GreenSports - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 22 Feb 2024 07:55:44 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg GreenSports - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mazingira kipaumbele cha Ujerumani Euro 2024 https://www.greensports.co.tz/2024/02/22/mazingira-kipaumbele-cha-ujerumani-euro-2024/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/22/mazingira-kipaumbele-cha-ujerumani-euro-2024/#respond Thu, 22 Feb 2024 07:55:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9843 Berlin, UjerumaniUjerumani ndiye mwenyeji wa fainali za soka za Kombe la Ulaya 2024 au Euro 2024, nchi hiyo imeamua fainali hizo hazitoishia kwenye soka tu, bali suala la utunzaji mazingira nalo limepewa kipaumbele.Habari ya hivi karibuni ya DW imeeleza kuwa wanamazingira nchini humo wamepongeza mpango huo unaosimamiwa na Shirikisho la Soka Ujerumani (DFD) kwa kushirikiana […]

The post Mazingira kipaumbele cha Ujerumani Euro 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Berlin, Ujerumani
Ujerumani ndiye mwenyeji wa fainali za soka za Kombe la Ulaya 2024 au Euro 2024, nchi hiyo imeamua fainali hizo hazitoishia kwenye soka tu, bali suala la utunzaji mazingira nalo limepewa kipaumbele.
Habari ya hivi karibuni ya DW imeeleza kuwa wanamazingira nchini humo wamepongeza mpango huo unaosimamiwa na Shirikisho la Soka Ujerumani (DFD) kwa kushirikiana na Umoja wa Vyama vya Soka Ulaya (Uefa) ingawa wamesisitiza mkazo zaidi katika suala hilo.
Katika kulifanyia kazi jambo hilo wenyeji wametoa vipeperushi vyenye kauli mbiu ya Msimamo Mmoja wa Mazingira Endelevu katika Uefa Euro 2024, michuano itakayoanza Juni 14 na kufikia ukomo Julai 14, 2024.
Moja ya hatua zinazofanyiwa kazi na wenyeji wa Euro 2024 ni kuweka mazingira ya kuzuia ongezeko la hewa ukaa ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira na kusababisha mabadiliko ya tabia nchi.
Katika hilo wenyeji wanaanda mpango wa usafiri wa umma kwenye miji yote ambayo ina viwanja vitakavyotumika kwa fainali hizo huku magari ya umeme na baiskeli pia vikitajwa kuwa ni aina ya usafiri unaotumiwa nchini Ujerumani na utasaidia katika hilo.


Zaidi ya hilo viwanja vyote 10 ambavyo vitatumika kwa mechi za fainali za Euro 2024, umeme wake utakuwa ni ule wa nishati jadidifu (renewable energy) nishati ambayo imekuwa ikihimizwa na wanamazingira dunaini kote kwa kuwa ni nishati salama kwa mazingira.
Mpango mwingine wa wenyeji katika utunzaji mazingira ni kudhibiti takataka za vyakula na nyinginezo kutokana na ugeni ambao utakuwa nchini Ujerumani kwa kipindi chote cha fainali hizo.
Katika hilo mpango uliopo ni kuwa na matumizi ya vifaa sahihi vya kubebea chakula vinavyoweza kutumika zaidi ya mara moja badala ya vile vinavyotumika mara moja na kutupwa.
Akiupongeza mpango huo, mkuu wa idara ya huduma ya Mazingira, Thomas Fischer alisema anaamini Ujerumani ambayo aliitaja kuwa ni nchi ya soka ina fursa nzuri za kuandaa fainali za Euro za kipekee na za mfano kwa wakati wote zitakazojali utunzaji mazingira.
Fischer pia alisema kwamba wanamazingira wangependa kuona viwanja vinakuwa na sehemu kubwa ya maegesho ya baiskeli na kuzuia magari viwanjani huku akitaka timu ya taifa ya Ujerumani iwe mfano kwa kuachana na usafiri wa ndege badala yake watumie treni.

The post Mazingira kipaumbele cha Ujerumani Euro 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/22/mazingira-kipaumbele-cha-ujerumani-euro-2024/feed/ 0
Olimpiki Paris wapania kupunguza hewa ukaa https://www.greensports.co.tz/2023/12/28/olimpiki-paris-wapania-kupunguza-hewa-ukaa/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/28/olimpiki-paris-wapania-kupunguza-hewa-ukaa/#respond Thu, 28 Dec 2023 14:10:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9042 Paris, UfaransaWenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 wameahidi kuifanya michezo hiyo kuwa ya mfano wa kipekee katika kuhakikisha haihusishi uharibifu wa mazingira ikiwamo kupunguza kiwango cha hewa ukaa kwa asilimia 50.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Paris 2024, Tony Estanguet amesema kwamba Michezo ya Olimpiki mwakani itakuwa mfano mpya wa kipekee katika kuandaa michezo ya […]

The post Olimpiki Paris wapania kupunguza hewa ukaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Paris, Ufaransa
Wenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 wameahidi kuifanya michezo hiyo kuwa ya mfano wa kipekee katika kuhakikisha haihusishi uharibifu wa mazingira ikiwamo kupunguza kiwango cha hewa ukaa kwa asilimia 50.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Paris 2024, Tony Estanguet amesema kwamba Michezo ya Olimpiki mwakani itakuwa mfano mpya wa kipekee katika kuandaa michezo ya aina hiyo duniani kote.
Estanguet alinukuliwa na BBC akisema kwamba Paris inataka kuwa mfano wa sehemu nyingine duniani katika kuandaa Michezo ya Olimpiki katika namna ambayo mazingira yatalindwa.

“Tunataka kudhihirisha kwamba Paris na Ufaransa wanaweza kuwa wenyeji wa michezo ambayo itakuwa katika namna tofauti na ambavyo imekuwa ikifanyika siku za nyuma” alisema Estanguet katika mazungumzo yake na BBC.


Michezo ya Olimiki itafanyika kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11 mwakani katika jiji la Paris na kufuatiwa na Michezo ya Olimpiki Maalum au Paralympics inayohusisha walemavu wa viungo ambayo itafanyika kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 8.
Moja ya malengo ya waandaji ni kuhakikisha kunakuwa na mpango maalum wenye nia ya kupunguza hewa ukaa kwa asilimia 50 zaidi ya ilivyokuwa katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2012 na 2016.
Paris hata hivyo wana kazi kubwa ya kufikia malengo hayo hasa baada ya Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020 ambayo ilifanyika mwaka 2021 ambayo iliweka rekodi kwa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza kiwango cha hewa ukaa.
Tafiti hata hivyo zilionesha kwamba Tokyo walifanikiwa kwa sababu ya ugonjwa wa korona ambao kwanza ulisababisha michezo hiyo kufanyika mwaka 2021 badala ya 2022 lakini pia ugonjwa huo ulisababisha mashabiki na hata washiriki kuwa wachache kutokana na zuio la kusafiri.
Michezo ya Olimpiki ni aina ya tamasha kubwa la michezo duniani linaloongoza duniani kwa kushirikisha michezo na wanamichezo wengi kutoka mataifa karibu yote duniani.

The post Olimpiki Paris wapania kupunguza hewa ukaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/28/olimpiki-paris-wapania-kupunguza-hewa-ukaa/feed/ 0
Roger Milla ageukia ujasiriamali, utunzaji mazingira https://www.greensports.co.tz/2023/12/22/roger-milla-ageukia-ujasiriamali-utunzaji-mazingira/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/22/roger-milla-ageukia-ujasiriamali-utunzaji-mazingira/#respond Fri, 22 Dec 2023 16:32:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8980 Yaounde, CameroonMshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon, Roger Milla ameigeukia biashara ya utunzaji na usafi wa mazingira kwa kukusanya taka za plastiki, kuzirudisha kiwandani na kuzalisha vitofali na bidhaa nyingine.Lengo la mradi huo wa Roger Milla ni kupunguza takataka za plastiki mitaani ambazo pia zinachangia uharibifu wa mazingira na kusababisha mafuriko pamoja […]

The post Roger Milla ageukia ujasiriamali, utunzaji mazingira first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Yaounde, Cameroon
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon, Roger Milla ameigeukia biashara ya utunzaji na usafi wa mazingira kwa kukusanya taka za plastiki, kuzirudisha kiwandani na kuzalisha vitofali na bidhaa nyingine.
Lengo la mradi huo wa Roger Milla ni kupunguza takataka za plastiki mitaani ambazo pia zinachangia uharibifu wa mazingira na kusababisha mafuriko pamoja na kutoa ajira kwa vijana.
Cameroon ni nchi mojawapo inayoathiriwa kwa kiasi kikubwa na mafuriko sababu mojawapo ikiwa ni mvua lakini pia kuwapo kwa taka za plastiki zinazoziba mifereji hivyo mradi huo unatajwa kusaidia kupunguza tatizo la mafuriko.
Mradi huo upo katika jiji la Yaounde tangu mwaka 2017 na umeajiri vijana zaidi ya 700 ambazo si ajira rasmi lakini wapo wengine zaidi ya 20 wenye ajira za kudumu na hadi sasa tayari wamekusanya tani zaidi ya 50 za takataka za plastiki.
Baada ya jiji la Yaounde, Roger Milla yuko katika hatua za mwisho za kufungua mradi kama huo katika jiji la Douala na baada ya hapo mpango wake ni kufungua mradi huo nje ya Cameroon katika nchi za Benin na Burkina Faso huku lengo likiwa ni kuajiri vijana zaidi ya 2,500.
Roger Milla anakumbukwa kwa kuiwakilisha Cameroon kwenye fainali za soka za Kombe la Dunia mwaka 1990 na kuifungia mabao manne yaliyoiwezesha timu hiyo kuweka rekodi ya kuwa nchi ya kwanza ya Afrika kufikia hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia.
Wakati Roger Milla akiweka rekodi hiyo alikuwa na miaka 38 na miaka minne baadaye wakati huo akiwa na miaka 42 pia aliitwa kwenye timu ya taifa ya Cameroon iliyofuzu na kushiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Marekani.
Roger Milla mbali na kuweka rekodi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mara mbili akiwa na umri mkubwa, anakumbukwa kwa namna alivyokuwa akishangilia bao alilofunga kwa kwenda kwenye kibendera na kukata mauno.

The post Roger Milla ageukia ujasiriamali, utunzaji mazingira first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/22/roger-milla-ageukia-ujasiriamali-utunzaji-mazingira/feed/ 0
Ihefu kinara Sao Hill Bonanza 2023 https://www.greensports.co.tz/2023/12/18/ihefu-yangara-sao-hill-bonanza-2023/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/18/ihefu-yangara-sao-hill-bonanza-2023/#respond Mon, 18 Dec 2023 20:37:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8922 Na mwandishi wetuTimu ya soka ya Ihefu imeibuka mashindi wa soka wa bonanza la michezo la Misitu ya Sao Hill lililofanyika kuanzia Desemba 9 mwaka huu na kufikia tamati mwishoni mwa wiki kwenye Shamba la Miti la Sao Hill wilayani Mufindi.Katika mechi ya soka ya kufunga Bonanza hilo ambayo ilivuta hisia za mashabiki wengi, vinara […]

The post Ihefu kinara Sao Hill Bonanza 2023 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya soka ya Ihefu imeibuka mashindi wa soka wa bonanza la michezo la Misitu ya Sao Hill lililofanyika kuanzia Desemba 9 mwaka huu na kufikia tamati mwishoni mwa wiki kwenye Shamba la Miti la Sao Hill wilayani Mufindi.
Katika mechi ya soka ya kufunga Bonanza hilo ambayo ilivuta hisia za mashabiki wengi, vinara Ihefu waliibwaga Mgololo Misitu kwa penalti 4-3 baada ya sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida.
Kwa ushindi huo, Ihefu wanakuwa wametetea vyema taji hilo ambalo pia walilibeba katika mashindano hayo kwa msimu uliopita.
Mbali na soka, Bonanza hilo pia lilishirikisha michezo mbalimbali ikiwamo kuvuta kamba, kukimbia kwenye magunia, kucheza draft na bao, riadha mbio ndefu na fupi, mpira wa wavu na netiboli na washindi kupewa zawadi mbalimbali.
Bonanza hilo la kila mwaka na ambalo linafanyika kwa mara ya tisa sasa kwenye shamba la misitu la Sao Hill, lengo lake ni kuhimiza upandaji miti na kuimarisha ujirani mwema.
Bonanza hilo limeendelea kuwa mfano halisi wa kutumia michezo na burudani kuhamasisha upandaji miti, kauli mbiu yake inasema: ‘Panda miti kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.’

The post Ihefu kinara Sao Hill Bonanza 2023 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/18/ihefu-yangara-sao-hill-bonanza-2023/feed/ 0
Wanamazingira wavamia mashindano ya tenisi https://www.greensports.co.tz/2023/07/06/wanamazingira-wavuruga-mashindano-ya-tenisi/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/06/wanamazingira-wavuruga-mashindano-ya-tenisi/#respond Thu, 06 Jul 2023 20:45:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6832 London, EnglandWanaharakati za mazingira wa kundi la Just Stop Oil jana Jumatano waliandamana na kufanya vurugu kwenye mashindano ya tenisi ya Wimbledon kwa kuvamia sehemu ya kuchezea na kutupa maganda ya machungwa.Tukio la kwanza la wanamazingira hao lilitokea wakati wa mechi kati ya Sho Shimabukuro na Grigor Dimitrov hali iliyosababisha mechi hiyo kusimama kwa muda.Katika […]

The post Wanamazingira wavamia mashindano ya tenisi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Wanaharakati za mazingira wa kundi la Just Stop Oil jana Jumatano waliandamana na kufanya vurugu kwenye mashindano ya tenisi ya Wimbledon kwa kuvamia sehemu ya kuchezea na kutupa maganda ya machungwa.
Tukio la kwanza la wanamazingira hao lilitokea wakati wa mechi kati ya Sho Shimabukuro na Grigor Dimitrov hali iliyosababisha mechi hiyo kusimama kwa muda.
Katika tukio la pili wanamazingira hao walisababisha mechi nyingine kati ya Katie Boulter na Daria Saville kusimama kwa muda huku uwanja ikiwa umetapakaa maganda ya machungwa.
Hata hivyo tukio hilo lililoongozwa na waandamanaji wawili walioingia sehemu za kuchezea tenisi halikuchukua muda kwani wana usalama waliwadhibiti na baadaye wachezaji wakasaidia kusafisha uwanja uliotapakaa maganda ya machungwa.
Baadaye taarifa ya polisi ilithibitisha kukamatwa kwa waandamanaji wawili waliokuwa mstari wa mbele mmoja mwanaume na mwingine mwanamke ambao umri wao wote ni miaka zaidi ya 60.
Ulinzi ulikuwa mkali safari hii kuliko mwaka jana ingawa baadhi ya mashabiki wamelalamikia ulinzi huo kwa namna ulivyowachelewesha kuingia uwanjani kwani muda mwingi ulitumika kukagua mashabiki.
Muungano wa kundi la Just Stop Oil linalohusisha wanamazingira wamekuwa wakifanya vurugu katika michezo mbalimbali zikiwamo mechi za soka za Ligi Kuu England pamoja na zile za ligi ya rugby.
Miongoni mwa madai ya wanamazingira wa Just Stop Oil ni pamoja na kuitaka Serikali ya Uingereza iache kutoa leseni mpya katika miradi ya gesi, mafuta na makaa ya mawe.

The post Wanamazingira wavamia mashindano ya tenisi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/06/wanamazingira-wavuruga-mashindano-ya-tenisi/feed/ 0
Neymar atozwa faini kwa kuharibu mazingira https://www.greensports.co.tz/2023/07/05/neymar-atozwa-faini-kwa-kuharibu-mazingira/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/05/neymar-atozwa-faini-kwa-kuharibu-mazingira/#respond Wed, 05 Jul 2023 18:46:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6824 Rio de Janeiro, BrazilMamlaka nchini Brazil zimemtoza faini ya Dola 3.3 milioni mshambuliaji wa PSG, Neymar kwa kosa la kuharibu mazingira katika ujenzi wa mjengo wake wa kifahari uliopo pwani ya mji wa Mangaratiba nje kidogo ya jiji maarufu la Rio de Janeiro.Kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka za mji wa Mangaratiba, Neymar ameadhibiwa kwa […]

The post Neymar atozwa faini kwa kuharibu mazingira first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rio de Janeiro, Brazil
Mamlaka nchini Brazil zimemtoza faini ya Dola 3.3 milioni mshambuliaji wa PSG, Neymar kwa kosa la kuharibu mazingira katika ujenzi wa mjengo wake wa kifahari uliopo pwani ya mji wa Mangaratiba nje kidogo ya jiji maarufu la Rio de Janeiro.
Kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka za mji wa Mangaratiba, Neymar ameadhibiwa kwa kosa la kujenga bwawa lisilo rasmi katika mjengo wake kwenye pwani hiyo jambo ambalo ni kinyume na sheria za mazingira.
Neymar ana haki ya kukata rufaa adhabu hiyo lakini watu wake hawakuwa tayari kuzungumza lolote kama wataamua kulipa faini hiyo au watakata rufaa.
Adhabu hiyo imekuja ikiwa ni takriban siku 10 zimepita baada ya maofisa wa idara ya mazingira kufanya ukaguzi katika mjengo wa Neymar na kukuta ujenzi mkubwa ukiendelea bila ya kibali cha mamlaka za usimamizi wa mazingira.
Kwa mujibu wa maofisa wa idara ya mazingira katika ujenzi huo kuna uharibifu mkubwa uliofanywa katika pwani hiyo ikiwamo kuchepusha maji ya ziwa pamoja na uharibifu wa uoto wa asili.

“Idara ya Mazingira mbali na kutoza faini pia kwa kuzingatia uharibifu uliofanyika na kutoheshimu sheria za mazingira imewasilisha tukio hilo kwa ofisi ya mwendesha mashitaka, polisi na bodi nyingine zinazohusika na usimamizi wa mazingira,” ilieleza taarifa ya mamlaka ya mji wa Mangaratiba.


Habari zaidi zinadai kwamba Neymar da Silva Santos ambaye ni baba mzazi wa Neymar aliwatolea maneno makali maofisa wa idara ya mazingira waliofika kukagua ujenzi wa mjengo wa mtoto wake.
Sehemu ya bwawa ambalo Neymar anadaiwa kujenga lina ukubwa wa mita za mraba 1,000 na hadi maofisa wa mazingira wanafanya ukaguzi wao tayari mchezaji huyo alikuwa ametumia zaidi ya Dola 25,000 katika ujenzi huo.

The post Neymar atozwa faini kwa kuharibu mazingira first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/05/neymar-atozwa-faini-kwa-kuharibu-mazingira/feed/ 0
Wanamichezo waienzi Siku ya Mazingira https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/wanamichezo-waienzi-siku-ya-mazingira/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/wanamichezo-waienzi-siku-ya-mazingira/#respond Tue, 06 Jun 2023 06:43:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6469 Na mwandishi wetuJuni 5 ya kila mwaka ni Siku ya Mazingira Duniani, makundi ya wanamazingira huitumia siku hiyo kuihamasisha jamii umuhimu wa kuyajali, kuyatunza na kuyalinda mazingira.Juni 5 imekuwa ikifanywa Siku ya Mazingira Duniani tangu miaka 50 iliyopita, sherehe zimekuwa zikifanyika huku kukiwa na kauli mbiu tofauti zinazoandamana na tukio zima la Siku ya Mazingira.Kwa […]

The post Wanamichezo waienzi Siku ya Mazingira first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Juni 5 ya kila mwaka ni Siku ya Mazingira Duniani, makundi ya wanamazingira huitumia siku hiyo kuihamasisha jamii umuhimu wa kuyajali, kuyatunza na kuyalinda mazingira.
Juni 5 imekuwa ikifanywa Siku ya Mazingira Duniani tangu miaka 50 iliyopita, sherehe zimekuwa zikifanyika huku kukiwa na kauli mbiu tofauti zinazoandamana na tukio zima la Siku ya Mazingira.
Kwa mwaka huu mwenyeji wa Siku ya Mazingira Duniani ni nchi ya Ivory Coast ambapo kauli mbiu ya siku hiyo inahusu suluhisho la uchafu utokanao na plastiki.
Wakati makundi mbalimbali yakijitahidi kuienzi na kuipa thamani Siku ya Mazingira Duniani, kwa wanamichezo hasa wa Tanzania bado mwamko umekuwa mdogo katika kuipa hadhi siku hiyo.
Kwa mfano licha ya kuwapo umuhimu mkubwa wa kuyatunza mazingira kwa ustawi wa michezo, ni wanamichezo wachache mno nchini kama wapo wanaojua kwamba jana Jumatatu Juni 5, ilikuwa Siku ya Mazingira Duniani.
GreenSports tunaamini nguvu ya wanamichezo inahitajika katika kuitumia siku hii kuihamasisha jamii umuhimu wa kuyatunza na kuyalinda mazingira ili kukabiliana na matatizo mbalimbali yanayotokana na uharibifu wa mazingira yakiwamo Mabadiliko ya Tabianchi.
Suluhisho la matatizo mengi yanayotokana na ubaribifu wa mazingira ni upandaji miti, GreenSports tunadhani hili ni eneo ambalo wanamichezo wanatakiwa kusimama kidete katika kuunga mkono kampeni ya upandaji miti inayoongozwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
Wanamazingira mara kadhaa wamekuwa wakizitaja faida za misitu, mojawapo ni ukweli kwamba miti ni chanzo cha hewa safi hivyo wanamichezo lazima watambue kwamba upandaji miti ni jambo lenye faida kwao na wana wajibu wa kuunga mkono kampeni ya upandaji miti kwani raha ya michezo ni pamoja na uwapo wa hewa safi.
Katika hili wanamichezo waige mfano wa mwanariadha wa Kenya, Eliud Kipchoge ambaye ni bingwa mara mbili wa mbio za Olimpiki, amewahi kusema kwamba majanga ya uharibifu wa mazingira yanaweza kumfanya ahindwe kufurahia mchezo wa riadha anaoupenda.
Mwanariadha huyu anaamini kwamba hewa safi ni kitu muhimu katika kumfanya akimbie vizuri na kuufurahia mchezo wa riadha.
Kwa sasa Kipchoge (pichani juu) anaendesha kampeni za upandaji miti nchini Kenya akishirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Kenya (KFS) akiamini kwamba kuna uhusiano mkubwa kati ya hewa safi, mchezo wa riadha na michezo mingine.
Nchini Sweden katika hafla ya Siku ya Mazingira Duniani mwaka 2022, nchi hiyo iliwatumia vizuri wanamichezo katika kuipa thamani na hadhi siku hiyo na kuihamasisha jamii kutunza mazingira.
Katika hilo watoto zaidi ya 6,000 walishiriki katika mbio fupi katika Jiji la Stockholm ili kuonyesha uhusiano uliopo kwenye michezo na umuhimu wa hewa safi kwa wanamichezo wa sasa na baadaye.
Kwa mantiki hiyo, GreenSports tunaamini huu ni wakati sahihi kwa wanamichezo wetu si tu kujua uwapo wa Siku ya Mazingira Duniani bali pia kuienzi siku hiyo na kuipa thamani yake kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya michezo.

The post Wanamichezo waienzi Siku ya Mazingira first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/wanamichezo-waienzi-siku-ya-mazingira/feed/ 0
Mashabiki Japan wazoa takataka uwanjani https://www.greensports.co.tz/2022/11/24/mashabiki-japan-wazoa-takataka-uwanjani/ https://www.greensports.co.tz/2022/11/24/mashabiki-japan-wazoa-takataka-uwanjani/#respond Thu, 24 Nov 2022 09:31:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=3911 Doha, QatarBaada ya Japan kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ujerumani, mashabiki wake waliahirisha sherehe za ushindi, wakaamua kujitolea kuokota uchafu kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Khalifa.Kwenye viwanja vya soka, mechi inapomalizika kunakuwa na uchafu wa kila aina, kuanzia chupa za maji na vinywaji vingine, mabaki ya vyakula mbalimbali na vifungashio vyake, kwa mashabiki […]

The post Mashabiki Japan wazoa takataka uwanjani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Doha, Qatar
Baada ya Japan kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ujerumani, mashabiki wake waliahirisha sherehe za ushindi, wakaamua kujitolea kuokota uchafu kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Khalifa.
Kwenye viwanja vya soka, mechi inapomalizika kunakuwa na uchafu wa kila aina, kuanzia chupa za maji na vinywaji vingine, mabaki ya vyakula mbalimbali na vifungashio vyake, kwa mashabiki wa Japan hali hiyo waliamua kuitumia kutoa somo la kujali mazingira na usafi.
Kutoka na ushindi mbele ya Ujerumani, Taifa kubwa kwenye soka duniani, halikuwa jambo dogo, ilihitaji kulifurahia mara baada ya filimbi ya kumaliza mchezo kupulizwa, lakini mashabiki wa Japan wakajisahaulisha na kuukumbusha uma wa wanamichezo kwamba usafi na utunzaji mazingira ni jambo lenye maana kubwa pengine kuliko ushindi dhidi ya Ujerumani.
Kwa watu wa Japan suala la usafi ni kama utamaduni ambao mtoto anafundishwa tangu akiwa mdogo na ndio maana haishangazi kuona mashabiki wa soka wa nchi hiyo, maarufu Samurai Blue wakijitoa kimasomaso bila malipo kuokota uchafu.
Tukio hilo la Qatar si la kwanza kwa mashabiki hao, miaka mianne iliyopita walifanya hivyo nchini Urusi mara baada ya mechi yao na Ubelgiji, mechi ambayo walifungwa mabao 3-2 lakini baada tu ya matokeo hayo mabaya, mashabiki hao wakaanza wakaanza kuokota uchafu wakiwa na huzuni lakini majuzi wameifanya kazi hiyo wakiwa na furaha kuonyesha kwamba usafi ni utamaduni wao.
Mashabiki hao pia waliifanya kazi hiyo ya kuokota uchafu katika mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji Qatar na Ecuador na hivyo kudhihirisha kwamba wanachokifanya wamekidhamiria.
Japan ambayo ipo Kundi E, itacheza mechi yake ya pili Jumapili dhidi ya Costa Rica kabla ya kumalizia mechi za makundi dhidi ya Hispania Alhamisi ijayo.

The post Mashabiki Japan wazoa takataka uwanjani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/11/24/mashabiki-japan-wazoa-takataka-uwanjani/feed/ 0
Bellerin, staa wa Arsenal mwanamazingira https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/bellerin-staa-wa-arsenal-mwanamazingira/ https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/bellerin-staa-wa-arsenal-mwanamazingira/#respond Wed, 10 Nov 2021 14:17:52 +0000 https://greensports.co.tz/?p=378 Barcelona, HispaniaStaa wa Arsenal, Hector Bellerin anakumbuka vizuri utamaduni wa kutunza mazingira aliojifunza kwa babu yake tangu akiwa mtoto mdogo katika viunga vya jiji la Barcelona. Katika kuuendeleza utamaduni huo, Bellerin ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Real Betis ya Hispania, anaendesha kampeni ya upandaji miti lengo likiwa ni kupendezesha na kusaidia […]

The post Bellerin, staa wa Arsenal mwanamazingira first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Staa wa Arsenal, Hector Bellerin anakumbuka vizuri utamaduni wa kutunza mazingira aliojifunza kwa babu yake tangu akiwa mtoto mdogo katika viunga vya jiji la Barcelona.

Katika kuuendeleza utamaduni huo, Bellerin ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Real Betis ya Hispania, anaendesha kampeni ya upandaji miti lengo likiwa ni kupendezesha na kusaidia utunzaji na uhifadhi wa mazingira duniani.

“Nikiwa mdogo niliishi na babu yangu Barcelona, nilikuwa nakwenda naye kwenye bustani yake na huko tulipanda miti na kucheza kwenye pori dogo, kwa hiyo hili ni jambo linalougusa moyo wangu,” alisema Bellerin katika moja ya mahojiano aliyowahi kufanya.

Wakati Ligi Kuu England msimu wa 2019/20 ikiwa imesimama Machi mwaka jana kutokana na janga la Corona, mbali na juhudi za kujiweka fiti, Bellerin pia alitumia muda huo kuendeleza harakati zake za upandaji miti na utunzaji mazingira jambo ambalo analifanya kutokana na mapenzi aliyonayo katika jambo hilo.

Katika kuifanyia kazi kampeni hiyo, Bellerin aliahidi kupanda miti 3,000 kwa kila mechi ambayo klabu yake ya Arsenal ingeibuka na ushindi katika mechi zilizobaki za msimu huo.

Bellerin pia amekuwa akiwahimiza wachezaji wenzake kusaidia katika kampeni za utunzaji mazingira na upandaji miti, “Ni jambo zuri kujivunia kwa kile tulichonacho, iwe ni magari yetu, saa za bei mbaya lakini pia ni muhimu kuwasilisha ujumbe wenye maana, angalia katika hilo tuko kimya,” alisema Bellerin katika moja ya mahojiano.

Septemba mwaka jana, Bellerín alitangazwa kuwa mwanahisa wa pili kuwa na hisa nyingi katika klabu ya Forest Green Rovers ya England inayoshiriki ligi ya EFL (League II) , aliipongeza klabu hiyo kwa kampeni yake ya kuhimiza ulaji mboga na matunda (veganism) na kampeni za utunzaji mazingira.

Bellerin ambaye mwaka 2017, alianza kuwa mlaji wa mboga na matunda (vegan) jambo ambalo anasema limemsaidia kuimarisha afya yake, moja ya mikakati yake kwa sasa ni kushiriki kupanda miti katika msitu maarufu wa Amazon (Mapafu ya Dunia) ambao kwa sehemu kubwa upo nchini Brazil. Katika hilo, Bellerin anashirikiana na taasisi ya One Tree Planted.

The post Bellerin, staa wa Arsenal mwanamazingira first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/bellerin-staa-wa-arsenal-mwanamazingira/feed/ 0