Azam - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 19 Jul 2023 12:27:54 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Azam - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Bajana asifia mazoezi Azam https://www.greensports.co.tz/2023/07/19/bajana-asifia-mazoezi-azam/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/19/bajana-asifia-mazoezi-azam/#respond Wed, 19 Jul 2023 12:27:30 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7019 Na mwandishi wetuNahodha wa Azam FC, Sospeter Bajana amesema mazoezi na mbinu wanazopewa na kocha mpya wa timu hiyo, Yossoufa Dabo zimekuwa zikiwasuka vilivyo hasa kuelekea michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.Azam ambayo imejichimbia Sousse, Tunisia kwa kambi ya maandalizi ya msimu ujao tayari imeshacheza mechi moja ya kirafiki na Al Hilal, na leo wakitaraji […]

The post Bajana asifia mazoezi Azam first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Nahodha wa Azam FC, Sospeter Bajana amesema mazoezi na mbinu wanazopewa na kocha mpya wa timu hiyo, Yossoufa Dabo zimekuwa zikiwasuka vilivyo hasa kuelekea michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Azam ambayo imejichimbia Sousse, Tunisia kwa kambi ya maandalizi ya msimu ujao tayari imeshacheza mechi moja ya kirafiki na Al Hilal, na leo wakitaraji kuikabili Esperance ya nchini humo.
“Mazoezi ni magumu, kama inavyofahamika mazoezi ya utimamu wa mwili yanahitaji uvumilivu na tumeonesha hilo, tunaomba tuendelee kuwa hivi hivi tuweze kukipata tunachokitaka kuelekea msimu ujao.
“Mazoezi yamekuwa na utofauti kidogo, walimu wapya wanasisitiza zaidi nidhamu na mbinu ambazo wanatuelekeza na sisi tupo tayari kuchukua vitu vyao vipya kwa ajili ya kufanya vizuri tuendako pia tuna michuano mikubwa iliyo mbele yetu,” alisema Bajana.
Alifafanua kuwa michezo yao ya kimataifa pia imekuwa ikiwasaidia mno kuwaweka vizuri ikizingatiwa wanakutana na timu kubwa, hivyo inawajenga vilivyo na inasaidia benchi la ufundi kufahamu mapungufu yao kwa timu kama hizo.

The post Bajana asifia mazoezi Azam first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/19/bajana-asifia-mazoezi-azam/feed/ 0
Azam yajipanga kuiadhibu Namungo https://www.greensports.co.tz/2023/05/13/azam-yajipanga-kuiadhibu-namungo/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/13/azam-yajipanga-kuiadhibu-namungo/#respond Sat, 13 May 2023 20:33:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6157 Na mwandishi wetuKuelekea mechi yao ya kesho ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Namungo, Azam imeleeza kuwa imejiandaa vya kutosha kuhakikisha inaibuka na ushindi ili kutimiza ndoto yao ya kumaliza ligi ndani ya tatu bora.Kocha Msaidizi wa Azam, Aggrey Morris alisema watahakikisha wanapata matokeo kwenye mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es […]

The post Azam yajipanga kuiadhibu Namungo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kuelekea mechi yao ya kesho ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Namungo, Azam imeleeza kuwa imejiandaa vya kutosha kuhakikisha inaibuka na ushindi ili kutimiza ndoto yao ya kumaliza ligi ndani ya tatu bora.
Kocha Msaidizi wa Azam, Aggrey Morris alisema watahakikisha wanapata matokeo kwenye mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam ingawa wanafahamu hiyo ni mechi ngumu kwao kutokana na uzuri wa kikosi cha Namungo.
“Maandalizi yemakamilika, tumewapa wachezaji maelekezo jinsi ya kucheza kutokana na mpinzani alivyo. Lengo ni kushinda mechi kutokana na msimamo wa ligi ulivyo, tunataka ushindi ili kujihakikishia kumaliza nafasi ya tatu, tutakwenda kupambana kupata ushindi,” alisema Aggrey.
Naye kocha wa makipa wa Namungo, Faroukh Ramadhani alisema: “Tumekuja kupambana na Azam, shida yetu ni ushindi na furaha ili tumalize kwenye nafasi ya tano. Tunataka kumaliza kwenye nafasi ya tano, tunahitaji ushindi kuanzia mechi hii na Azam ili tulifanikishe hilo.”
Timu hizo zinakutana, Azam ikiwa imetoka kuifumua Ruvu Shooting mabao 3-1 huku Namungo nayo ikitaka kuendeleza matokeo bora kwenye mechi hizi za mwisho kama ilivyofanya kwenye mechi yake iliyipita kwa kuilazimisha Simba sare ya bao 1-1.
Azam ipo nafasi ya tatu kwa pointi 53 ikihitaji ushindi kuikimbia Singida Big Stars iliyo nafasi ya nne kwa pointi 51, Namungo wapo nafasi ya sita kwa pointi 36 wakiifukuzia Geita Gold iliyo juu yao kwa pointi 37.
Mechi nyingine mbili zitazikutanisha Coastal Union dhidi ya Ihefu na Kagera Sugar itapepetana na Tanzania Prisons.

The post Azam yajipanga kuiadhibu Namungo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/13/azam-yajipanga-kuiadhibu-namungo/feed/ 0
Azam yataja kilichowakwaza NBC Ligi https://www.greensports.co.tz/2023/05/09/azam-yataja-kilichowakwaza-nbc-ligi/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/09/azam-yataja-kilichowakwaza-nbc-ligi/#respond Tue, 09 May 2023 18:47:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6075 Na mwandishi wetuTimu ya Azam imeeleza kuwa kuna mengi yamewakwamisha msimu huu wasifanye vizuri kwenye Ligi Kuu NBC lakini wamefurahi mno kutinga fainali ya Kombe la FA (ASFC).Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdulkarim Amin ‘Popat’ (pichani) amesema matarajio yao yalikuwa mengine kwenye ligi lakini ilipofikia sasa hawana cha kubadili zaidi ya kujipanga kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye […]

The post Azam yataja kilichowakwaza NBC Ligi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Azam imeeleza kuwa kuna mengi yamewakwamisha msimu huu wasifanye vizuri kwenye Ligi Kuu NBC lakini wamefurahi mno kutinga fainali ya Kombe la FA (ASFC).
Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdulkarim Amin ‘Popat’ (pichani) amesema matarajio yao yalikuwa mengine kwenye ligi lakini ilipofikia sasa hawana cha kubadili zaidi ya kujipanga kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye fainali ya Kombe la FA.
Jumapili iliyopita, Azam iliifunga Simba mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Nangwanda, Mtwara na sasa inasubiri mshindi wa mechi ya Singida BS dhidi ya Yanga icheze naye fainali.
Akitaja miongoni mwa sababu zilizowakwamisha kufanya vizuri kwenye ligi na kushindwa kuwania ubingwa licha ya kufanya usajili mzuri, Popat alisema ni kukandamizwa kwenye baadhi ya maamuzi ya mechi za ligi, kukosa matokeo ugenini huku akieleza wamejipanga kuhakikisha wanayamaliza hayo msimu ujao.
“Imeonekana tumesajili vizuri lakini bado tumekwama, kwa hiyo unaweza kupata jibu pamoja na kusajili vizuri lakini bado si suluhisho, Mungu amejaalia mechi imeisha tumeshinda 2-1 lakini tumenyimwa penalti ya wazi kabisa.
“Miaka mingine iliyopita tushafungwa kwenye mstari, mpira unarudishwa ndani tunafungwa, msimu huu pia tumefungwa na mkubwa mwingine mpira unatoka, unarudi ndani unafungwa, hatuna namna nyingine ya kubadilisha hali hiyo.

“Timu za Kariakoo ni kubwa kuliko sisi ndiyo maana tukiwafunga furaha yetu inakuwa kubwa sana, lakini pia timu nyingine tunazokutana nazo wao wanajipanga zaidi kwa kufahamu ni wadogo na sisi ni wakubwa kwa hiyo unakuta zinatusumbua kwenye matokeo,” alisema Popat.


Mtendaji huyo alisema safari hii wamefanya vizuri zaidi kwenye mechi za nyumbani kuliko ugenini hivyo hiyo pia ni sababu inayowaangusha ingawa tayari benchi la ufundi limeanza kulifanyia kazi hilo ili kubadili mwenendo msimu ujao na kufanya vizuri zaidi.
Kwenye ligi Azam inashika nafasi ya tatu kwa pointi 53 ikifuatiwa na Singida BS yenye pointi 51. Yanga SC iko kileleni kwa pointi 71, Simba ni ya pili ikiwa na pointi 64 baada ya timu zote kucheza mechi 27 zikisalia mechi tatu kufungwa rasmi pazia la ligi kuu msimu wa 2022-23.

The post Azam yataja kilichowakwaza NBC Ligi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/09/azam-yataja-kilichowakwaza-nbc-ligi/feed/ 0
Azam yatua fainali FA, yaibwaga Simba https://www.greensports.co.tz/2023/05/07/azam-yatua-fainali-fa-yaibwaga-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/07/azam-yatua-fainali-fa-yaibwaga-simba/#respond Sun, 07 May 2023 15:22:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6049 Na mwandishi wetuPrince Dube ameendelea kuinyanyasa Simba baada ya leo Jumapili kufunga bao la ushindi lililoiwezesha Azam kuilaza Simba mabao 2-1 na kufuzu fainali ya Kombe la Shirikisho Azam (FA) kwa ushindi wa mabao 2-1.Hilo ni bao la tatu kwa Dube kuifunga Simba akiwa tayari ameshainyanyasa timu hiyo mara mbili lakini ushindi wa leo umekuwa […]

The post Azam yatua fainali FA, yaibwaga Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Prince Dube ameendelea kuinyanyasa Simba baada ya leo Jumapili kufunga bao la ushindi lililoiwezesha Azam kuilaza Simba mabao 2-1 na kufuzu fainali ya Kombe la Shirikisho Azam (FA) kwa ushindi wa mabao 2-1.
Hilo ni bao la tatu kwa Dube kuifunga Simba akiwa tayari ameshainyanyasa timu hiyo mara mbili lakini ushindi wa leo umekuwa na maana kubwa kwa timu yake ambayo imepania kubeba taji la michuano hiyo msimu huu.
Kwa ushindi huo uliopatikana kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, Azam sasa inasubiri kwenda kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga kucheza mechi ya fainali dhidi ya mshindi wa mechi ya Yanga na Singida Big Stars.
Azam ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 22 mfungaji akiwa Lusajo Mwaikenda aliyemalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Ayoub Lyanga na kuokolewa na kipa wa Simba, Ally Salim.
Simba hata hivyo walipambana na dakika sita baadaye walifanikiwa kusawazisha bao hilo mfungaji akiwa ni Sadio Kanoute na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.
Mambo yalikwenda kombo kwa Simba katika dakka ya 75 baada ya Dube aliyetokea benchi kuinasa pasi ya kichwa akiwa upande wa kushoto wa Simba na kupiga mpira wa juu uliokwenda moja kwa moja wavuni.
Beki wa Simba, Henock Inonga alijaribu kuuwahi mpira huo huku mshambuliaji wa Azam, Abdul Sopu naye akiwa karibu kabisa na lango ili kumalizia kazi ya Dube kama kungekuwa na ulazima wa kufanya hivyo lakini si Inonga wala Sopu aliyeugusa mpira huo wa juu ambao ulijaa wavuni.
Simba ilipambana ikiwania kusawazisha bao hilo kabla ya kumuingiza mshambuliaji wake mkongwe John Bocco ambaye alifanikiwa kupiga shuti moja kali la mguu wa kushoto ambalo kama si umahiri wa kipa wa Azam Idris Abdoulah mambo yangekuwa mengine.
Simba pia ilipata pigo baada ya Kanoute kulimwa kadi ya pili ya njano na kutoka uwanjani kwa kucheza rafu na hivyo timu hiyo kubaki na wachezaji 10 uwanjani.
Akizungumzia matokeo hayo, kocha msaidizi Simba, Juma Mgunda alisema kwanza wameyakubali lakini pia yamewaamsha na kuwapa nafasi ya kujitathmini ili kuangalia marekebisho ya kufanya katika timu yao.
Naye kocha msaidizi Azam, Kally Ongalla aliwapongeza wachezaji wake kwa kupambana na kupata ushindi huku akisisitiza kwamba bado wana kazi ya kufanya kwani wanalitaka kombe la michuano hiyo ambayo mshindi wake hujikatia moja kwa moja tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

The post Azam yatua fainali FA, yaibwaga Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/07/azam-yatua-fainali-fa-yaibwaga-simba/feed/ 0
Azam: Simba inatuhofia https://www.greensports.co.tz/2023/05/03/azam-simba-inatuhofia/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/03/azam-simba-inatuhofia/#respond Wed, 03 May 2023 16:36:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5997 Na mwandishi wetuTimu ya Azam imesema kuwa Simba ina sababu ya kuwahofia kuelekea mechi yao ya nusu fainali ya Kombe la FA kutokana na rekodi nzuri waliyonayo msimu huu dhidi ya wapinzani wao hao.Simba na Azam zinatarajia kuumana Mei 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.Ofisa Habari wa Azam, Hashim Ibwe alisema kuwa […]

The post Azam: Simba inatuhofia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Azam imesema kuwa Simba ina sababu ya kuwahofia kuelekea mechi yao ya nusu fainali ya Kombe la FA kutokana na rekodi nzuri waliyonayo msimu huu dhidi ya wapinzani wao hao.
Simba na Azam zinatarajia kuumana Mei 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Ofisa Habari wa Azam, Hashim Ibwe alisema kuwa kikosi chao kinaendelea na maandalizi makali kwa ajili ya mchezo huo wakifahamu umuhimu wake na ingawa wana rekodi nzuri dhidi ya Simba msimu huu lakini wanaheshimu upinzani wa Wekundu hao.
“Tunafahamu hatutacheza na timu nyepesi, Simba hivi karibuni wamekuwa na wakat mzuri kwenye kalenda ya kimataifa na kwenye ligi wanashika nafasi ya pili kwahiyo sio mechi rahisi kucheza dhidi yao.

“Japokuwa sisi tuna rekodi nzuri dhidi yao, tuliwafunga mechi ya kwanza ligi kuu na tukatoka nao sare mechi ya pili, Azam ndiyo timu yenye rekodi nzuri zaidi dhidi ya simba msimu huu, hivyo Simba wana sababu ya kutuhofia na sisi pia kuwahofia, pia tunayo sababu ya kuheshimiana kwa hiyo Nangwanda itaamua,” alisema Ibwe.


Mechi ya kwanza baina ya timu hizo kwenye ligi msimu huu, Azam ilishinda kwa bao 1-0 kabla ya sare ya bao 1-1, hivyo mechi ya tatu baina yao inatarajiwa kuwa na upinzani mkali.
Ushindani wa mechi hiyo pia unachangiwa na ukweli kwamba timu hizo zitakuwa zikiwania kutwaa taji ambalo bingwa anakwenda kuiwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.
Mshindi wa mechi hiyo anatarajia kuumana na mshindi wa nusu fainali nyingine itakayozikutanisha Singida Big Stars na Yanga kwenye Uwanja wa Liti, Singida. Fainali itapigwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

The post Azam: Simba inatuhofia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/03/azam-simba-inatuhofia/feed/ 0
Azam, Ruvu Shooting vitani https://www.greensports.co.tz/2023/04/21/azam-ruvu-shooting-vitani/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/21/azam-ruvu-shooting-vitani/#respond Fri, 21 Apr 2023 19:53:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5892 Na mwandishi wetuTimu ya Azam imekiri kuwa na kibarua kigumu kuelekea mchezo wao wa kesho wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Ruvu Shooting, ikikiri ni mchezo mgumu kwao kulingana na mazingira ya timu zote mbili.Kocha Msaidizi wa Azam, Aggrey Morris amesema wanauchukulia mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kwa umakini mkubwa kutokana na nafasi […]

The post Azam, Ruvu Shooting vitani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Azam imekiri kuwa na kibarua kigumu kuelekea mchezo wao wa kesho wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Ruvu Shooting, ikikiri ni mchezo mgumu kwao kulingana na mazingira ya timu zote mbili.
Kocha Msaidizi wa Azam, Aggrey Morris amesema wanauchukulia mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kwa umakini mkubwa kutokana na nafasi iliyopo Ruvu wakitambua namna gani wapinzani wao wanauhitaji ushindi.
“Mchezo tunaocheza na Ruvu ni mchezo tunaouchukulia kwa umakini mkubwa, ukiangalia msimamo ulivyo, siku zote ukicheza na timu ya hali kama hii ndiyo inaogopesha kabisa, hilo tunalijua, tunaiheshimu ni timu ya ushindani, upinzani utakuwa mkubwa lakini tumejipanga kufanya vizuri,” alisema Aggrey.
Azam yenye pointi 50 katika nafasi ya nne, inautafuta ushindi kuipiku Singida BS iliyo nafasi ya tatu kwa pointi 51 wakati Ruvu iliyo nafasi ya 15 kwa pointi 20 inapambana kujinasua isishuke daraja.
Ofisa Habari wa Ruvu, Masau Bwire ameeleza kuwa wanatambua ugumu wa mechi hiyo kutokana na mahitaji ya timu zote mbili lakini mipango yao ni kutumia mechi nne zilizobaki kujinasua na janga la kushuka daraja hivyo anafahamu ugumu utakaokuwepo.
“Azam wanatafuta nafasi ya tatu ili pengine iwe rahisi kushiriki mashindano ya Caf (Shirikisho la Soka Afrika), na sisi tunapambana kuhakikisha tunashinda mechi zilizosalia ili tuendelee kuwepo kwenye ligi msimu ujao na hatuhitaji kupoteza mechi hizi, kuna marekebisho mengi tumefanya kuhakikisha tunasalia,” alisema Bwire.
Katika mechi tano za mwisho za ligi, Azam imeshinda mbili, sare moja na kufungwa mbili wakati Ruvu imeshinda michezo miwili na kufungwa mitatu. Mechi ya kwanza iliyozikutanisha timu hizo msimu huu iliisha kwa sare ya mabao 2-2.
Mechi nyingine ya ligi itakayopigwa kesho itazikutanisha Dodoma Jiji dhidi ya KMC Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Mechi ya kwanza, KMC ilishinda kwa bao 1-0.

The post Azam, Ruvu Shooting vitani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/21/azam-ruvu-shooting-vitani/feed/ 0
Simba, Azam kuvaana Mei 6 https://www.greensports.co.tz/2023/04/20/simba-azam-kuvaana-mei-6/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/20/simba-azam-kuvaana-mei-6/#respond Thu, 20 Apr 2023 20:58:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5886 Na mwandishi wetuRatiba ya mechi za nusu fainali ya Kombe la FA (ASFC) imewekwa wazi leo Alhamisi ambapo mechi ya kwanza kati ya Azam na Simba itapigwa Mei 6, mwaka huu kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.Mechi ya pili ya michuano hiyo imeelezwa kuwa itachezwa Mei 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Liti, Singida baina […]

The post Simba, Azam kuvaana Mei 6 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Ratiba ya mechi za nusu fainali ya Kombe la FA (ASFC) imewekwa wazi leo Alhamisi ambapo mechi ya kwanza kati ya Azam na Simba itapigwa Mei 6, mwaka huu kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Mechi ya pili ya michuano hiyo imeelezwa kuwa itachezwa Mei 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Liti, Singida baina ya mabingwa watetezi, Yanga dhidi ya Singida Big Stars.
Ratiba hiyo iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), pia imeeleza kuwa michezo hiyo yote miwili itapigwa kuanzia saa 9.30 alasiri.
Kwa ratiba hiyo, Yanga sasa itakutana na Singida ndani ya wiki moja baada ya kupangwa kukutana tena Mei 4, mwaka huu kwenye mchezo wa Ligi Kuu NBC huku mechi zote mbili zikipigwa Uwanja wa Liti.
Singida ilitinga hatua hiyo baada ya kuifumua Mbeya City kwa mabao 4-1 wakati Yanga ilikata tiketi hiyo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold.
Simba ambayo itavaana na Azam wiki moja baada ya kumaliza mechi za hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad AC ya Morocco, yenyewe iliingia nusu fainali kwa kuitandika Ihefu mabao 5-1.
Azam ambao ni mabingwa wa michuano hiyo msimu wa 2018-19 wao walipenya nusu fainali baada ya kuibamiza Mtibwa Sugar mabao 2-0.

The post Simba, Azam kuvaana Mei 6 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/20/simba-azam-kuvaana-mei-6/feed/ 0
Kally ataja siri ya ushindi Azam https://www.greensports.co.tz/2023/04/04/kally-ataja-siri-ya-ushindi-azam/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/04/kally-ataja-siri-ya-ushindi-azam/#respond Tue, 04 Apr 2023 19:02:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5685 Na mwandishi wetuKocha Msaidizi wa Azam FC, Kally Ongala amesema siri ya ushindi wao dhidi ya Mtibwa Sugar ni wachezaji wake kuutawala mchezo na kufuata vyema maelekezo aliyowapa .Azam jana iliungana na Singida Big Stars kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la FA (ASFC), baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 2-0 kwenye Uwanja wa […]

The post Kally ataja siri ya ushindi Azam first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Msaidizi wa Azam FC, Kally Ongala amesema siri ya ushindi wao dhidi ya Mtibwa Sugar ni wachezaji wake kuutawala mchezo na kufuata vyema maelekezo aliyowapa .
Azam jana iliungana na Singida Big Stars kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la FA (ASFC), baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Kocha huyo alikiri kuwa timu yake haikucheza vizuri hasa kipindi cha kwanza lakini nidhamu iliyooneshwa na wachezaji wake na ushindi walioupata imemfanya ajisikie furaha.

“Tulicheza pungufu kwa dakika 70 lakini nawapongeza wachezaji wangu kwa kuwaheshimu Mtibwa na kucheza kwa nidhamu muda wote wa dakika 90, naamini pamoja na kuwa pungufu lakini tulistahili kushinda,” alisema Kally.


Kocha huyo ameeleza kuwa baada ya ushindi huo wanarudi kwenye uwanja wa mazoezi kuangalia mapungufu yao ili kuyarekebisha na kujipanga kwa ajili ya mchezo ujao lengo likiwa ni kufanya vizuri na kusonga hatua inayofuata.
Alisema anatambua kuwa hatua inayofuata itakuwa ngumu zaidi lakini dhamira yao msimu huu ni kuwa mabingwa wa Kombe la FA hivyo watajipanga vizuri na kurekebisha mapungufu yao ili kushinda mchezo huo.
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Salum Mayanga ameeleza kuwa kipigo walichokipata kutoka kwa wapinzani wao kimetokana na makosa ambayo waliyafanya ikiwemo kushindwa kutumia faida ya wapinzani wao kuwa pungufu uwanjani.
“Tumepoteza mchezo kwa uzembe wetu wenyewe, tulifanya makosa wenzetu wameyatumia, lakini hata sisi tulitengeneza nafasi tukashindwa kuzitumia kitu ambacho kimetugharimu na kujikuta tunatolewa kwenye mashindano,” alisema Mayanga.
Kocha huyo ameeleza kuwa wamekubali matokeo na wanarudi kujipanga kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya mwaka ujao .

The post Kally ataja siri ya ushindi Azam first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/04/kally-ataja-siri-ya-ushindi-azam/feed/ 0
Kali aomba radhi mashabiki https://www.greensports.co.tz/2023/03/14/kali-aomba-radhi-mashabiki/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/14/kali-aomba-radhi-mashabiki/#respond Tue, 14 Mar 2023 12:42:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5494 Na mwandishi wetuTimu ya Azam imeibuka na kuomba radhi kwa kipigo cha bao 1-0 walichopokea jana Jumatatu dhidi ya Ihefu katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa kwenye Uwanja wa Highland Estates, Mbeya.Kocha Msaidizi wa Azam, Kali Ongalla alisema hajaridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake na kuwataka kujirekebisha ili walichokionesha katika mechi hiyo kisijirudie […]

The post Kali aomba radhi mashabiki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Azam imeibuka na kuomba radhi kwa kipigo cha bao 1-0 walichopokea jana Jumatatu dhidi ya Ihefu katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa kwenye Uwanja wa Highland Estates, Mbeya.
Kocha Msaidizi wa Azam, Kali Ongalla alisema hajaridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake na kuwataka kujirekebisha ili walichokionesha katika mechi hiyo kisijirudie katika mchezo ujao.
Alisema, licha ya matokeo hayo kumuumiza na kumpa majonzi lakini hawana budi kurudi na kujipanga kwa michezo inayokuja ili kufanya vizuri zaidi.
“Wachezaji wangu wamecheza kiwango kibaya sana, yaani hiki tulichokionesha naomba kisijirudie tena, tunahitaji kujirekebisha makosa yasijirudie kiasi hiki, hatukuwa vizuri uwanjani, tylijaribu kufanya mengi ya kimbinu lakini ilishindikana.

“Kiujumla nadhani tulishindwa kufuata mpango wetu mkakati, mwisho wa siku imetuangusha sana, hatukuwa kazini kama ilivyotarajiwa, kwenye kutengeneza nafasi hatukuwa vizuri pia, tunaomba msamaha, mashabiki wetu wanastahili kitu kizuri zaidi,” alisema Ongala.


Naye Kocha wa Ihefu, Zuberi Katwila alisema nidhamu ya wachezaji wake imesaidia wao kupata ushindi ikiwemo kujitahidi kutofanya makosa na mwisho Azam iliingia kwenye mfumo wao ndio maana walifanikiwa.
“Niwapongeze wachezaji kwa kufanya vizuri na kutuwezesha kupata ushindi, makosa hayakuwa mengi, muda wote tulikuwa makini kwa ajili ya kuhakikisha tunapata matokeo na mwisho nidhamu imesaidia kushinda,” alisema.
Ihefu imefanikiwa kuzifunga baadhi ya timu kubwa kama Yanga kwenye uwanja wake wa Highland Estate na sasa imeichapa Azam huku mechi ijayo ikitarajiwa kuumana na Simba.
Timu hiyo ambayo sasa inashika nafasi ya sita kwa pointi 33, pointi moja nyuma ya Geita Gold inayoshika nafasi ya tano, imekuwa ikionesha kiwango bora kwa siku za karibuni ikionekana ni ubora wa kikosi walichoboresha katika dirisha dogo la usajili wa Januari, mwaka huu.
Azam inashikilia nafasi ya nne kwa pointi 47 baada ya mechi 25, ikipambana kumaliza nafasi ya tatu dhidi ya Singida Big Stars wanaoshikilia nafasi hiyo wakiwa na pointi 48.

The post Kali aomba radhi mashabiki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/14/kali-aomba-radhi-mashabiki/feed/ 0
16 bora ASFC kufikia tamati https://www.greensports.co.tz/2023/03/05/16-bora-asfc-kufikia-tamati-leo/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/05/16-bora-asfc-kufikia-tamati-leo/#respond Sun, 05 Mar 2023 10:43:03 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5398 Na mwandishi wetuHatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) inatarajiwa kumalizika leo Jumapili kwa mechi mbili zinazotarajiwa kuchezwa kwenye viwanja viwili vya miji tofauti.Kagera Sugar ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba itawaalika Mbeya City na Azam FC itakuwa mwenyeji wa Mapinduzi ya Mwanza kwenye Uwanja wa Azam […]

The post 16 bora ASFC kufikia tamati first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) inatarajiwa kumalizika leo Jumapili kwa mechi mbili zinazotarajiwa kuchezwa kwenye viwanja viwili vya miji tofauti.
Kagera Sugar ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba itawaalika Mbeya City na Azam FC itakuwa mwenyeji wa Mapinduzi ya Mwanza kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Washindi wa mechi hizo wataungana na timu za Simba, Yanga, Singida Big Stars, Ihefu, Geita Gold na Mtibwa Sugar kwenye hatua ya robo fainali.
Kocha Mkuu wa Kagera, Mecky Maxime alisema wamejiandaa vema na mchezo huo kwani ni muhimu kwao kufuzu robo fainali na wataingia kwa tahadhari kwa sababu Mbeya City si timu ya kubeza.

“Tumejiandaa vema na mchezo na wachezaji wana morali na tutaingia kwa tahadhari uwanjani kwa sababu Mbeya City ina wachezaji bora kama ilivyo kwa kikosi chetu,” alisema Maxime.


Aidha, Kocha Msaidizi wa Mbeya City, Noliega Mwamlima alisema wamejiandaa vya kutosha kwa mchezo huo na tayari wamewasili na kikosi chake Bukoba mapema tayari kwa mchezo huo.
“Tunajua tunacheza na mwenyeji ambaye anajua kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani ila na sisi tumejiandaa vema kuhakikisha tunapata ushindi na kufuzu robo fainali msimu huu,” alisema Mwamlima.
Kwa upande wa kocha msaidizi Azam, Kali Ongala alisema wamejiandaa dhidi ya wapinzani wao kwa kuupa uzito mchezo huo kwa namna unavyostahili licha ya kuwa wanacheza na timu ya daraja la chini.
“Mapinduzi ni mabingwa wa mkoa wa Mwanza na sisi tunajua timu za madaraja ya chini zinajua kung’ang’ania timu kubwa, tumejiandaa kuhakikisha tunashinda, mchezo huu muhimu kwetu,” alisema.
Martin Mahimbo ambaye ni kocha mkuu wa Mapinduzi alisema wamekuja Dar es Salaam kwa kazi moja ya kutafuta ushindi kwani kikosi chake kimeiva na kipo kamili kuivaa Azam FC.
“Tumefika hapa, hatua hii kutokana na kiwango chetu kuwa bora na kesho (leo) tunaenda kuwaonesha Azam kandanda halisi linavyosakatwa, hivyo tunawaomba Wanamwanza waishio Dar es Salaam waje kwa wingi kuwashangilia vijana wao,” alisema.

The post 16 bora ASFC kufikia tamati first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/05/16-bora-asfc-kufikia-tamati-leo/feed/ 0