Tuchel - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 19 Jul 2026 14:57:26 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Tuchel - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Trump naye amlaumu Tuchel https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/trump-naye-amlaumu-tuchel/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/trump-naye-amlaumu-tuchel/#respond Sun, 19 Jul 2026 11:32:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14805 New York, MarekaniRais wa Marekani, Donald Trump naye ameibuka na kumlaumu kocha wa England, Thomas Tuchel kwa mbinu alizotumia katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Argentina.Katika hoja yake hiyo, Trump kwa kiasi kikubwa amehoji majukumu ya ulinzi ambayo Thuchel alimpa mshambuliaji wa timu hiyo, Harry Kane hasa katika kipindi cha […]

The post Trump naye amlaumu Tuchel first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Rais wa Marekani, Donald Trump naye ameibuka na kumlaumu kocha wa England, Thomas Tuchel kwa mbinu alizotumia katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Argentina.
Katika hoja yake hiyo, Trump kwa kiasi kikubwa amehoji majukumu ya ulinzi ambayo Thuchel alimpa mshambuliaji wa timu hiyo, Harry Kane hasa katika kipindi cha pili.
Tuchel ameshutumiwa baada ya England kufungwa mabao 2-1 na Argentina na kutolewa katika hatua ya nusu ya fainali ingawa bado anaungwa mkono na mabosi wa Chama cha Soka England na inaaminika ndiye atakayeiongoza timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Ulaya 2028 au Euro 2028.
England walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Anthony Gordon dakika ya 55 na baada ya hapo Tuchel alijaza mabeki sita nyuma lakini Argentina walimzidi ujanja na kufunga mabao mawili dakika za 85 na 92 (90+2).
Akitoa hoja yake dhidi ya mbinu za Tuchel, Trump awali alianza kwa kumsifia Kane na kukumbushia walivyowahi kucheza naye golfu kwenye ufukwe wa West Palm takriban miezi 18 iliyopita.

“England mna mchezaji mzuri, mchezaji ambaye niliwahi kucheza naye golfu, mnamjua huyo? ni Harry ambaye amekuwa mchezaji mahiri, nafikiri walikosea kumfanya awe mchezaji wa ulinzi,” alisema Trump.

Trump alifafanua akisema kilichotokea ni kwamba England walipata bao la kuongoza na baada ya hapo walichofanya ni kumchukua mchezaji wao bora na kumuweka katika eneo la ulinzi.

The post Trump naye amlaumu Tuchel first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/trump-naye-amlaumu-tuchel/feed/ 0
Tuchel ajitetea baada ya England kutolewa https://www.greensports.co.tz/2026/07/18/tuchel-ajitetea-baada-ya-england-kutolewa/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/18/tuchel-ajitetea-baada-ya-england-kutolewa/#respond Sat, 18 Jul 2026 19:34:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14802 Miami, MarekaniKocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Thomas Tuchel ametetea maamuzi yake katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Argentina licha ya timu hiyo kushindwa.Akizungumza kabla ya mechi ya kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Ufaransa, kocha huyo Mjerumani alisema kama anahitajika mtu wa kulaumiwa basi yeye yuko […]

The post Tuchel ajitetea baada ya England kutolewa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Miami, Marekani
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Thomas Tuchel ametetea maamuzi yake katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Argentina licha ya timu hiyo kushindwa.
Akizungumza kabla ya mechi ya kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Ufaransa, kocha huyo Mjerumani alisema kama anahitajika mtu wa kulaumiwa basi yeye yuko tayari kubeba zigo la lawama.
Tuchel hata hivyo alisema hana cha kujutia na kuongeza kuwa timu yake ndiyo iliyoumizwa zaidi kuliko yeyote na kwamba kilichotokea ni jeraha ambalo wanalazimika kulibeba.
Katika mechi hiyo, England walikuwa wakipambana kuweka rekodi ya kufikia hatua ya fainali ya Kombe la Dunia mara ya kwanza tangu kufanya hivyo mara ya mwisho mwaka 1966, miaka 60 iliyopita.
Kilichotokea katika mechi hiyo kiliiumiza mno England kwani baada ya kuongoza kwa bao 1-0 mambo yalibadilika mwishoni na kujikuta wakilala kwa mabao 2-1 huku wakipigwa presha na Messi.
Mabao ya Argentina yaliyopatikana dakika za 85 na 90 (+2) yaliwaumiza mno mashabiki wa England huku baadhi ya wachambuzi wakilaumu maamuzi kadhaa ya Tuchel ikiwamo kujihami zaidi badala ya kushambulia.
Alipoulizwa ni kwa nini timu yake ilicheza kwa kujihami zaidi Tuchel alisema hicho ndicho kilichotakiwa kufanywa kwa namna Argentina walivyokuwa na hajutii uamuzi wake katika hilo.

“Nilichukua maamuzi mengi, niliamini fikra zangu, uzoefu wangu, niliamini katika upambanaji wangu na nilichukua maamuzi kwa lengo la kuisaidia timu kupata matokeo lakini hatukupata matokeo,” alisema Tuchel.


England inacheza mechi ya kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Ufaransa, mechi itakayopigwa Jumamosi Julai 18, 2026 wakati mechi ya fainali kati ya Argentina na Hispania itapigwa Jumapili Julai 19, 2026.

The post Tuchel ajitetea baada ya England kutolewa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/18/tuchel-ajitetea-baada-ya-england-kutolewa/feed/ 0
Tuchel ataka England wacheze kwa raha zao https://www.greensports.co.tz/2025/06/10/tuchel-ataka-england-wacheze-kwa-raha-zao/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/10/tuchel-ataka-england-wacheze-kwa-raha-zao/#respond Tue, 10 Jun 2025 09:59:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13565 London, EnglandKocha wa England, Thomas Tuchel amewataka wachezaji kucheza kama wanapokuwa mazoezini kwa kucheza wakiwa na nyuso za furaha wakati wakijiandaa kuivaa Senegal, leo Jumanne, Juni 10, 2025.Tuchel, alionekana kutofurahia uchezaji wa timu yake licha ya ushindi wa bao 1-0 ambao timu hiyo iliupata dhidi ya Andorra katika mechi ya kufuzu fainali za Kombe la […]

The post Tuchel ataka England wacheze kwa raha zao first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
London, England
Kocha wa England, Thomas Tuchel amewataka wachezaji kucheza kama wanapokuwa mazoezini kwa kucheza wakiwa na nyuso za furaha wakati wakijiandaa kuivaa Senegal, leo Jumanne, Juni 10, 2025.
Tuchel, alionekana kutofurahia uchezaji wa timu yake licha ya ushindi wa bao 1-0 ambao timu hiyo iliupata dhidi ya Andorra katika mechi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia, Jumamosi iliyopita.
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea alisema kwamba wachezaji wake walifanya mazoezi tofauti na sasa amewataka kucheza wakiwa huru na kufuata maelekezo.
Tuchel ambaye ni Mjerumani, alianza kazi ya kuinoa England Januari mwaka huu na mechi ya leo ya kirafiki dhidi ya Senegal ni mechi yake ya nne akiwa na timu hiyo.
“Naona tunafanya mazoezi tukiwa na tabasamu lakini hatuchezi mechi tukiwa na tabasamu, kwa hakika tunahitaji kuwa bora zaidi, tunatakiwa kuchangamka katika kundi letu, naona kama tunajitenga uwanjani,” alisema Tuchel.
Tuchel aliongeza kwa kusema kwamba timu hiyo ina mambo mengi mazuri ya kuyafanya nje ya uwanja wa mazoezi ambayo amekuwa akiyaona na kinachotakiwa ni kuhakikisha yote yanahamia uwanjani wakiwa kwenye mechi.
“Jambo la muhimu ni kuweka umakini katika kanuni za mchezo, kupeana maelekezo sahihi miongoni mwa wachezaji na kile tunachokitarajia katika majukumu yao,” alisema Tuchel.

The post Tuchel ataka England wacheze kwa raha zao first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/10/tuchel-ataka-england-wacheze-kwa-raha-zao/feed/ 0
Tuchel aanza kibarua England https://www.greensports.co.tz/2025/01/01/tuchel-aanza-kibarua-england/ https://www.greensports.co.tz/2025/01/01/tuchel-aanza-kibarua-england/#respond Wed, 01 Jan 2025 20:22:00 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12555 London, EnglanedKocha wa zamani wa Chelsea na Bayern Munich, Thomas Tuchel, leo Januari Mosi, 2025 ameanza rasmi kazi yake mpya ya kuinoa timu ya taifa ya England akiwa na mkataba wa miezi 18.Tuchel ambaye Oktoba mwaka jana, alitangazwa rasmi kuchukua nafasi hiyo iliyokuwa ikishikliwa na Gareth Southgate ataiongoza timu hiyo hadi baada ya fanali za […]

The post Tuchel aanza kibarua England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, Englaned
Kocha wa zamani wa Chelsea na Bayern Munich, Thomas Tuchel, leo Januari Mosi, 2025 ameanza rasmi kazi yake mpya ya kuinoa timu ya taifa ya England akiwa na mkataba wa miezi 18.
Tuchel ambaye Oktoba mwaka jana, alitangazwa rasmi kuchukua nafasi hiyo iliyokuwa ikishikliwa na Gareth Southgate ataiongoza timu hiyo hadi baada ya fanali za Kombe la Dunia 2026.
Ikiwa na Southgate, England ilifikia hatua ya fainali ya Kombe la Ulaya 2024 au Euro 2024 nchini Ujerumani lakini licha ya matarajio makubwa timu hiyo ilishindwa kutamba mbele ya Hispania waliobeba taji hilo.
Katika kibarua hicho kipya, Tuchel atakuwa akisaidiwa na Anthony Barry ambaye pia amefanya naye kazi tangu akiwa Chelsea na baadaye Bayern Munich.
England kwenye kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia 2026 imepangwa kundi moja na timu za Serbia, Latvia, Albania na Andora.
Kati ya timu hizo, Tuchel ambaye pia amewahi kuzinoa timu za Borussia Dortmund ya Ujeruani na PSG ya Ufaransa alisema anaziheshimu Serbia na Albania ambazo alisema zina uwezo wa kuibua mshangao.
Kibarua cha kwanza kwa Tuchel na timu ya England kwenye kufuzu Kombe la Dunia 2026 kitakuwa Machi 21 mwaka huu dhidi ya Albania na siku tatu baadaye dhidi ya Latvia mechi ambazo zitapigwa kwenye dimba la Wembley.
Mara baada ya kuondoka kwa Southgate, England imekuwa chini ya kocha wa muda, Lee Carsey ambaye ana rekodi ya kushinda mechi tano kati ya sita.

The post Tuchel aanza kibarua England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/01/01/tuchel-aanza-kibarua-england/feed/ 0
Tuchel kuinoa England? https://www.greensports.co.tz/2024/10/16/tuchel-kupewa-majukumu-england/ https://www.greensports.co.tz/2024/10/16/tuchel-kupewa-majukumu-england/#respond Wed, 16 Oct 2024 06:03:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12010 London, EnglandChama cha Soka England, (FA) kinadaiwa kuanza mazungumzo na kocha wa zamani wa klabu za Chelsea na Bayen Munich, Thomas Tuchel ili akabidhiwe jukumu la kuinoa timu ya taifa ya England.Iwapo mpango huo utafanikiwa Tuchel atakuwa kocha wa tatu wa kigeni kuinoa timu hiyo baada ya Sven Goran Eriksson wa Sweden na Fabio Capelo […]

The post Tuchel kuinoa England? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Chama cha Soka England, (FA) kinadaiwa kuanza mazungumzo na kocha wa zamani wa klabu za Chelsea na Bayen Munich, Thomas Tuchel ili akabidhiwe jukumu la kuinoa timu ya taifa ya England.
Iwapo mpango huo utafanikiwa Tuchel atakuwa kocha wa tatu wa kigeni kuinoa timu hiyo baada ya Sven Goran Eriksson wa Sweden na Fabio Capelo wa Italia kuwahi kuinoa timu hiyo.
Kwa sasa timu ya England inanolewa na kocha wa muda, Lee Carsley ambaye amekuwa akiinoa timu hiyo tangu kujiuzulu kwa Gareth Southgate ambaye alidumu kwa miaka minane.
Southgate aliamua kujiuzulu baada ya tmu hiyo kufikia hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Ulaya au Euro 2024 nchini Ujerumani lakini ikashindwa kutamba mbele ya Hispania waliobeba taji.
Taarifa kuhusu mpango huo ilieleza kuwa mazungumzo ya awali na kocha huyo Mjerumani yameshafanyika huku kocha huyo akipewa nafasi kubwa ya kuchukua kibarua hicho.
Tuchel alilazimika kuachana na klabu ya Bayern Mei mwaka huu licha ya kuwa na mwaka mmoja katika mkataba wake lakini aliondoka kwa kuwa mwenendo wa timu haukuwafurahisha mabosi wake.
Kocha huyo ambaye aliiwezesha Chelsea kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, mambo yake hayakuwa mazuri Bayern baada ya timu hiyo kushindwa kubeba taji la Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga ikiwa ni mara ya kwanza tangu msimu wa 2011-12.

The post Tuchel kuinoa England? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/10/16/tuchel-kupewa-majukumu-england/feed/ 0
Tuchel akataa kumrithi Ten Hag https://www.greensports.co.tz/2024/06/10/tuchel-akataa-kumrithi-ten-hag/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/10/tuchel-akataa-kumrithi-ten-hag/#respond Mon, 10 Jun 2024 07:30:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11284 Munich, UjerumaniKocha wa zamani wa Bayern Munich na Chelsea, Thomas Tuchel ambaye amekuwa akihusishwa na mipango ya kujiunga na Man United amejiweka kando na kazi hiyo kwa alichodai kuwamba kwa sasa anataka kupumzika.Tuchel, 50, ni kati ya makocha ambao katika siku za karibuni wamekuwa wakipewa nafasi kubwa ya kumrithi Erik Ten Hag ambaye kwa muda […]

The post Tuchel akataa kumrithi Ten Hag first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Kocha wa zamani wa Bayern Munich na Chelsea, Thomas Tuchel ambaye amekuwa akihusishwa na mipango ya kujiunga na Man United amejiweka kando na kazi hiyo kwa alichodai kuwamba kwa sasa anataka kupumzika.
Tuchel, 50, ni kati ya makocha ambao katika siku za karibuni wamekuwa wakipewa nafasi kubwa ya kumrithi Erik Ten Hag ambaye kwa muda mrefu sasa hatma yake Man United ipo njia panda.
Kwa sasa vigogo wa Man United wanafanya tathmini ya mwenendo wa timu yao kwa msimu mzima wa 2023-24 na bado hawajatoa hitimisho la nini kitafanyika kuelekea msimu ujao na hata Ten Hag hajawa na uhakika kama ataendelea kuinoa timu hiyo au la.
Wakati hayo yakiendelea zipo habari kwamba Tuchel aliwahi kukutana na mmiliki mwenza wa Man United Sir Jim Ratcliffe nchini Ufaransa ingawa undani wa mazungumzo ya wawili hao haukuwahi kuwekwa wazi.
Kwa upande wake, Tuchel ambaye pia amewahi kuzinoa klabu za PSG na Borussia Dortmund hata hivyo amedai kwamba kwa sasa anataka kupumzika baada ya kuachana na Bayern mwishoni mwa msimu.
Makocha wengine ambao wamekuwa wakitajwa kuchukua nafasi ya Ten Hag Man United ni pamoja na Graham Potter, Thomas Frank pamoja na kocha wa England, Gareth Southgate.

The post Tuchel akataa kumrithi Ten Hag first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/10/tuchel-akataa-kumrithi-ten-hag/feed/ 0
Tuchel atangaza, anaondoka Bayern https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/tuchel-atangaza-anaondoka-bayern/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/tuchel-atangaza-anaondoka-bayern/#respond Sat, 18 May 2024 17:06:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11011 Munich, UjerumaniKocha wa Bayern Munich, Thomas Tuchel amethibitisha kuwa ataachana na timu hiyo mara baada ya msimu huu licha ya kuwapo mazungumzo kuhusu uwezekano wa kuendelea na kibarua hicho.Bayern ilitangaza Februari mwaka huu kwamba imekubliana na Tuchel mwenye umri wa miaka 50 kuwa ataachana na timu hiyo akiwa amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake.Tuchel amepitia […]

The post Tuchel atangaza, anaondoka Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Kocha wa Bayern Munich, Thomas Tuchel amethibitisha kuwa ataachana na timu hiyo mara baada ya msimu huu licha ya kuwapo mazungumzo kuhusu uwezekano wa kuendelea na kibarua hicho.
Bayern ilitangaza Februari mwaka huu kwamba imekubliana na Tuchel mwenye umri wa miaka 50 kuwa ataachana na timu hiyo akiwa amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake.
Tuchel amepitia katika msimu mgumu na timu hiyo ambayo imepoteza taji la Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga mbele ya Bayer Leverkusen baada ya kulibeba kwa miaka 11 mfululizo.
Baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo walisikika hivi karibuni wakiendesha kampeni kumtaka kocha huyo wa zamani wa Chelsea kuendelea kuinoa timu hiyo lakini Tuchel amesema kwamba hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa katika suala hilo.
“Makubaliano yetu ya tangu Februari yanabaki kama yalivyo,” alisema Tuchel ambaye alikabidhiwa majukumu ya kuinoa timu hiyo, Machi 2023.
Habari za Tuchel kubaki Bayern zilipata nguvu baada ya kocha huyo kuiwezesha timu hiyo kuitoa Arsenal katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini ilijikuta ikishindwa kutamba mbele ya Real Madrid katika nusu fainali ya ligi hiyo.
Bayern imekuwa ikihaha kusaka mrithi wa Tuchel ambaye katika siku za karibuni zimekuwapo habari kwamba huenda akajiunga na Man United kuchukua nafasi ya Erik ten Hag.
Makocha waliotajwa kuwindwa na Bayern, Xabi Alonso wa Leverkusen na Ralf Rangnick wa timu ya taifa ya Austria wote wameikataa ofa hiyo.
Alonso alikataa ofa hiyo akidai kwamba anaamini bado anahitaji kumalizia kazi aliyoianza akiwa na Leverkusen wakati Rangnick naye alisema anataka kuendelea na kibarua chake Austria.

The post Tuchel atangaza, anaondoka Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/tuchel-atangaza-anaondoka-bayern/feed/ 0
Tuchel: Mwamuzi kaisaliti Bayern https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/tuchel-mwamuzi-kaisaliti-bayern/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/tuchel-mwamuzi-kaisaliti-bayern/#respond Fri, 10 May 2024 07:34:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10901 Madrid, HispaniaKocha wa Bayern Munich, Thomas Tuchel amesema kitendo cha mwamuzi kusimamisha mchezo kabla ya timu yake kufunga bao la kusawazisha katika mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid ni mfano wa usaliti.Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumatano usiku kwenye dimba la Bernabeu, Bayern walikuwa mbele kwa bao 1-0 hadi […]

The post Tuchel: Mwamuzi kaisaliti Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kocha wa Bayern Munich, Thomas Tuchel amesema kitendo cha mwamuzi kusimamisha mchezo kabla ya timu yake kufunga bao la kusawazisha katika mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid ni mfano wa usaliti.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumatano usiku kwenye dimba la Bernabeu, Bayern walikuwa mbele kwa bao 1-0 hadi dakika ya 88 baada ya Joselu aliyeingia kipindi cha pili kufunga bao la kwanza na kuongeza la pili katika dakika tatu.
Wakati Bayern ikiwa nyuma kwa mabao 2-1 katika dakika za nyongeza, Matthijs de Ligt aliifungia Bayern bao na kudhani kuwa alisawazisha lakini mshika kibendera tayari aliinua kidendera kuashiria kwamba mfungaji alikuwa ameotea.
Mabeki wa Real Madrid, walisimama kabla ya De Ligt kuujaza mpira wavuni na baadaye marudio ya kwenye televisheni yalionesha kuwa uamuzi wa awali usingekuwa wa mchezaji kuotea na hilo lingeweza kufanyiwa mapitio ya VAR.
Hata hivyo kwa kuwa mchezo ulishasimamishwa, VAR haikuweza kutumiwa jambo ambalo Tuchel amelitaja kuwa ni uamuzi mbaya mno na ambao pia ni kinyume na taratibu.
“Kumekuwa na uamuzi wa hovyo kutoka kwa mshika kibendera na mwamuzi, mwisho wa yote tunaona kama ni kusalitiwa,” alisema Tuchel.

“Mshika kibendera alisema samahani lakini hilo halisaidii kitu, kuinua kibendera katika kipindi kama hicho, mwamuzi aliona tulikuwa tunaupata mpira na kuupiga golini, ni ngumu kukubali lakini hivyo ndivyo mambo yalivyo,” alisema Tuchel.


Baadaye Tuchel alisema kwamba mwamuzi Szymon Marciniak ambaye pia ndiye aliyechezesha mechi ya fainali ya Kombe la Dunia 2022 pia aliomba msamaha lakini kwa Tuchel jambo hilo pia haliwezi kusaidia kitu.
Kwa ushindi huo, Real sasa inasubiri kuumana na Borussia Dortmund katika mechi ya fainali ambayo itapigwa Juni Mosi mwaka huu kwenye dimba la Wembley.

The post Tuchel: Mwamuzi kaisaliti Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/tuchel-mwamuzi-kaisaliti-bayern/feed/ 0
Tuchel anaweza kubaki Bayern https://www.greensports.co.tz/2024/05/04/tuchel-anaweza-kubaki-bayern/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/04/tuchel-anaweza-kubaki-bayern/#respond Sat, 04 May 2024 18:41:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10833 Munich, UjerumaniKocha wa Bayern Munich ambaye tayari amefikia makubaliano ya kuachana na timu hiyo baada ya msimu huu, Thomas Tuchel amesema pamoja na makubaliano hayo lakini lolote linawezekana.Mapema Feberuari mwaka huu klabu ya Bayern ilitangaza kuwa Tuchel ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 50 ataachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu baada ya […]

The post Tuchel anaweza kubaki Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Kocha wa Bayern Munich ambaye tayari amefikia makubaliano ya kuachana na timu hiyo baada ya msimu huu, Thomas Tuchel amesema pamoja na makubaliano hayo lakini lolote linawezekana.
Mapema Feberuari mwaka huu klabu ya Bayern ilitangaza kuwa Tuchel ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 50 ataachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu baada ya makubaliano ya pande zote mbili.
Uamuzi wa Bayern umetokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo kwenye Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga ambapo timu hiyo iliyokuwa ikiwania kulibeba taji hilo kwa mara ya 12 mfululizo imeshindwa kufanya hivyo.
Badala yake Bayer Leverkusen imeibuka kuwa tishio kwenye ligi hiyo na tayari imeshatawazwa kuwa bingwa mpya wa taji hilo na kuiacha Bayern na rekodi yake ya kubeba taji la ligi hiyo kwa misimu 11 mfululizo.
Mambo hata hivyo yako tofauti kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo timu hiyo imefuzu hatua ya nusu fainali na katika mechi ya kwanza dhidi ya Real Madrid imefanikiwa kutoka sare ya mabao 2-2.
Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kuendelea kuwa na timu hiyo Tuchel alisema kwamba hayo ni makubaliano ambayo hayawezi kubadilika lakini hapo hapo akasema kwamba lolote linawezekana.

“Ni kweli kwamba unaweza kubadili mkataba wowote kwa makubaliano, na hapa tuna mkataba ambao tulikubaliana kuumaliza mapema, lakini katika mkataba huo pia lolote linawezekana,” alisema Tuchel.


Taarifa nyingine hata hivyo zinadai kwamba Tuchel anajiandaa kuachana na timu hiyo na hesabu zake zipo katika klabu ya Man United ambayo kocha wake, Erik ten Hag naye anapitia wakati mgumu.

The post Tuchel anaweza kubaki Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/04/tuchel-anaweza-kubaki-bayern/feed/ 0
Tuchel kwa raha zake https://www.greensports.co.tz/2024/04/18/tuchel-kwa-raha-zake/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/18/tuchel-kwa-raha-zake/#respond Thu, 18 Apr 2024 06:19:36 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10650 Munich, UjerumaniKocha wa Bayern Munich anayejiandaa kuachana na timu hiyo, Thomas Tuchel amejawa furaha akijivunia kuiwezesha timu hiyo kufuzu nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuichapa Arsenal bao 1-0.Ushindi huo unakuwa faraja kubwa kwa kocha huyo anayepitia katika kipindi kigumu cha lawama na shutuma akiwa tayari ametangaziwa rasmi siku ya kuondoka katika timu […]

The post Tuchel kwa raha zake first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Kocha wa Bayern Munich anayejiandaa kuachana na timu hiyo, Thomas Tuchel amejawa furaha akijivunia kuiwezesha timu hiyo kufuzu nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuichapa Arsenal bao 1-0.
Ushindi huo unakuwa faraja kubwa kwa kocha huyo anayepitia katika kipindi kigumu cha lawama na shutuma akiwa tayari ametangaziwa rasmi siku ya kuondoka katika timu hiyo baada ya mabosi Bayern kutoridhishwa na utendaji wake.
Arsenal na Bayern ziliumana jana Jumatano usiku katika mechi ya marudiano ya robo fainali ya ligi hiyo na Bayern kutoka na ushindi wa bao hilo pekee lililofungwa na Joshua Kimmich baada ya sare ya mabao 2-2 katika mechi ya kwanza.
Katika siku za karibuni Tuchel amekuwa akishutumiwa kwa matokeo mabaya ya timu hiyo ikiwamo kupoteza taji la Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga kwa mara ya kwanza baada ya kuweka rekodi ya kulibeba kwa miaka 11 mfululizo.
Mwenendo mbaya wa timu hiyo uliwafanya mabosi wa Bayern kutangaza hivi karibuni uamuzi wa kuachana na kocha huyo mara baada ya msimu huu.
“Hivyo ndivyo ilivyo, nilijitoa kwa yote tangu siku ya kwanza na nimejitoa hadi siku ya mwisho,” alisema Tuchel ambaye sasa anakuwa kocha wa kwanza Mjerumani mwenye rekodi ya kuzifikisha timu za mataifa matatu tofauti nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, alifanya hivyo na Chelsea mwaka 2021 pamoja na PSG mwaka 2020.

“Nusu fainali ni hatua kubwa, timu nne za mwisho, inafurahisha, ni jambo kubwa furaha na faraja, hii ni hatua ya kipekee, tumeifunga moja ya timu kubwa katika Ligi Kuu England, tunasubiri kuona ushindi huu utakuwa na maana gani kwa klabu hii, msimu hata hivyo bado haujafikia mwisho,” alisema Tuchel.


Tuchel aliongeza kuwa wanajivunia kufikia hatua hiyo kubwa na sasa wanasubiri kuona hali itakavyokuwa katika wiki mbili zijazo kwenye mechi ya kwanza ya nusu fainali dhidi ya Real Madrid.
Wakati huo huo, rais wa Bayern, Herbert Hainer baada ya ushindi dhidi ya Arsenal, alimpongeza Tuchel na kusifia kazi yake akisema kwamba mbinu za kocha huyo zilikuwa za kipekee.
Man City nje
Katika mechi nyingine ya nusu fainali mabingwa watetezi Man City ambao msimu uliopita walibeba mataji matatu, ‘treble’ ndoto zao za kubeba taji hilo msimu huu ziliota mbawa baada ya sare ya bao 1-1 na Real Madrid na hatimaye Real Madrid kusonga mbele kupitia penalti.
Katika mechi hiyo ambayo Man City walikuwa nyumbani Itihad, Real Madrid ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Rodrygo katika dakika ya 12 wakati Man City walisawazisha kupitia kwa De Bruyne dakika ya 76.
Katika mechi ya kwanza baina ya timu hizo iliyopigwa kwenye dimba la Barnebeu, mechi iliisha kwa sare ya mabao 3-3 na hivyo matokea ya jumla kuwa sare ya 4-4 na hatimaye Real Madrid kusonga mbele kwa mikwaju ya penalti 4-3 ambapo waliofunga kwa Real Madrd ni Bellingham, Lucas Vazquez, Nacho Fernandez na Antonio Rudiger wakati Luka Modric alikosa. Kwa City waliofunga ni Julian Alvarez, Phil Foden na Ederson Moraes wakati Mateo Kovacic na Bernado Silva walikosa.
Mechi za nusu fainali zitakazopigwa Aprili 30 na Mei mosi ni kama ifuatavyo
Real Madrid v Bayern Munich
PSG v B.Dortmund

The post Tuchel kwa raha zake first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/18/tuchel-kwa-raha-zake/feed/ 0