Messi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 13 Jun 2024 07:43:03 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Messi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Messi kustaafia Inter Miami https://www.greensports.co.tz/2024/06/13/messi-kustaafia-inter-miami/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/13/messi-kustaafia-inter-miami/#respond Thu, 13 Jun 2024 07:43:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11320 New York, MarekaniNahodha wa timu ya taifa ya Argentina na mshambuliaji wa Inter Miami FC ya Marekani, Lionel Messi, 36, amesema huenda Inter Miami ikawa timu yake ya mwisho kucheza soka la ushindani kwani anafikiri kustaafia hapo.Messi ambaye ni mshindi wa tuzo za Ballon d’Or mara nane alijiunga na klabu hiyo ya Marekani majira ya […]

The post Messi kustaafia Inter Miami first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina na mshambuliaji wa Inter Miami FC ya Marekani, Lionel Messi, 36, amesema huenda Inter Miami ikawa timu yake ya mwisho kucheza soka la ushindani kwani anafikiri kustaafia hapo.
Messi ambaye ni mshindi wa tuzo za Ballon d’Or mara nane alijiunga na klabu hiyo ya Marekani majira ya kiangazi mwaka jana baada ya kuachana na PSG ya Ufaransa.
Kabla ya kujiunga na PSG, Messi alicheza kwa mafanikio na Barcelona ambapo alishinda mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mara nne pamoja na Ligi Kuu Hispania au La Liga mara 10.
Messi ambaye mwaka 2022 aliiwezesha Argentina kubeba Kombe la Dunia, mkataba wake wa sasa na Inter Miami unafikia okomo mwaka 2025 ingawa ana nafasi ya kuongeza mwaka mwingine mmoja.

“Nafikiri kwa wakati huu hii inaweza kuwa klabu yangu ya mwisho, japo sina mpango wa kuachana na soka moja kwa moja,” alisema Messi.


Kwa kiwango ambacho amekuwa akikionesha Messi haoneshi dalili zozote za kuelekea kustaafu, msimu huu amefunga mabao 12 na kutoa asisti 13 kwa Inter Miami inayoshika usukani wa Ligi Kuu Marekani maarufu MLS.
Messi kwa sasa anasubiri kuiwakilisha kwa mara nyingine Argentina katika fainali za Copa America zitakazofanyika nchini Marekani ambapo Argentina itakuwa ikiwania kulibeba taji hilo ambalo ililibeba mwaka 2021.
Akizungumzia maisha ya soka nchini Marekani, Messi alisema kwamba ulikuwa uamuzi mgumu kwa yeye kuondoka Ulaya na kuhamia Marekani lakini ushindi wake wa Kombe la Dunia umemfanya aweze kufikiria mambo kwa namna tofauti.
Messi pia alisema kwamba siku zote anapenda kucheza soka na kufanya mazoezi ya kujiandaa na mechi za kila mara lakini kidogo ana ameanza kuwa na hofu kwamba yote hayo yanaelekea mwisho hivyo analazimika kufurahia kila kitu kwa wakati huu.

The post Messi kustaafia Inter Miami first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/13/messi-kustaafia-inter-miami/feed/ 0
Messi aitaja siku ya kustaafu https://www.greensports.co.tz/2024/03/28/messi-aitaja-siku-ya-kustaafu/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/28/messi-aitaja-siku-ya-kustaafu/#respond Thu, 28 Mar 2024 07:13:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10399 New York, MarekaniNahodha wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi amesema umri pekee hauwezi kuwa sababu ya yeye kustaafu soka badala yake atafanya hivyo siku atakayoona hawezi tena kuisaidia timu kupata mafanikio.Messi, 36, ambaye aliiongoza Argentina kubeba Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar, hadi sasa hajaonesha dalili yoyote ya lini atastaafu na mkataba […]

The post Messi aitaja siku ya kustaafu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi amesema umri pekee hauwezi kuwa sababu ya yeye kustaafu soka badala yake atafanya hivyo siku atakayoona hawezi tena kuisaidia timu kupata mafanikio.
Messi, 36, ambaye aliiongoza Argentina kubeba Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar, hadi sasa hajaonesha dalili yoyote ya lini atastaafu na mkataba wake na klabu anayoichezea sasa ya Inter Miami FC ya Marekani unafikia ukomo Desemba 2025.
“Najua wakati ambao nitakuwa sichezi vizuri, wakati ambao nitakuwa mimi mwenyewe sifurahii, wakati ambao sitokuwa mwenye kuwasaidia wachezaji wenzangu,” alisema Messi.

“Huwa napenda kujifanyia tathmini, najua wakati nikiwa vizuri na wakati nikiwa hovyo, wakati nacheza vizuri na wakati nacheza vibaya na nitakapoona ni wakati wa kuchukua uamuzi wa kustaafu nitafanya hivyo bila kufikiria umri, nikijiona niko vizuri wakati wote nitajaribu kuendelea kushindana kwa sababu ni kitu ninachokipenda na najua namna ya kukifanya,” alisema Messi.


Messi ambaye amejipatia mafanikio zaidi akiwa na klabu ya Barcelona kabla ya kuhamia PSG ana rekodi ya kubeba tuzo nane za Ballon d’Or na anatarajia kuiongoza Argentina kwenye fainali za Copa America baadaye mwaka huu.
Akimzungumzia Messi hivi karibuni, kocha wa Inter Miami, Gerardo ‘Tata’ Martino alisema bado ni yule yule mwenye shauku ya ushindi kama ambavyo ilikuwa wakati akiwa kocha wake katika klabu ya Barcelona.
Naye kocha wa Argentina, Lionel Scaloni akimzungumzia Messi ambaye kwa sasa ni majeruhi, alisema ni mchezaji pekee ambaye ana uhakika wa nafasi kwenye kikosi chake.

The post Messi aitaja siku ya kustaafu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/28/messi-aitaja-siku-ya-kustaafu/feed/ 0
Messi aondolewa timu ya taifa https://www.greensports.co.tz/2024/03/19/messi-aondolewa-timu-ya-taifa/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/19/messi-aondolewa-timu-ya-taifa/#respond Tue, 19 Mar 2024 05:50:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10252 Buenos Aires, ArgentinaMshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi atazikosa mechi za kirafiki za timu hiyo dhidi ya El Salvador na Costa Rica kutokana na matatizo ya misuli yanayomkabili.Messi ambaye kwa sasa anaichezea Inter Miami FC ya Marekani wiki iliyopita alilazimika kuwekwa benchi muda mfupi baada ya kuanza kipindi cha pili […]

The post Messi aondolewa timu ya taifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Buenos Aires, Argentina
Mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi atazikosa mechi za kirafiki za timu hiyo dhidi ya El Salvador na Costa Rica kutokana na matatizo ya misuli yanayomkabili.
Messi ambaye kwa sasa anaichezea Inter Miami FC ya Marekani wiki iliyopita alilazimika kuwekwa benchi muda mfupi baada ya kuanza kipindi cha pili katika mechi ya taji la Concacaf Championship dhidi ya Nashvile ambayo Miami ilitoka na ushindi wa 3-1.
Mchezaji huyo pia Jumamosi iliyopita alikaa benchi tangu mwanzo katika mechi ya ligi dhidi ya D.C United na kocha wake, Gerardo “Tata” Martino kuahidi kufanya ufuatiliaji wa karibu ili kujua ukubwa wa majeraha yanayomsumbua mchezaji huyo.
Siku chache zilizopita jina la Messi lilitajwa katika kikosi cha Argentina kwa ajili ya mechi hizo zitakazopigwa mjini Los Angeles, Marekani lakini jana Jumatatu Chama cha Soka Argentina (AFA) kilitangaza kumuondoa mchezaji huyo aliyeiwezesha Argentina kubeba Kombe la Dunia mwaka 2022.
Taarifa ya AFA pia ilieleza kuwa Messi atakuwa karibu na timu ya taifa baadaye wiki hii ili kupata tiba na madaktari wa timu hiyo lengo likiwa ni kumfuatilia kwa karibu.
Argentina ambayo pia itawakosa mshambuliaji Paulo Dybala na kiungo Exequeil Palacio kutokana na kuwa majeruhi, imeandaa mechi hizo kujinoa kwa ajili ya michuano ya Copa America ambayo itafanyika Juni na Julai nchini Marekani.

The post Messi aondolewa timu ya taifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/19/messi-aondolewa-timu-ya-taifa/feed/ 0
Messi mchezaji bora wa Fifa https://www.greensports.co.tz/2024/01/16/messi-mchezaji-bora-wa-fifa/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/16/messi-mchezaji-bora-wa-fifa/#respond Tue, 16 Jan 2024 06:56:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9326 London, UingerezaNahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi ameshinda tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa Fifa wakati kocha wa Man City Pep Guardiola akishinda tuzo ya kocha bora.Messi ambaye pia anaichezea klabu ya Inter Miami ya Marekani, amewabwaga washambuliaji wawili mahiri, Erling Haaland wa Man City na Kylian Mbappe.Katika tuzo […]

The post Messi mchezaji bora wa Fifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, Uingereza
Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi ameshinda tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa Fifa wakati kocha wa Man City Pep Guardiola akishinda tuzo ya kocha bora.
Messi ambaye pia anaichezea klabu ya Inter Miami ya Marekani, amewabwaga washambuliaji wawili mahiri, Erling Haaland wa Man City na Kylian Mbappe.
Katika tuzo hizo, kipa wa Man City Ederson yeye ametwaa tuzo ya kipa bora akimbwaga kipa wa Real Madrid, Thibaut Courtois na Yassine Bounou wa Al Hilal.
Mafanikio ya kipa wa Man City kwa kiasi kikubwa yamebebwa na rekodi nzuri ya klabu hiyo kwenye msimu wa 2022-23 baada ya kubeba mataji matatu (treble) ya Ligi ya Mabingwa, FA pamoja na Ligi Kuu England.
Kwa Messi, nyota wa zamani wa Barcelona na PSG, hii inakuwa mara ya tatu kubeba tuzo hiyo ya Fifa tangu utaratibu wa tuzo hizo uanzishwe mwaka 2016, awali alibeba mwaka 2019 na 2022.
Wachezaji wafuatao pia wameteuliwa katika timu bora ya mwaka kwa upande wa wanaume; Thibaut Courtois (Real Madrid), John Stones, Kyle Walker, Ruben Dias na Bernardo Silva (Man City), Jude Bellingham (Real Madrid), Kevin de Bruyne na Erling Haaland (Man City), Kylian Mbappe (PSG), Lionel Messi (Inter Miami) na Vinicius Jr (Real Madrid).
Tuzo za mwanasoka bora wa mwaka wa Fifa huwa zinaangalia kalenda ya mwaka, ni tofauti na tuzo maarufu za Ballon d’Or ambazo zinaangalia mafanikio ya mchezaji husika katika msimu mmoja.

The post Messi mchezaji bora wa Fifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/16/messi-mchezaji-bora-wa-fifa/feed/ 0
Messi, Haaland, Mbappe wawania tuzo Fifa https://www.greensports.co.tz/2023/12/15/messi-haaland-mbappe-wawania-tuzo-fifa/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/15/messi-haaland-mbappe-wawania-tuzo-fifa/#respond Fri, 15 Dec 2023 12:26:36 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8879 Nyon, SwitzerlandBaada ya kubeba tuzo ya Ballon d’Or, Lionel Messi, kwa mara nyingine atachuana na washambuliaji wenzake, Erling Haaland na Kylian Mbappe katika tuzo za mwaka ya mchezaji bora wa Fifa mwaka 2023.Wakati Messi akichauana na kina Mbappe na Haaland, kwa upande wa wanawake mchuano utakuwa kati ya Aitana Bonmati, Linda Caicedo na Jennifer Hermoso […]

The post Messi, Haaland, Mbappe wawania tuzo Fifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Nyon, Switzerland
Baada ya kubeba tuzo ya Ballon d’Or, Lionel Messi, kwa mara nyingine atachuana na washambuliaji wenzake, Erling Haaland na Kylian Mbappe katika tuzo za mwaka ya mchezaji bora wa Fifa mwaka 2023.
Wakati Messi akichauana na kina Mbappe na Haaland, kwa upande wa wanawake mchuano utakuwa kati ya Aitana Bonmati, Linda Caicedo na Jennifer Hermoso ambapo mshindi atatangazwa Januari 15 mwakani jijini London.
Kwa upande wa tuzo ya Puskas ambayo inahusisha goli bora la mwaka, mchuano utakuwa kati ya Julio Enciso, Guilherme Madruga na Nuno Santos.
Sarina Wiegman, Emma Hayes na Pep Guardiola wamo kwenye orodha ya tuzo ya kocha bora wakati kwenye tuzo ya kipa wamo Mary Earps na Ederson.
Gumzo kubwa litakuwa kati ya Haaland wa Man City, Mbappe wa PSG na Messi wa Inter Miami ya Marekani ambao wamo kwenye orodha ya wachezaji 12 wanaowania tuzo hiyo.
Orodha ya wachezaji wanaowania tuzo, timu wanazochezea na mataifa yao ni kama ifuatavyo…
Wanaume:
Erling Haaland (Norway-Man City)
Kylian Mbappe (Ufaransa-PSG)
Lionel Messi (Argentina-Inter Miami)
Wanawake:
Aitana Bonmati (Hispania-Barcelona)
Linda Caicedo (Colombia-Real Madrid)
Jenni Hermoso (Hispania-Pachuca)

The post Messi, Haaland, Mbappe wawania tuzo Fifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/15/messi-haaland-mbappe-wawania-tuzo-fifa/feed/ 0
Ronaldo, Messi kukutana Saudi Arabia https://www.greensports.co.tz/2023/12/12/ronaldo-messi-kukutana-saudi-arabia/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/12/ronaldo-messi-kukutana-saudi-arabia/#respond Tue, 12 Dec 2023 17:47:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8852 Riyadh, Saudi ArabiaMastaa wa soka duniani, Lionel Messi wa Inter Miami FC ya Marekani na Cristiano Ronaldo wa A Nassr ya Saudi Arabia watakutana katika mechi ya Kombe la Saudi mapema mwakani.Hatua hiyo imekuja baada ya uongozi wa Inter Miami jana Jumatatu kwamba timu yao itashiriki katika michuano hiyo itakayopigwa mjini Riyadh ambapo Miami itacheza […]

The post Ronaldo, Messi kukutana Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabia
Mastaa wa soka duniani, Lionel Messi wa Inter Miami FC ya Marekani na Cristiano Ronaldo wa A Nassr ya Saudi Arabia watakutana katika mechi ya Kombe la Saudi mapema mwakani.
Hatua hiyo imekuja baada ya uongozi wa Inter Miami jana Jumatatu kwamba timu yao itashiriki katika michuano hiyo itakayopigwa mjini Riyadh ambapo Miami itacheza na Al Hilal Januari 29 na Februari mosi itaumana na Al Nassr.

“Mechi hizi zitatoa changamoto muhimu kwa timu zetu jambo ambalo litatufaidisha wakati tukielekea kwenye msimu mpya, tuna furaha katika kundi letu kwa kupata nafasi ya kuumana na timu za hadhi ya juu za Al Nassr na Al Hilal,” alisema mkurugenzi wa michezo wa Inter Miami, Chris Henderson.


Mechi hizo hazitokuwa mara ya kwanza kwa Ronaldo na Messi kukutana, kabla ya hapo wamewahi kukutana mara 35 kwenye klabu walizokuwa wakizichezea hapo kabla pamoja na timu zao za taifa.
Kwa mujibu wa rekodi katika mechi hizo, timu alizoziwakilisha Messi zilishinda mara 16 na Ronaldo mara 10 na sare mara tisa.
Katika mechi hizo za wafalme hao wa soka duniani, Messi ana mabao 21 na asisti 12 wakati Ronaldo ana mabao 20 na asisti moja.
Messi aliyetamba na Barcelona, majira ya kiangazi mwaka huu aliachana na klabu ya PSG na kujiunga na Inter Miami wakati Ronaldo ambaye pia amewahi kuzichezea timu kadhaa ikiwao Real Madrid aliachana na Man United Januari mwaka huu na kujiunga na Al Nassr.

The post Ronaldo, Messi kukutana Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/12/ronaldo-messi-kukutana-saudi-arabia/feed/ 0
Messi atakiwa asiwaze kustaafu https://www.greensports.co.tz/2023/11/29/messi-atakiwa-asiwaze-kustaafu/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/29/messi-atakiwa-asiwaze-kustaafu/#respond Wed, 29 Nov 2023 19:03:26 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8678 Buenos Aires, ArgentinaKocha wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Scaloni amemtaka nahodha na mshambuliaji wa timu hiyo, Lionel Messi kuendelea kucheza soka kadri inavyowezekana na kuachana na mpango wa kustaafu.Messi, 36 kwa sasa anacheza soka nchini Marekani katika Ligi ya MLS na timu ya Inter Miami FC huu ukiwa ndio msimu wake wa kwanza, […]

The post Messi atakiwa asiwaze kustaafu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Buenos Aires, Argentina
Kocha wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Scaloni amemtaka nahodha na mshambuliaji wa timu hiyo, Lionel Messi kuendelea kucheza soka kadri inavyowezekana na kuachana na mpango wa kustaafu.
Messi, 36 kwa sasa anacheza soka nchini Marekani katika Ligi ya MLS na timu ya Inter Miami FC huu ukiwa ndio msimu wake wa kwanza, bado hajasema lolote kuhusu lini hasa atastaafu hasa timu ya taifa.
“Tunamwambia Messi aendelee kucheza kadri atakavyoweza, amedhihirisha bado hajafikia mwisho, hujui ni lini ataachana na soka, ni jambo la kipekee,” alisema.
“Ni mtu mwenye furaha akiwa kwenye uwanja wa soka, na katika hilo nadhani ni vigumu kuwa kama Leo (Messi), uwanjani kwenye mpira ni mahali ambapo anakuwa mwenye furaha,” alisema Scaloni.

Mwaka jana Messi na Scaloni waliiongoza vyema Argentina na kushinda Kombe la Dunia katika fainali zilizofanyika Qatar na baada ya mafanikio hayo kulikuwa na fununu kwamba Messi angestaafu timu ya taifa jambo ambalo hadi sasa hajalifanya.
Messi kwa sasa ni majeruhi baada ya kuumia hivi karibuni wakati akiiwakilisha Argentina katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Brazil, mechi ambayo Argentina ilishinda kwa bao 1-0.

“Sijui kama nimebakisha mengi au machache katika soka lakini kwa mafanikio niliyoyapata kitu pekee nilichobakiza ni kuendelea kufurahia soka, na kwa kuwa niko fiti nitaendelea kushindana katika soka na natumaini itakuwa hivyo kwa muda mrefu,” alisema Messi.


Katika fainali za Kombe la Dunia 2022, Messi aliibuka mchezaji bora wa fainali hizo na mwezi uliopita alitwaa tuzo ya Ballon d’Or akiwabwaga washindani wake wa karibu, Kylian Mbappe wa PSG na Erling Haaland wa Man City.

The post Messi atakiwa asiwaze kustaafu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/29/messi-atakiwa-asiwaze-kustaafu/feed/ 0
Messi atamani kuagwa rasmi Barca https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/messi-atamani-kuagwa-rasmi-barca/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/messi-atamani-kuagwa-rasmi-barca/#respond Wed, 01 Nov 2023 06:55:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8316 Paris, UfaransaMshambuliaji wa Inter Miami FC ya Marekani, Lionel Messi amesema anadhani anatakiwa kupewa nafasi ya kuaga rasmi katika timu yake ya zamani ya Barcelona katika tukio ambalo angependa liambatane na mechi maalum.Tangu aondoke Barca Agosti 2021 na kujiunga na PSG ya Ufaransa akiwa mchezaji huru, kumekuwa na mazungumzo ya mchezaji huyo kuandaliwa mechi maalum […]

The post Messi atamani kuagwa rasmi Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Paris, Ufaransa
Mshambuliaji wa Inter Miami FC ya Marekani, Lionel Messi amesema anadhani anatakiwa kupewa nafasi ya kuaga rasmi katika timu yake ya zamani ya Barcelona katika tukio ambalo angependa liambatane na mechi maalum.
Tangu aondoke Barca Agosti 2021 na kujiunga na PSG ya Ufaransa akiwa mchezaji huru, kumekuwa na mazungumzo ya mchezaji huyo kuandaliwa mechi maalum ya kumpa heshima mchezaji huyo.
Mechi ya mwisho ya Messi akiwa na Barca ilikuwa Mei, 2021 dhidi ya Celta Vigo, mechi ambayo Barca ililala kwa mabao 2-1 lakini haikuwa na mashabiki kutokana na uwapo wa janga la Covid-19.
“Ningependa niwe na nafasi ya kuaga watu katika namna tofauti,” alisema Messi wakati akikabidhiwa tuzo ya Ballon d’Or, Jumatatu usiku jijini Paris, Ufaransa.
“Nafikiri kulikuwa na hali isiyopendeza wakati naondoka pale, si jambo zuri kwa mambo ambayo tulishirikiana nikiwa pale na kuishi pamoja, ninatakiwa kupata nafasi ya kuwaaga watu, Barcelona ni nyumbani, naipenda klabu na watu wa pale, kama kutakuwa na mechi maalum ningependa kuwa pale,” alisema Messi.
Messi ambaye ana rekodi ya kuifungia Barca mabao mengi, amekuwa na klabu hiyo kwa miaka 20 na kushinda jumla ya mataji 35 lakini kubwa zaidi ni.pale alipoiwezesha timu ya taifa ya Argentina kubeba Kombe la Dunia mwaka jana katika fainali zilizofanyika Qatar.
Mkurugenzi wa michezo wa Barca, Deco hivi karibuni alisema kwamba Messi atacheza mechi maalum ya kumuaga wakati rais wa klabu hiyo, Joan Laporta aliwahi kusema kwamba itapendeza Messi akiagwa rasmi katika mechi maalum ya kuumzindua uwanja mpya wa Nou Camp katika msimu wa 2025-26.
Naye mkurugenzi na mmiliki wa klabu ya sasa ya Messi ya Inter Miami, Jorge Mas alisema kwamba anaamini ni muhimu kwa Messi kupewa nafasi ya kuwaaga mashabiki wa Barca.

The post Messi atamani kuagwa rasmi Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/messi-atamani-kuagwa-rasmi-barca/feed/ 0
Messi atwaa Ballon d’Or https://www.greensports.co.tz/2023/10/31/messi-atwaa-ballon-dor/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/31/messi-atwaa-ballon-dor/#comments Tue, 31 Oct 2023 07:28:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8295 Paris, UfaransaMshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na Inter Miami FC ya Marekani, Lionel Messi ameibuka kinara wa tuzo ya Ballon d’Or kwa mara ya nane na kumbwaga mshambuliaji wa Man City, Erling Haaland ambaye pia alikuwa akipewa nafasi ya kubeba tuzo hiyo.Messi alipewa tuzo hiyo Jumatatu hii usiku katika hafla iliyofanyika jijini Paris, […]

The post Messi atwaa Ballon d’Or first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Paris, Ufaransa
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na Inter Miami FC ya Marekani, Lionel Messi ameibuka kinara wa tuzo ya Ballon d’Or kwa mara ya nane na kumbwaga mshambuliaji wa Man City, Erling Haaland ambaye pia alikuwa akipewa nafasi ya kubeba tuzo hiyo.
Messi alipewa tuzo hiyo Jumatatu hii usiku katika hafla iliyofanyika jijini Paris, akibebwa na mafanikio ya Argentina aliyoiongoza kubeba Kombe la Dunia mwaka jana katika fainali zilizofanyika Qatar.
Wakati Messi akiibeba tuzo hiyo, kiungo wa England na klabu ya Real Madrid ya Hispania, Jude Bellingham ametwaa tuzo ya mwanasoka bora kijana wa umri chini ya miaka 21 maarufu Kopa Trophy.
Mshambuliaji wa PSG na timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe ambaye alifunga hat trick katika mechi ya fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Argentina, katika kinyang’anyiro cha Ballon d’Or msimu huu ameshika nafasi ya tatu nyuma ya Haaland.

“Ni jambo zuri kuwa hapa kwa mara nyingine kufurahia tukio hili, kufanikiwa kubeba Kombe la Dunia pamoja na kutimiza ndoto yangu,” alisema Messi, nyota wa zamani wa Barcelona na PSG.


“Sikuweza kufikiria kwa namna nilivyopitia katika maisha yangu ya soka na kufanikiwa kushinda kila kitu nilichoshinda, bahati niliyo nayo ya kuwa katika timu bora ya kihistoria,” alisema Messi.
Kwa upande wa Haaland ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Norway ambaye ana rekodi ya kufunga mabao 36 katika mechi 35 za mashindano yote msimu uliopita na ambaye ameisaidia Man City kubeba mataji matatu ya Ligi Kuu England, FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya, amepewa heshima kwa tuzo ya Gerd Mulller kwa kuwa mfungaji bora.

“Napenda kuwashukuru Manchester City, klabu yote, pia napenda kuishukuru familia yangu na watu wote walio karibu nami kwa kuniwezesha kufika hapa nilipo leo,” alisema Haaland.


Messi kwa sasa ndiye anayeongoza kwa kutwaa tuzo ya Ballon d’Or mara nyingi akiwa amefanya hivyo mara nane na kumzidi mpinzani wake Cristiano Ronaldo ambaye mara ya mwisho alitwaa tuzo hiyo mwaka 2017.
Ronaldo ambaye ametwaa tuzo hiyo mara tano, safari hii jina lake halikuwamo katika orodha ya wachezaji waliotajwa kuwania tuzo hiyo ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 2003.
Kipa wa Argentina na klabu ya Aston Villa, Emiliano Martinez yeye ametwaa tuzo ya kipa bora maarufu Yashin Trophy
Martinez hata hivyo alijikuta katika wakati mgumu katika hafla ya utoaji tuzo hiyo kwa baadhi ya watu kuguna kwa kinachoaminika kuwa mashabiki walio wengi hawakufurahia aina ya ushangiliaji wake kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Vinicius Jr
Naye mshambuliaji wa Real Madrid, Vinicius Junior yeye alipewa tuzo ya Socrates kwa mchango wake wa nje ya uwanja na kuahidi kuendeleza vita dhidi ya ubaguzi wa rangi baada ya kujikuta akisakamwa na kadhia ya ubaguzi.
Vinicius Jr amepewa tuzo hiyo kwa kuanzisha taasisi ambayo inajenga shule kwenye maeneo ya watu wanaoishi katika mazingira magumu na pia amewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye elimu kwao nchini Brazil.
“Nitaendelea kuwa imara katika kupiga vita ubaguzi wa rangi, inasikitisha kuzungumzia habari za ubaguzi wa rangi siku hizi, lakini tunalazimika kuendelea na vita hii ili watu wasiathiriwe kwa sana,” alisema Vinicius.
Kiungo wa zamani wa Man United, Real Madrid na timu ya taifa ya England, David Beckham ndiye aliyemkabidhi Messi tuzo ya Ballon d’Or lakini kabla ya kumkabidhi alitoa salamu za heshima kwa marehemu Sir Bobby Charlton.
Sir Bobby Charlton ambaye alifariki dunia hivi karibuni akiwa na miaka 86 alikuwamo katika kikosi cha England kilichobeba Kombe la Dunia mwaka 1966.
Orodha ya wanasoka waliowania Ballon d’Or ni kama ifuatavyo…
Lionel Messi
Erling Haaland
Kylian Mbappe
Kevin De Bruyne
Rodri
Vinicius Jr
Julian Alvarez
Victor Osimhen
Bernardo Silva
Luka Modric
Ballon d’Or Wanawake
Naye kiungo wa timu ya wanawake ya Barcelona, Aitana Bonmatí (pichani chini) ameshinda tuzo ya Ballon d’Or kwa upande wa wanawake akibebwa na mafanikio yake katika timu hiyo pamoja na timu ya taifa ya Hispania.
Bonmatí, 25 ameiwezesha Barca kubeba taji la Ligi Kuu ya Wanawake Hispania au Liga F pamoja na lile la Ligi ya Mabingwa Ulaya na zaidi ya yote aliisaidia hispania kubeba Kombe la Dunia la Wanawake (WWC).

Katika fainali za WWC zilizofanyika hivi karibuni katika nchi za Australia na New Zealand aliibuka mchezaji bira na hivi karibuni Umoja wa Vyama vya Soka Ulaya (Uefa) ulimpa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka mwanamke.
Katika tuzo ya Ballon d’Or, Aitana aliwabwaga mshambuliaji wa Australia, Sam Kerr pamoja na winga wa Hispania, Salma Paralluelo.

The post Messi atwaa Ballon d’Or first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/31/messi-atwaa-ballon-dor/feed/ 1
Scaloni aikataa hadithi ya Messi kustaafu https://www.greensports.co.tz/2023/10/17/scaloni-aikataa-hadithi-ya-messi-kustaafu/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/17/scaloni-aikataa-hadithi-ya-messi-kustaafu/#respond Tue, 17 Oct 2023 06:48:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8120 Lima, PeruKocha wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Scaloni amewashangaa wanaohoji kustaafu kwa Lionel Messi kwenye timu ya taifa akidai kwamba yeye hawezi kupanga siku ya mchezaji huyo kustaafu.Messi, 36, mwishoni mwa mwaka jana aliiongoza Argentina kubeba Kombe la Dunia, amekuwa akihusishwa na mpango wa kustaafu soka la kimataifa lakini mwenyewe hajasema lini atachukua […]

The post Scaloni aikataa hadithi ya Messi kustaafu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Lionel Messi baada ya kubeba Kombe la Dunia 2022 katika fainali zilizofanyika Qatar.

Lima, Peru
Kocha wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Scaloni amewashangaa wanaohoji kustaafu kwa Lionel Messi kwenye timu ya taifa akidai kwamba yeye hawezi kupanga siku ya mchezaji huyo kustaafu.
Messi, 36, mwishoni mwa mwaka jana aliiongoza Argentina kubeba Kombe la Dunia, amekuwa akihusishwa na mpango wa kustaafu soka la kimataifa lakini mwenyewe hajasema lini atachukua uamuzi huo.
Alipoulizwa katika mkutano na waandishi wa habari, jana Jumatatu kuhusu mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Peru kama atajizoeza kupanga timu bila ya Messi, kocha huyo alisema, “Tuweke katika akili zetu kwamba Messi bado yuko na timu hii.”
“Ya nini kufikiria kuhusu siku ya kuondoka kwake, ukweli ni kwamba bado ana nguvu, tumuache, je tumeamua kuanza kumstaafisha, tunaharakisha mambo, ajabu,” alisema Scalloni.
Alhamisi iliyopita, Messi ambaye ni nahodha wa Argentina alianzia benchi na kuingia dakika ya 40 katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Paraguay, mechi ambayo Argentina ilishinda kwa bao 1-0.
Mwezi uliopita, Messi aliichezea Argentina na kufunga bao katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Ecuador lakini akakosekana katika mechi iliyofuata dhidi ya Bolivia ambayo Argentina ilishinda kwa mabao 3-0.
Katika siku za karibuni, Messi amekuwa akisumbuliwa na tatizo la misuli na licha ya matatizo hayo, Scalloni aliweka wazi nafasi ya mchezaji huyo katika timu yake ambayo kesho Jumatano itaumana na Peru.

“Messi yuko vizuri, amekuwa akiongeza dakika za mazoezi, tutafanya uamuzi Jumanne, ni suala la dakika anazoongeza na atacheza kwa muda gani, kama yuko vizuri mnajua ninachokifikiria, atacheza,” alisema Scaloni.


The post Scaloni aikataa hadithi ya Messi kustaafu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/17/scaloni-aikataa-hadithi-ya-messi-kustaafu/feed/ 0