Cristiano Ronaldo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 08 Jul 2026 20:28:49 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Cristiano Ronaldo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Ronaldo astaafu timu ya taifa https://www.greensports.co.tz/2026/07/07/ronaldo-astaafu-timu-ya-taifa/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/07/ronaldo-astaafu-timu-ya-taifa/#respond Tue, 07 Jul 2026 12:51:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14770 Arlington, TexasZama za mwanasoka mahiri duniani, Cristiano Ronaldo kwenye timu ya taifa ya Ureno zimefika mwisho baada ya timu hiyo kutolewa kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 na yeye kutoka mikono mitupu kwenye michuano hiyo.Ureno imetolewa na Hispania kwa kuchapwa bao 1-0 katika mechi ya hatua ya mtoano (16 bora) iliyopigwa mjini Dallas, Jumatatu […]

The post Ronaldo astaafu timu ya taifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Arlington, Texas
Zama za mwanasoka mahiri duniani, Cristiano Ronaldo kwenye timu ya taifa ya Ureno zimefika mwisho baada ya timu hiyo kutolewa kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 na yeye kutoka mikono mitupu kwenye michuano hiyo.
Ureno imetolewa na Hispania kwa kuchapwa bao 1-0 katika mechi ya hatua ya mtoano (16 bora) iliyopigwa mjini Dallas, Jumatatu Julai 6, 2026 huku Ronaldo akiaga na kutangaza mapema kuwa hizi ni fainali zake za mwisho.
Bao hilo pekee la dakika ya 46 lililofungwa na Mikel Merino limemfanya Ronaldo kuungana na nyota wa Brazil, Neymar Jr ambaye naye ameachana na timu hiyo huku wote wakitoka uwanjani na vilio baada ya timu zao kutolewa.
Kutolewa kwa Ureno kunamfanya Ronaldo aondoke katika timu hiyo akiwa hajawahi kubeba Kombe la Dunia licha ya mafanikio makubwa aliyopata katika soka ikiwamo kutwaa tuzo ya Ballon d’Or mara tano.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 41 mbali na Ballon d’Or na Kombe la Ulaya alilobeba mwaka 2016 (Euro 2016) ana rekodi ya kubeba mataji ya ligi mbalimbali kubwa Ulaya ikiwamo Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tano.
Mchezaji huyo anaachana na timu ya Ureno akiwa ameiwakilisha kwenye fainali sita za Kombe la Dunia na mafanikio yake katika michuano hiyo ni mwaka 2006 katika fainali zake za kwanza ambapo Ureno ilifikia hatua ya nusu fainali.
Ushiriki wa Ronaldo katika fainali za Kombe la Dunia 2026 zinazofanyika katika mataifa ya Canada, Marekani na Mexico ulipingwa na baadhi ya wachambuzi kwa hoja kwamba mchezaji huyo amefikia mwisho.
Kocha wa Ureno, Roberto Martinez amekuwa na mtazamo tofauti na wachambuzi hao kwa kumtetea Ronaldo hata baada ya Ureno kutolewa na rekodi kuonesha kwamba mchezaji huyo hakuwa na mchango wa maana kwenye timu.

The post Ronaldo astaafu timu ya taifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/07/ronaldo-astaafu-timu-ya-taifa/feed/ 0
Ronaldo atajwa Kombe la Dunia 2030 https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/ronaldo-atajwa-kombe-la-dunia-2030/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/ronaldo-atajwa-kombe-la-dunia-2030/#respond Sun, 31 May 2026 08:51:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14662 Porto, UrenoKocha wa timu ya Ureno, Roberto Martinez amesema hakuna wa kutilia shaka habari kuwa Cristiano Ronaldo anaweza kucheza katika fainali za Kombe la Dunia 2030 wakati huo akiwa na miaka 45.Ronaldo atakuwa na timu ya Ureno kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 zinazotarajia kutimua vumbi Juni 11 katika nchi za Marekani, Mexico na […]

The post Ronaldo atajwa Kombe la Dunia 2030 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Porto, Ureno
Kocha wa timu ya Ureno, Roberto Martinez amesema hakuna wa kutilia shaka habari kuwa Cristiano Ronaldo anaweza kucheza katika fainali za Kombe la Dunia 2030 wakati huo akiwa na miaka 45.
Ronaldo atakuwa na timu ya Ureno kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 zinazotarajia kutimua vumbi Juni 11 katika nchi za Marekani, Mexico na Canada, hii ikiwa ni mara ya sita kwa mchezaji huyo kushiriki fainali hizo.
Fainali za Kombe la Dunia 2030 zitafanyika kwa ushirikiano katika mataifa ya Mexico na Hispania na Martinez anaamini kwa wakati huo haitokuwa ajabu jina la Ronaldo kuwamo kwenye kikosi cha Ureno.
Ronaldo alianza kuichezea Ureno mara ya kwanza mwaka 2003, kwa sasa ndiye anayeongoza kuichezea timu hiyo mara nyingi (226) akiwa amefunga mabao 143 na ni mchezaji pekee mwenye rekodi ya kufunga mabao katika fainali tano za Kombe la Dunia.
Martinez aliulizwa swali iwapo Ronaldo ataweza kushiriki fainali za Kombe la Dunia 2030 ambapo kocha huyo alisema hakuna anayeweza kutilia shaka jambo hilo.
Kauli ya Martinez imekuja wakati Ronaldo mwenyewe hajaweka wazi ni lini hasa atastaafu kuichezea timu hiyo hivyo haitokuwa ajabu akiwa na timu hiyo.
Ronaldo ambaye pia amewahi kutamba na timu za Man United na Real Madrid, kwa sasa anacheza soka Saudi Arabia katika klabu ya Al Nassr akiwa ndiye mchezaji anayelipwa fedha nyingi.
Ureno ipo Kundi K, itacheza mechi yake ya kwanza ya Kombe la Dunia Juni 17 dhidi ya DR Congo na kufuatiwa na mechi dhidi ya Uzbekistan Juni 23 na kumalizia mechi za makundi dhidi ya Colombia Juni 27.

The post Ronaldo atajwa Kombe la Dunia 2030 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/ronaldo-atajwa-kombe-la-dunia-2030/feed/ 0
Ronaldo apiga bao, Al Nassr kileleni https://www.greensports.co.tz/2026/02/26/ronaldo-apiga-bao-al-nassr-kileleni/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/26/ronaldo-apiga-bao-al-nassr-kileleni/#respond Thu, 26 Feb 2026 19:11:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14370 Riyadh, Saudi ArabiaCristiano Ronaldo ametupia kambani katika ushindi wa mabao 5-0 ambao Al Nassr iliupata jana Jumatano Februari 25, 2026 dhidi ya Al Najma na kuiwezesha timu hiyo kushika usukani kwenye msimamo wa ligi.Hilo ni bao la tatu kwa Ronaldo tangu asitishe mgomo baridi na kuanza kuitumikia timu hiyo inayopambana katika mechi za Ligi Kuu […]

The post Ronaldo apiga bao, Al Nassr kileleni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabia
Cristiano Ronaldo ametupia kambani katika ushindi wa mabao 5-0 ambao Al Nassr iliupata jana Jumatano Februari 25, 2026 dhidi ya Al Najma na kuiwezesha timu hiyo kushika usukani kwenye msimamo wa ligi.
Hilo ni bao la tatu kwa Ronaldo tangu asitishe mgomo baridi na kuanza kuitumikia timu hiyo inayopambana katika mechi za Ligi Kuu Saudi Arabia maarufu Saudi Pro League.
Ronaldo ndiye aliyeanza kufungua ukurasa wa mabao baada ya kufunga kwa mkwaju wa penalti mapema dakika ya saba ya mchezo na hivyo kumfanya afikishe mabao 20 msimu huu akiwa amezidiwa katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu na Ivan Toney wa Al Ahli mwenye mabao 23.
Kasi ya Al Nassr iliendelea na kuzaa mabao mawili yaliyofungwa na Kingsley Coman na Inigo Martinez, mabao ambayo yalizifanya timu hizo ziende mapumziko Al Nassr wakiwa mbele kwa mabao 3-0.
Mabao mengine ya Al Nassr yalipachikwa wavuni na Sadio Mane mapema katika kipindi cha pili wakati ambao kocha wa timu hiyo, Jorge Jesus alianza kufanya mabadiliko kwa kuwatoa baadhi ya mastaa akiwamo Ronaldo.
Al Nassr inashika usukani wa ligi hiyo ikiwa imefikisha pointi 58 katika mechi 23 na hadi sasa imepoteza mechi moja tu na imewazidi kwa pointi mbili, Al Ahli wanaoshika nafasi ya pili.
Mapema mwezi huu Ronaldo alikosa mechi mbili za timu yake dhidi ya Al Ittihad na Al Riyadh kutokana na kilichodaiwa kuwa ni mgomo baridi aliouanzisha akipinga masuala kadhaa ya uendeshaji wa klabu na ligi ya Saudi Arabia.

The post Ronaldo apiga bao, Al Nassr kileleni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/26/ronaldo-apiga-bao-al-nassr-kileleni/feed/ 0
Ronaldo asitisha mgomo baridi https://www.greensports.co.tz/2026/02/15/ronaldo-asitisha-mgomo-baridi/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/15/ronaldo-asitisha-mgomo-baridi/#respond Sun, 15 Feb 2026 11:05:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14338 Riyadh, Saudi ArabiaCristiano Ronaldo amerejea kwa mara nyingine katika kikosi cha kwanza cha Al Nassr katika mechi dhidi ya Al Fateh baada ya kuwa kwenye mgomo baridi uliomfanya akose mechi mbili zilizopita za timu hiyo.Katika mechi hiyo iliyochezwa Jumamosi Februari 14, 2026, Ronaldo alikuwamo katika kikosi cha kwanza akiwa ndiye nahodha wa timu yake iliyotoka […]

The post Ronaldo asitisha mgomo baridi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabia
Cristiano Ronaldo amerejea kwa mara nyingine katika kikosi cha kwanza cha Al Nassr katika mechi dhidi ya Al Fateh baada ya kuwa kwenye mgomo baridi uliomfanya akose mechi mbili zilizopita za timu hiyo.
Katika mechi hiyo iliyochezwa Jumamosi Februari 14, 2026, Ronaldo alikuwamo katika kikosi cha kwanza akiwa ndiye nahodha wa timu yake iliyotoka na ushindi wa mabao 2-0.
Akiwa sambamba na mastaa wengine wa timu hiyo kina João Félix, Sadio Mané na Kingsley Coman, Ronaldo ndiye aliyefunga bao la kwanza la timu yake katika dakika ya 18.
Al Nassr iliongeza bao la pili katika dakika ya 70 mfungaji akiwa ni Ayman Yahya, ushindi ambao umeifanya Al Nassr ijiimarishe katika nafasi ya pili ikiwa imezidiwa na vinara Al Hilal kwa tofauti ya pointi moja.
Katika wiki tatu za hivi karibuni Ronaldo alikuwa katika mgomo uliomfanya azikose mechi za Al Nassr dhidi ya Al Riyadh na Al Ittihad na kukawa na habari kwamba timu hiyo ilikuwa tayari kumruhusu aondoke.
Katika mgomo huo, Ronaldo alikuwa akilalamikia uendeshaji wa Ligi Kuu Saudi Arabia au Saudi Pro League na zaidi kitendo cha uongozi wa klabu ya Al Nassr kutoongeza nguvu katika uwekezaji wa timu kama ilivyo kwa mahasimu wao, Al Hilal.
Ronaldo hajafurahishwa na hali hiyo hasa baada ya Al Hilal kumsajili Karim Benzema kutoka Al Ittihad, Benzema nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa, aliwahi kucheza na Ronaldo katika klabu ya Real Madrid.
Baada ya mgomo huo, mamlaka ya uendeshaji wa ligi hiyo ilitoa taarifa yenye kutoa msisitizo kwa klabu zote kusimamia masuala yao ya kifedha na uendeshaji wa klabu kwa namna zinavyoona kuwa sahihi.
Ronaldo hadi sasa amefikisha mabao 18 katika ligi hiyo kwa msimu huu akiwa amefungana na Julian Quinones wa Al Gadsiah ambao wote wanawania kiatu cha dhahabu sawa na Ivan Toney wa Al Hilal mwenye mabao 16.

The post Ronaldo asitisha mgomo baridi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/15/ronaldo-asitisha-mgomo-baridi/feed/ 0
Siku za Ronaldo zahesabika Al Nassr https://www.greensports.co.tz/2026/02/07/siku-za-ronaldo-zahesabika-al-nassr/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/07/siku-za-ronaldo-zahesabika-al-nassr/#respond Sat, 07 Feb 2026 14:15:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14318 Riyadh, Saudi ArabiaSasa ni wazi kuwa siku za Cristiano Rinaldo katika klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia zinahesabika na zipo habari kwamba klabu hiyo imetangaza kuwa tayari kumuuza winga huyo kwa ada ya Pauni 42.9 milioni.Ronaldo, 41, hatma yake katika klabu hiyo kwa siku za karibuni imekuwa katika sintofahamu hali ambayo imeonesha kuwa hana […]

The post Siku za Ronaldo zahesabika Al Nassr first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabia
Sasa ni wazi kuwa siku za Cristiano Rinaldo katika klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia zinahesabika na zipo habari kwamba klabu hiyo imetangaza kuwa tayari kumuuza winga huyo kwa ada ya Pauni 42.9 milioni.
Ronaldo, 41, hatma yake katika klabu hiyo kwa siku za karibuni imekuwa katika sintofahamu hali ambayo imeonesha kuwa hana muda mrefu ataachana na klabu hiyo tajiri barani Asia.
Katika hali ambayo haikutarajiwa, Ronaldo kwa mara ya pili mfululizo aliachwa kwenye kikosi cha timu hiyo, kwanza aliikosa mechi ya Jumatatu iliyopita dhidi ya Al Riyadh na jana Ijumaa akaikosa mechi nyingine dhidi ya Al Ittihad.
Kukosekana kwa Ronaldo katika mechi hizo mbili kunatosha kuibua hisia kwamba kuna kitu kibaya kinaendelea kati ya Ronaldo na klabu hiyo na kilicho wazi ni kwamba wakati wowote atapewa mkono wa kwaheri.
Habari za ndani zinadai kwamba Ronaldo ameanza mgomo baridi akidaiwa kutoridhishwa na mfumo wa uendeshaji wa Ligi Kuu ya Saudi Arabia maarufu Saudi Pro League.
Katika madai yake, Ronaldo ametaka ahakikishiwe kufanyika mabadiliko ya mfumo wa ligi hiyo jambo ambalo hajahakikishiwa na mchezaji huyo wa zamani wa klabu za Real Madrid na Man United anaona kama amepuuzwa.
Al Nassr pamoja na kucheza bila Ronaldo, ilipata ushindi wa mabao 2-0 katika mechi dhidi ya Al Ittihad ingawa mashabiki walionekana kumuunga mkono Ronaldo kwa kuinua jezi na alama za rangi ya njano zenye picha ya mchezaji huyo.
Baada ya ushindi huo Al Nassr imepanda hadi nafasi ya pili katika ligi hiyo ikiwa nyuma ya vinara Al Hilal kwa tofauti ya pointi moja.
Wasimamizi wa Ligi Kuu Saudi Arabia, juzi Alhamisi walitoa taarifa wakimuonya Ronaldo kuwa hakuna mchezaji mwenye uwezo wa kushawishi maamuzi zaidi ya timu yake.

The post Siku za Ronaldo zahesabika Al Nassr first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/07/siku-za-ronaldo-zahesabika-al-nassr/feed/ 0
Fernandes: Ureno yenye Ronaldo ‘tamu’ https://www.greensports.co.tz/2025/12/19/fernandes-ureno-yenye-ronaldo-tamu/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/19/fernandes-ureno-yenye-ronaldo-tamu/#respond Fri, 19 Dec 2025 18:34:31 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14208 Manchester, EnglandKiungo wa Man United, Bruno Fernandes amesema Cristiano Ronaldo bado ana mchango mkubwa kwa timu ya taifa ya Ureno na hakubaliani na wanaodai kuwa timu hiyo inacheza vizuri ikimkosa mchezaji huyo.Katika mechi ya hivi karibuni, Ureno ikiwa bila ya Ronaldo aliyekuwa akitumikia adhabu ilipata ushindi wa mabao 9-1 dhidi ya Armenia na hatimaye kufuzu […]

The post Fernandes: Ureno yenye Ronaldo ‘tamu’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kiungo wa Man United, Bruno Fernandes amesema Cristiano Ronaldo bado ana mchango mkubwa kwa timu ya taifa ya Ureno na hakubaliani na wanaodai kuwa timu hiyo inacheza vizuri ikimkosa mchezaji huyo.
Katika mechi ya hivi karibuni, Ureno ikiwa bila ya Ronaldo aliyekuwa akitumikia adhabu ilipata ushindi wa mabao 9-1 dhidi ya Armenia na hatimaye kufuzu moja kwa moja kucheza fainali za Kombe la Dunia 2026.
Fernandes ambaye pia ni nahodha wa Man United, pamoja na matokeo ya mechi dhidi ya Armenia hata hivyo bado anaamini Ronaldo akiwa ndani ya eneo la boksi anabaki kuwa mchezaji wa kiwango cha juu.

“Ronaldo anawachanganya mabeki na kutengeneza nafasi kwa wachezaji wengine,” alisema Fernandes akimpamba mchezaji huyo mkongwe aliyewahi kuzichezea Man United na Real Madrid.


Akifafanua zaidi Fernandes alisema anatambua kile watu wanachofikiria kwamba huwa wanacheza vizuri na kuwa huru bila ya Ronaldo lakini kama hilo linatokea tatizo ni wao wenyewe kwani hawatakiwi kuwa na hofu Ronaldo anapokuwa uwanjani kwa sababu mchezaji huyo anaweza kuwapa vitu zaidi.
Nafasi ya Ronaldo kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya Ureno ilianza kuwa mashakani baada ya kuwekwa benchi na kocha Fernando Santos kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022.
Mambo hata hivyo yalibadilika kwa mchezaji huyo wa Al Nassr ya Saudi Arabia baada ya kuanza tena kuonesha makali yake kwa mara nyingine timu ikiwa chini ya kocha Roberto Martinez.
Ronaldo, 40, ambaye alianza kuichezea timu ya taifa ya Ureno kwa mara ya kwanza mwaka 2003, kwa sasa ndiye mchezaji anayeongoza kwa kuifungia mabao mengi timu hiyo, mabao 143 katika mechi 226.

The post Fernandes: Ureno yenye Ronaldo ‘tamu’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/19/fernandes-ureno-yenye-ronaldo-tamu/feed/ 0
Ronaldo: Kombe la Dunia 2026 mwisho https://www.greensports.co.tz/2025/11/12/ronaldo-kombe-la-dunia-2026-mwisho/ https://www.greensports.co.tz/2025/11/12/ronaldo-kombe-la-dunia-2026-mwisho/#respond Wed, 12 Nov 2025 08:41:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14099 Porto, UrenoMshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, amethibitisha kuwa fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakuwa za mwisho kwake.Ronaldo, nyota wa zamani wa timu za Sporting Lisbon, Man United, Real Madrid na Juventus kwa sasa ana miaka 40 akiwa na rekodi ya kufunga mabao 952 kwa klabu alizochezea na timu yake ya […]

The post Ronaldo: Kombe la Dunia 2026 mwisho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Porto, Ureno
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, amethibitisha kuwa fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakuwa za mwisho kwake.
Ronaldo, nyota wa zamani wa timu za Sporting Lisbon, Man United, Real Madrid na Juventus kwa sasa ana miaka 40 akiwa na rekodi ya kufunga mabao 952 kwa klabu alizochezea na timu yake ya taifa, pia amesema atastaafu soka mwaka mmoja au miwili ijayo.
Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitafanyika katika nchi za Canada, Mexico na Marekani na kama Ronaldo atakuwamo kwenye fainali hizo basi atakuwa ameweka rekodi ya kushiriki fainali za michuano hiyo mikubwa ya soka duniani kwa mara sita.
Ronaldo ambaye kwa sasa anaichezea Al Nasr ya Saudi Arabia anashika nafasi ya kwanza kwa kuwa mchezaji mwenye rekodi ya kufunga mabao mengi katika mechi za kimataifa, mabao 143.
Akijibu swali aliloulizwa iwapo atastaafu baada ya Kombe la Dunia 2026, Ronaldo alijibu kwa kifupi akisema ndio huo utakuwa mwisho wake katika tukio hilo kubwa (Kombe la Dunia) na hapo hapo akazungumzia kustaafu soka moja kwa moja.

“Ndio, hilo ni wazi, wakati huo nitakuwa na miaka 41 na nafikiri huo utakuwa mwisho katika michuano mikubwa, na pia ngoja tu niwe wazi, nikisema hivi karibuni namaanisha mwaka mmoja au miwili bado nitakuwa kwenye mchezo huu (soka),” alisema Ronaldo.


Ronaldo pamoja na kuwa kwenye soka kwa kipindi kirefu na kubeba mataji na tuzo mbalimbali kubwa, hajaweza kubeba Kombe la Dunia, mafanikio pekee makubwa kwa timu yake ya taifa ni yale ya mwaka 2016 alipobeba taji la Euro na timu ya Ureno.
Ureno hata hivyo hadi sasa bado haijawa na uhakika wa kucheza fainali za Kombe la Dunia 2026 na ili kupata nafasi hiyo italazimika kupata ushindi katika mechi yao ya Alhamisi dhidi ya Jamhuri ya Ireland.

The post Ronaldo: Kombe la Dunia 2026 mwisho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/11/12/ronaldo-kombe-la-dunia-2026-mwisho/feed/ 0
Haaland ajitenga na Messi, Ronaldo https://www.greensports.co.tz/2025/11/05/haaland-ajitenga-na-messi-ronaldo/ https://www.greensports.co.tz/2025/11/05/haaland-ajitenga-na-messi-ronaldo/#respond Wed, 05 Nov 2025 08:09:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14066 Manchester, EnglandMshambuliaji nyota wa Man City, Erling Haaland amepuuza kitendo cha kulinganishwa na mastaa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wanaotamba katika rekodi za mabao akisema hakuna wa kusogelea rekodi za mabao za wachezaji hao.Haaland mwenye umri wa miaka 26, amefunga mabao 26 katika mashindano yote kwa Man City na timu yake ya taifa ya Norway […]

The post Haaland ajitenga na Messi, Ronaldo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Mshambuliaji nyota wa Man City, Erling Haaland amepuuza kitendo cha kulinganishwa na mastaa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wanaotamba katika rekodi za mabao akisema hakuna wa kusogelea rekodi za mabao za wachezaji hao.
Haaland mwenye umri wa miaka 26, amefunga mabao 26 katika mashindano yote kwa Man City na timu yake ya taifa ya Norway katika kipindi cha karibuni hivyo kufikisha jumla ya mabao 327 katika soka la ushindani hadi sasa.
Mchezaji huyo pamoja na rekodi hiyo ya kuvutia bado ameachwa mbali na wakongwe, Messi mwenye miaka 38 akiwa hadi sasa na jumla ya mabao 892 na Ronaldo mwenye miaka 40 akiwa na mabao 952 huku malengo yake yakiwa kufikisha mabao 1000.
Alipoulizwa kama anajiona kuwa karibu na mastaa hao, Haaland alikataa kulinganishwa na Messi na Ronaldo na kufafanua kuwa hakuna ambaye ataweza kuwasogelea wawili hao katika rekodi ya kufunga mabao.
Haaland alijiunga na Man City msimu wa 2022-23 akitokea Borussia Dortmund na katika msimu huo wa kwanza alifunga mabao 56, idadi ambayo hadi sasa ndiyo kubwa zaidi kwa mchezaji huyo kwa msimu mmoja.
Alipoulizwa kuhusu rekodi hiyo kama ana mpango wa kuivunja msimu huu, Haaland alisema kwa sasa anajiona yuko katika mazingira mazuri lakini suala la rekodi wala halipo katika fikra zake ikiwamo rekodi ya mabao katika Ligi Kuu England iliyowekwa na Alan Shearer.

“Kufikiria rekodi ninazoweza kuzivunja hilo ni jambo la mwisho katika fikra zangu, ninachofanya kwa sasa ni kuisaidia timu ishinde mechi zake, hiyo ndiyo kazi yangu na ndilo ninalolifikiria,” alisema Haaland.

The post Haaland ajitenga na Messi, Ronaldo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/11/05/haaland-ajitenga-na-messi-ronaldo/feed/ 0
Ten Hag amtetea Ronaldo https://www.greensports.co.tz/2025/08/09/ten-hag-amtetea-ronaldo/ https://www.greensports.co.tz/2025/08/09/ten-hag-amtetea-ronaldo/#respond Sat, 09 Aug 2025 17:07:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13812 London, EnglandKocha wa zamani wa Man United, Erik Ten Hag amesema aliyekuwa mchezaji wake katika timu hiyo, Cristiano Ronaldo hakuwahi kuwa tatizo wakati wake akiwa kocha.Ronaldo aliyetamba Man United kwa miaka mingi kabla ya kurejea mara ya pili mwaka 2021, alionekana kutokuwa na maelewano mazuri na Ten Hag hadi akaamua kundoka baada ya mwaka mmoja.Ten […]

The post Ten Hag amtetea Ronaldo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa zamani wa Man United, Erik Ten Hag amesema aliyekuwa mchezaji wake katika timu hiyo, Cristiano Ronaldo hakuwahi kuwa tatizo wakati wake akiwa kocha.
Ronaldo aliyetamba Man United kwa miaka mingi kabla ya kurejea mara ya pili mwaka 2021, alionekana kutokuwa na maelewano mazuri na Ten Hag hadi akaamua kundoka baada ya mwaka mmoja.
Ten Hag naye alitimuliwa Oktoba mwaka jana akiwa katika siku zake za mwanzo mwanzo za msimu wa 2024-25 kutokana na mwenendo usiopendeza wa timu hiyo na kocha huyo baadaye akajiunga na Bayer Leverkusen ya Ujerumani.
Akizungumza Ijumaa Agosti 8, 2025 baada ya mechi ya kirafiki kati ya Leverkusen na Chelsea, mechi iliyopigwa Stamford Bridge na Chelsea kushinda kwa mabao 2-0, Ten Hag alisema kwa yeye Ronaldo hakuwahi kuwa tatizo ingawa jambo hilo limepita.
Uhusiano duni kati ya Ronaldo na Ten Hag ulikuwa gumzo na kumulikwa na vyombo vya habari kwa kipindi ambacho winga huyo kutoka Ureno alikuwa na timu hiyo.

“Nafikiri ilikuwa kama ilivyokuwa, ni mambo yaliyopita na baada ya hapo tulishinda mataji mawili na Manchester United, namtakia kila la kheri kwa mambo yake ya baadaye na namtakia yote yaliyo mazuri,” alisema Ten Hag.


Ten Hag ambaye mbele ya wengi alionekana kufeli akiwa Man United lakini hadi anaondoka aliiwezesha timu hiyo kubeba mataji mawili, la Carabao mwaka 2023 pamoja na lile la FA mwaka 2024.
Kitendo cha kocha huyo kubeba taji la FA kiliwashangaza wengi kwa kuwa alishinda kwa kuwabwaga mahasimu wao Man City ambao walikuwa vinara na tishio kwenye Ligi Kuu England.
Ten Hag hata hivyo hakutaka kuzungumza kwa sana kuhusu Ronaldo badala yake alisisitiza kuwa anapenda kushinda mataji na ndilo jambo ambalo amekuwa akilifanya kwa maisha yake yote ya soka na anataka kuendelea na hilo na ndiyo changamoto aliyonayo wakati huu akiwa kocha wa Leverkusen.

The post Ten Hag amtetea Ronaldo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/08/09/ten-hag-amtetea-ronaldo/feed/ 0
Ronaldo aitamani Ligi ya Mabingwa Ulaya https://www.greensports.co.tz/2024/08/30/ronaldo-aitamani-ligi-ya-mabingwa-ulaya/ https://www.greensports.co.tz/2024/08/30/ronaldo-aitamani-ligi-ya-mabingwa-ulaya/#respond Fri, 30 Aug 2024 19:18:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11846 Monaco, UfaransaNahodha na winga wa timu ya Al Nassr ya Saudi Arabia, Cristiano Ronaldo amesema kwamba milango bado ipo wazi kwa upande wake kucheza Ligi ya Mabngwa Ulaya kwa mara nyingine.Kauli ya Ronaldo nyota wa zamani wa timu za Man United, Real Madrid na Juventus imekuja baada ya mchezaji huyo kuhusika katika droo ya mfumo […]

The post Ronaldo aitamani Ligi ya Mabingwa Ulaya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Monaco, Ufaransa
Nahodha na winga wa timu ya Al Nassr ya Saudi Arabia, Cristiano Ronaldo amesema kwamba milango bado ipo wazi kwa upande wake kucheza Ligi ya Mabngwa Ulaya kwa mara nyingine.
Kauli ya Ronaldo nyota wa zamani wa timu za Man United, Real Madrid na Juventus imekuja baada ya mchezaji huyo kuhusika katika droo ya mfumo mpya wa michuano hiyo kwa msimu huu wa 2024-25 iliyofanyika jana Alhamisi.
Ronaldo ambaye pia amewahi kuichezea klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno katika tukio hilo pia alipewa tuzo ya kuwa mfungaji mwenye rekodi ya mabao mengi (140) katika historia ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Alipotaniwa na rais wa Umoja wa Vyama vya Soka Ulaya (Uefa), Aleksander Ceferin kwa kutocheza tena Ligi ya Mabingwa, Ronaldo hakufuta moja kwa moja uwezekano wa siku moja kurudi kwenye michuano hiyo.
“Usisahau kwamba nacheza Asia (Ligi ya Mabingwa), kwangu ni furaha kubwa kuwa hapa, asante kwa tuzo hii ya kipekee, ina maana kubwa kwangu,” alisema Ronaldo.

“Kama unavyofahamu, Ligi ya Mabingwa ni michuano ya juu kwenye soka, nimewahi si tu kupata fursa katika michuano hiyo, si wewe tu unayefahamu bali rekodi zinazungumza lakini simaanishi hilo bali namaanisha furaha ya kucheza katika michuano hii, ni hamasa kubwa,” alisema Ronaldo.


Akifafanua uwezekano wa kurudi katika michuano hiyo, Ronaldo ambaye amebeba taji la michuano hiyo mara tano, mara nne na Real Madrid na mara moja na Man United alisema, “katika soka huwezi kujua nini kitatokea, ngoja tuone yajayo yatakavyokuwa.”

The post Ronaldo aitamani Ligi ya Mabingwa Ulaya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/08/30/ronaldo-aitamani-ligi-ya-mabingwa-ulaya/feed/ 0