchini katika uzani wa super middle kupigwa kwa Knock Out (KO) ya raundi ya nne Machi 31, mwaka huu na Callum Simpson bondia namba 36 kidunia na namba tatu Uingereza katika uzani wa super middle.
Aidha, adhabu kama hiyo iliwahi kumkumba bondia Hassan Mwakinyo ambaye ni namba moja nchini kwenye uzani wa super welter mara baada ya pambano lake la Septemba 3 mwaka 2022,l alipochapwa kwa Technical Knock Out (TKO) ya raundi ya nne la Liam Smith.
Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), Chaurembo Palasa ameiambia GreenSports kuwa adhabu hiyo itaisha kwa Mbabe baada ya muda mchache na ilitokana na kupigwa KO nchini humo, hivyo bodi ya huko imemfungia kwa muda asipigane kwao ili kuangalia afya yake.

The post Dullah Mbabe apigwa stop Uingereza first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/16/dullah-mbabe-apigwa-stop-uingereza/feed/ 0
Ngumi kufutwa kwenye Olimpiki? https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/ngumi-kufutwa-kwenye-olimpiki/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/ngumi-kufutwa-kwenye-olimpiki/#respond Thu, 04 Apr 2024 20:39:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10516 Lausanne, UswisiKamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) imesema inahitaji kupata bodi mpya sahihi ya kimataifa ya kusimamia mchezo wa ngumi vinginevyo iufute mchezo huo katika Michezo ya Olimpiki ya Los Angeles, Marekani mwaka 2028.IOC ilitangaza kulivua Shirikisho la Kimataifa la Ngumi (IBA) haki ya kusimamia ngumi katika Michezo ya Olimpili ya Tokyo mwaka 2021 na […]

The post Ngumi kufutwa kwenye Olimpiki? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Lausanne, Uswisi
Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) imesema inahitaji kupata bodi mpya sahihi ya kimataifa ya kusimamia mchezo wa ngumi vinginevyo iufute mchezo huo katika Michezo ya Olimpiki ya Los Angeles, Marekani mwaka 2028.
IOC ilitangaza kulivua Shirikisho la Kimataifa la Ngumi (IBA) haki ya kusimamia ngumi katika Michezo ya Olimpili ya Tokyo mwaka 2021 na ile ya Paris ambayo inatarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Juzi Jumanne Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhisho wa Michezo (CAS) ilitangaza kuunga mkono maamuzi ya IOC ya kutoitambua IBA na hata kuitoa moja kwa moja katika Olimpiki.
Kwa kipindi kirefu IOC imeelezea wasiwasi wake kuhusu uongozi wa IBA na nidhamu ya usimamizi katika mapambano ya ngumi namna mapambano hayo yanavyosimamiwa na majaji wake.
Mwaka jana viongozi wa IOC walimlalamikia Rais wa IBA-Urusi, Umar Kremlev kwa kutumia lugha za shari na vitisho kwa maofisa waandamizi wa IOC.
IOC imewataka viongozi wa mashirikisho ya ngumi kwa kila nchi na kamati za olimpiki kila nchi kusaidia kuundwa bodi mpya ya kimataifa ya kusimamia mchezo wa ngumi kwa lengo la kuupa nafasi mchezo huo katika Michezo ya Olimpiki ya Los Angeles.
Katika agizo hilo IOC imetaka kuona inakuwa na mshirika wa ngumi kwenye Olimpiki ambaye ni bodi mpya ya kimataifa ya mchezo huo mapema mwaka 2025 ili kuupa nafasi mchezo huo kwenye Olimpiki.
IOC haijataja jina la bodi mpya lakini inadhaniwa huenda ikawa ni World Boxing, umoja ambao unaundwa na maofisa wa Marekani na Uingereza ambao mwaka jana walijitoa IBA na kumteua, Boris van der Vorst wa Uholanzi kuwa rais wao.

The post Ngumi kufutwa kwenye Olimpiki? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/ngumi-kufutwa-kwenye-olimpiki/feed/ 0
Dulla Mbabe apeleka ubabe Uingereza https://www.greensports.co.tz/2024/03/29/dulla-mbabe-apeleka-ubabe-uingereza/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/29/dulla-mbabe-apeleka-ubabe-uingereza/#respond Fri, 29 Mar 2024 09:04:26 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10431 Na mwandishi wetuBondia wa ngumi za kulipwa, Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ amesema yuko tayari kwa pambano lake la kimataifa lisilo la ubingwa dhidi ya Callum Simpson wa Uingereza litakalopigwa Machi 31, mwaka huu.Pambano hilo la raundi 10 litafanyika kwenye ukumbi wa O2 Arena, Greenwich jijini London ambapo Dullah anaenda kwenye pambano hilo akiwa na kumbukumbu […]

The post Dulla Mbabe apeleka ubabe Uingereza first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Bondia wa ngumi za kulipwa, Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ amesema yuko tayari kwa pambano lake la kimataifa lisilo la ubingwa dhidi ya Callum Simpson wa Uingereza litakalopigwa Machi 31, mwaka huu.
Pambano hilo la raundi 10 litafanyika kwenye ukumbi wa O2 Arena, Greenwich jijini London ambapo Dullah anaenda kwenye pambano hilo akiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda pambano lake la mwisho la kimataifa la Januari Mosi.
Katika pambano hilo lililofanyika jijini Tanga, Dulla alimbwaga Limbani Lano wa Malawi kwa matokeo ya pointi za majaji wote watatu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Dulla alisema kama bondia muda wote anapaswa kuwa fiti ili aweze kucheza mapambano mengi na kutwaa mikanda ili apande kwenye viwango vya ubora.
“Kazi yangu ni ngumi na kuwafanya wapenzi wa ngumi wafurahi ndio maana najifua ili nishinde kila pambano lililo mbele yangu japokuwa siwezi kumzungumzia mpinzani nitakayekutana naye,” alisema Dullah.

The post Dulla Mbabe apeleka ubabe Uingereza first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/29/dulla-mbabe-apeleka-ubabe-uingereza/feed/ 0
Mwankemwa atamba kumchapa Okwiri https://www.greensports.co.tz/2024/03/26/mwankemwa-atamba-kumchapa-okwiri/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/26/mwankemwa-atamba-kumchapa-okwiri/#respond Tue, 26 Mar 2024 07:19:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10355 Na mwandishi wetuBondia wa ngumi za kulipwa nchini, Meshack Mwankemwa amesema kuwa maandalizi ya pambano lake la kuwania ubingwa wa World Boxing Foundation International Middleweight (WBF) dhidi ya Rayton Okwiri wa Kenya, yamekamilika kilichobaki ni kwenda kuimaliza kazi ulingoni.Pambano hilo la raundi 10 litafanyika ukumbi wa Chartel, Nairobi, Kenya ambapo Mwankemwa ataingia ulingoni akiwa na […]

The post Mwankemwa atamba kumchapa Okwiri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Meshack Mwankemwa amesema kuwa maandalizi ya pambano lake la kuwania ubingwa wa World Boxing Foundation International Middleweight (WBF) dhidi ya Rayton Okwiri wa Kenya, yamekamilika kilichobaki ni kwenda kuimaliza kazi ulingoni.
Pambano hilo la raundi 10 litafanyika ukumbi wa Chartel, Nairobi, Kenya ambapo Mwankemwa ataingia ulingoni akiwa na kumbukumbu ya kushinda pambano lake la mwisho kwa KO kwa kumchapa Said Hamdan, Februari 3, mwaka huu.
Akizungumza Jumatatu hii, Mwankemwa alisema anajua kiu ya mashabiki wake ni kuona anaibuka na ushindi katika pambano lijalo ili kuendeleza ubabe wake Afrika pamoja na kuipeperusha bendera ya Tanzania katika mchezo wa ngumi.
“Najua mashabiki wangu wanatamani kuona kile kilichotokea katika michezo iliyopita, nawaahidi kuwa pambano hili litakuwa la kuweka heshima na kurudi nyumbani na mkanda,” alisema.

The post Mwankemwa atamba kumchapa Okwiri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/26/mwankemwa-atamba-kumchapa-okwiri/feed/ 0
Katoto avunjika mkono Ghana https://www.greensports.co.tz/2024/03/17/katoto-avunjika-mkono-ghana/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/17/katoto-avunjika-mkono-ghana/#respond Sun, 17 Mar 2024 13:18:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10235 Na mwandshi wetuBondia wa Tanzania, Abdallah Abdallah ‘Katoto’ amevunjika mkono kwenye raundi ya mwisho ya pambano lake dhidi ya bondia wa Ethiopia, Wibshet Bekele katika michezo ya Afrika inayoendelea nchini Ghana.Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT), Lukelo Willilo, Katoto alipata ajali hiyo akijiandaa kufanya shambulizi dhidi ya mpinzani wake raundi ya […]

The post Katoto avunjika mkono Ghana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandshi wetu
Bondia wa Tanzania, Abdallah Abdallah ‘Katoto’ amevunjika mkono kwenye raundi ya mwisho ya pambano lake dhidi ya bondia wa Ethiopia, Wibshet Bekele katika michezo ya Afrika inayoendelea nchini Ghana.
Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT), Lukelo Willilo, Katoto alipata ajali hiyo akijiandaa kufanya shambulizi dhidi ya mpinzani wake raundi ya tatu na ya mwisho ya mchezo huo wa hatua ya 16 bora uliochezwa jana Ijumaa.
“Mwamuzi alilazimika kusimamisha pambano, Katoto tulimuwahisha kwenda University of Ghana Medical Center kwa ajili ya matibabu; na baada ya kuchukuliwa vipimo alionekana amevunjika sehemu ya katikati ya mkono.
“Ila tunashukuru Mungu hali yake inaendelea vizuri ingawa hataweza kucheza kwa kipindi cha karibuni,” alisema kocha msaidizi wa timu ya taifa ya ngumi, Muhsini Mng’ola.
Baada ya pambano hilo, Katoto alikuwa apambane hatua ya robo fainali dhidi ya Patrick Chinyemba kutoka Zambia ambaye ni Bingwa wa Afrika na tayari ameshakata tiketi ya kufuzu kushiriki Olimpiki ya Paris 2024.

“Ndoto yangu kubwa ilikuwa katika pambano langu la robo fainali dhidi ya Chinyemba wa Zambia na kutaka kuishangaza Afrika na dunia kwa uwezo wangu, pambano hili la Muethiopia nilikuwa nina uhakika na ushindi kwa maandalizi mazuri tuliyoyapata,” alisema Katoto.


Kwa upande wake Willilo alisema: “Tunamshukuru Mungu kwa yote, ndio mchezo ulivyo, zilikuwa zimebaki sekunde chache pambano liishe huku tukiongoza kwa matokeo, lakini mchezo wakati mwingine una matokeo katili.”

The post Katoto avunjika mkono Ghana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/17/katoto-avunjika-mkono-ghana/feed/ 0
Mwakinyo, Mbabe kila mmoja na lake jambo https://www.greensports.co.tz/2024/03/13/mwakinyo-mbabe-kila-mmoja-na-lake-jambo/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/13/mwakinyo-mbabe-kila-mmoja-na-lake-jambo/#respond Wed, 13 Mar 2024 05:54:30 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10162 Na mwandishi wetuMabondia Hassan Mwakinyo (pichani juu) na Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’, kila mmoja ameweka bayana kuwa yuko jikoni akijiandaa na jambo kubwa.Mwakinyo aliyeshinda pambano la hivi karibuni dhidi ya bondia kutoka Ghana, Elvis Ahorgah lililofanyika Zanzibar alisema anajiandaa na pambano kubwa Aprili, mwaka huu.“Kuna kitu tunapika, nina hamu ya kuonesha,” aliandika ujumbe huo kwenye […]

The post Mwakinyo, Mbabe kila mmoja na lake jambo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mabondia Hassan Mwakinyo (pichani juu) na Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’, kila mmoja ameweka bayana kuwa yuko jikoni akijiandaa na jambo kubwa.
Mwakinyo aliyeshinda pambano la hivi karibuni dhidi ya bondia kutoka Ghana, Elvis Ahorgah lililofanyika Zanzibar alisema anajiandaa na pambano kubwa Aprili, mwaka huu.
“Kuna kitu tunapika, nina hamu ya kuonesha,” aliandika ujumbe huo kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram.
Hata hivyo, kwa mujibu wa mtandao wa ngumi wa kimataifa wa boxrec, Mwakinyo anatarajia kupanda ulingoni Aprili 27, mwaka huu kuchuana na Rasheed Adeyamo kutoka Nigeria kuwania mkanda wa WBO Afrika.
Kwa upande wake Dulla Mbabe (pichani chini) ameiambia GreenSports: “Ninajipanga, kuna jambo kubwa nitatangaza Machi 31, niwaambie mashabiki zangu wakae mkao wa kula, kwani kimya kingi kina mshindo mbele.”


Mara ya mwisho, Dulla Mbabe alimchapa bondia kutoka Malawi, Limbani Lano kwenye pambano lililopigwa mkoani Tanga, Januari, mwaka huu ikiwa ni wiki chache tangu alipotoka kupoteza dhidi ya Erick Katompa wa DR Congo, Novemba, mwaka jana.

The post Mwakinyo, Mbabe kila mmoja na lake jambo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/13/mwakinyo-mbabe-kila-mmoja-na-lake-jambo/feed/ 0
Joshua amchakaza Ngannou mapema https://www.greensports.co.tz/2024/03/09/joshua-amchakaza-ngannou-mapema/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/09/joshua-amchakaza-ngannou-mapema/#respond Sat, 09 Mar 2024 08:39:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10098 Riyadh, Saudi ArabiaBondia Anthony Joshua amemchakaza kwa KO ya raundi ya pili mpinzani wake, Francis Ngannou katika pambano la ngumi za uzito wa juu lililofanyika usiku wa jana Ijumaa mjini Riyadh.Ngannou alikumbana na kipigo hicho kwa ngumi ya mkono wa kushoto iliyomkuta chini ya kidevu kabla ya kuanguka chini na kujikuta akipoteza fahamu.Baada ya kuanza […]

The post Joshua amchakaza Ngannou mapema first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabia
Bondia Anthony Joshua amemchakaza kwa KO ya raundi ya pili mpinzani wake, Francis Ngannou katika pambano la ngumi za uzito wa juu lililofanyika usiku wa jana Ijumaa mjini Riyadh.
Ngannou alikumbana na kipigo hicho kwa ngumi ya mkono wa kushoto iliyomkuta chini ya kidevu kabla ya kuanguka chini na kujikuta akipoteza fahamu.
Baada ya kuanza kuhesabiwa na kukaa sawa, Ngannou, mwenye umri wa miaka 37 ilidhihirika wazi kwamba asingeweza kuendelea na pambano hilo hasa baada ya watu wa huduma ya kwanza kuanza kumpa msaada.
Katika pambano hilo, Joshua alianza kuonesha makali yake raundi ya kwanza baada ya kumchapa Ngannou ngumi kali ya mkono wa kulia ambayo ilimyumbisha lakini aliweza kusimama imara na kuendelea na pambano.
Johua, 34 katika raundi ya pili aliendeleza makali yake kwa kumchapa Ngannou ngumi nyingine ambayo ilimpiga kisawasawa kwenye sehemu ya sikio la upande wa kushoto.


Ngumi hiyo kali hata hivyo haikumtetemesha sana Ngannou ambaye alionekana kuwa imara na kuendelea na pambano lakini alikutana na ngumi nyingine kali ya mkono wa kulia iliyotosha kumfanya alambe sakafu na kushinda kuendelea na pambano.
Unapoelekea kwenye kuutafuta ubingwa wakati wote unatakiwa kuwa makini, huyu ni mimi ambaye nilijitoa kwa ajili ya mpango huo,” alisema Joshua baada ya ushindi huo.
“Nilipomuona Ngannou kwenye pambano na Tyson Fury nilijisemea, kumbe huyu jamaa anaweza kupigana, nahitaji ‘kitu cha aina hii’,” alisema Joshua.
Baada ya kipigo hicho, Ngannou aliibukia kwenye mitandao ya kijamii akitumia akaunti yake ya Twitter au X kuwaomba radhi mashabiki wake kwa madai kwamba amewaangusha lakini akawataka wasikate tamaa.

“Samahani jamani, nimewaangusha, leo ilikuwa siku mbaya kwenye ofisi yangu lakini kesho itakuwa siku nyingine, asanteni kwa mapenzi yenu,” alisema Ngannou.


The post Joshua amchakaza Ngannou mapema first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/09/joshua-amchakaza-ngannou-mapema/feed/ 0