Yanga - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 18 Aug 2026 18:23:42 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Yanga - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Tamasha Yanga Day laingia doa https://www.greensports.co.tz/2026/08/18/tamasha-yanga-day-laingia-doa/ https://www.greensports.co.tz/2026/08/18/tamasha-yanga-day-laingia-doa/#respond Tue, 18 Aug 2026 18:23:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14831 Na mwandishi wetuTamasha ya Yanga Day limeingia doa baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 2-1 na timu ya Aigles du Congo ya DR Congo katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Jumapili Agosti 8, 2026 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Katika mchezo huo uliotanguliwa na shamrashamra za kuwatambulisha wachezaji wapya wa Yanga kwa ajili ya msimu […]

The post Tamasha Yanga Day laingia doa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Tamasha ya Yanga Day limeingia doa baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 2-1 na timu ya Aigles du Congo ya DR Congo katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Jumapili Agosti 8, 2026 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliotanguliwa na shamrashamra za kuwatambulisha wachezaji wapya wa Yanga kwa ajili ya msimu mpya wa 2026-26, Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na mchezaji wao mpya, Peter Shalulile.
Shalulile alifunga bao hilo katika dakika ya 27 kwa mkwaju wa penalti lakini iliwachukua Aigles dakika 10 kupata bao la kusawazisha lililofungwa na Talasy Tonny na kuzifanya timu ziende mapumziko zikiwa sare.
Aigles waliandika bao la pili katika dakika ya 65, mfungaji kwa mara nyingine akiwa Tony na kuifanya timu yake itoke uwanjani na ushindi.
Mchezo huo umelipa benchi la ufundi la Yanga nafasi nzuri ya kukifanyia tathmini kikosi hicho kipya kabla ya kuanza mbio za kulitetea taji la Ligi Kuu NBC msimu wa 2026-27.
Yanga itaanza kuufungua msimu mpya kwa kuumana na mahasimu wao Simba katika mechi ya Ngao ya Jamii itakayopigwa Jumatano Agosti 12, 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.

The post Tamasha Yanga Day laingia doa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/08/18/tamasha-yanga-day-laingia-doa/feed/ 0
Hersi apewa miaka mingine minne Yanga https://www.greensports.co.tz/2026/08/09/hersi-apewa-miaka-mingine-minne-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2026/08/09/hersi-apewa-miaka-mingine-minne-yanga/#respond Sun, 09 Aug 2026 19:05:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14820 Na mwandishi wetuInjinia Hersi Said ataendelea kuiongoza klabu ya Yanga kwa kipindi kingine cha miaka minne baada ya kupita bila kupingwa katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam Jumapili, Agosti 2, 2026.Ushindi huo umekuja katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa klabu hiyo ambapo kiongozi huyo hakuwa na mpinzani kama ilivyokuwa kwa […]

The post Hersi apewa miaka mingine minne Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Injinia Hersi Said ataendelea kuiongoza klabu ya Yanga kwa kipindi kingine cha miaka minne baada ya kupita bila kupingwa katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam Jumapili, Agosti 2, 2026.
Ushindi huo umekuja katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa klabu hiyo ambapo kiongozi huyo hakuwa na mpinzani kama ilivyokuwa kwa makamu wake, Arafat Haji ambao wataendelea kuiongoza klabu hiyo.
Katika nafasi za wajumbe watano wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo, walioshinda ni Munir Seleman, Alexander Ngai, Yanga Makaga, Julius Koi na Fahd Afif.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Hersi aliwataka wanachama wa klabu hiyo kuvunja kambi zilizotokana na makundi ya uchaguzi na kuwa kitu kimoja.
Kwa upande wa wagombea walioshindwa katika uchaguzi huo, Hersi aliwataka kutoyapokea matokeo hayo kwa chuki kwa kuwa wao bado ni wanachama wa Yanga.
Hersi aliwapongeza wagombea ambao wamefanikiwa kushinda katika nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji wakiwamo wawili aliosema kuwa ni wapya na wengine watatu wamebaki.
“Wagombea waliokosa nafasi nao ni washindi licha ya kwamba kura hazikutosha, hawatakiwi kuwa maadui wa klabu yetu badala yake wanapaswa kuwa sehemu ya klabu yao,” alisema Hersi.
Katika mkutano huo, Hersi pia alipata nafasi ya kuwaeleza wanachama mafanikio ya uongozi wake tangu akabidhiwe jukumu hilo takriban miaka minne iliyopita.

The post Hersi apewa miaka mingine minne Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/08/09/hersi-apewa-miaka-mingine-minne-yanga/feed/ 0
Yanga yatambulisha kocha mpya https://www.greensports.co.tz/2026/07/12/yanga-yatambulisha-kocha-mpya/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/12/yanga-yatambulisha-kocha-mpya/#respond Sun, 12 Jul 2026 19:02:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14790 Na mwandishi wetuKlabu ya soka ya Yanga imemtambulisha, Manqoba Mngqithi kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo ambaye anaanza rasmi kazi kwa ajili ya msimu mpya wa 2026-27.Taarifa za Yanga kutambulisha kocha mpya zilianza kuonekana katika mitandao ya kijamii Jumamosi Julai 10, 2026 baada ya kuwapo fununu zikihusisha makocha kadhaa akiwamo aliyewahi kuwa kocha wa […]

The post Yanga yatambulisha kocha mpya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya soka ya Yanga imemtambulisha, Manqoba Mngqithi kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo ambaye anaanza rasmi kazi kwa ajili ya msimu mpya wa 2026-27.
Taarifa za Yanga kutambulisha kocha mpya zilianza kuonekana katika mitandao ya kijamii Jumamosi Julai 10, 2026 baada ya kuwapo fununu zikihusisha makocha kadhaa akiwamo aliyewahi kuwa kocha wa Simba, Fadlu Davids.
Manqoba, 55, anachukua nafasi ya Pedro Concalves aliyetimuliwa mwezi Machi, 2026 na nafasi yake kukaimiwa na Abdihamid Moalin ambaye aliiwezesha Yanga kulitetea taji la Ligi Kuu NBC msimu uliopita wa 2025-26.
Kocha huyo mpya ni jina maarufu ukanda wa Afrika hasa kwao Afrika Kusini ambapo ametamba kwa muda mrefu na kikosi cha Mamelodi Sundowns, moja ya timu zenye mafanikio barani Afrika.
Akiwa na timu hiyo aliiwezesha kutawala soka nchini Afrika Kusini kwa kubeba mataji kadhaa pamoja na kuonesha ushindani katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Timu nyingine ambazo Manqoba amewahi kuzinoa mbali na Mamelodi ni Moja United, Amazulu FC, University of KwaZulu-Natal, Chippa United na timu yake ya mwisho ni Golden Arrows.
Mtihani wa kwanza kwa kocha huyo mwenye leseni ya Uefa utakuwa Agosti 12, 2026, Yanga itakapoumana na mahasimu wao Simba katika mechi ya Ngao ya Jamii, mechi ambayo ni rasmi kwa ufunguzi wa Ligi Kuu NBC msimu wa 2026-27.

The post Yanga yatambulisha kocha mpya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/12/yanga-yatambulisha-kocha-mpya/feed/ 0
Yanga yatozwa faini Sh milioni 100 https://www.greensports.co.tz/2026/07/04/yanga-yatozwa-faini-sh-milioni-100/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/04/yanga-yatozwa-faini-sh-milioni-100/#respond Fri, 03 Jul 2026 22:14:40 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14755 Na mwandishi wetuKlabu ya soka ya Yanga imetozwa faini ya Sh milioni 100 wakati rais wa klabu hiyo, Hersi Said na ofisa mtendaji mkuu wake, Andre Mtine wamepelekwa kamati ya maadili kujieleza.Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) iliyokutana Alhamisi, Julai 2, 2026 na […]

The post Yanga yatozwa faini Sh milioni 100 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya soka ya Yanga imetozwa faini ya Sh milioni 100 wakati rais wa klabu hiyo, Hersi Said na ofisa mtendaji mkuu wake, Andre Mtine wamepelekwa kamati ya maadili kujieleza.
Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) iliyokutana Alhamisi, Julai 2, 2026 na kupitia mwenendo na matukio mbalimbali ya ligi hiyo.
Taarifa ya kamati hiyo iliyopatikana Ijumaa Julai 3, 2026 imeeleza kuwa Yanga imetozwa faini hiyo kwa kosa la kutotumia chumba rasmi cha kubadilishia nguo kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo na kutumia nyumba iliyo jirani na uwanja huo.
Yanga katika mechi hiyo ya mwisho ya ligi msimu wa 2025-26 iliyochezwa Jumanne Juni 30, 2026 dhidi ya JKT Tanzania, iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 na kutawazwa rasmi bingwa wa ligi hiyo.
Kuhusu viongozi wa klabu hiyo, wametakiwa kufika kamati ya maadili ili kwenda kujieleza kwa kuwa kosa hilo la uvunjifu wa kanuni limejirudia kwa mara ya pili.
Mwezi Mei mwaka huu, Yanga ilitozwa faini ya Sh 30 milioni 30 kwa kosa hilo hilo la kutotumia vyumba rasmi vya kubadilishia nguo katika mechi yao na Simba iliyochezwa kwenye uwanja huo huo na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Kamati hiyo pia imetoa onyo kali kwa timu ya KMC baada ya wachezaji wake watatu, Aimar Said Twalib jezi namba 71, Steven Donald Mgimwa jezi namba 80 na Hussein Kihiyo jezi namba 86 kwa kuvaa jezi inayozidi namba 70.
Wachezaji hao walivaa jezi hizo katika mechi yao na Simba ambayo walifungwa bao 1-0 na kitendo hicho ni kwenda kinyume na kanuni 17.2 ya ligi kuu inayohusu taratibu za mchezo.
Nayo klabu ya Mtibwa Sugar imetozwa faini ya Sh milioni 5 kwa kosa la wachezaji wake kutotumia chumba rasmi cha kubadilishia nguo kwenye Uwanja wa Majaliwa, Lindi katika mechi yao na Namungo FC, mechi ambayo Mtibwa ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1.
Ligi Daraja la Kwanza
Katika mapitio ya mechi za ligi daraja la kwanza, kamati ilipitia matukio ya mechi kati ya Stand FC Masasi na Pan African na kumfungia mchezaji wa Lindi Soccer Academy, Ramadhan Mlaponi kujihusisha na soka kwa miezi 12.
Mlaponi alifungiwa kwa kosa la kutumia leseni ya Swizan Edwin ambaye ni mchezaji halali wa Stand FC ili apate nafasi ya kucheza mechi hiyo.
Stand FC, timu kutoka Mtwara ambayo ndiyo iliyoshinda mchezo huo kwa bao 1-0, pia imeporwa ushindi huo na Pan African ya Dar es Salaam kupewa pointi tatu na mabao matatu.
Sambamba na hilo, kocha wa Stand FC, Mbano Kizito amefungiwa miezi 12 na kutozwa faini ya Sh 500,000 kwa kumchezesha mchezaji ambaye ni batili kiusajili.

The post Yanga yatozwa faini Sh milioni 100 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/04/yanga-yatozwa-faini-sh-milioni-100/feed/ 0
Yanga yabeba taji la tano ligi kuu https://www.greensports.co.tz/2026/07/01/yanga-yabeba-taji-la-tano-ligi-kuu/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/01/yanga-yabeba-taji-la-tano-ligi-kuu/#respond Wed, 01 Jul 2026 20:07:12 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14749 Na mwandishi wetuYanga hatimaye imetwaa taji la Ligi Kuu NBC msimu wa 2025-26 na kuweka rekodi ya kulitwaa taji hilo mara ya tano mfululizo.Mafanikio hayo yamekuja baada ya kuilaza JKT Tanzania mabao 3-0 katika mechi ya mwisho ya ligi hiyo iliyochezwa Jumanne, Juni 30, 2026 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamhuyo, Dar es Salaam.Baada ya […]

The post Yanga yabeba taji la tano ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga hatimaye imetwaa taji la Ligi Kuu NBC msimu wa 2025-26 na kuweka rekodi ya kulitwaa taji hilo mara ya tano mfululizo.
Mafanikio hayo yamekuja baada ya kuilaza JKT Tanzania mabao 3-0 katika mechi ya mwisho ya ligi hiyo iliyochezwa Jumanne, Juni 30, 2026 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamhuyo, Dar es Salaam.
Baada ya ushindi huo, Yanga imekamilisha mechi za ligi hiyo ikiwa na pointi 75 wakati mahasimu wao Simba waliokuwa wakitoa ushindani wameishia kumaliza ligi nafasi ya pili na pointi 73 baada ya kuichapa KMC bao 1-0.
JKT waliuanza mchezo kwa kujiamini na kuonesha dalili zote za kuizuia Yanga kuweka rekodi ya kulibeba taji hilo lakini mambo yakaanza kuwa tofauti katika dakika ya nane kwa Yanga kupata bao ambalo lilifungwa na Prince Dube baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Max Nzengeli.
Wakati Yanga ikisaka bao la kuongeza na JKT ikisaka bao la kusawazisha, Yanga walipata pigo dakika ya 45 baada ya kiungo wao Pacome Zouzoua kuumia alipochezewa vibaya na beki wa JKT, Hassan Wahabi.
Tukio hilo lilisababisha kuwapo hali ya huzuni kwa wachezaji wa timu zote ambao walionekana kumsikitia Pacome wakati akipewa huduma ya kwanza kwa kilichoonekana kuwa alipata maumivu makubwa.
Mwamuzi wa mchezo huo Hassan Katanga awali alimpa kadi ya njano beki huyo wa JKT lakini baadaye aliifuta na kumpa nyekundu.
Dakika tano baada ya timu kutoka mapumziko, Yanga walipata bao la pili lililofungwa na Max Nzengeli, bao lililotokana na krosi ya chini iliyopigwa na Allan Okello.
Yanga walikamilisha bao la tatu lililofungwa na Depu katika dakika ya 60 na baada ya kufunga bao hilo aliinua juu jezi ya Pacome akiwaonesha mashabiki wa Yanga.
KMC yapewa kipigo cha mwisho
Wakati Yanga wakipata ushindi wa mwisho uliowapa taji hilo, KMC wao walipewa kipigo cha mwisho cha kuaga ligi hiyo walipofungwa bao 1-0 na Simba.
Bao hilo pekee la ushindi kwa Simba lilipatikana katika dakika ya 55 kwa mkwaju wa penalti, mfungaji akiwa ni Jospin Loemba.
KMC sasa inaaga rasmi ligi hiyo pamoja na Mtibwa Sugar wakati mechi za play off za kuwania kubaki katika ligi hiyo zitawahusisha mafahari wa jiji la Mbeya timu za Prisons na Mbeya City zilizomaliza nafasi ya 13 na 14.
Matokeo ya mechi za mwisho za ligi hiyo ni kama ifuatavyo…
Azam 2-0 Dodoma Jiji
Mashujaa 0-1 Prisons
Namungo 2-1 Mtibwa
Mbeya City 0-0 TRA United
Coastal Union 2-1 Pamba Jiji
Fountain Gate 4-3 Singida BS

The post Yanga yabeba taji la tano ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/01/yanga-yabeba-taji-la-tano-ligi-kuu/feed/ 0
Yanga yapigwa faini Sh milioni 30, yatembeza bakuli https://www.greensports.co.tz/2026/05/12/yanga-yapigwa-faini-sh-milioni-30-yatembeza-bakuli/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/12/yanga-yapigwa-faini-sh-milioni-30-yatembeza-bakuli/#respond Tue, 12 May 2026 08:26:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14650 Na mwandishi wetuKlabu ya soka ya Yanga imetozwa faini ya Sh milioni 30 kwa kosa la wachezaji wake na maofisa wa benchi la ufundi kukataa kutumia chumba kilichotengwa kwa ajili ya kubadilishia nguo kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamhuyo, Dar es Salaam.Tukio hilo lilitokea wakati wa mechi baina yao na Simba iliyochezwa Mei 3, 2026 […]

The post Yanga yapigwa faini Sh milioni 30, yatembeza bakuli first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya soka ya Yanga imetozwa faini ya Sh milioni 30 kwa kosa la wachezaji wake na maofisa wa benchi la ufundi kukataa kutumia chumba kilichotengwa kwa ajili ya kubadilishia nguo kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamhuyo, Dar es Salaam.
Tukio hilo lilitokea wakati wa mechi baina yao na Simba iliyochezwa Mei 3, 2026 kwenye uwanja huo ambapo Yanga inadaiwa badala yake walitumia nyumba iliyo karibu na uwanja huo kitendo ambacho ni kinyume na kanuni.
Adhabu hiyo imetokana na kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kilichokaa Mei 9, 2026 na taarifa hiyo kutolewa Jumatatu Mei 10, 2026 na tayari klabu hiyo imeanza kuembeza bakuli ikiomba kuchangiwa fedha hizo na wanachama na mashabiki wake.
Katika adhabu hiyo, meneja wa Yanga Walter Harson pia amefungiwa mechi tatu pamoja na kutozwa faini ya Sh milioni moja kwa kosa la kumsukuma kiungo wa Simba, Clatous Chama.
Yanga pia imepewa onyo kali kwa kosa la kuchelewa kuwasili uwanjani siku ya mechi hiyo, ambapo badala ya kuwasili saa 10:30 alasiri wao waliwasili saa 10:35 yaani dakika tano baadaye.
Katika adhabu hizo hizo, shabiki wa Yanga aliyetajwa kwa jina la Mohamed Mposo ambaye amekuwa akiambatana na maofisa wa ufundi wa klabu hiyo amefungiwa kuingia uwanjani kwa kipindi cha miezi 12.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, shabiki huyo anadaiwa kuingia kwenye eneo la kuchezea wakati wa mapumziko jambo ambalo ni kinyume cha sheria lakini pia alionekana akimwaga vimiminika tukio ambalo linahusishwa na ushirikina.
Nayo klabu ya Dodoma Jiji imetozwa faini ya Sh milioni tano kwa kosa la kuchelewa kufika kwenye kikao cha maandalizi ya kabla ya mechi yao na Mtibwa Sugar na kufika wakiwa pungufu bila ya vifaa vyote vinavyohitajika kwa mujibu wa taratibu.
Katika Ligi ya Championship, klabu ya Hausung FC ya Njombe imetozwa faini ya Sh milioni moja kwa kosa la kuchelewa kwa dakika 20 kufika kwenye kikao cha maandalizi ya mechi yao na Geita Gold.
Mchezaji Said Kubwa wa TMA FC amefungiwa michezo mitatu na faini ya Sh 500,000 kwa makosa yanayohusishwa na vitendo vya ushirikina kwa kumwaga vimiminika uwanjani, katika mechi yao na Gunners FC.
Adhabu kama hiyo pia imetolewa kwa Mohamed Lipangala na Joel Stephano pia wa TMA ambao pia wanadaiwa kuonekana wakichimba vitu kwenye nguzo za goli la timu yao, vitendo vyote hivyo vinahusishwa na ushirikina.
Klabu ya Hausung imepoteza mchezo wake na Mbeya Kwanza kwa kosa la kushindwa kufika uwanjani bila sababu, badala yake Mbeya Kwanza imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu.
Hausung pia kwa kosa hilo hilo imetozwa faini ya Sh milioni moja pamoja na mwenyekiti wake, Erasto Haule kufungiwa kujihusisha na soka kwa kipindi cha miezi 12.

The post Yanga yapigwa faini Sh milioni 30, yatembeza bakuli first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/12/yanga-yapigwa-faini-sh-milioni-30-yatembeza-bakuli/feed/ 0
Kocha Pedro atimuliwa Yanga https://www.greensports.co.tz/2026/05/06/kocha-pedro-atimuliwa-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/06/kocha-pedro-atimuliwa-yanga/#respond Wed, 06 May 2026 19:43:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14608 Na mwandishi wetuUongozi wa Yanga umetangaza kumtimua kocha wake mkuu, Pedro Concalves na kwa kipindi hiki hadi mwisho wa msimu timu itakuwa chini ya makocha Abdihamid Moalim na Patrick Mabedi.Taarifa ya mtendaji mkuu wa klabu hiyo iliyopatikana leo Jumatano Mei 6, 2026 imemshukuru Pedro kwa kipindi chote ambacho amekuwa na timu hiyo na kumtakia kila […]

The post Kocha Pedro atimuliwa Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Uongozi wa Yanga umetangaza kumtimua kocha wake mkuu, Pedro Concalves na kwa kipindi hiki hadi mwisho wa msimu timu itakuwa chini ya makocha Abdihamid Moalim na Patrick Mabedi.
Taarifa ya mtendaji mkuu wa klabu hiyo iliyopatikana leo Jumatano Mei 6, 2026 imemshukuru Pedro kwa kipindi chote ambacho amekuwa na timu hiyo na kumtakia kila la heri katika majukumu yake yajayo.
Yanga katika taarifa hiyo hata hivyo haikuweka bayana nini hasa sababu ya kufikia uamuzi wa kuachana na Pedro lakini inadhaniwa kuwa mwenendo wa timu hiyo haukuwa ukiwafurahisha viongozi.
Kabla ya mechi yao ya fainali ya Kombe la Muungano dhidi ya mahasimu wao Simba iliyochezwa Aprili 29, 2026, kulikuwa na fununu za kocha huyo kutimuliwa.
Pedro hata hivyo alikuwa na timu hiyo lakini mwisho wa siku walishindwa kutamba baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 na uvumi wa kutimuliwa ukaibuka tena kwa kasi.
Simba walicheza mechi nyingine na Yanga Mei 3, 2026, mechi ya Ligi Kuu NBC na kutoka sare ya mabao 2-2 na mara baada ya mechi hiyo habari za kutimuliwa kocha huyo ziliibuka tena kwa kasi zaidi.
Katika habari hizo ilikuwapo moja ya uwongo kwenye mitandao ya jamii ikiuhusisha uongozi wa Yanga na uamuzi wa kumtimua kocha huyo lakini hakukuwa na ukweli wowote hadi ilipotoka taarifa rasmi ya leo.
Pedro kocha ambaye anatokea nchini Ureno, alianza rasmi kuinoa Yanga Oktoba mwaka jana akiichukua timu kutoka kwa Roman Folz.

The post Kocha Pedro atimuliwa Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/06/kocha-pedro-atimuliwa-yanga/feed/ 0
Yanga yaisulubu Mbeya City 6-0 https://www.greensports.co.tz/2026/04/18/yanga-yaisulubu-mbeya-city-6-0/ https://www.greensports.co.tz/2026/04/18/yanga-yaisulubu-mbeya-city-6-0/#respond Sat, 18 Apr 2026 19:53:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14537 Na mwandishi wetuVinara wa Ligi Kuu NBC, Yanga wameendelea kudhihirisha umahiri wao katika ligi hiyo kwa kuichapa Mbeya City mabao 6-0 katika mechi iliyopigwa Alhamisi Machi 16, 2026 kwenye dimba la KMC, Mwenge Dar es Salaam.Yanga ilianza kuonesha makali yake katika dakika ya saba ya mchezo huo kwa bao la Prince Dube aliyeutumia vyema mpira […]

The post Yanga yaisulubu Mbeya City 6-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Vinara wa Ligi Kuu NBC, Yanga wameendelea kudhihirisha umahiri wao katika ligi hiyo kwa kuichapa Mbeya City mabao 6-0 katika mechi iliyopigwa Alhamisi Machi 16, 2026 kwenye dimba la KMC, Mwenge Dar es Salaam.
Yanga ilianza kuonesha makali yake katika dakika ya saba ya mchezo huo kwa bao la Prince Dube aliyeutumia vyema mpira wa kona uliopigwa na Pacome Zouzoua.
Wakati Mbeya City wakianza kupambana kutaka kusawazisha bao hilo, dakika tatu baadaye walikatishwa tamaa kwa kufungwa bao la pili lililofungwa na Pacome.
Hali ikazidi kuwa ngumu kwa timu hiyo kutoka Mbeya baada ya kuchapwa bao la tatu mfungaji akiwa Maxi Nzengeli kabla ya timu hiyo kuokota tena mpira kwenye nyavu zao dakika ya 44 kwa bao la Pacome.
Katika dakika za nyongeza kabla ya timu kwenda mapumziko, Mohamed Hussein Zimbwe Jr aliipatia Yanga bao la tano baada ya kuinasa pasi ya Alan Okelo na kuzifanya timu hizo kwenda mapumziko Yanga wakiwa mbele kwa mabao 5-0.
Bao la sita lililohitimisha karamu ya mabao ya Yanga lilijazwa wavuni kwa mara nyingine na Prince Dube katika dakika ya 82
Ushindi huo unazidi kuiimarisha Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi wakati kwa Mbeya City hali inazidi kuwa mbaya ambapo katika mechi zake 19, timu hiyo imekusanya pointi 17 tu ikizidi kujiweka katika hatari ya kushuka daraja.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo, Mashujaa na Singida Black Stars ziligawana pointi moja moja baada ya kutoka sare ya bao 1-1, mabao ya washindi yakifungwa na Elvis Rupia kwa Singida BS na Mgandila Shaaban kwa Mashujaa.

The post Yanga yaisulubu Mbeya City 6-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/04/18/yanga-yaisulubu-mbeya-city-6-0/feed/ 0
Matokeo ya sare yaongezeka Yanga https://www.greensports.co.tz/2026/03/19/matokeo-ya-sare-yaongezeka-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/19/matokeo-ya-sare-yaongezeka-yanga/#respond Thu, 19 Mar 2026 13:00:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14462 Na mwandishi wetuMatokeo ya sare ya 0-0 yameendelea kushika kasi kwa timu ya Yanga katika Ligi Kuu NBC baada ya kupata matokeo hayo mara nyingine katika mechi na TRA United iliyopigwa Jumatano Machi 18, 2026 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.Hii ni sare ya tatu katika mechi za hivi karibuni za timu hiyo baada […]

The post Matokeo ya sare yaongezeka Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Matokeo ya sare ya 0-0 yameendelea kushika kasi kwa timu ya Yanga katika Ligi Kuu NBC baada ya kupata matokeo hayo mara nyingine katika mechi na TRA United iliyopigwa Jumatano Machi 18, 2026 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Hii ni sare ya tatu katika mechi za hivi karibuni za timu hiyo baada ya kupata matokeo kama hayo dhidi ya Simba na Azam FC na sasa TRA United.
Yanga hata hivyo ilicheza mechi hiyo bila ya wachezaji wake kadhaa tegemeo kina Dickson Job, Ibrahim Bacca, Depu na wengineo na kama hiyo haitoshi timu hiyo ilipata pigo baada ya mshambuliaji wake Prince Dube kushindwa kumaliza mchezo.
Dube aliyeianza mechi kwa matumaini makubwa aliishia dakika ya 21 na nafasi yake kuingia Emmanuel Mwanengo ambaye dakika 10 baada ya kuanza kipindi cha pili alipata nafasi ya kufunga lakini mpira wa kichwa alioupiga uliokolewa.
Safu ya ulinzi ya Yanga pamoja na kuwakosa nyota wake mahiri lakini ikiwa chini ya kipa Djigui Diarra, Bakari Mwamnyeto na Frank Assinki ilifanikiwa kudhibiti mashambulizi ya hapa na pale ya TRA.
TRA kwa muda mrefu ilipambana ikitengeneza mashambulizi kutokea pembeni yakiongozwa na Ramadhan Chobwedo na Joseph Akandwabo lakini uimara wa mabeki wa pembeni wa Yanga, Mohamed Hussein aliyekuwa upande wa kushoto na Israel Mwenda aliyekuwa kulia walidhibiti mashambulizi hayo.
Mwenda naye hakuweza kumaliza dakika zote 90 kwani mapema kipindi cha pili alitolewa na nafasi yake kuingia Yao Kouassi ambaye amekuwa majeruhi kwa muda mrefu.
Mambo yaliwaendea kombo TRA na kulazimika kucheza na wachezaji 10 kwa takriban dakika 20 baada ya Mzamiru Yassin kupewa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje ingawa TRA walijipanga vizuri kwa dakika zilizobaki na kuidhibiti Yanga.
Mara baada ya dakika 90 kukamilika, Yanga walionekana kuwa katika hali ya huzuni wakati kwa TRA ilikuwa shangwe wakifurahia matokeo ya sare dhidi ya Yanga ambao pia ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo.
Sare hiyo hata hivyo haijaweza kuishusha Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, badala yake timu hiyo inaendelea kushika usukani ikiwa na pointi 37 katika michezo 15 ikijivunia kutopoteza mchezo hata mmoja.

The post Matokeo ya sare yaongezeka Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/19/matokeo-ya-sare-yaongezeka-yanga/feed/ 0
Bao la Depu laibeba Yanga https://www.greensports.co.tz/2026/03/13/bao-la-depu-laibeba-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/13/bao-la-depu-laibeba-yanga/#respond Fri, 13 Mar 2026 17:23:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14422 Na mwandishi wetuBao pekee la Depu limeiwezesha Yanga kunyakua pointi tatu muhimu katika mechi ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Prisons, mechi iliyopigwa Alhamisi, Machi 12 2026 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.Haikuwa rahisi kwa Yanga kupata bao hilo badala yake walihitaji dakika 79 za kupambana ndipo Laurindo Aurélio au Depu alipofunga bao hilo baada […]

The post Bao la Depu laibeba Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Bao pekee la Depu limeiwezesha Yanga kunyakua pointi tatu muhimu katika mechi ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Prisons, mechi iliyopigwa Alhamisi, Machi 12 2026 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Haikuwa rahisi kwa Yanga kupata bao hilo badala yake walihitaji dakika 79 za kupambana ndipo Laurindo Aurélio au Depu alipofunga bao hilo baada ya kipa wa Prisons, Mussa Mbisa kushindwa kuokoa mpira wa adhabu uliopigwa na Alan Okelo.
Mbisa awali aliuzuia mpira huo lakini ulirudi uwanjani na ndipo Depu alipoiwahi na kupata bao lililoamsha shangwe za mashabiki wa Yanga ambao walionekana kuanza kukata tamaa.
Prisons kwa muda mrefu wa mchezo huo ni kama vile waliingia uwanjani kwa lengo la kuizuia Yanga isipate bao mpango ambao ulionekana kuzaa matunda kwa kipindi chote cha kwanza kabla mambo hayajawaendea kombo dakika ya 79.
Ushindi huo unazidi kuiimarisha Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo na sasa inakuwa imefikisha pointi 35 katika mechi 13 ikifuatiwa na JKT Tanzania inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 27.
Ligi hiyo inaendelea Ijumaa Machi 13, 2026 kwa mechi kati ya Mashujaa watakaokuwa wenyeji wa Fountain Gate kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

The post Bao la Depu laibeba Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/13/bao-la-depu-laibeba-yanga/feed/ 0