Mashujaa - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 18 Apr 2024 19:36:17 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mashujaa - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Dabo aikubali kazi ya Mashujaa https://www.greensports.co.tz/2024/04/18/dabo-aikubali-kazi-ya-mashujaa/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/18/dabo-aikubali-kazi-ya-mashujaa/#respond Thu, 18 Apr 2024 19:36:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10662 Na mwandishi wetuBaada ya matokeo ya 0-0 jana Jumatano dhidi ya Mashujaa, kocha msaidizi wa Azam, Yuoussuf Dabo amesema walipambana na kufanya kila kitu ili kushinda mchezo huo lakini wapinzani wao walisimama imara na mwisho wamekubali kuvuna pointi moja.Azam ilipata matokeo hayo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na kupunguza utofauti wa pointi […]

The post Dabo aikubali kazi ya Mashujaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Baada ya matokeo ya 0-0 jana Jumatano dhidi ya Mashujaa, kocha msaidizi wa Azam, Yuoussuf Dabo amesema walipambana na kufanya kila kitu ili kushinda mchezo huo lakini wapinzani wao walisimama imara na mwisho wamekubali kuvuna pointi moja.
Azam ilipata matokeo hayo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na kupunguza utofauti wa pointi moja pekee na kinara Yanga mwenye pointi 56 baada ya mechi 21 dhidi yao wenye pointi 51 kwa mechi 23.
“Haiwezekani kushinda kila mchezo, tumejaribu kushinda, timejaribu kucheza vizuri lakini wapinzani nao walikuwa vizuri. Ni kweli inawezekana kushinda kila mchezo lakini lazima ukubali kuwa kuna muda unakutana na mpinzani ana wachezaji wazuri pia.
“Kwa hiyo tunakubali na tunaendelea kupambana na mechi zijazo ingawa matokeo haya yametufunza kitu na tunapaswa kubadili mawazo yetu kuhusu ushindi na kuendelea kupambana bado safari haijaisha,” alisema Dabo.
Naye kocha mkuu wa Mashujaa, Abdallah Mohamed ‘Baresi’ ambaye timu yake imepanda kwa nafasi moja ikiwa nafasi ya 14 kwa pointi 22, alisema kucheza kwa mitego na dhamira yao ya kutopoteza mechi hiyo, viliwasaidia kuondoka na pointi moja ugenini.

“Tuliingia uwanjani kwanza hatukutaka kupoteza mechi kwa kufahamu Azam ni timu nzuri ina matokeo mazuri, kwa hiyo tunaamini tukifanya makosa watatuadhibu kwa makosa yetu,” alisema Baresi.


Baresi apia alisema kwamba hata timu yake ilitengeneza nafasi muhimu na kukosa alama tatu zilizokuwa muhimu zaidi ila wanashukuru wamepata pointi moja kwa kuwa mechi hiyo ilikuwa na ufundi zaidi.

The post Dabo aikubali kazi ya Mashujaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/18/dabo-aikubali-kazi-ya-mashujaa/feed/ 0
Baresi akiri ugumu, ajipa matumaini https://www.greensports.co.tz/2024/04/17/baresi-akiri-ugumu-ajipa-matumaini/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/17/baresi-akiri-ugumu-ajipa-matumaini/#respond Wed, 17 Apr 2024 06:45:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10630 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Mashujaa, Abdallah Mohamed ‘Baresi’ amekiri kuwa hali waliyonayo kwenye Ligi Kuu NBC ni ngumu lakini watahakikisha wanaanza kukaa vyema kupitia mechi yao ya Jumatano hii dhidi ya Azam FC.Baresi amezungumza hayo Jumanne hii jijini Dar es Salaam akifafanua kuwa kikosi chake kipo kwenye morali nzuri ya mchezo tangu walipowasili Dar […]

The post Baresi akiri ugumu, ajipa matumaini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Mashujaa, Abdallah Mohamed ‘Baresi’ amekiri kuwa hali waliyonayo kwenye Ligi Kuu NBC ni ngumu lakini watahakikisha wanaanza kukaa vyema kupitia mechi yao ya Jumatano hii dhidi ya Azam FC.
Baresi amezungumza hayo Jumanne hii jijini Dar es Salaam akifafanua kuwa kikosi chake kipo kwenye morali nzuri ya mchezo tangu walipowasili Dar es Salaam.
Kocha huyo alikiri kuwa timu yake inafahamu kuhusu ubora wa Azam lakini watapambana kupata matokeo na kujiweka kwenye nafasi nzuri.
“Tumepoteza mechi mbili zilizopita na kabla ya hapo tulikuwa tunaenda vizuri na sasa hatuna hali nzuri kwenye ligi hivyo tunapambana na tuko sawa kuhakikisha tunapata matokeo mchezo wa kesho. Tunajua Azam ni timu nzuri wana kikosi kizuri hivyo hautakuwa mchezo rahisi lakini nasi tutacheza kwa ubora wetu tukihitaji matokeo.
Katika mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 2.30 usiku, Mashujaa itaingia dimbani ikiwa na pointi 21, nafasi ya 15 baada ya mechi 22.
Kwa upande wa Azam timu hiyo pia imecheza idadi ya mechi kama za Mashujaa lakini wao wanashikilia nafasi ya pili wakiwa wamekusanya pointi 50.

The post Baresi akiri ugumu, ajipa matumaini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/17/baresi-akiri-ugumu-ajipa-matumaini/feed/ 0
Baresi aupa tano uongozi Mashujaa https://www.greensports.co.tz/2024/03/04/baresi-aupa-tano-uongozi-mashujaa/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/04/baresi-aupa-tano-uongozi-mashujaa/#respond Mon, 04 Mar 2024 06:10:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10007 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa Mashujaa FC, Mohamed Abdallah ‘Baresi’ ameupongeza uongozi wa timu hiyo kwa maboresho waliyoyafanya kwenye dirisha dogo ambayo yamebadilisha mwenendo wa kikosi hicho.Kocha huyo alisema siri ya timu hiyo kufanya vizuri tangu kuanza kwa mzunguko wa pili ni ubora wa maingizo mapya kwenye usajili wa dirisha dogo.“Naupongeza uongozi kwa kunisikiliza na […]

The post Baresi aupa tano uongozi Mashujaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Mashujaa FC, Mohamed Abdallah ‘Baresi’ ameupongeza uongozi wa timu hiyo kwa maboresho waliyoyafanya kwenye dirisha dogo ambayo yamebadilisha mwenendo wa kikosi hicho.
Kocha huyo alisema siri ya timu hiyo kufanya vizuri tangu kuanza kwa mzunguko wa pili ni ubora wa maingizo mapya kwenye usajili wa dirisha dogo.
“Naupongeza uongozi kwa kunisikiliza na kutekeleza kile nilichowaomba, kwa namna tulivyo sasa tunaweza kupambana na timu yoyote na kupata matokeo mazuri bila shaka,” alisema Baresi.
Kocha huyo alisema kufanya vibaya kwa timu hiyo kwenye mzunguko wa kwanza kulitokana na kukosa wachezaji wenye uzoefu wa ligi hiyo lakini maingizo waliyofanya kwenye dirisha dogo yameziba madhaifu yaliyokuwepo.
Alisema baada ya kutoka nafasi ya 15 waliyokuwepo kwa muda mrefu mikakati yao kwa sasa ni kuendelea kupambana ili kupata matokeo mazuri yatakayowapandisha kwenye nafasi za katikati ya msimamo wa ligi.
Mashujaa juzi iliizamisha Namungo bao 1-0 na kupanda hadi nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikifikisha pointi 18 katika michezo 19 iliyocheza.

The post Baresi aupa tano uongozi Mashujaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/04/baresi-aupa-tano-uongozi-mashujaa/feed/ 0
Lusajo kutupia mabao ya kutosha Mashujaa https://www.greensports.co.tz/2024/02/28/lusajo-kutupia-mabao-ya-kutosha-mashujaa/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/28/lusajo-kutupia-mabao-ya-kutosha-mashujaa/#respond Wed, 28 Feb 2024 07:07:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9910 Na mwandishi wetuMshambuliaji wa Mashujaa, Reliant Lusajo ametamba kuifungia timu hiyo mabao ya kutosha kuliko alivyokuwa Namungo FC.Akizungumza na GreenSports, mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga alisema anaamini atalitimiza hilo kutokana na uwepo wa viungo wenye uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi.“Kazi yangu ni kufunga na ninaamini nitafunga mabao mengi sana sababu tuna viungo wenye uwezo […]

The post Lusajo kutupia mabao ya kutosha Mashujaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Mashujaa, Reliant Lusajo ametamba kuifungia timu hiyo mabao ya kutosha kuliko alivyokuwa Namungo FC.
Akizungumza na GreenSports, mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga alisema anaamini atalitimiza hilo kutokana na uwepo wa viungo wenye uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi.
“Kazi yangu ni kufunga na ninaamini nitafunga mabao mengi sana sababu tuna viungo wenye uwezo wa kutoa pasi za mwisho na kufunga lakini pia nafasi ambayo kocha ananipanga inanipa urahisi wa kufanya hivyo,” alisema Lusajo.
Mchezaji huyo alisema mbali na uwepo wa viungo wengi wa kutengeneza nafasi lakini ana ushirikiano mzuri na mshambuliaji mwenzake Adam Adam hivyo hilo ni moja ya jambo ambalo linampa nguvu ya kuendeleza kile alichokifanya akiwa Namungo.
Alisema lengo lao yeye na mwenzake ni kuipigania timu hiyo kuondoka nafasi mbaya iliyopo hivi sasa na kukaa nafasi za juu ili kuendelea kushiriki Ligi Kuu NBC msimu ujao.
Lusajo aliyejiunga na timu hiyo kwenye dirisha dogo msimu huu, tayari ameifungia Mashujaa yenye maskani yake Kigoma mabao mawili katika michezo minne iliyopita.

The post Lusajo kutupia mabao ya kutosha Mashujaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/28/lusajo-kutupia-mabao-ya-kutosha-mashujaa/feed/ 0
Baresi afurahia usajili Mashujaa https://www.greensports.co.tz/2024/01/11/baresi-afurahia-usajili-mashujaa/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/11/baresi-afurahia-usajili-mashujaa/#respond Thu, 11 Jan 2024 07:39:30 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9255 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Mashujaa, Abdallah Mohamed ‘Baresi’ amesema anafurahishwa na usajili unaoendelea kufanywa na uongozi wake katika dirisha hili la usajili.Mashujaa hadi sasa wamekamilisha usajili wa wachezaji wanne ambao ni Mapinduzi Balama, Emmanuel Mtumbuka, Nyenyezi Juma na Abrahman Mussa.Akizungumza jana, Baresi alisema maboresho yaliyofanyika kwenye kikosi chake yataleta mabadiliko chanya kutokana na aina […]

The post Baresi afurahia usajili Mashujaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Mashujaa, Abdallah Mohamed ‘Baresi’ amesema anafurahishwa na usajili unaoendelea kufanywa na uongozi wake katika dirisha hili la usajili.
Mashujaa hadi sasa wamekamilisha usajili wa wachezaji wanne ambao ni Mapinduzi Balama, Emmanuel Mtumbuka, Nyenyezi Juma na Abrahman Mussa.
Akizungumza jana, Baresi alisema maboresho yaliyofanyika kwenye kikosi chake yataleta mabadiliko chanya kutokana na aina ya wachezaji walioingia kikosini kwenye dirisha hili la usajili.
“Ukiangalia usajili tuliofanya katika kipindi hiki cha usajili kwa kuongeza wachezaji wazoefu ili watusaidie kutukwamua hapa tulipo ambapo tunapaswa kupambana ili kusogea juu ya msimamo.

“Tuko kwenye nafasi mbaya kwenye msimamo ambayo tunahitaji kufanya jitihada kubwa ili tujikwamue na kutimiza malengo ya kujiondoa chini katika nafasi za msimamo wa ligi,” alisema Baresi.


Alisema hawezi kusema wachezaji waliosajiliwa wanatosha ila anaendelea kuisubiri kamati ya usajili kuona kama watamwongezea wachezaji zaidi.

The post Baresi afurahia usajili Mashujaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/11/baresi-afurahia-usajili-mashujaa/feed/ 0
Mashujaa yasajili watatu wapya https://www.greensports.co.tz/2024/01/02/mashujaa-yasajili-watatu-wapya/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/02/mashujaa-yasajili-watatu-wapya/#respond Tue, 02 Jan 2024 19:47:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9121 Na mwandishi wetuTimu ya Mashujaa imeanza kuimarisha kikosi chao baada ya kukamilisha usajili wa wachezaji watatu katika dirisha hili la usajili tangu lilipofunguliwa Desemba, mwaka jana.Nyota ambao hadi sasa wamemwaga wino wa kuitumikia Mashujaa ni Nyenyezi Juma kutoka Inter Stars ya Ligi Kuu Burundi, Balama Mapinduzi mchezaji huru baada ya kuachana na Coastal Union na […]

The post Mashujaa yasajili watatu wapya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Mashujaa imeanza kuimarisha kikosi chao baada ya kukamilisha usajili wa wachezaji watatu katika dirisha hili la usajili tangu lilipofunguliwa Desemba, mwaka jana.
Nyota ambao hadi sasa wamemwaga wino wa kuitumikia Mashujaa ni Nyenyezi Juma kutoka Inter Stars ya Ligi Kuu Burundi, Balama Mapinduzi mchezaji huru baada ya kuachana na Coastal Union na Emmanuel Mtumbuka kutoka Stand United.
Akizungumza na GreenSports, kocha mkuu wa Mashujaa, Abdallah Mohamed ‘Baresi’ alisema kuwa lengo la kufanya sajili hizo ni kuimarisha kikosi chao ambacho kipo nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC.
“Tunataka kutumia dirisha hili la usajili kujiimarisha, hatuko kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hivyo tunapaswa kubadilika na wakati ndio huu ligi kuu ikiwa imesimama.

“Kuna baadhi ya wachezaji tunaenda kuachana nao kwenye kipindi hiki na kuleta nyota wapya ambao watakuja kuleta kitu kipya na kutuondoa mahali tulipo hivi sasa,” alisema Baresi.


The post Mashujaa yasajili watatu wapya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/02/mashujaa-yasajili-watatu-wapya/feed/ 0
Baresi, Mashujaa waamua kuyajenga https://www.greensports.co.tz/2023/12/17/baresi-mashujaa-waamua-kuyajenga/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/17/baresi-mashujaa-waamua-kuyajenga/#respond Sun, 17 Dec 2023 17:28:40 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8917 Na mwandishi wetuTaarifa mpya ni kuwa uongozi wa timu ya Mashujaa na kocha wa timu hiyo, Abdallah Mohamed ‘Baresi’ wamekaa mezani kuyamaliza na sasa kocha huyo ataendelea kukinoa kikosi hicho.Pande hizo mbili zimelazimika kukutana hivi karibuni baada ya wiki iliyopita, Baresi kuandika barua ya kuachia ngazi kutokana na matokeo mabovu mfululizo ya timu hiyo iliyopanda […]

The post Baresi, Mashujaa waamua kuyajenga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Taarifa mpya ni kuwa uongozi wa timu ya Mashujaa na kocha wa timu hiyo, Abdallah Mohamed ‘Baresi’ wamekaa mezani kuyamaliza na sasa kocha huyo ataendelea kukinoa kikosi hicho.
Pande hizo mbili zimelazimika kukutana hivi karibuni baada ya wiki iliyopita, Baresi kuandika barua ya kuachia ngazi kutokana na matokeo mabovu mfululizo ya timu hiyo iliyopanda kushiriki Ligi Kuu NBC msimu huu.
Akizungumza na GreenSports, Baresi alieleza kuwa kwa sasa hakuna tena mipango ya kuihama Mashujaa yenye maskani yake Kigoma baada ya kukutana na kuzungumza na uongozi.

“Kama ulivyosikia, niliwapa barua viongozi ya kujiuzulu lakini baadae nilikutana na uongozi, tukazungumza na kukubaliana baadhi ya vitu na ieleweke tu kwamba tumeyamaliza na tunaendelea kuipigania Mashujaa,” alisema Baresi.


Alisema kwa sasa wako kwenye maandalizi kabambe ya kuhakikisha wanapata matokeo kwenye mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro.
Mashujaa itaingia uwanjani ikitafuta ushindi iliyoukosa katika mechi nane mfululizo zilizopita, wakipoteza mechi sita na kuambulia sare mbili na sasa wanashika nafasi ya 15 kwa pointi tisa huku Mtibwa ikiburuza mkia katika nafasi ya 16 ikiwa na pointi tano pekee.

The post Baresi, Mashujaa waamua kuyajenga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/17/baresi-mashujaa-waamua-kuyajenga/feed/ 0
Baresi aziandalia dozi Simba, Yanga https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/baresi-aziandalia-dozi-simba-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/baresi-aziandalia-dozi-simba-yanga/#respond Wed, 30 Aug 2023 07:56:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7574 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Mashujaa, Abdallah Mohamed ‘Baresi’ amesema ameandaa dozi nzito kwa kila timu itakayokanyaga Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma wakiwemo vigogo Simba na Yanga.Mashujaa ambayo inashiriki Ligi Kuu NBC kwa mara ya kwanza msimu huu kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo ikikusanya pointi nne katika mechi mbili […]

The post Baresi aziandalia dozi Simba, Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Mashujaa, Abdallah Mohamed ‘Baresi’ amesema ameandaa dozi nzito kwa kila timu itakayokanyaga Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma wakiwemo vigogo Simba na Yanga.
Mashujaa ambayo inashiriki Ligi Kuu NBC kwa mara ya kwanza msimu huu kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo ikikusanya pointi nne katika mechi mbili ilizocheza kwenye uwanja huo.
Kocha huyo alieleza kuwa lengo lao kuu msimu huu wa kwanza ni kuhakikisha hawapotezi mchezo wa nyumbani lakini pia wanamaliza msimu wakiwa nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi.

“Suala la kufukuzia ubingwa niseme kweli siwezi kuliwazia sababu huu ndio msimu wa kwanza kushiriki ligi kuu, bado tunahitaji uzoefu kwa misimu miwili hivi baada ya hapo tutaanza kufikiria ubingwa lakini katika kipindi chote hicho mkakati wetu ni kuugeuza uwanja wa nyumbani kuwa shubiri kwa mgeni bila kujali ni timu gani tunacheza nayo,” alisema Baresi.


Kocha huyo alisema yeye na wasaidizi wake wamejipanga kuhakikisha wanajenga kikosi imara kitakachotoa upinzani na kupata matokeo mazuri, siyo tu kwenye uwanja wa nyumbani bali hata mechi watakazocheza ugenini.
Baresi pia alisema anafurahishwa na hamasa kubwa kutoka kwa mashabiki wa mkoa huo ambao wamekuwa wakitoa sapoti kubwa kwa timu hiyo pindi inapocheza nyumbani na amewaomba waendelee kuwa hivyo hata watakapocheza na timu za Simba na Yanga.
Mashujaa ilianza vyema ligi msimu wa 2023-24 kwa kuifunga timu kongwe ya Kagera Sugar mabao 2-0 kisha ikatoka sare ya bao 1-1 na Geita Gold, mechi zote zikichezwa Uwanja wa Lake Tanganyika.

The post Baresi aziandalia dozi Simba, Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/baresi-aziandalia-dozi-simba-yanga/feed/ 0
Mashujaa yabaki na 16 wa zamani https://www.greensports.co.tz/2023/07/27/mashujaa-yabaki-na-16-wa-zamani/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/27/mashujaa-yabaki-na-16-wa-zamani/#respond Thu, 27 Jul 2023 12:43:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7154 Na mwandishi wetuTimu ya Mashujaa ya Kigoma imefunguka kuwa imepunguza wachezaji wake wa awali na kubakiza wachezaji 16 pekee watakaoungana na wengine wapya kuipigania timu hiyo msimu ujao wa 2023-24.Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Mashujaa, Edward Swai aliyefunguka kuwa hiyo ni mipango yao thabiti kuelekea Ligi Kuu Bara baada ya kupanda daraja mwishoni mwa msimu […]

The post Mashujaa yabaki na 16 wa zamani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Mashujaa ya Kigoma imefunguka kuwa imepunguza wachezaji wake wa awali na kubakiza wachezaji 16 pekee watakaoungana na wengine wapya kuipigania timu hiyo msimu ujao wa 2023-24.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Mashujaa, Edward Swai aliyefunguka kuwa hiyo ni mipango yao thabiti kuelekea Ligi Kuu Bara baada ya kupanda daraja mwishoni mwa msimu wa 2022-23.
“Tupo kwenye mipango ya kuhakikisha tunakuwa bora zaidi, tunaendelea kusuka kikosi chetu kikamilifu na tumewabakiza wachezaji takribani 16 katika wale tuliokuwa nao msimu uliopita, tumeongeza wengine kina Adam Adam, Zuberi Dabi na maingizo mengine ambayo tutayaweka wazi hivi karibuni,” alisema Swai.
Alisema kuwa kikosi chao kwa sasa kipo Zanzibar kikiendelea kujifua huku kocha wao mkuu, Mohamed Abdaalah ‘Baresi’ akihitaji maandalizi yafanyike huko kutokana na ugeni wa timu akiamini hapo ni sehemu pekee ya kuunda vyema kikosi cha mapigano ya ligi kuu msimu ujao.
“Kikosi kipo Zanzibar kutokana na malengo mbalimbali, ikiwemo kocha kuhitaji sehemu tulivu ili kusuka kikosi cha wachezaji wa zamani na wapya wanaoendelea kusajiliwa akiamini timu inahitaji utulivu na sehemu sahihi kama Zanzibar,” alisema Swai.

The post Mashujaa yabaki na 16 wa zamani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/27/mashujaa-yabaki-na-16-wa-zamani/feed/ 0
Bares awatoa hofu mashabiki Mashujaa https://www.greensports.co.tz/2023/07/13/bares-awatoa-hofu-mashabiki-mashujaa/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/13/bares-awatoa-hofu-mashabiki-mashujaa/#respond Thu, 13 Jul 2023 19:19:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6942 Na mwandishi wetuKocha Mkuu mpya wa Mashujaa, Mohamed Abadallah ‘Bares’ amewataka mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na wasiwasi kwani anaisuka timu ya ushindani kwelikweli kuelekea msimu ujao.Bares aliyechukua mikoba ya kocha Abdul Mingange amefafanua kuwa licha ya ugeni wa timu hiyo iliyopanda kushiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao lakini anaamini atawaandaa vilivyo wachezaji wake kuhakikisha […]

The post Bares awatoa hofu mashabiki Mashujaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu mpya wa Mashujaa, Mohamed Abadallah ‘Bares’ amewataka mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na wasiwasi kwani anaisuka timu ya ushindani kwelikweli kuelekea msimu ujao.
Bares aliyechukua mikoba ya kocha Abdul Mingange amefafanua kuwa licha ya ugeni wa timu hiyo iliyopanda kushiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao lakini anaamini atawaandaa vilivyo wachezaji wake kuhakikisha wanapambania mno matokeo ya timu hiyo.
“Tupo kwenye maandalizi kiujumla, hatujaanza mazoezi lakini tunaendelea na michakato mingine ya usajili na vitu vingine muhimu kuhakikisha timu inakuwa nzuri na ngumu kwa ajili ya mashindano ya msimu ujao.
“Wachezaji wengi wanafanana isipokuwa ni namna gani unawaandaa, hivyo tutawaandaa kiushindani na kuipa timu matokeo, tufanye vizuri na mashabiki pia wafurahi na waje kuangalia timu yao,” alisema Bares.
Mashujaa yenye maskani yake mkoani Kigoma, imepanda ligi kuu baada ya kuizamisha Mbeya City kwa jumla ya mabao 4-1 katika mechi mbili za mtoano za kuwania kushiriki ligi hiyo msimu ujao wa 2023-24.

The post Bares awatoa hofu mashabiki Mashujaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/13/bares-awatoa-hofu-mashabiki-mashujaa/feed/ 0