Iran-US - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 11 May 2026 19:41:42 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Iran-US - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mwenyeji wetu Kombe la Dunia ni Fifa si Trump-Iran https://www.greensports.co.tz/2026/05/11/mwenyeji-wetu-kombe-la-dunia-ni-fifa-si-trump-iran/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/11/mwenyeji-wetu-kombe-la-dunia-ni-fifa-si-trump-iran/#respond Mon, 11 May 2026 09:23:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14633 Tehran, IranRais wa Shirikisho la Soka Iran (FFIRI), Mehdi Taj (pichani) amesema kwamba mwenyeji wao kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 ni Fifa si Marekani wala rais wa nchi hiyo, Donald Trump.Iran imetaka heshima timu yake ikiwa nchini Marekani kwenye fainali za Kombe la Dunia ambazo zitaanza kutimua vumbi kuanzia Juni 11 mwaka huu […]

The post Mwenyeji wetu Kombe la Dunia ni Fifa si Trump-Iran first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Tehran, Iran
Rais wa Shirikisho la Soka Iran (FFIRI), Mehdi Taj (pichani) amesema kwamba mwenyeji wao kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 ni Fifa si Marekani wala rais wa nchi hiyo, Donald Trump.
Iran imetaka heshima timu yake ikiwa nchini Marekani kwenye fainali za Kombe la Dunia ambazo zitaanza kutimua vumbi kuanzia Juni 11 mwaka huu katika nchi za Marekani, Canada na Mexico.
Mehdi hivi karibuni alikuwa mmoja wa wajumbe wa Iran kwenye mkutano wa Fifa mjini Vancouver, Canada lakini walikwama kushiriki mkutano huo kwa kilichodaiwa kuwa ni kukosewa heshima na maofisa uhamiaji wa Canada.
Katika tukio hilo Mehdi na ujumbe wake waliamua kurudi Iran uamuzi ambao Mehdi ameutetea ingawa wizara ya mambo ya ndani ya Canada ilieleza kuwa visa ya kiongozi huyo wa Iran ilifutwa kwa sababu ya kuhusishwa kwake na kundi la Islamic Revolutionary Guard Corps (IRGC).
IRGC ni kundi maalum lililoanzishwa Iran kwa lengo la kulinda maslahi ya taifa hilo kisiasa, kiuchumi na katika nyanja mbalimbali na hadi sasa linafahamika kuwa kundi lenye nguvu za kijeshi.
Katika nchi za Marekani na Canada, IRGC ni kundi linalohusishwa na ugaidi na inadaiwa katika nchi hizo mtu yeyote mwenye ukaribu na IRGC haruhusiwi kuingia nchi hizo.
Mehdi kwa upande wake alisema wanachotaka ni kuhakikishiwa kwamba hawatakosewa heshima kwa namna yoyote ile ikiwamo kulidhalilisha kundi la IRGC ambalo alilitaja kuwa ni alama muhimu katika mfumo wa taifa la Iran.
Kiongozi huyo pia alisisitiza kuwa Iran imefuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia na inakwenda kushiriki na mwenyeji wao ni Fifa.

“Tunakwenda kushiriki fainali za Kombe la Dunia kwa sababu tumefuzu na mwenyeji wetu huko ni Fifa si Trump au Marekani,” alisema Mehdi.


Katika siku za karibuni kumekuwapo mjadala kuhusu hatma ya Iran na ushiriki wao kwenye fainali za Kombe la Dunia licha ya Rais wa Fifa, Gianni Infantino kusisitiza kuwa Iran itashiriki fainali hizo.
Iran imepangwa kucheza mechi zake mbili za awali mjini Los Angeles dhidi ya New Zealand na Ubelgiji, mechi ambazo zitachezwa Juni 15 na 21 na mechi yao ya mwisho ya makundi itakuwa Juni 26 dhidi ya Misri mjini Seattle.
Hali ya utata kuhusu hatma ya Iran kushiriki fainali hizo imejitokeza tangu kuibuka kwa vita ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

The post Mwenyeji wetu Kombe la Dunia ni Fifa si Trump-Iran first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/11/mwenyeji-wetu-kombe-la-dunia-ni-fifa-si-trump-iran/feed/ 0
Fifa, Iran kukaa mezani https://www.greensports.co.tz/2026/05/02/fifa-iran-kukaa-mezani/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/02/fifa-iran-kukaa-mezani/#respond Sat, 02 May 2026 20:19:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14590 Geneva, SwitzerlandMaofisa wa soka wa Iran watafanya kikao na wenzao wa Fifa katika siku za karibuni kwa lengo la kuweka sawa mipango ya mechi za Iran kwenye fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza mwezi ujao nchini Marekani.Bosi wa Shirikisho la Soka Iran, Mehdi Taj amesema wana mambo ya kujadili baada ya kurudi nyumbani akiwa ameshindwa […]

The post Fifa, Iran kukaa mezani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Geneva, Switzerland
Maofisa wa soka wa Iran watafanya kikao na wenzao wa Fifa katika siku za karibuni kwa lengo la kuweka sawa mipango ya mechi za Iran kwenye fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza mwezi ujao nchini Marekani.
Bosi wa Shirikisho la Soka Iran, Mehdi Taj amesema wana mambo ya kujadili baada ya kurudi nyumbani akiwa ameshindwa kushiriki mkutano mkuu wa mwaka wa Fifa uliofanyika Alhamisi Aprili 30, 2026 mjini Vancouver, Canada.
Katibu Mkuu wa Fifa, Mattias Grafström amewaalika maofisa wa soka nchini Iran kukutana nao katika makao makuu ya Fifa mjini Zurich, kikao ambacho kinatarajia kufanyika Mei 20, 2026 au kabla ya hapo.
Lengo ni kuhakikisha kikao hicho kinafanyika wiki tatu kabla timu ya Iran haijawasili Marekani kuweka kambi ya mazoezi mjini Arizona na kujiandaa na mechi tatu za makundi zitakazochezwa Seattle, California na Inglewood.

“Msimamo wetu ni kwamba hivi karibuni tutakuwa na kikao na watu wa Fifa,” alisema Taj katika mazungumzo yake na chanzo kimoja cha habari nchini Iran.


Awali Rais wa Fifa, Gianni Infantino katika hotuba yake ya ufunguzi mbele ya viongozi wa soka duniani isipokuwa wa Iran, alisisitiza Iran itacheza mechi za Kombe la Dunia nchini Marekani kama ilivyopangwa.
Kauli hiyo ilifuatiwa na kauli ya Rais wa Marekani, Donald Trump ambaye alithibitisha kuiunga mkono timu ya Iran na kuongeza kuwa kama Infantino hana tatizo na yeye Trump hana tatizo ingawa awali Trump alisema anaikaribisha Iran lakini hawezi kuihakikishia usalama.
Katika hoja ya awali, Iran walitaka mechi zao zisichezwe nchini Marekani, hoja ambayo hata hivyo haikuungwa mkono na Rais wa Fifa ambaye amekuwa na ukaribu na Rais Trump katika miezi ya karibuni na amewahi kumpa tuzo kiongozi huyo wa Marekani jambo lililoibua mjadala..
Tangu kuanza kwa vita kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran kumekuwa na mgogoro mkubwa kuhusu hatma ya timu ya taifa ya Iran kushiriki fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwezi ujao katika nchi za Marekani, Canada na Mexico.

The post Fifa, Iran kukaa mezani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/02/fifa-iran-kukaa-mezani/feed/ 0
‘Iran itashiriki Kombe la Dunia’ https://www.greensports.co.tz/2026/05/01/iran-itashiriki-kombe-la-dunia/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/01/iran-itashiriki-kombe-la-dunia/#respond Fri, 01 May 2026 19:07:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14569 Vancouver, CanadaRais wa Fifa, Gianni Infantino amesisitiza kwa mara ya pili kuwa Iran itashiriki fainali za Kombe la Dunia na kucheza mechi zake nchini Marekani kama ilivyopangwa kwa mujibu wa ratiba ya awali.Kauli ya rais wa Fifa imekuja kwa mara ya pili baada ya kuwapo habari kuwa ujumbe wa Iran ulizuiwa kuingia katika mkutano mkuu […]

The post ‘Iran itashiriki Kombe la Dunia’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Vancouver, Canada
Rais wa Fifa, Gianni Infantino amesisitiza kwa mara ya pili kuwa Iran itashiriki fainali za Kombe la Dunia na kucheza mechi zake nchini Marekani kama ilivyopangwa kwa mujibu wa ratiba ya awali.
Kauli ya rais wa Fifa imekuja kwa mara ya pili baada ya kuwapo habari kuwa ujumbe wa Iran ulizuiwa kuingia katika mkutano mkuu wa Fifa nchini Canada ingawa taaifa ya wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo ilidai kuwa kuzuiwa huko halikuwa jambo lililokusudiwa.
Habari za Alhamisi Aprili 30, 2026, zilidai kuwa wajumbe wawili wa Iran waliruhusiwa kuingia Canada lakini wakagoma kuingia katika mkutano baada ya mwenzao mmoja kukwama sababu ikiwa ni tatizo lililohusisha idara ya uhamiaji nchini humo.
Ilidaiwa kuwa maofisa wa Fifa walitaka Iran wawepo kwenye mkutano huo licha ya tatizo la mwenzao na idara ya uhamiaji lakini wakati wa ukaguzi wa washiriki, ilibainika kuwa ujumbe wa Iran haukuwapo kwenye ukumbi wa mkutano.
Kwa upande wake Infantino licha ya utata huo alisisitiza kwamba Iran itashiriki fainali za Kombe la Dunia kwa sababu ni jukumu lake kuwaleta watu pamoja na kuleta umoja.

“Ukweli ni kwamba Iran watashiriki fainali za Fifa za Kombe la Dunia 2026, watacheza mechi zao Marekani, sababu ya hilo ni rahisi tu marafiki zangu, ni kwa sababu lazima tuwe wamoja,” alisema Infantino.


Baadaye Rais wa Marekani, Donald Trump aliwaambia waandishi wa habari kwamba kama Infantino hana tatizo na Iran kushiriki fainali za Kombe la Dunia na yeye Trump hana tatizo katika hilo.
Kauli hiyo ya Trump ni tofauti na kauli yake ya awali aliposema kwamba anaikaribisha timu ya Iran nchini Marekani kushiriki fainali za Kombe la Dunia lakini hawezi kuwahakikishia usalama.
Tangu kuibuka kwa vita kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, imekuwapo hofu ya Iran kushiriki fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza mapema mwezi ujao katika nchi za Marekani, Canada na Mexico hadi taifa hilo kutoa sharti la kutaka mechi zao zihamishiwe nchi nyingine.

The post ‘Iran itashiriki Kombe la Dunia’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/01/iran-itashiriki-kombe-la-dunia/feed/ 0
Rais Fifa: Iran itashiriki Kombe la Dunia https://www.greensports.co.tz/2026/04/01/rais-fifa-iran-itashiriki-kombe-la-dunia/ https://www.greensports.co.tz/2026/04/01/rais-fifa-iran-itashiriki-kombe-la-dunia/#respond Wed, 01 Apr 2026 18:06:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14511 Davos, UswisiRais wa Fifa, Gianni Infantino (pichani) amesema kwamba nchi ya Iran itacheza mechi zake za fainali za Kombe la Dunia nchini Marekani kama ilivyopangwa.Kumekuwa na hofu juu ya ushiriki wa Iran kwenye faianli za Kombe la Dunia zitakazoanza kutimua vumbi Juni 11, 2026 katika nchi za Marekani, Canada na Mexico kutokana na vita inayoendelea […]

The post Rais Fifa: Iran itashiriki Kombe la Dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
TOPSHOT – FIFA president Gianni Infantino poses with Al Rihla, the official match ball before a press conference during the 72th FIFA Congress in the Qatari capital Doha, on March 31, 2022. – The countdown towards the most controversial World Cup in history really begins tomorrow as the draw for Qatar 2022 takes place in Doha 2022, less than eight months befor the start of the tournament itself. (Photo by FRANCK FIFE / AFP)

Davos, Uswisi
Rais wa Fifa, Gianni Infantino (pichani) amesema kwamba nchi ya Iran itacheza mechi zake za fainali za Kombe la Dunia nchini Marekani kama ilivyopangwa.
Kumekuwa na hofu juu ya ushiriki wa Iran kwenye faianli za Kombe la Dunia zitakazoanza kutimua vumbi Juni 11, 2026 katika nchi za Marekani, Canada na Mexico kutokana na vita inayoendelea kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
Shirikisho la Soka Iran hivi karibuni lilitoa taarifa likidai kwamba linafanya mazungumzo na Fifa ili mechi zao zisichezewe nchini Marekani badala yake zihamishiwe Mexico.
Taarifa ya shirikisho hilo inahusishwa na kauli iliyowahi kutolewa na Rais wa Marekani, Donald Trump ambaye alisema kwamba anaikaribisha Iran nchini Marekani lakini hawezi kuihakikishia usalama.
Kwa upande mwingine kauli ya Infantino kuthibitisha ushiriki wa Iran inatafsiriwa kuwa huenda imetokana na mazungumzo na Shirkisho la Soka Iran na hivyo ushiriki wa Iran kwenye fainali hizo utakuwa kama ilivyopangwa na Fifa.

“Iran itakuwapo kwenye Kombe la Dunia, tuna furaha kwa sababu wana timu imara sana, nina furaha kwa hilo, mechi zitachezwa pale zinapotakiwa kuchezwa kwa mujibu wa ratiba,” alisema Infantino.


Iran itaanza mechi zake kwa kuivaa New Zealand na baadaye Ubelgiji, mechi zitakazochezwa mjini Los Angeles Juni 15 na Juni 21 na Juni 26 itacheza na Misri mjini Seattle.
Naye Rais wa Mexico, Claudia Sheinbaum alisema kwamba nchi yake inajiandaa kuikaribisha Iran kucheza mechi zake za Kombe la Dunia katika taifa hilo.
Kauli ya Rais wa Mexico inapingana na ile ya Infantino ambaye alishuhudia Iran ikiichapa Costa Rica mabao 5-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa nchini Uturuki.
Baada ya mechi hiyo Infantino alisisitiza kwamba Iran itashiriki fainali za Kombe la Dunia kama ilivyopangwa na ameiona timu, amezungumza na wachezaji na kila kitu kipo sawa.

The post Rais Fifa: Iran itashiriki Kombe la Dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/04/01/rais-fifa-iran-itashiriki-kombe-la-dunia/feed/ 0
Wachezaji Iran wabeba mabegi ya shule kuipinga Marekani https://www.greensports.co.tz/2026/03/28/wachezaji-iran-wabeba-mabegi-ya-shule/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/28/wachezaji-iran-wabeba-mabegi-ya-shule/#respond Sat, 28 Mar 2026 15:22:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14493 Belek, UturukiTimu ya soka ya taifa ya Iran imeingia uwanjani na vitambaa vya rangi nyeusi na mabegi ya watoto wa shule kabla ya mechi yao na Nigeria ikiwa ni ishara ya kupinga mashambulizi yaliyosababisha maafa katika moja ya shule nchini humo.Kwa mujibu wa taarifa za nchini Iran, vita inayoendelea kati ya Marekani na Israel dhidi […]

The post Wachezaji Iran wabeba mabegi ya shule kuipinga Marekani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Belek, Uturuki
Timu ya soka ya taifa ya Iran imeingia uwanjani na vitambaa vya rangi nyeusi na mabegi ya watoto wa shule kabla ya mechi yao na Nigeria ikiwa ni ishara ya kupinga mashambulizi yaliyosababisha maafa katika moja ya shule nchini humo.
Kwa mujibu wa taarifa za nchini Iran, vita inayoendelea kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran katika siku yake ya kwanza ilisababisha vifo vya watu wapatao 168 wakiwamo watoto 110 waliokuwa shule.
Mashambulizi hayo ya anga yalifanywa katika Shule ya Shajareh Tayyebeh Kusini mwa Iran ingawa taarifa za nchini Marekani zinadai kuwa mashambulizi hayo yalifanywa kimakosa na jeshi la nchi hiyo.
Katika kupinga mashambulizi hayo, kabla ya kuanza kwa mechi ya kirafiki na Nigeria mjini Balek, Uturuki, wachezaji wa Iran walionekana wakiwa na mabegi ya watoto wakiongozwa na mshambuliaji nyota wa zamani wa klabu za FC Porto na Inter Milan, Mehdi Taremi.
Taarifa ya chanzo kimoja nchini Iran ilieleza kuwa wachezaji hao wamebeba mageni ya rangi ya pinki na zambarau ili kuwakumbuka watoto wa shule waliouliwa katika shambulizi lililofanywa na Jeshi la Marekani.
Maofisa wa Iran walizilaumu Marekani na Israel kwa shambulizi walilofanya kwenye shule hiyo ambayo ipo karibu na kituo kimoja cha jeshi ingawa nchi hizo mbili hazijakiri kuhusika na shambulizi hilo.
Iran ni kati ya nchi ambazo zimefuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico ingawa ushiriki wa Iran upo njia panda kwa kuwa haitaki mechi zao zichezwe Marekani licha ya ratiba kupangwa hivyo.
Fainali za Kombe la Dunia zimepangwa kuanza Juni 11, 2026 na Iran imechukua msimamo wa kukataa kupeleka timu Marekani hasa baada ya rais wa nchi hiyo, Donald Trump kusema kuwa anawakaribisha Iran lakini hawezi kuwahakikishia usalama wao.
Wakati huo huo, Iran imepiga marufuku timu zao za michezo kwenda katika nchi ambazo zina ugomvi nao, kauli ambayo imekuja wakati timu ya soka ya Traktor Sazi ya nchini Iran ikijiandaa kwenda Saudi Arabia.
Traktor ikiwa Saudi Arabia inatarajia kucheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Asia dhidi ya Shabab Al Ahli ya Dubai, mechi iliyopangwa kuchezwa Alhamisi ijayo.
Taarifa ya katazo hilo imetolewa na Wizara ya Michezo ya Iran na huenda ikaathiri moja kwa moja ushiriki wa Iran kwenye Kombe la Dunia kama Fifa hawatohamisha mechi za taifa hilo na kuzipeleka katika nchi nyingine mwenyeji kati ya Mexico au Canada.

The post Wachezaji Iran wabeba mabegi ya shule kuipinga Marekani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/28/wachezaji-iran-wabeba-mabegi-ya-shule/feed/ 0
Iran: Tunaipinga Marekani si Kombe la Dunia https://www.greensports.co.tz/2026/03/20/iran-tunaipinga-marekani-si-kombe-la-dunia/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/20/iran-tunaipinga-marekani-si-kombe-la-dunia/#respond Fri, 20 Mar 2026 14:21:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14470 Tehran, IranShirikisho la Soka Iran limesisitiza kuwa nchi yao inaipinga Marekani na si fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini humo kuanzia Juni 11, 2026.Kwa mujibu wa chanzo cha habari nchini Iran, Far News Agency, chanzo hicho kimemnukuu kiongozi mkuu wa Shirikisho la Soka Iran, Mehdi Taj akitoa msimamo huo Jumatano Machi 18, 2026.Katika siku […]

The post Iran: Tunaipinga Marekani si Kombe la Dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Tehran, Iran
Shirikisho la Soka Iran limesisitiza kuwa nchi yao inaipinga Marekani na si fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini humo kuanzia Juni 11, 2026.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari nchini Iran, Far News Agency, chanzo hicho kimemnukuu kiongozi mkuu wa Shirikisho la Soka Iran, Mehdi Taj akitoa msimamo huo Jumatano Machi 18, 2026.
Katika siku za hivi karibuni msimamo wa Iran kushiriki fainali hizo ambazo Marekani itakuwa mwenyeji na nchi za Mexico na Canada, umekuwa njia panda tangu Marekani na Israel zifanye mashambulizi ya anga nchini Irani mwishoni mwa mwezi uliopita.
Timu ya taifa ya Iran katika fainali hizo inatarajia kucheza mechi zake tatu za awali nchini Marekani na kwa mujibu wa Taj, watajiandaa kwa mechi hizo lakini wataipinga Marekani na si fainali za Kombe la Dunia.
Taj pia alitumia mtandao wa Twitter au X kufafanua kuwa katika mkakati huo wa kuipinga Marekani, kwa sasa wapo katika mazungumzo na Fifa kwa lengo la kuhakikisha mechi zao zinahamishiwa nchini Mexico.

“Rais Donald Trump aliposema wazi kwamba hawezi kuihakikishia usalama timu ya taifa ya Iran, maana yake ni kwamba hatuwezi kwenda Marekani, tunawasiliana na Fifa ili mechi zetu zihamishiwe Mexico,” alisema Taj.


Kwa upande mwingine Rais wa Fifa, Gianni Infantino alinukuliwa akisema kwamba anatarajia timu zote zilizofuzu fainali za Kombe la Dunia kushiriki katika misingi ya haki na kuheshimiana na matumaini ya Fifa ni kuona fainali hizo zinafanyika kama zilivyopangwa.
Ikitokea mechi za Iran kuhamishiwa Mexico bado timu hizo zinaweza kukutana katika raundi ya pili ya michuano hiyo nchini Marekani kwa kuzingatia nafasi zitakazoshika katika makundi yao.

The post Iran: Tunaipinga Marekani si Kombe la Dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/20/iran-tunaipinga-marekani-si-kombe-la-dunia/feed/ 0
Iran ikikataa Kombe la Dunia, Trump awaita, atoa tahadhari https://www.greensports.co.tz/2026/03/15/iran-ikikataa-kombe-la-dunia-trump-awaita-atoa-tahadhari/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/15/iran-ikikataa-kombe-la-dunia-trump-awaita-atoa-tahadhari/#respond Sun, 15 Mar 2026 14:02:18 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14431 New York, MarekaniRais wa Marekani, Donald Trump amesema itakuwa sahihi kwa Iran kutoshiriki fainali za Kombe la Dunia 2026 kwa usalama wao na maisha yao wakati Iran wamedai kuwa sababu ya wao kutoshiriki fainali hizo ni Marekani.Katika andiko lake kupitia mitandao ya kijamii, Rais Trump alisema anaikaribisha Iran kwenye fainali hizo lakini hapo hapo akasema […]

The post Iran ikikataa Kombe la Dunia, Trump awaita, atoa tahadhari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Rais wa Marekani, Donald Trump amesema itakuwa sahihi kwa Iran kutoshiriki fainali za Kombe la Dunia 2026 kwa usalama wao na maisha yao wakati Iran wamedai kuwa sababu ya wao kutoshiriki fainali hizo ni Marekani.
Katika andiko lake kupitia mitandao ya kijamii, Rais Trump alisema anaikaribisha Iran kwenye fainali hizo lakini hapo hapo akasema kwamba anadhani hawapaswi kushiriki.
Kauli ya Trump imekuja baada ya Waziri wa Michezo na Vijana wa Iran, Ahmad Donyamali kusema kwamba nchi yake haiko katika nafasi ya kushiriki fainali hizo ambazo zitafanyika katika nchi za Marekani, Mexico na Canada kuanzia Juni 11 mwaka huu.
Katika fainali hizo Iran imepangwa kuanza mechi zake Juni 15 dhidi ya New Zealand na Juni 21 dhidi ya Ubelgiji zitakazopigwa mjini Los Angeles na kumalizia na mechi dhidi ya Misri itakayopigwa Juni 26 mjini Seattle.
Ushiriki wa timu ya Iran hata hivyo bado upo njia panda tangu Marekani na Israel waanze mashambulizi ya anga dhidi ya taifa hilo na kumuua kiongozi wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.
Iran nayo ikajibu mapigo kwa kufanya mashambulizi kama hayo Israel na mengine katika nchi za Bahrain, Qatar, Kuwait na Umoja wa Falme za Kiarabu, nchi ambazo zina kambi za kijeshi za Marekani.

“Timu ya taifa ya soka ya Iran inakaribishwa kwenye Kombe la Dunia lakini kwa hakika siamini kama ni sahihi wao kuwa hapa, ni kwa usalama wao na maisha yao,” alisema Trump katika andiko lake.


Ujumbe wa Iran hata hivyo umekuwa tofauti kuhusu hoja hiyo ya Trump baada ya kudai kuwa waandaaji wa fainali za Kombe la Dunia ni Fifa (Shirikisho la Soka la Kimataifa) na si nchi yoyote.

“Timu ya taifa ya Iran pia imefuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia na hiyo ni baada ya kupata ushindi na kuwa moja ya timu za kwanza kufikia katika hatua hii muhimu,” ilieleza taarifa ya kutoka Iran.


Taarifa hiyo pia ilifafanua kwamba nchi ambayo inaweza kutolewa kwenye fainali za Kombe la Dunia ni ile ambayo imebeba hadhi ya kuwa nchi mwenyeji lakini haina uwezo wa kuzihakikishia usalama timu zinazoshiriki fainali hizo.
Awali Rais wa Fifa, Gianni Infantino alisema kwamba Rais Trump alimwambia kuwa Iran inakaribishwa kushiriki kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Wakati Infantino akitoa kauli hiyo, Waziri wa Michezo wa Iran alinukuliwa akisema kwa sababu serikali dhalimu imemuua kiongozi wao haoni kama wapo katika nafasi nzuri ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia.
Ikitokea Iran ikajitoa katika fainali hizo, kanuni za Fifa zinalipa shirikisho hilo nafasi ya kuchagua timu ya kushiriki badala ya Iran ingawa hadi sasa haijaweza kufahamika timu inayoweza kupewa nafasi hiyo.

The post Iran ikikataa Kombe la Dunia, Trump awaita, atoa tahadhari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/15/iran-ikikataa-kombe-la-dunia-trump-awaita-atoa-tahadhari/feed/ 0