Saudi Arabia - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 12 Dec 2024 10:37:31 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Saudi Arabia - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Rasmi, Saudia mwenyeji Kombe la Dunia 2034 https://www.greensports.co.tz/2024/12/11/rasmi-saudia-mwenyeji-kombe-la-dunia-2034/ https://www.greensports.co.tz/2024/12/11/rasmi-saudia-mwenyeji-kombe-la-dunia-2034/#respond Wed, 11 Dec 2024 19:38:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12386 Nyon, SwitzerlandFainali za Kombe la Dunia za Wanaume za 2034 zitafanyika nchini Saudi Arabia wakati Hispania, Ureno na Morocco kwa pamoja wataandaa fainali hizo kwa mwaka 2030.Sambamba na hilo, mechi tatu za fainali michuano hiyo kwa mwaka 2030, zitachezwa katika nchi za Argentina, Paraguay na Uruguay kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 100 ya Fifa.Uamuzi […]

The post Rasmi, Saudia mwenyeji Kombe la Dunia 2034 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Nyon, Switzerland
Fainali za Kombe la Dunia za Wanaume za 2034 zitafanyika nchini Saudi Arabia wakati Hispania, Ureno na Morocco kwa pamoja wataandaa fainali hizo kwa mwaka 2030.
Sambamba na hilo, mechi tatu za fainali michuano hiyo kwa mwaka 2030, zitachezwa katika nchi za Argentina, Paraguay na Uruguay kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 100 ya Fifa.
Uamuzi huo uliotangazwa siku za nyuma ulithibitishwa rasmi leo Jumatano katika mkutano mkuu wa Fifa uliohusisha wajumbe wote wa mataifa 211 waliopiga kura kwa njia ya mtandao.
Nchi ya Norway ilitangaza kujitenga katika zoezi hilo kwa sababu ya kutokuwa na imani na taratibu za Fifa za kuteua nchi mwenyeji wa fainali hizo na si kwa sababu Saudi Arabia au Saudia imetangazwa kuwa mwenyeji.
Nayo Switzerland iliomba kupitia chama chake cha soka uwakilishi wao utambuliwe katika mukhtasari wa vikao vya mkutano mkuu.
Jana Jumanne Chama cha Soka Switzerland kilitoa taarifa kikidai kwamba kitaridhia Saudi Arabia kuwa mwenyeji wa fainali hizo lakini kikataka masuala ya haki za binadamu nchini humo yasimamiwe na Fifa pamoja na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Denmark nayo kupitia chama chake cha soka yaani DBU kilitangaza kuunga mkono taratibu zote za kuipa Saudi Arabia uenyeji wa fainali hizo lakini kikataka Fifa waangazie masuala ya haki za binadamu nchini humo.
Saudi Arabia imekuwa ikituhumiwa kwa kutumia fedha nyingi kwenye michezo kama kinga ya kuusafisha utawala wa kifalme na rekodi mbaya ya haki za binadamu.
Tayari Saudi Arabia imejenga viwanja vya soka vinne kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2034 na mpango uliopo ni kujenga viwanja 15.

The post Rasmi, Saudia mwenyeji Kombe la Dunia 2034 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/12/11/rasmi-saudia-mwenyeji-kombe-la-dunia-2034/feed/ 0
Baada ya shabiki kumchapa bakora mchezaji… https://www.greensports.co.tz/2024/04/16/baada-ya-shabiki-kumchapa-bakora-mchezaji/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/16/baada-ya-shabiki-kumchapa-bakora-mchezaji/#respond Tue, 16 Apr 2024 07:13:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10616 Abu Dhabi, UAEShirikisho la Soka Saudi Arabia (SAFF) litapitia upya sheria zinazowahusu mashabiki wa soka baada ya tukio la shabiki mmoja kumchapa bakora mshambuliaji wa klabu ya Al Ittihad, Abderrazak Hamdallah.Katika hafla ya utoaji tuzo baada ya Al Hilal kuichapa Al Ittihad mabao 4-1 kwenye mechi ya fainali ya Saudi Super Cup mjini Abu Dhabi, […]

The post Baada ya shabiki kumchapa bakora mchezaji… first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Abu Dhabi, UAE
Shirikisho la Soka Saudi Arabia (SAFF) litapitia upya sheria zinazowahusu mashabiki wa soka baada ya tukio la shabiki mmoja kumchapa bakora mshambuliaji wa klabu ya Al Ittihad, Abderrazak Hamdallah.
Katika hafla ya utoaji tuzo baada ya Al Hilal kuichapa Al Ittihad mabao 4-1 kwenye mechi ya fainali ya Saudi Super Cup mjini Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), shabiki mmoja alitoka jukwaani akaingia uwanjani na kumchapa bakora, Hamdallah.
Hamdallah ambaye pia ni mchezaji wa kimataifa wa Morocco baada ya kufanyiwa kitendo hicho, kitu pekee alichofanya ni kummwagia shabiki huyo maji baada ya mzozo baina ya wawili hao.
SAFF kwa kushirikiana na Chama cha Wanasoka Saudi Arabia (PFA) katika taarifa yake ilieleza kushtushwa na tukio hilo la shabiki kumvamia mchezaji wa klabu ya Al Ittihad.

“Kama ilivyo kwa mashirikisho mengine ya soka ya AFC (Asia) na wanachama wengine wa Fifa, kipaumbele cha SAFF ni kulinda usalama na kuhakikisha burudani kwa kila ambaye anapenda kuangalia na kucheza soka,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.


Taarifa hiyo pia ilifafanua kuwapo mpango wa kufanya mapitio ya kina kwenye kanuni za usimamizi una lengo la kuhakikisha sheria na kanuni zinawekwa kwa lengo la kutoa adhabu ili kuzuia kujirudia kwa tukio hilo.
“Na ingawa tukio hilo lilitokea nje ya Saudi Arabia, lakini SAFF na PFA tunasimama pamoja katika kipaumbele cha kuhakikisha ustawi wa viwanja vya soka na tutaendelea kutekeleza hatua stahiki ili kuweka mazingira salama kwa kila mmoja anayehusika na soka.”

The post Baada ya shabiki kumchapa bakora mchezaji… first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/16/baada-ya-shabiki-kumchapa-bakora-mchezaji/feed/ 0
Yaya Toure kocha msaidizi Saudi Arabia https://www.greensports.co.tz/2023/11/03/yaya-toure-kocha-msaidizi-saudi-arabia/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/03/yaya-toure-kocha-msaidizi-saudi-arabia/#respond Fri, 03 Nov 2023 17:03:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8357 Riyadh, Saudi ArabiaKiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu za Barcelona na Man City, Yaya Toure (pichani) ameteuliwa kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Saudi Arabia na atakuwa msaidizi wa Roberto Mancini.Yaya aliwahi kuwa chini ya Mancini katika klabu ya Man City, amepewa jukumu hilo ikiwa ni miezi […]

The post Yaya Toure kocha msaidizi Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabia
Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu za Barcelona na Man City, Yaya Toure (pichani) ameteuliwa kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Saudi Arabia na atakuwa msaidizi wa Roberto Mancini.
Yaya aliwahi kuwa chini ya Mancini katika klabu ya Man City, amepewa jukumu hilo ikiwa ni miezi takriban mitatu imepita tangu Mancini apewe majukumu ya kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.
Nyota huyo wa zamani wa Barca, aliichezea Man City kwa miaka minane kuanzia mwaka 2010 na kuanza kazi ya ukocha ambapo amewahi kuwa kocha katika akademi ya klabu ya Tottenham Hotspur.
Yaya mwenye umri wa miaka 40 sasa, pia amewahi kufanya kazi ya ukocha katika klabu za Donetsk Olympic ya Ukraine na Grozny ya Urusi.
Wakati akicheza soka la ushindani, ameiwakilisha timu ya taifa ya Ivory Coast mara 101 na kuiwezesha kubeba Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015 na kushinda mataji 18 katika klabu mbalimbali barani Ulaya katika nchi za Ugiriki, Hispania, England na China.
Saudi Arabia kwa sasa inapambana kuinua hadhi ya soka lake ikitajwa kuwa katika maandalizi makali ya fainali za Kombe la Dunia 2034 ambapo nchi hiyo inatajwa kuwa mwenyeji.

The post Yaya Toure kocha msaidizi Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/03/yaya-toure-kocha-msaidizi-saudi-arabia/feed/ 0
Saudi Arabia mwenyeji Kombe la Dunia 2034 https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/saudi-arabia-mwenyeji-kombe-la-dunia-2034/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/saudi-arabia-mwenyeji-kombe-la-dunia-2034/#respond Wed, 01 Nov 2023 19:44:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8327 Riyadh, Saudi ArabiaSaudi Arabia ndio nchini pekee iliyoomba kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2034 na hivyo inapewa nafasi kubwa ya kuandaa fainali hizo baada ya Australia kutangaza kujitoa.Chama cha Soka Australia kilithibitisha uamuazi wake wa kujitoa katika mbio hizo saa chache kabla ya jana Jumanne ambayo ni siku ya mwisho iliyowekwa na […]

The post Saudi Arabia mwenyeji Kombe la Dunia 2034 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabia
Saudi Arabia ndio nchini pekee iliyoomba kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2034 na hivyo inapewa nafasi kubwa ya kuandaa fainali hizo baada ya Australia kutangaza kujitoa.
Chama cha Soka Australia kilithibitisha uamuazi wake wa kujitoa katika mbio hizo saa chache kabla ya jana Jumanne ambayo ni siku ya mwisho iliyowekwa na Fifa kwa nchi kuthibitisha nia ya kuandaa fainali hizo.
“Tumefikia hitimisho la kutoomba kuwa wenyeji katika michuano ya 2034,” ilieleza taarifa ya Chama cha Soka Australia.
Badala yake chama hicho kimetangaza nia yake ya kuweka nguvu katika mpango wa kuandaa fainali za Kombe la Asia kwa wanawake mwaka 2026 pamoja na Kombe la Dunia la Klabu kwa mwaka 2029.
Fainali za Kombe la Dunia 2026 zinatarajia kufanyika katika nchi za Marekani, Mexico na Canada wakati Moroco, Ureno na Hispania zitakuwa wenyeji wa fainali za mwaka 2030 ambapo pia mechi nyingine tatu za fainali hizo zitafanyika katika nchi za Argentina, Paragua na Uruguay.
Awali Fifa walidai kuwa fainali za Kombe la Dunia 2034 zingefanyika kati ya Asia au Oceania na nia ya Australia kutaka kuwa mwenyeji ilionekana kama ndio nchi pekee ambayo ingeweza kushindana na Saudi Arabia katika mbio hizokabla ya kutangaza kujitoa katika hatua za mwisho.
Saudi Arabia pamoja na kulalamikiwa kwa kukiuka haki za binadamu lakini inapewa nafasi kubwa ya kuandaa fainali hizo katika ubora hasa baada ya Qatar iliyotiliwa shaka kufanikiwa kuandaa fainali hizo mwaka jana kwa mafanikio makubwa.

The post Saudi Arabia mwenyeji Kombe la Dunia 2034 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/saudi-arabia-mwenyeji-kombe-la-dunia-2034/feed/ 0
Al-Ittihad wamfuata Salah England https://www.greensports.co.tz/2023/09/05/al-ittihad-wamfuata-salah-england/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/05/al-ittihad-wamfuata-salah-england/#respond Tue, 05 Sep 2023 07:50:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7665 London, EnglandJopo la vigogo wa klabu ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia limetua England kuishawishi Liverpool kwa mara ya mwisho ili ikubali kuwauzia mshambuliaji wao, Mohamed Salah kwa ada inayofikia Pauni 200 milioni kabla ya keshokutwa Alhamisi.Alhamisi ndiyo siku ya mwisho kabla ya kufungwa rasmi kwa dirisha la usajili kwa ligi ya soka ya Saudi Arabia […]

The post Al-Ittihad wamfuata Salah England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Jopo la vigogo wa klabu ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia limetua England kuishawishi Liverpool kwa mara ya mwisho ili ikubali kuwauzia mshambuliaji wao, Mohamed Salah kwa ada inayofikia Pauni 200 milioni kabla ya keshokutwa Alhamisi.
Alhamisi ndiyo siku ya mwisho kabla ya kufungwa rasmi kwa dirisha la usajili kwa ligi ya soka ya Saudi Arabia au Saudi Pro Ligi na kama Al-Ittihad itamkosa kabla ya siku hiyo mpango huo utakuwa umefeli.
Liverpool tayari imeshasema kwamba mshambuliaji huyo kutoka Misri ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 31 hauzwi, hiyo ni baada ya awali Al-Ittihad kumtangazia ofa ya Pauni 150 milioni.
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp hataki kusikia habari ya Salah kuuzwa na kama akiuzwa mtu wa kwanza kukasirika atakuwa kocha huyo ambaye anaamini Salah ni mchezaji muhimu kwenye kikosi chake.
Juzi Jumapili, Salah aliifungia Liverpool bao wakati timu hiyo ikiibwaga Aston Villa 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu England huku Klopp akisema Salah amejidhatiti kuhakikisha anabaki Liverpool msimu huu.
Klopp pamoja na kutoa kauli hiyo lakini kinachoonekana ni kama vile hana uhakika wa asilimia 100 kwamba Salah ni lazima abaki Liverpool.

“Hakuniambia (kama anabaki) lakini hana sababu ya kuniambia hilo, kila kitu kinaonekana, ni kama anazungumza hilo mazoezini kwa kujituma kwake na tabia zake, tulikuwa na kikao wiki hii na kikao hakikuwa kuhusu tuliyoyafanya siku za nyuma bali kilihusu nini tutakifanya siku zijazo,” alisema Klopp.


Wakati hatma ya Salah ikiwa hivyo, mchezaji huyo tayari amewashuhudia wachezaji wenzake aliowahi kuwa nao Liverpool kina Fabinho, Roberto Firmino, Jordan Anderson na Sadio Mane wote wakitimkia Saudi Arabia.

The post Al-Ittihad wamfuata Salah England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/05/al-ittihad-wamfuata-salah-england/feed/ 0
Liverpool yasisitiza, Salah hauzwi. https://www.greensports.co.tz/2023/09/02/liverpool-yasisitiza-salah-hauzwi/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/02/liverpool-yasisitiza-salah-hauzwi/#respond Sat, 02 Sep 2023 19:47:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7642 Liverpool, EnglandKlabu ya Liverpool imekataa ofa ya Pauni milioni 150 kutoka klabu ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia inayomtaka mshambuliaji wake, Mohamed Salah (pichani) na kusisitiza kuwa mshambuliaji huyo hauzwi.Salah alijiunga na Liverpool, mwaka 2017 akitokea Roma ya Italia, mwaka jana alisaini mkataba mpya na Liverpool wa miaka mitatu lakini katika siku za karibuni amekuwa akitakiwa […]

The post Liverpool yasisitiza, Salah hauzwi. first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Liverpool, England
Klabu ya Liverpool imekataa ofa ya Pauni milioni 150 kutoka klabu ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia inayomtaka mshambuliaji wake, Mohamed Salah (pichani) na kusisitiza kuwa mshambuliaji huyo hauzwi.
Salah alijiunga na Liverpool, mwaka 2017 akitokea Roma ya Italia, mwaka jana alisaini mkataba mpya na Liverpool wa miaka mitatu lakini katika siku za karibuni amekuwa akitakiwa na Al-Ittihad.
Wiki iliyopita, kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp alisema kwamba Salah amejitoa kwa asilimia 100 kwa ajili ya klabu hiyo ya Anfield na jana Ijumaa kocha huyo alisisitiza kwa mara nyingine akisema kwmaba mchezaji huyo hauzwi.
“Msimamo unabaki vile vile, hakika hakuna shaka katika hilo, hivyo ndivyo ilivyo na hakuna zaidi ya hilo,” alisema Klopp.
Na ingawa hadi jana Ijumaa usiku ambayo ilikuwa siku ya mwisho kwa usajili Liverpool ilikuwa na hofu ya kumpoteza mshambuliaji huyo ingawa hata sasa lolote linaweza kutokea kwa kuwa kipindi cha usajili kwa ligi ya Saudi Arabia kinafikia ukomo Septemba 7.
Katika mechi tatu alizocheza tangu kuanza kwa msimu mpya wa 2023-24, Salah tayari ameifungia Liverpool bao moja na ana asisti mbili huku akiwa mmoja wa washambuliaji tegemeo wa timu hiyo.

“Mohamed anabaki kuwa mchezaji wa Liverpool, kama tungekuwa na mpango wa kuondoka Liverpool mwaka huu tusingesaini mkataba mpya mwaka jana,” alisema Ramy Abbas Issa ambaye ni wakala wa Salah.


The post Liverpool yasisitiza, Salah hauzwi. first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/02/liverpool-yasisitiza-salah-hauzwi/feed/ 0
Rais Uefa apuuza kinachoendelea Saudi Arabia https://www.greensports.co.tz/2023/09/01/rais-uefa-apuuza-kinachoendelea-saudi-arabia/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/01/rais-uefa-apuuza-kinachoendelea-saudi-arabia/#respond Fri, 01 Sep 2023 12:49:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7633 London, EnglandRais wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) Aleksander Ceferin (pichani) amepuuza kinachoitwa ushindani na tishio kutoka ligi ya soka Saudi Arabia ‘Saudi Pro Ligi’ akiifananisha ligi hiyo na ile ya China iliyokuja juu mwishowe ikakwama.Katika siku za karibuni, wachezaji mastaa wa Ulaya wamekuwa wakikimbilia Saudi Arabia baada ya kutangaziwa mikataba minono yenye fedha nyingi.Ceferin […]

The post Rais Uefa apuuza kinachoendelea Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Aleksandre Ceferine

London, England
Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) Aleksander Ceferin (pichani) amepuuza kinachoitwa ushindani na tishio kutoka ligi ya soka Saudi Arabia ‘Saudi Pro Ligi’ akiifananisha ligi hiyo na ile ya China iliyokuja juu mwishowe ikakwama.
Katika siku za karibuni, wachezaji mastaa wa Ulaya wamekuwa wakikimbilia Saudi Arabia baada ya kutangaziwa mikataba minono yenye fedha nyingi.
Ceferin hata hivyo amesema kwamba makosa yaliyofanywa katika Ligi ya China ni hayo hayo ambayo sasa yanafanywa na Saudi Arabia na kwamba hiyo si namna nzuri.
“Walinunua wachezaji wanaoelekea mwisho kwenye soka kwa kuwatangazia pesa nyingi, soka la China halikuendelea na mwisho wa yote China hawakufuzu Kombe la Dunia,” alisema Ceferin.
Hii ni mara ya pili kwa Ceferin kutoa kauli hiyo akionekana kutoihofia Saudi Arabia ingawa watu wengine wamekuwa na hisia tofauti kuhusu nchi hiyo hasa inapolinganishwa na China.
China iliutikisa ulimwengu wa soka kwa fujo kwa kusajili wachezaji mastaa wa Ulaya kabla ya kuanza kukwama mwaka 2017 na hadi sasa jambo hilo halipo tena.
Saudi Arabia nayo inahofiwa kuangukia katika mtego wa China licha ya kuelezwa kuwa mbali na kutoa fedha nyingi za usajili, nchi hiyo pia ina mipango ya muda mrefu ya uwekezaji katika soka la vijana na imemteua Michael Emenalo kuwa mkurugenzi wa soka anayesimamia mipango ya maendeleo ya vijana.
Kocha wa Man City, Pep Guardiola ambaye wachezaji wake wawili nyota Riyad Mahrez na Aymeric Laporte wametimkia Saudi Arabia amesema nguvu ya fedha ya nchi hiyo imebadili soko la uhamisho wa wachezaji na kuzitaka klabu kubwa Ulaya kuwa makini na kinachoendelea.
Kwa upande wake, mkurugenzi mkuu wa Ligi Kuu England (EPL), Richard Masters amesema kwamba umaarufu unaojitokeza katika soka la Saudi Arabia hauwezi kumfanya awe na hofu kwa sana.

The post Rais Uefa apuuza kinachoendelea Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/01/rais-uefa-apuuza-kinachoendelea-saudi-arabia/feed/ 0
Mancini kocha mkuu Saudi Arabia https://www.greensports.co.tz/2023/08/28/mancini-kocha-mkuu-saudi-arabia/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/28/mancini-kocha-mkuu-saudi-arabia/#respond Mon, 28 Aug 2023 18:37:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7555 Riyadh, Saudi ArabiaAliyekuwa kocha wa timu ya Taifa ya Italia, Roberto Mancini ameteuliwa kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Saudi Arabia ikiwa ni takriban wiki mbili baada ya kujiuzulu kuinoa timu ya Italia.Mancini ameiongoza vyema Italia katika fainali za Kombe la Ulaya 2020 ‘Euro 2020’ na kuiwezesha kubeba taji hilo kwa kuwabwaga […]

The post Mancini kocha mkuu Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabia
Aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa ya Italia, Roberto Mancini ameteuliwa kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Saudi Arabia ikiwa ni takriban wiki mbili baada ya kujiuzulu kuinoa timu ya Italia.
Mancini ameiongoza vyema Italia katika fainali za Kombe la Ulaya 2020 ‘Euro 2020’ na kuiwezesha kubeba taji hilo kwa kuwabwaga wenyeji England kwa penalti katika mechi iliyopigwa kwenye dimba la Wembley.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 58 ambaye pia amewahi kuinoa Man City, akiwa na timu ya Italia amejiwekea rekodi ya kuiongoza katika mechi 37 bila kupoteza hata moja hadi kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2022 zilizofanyika Qatar, Novemba hadi Desemba mwaka jana.
Mancini amesaini mkataba wa kuinoa timu ya Saudi Arabia hadi mwaka 2027 na mtihani wake wa kwanza utakuwa Septemba 8 katika mechi ya kirafiki na Costa Rica itakayopigwa St James’ Park, Newcastle.

“Naamini hii ni fursa kubwa kwangu, kupata uzoefu wa soka katika nchi mpya hususan kutokana na kukuwa kwa umaarufu wa soka katika bara la Asia,” alisema Mancini.


Mancini ambaye ndiye aliyeipa Man City taji la kwanza la Ligi Kuu England, pia amewahi kuzinoa timu za Inter Milan, Lazio, Fiorentina, Galatasaray na Zenit St Petersburg.
Katika fainali za Kombe la Dunia mwaka jana, timu ya Saudi Arabia ikiwa chini ya kocha Mfaransa, Herve Renard iliushtua ulimwengu kwa kuilaza mabao 2-1 Argentina ambayo baadaye ndiyo iliyobeba taji hilo ingawa pamoja na ushindi huo, timu hiyo haikuweza kuvuka hatua ya makundi.

The post Mancini kocha mkuu Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/28/mancini-kocha-mkuu-saudi-arabia/feed/ 0
Saudi Arabia kwamvutia Mane https://www.greensports.co.tz/2023/07/25/saudi-arabia-kwamvutia-mane/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/25/saudi-arabia-kwamvutia-mane/#respond Tue, 25 Jul 2023 05:22:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7098 Munich, UjerumaniMshambuliaji wa Bayern Munich, Sadio Mane ameanza kuipigia hesabu ofa ya klabu ya Al-Nasr ya Saudi Arabia ambayo imeonesha nia ya kumsajili.Mane alijiunga na Bayern kabla ya msimu uliopita wa 2022-23 kwa ada ya Pauni 35 milioni akitokea Liverpool lakini hakuweza kuonesha makali aliyokuwa nayo wakati akiwa Liverpool na zipo habari kwamba Bayern ipo […]

The post Saudi Arabia kwamvutia Mane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Mshambuliaji wa Bayern Munich, Sadio Mane ameanza kuipigia hesabu ofa ya klabu ya Al-Nasr ya Saudi Arabia ambayo imeonesha nia ya kumsajili.
Mane alijiunga na Bayern kabla ya msimu uliopita wa 2022-23 kwa ada ya Pauni 35 milioni akitokea Liverpool lakini hakuweza kuonesha makali aliyokuwa nayo wakati akiwa Liverpool na zipo habari kwamba Bayern ipo tayari kumpiga bei.
Kocha wa timu hiyo, Thomas Tuchel anaonekana kupoteza matumaini na mchezaji huyo na hivyo yupo tayari kufanya biashara na klabu yoyote itakayojitokeza wakati Mane naye inadaiwa tayari amefanya mazungumzo ya awali na mabosi wa Al-Nasr.
Akiwa Liverpool, Mane alijipatia mafanikio kwa kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi Kuu England kabla ya kutimkia Bayern akidai kwamba ulikuwa wakati sahihi kwake kupata changamoto mpya ingawa mambo hayakwenda kama yalivyotarajiwa.
Kibaya zaidi, Mane aliingia katika mzozo na mchezaji mwenzake wa Bayern, Leroy Sane akidaiwa kumpiga ngumi Aprili mwaka huu baada ya timu hiyo kushindwa kutamba katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Man City.
Tukio hilo lilimfanya aondolewe kwenye kikosi cha Bayern na kutozwa faini ingawa baadaye alirudishwa lakini hadi mwisho wa msimu aliishia kufunga mabao 12 katika mechi 38.
Kocha Tuchel aliwahi kusema kwamba mambo hayajawa rahisi kwa Mane kwenye kikosi cha kwanza na ushindani umekuwa mkubwa mno kwake na mchezaji huyo anafahamu hilo na anaujua msimamo wa klabu.
Ikitokea mpango wa Mane kwenda klabu ya Al-Nasr ukafanikiwa, mchezaji huyo atakuwa ameungana na winga wa zamani wa klabu za Real Madrid na Mancheter United, Cristiano Ronaldo.

The post Saudi Arabia kwamvutia Mane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/25/saudi-arabia-kwamvutia-mane/feed/ 0
Mahrez naye Saudi Arabia kunamhusu https://www.greensports.co.tz/2023/07/14/mahrez-naye-saudi-arabia-kunamhusu/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/14/mahrez-naye-saudi-arabia-kunamhusu/#respond Fri, 14 Jul 2023 08:55:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6962 Riyadh, Saudi ArabiaKlabu ya Al Ahli ya Saudi Arabia inadaiwa kujiandaa kumnunua winga wa Man City, Riyad Mahrez (pichani) kwa ada inayotajwa kufikia Pauni 30 milioni.Habari za ndani zinadai kwamba kocha wa Man City, Pep Guardiola anajiandaa kufanya mazungumzo na Mahrez huku suala la ofa ya Saudi Arabia kwa mchezaji huyo likitarajiwa kutawala mjadala huo.Mahrez […]

The post Mahrez naye Saudi Arabia kunamhusu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabia
Klabu ya Al Ahli ya Saudi Arabia inadaiwa kujiandaa kumnunua winga wa Man City, Riyad Mahrez (pichani) kwa ada inayotajwa kufikia Pauni 30 milioni.
Habari za ndani zinadai kwamba kocha wa Man City, Pep Guardiola anajiandaa kufanya mazungumzo na Mahrez huku suala la ofa ya Saudi Arabia kwa mchezaji huyo likitarajiwa kutawala mjadala huo.
Mahrez ambaye pia ni nyota wa timu ya Taifa ya Algeria, mwenye umri wa miaka 32 anadaiwa kuwa tayari kuchangamkia ofa hiyo licha ya umuhimu alionao katika kikosi cha Man City lakini zipo habari kwamba amekuwa akitaka nyongeza ya mshahara.
Klabu ya Al Ahli katika mkakati wa kumpata Mahrez inadaiwa kumtengea Pauni 865,000 kwa wiki na mchezaji huyo ambaye amebakiwa na miaka miwili katika mkataba wake na Man City wenye thamani inayotajwa kufikia Pauni 6 milioni.
Katika msimu uliopita wa 2022-23 ambao Man City imeweka rekodi kwa kubeba mataji matatu kuanzia Ligi Kuu England (EPL) FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mahrez ameifungia timu hiyo mabao 10 katika mechi 41.
Wakati mpango wa Mahrez ukiwa hatua za awali, mchezaji mwingine ambaye huenda akaelekea Saudi Arabia ni nahodha wa Liverpool, Jordan Henderson ambaye amepewa ofa ya Pauni 700,000 kwa wiki ili kujiunga na timu ya Al-Ittifaq inayonolewa na nahodha wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard.

The post Mahrez naye Saudi Arabia kunamhusu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/14/mahrez-naye-saudi-arabia-kunamhusu/feed/ 0