Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 19 Jul 2026 23:05:29 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Hispania bingwa Kombe la Dunia 2026 https://www.greensports.co.tz/2026/07/20/hispania-bingwa-kombe-la-dunia-2026/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/20/hispania-bingwa-kombe-la-dunia-2026/#respond Sun, 19 Jul 2026 23:05:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14816 New York, MarekaniFerran Torres ameibuka shujaa baada ya kufunga bao pekee na kuiwezesha Hispania kutoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Argentina na kutwaa Kombe la Dunia 2026.Iliwachukua Hispania dakika 106 kupata bao hilo licha ya kuutawala mchezo na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Argentina lakini mashambulizi hayo hayakuweza kuzaa bao kwa dakika 90 […]

The post Hispania bingwa Kombe la Dunia 2026 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Ferran Torres ameibuka shujaa baada ya kufunga bao pekee na kuiwezesha Hispania kutoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Argentina na kutwaa Kombe la Dunia 2026.
Iliwachukua Hispania dakika 106 kupata bao hilo licha ya kuutawala mchezo na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Argentina lakini mashambulizi hayo hayakuweza kuzaa bao kwa dakika 90 za kawaida.
Kikwazo kikubwa kwa Hispania alikuwa kipa wa Argentina, Emilio Martinez ambaye aliokoa michomo kadhaa ya Hispania hadi kumaliza dakika 90 timu hizo zikiwa hazijafungana ndipo zilipoongezwa dakika 30.
Katika dakika 30 za nyongeza Hispania waliendelea kulisakama lango la Argentina huku Argentina wakitumia muda mwingi kujihami kabla hawajaadhibiwa dakika ya 106 na Torres aliyefunga bao kwa shuti kali la mguu wa kushoto.
Bao hilo lilianzia kwa mpira mrefu uliopigwa na Lamine Yamal na kumkuta Nico William ambaye alimuunganishia Torres pasi ya kichwa na Torres kufumua shuti lililomshinda Martinez.
Baada ya kuingia bao hilo, Argentina waliokuwa wamezidiwa kila idara, waliamka na kuanza mashambulizi wakiongozwa na Lionel Messi na kuibua hali ya hofu kwa Hispania.
Messi ambaye alishindwa kuonesha umahiri wake kwa kipindi kirefu, bao la Hispania ni kama lilimpa nguvu ya kuongoza mashambulizi yaliyozaa kona mbili za haraka kwenye lango la Hispania.
Ukiachana na mashambulizi hayo yaliyopamba moto baada ya Argentina kufungwa, kwa dakika zote 120, timu hiyo ilifanikiwa kupiga mashuti mawili tu ya maana langoni mwa Hispania.
Dalili za Hispania kutoka na ushindi zilianza kuonekana mapema kwa namna walivyotawala mchezo na kulisakama lango la Argentina waliokuwa na kazi ya kujihami huku wakishindwa kutengeneza mashambulizi ya maana.
Kasi ya mashambulizi ya Hispania kwenye lango la Argentina ilianza kuonekana mapema dakika za 4 na 5, Lamine Yamal alionesha umahiri lakini mashuti yake mawili yaliishia mikononi mwa kipa Martinez.
Hispania kwa mara nyingine dakika ya 38 ilifanya shambulizi langoni mwa Argentina lakini shuti la chinichini la mguu wa kushoto lililopigwa na Mikel Oyarzabal lilidakwa na kipa Martinez.
Hispania pia mara kadhaa ilifanya mashambulizi yaliyotokea upande wa kushoto kwa beki Cucurella lakini krosi za beki huyo ziliokolewa au kutoka nje ya lango.
MAmbo yalizidi kuwaharibikia Argentina baada ya nyota wao Enzo Fernandes kulimwa kadi ya pili ya njano kwa kucheza rafu na hivyo kutoka uwanjani akiwaacha wenzake 10 kupambana katika dakika 30 za nyongeza.
Hispania ambao mara ya mwisho walilibeba Kombe la Dunia mwaka 2010 katika fainali zilizofanyika nchini Afrika Kusini, pia ndio mabingwa wa Kombe la Ulaya 2024 au Euro 2024.
Fainali za Kombe la Dunia zilianza kutimua vumbi Juni 11, 2026 katika nchi za Canada, Mexico na kuhitimishwa Jumapili, Julai 19, 2026 nchini Marekani kwa mechi iliyopigwa mjini New York kwenye Uwanja wa New Jersey.

The post Hispania bingwa Kombe la Dunia 2026 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/20/hispania-bingwa-kombe-la-dunia-2026/feed/ 0
Kelvin Nashon rasmi mali ya Simba https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/kelvin-nashon-rasmi-mali-ya-simba/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/kelvin-nashon-rasmi-mali-ya-simba/#respond Sun, 19 Jul 2026 14:56:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14813 Na mwandishi wetuBaada ya kuwapo uvumi kuhusu Kelvin Nashon kutua Simba, hatimaye klabu hyo imemtangaza rasmi kiungo huyo kuwa mchezaji wao mpya atakayeitumikia timu hiyo kuanzia msimu mpya wa 2026-27.Taarifa hiyo rasmi imepatikana leo Jumapili Julai 19, 2026 kwenye mitandao ya kijamii ya klabu hiyo ikiambatana na picha ya kumkaribisha kiungo huyo fundi kutoka Pamba […]

The post Kelvin Nashon rasmi mali ya Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Baada ya kuwapo uvumi kuhusu Kelvin Nashon kutua Simba, hatimaye klabu hyo imemtangaza rasmi kiungo huyo kuwa mchezaji wao mpya atakayeitumikia timu hiyo kuanzia msimu mpya wa 2026-27.
Taarifa hiyo rasmi imepatikana leo Jumapili Julai 19, 2026 kwenye mitandao ya kijamii ya klabu hiyo ikiambatana na picha ya kumkaribisha kiungo huyo fundi kutoka Pamba Jiji.
Habari za Kelvin kujiunga na Simba zimekuwapo kwa miezi kadhaa lakini hazikuwa zimethibitishwa na klabu hiyo na hivyo sasa ni rasmi kuanzia msimu ujao nyota huyo ambaye pia amewahi kuichezea Singida Black Stars atavaa jezi ya Simba.
Habari za Simba kumtaka kiungo huyo ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, zilianza kusikika wakati akiwa Singida Black Stars kabla ya kwenda Pamba Jiji, Januari 2025.
Simba ambayo imemaliza Ligi Kuu NBC msimu ulioisha wa 2025-26 ikiwa nafasi ya pili, inaendelea kuimarisha kikosi chake ikiacha baadhi ya wachezaji na kusajili wapya kwa ajili ya msimu mpya wa ligi hiyo na michuano ya kimataifa.
Azam, Yanga nazo zasajili
Wakati Simba ikikamilisha usajili huo Azam FC nao wameendelea kukiimarisha kikosi chao kwa kumsajili winga Henoc Nolia kutoka FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Mitadao ya Azam kuanzia Jumamosi Julai 18, 2026 imepambwa na picha za mchezaji huyo mpya ambaye ataongeza nguvu katika kikosi cha timu hiyo iliyomaliza nafasi ya tatu katika Ligi Kuu NBC msimu wa 2025-26.
Nao mabingwa watetezi wa Ligi Kuu NBC, Yanga wametangaza kumsajili mshambuliaji Juma Issa Abushiri maarufu Chuga Boy kutoka Fountain Gate FC.
Chuga ndiye mchezaji wa kwanza kutambulishwa na Yanga kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa 2026-27.

The post Kelvin Nashon rasmi mali ya Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/kelvin-nashon-rasmi-mali-ya-simba/feed/ 0
England yashika nafasi ya tatu https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/england-yashika-nafasi-ya-tatu/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/england-yashika-nafasi-ya-tatu/#respond Sun, 19 Jul 2026 14:53:40 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14810 Miami, MarekaniEngland imeshika nafasi ya tatu kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 ikiilaza Ufaransa mabao 6-4 huku Jude Bellingham akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kufunga mabao saba katika moja ya Kombe la Dunia.Timu hizo ziliumana katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu Jumamosi Julai 18, 2026 huku mechi ya […]

The post England yashika nafasi ya tatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Miami, Marekani
England imeshika nafasi ya tatu kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 ikiilaza Ufaransa mabao 6-4 huku Jude Bellingham akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kufunga mabao saba katika moja ya Kombe la Dunia.
Timu hizo ziliumana katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu Jumamosi Julai 18, 2026 huku mechi ya fainali kati ya Hispania na Argentina ikisubiriwa kupigwa Jumapili Julai 19, 2026.
Bellingham ambaye pia ni kiungo wa Real Madrid, awali alifungana na nahodha na mshambuliaji wa England, Harry Kane aliyefunga mabao sita katika fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
Rekodi kama hiyo ya mabao sita kabla ya hapo ilikuwa ikishikiliwa na Garry Lineker aliyeifungia England idadi mabao kama hiyo ya mabao kwenye fainali za Kombe la Dunia 1986 nchini Mexico.
Katika mechi dhidi ya Ufaransa, Bellingham, 23, aliingizwa uwanjani dakika ya 79 na kufunga bao lililotokana na shambulizi la kushtukiza.
Dakika 12 kabla ya hapo alikuwa afunge bao kwa mkwaju wa penalti lakini akaamua kumpa nafasi hiyo Bukayo Saka ambaye hakumuangusha, aliitumia vyema penalti hiyo kuipatia England bao.
Saka hata hivyo baada ya mechi alisema kwamba ni Bellingham ndiye aliyemwambia aende akapige mpira huo wa penalti ili apate hat trick (mabao matatu).
Katika mechi hiyo mbali na Bellingham, mabao mengine ya England yalifungwa na Declan Rice dakika ya tatu, Konsa dakika ya 18 na Saka ambaye alifunga dakika za 37, 45 na 87.
Mabao ya Ufaransa yalifungwa na Kylian Mbappe aliyefunga mawili dakika za 48 na 66 wakati mengine mawili yalifungwa na Barcola dakika ya 54 na Dembele dakika ya 90.

The post England yashika nafasi ya tatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/england-yashika-nafasi-ya-tatu/feed/ 0
Chasambi aachwa Simba https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/chasambi-aachwa-simba/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/chasambi-aachwa-simba/#respond Sun, 19 Jul 2026 11:34:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14807 Na mwandishi wetuKlabu ya soka ya Simba imetangaza kuachanana winga wake Ladack Chasambi ambaye sasa ni rasmi hatokuwa na timu hiyo kwa msimu ujao wa 2026-27.Taarifa iliyopatikana Jumamosi Julai 18, 2026 kwenye vyanzo vya habari vya klabu hiyo, imemtaja mchezaji huyo kuwa mmoja wa wachezaji ambao wamepewa nafasi ya kutafuta maisha nje ya Simba.Chasambi alijiunga […]

The post Chasambi aachwa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya soka ya Simba imetangaza kuachanana winga wake Ladack Chasambi ambaye sasa ni rasmi hatokuwa na timu hiyo kwa msimu ujao wa 2026-27.
Taarifa iliyopatikana Jumamosi Julai 18, 2026 kwenye vyanzo vya habari vya klabu hiyo, imemtaja mchezaji huyo kuwa mmoja wa wachezaji ambao wamepewa nafasi ya kutafuta maisha nje ya Simba.
Chasambi alijiunga na Simba Januari 2024 akitokea Mtibwa Sugar ambapo alipandishwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo baada ya kuonesha uwezo wake kwenye timu ya vijana kabla ya Simba kuvutiwa naye.
Alisajiliwa na Simba wakati huo ikiwa chini ya kocha Abdelhak Benchikha akitajwa kuwa mmoja wa wachezaji waliopewa matumaini makubwa ya kutamba kutokana na uwezo alioanza kuuonesha.
Hali hata hivyo imekuwa tofauti kwa mchezaji huyo ambaye hatimaye Simba imetangaza rasmi kuachana naye.
Chasambi sasa anaungana na mshambuliaji wa timu hiyo, Jonathan Sowah ambaye naye alitangaza kuachwa baada ya kuichezea timu hiyo kwa msimu mmoja tu akitokea Singida Black Stars.
Mchezaji mwingine ambaye Simba imetangaza kuachana naye hivi karibuni ni kiungo mkongwe, Muzamir Yassin ambaye amekuwa na timu hiyo akicheza kwa mafanikio kwa takriban miaka 10.

The post Chasambi aachwa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/chasambi-aachwa-simba/feed/ 0
Trump naye amlaumu Tuchel https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/trump-naye-amlaumu-tuchel/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/trump-naye-amlaumu-tuchel/#respond Sun, 19 Jul 2026 11:32:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14805 New York, MarekaniRais wa Marekani, Donald Trump naye ameibuka na kumlaumu kocha wa England, Thomas Tuchel kwa mbinu alizotumia katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Argentina.Katika hoja yake hiyo, Trump kwa kiasi kikubwa amehoji majukumu ya ulinzi ambayo Thuchel alimpa mshambuliaji wa timu hiyo, Harry Kane hasa katika kipindi cha […]

The post Trump naye amlaumu Tuchel first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Rais wa Marekani, Donald Trump naye ameibuka na kumlaumu kocha wa England, Thomas Tuchel kwa mbinu alizotumia katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Argentina.
Katika hoja yake hiyo, Trump kwa kiasi kikubwa amehoji majukumu ya ulinzi ambayo Thuchel alimpa mshambuliaji wa timu hiyo, Harry Kane hasa katika kipindi cha pili.
Tuchel ameshutumiwa baada ya England kufungwa mabao 2-1 na Argentina na kutolewa katika hatua ya nusu ya fainali ingawa bado anaungwa mkono na mabosi wa Chama cha Soka England na inaaminika ndiye atakayeiongoza timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Ulaya 2028 au Euro 2028.
England walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Anthony Gordon dakika ya 55 na baada ya hapo Tuchel alijaza mabeki sita nyuma lakini Argentina walimzidi ujanja na kufunga mabao mawili dakika za 85 na 92 (90+2).
Akitoa hoja yake dhidi ya mbinu za Tuchel, Trump awali alianza kwa kumsifia Kane na kukumbushia walivyowahi kucheza naye golfu kwenye ufukwe wa West Palm takriban miezi 18 iliyopita.

“England mna mchezaji mzuri, mchezaji ambaye niliwahi kucheza naye golfu, mnamjua huyo? ni Harry ambaye amekuwa mchezaji mahiri, nafikiri walikosea kumfanya awe mchezaji wa ulinzi,” alisema Trump.

Trump alifafanua akisema kilichotokea ni kwamba England walipata bao la kuongoza na baada ya hapo walichofanya ni kumchukua mchezaji wao bora na kumuweka katika eneo la ulinzi.

The post Trump naye amlaumu Tuchel first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/trump-naye-amlaumu-tuchel/feed/ 0
Tuchel ajitetea baada ya England kutolewa https://www.greensports.co.tz/2026/07/18/tuchel-ajitetea-baada-ya-england-kutolewa/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/18/tuchel-ajitetea-baada-ya-england-kutolewa/#respond Sat, 18 Jul 2026 19:34:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14802 Miami, MarekaniKocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Thomas Tuchel ametetea maamuzi yake katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Argentina licha ya timu hiyo kushindwa.Akizungumza kabla ya mechi ya kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Ufaransa, kocha huyo Mjerumani alisema kama anahitajika mtu wa kulaumiwa basi yeye yuko […]

The post Tuchel ajitetea baada ya England kutolewa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Miami, Marekani
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Thomas Tuchel ametetea maamuzi yake katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Argentina licha ya timu hiyo kushindwa.
Akizungumza kabla ya mechi ya kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Ufaransa, kocha huyo Mjerumani alisema kama anahitajika mtu wa kulaumiwa basi yeye yuko tayari kubeba zigo la lawama.
Tuchel hata hivyo alisema hana cha kujutia na kuongeza kuwa timu yake ndiyo iliyoumizwa zaidi kuliko yeyote na kwamba kilichotokea ni jeraha ambalo wanalazimika kulibeba.
Katika mechi hiyo, England walikuwa wakipambana kuweka rekodi ya kufikia hatua ya fainali ya Kombe la Dunia mara ya kwanza tangu kufanya hivyo mara ya mwisho mwaka 1966, miaka 60 iliyopita.
Kilichotokea katika mechi hiyo kiliiumiza mno England kwani baada ya kuongoza kwa bao 1-0 mambo yalibadilika mwishoni na kujikuta wakilala kwa mabao 2-1 huku wakipigwa presha na Messi.
Mabao ya Argentina yaliyopatikana dakika za 85 na 90 (+2) yaliwaumiza mno mashabiki wa England huku baadhi ya wachambuzi wakilaumu maamuzi kadhaa ya Tuchel ikiwamo kujihami zaidi badala ya kushambulia.
Alipoulizwa ni kwa nini timu yake ilicheza kwa kujihami zaidi Tuchel alisema hicho ndicho kilichotakiwa kufanywa kwa namna Argentina walivyokuwa na hajutii uamuzi wake katika hilo.

“Nilichukua maamuzi mengi, niliamini fikra zangu, uzoefu wangu, niliamini katika upambanaji wangu na nilichukua maamuzi kwa lengo la kuisaidia timu kupata matokeo lakini hatukupata matokeo,” alisema Tuchel.


England inacheza mechi ya kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Ufaransa, mechi itakayopigwa Jumamosi Julai 18, 2026 wakati mechi ya fainali kati ya Argentina na Hispania itapigwa Jumapili Julai 19, 2026.

The post Tuchel ajitetea baada ya England kutolewa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/18/tuchel-ajitetea-baada-ya-england-kutolewa/feed/ 0
Serengeti Boys wapewa Sh milioni 500 https://www.greensports.co.tz/2026/07/15/serengeti-boys-wapewa-sh-milioni-500/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/15/serengeti-boys-wapewa-sh-milioni-500/#respond Wed, 15 Jul 2026 19:38:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14800 Na mwandishi wetuSerikali imetekeleza ahadi ya zawadi ya fedha kwa timu za vijana chini ya miaka 17 au Serengeti Boys na wasichana chini ya miaka 20 maaufu Tanzanite Queens kutokana na mafanikio waliyoyapata.Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyopatikana leo Jumatano Julai 15, 2026 ilieleza kuwa Serengeti Boys wamepewa zawadi yao ya Sh milioni […]

The post Serengeti Boys wapewa Sh milioni 500 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Serikali imetekeleza ahadi ya zawadi ya fedha kwa timu za vijana chini ya miaka 17 au Serengeti Boys na wasichana chini ya miaka 20 maaufu Tanzanite Queens kutokana na mafanikio waliyoyapata.
Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyopatikana leo Jumatano Julai 15, 2026 ilieleza kuwa Serengeti Boys wamepewa zawadi yao ya Sh milioni 500 na Tanzanite Queens wamepewa zawadi ya Sh milioni 50.
Serengeti Boys imefuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Qatar na timu hiyo pia ilifanikiwa kucheza hatua ya fainali ya Afcon dhidi ya Senegal lakini ilishindwa kubeba taji.
Kwa upande wa Tanzanite Queens wao wamefuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia ambazo zimepangwa kufanyika Septemba mwaka huu nchini Poland.
TFF katika taarifa hiyo waliishukuru serikali kwa kutekeleza ahadi ya zawadi hiyo ambayo wanaamini ilikuwa motisha kwa timu hizo.

The post Serengeti Boys wapewa Sh milioni 500 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/15/serengeti-boys-wapewa-sh-milioni-500/feed/ 0
Mbappe ahoji mbinu za Deschamps https://www.greensports.co.tz/2026/07/15/mbappe-ahoji-mbinu-za-deschamps/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/15/mbappe-ahoji-mbinu-za-deschamps/#respond Wed, 15 Jul 2026 19:36:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14798 Arlington, TexasNahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe inaonekana hajakubaliana na mbinu za kocha wa timu hiyo, Didier Deschamps katika mechi yao ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Hispania.Ufaransa iliumana na Hispania Jumanne Julai 14, 2026 na kulala kwa mabao 2-0 na hivyo kuinyima timu hiyo rekodi […]

The post Mbappe ahoji mbinu za Deschamps first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Arlington, Texas
Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe inaonekana hajakubaliana na mbinu za kocha wa timu hiyo, Didier Deschamps katika mechi yao ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Hispania.
Ufaransa iliumana na Hispania Jumanne Julai 14, 2026 na kulala kwa mabao 2-0 na hivyo kuinyima timu hiyo rekodi ya kufuzu hatua ya fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya tatu mfululizo.
Mbappe ameifungia Ufaransa mabao manane katika fainali hizo na sasa anasubiri mechi ya kusaka mshindi wa tatu itakayopigwa Jumamosi Julai 18, 2026 dhidi ya England au Argentina.
Idadi hiyo ya mabao ya Mbappe ni sawa na yale aliyofunga miaka minne iliyopita katika fainali za Kombe la Dunia za Qatar 2022 ambapo timu hiyo ilifikia hatua ya fainali na kupoteza kwa mikwaju ya penalti mbele ya Argentina.
Akifafanua zaidi kuhusu mechi yao na Hispania ilivyokuwa Mbappe alisema kwamba timu ilzidiwa na kutaja eneo la kiungo ambalo alisema Hispania walionekana kuwa wengi.

“Katika mechi na Hispania katikati ilikuwa watatu dhidi ya wawili, hapo kuna ugumu na Fabian (Ruiz) na Rodri walikuwa na fursa ya kujidai, nafikiri ilipaswa kuwa mtu na mtu, kuwalazimisha wakimbizane na sisi,” alisema Mbappe.


Mbappe alisema Ufaransa hawakucheza mchezo walioutaka kimbinu na kiufundi na ndio maana walishindwa kwa sababu hawakufanya kilichotakiwa kufanywa katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia.
Kwa upande mwingine alisema Hispania waliheshimu aina yao ya uchezaji na kile wanachokifanya siku zote yaani kupenda kumiliki mipira na kuwa na kasi na mbinu ya Ufaransa ilitakiwa ya kuwabana ili wasiwe katika aina yao ya uchezaji.
Mbappe pia aliwalaumu wachezaji wenzake hasa walipofanya kosa na Hispania wakafanikiwa kuupata mpira na hata ilipotokea wakaupata bado hawakuwa katika ubora na hilo likasababisha wafungwe.
Deschamps ambaye ameachana na Ufaransa, ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo iliyobeba Kombe la Dunia mwaka 1998, akiwa kocha pia ameweka rekodi kwa kubeba Kombe la Dunia na timu hiyo mwaka 2018.
Nafasi ya Deschamps inatajwa kuchukuliwa na Zinedine Zidane au Zizou, mchezaji mwenzake wa zamani ambaye walikuwa pamoja katika kikosi cha Ufaransa kilichobeba Kombe la Dunia mwaka 1998.

The post Mbappe ahoji mbinu za Deschamps first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/15/mbappe-ahoji-mbinu-za-deschamps/feed/ 0
Azam yapigwa faini milioni 50 https://www.greensports.co.tz/2026/07/13/azam-yapigwa-faini-milioni-50/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/13/azam-yapigwa-faini-milioni-50/#respond Mon, 13 Jul 2026 20:05:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14795 Na mwandishi wetuAzam FC imetozwa faini ya Sh milioni 50 na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kosa la kususia sherehe za kukabidhiwa tuzo na zawadi za washindi wa Kombe la Shirikisho CRDB.Azam na Simba ziliumana katika mechi ya fainali ya michuano hiyo, mechi iliyopigwa Julai 4, 2026 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba na Simba […]

The post Azam yapigwa faini milioni 50 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Azam FC imetozwa faini ya Sh milioni 50 na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kosa la kususia sherehe za kukabidhiwa tuzo na zawadi za washindi wa Kombe la Shirikisho CRDB.
Azam na Simba ziliumana katika mechi ya fainali ya michuano hiyo, mechi iliyopigwa Julai 4, 2026 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba na Simba kutoka na ushindi wa bao 1-0.
Taarifa ya TFF iliyopatikana Jumatatu Julai 13, 2026 ilieleza kuwa adhabu hiyo imetokana na kikao cha kamati ya mashindano ya TFF, kilichokutana na kupitia taarifa za mechi hiyo ya fainali ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Benki ya CRDB.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Azam walisusia sherehe za kukabidhi zawadi na tuzo hizo, sherehe ambazo zilifanyika mara baada ya mechi hiyo kwa kilichodaiwa kuwa ni kutoridhishwa na maamuzi mbalimbali.
Kamati hiyo pia imemtoza faini ya Sh milioni mbili na kumfungia mechi nne, kocha wa makipa wa Azam, Roudy Mountaro kwa kosa la kumshambulia mwamuzi wa mchezo huo mara baada ya mechi kumalizika.
Kipa wa Azam, Zubeir Foba yeye amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya Sh milioni mbili kwa kosa la kumshambulia mwamuzi baada ya mechi kumalizika.
Kamati hiyo pia imewapeleka kwenye kamati ya nidhamu ya TFF, kiongozi wa Azam, Jamal Salum Mohamed na ofisa wa klabu ya Simba, Ally Shatry kwa kuhusika na vitendo vya utovu wa nidhamu.

The post Azam yapigwa faini milioni 50 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/13/azam-yapigwa-faini-milioni-50/feed/ 0
Viní Jr awaomba radhi mashabiki Brazil https://www.greensports.co.tz/2026/07/13/vini-jr-awaomba-radhi-mashabiki-brazil/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/13/vini-jr-awaomba-radhi-mashabiki-brazil/#respond Mon, 13 Jul 2026 19:58:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14793 Rio de Janeiro, BrazilMshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil, Vinícius Junior ‘Vini Jr’ amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo baada ya kutolewa na Norway kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 hatua ya 16 bora.Umahiri na ubora wa mshambuliaji wa Man City, Erling Haaland ulitosha kuwatoa mashindanoni, Brazil wakiwa chini ya kocha mkongwe, Carlo […]

The post Viní Jr awaomba radhi mashabiki Brazil first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rio de Janeiro, Brazil
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil, Vinícius Junior ‘Vini Jr’ amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo baada ya kutolewa na Norway kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 hatua ya 16 bora.
Umahiri na ubora wa mshambuliaji wa Man City, Erling Haaland ulitosha kuwatoa mashindanoni, Brazil wakiwa chini ya kocha mkongwe, Carlo Ancelotti.
Brazil imeingia katika mechi hiyo ikiwa na tatizo la mastaa wake wa safu ya ushambuliaji kuwa majeruhi kina Rodrigo na Estevao huku mastaa wengine kina Raphinha na Lucas Paqueta kukwama mapema.
Inaaminika kuwa hali hiyo ilimuweka katika wakati mgumu Vinicius akiaminiwa kuipa mafanikio Brazil lakini aliishia kuifungia mabao manne na kutoa asisti moja katika mechi tano za timu hiyo.

“Ni takriban miaka minne baadaye najikuta katika kufikiria nini cha kuandika kwa mara nyingine baada ya mambo kuwa mabaya kwenye fainali za Kombe la Dunia,” alisema Vini.


Vini alisema kuwa amekuwa akiwaona watu wengi wa rika tofauti wakimuunga mkono na kushikamana na ndoto yao na isingekuwa sahihi kwake kukaa kimya ingawa alihitaji siku kadhaa za kutafakari.
Alisema kwamba kuvaa jezi ya timu ya taifa ni jambo kubwa na la kujivunia katika maisha yake na kutolewa katika fainali za Kombe la Dunia katika hatua ya 16 bora ni jambo gumu kulielezea.
Kutolewa kwa Brazil katika fainali hizo hata hivyo hakujawa sababu ya viongozi wa shirikisho la soka nchini humo kubadili msimamo kuhusu kuendelea kufanya kazi na kocha Carlo Ancelotti.
Kwa mantiki hiyo, Ancelotti, kocha wa zamani wa Real Madrid na kocha wa kwanza wa kigeni kuinoa timu ya Brazil ataendelea kuwa na timu hiyo.

The post Viní Jr awaomba radhi mashabiki Brazil first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/13/vini-jr-awaomba-radhi-mashabiki-brazil/feed/ 0