Declan Rice - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 03 Jun 2026 18:00:30 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Declan Rice - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Declan Rice ajivunia Arsenal https://www.greensports.co.tz/2026/06/03/declan-rice-ajivunia-arsenal/ https://www.greensports.co.tz/2026/06/03/declan-rice-ajivunia-arsenal/#respond Wed, 03 Jun 2026 18:00:26 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14673 Budapest, HungaryKiungo wa Arsenal, Declan Rice amesema ameumizwa baada ya kushindwa kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini anajivunia yeye na wachezaji wenzake kwa kufikia hatua ya fainali.Arsenal ilishindwa kutamba katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya PSG kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya sare ya bao 1-1 katika […]

The post Declan Rice ajivunia Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Budapest, Hungary
Kiungo wa Arsenal, Declan Rice amesema ameumizwa baada ya kushindwa kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini anajivunia yeye na wachezaji wenzake kwa kufikia hatua ya fainali.
Arsenal ilishindwa kutamba katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya PSG kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida na 30 za nyongeza mechi iliyochezwa Jumamosi Mei 30, 2026.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu England walikuwa na matumaini makubwa ya kubeba taji hilo ikiwa ni mara yao ya kwanza kufikia hatua ya fainali ya michuano hiyo mikubwa ya klabu tangu wafanye hivyo mara ya mwisho mwaka 2006.
Rice alisema inaumiza na kukatisha tamaa unapolikosa taji la Ligi ya Mabigngwa Ulaya katika hatua ya fainali kwa mikwaju ya penalti.

“Tunajaribu kuchukua mitazamo mingi kwa kuzingatia hatua kubwa tuliyofikia tukiwa timu, ni msimu wa kipekee, hii mechi yetu ya mwisho ni ya 63 katika michuano yote, tulijitoa kwa kila kitu hadi hatua hii tuliyofikia,” alisema Rice.


Rice alisema waliifikisha mechi kwenye hatua ya penalti na aliifahamu hatua hiyo ni kamari lakini anaamini katika soka ni unashinda au unashindwa kwenye penalti, na zipo timu bora ambazo zimepoteza mechi kwenye penalti katika fainali.
Alisema wao Arsenal wapo katika kundi lililoshindwa lakini cha msingi ni kwamba wameshinda pamoja na kushindwa pamoja.
Rice aliongeza kwa kusema kuwa ingawa ameumizwa lakini akikumbuka jinsi walivyouanza msimu mwezi Julai na hadi walipofikia sasa kila kitu kinaonesha kuwa ilikuwa safari nzuri ya msimu.

The post Declan Rice ajivunia Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/06/03/declan-rice-ajivunia-arsenal/feed/ 0
Declan Rice, mechi ya 50, nahodha England https://www.greensports.co.tz/2024/03/26/declan-rice-mechi-ya-50-nahodha-england/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/26/declan-rice-mechi-ya-50-nahodha-england/#respond Tue, 26 Mar 2024 07:15:31 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10351 London, EnglandKiungo wa Arsenal, Declan Rice amefurahia kupewa nafasi ya kuwa nahodha wa timu ya England katika mechi ya leo Jumanne dhidi ya Ubelgiji ambayo pia inakuwa mechi yake ya 50 na timu hiyo.Rice, 25, amekuwa mchezaji muhimu England tangu apate nafasi ya kuichezea timu hiyo mara ya kwanza mwaka 2019 na leo kwenye dimba […]

The post Declan Rice, mechi ya 50, nahodha England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kiungo wa Arsenal, Declan Rice amefurahia kupewa nafasi ya kuwa nahodha wa timu ya England katika mechi ya leo Jumanne dhidi ya Ubelgiji ambayo pia inakuwa mechi yake ya 50 na timu hiyo.
Rice, 25, amekuwa mchezaji muhimu England tangu apate nafasi ya kuichezea timu hiyo mara ya kwanza mwaka 2019 na leo kwenye dimba la Wembley atakuwa nahodha katika mechi hiyo ya kirafiki.
Mchezaji huyo amepewa nafasi hiyo baada ya nahodha mkuu Harry Kane na msaidizi wake, Kyle Walker kuwa majeruhi na hivyo hawatakuwamo katika kikosi cha England kwenye mechi ya leo.

“Mechi yangu ya 50 nakwenda kwenye dimba la Wembley mbele ya familia yangu na marafiki, ni heshima kubwa, najikuta sina la kusema,” alisema Rice.


Tukio la Rice kupewa unahodha katika mechi yake ya 50 linaweza pia kumkumbusha miaka mitano iliyopita alipopata nafasi ya kuichezea England kwa mara ya kwanza dhidi ya Jamhuri ya Czech mwaka 2019 na sasa anajivunia kuifikisha timu hiyo kwenye hatua ya fainali ya Euro 2020 na robo fainali ya Kombe la Dunia 2022.
“Nimepiga hatua kubwa kiuchezaji, na kama binadamu tangu nije katika kundi hili kwa mara ya kwanza, kadri muda ulivyokwenda nimeweza kucheza mechi kubwa zaidi za michuano mikubwa, nimekuwa nikifurahia kila hatua,” alisema Rice.
Kikosi cha England chini ya kocha Gareth Southgate kinaandamwa na janga la majeruhi ambapo mbali na Walker na Kane, wengine ni Bukayo Saka, Luke Shaw, Harry Maguire, Sam Johnstone na Trent Alexander-Alexander.
Mechi za kimataifa za kirafiki leo Jumanne Machi 26, 2024
England v Ubelgiji
Uganda v Ghana
Finland v Estonia
Latvia v Liechtenstein
Hungary v Kosovo
Malta v Belarus
Norway v Slovakia
Jamhuri ya Czech v Armenia
Colombia v Romania
Ivory Coast v Uruguay
Senegal v Benin
Austria v Uturuki
Ujerumani v Uholanzi
Luxembourg v Kazakhstan
Jamhuri ya Ireland v Uswisi
Scotland v Ireland Kask
Slovenia v Ureno
Misri v Croatia
Ufaransa v Chile
Mali v Nigeria
New Zealand v Tunisia
Hispania v Brazil
Algeria v Afrika Kusini
Morocco v Mauritania

The post Declan Rice, mechi ya 50, nahodha England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/26/declan-rice-mechi-ya-50-nahodha-england/feed/ 0
Hatimaye Rice asaini Arsenal https://www.greensports.co.tz/2023/07/15/hatimaye-rice-asaini-arsenal/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/15/hatimaye-rice-asaini-arsenal/#respond Sat, 15 Jul 2023 17:57:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6982 London, EnglandArsenal hatimaye imemsajili kiungo Declan Rice kutoka West Ham kwa ada ya Pauni 100 milioni ikiibwaga Man City ambayo pia ilikuwa ikimtaka mchezaji huyo.Rice mwenye umri wa miaka 24 amesaini mkataba wa miaka mitano na Arsenal huku kukiwa na kipengele kinachompa nafasi ya kuongeza mwaka mwingine mmoja.Katika siku za karibuni, klabu za Arsenal na […]

The post Hatimaye Rice asaini Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Arsenal hatimaye imemsajili kiungo Declan Rice kutoka West Ham kwa ada ya Pauni 100 milioni ikiibwaga Man City ambayo pia ilikuwa ikimtaka mchezaji huyo.
Rice mwenye umri wa miaka 24 amesaini mkataba wa miaka mitano na Arsenal huku kukiwa na kipengele kinachompa nafasi ya kuongeza mwaka mwingine mmoja.
Katika siku za karibuni, klabu za Arsenal na Man City zilikuwa vitani katika kuisaka saini ya Rice ambaye hata hivyo iliwahi kuelezwa kwamba mwenyewe anaitamani zaidi Arsenal kuliko Man City
“Nimekuwa nikiiangalia Arsenal kwa misimu kadhaa iliyopita, ni timu yenye malengo inayoendelea nayo,” alisema Rice.
“Si msimu uliopta tu bali hata msimu kabla ya huu, walimaliza nafasi ya tano lakini unaweza kuona aina yao ya uchezaji aliyokuwa akiifanyia kazi Mikel (Arteta),” aliongeza Rice.
“Msimu uliopita ulikuwa wa kipekee waliibwaga karibu kila timu kwenye maji isipokuwa Manchester City,” aliongeza Rice.
Rice amekuwa kivutio katika timu ya West Ham chini ya kocha David Moyes lakini umaarufu wake ulikuwa juu zaidi akiwa na timu ya England kwenye fainali za Kombe la Dunia, akazidi kuzungumzwa alipoiwezesha West Ham kubeba taji la Europa Conference Ligi.
Usajili wa Rice ni wa tatu katika kikosi cha Arsenal, timu ambayo imedhamiria kuwa bora zaidi baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu England (EPL) msimu uliopita wa 2022-23.


Arsenal tayari imekamilisha usajili wa Mjerumani Kai Havert kutoka Chelsea kwa ada ya Pauni 65 milioni pamoja na beki Mholanzi, Jurrien Timber kutoka Ajax kwa ada inayotajwa kufikia Pauni 38.5 milioni.
Akimzungumzia Rice, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta alisema kwamba hakuna ubishi kwamba ataingiza kiwango bora katika timu na ana kipaji kikubwa ambacho kitampa nafasi ya kupata mafanikio akiwa Arsenal.
“Declan ana uzoefu katika Ligi Kuu England akiwa ndio kwanza ana miaka 24, amekuwa nahodha wa klabu nzuri ya West Ham kama ambavyo wengi tumemshuhudia na hivi karibuni amebeba taji la Ulaya,” alisema Arteta.
Arsenal imefanikiwa kuinasa saini ya Rice baada ya ofa zao mbili kukataliwa wakati Man City wao ofa yao moja ya Pauni 90 milioni ilikataliwa.
Rice ameifungia West Ham mabao 15 katika mechi 245, alijiunga na akademi ya timu hiyo akiwa na miaka 14 baada ya kuachwa kwenye akademi ya Chelsea.
Alisaini mkataba na kikosi cha kwanza cha West Ham, Desemba 2015 na kuanza kuiwakilisha timu hiyo kwenye EPL msimu wa 2016-17 akiingia kutokea benchi kwenye mechi na Burnley kabla ya kuanza kipindi cha kwanza mara ya kwanza msimu huo huo katika mechi na Southampton.


Rice alikabidhiwa unahodha West Ham mwaka jana baada ya Mark Noble kustaafu na ingawa huo ulikuwa msimu wake wa mwisho, Rice amemaliza vizuri kwa kubeba taji la Europa Conference na kufuta ukame wa miaka 43 wa timu hiyo bila taji lolote kubwa.
“Katika soka fursa kubwa hujitokeza, klabu kubwa kama Arsenal imekuja kwangu na kwa hakika ni vigumu kuikataa, nayaangalia yajayo ya Arsenal kutokana na aina ya kikosi ambacho Mikel anakitengeneza, nina furaha kubwa kufanya kazi na Mikel,” alisema Rice.

“Kwangu mimi kama mchezaji nimekuja hapa nikiwa mwenye njaa ya kupata mafanikio zaidi na kutumia vizuri muda wangu nikiwa na klabu hii kubwa,” alisema Rice.


Arteta alisema kwamba Rice ataipa nguvu na kutoa mwelekeo wa timu hiyo katika eneo la kati, jambo ambalo limekosekana na hivyo tayari ameanza kuonekana kama ndiye ‘Vieira’ (Patrick) mpya. Vieira alikuwa nahodha na kiungo tishio katika zama za mafanikio ya Arsenal miaka ya 2000.

The post Hatimaye Rice asaini Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/15/hatimaye-rice-asaini-arsenal/feed/ 0
Rice aikataa Man City, aitaka Arsenal https://www.greensports.co.tz/2023/06/23/rice-aikataa-man-city-aitaka-arsenal/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/23/rice-aikataa-man-city-aitaka-arsenal/#respond Fri, 23 Jun 2023 20:57:49 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6707 London, EnglandKiungo wa West Ham na timu ya Taifa ya England, Declan Rice (pichani) ambaye anawaniwa na timu za Arsenal na Manchester City inadaiwa anapendelea zaidi kujiunga Arsenal badala ya Man City.Uamuzi huo wa Rice umekuja baada ya Man City kudaiwa kuingia katika mbio za kumtaka mchezaji huyo wakati huu ofa mbili za Arsenal zikiwa […]

The post Rice aikataa Man City, aitaka Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kiungo wa West Ham na timu ya Taifa ya England, Declan Rice (pichani) ambaye anawaniwa na timu za Arsenal na Manchester City inadaiwa anapendelea zaidi kujiunga Arsenal badala ya Man City.
Uamuzi huo wa Rice umekuja baada ya Man City kudaiwa kuingia katika mbio za kumtaka mchezaji huyo wakati huu ofa mbili za Arsenal zikiwa zimekataliwa ikiwamo ya mwisho ya Pauni 90 milioni.
Kitendo cha Man City kumtaka mchezaji huyo kinaiweka pagumu Arsenal na haijaweza kufahamika mara moja kama timu hiyo itakuwa tayari kushindana katika kuisaka saini ya mchezaji huyo.
Man City tayari imeonesha nia ya kumsajili Rice ikidaiwa kuwa tayari kutoa Pauni 100 milioni ikiamini mchezaji huyo ni mtu sahihi kuziba pengo la kiungo wao, Ilkay Gundogan aliyehamia Barcelona.
Kwa upande mwingine uamuzi wa Rice kuichagua Arsenal linakuwa jambo zuri kwa kocha Mikel Arteta ambaye anaamini mchezaji huyo ni nahodha wa baadaye wa timu yake na sasa wanajiandaa kupeleka West Ham ofa yao kwa mara ya tatu.
Rice amekuwa na msimu mzuri katika kikosi cha West Ham akiisaidia timu hiyo kubeba taji la Europa Conference Ligi lakini pia ameonesha uwezo katika kikosi cha timu ya Taifa ya England na hadi sasa hatma yake imekuwa mjadala kila kona hasa baada ya yeye mwenyewe kusema kwamba angependa kusaka changamoto katika klabu nyingine.

The post Rice aikataa Man City, aitaka Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/23/rice-aikataa-man-city-aitaka-arsenal/feed/ 0
Rice aziingiza vitani Arsenal, Man City https://www.greensports.co.tz/2023/06/22/rice-aziingiza-vitani-arsenal-man-city/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/22/rice-aziingiza-vitani-arsenal-man-city/#respond Thu, 22 Jun 2023 18:44:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6703 London, EnglandArsenal sasa italazimika kukaza buti ili kuingia vitani na Man City katika kuiwania saini ya kiungo wa West Ham, Declan Rice (pichani) baada ya Man City nao kuwasilisha ofa ya kumtaka mchezaji huyo.Kwa kipindi kirefu Arsenal imekuwa ikitajwa kumtaka Rice ambaye hivi karibuni aliweka rekodi kwa kuiwezesha West Ham kutwaa taji la Europa Conference […]

The post Rice aziingiza vitani Arsenal, Man City first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Arsenal sasa italazimika kukaza buti ili kuingia vitani na Man City katika kuiwania saini ya kiungo wa West Ham, Declan Rice (pichani) baada ya Man City nao kuwasilisha ofa ya kumtaka mchezaji huyo.
Kwa kipindi kirefu Arsenal imekuwa ikitajwa kumtaka Rice ambaye hivi karibuni aliweka rekodi kwa kuiwezesha West Ham kutwaa taji la Europa Conference Ligi huku akiwa mmoja wa wachezaji ambao soka lao lilivutia wengi.
Tayari ofa za Arsenal zimekataliwa mara mbili, ya mwisho ilikuwa ya Pauni 90 milioni iliyokataliwa juzi Jumanne lakini habari za leo Alhamisi kuhusu City kumtaka mchezaji huyo zinaifanya Arsenal kupata mpinzani wa kwanza katika mpango huo.
Habari za ndani zinadai kwamba City walikuwa wakisubiri kujua hatma ya kiungo na nahodha wao Ilkay Gundogan kama angebaki katika klabu hiyo.
Gundogan hata hivyo amekataa kusaini mkataba mpya na City na kuamua kujiunga na Barcelona, kocha wa Man City, Pep Guardiola sasa anaamini Rice ambaye pia anaichezea timu ya Taifa ya England ndiye mtu sahihi wa kuchukua nafasi ya Gundogan.
Uamuzi wa Man City umekuja wakati ambao Arsenal wanajiandaa kuja na ofa nyingine kwa mara ya tatu huku kukiwa na habari kwamba West Ham wanaamini thamani ya Rice ni zaidi ya Pauni 100 milioni.
Na ingawa Arsenal wamekuwa wakijiamini kuwa na uwezo wa kumpata mchezaji huyo lakini kwa sasa itabidi ijulikane kwanza ofa ambayo Man City wamejiandaa kuiweka mezani.
Kwa upande wa Rice ambaye ana mkataba na West Ham unaofikia ukomo mwaka 2024, amewahi kunukuliwa akisema kwamba anataka kwenda kusaka changamoto mpya nje ya klabu hiyo.

The post Rice aziingiza vitani Arsenal, Man City first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/22/rice-aziingiza-vitani-arsenal-man-city/feed/ 0
Declan Rice aagwa West Ham https://www.greensports.co.tz/2023/06/09/declan-rice-aagwa-west-ham/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/09/declan-rice-aagwa-west-ham/#respond Fri, 09 Jun 2023 15:09:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6529 London, EnglandMwenyekiti wa klabu ya West Ham, David Sullivan ameamua kumuaga kiaina nahodha wao, Declan Rice baada ya kusema ana uhakika asilimia 99 mchezaji huyo ataondoka katika klabu hiyo.Sullivan alitoa kauli hiyo mara baada ya timu hiyo kubeba taji la Europa Conference Ligi kwa kuichapa Fiorentina mabao 2-1 na kuweka historia kwa kubeba taji la […]

The post Declan Rice aagwa West Ham first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Mwenyekiti wa klabu ya West Ham, David Sullivan ameamua kumuaga kiaina nahodha wao, Declan Rice baada ya kusema ana uhakika asilimia 99 mchezaji huyo ataondoka katika klabu hiyo.
Sullivan alitoa kauli hiyo mara baada ya timu hiyo kubeba taji la Europa Conference Ligi kwa kuichapa Fiorentina mabao 2-1 na kuweka historia kwa kubeba taji la kwanza kubwa baada ya miaka 43.
Rice (pichani) katika siku za karibuni amekuwa akitajwa kuwindwa na klabu za barani Ulaya lakini Sullivan alisema walimpa ahadi kwamba akijitoa kwa hali na mali kwa timu hiyo watampa nafasi ya kuondoka.

“Tulimpa ahadi, majira ya kiangazi msimu uliopita kwamba akiweza kutupa kila kitu tutamruhusu aondoke katika klabu, hivyo kwa sasa ni jambo la haki na sahihi kulifanya,” alisema Sullivan.


Juzi Jumatano Rice alikuwa nahodha wa tatu katika historia ya klabu hiyo kubeba taji la klabu hiyo akifuata nyayo za watangulizi wake Bobby Moore aliyebeba taji la Washindi Ulaya mwaka 1965 na Billy Bonds aliyebeba taji la FA mwaka 1975 na 1980.
Tangu atue kikosi cha kwanza cha West Ham msimu wa 2016-17 akitokea katika akademi ya klabu hiyo, Rice ameichezea timu hiyo mara 245 na kufunga mabao 15 huku akionyesha uwezo katika nafasi ya kiungo.
Awali aliiwakilisha timu ya Jamhuri ya Ireland mara tatu kabla ya kubadili na kuanza kuichezea timu ya England na hadi sasa ameichezea timu hiyo mara 41 na alicheza mechi tano za England kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 zilizofanyika Qatar.
Katika mkataba wake na West Ham, Rice amebakisha mwaka mmoja lakini kinachosubiriwa sasa ni kujua timu anayoelekea huku Arsenal ikitajwa kuwa moja ya timu zinazovutiwa na mchezaji huyo.
Rice ambaye ametangazwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka wa Uefa Conference Ligi, amejijengea umaarufu kwa kucheza soka la kuvutia katika eneo la kiungo kwa namna anavyojua kuusoma mchezo na kutopoteza mipira.

The post Declan Rice aagwa West Ham first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/09/declan-rice-aagwa-west-ham/feed/ 0