Yanga Princess - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 29 Mar 2025 18:54:04 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Yanga Princess - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Yanga Princess yaipiga Simba Queens https://www.greensports.co.tz/2025/03/18/yanga-princess-yaipiga-simba-queens/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/18/yanga-princess-yaipiga-simba-queens/#respond Tue, 18 Mar 2025 19:56:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13148 Na mwandishi wetuYanga Princess imewatambia mahasimu wake, Simba Queens kwa kuwachapa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Wanawake (TWPL) iliyopigwa leo Jumanne, Machi 18, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge, Dar es Salaam.Baada ya mpambano mkali, dakika 45 za kwanza zilimalizika bila timu kupata bao kabla ya Yanga kupata bao hilo pekee dakika nne […]

The post Yanga Princess yaipiga Simba Queens first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Yanga Princess imewatambia mahasimu wake, Simba Queens kwa kuwachapa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Wanawake (TWPL) iliyopigwa leo Jumanne, Machi 18, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge, Dar es Salaam.
Baada ya mpambano mkali, dakika 45 za kwanza zilimalizika bila timu kupata bao kabla ya Yanga kupata bao hilo pekee dakika nne baada ya mapumziko lililofungwa na Jeannine Mukandayisenga.
Jeannine ambaye ni mchezaji kutoka nchini Rwanda alimchambua vyema kipa wa Simba Queens, Winfrida Ouko kutoka Kenya na kuihakikishia timu yake pointi tatu muhimu.
Yanga Princess pamoja na ushindi huo, inaendelea kushika nafasi ya tatu hivyo bado ina kazi ya kufanya ili kuwaengua kileleni Simba Queens ambao ndio mabingwa watetezi.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo yenye timu 10 zilizochezwa leo, matokeo ni kama ifuatavyo: Ceasiaa Queens iliichapa Mlandizi Queens mabao 5-2, Allance Queens ilipata ushindi wa bao 1-0 mbele ya Gets Program wakati kesho Mashujaa Queens watacheza na JKT Queens.

The post Yanga Princess yaipiga Simba Queens first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/18/yanga-princess-yaipiga-simba-queens/feed/ 0
Simba Queens hoi kwa Yanga Princess https://www.greensports.co.tz/2024/10/03/simba-queens-hoi-kwa-yanga-princess/ https://www.greensports.co.tz/2024/10/03/simba-queens-hoi-kwa-yanga-princess/#respond Thu, 03 Oct 2024 07:14:49 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11972 Na mwandishi wetuTimu ya soka ya wanawake ya Yanga Princess imeibuka kidedea katika mechi ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii kwa kuwalaza mahasimu wao wa Simba Queens kwa penalti 4-3.Kwa ushindi huo, Yanga Princess wanasubiri kuumana na JKT Queens ambao katika mechi ya awali waliibugiza Ceasiaa Queens mabao 7-0. Mechi zote hizo zilipigwa kwenye […]

The post Simba Queens hoi kwa Yanga Princess first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya soka ya wanawake ya Yanga Princess imeibuka kidedea katika mechi ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii kwa kuwalaza mahasimu wao wa Simba Queens kwa penalti 4-3.
Kwa ushindi huo, Yanga Princess wanasubiri kuumana na JKT Queens ambao katika mechi ya awali waliibugiza Ceasiaa Queens mabao 7-0. Mechi zote hizo zilipigwa kwenye Uwanja wa KMC, Kinondoni, Dar es Salaam.
Katika mechi ya mahasimu, Yanga ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika za awali lililofungwa na Agnes Palangyo bao ambalo lilidumu kwa dakika zote 45 za kwanza.
Simba Queens walipambana na juhudi zao kuzaa matunda zikiwa zimebakia dakika mbili kabla ya mchezo kumalizika kwa kupata bao lililofungwa na Jentrix Shikangwa na hatimaye timu hizo kupigiana penalti.
Simba baada ya kupoteza mchezo huo sasa wataumana na Ceasiaa Queens katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu, ambayo kama ilivyo mechi ya fainali, zote zitapigwa Jumamosi ya Oktoba 5 mwaka huu.
Michuano ya Ngao ya Jamii kwa wanawake inaashiria ufunguzi wa Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake (TWPL) ambayo inashirikisha timu 10 na kwa msimu huu wa 2024-25 itaanza rasmi kutimua vumbi Oktoba 9.

The post Simba Queens hoi kwa Yanga Princess first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/10/03/simba-queens-hoi-kwa-yanga-princess/feed/ 0
Simba Queens yaitesa Yanga Princess https://www.greensports.co.tz/2024/04/26/simba-queens-yaitesa-yanga-princess/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/26/simba-queens-yaitesa-yanga-princess/#respond Fri, 26 Apr 2024 20:40:36 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10744 Na mwandishi wetuSimba Queens imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) baada ya kuwalaza mahasimu wao Yanga Princess kwa mabao 3-1.Katika mechi hiyo iliyopigwa Alhamisi hii jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Queens walianza kuandika bao la kwanza dakika nne baada ya mapumziko mfungaji akiwa ni Aisha […]

The post Simba Queens yaitesa Yanga Princess first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba Queens imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) baada ya kuwalaza mahasimu wao Yanga Princess kwa mabao 3-1.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Alhamisi hii jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Queens walianza kuandika bao la kwanza dakika nne baada ya mapumziko mfungaji akiwa ni Aisha Mnuka.
Dakika 16 baada ya kuingia bao hilo, Princess walijikuta wakichapwa bao la pili lililofungwa na Jentrix Shikangwa, bao ambalo liliwafanya baadhi ya mashabiki kuamini kuwa mechi hiyo ingeisha kwa matokeo hayo.
Hali hata hivyo ikawa tofauti baada ya Aisha kwa mara nyingine kuipatia Queens bao la tatu katika dakika ya pili ya muda wa nyongeza (90+2) kabla ya mpira kumalizika.
Princess nao hawakukata tamaa kwani katika dakika hizo hizo za nyongeza, dakika ya tano (90+5) walifanikiwa kupata bao pekee la kufutia machozi lililofungwa na Kaeda Wilson.
Ushindi huo unawafanya Queens kuendeleza ubabe dhidi ya Princess katika msimu huu kwani katika mechi ya mzunguko wa kwanza, timu hiyo pia ilitoka uwanjani na ushindi kama huo.
Queens pia wanaendelea kushikilia usukani wa ligi hiyo wakiwa wamekusanya jumla ya pointi 34 katika mechi 12 wakati Princess wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 21 nyuma ya JKT Queens wanaoshika nafasi ya pili.

The post Simba Queens yaitesa Yanga Princess first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/26/simba-queens-yaitesa-yanga-princess/feed/ 0
Simba Queens, Yanga Princess kukiwasha https://www.greensports.co.tz/2024/04/24/simba-queens-yanga-princess-kukiwasha/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/24/simba-queens-yanga-princess-kukiwasha/#respond Wed, 24 Apr 2024 20:16:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10729 Na mwandishi wetuTimu za Simba Queens na Yanga Princess zipo tayari kwa mchezo kwa kesho Alhamisi wa ‘derby’ utakaopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa michuano ya Ligi Kuu ya Wanawake.Wakizungumza leo Jumatano jijini Dar es Salaam makocha wa timu hiyo walisema wanafahamu ushindani uliopo wa ligi baina ya […]

The post Simba Queens, Yanga Princess kukiwasha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu za Simba Queens na Yanga Princess zipo tayari kwa mchezo kwa kesho Alhamisi wa ‘derby’ utakaopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa michuano ya Ligi Kuu ya Wanawake.
Wakizungumza leo Jumatano jijini Dar es Salaam makocha wa timu hiyo walisema wanafahamu ushindani uliopo wa ligi baina ya timu hizo na kila mmoja amejinasibu kujipanga vya kutosha kuhakikisha anaibuka na ushindi.
Kocha msaidizi wa Yanga, Fred Mbuna alisema: “Vijana wako salama na wameamka salama na tumefanya maandalizi ya kutosha kama makocha, tumeenda uwanja wa mazoezi tumejaribu kuondoa makosa tuliyokuwa nayo na tumejiandaa kwa ajili ya mchezo.
”Tunafahamu pia ni mechi ya ligi kuu, mechi kubwa, ni mechi ya ‘derby’ hivyo nasi tutaingia kikubwa, tutacheza kikubwa kwa ajili ya kupata matokeo kwenye mchezo huu,” alisema.


Naye, kocha msaidizi wa Simba, Mussa Hassan ‘Mgosi’ alifafanua kuwa wamekuwa na wakati mzuri wakati wa kujiandaa na mechi hiyo na kila mchezaji yuko tayari kupambania jezi ya Wekundu hao.
Mgosi alisema anaamini itakuwa mechi yenye mvuto na ushindani kulingana na malengo ya kila timu ingawa wao wamepania kuwapa furaha mashabiki wao kwa kuibuka na ushindi ili kitimiza malengo yao ya kutwaa ubingwa.
Timu hizo zenye maskani yake Kariakoo, Dar es Salaam zinakutana Simba ikiwa kileleni mwa msimamo kwa pointi 31 ilizokusanya kwenye mechi 11 wakati Yanga iliyocheza mechi 10 ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi 21.
Nafasi ya pili katika ligi hiyo inashikiliwa na mabingwa watetezi, JKT Queens wenye pointi 25 baada ya mechi 11.

The post Simba Queens, Yanga Princess kukiwasha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/24/simba-queens-yanga-princess-kukiwasha/feed/ 0
Bosi haifurahii Yanga Princess https://www.greensports.co.tz/2024/01/24/bosi-haifurahii-yanga-princess/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/24/bosi-haifurahii-yanga-princess/#respond Wed, 24 Jan 2024 06:03:18 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9397 Na mwandishi wetuMakamu Rais wa Klabu ya Yanga, Arafat Haji ameeleza kutofurahishwa na mwenendo mbaya wa timu yao ya wanawake, Yanga Princess na kuahidi kurekebisha baadhi ya mambo ili wapate furaha upande huo pia.Haji alisema hayo leo Jumanne kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ambapo alieleza kuwa bado wanaendelea kufanya maboresho ya kiufundi kwenye […]

The post Bosi haifurahii Yanga Princess first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Makamu Rais wa Klabu ya Yanga, Arafat Haji ameeleza kutofurahishwa na mwenendo mbaya wa timu yao ya wanawake, Yanga Princess na kuahidi kurekebisha baadhi ya mambo ili wapate furaha upande huo pia.
Haji alisema hayo leo Jumanne kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ambapo alieleza kuwa bado wanaendelea kufanya maboresho ya kiufundi kwenye maeneo kadhaa, kuanzia ndani ya uwanja hadi nje ya uwanja.
“Tutakubaliana kwa pamoja kwamba ilipo leo Yanga Princess sio ilipokuwa misimu kadhaa nyuma! Taratibu mabadiliko yanaendelea kufanyika na muda si mrefu watu wataanza kufurahia matunda,” aliandika Haji.
Alieleza, nguvu kubwa ya maboresho ilianza kwenye timu yao kubwa ya wanaume na baada ya kukaa vizuri na kubeba mataji kadhaa, sasa wameanza taratibu kuiboresha Yanga Princess na kushuka hadi timu zao za vijana za umri chini ya miaka 17 na 20.
Alisema mabadiliko yanapofanyika matokeo hayaonekani kwa haraka badala yake ni mchakato unaohitaji muda kwani hata walipoanza kwa timu ya wanaume iliwachukua misimu miwili kabla ya kuanza kubeba mataji.
Yanga Princess inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) ikiwa na pointi 12 baada ya kucheza mechi sita ikishinda mechi nne na kufungwa michezo miwili.

The post Bosi haifurahii Yanga Princess first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/24/bosi-haifurahii-yanga-princess/feed/ 0
Derby ya madada, Simba Queens, Yanga Princess https://www.greensports.co.tz/2023/12/09/derby-ya-madada-simba-queens-yanga-princess/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/09/derby-ya-madada-simba-queens-yanga-princess/#respond Sat, 09 Dec 2023 10:34:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8801 Na mwandishi wetuMichuano ya Ngao ya Jamii kwa Wanawake inatarajia kuchezwa kwa mara ya kwanza leo Jumamosi ambapo michezo miwili itapigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.Mchezo wa mapema ni saa 9.00 alasiri utakaozikutanisha JKT Queens dhidi ya Fountain Gate Princess na mchezo wa pili utawakutanisha watani wa jadi, Simba Queens dhidi ya […]

The post Derby ya madada, Simba Queens, Yanga Princess first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Michuano ya Ngao ya Jamii kwa Wanawake inatarajia kuchezwa kwa mara ya kwanza leo Jumamosi ambapo michezo miwili itapigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Mchezo wa mapema ni saa 9.00 alasiri utakaozikutanisha JKT Queens dhidi ya Fountain Gate Princess na mchezo wa pili utawakutanisha watani wa jadi, Simba Queens dhidi ya Yanga Princess utakaopigwa saa 12.00 jioni.
Washindi wa michezo hii watacheza fainali wakati waliopoteza watacheza mechi ya kutafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo. Mechi zote hizo zitachezwa Desemba 12, mwaka huu.
Akizungumzia mchezo huo, kocha msaidizi wa Simba, Mussa Hassan ‘Mgosi’, alisema: “Kwanza tunawapongeza TFF kwa kuhakikisha soka la wanawake lianzidi kukua kwa uwepo wa mechi kama hizi.
“Lakini tunaamini mechi haitakuwa rahisi kwa sababu timu zote zimejiandaa vizuri, tulikaa na kujiuliza tulipokosea msimu uliopita na tumeona mapungufu yetu na sasa tunataka kufanya vizuri katika mchezo huu wa Ngao ya Jamii.”
Kocha Mkuu wa Yanga Princess, Charles Haalubono alisema wamejiandaa vizuri kukabiliana na Simba ambao anaamini ni timu ngumu lakini kikosi chake kipo tayari kwa mchezo.
“Itakuwa mechi ya ushindani, natambua ni mechi kubwa na ‘derby’ lakini tumejipanga vizuri na tunatambua katika historia hatuna matokeo mazuri, hatutaki kuamini hayo kwa sababu wachezaji wangu wako tayari kwa ajili ya kutafuta matokeo mazuri,” alisema Haalubono.
Kocha Mkuu wa JKT Queens, Esther Chabruma alisema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika, wachezaji wako katika hali nzuri kwa ajili ya mchezo dhidi ya Fountain Gate Princess.


“Hatutakuwa na mabadiliko yoyote katika kikosi changu cha ushindani, nitawakosa nyota wangu wawili, katika mchezo hakuna kujiamini sana kwa sababu wachezaji wangu wengi walikuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa na tutapambana kupata matokeo mazuri,” alisema Chabruma.
Kocha mkuu wa Fountain Gate Princess, Masoud Juma alisema: “Tunaufahamu ubora wa JKT Queens, mechi ya mwisho walitufunga lakini sasa tumejipanga vizuri na tutaingia katika mchezo huu kwa nidhamu ya hali ya juu kwa sababu ni mechi ya kutafuta ushindi.”

The post Derby ya madada, Simba Queens, Yanga Princess first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/09/derby-ya-madada-simba-queens-yanga-princess/feed/ 0
Mmarekani wa Yanga Princess meno nje https://www.greensports.co.tz/2023/10/06/mmarekani-wa-yanga-princess-meno-nje/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/06/mmarekani-wa-yanga-princess-meno-nje/#respond Fri, 06 Oct 2023 07:14:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7963 Na mwandishi wetuMchezaji mpya wa Yanga Princess, Kaida Wilson raia wa Marekani amesema ana furaha kujiunga na timu hiyo akiahidi kufanya vizuri kuisaidia kufikisha malengo yake.Mchezaji huyo, 17, alisema yupo Yanga kucheza kwa msimu mmoja hadi mwakani ataondoka kurudi Marekani kwa ajili ya kuendelea na masomo. “Nina furaha kuwa hapa na naamini nitapata wakati mzuri […]

The post Mmarekani wa Yanga Princess meno nje first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mchezaji mpya wa Yanga Princess, Kaida Wilson raia wa Marekani amesema ana furaha kujiunga na timu hiyo akiahidi kufanya vizuri kuisaidia kufikisha malengo yake.
Mchezaji huyo, 17, alisema yupo Yanga kucheza kwa msimu mmoja hadi mwakani ataondoka kurudi Marekani kwa ajili ya kuendelea na masomo.

“Nina furaha kuwa hapa na naamini nitapata wakati mzuri wa kuisaidia timu pale nitakapopata nafasi, mimi ninacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji na niko hapa kupambana. Kidogo napata changamoto ya jua kali lakini taratibu naanza kuzoea ili kwenda sawa na wenzangu,”alisema.


Mratibu wa timu hiyo, Kibwana Matokeo aliyemuunganisha kiungo huyo na Yanga, alisema baba mzazi wa mtoto huyo alivutiwa na Yanga na ndipo akatamani mtoto wake aje kuitumikia Yanga Princess.
Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema kulingana na usajili wa wachezaji waliofanya msimu huu, anaamini timu hiyo itarudi katika ushindani kwenye Ligi Kuu ya Wanawake na kufanya vizuri ikiwezekana kutwaa ubingwa.

The post Mmarekani wa Yanga Princess meno nje first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/06/mmarekani-wa-yanga-princess-meno-nje/feed/ 0
‘Clara Luvanga ni mwanzo tu’ https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/clara-luvanga-ni-mwanzo-tu/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/clara-luvanga-ni-mwanzo-tu/#respond Wed, 30 Aug 2023 17:09:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7588 Na mwandishi wetuKlabu ya Yanga imeeleza kukamilika kwa dili la Clara Luvanga aliyetimkia Dux Logrono ya Hispania, ni mwanzo wa wachezaji wengi watakaowauza hivi karibuni kutoka timu yao ya wanawake ya Yanga Princess.Clara aliyevuma akiwa na kikosi cha timu ya U17 ya Tanzania kwenye fainali za Kombe la Dunia India 2022, amejiunga na Dux inayoshiriki […]

The post ‘Clara Luvanga ni mwanzo tu’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya Yanga imeeleza kukamilika kwa dili la Clara Luvanga aliyetimkia Dux Logrono ya Hispania, ni mwanzo wa wachezaji wengi watakaowauza hivi karibuni kutoka timu yao ya wanawake ya Yanga Princess.
Clara aliyevuma akiwa na kikosi cha timu ya U17 ya Tanzania kwenye fainali za Kombe la Dunia India 2022, amejiunga na Dux inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa mkataba wa miaka mitatu.
Mkurugenzi wa Mashindano Yanga, Saad Kawemba alisema wanafurahia kuwa na maendeleo ya namna hiyo katika klabu akisisitiza kuwa wapo wachezaji wengi wa Princess ambao wameshafanyiwa mipango na muda si mrefu wataweka wazi wanakoelekea nyota wao hao.
“Ni maendeleo kwa kweli na ni jambo jema kwa klabu, tuna idadi ndefu kidogo kuhusu uhamisho wa wachezaji wetu kwenda nje na hivi karibuni klabu itatoa taarifa rasmi kuhusiana na hilo.
“Nasema hivyo kwa sababu orodha ni ndefu kidogo ndio maana klabu itatoa taarifa rasmi kwa wanaoondoka, ni mipango mikubwa tuliyonayo kuhusiana na hilo na muda si mrefu itawekwa wazi,” alifafanua Kawemba.
Timu ya Dux Logrono ina miaka 15 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008 kabla ya Julai Mosi, mwaka juzi kuuzwa kwa Dux Gaming ambapo washirika wake ni DJ Mariio na kipa wa Real Madrid, Thibaut Courtois.
Timu hiyo kwa sasa inanolewa na Gerardo Leon, beki wa zamani wa timu za Villarreal, Valencia na Real Sociedad za Hispania.

The post ‘Clara Luvanga ni mwanzo tu’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/clara-luvanga-ni-mwanzo-tu/feed/ 0
Nkoma afutiwa mkataba Yanga Princess https://www.greensports.co.tz/2023/03/28/nkoma-afutiwa-mkataba-yanga-princess/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/28/nkoma-afutiwa-mkataba-yanga-princess/#respond Tue, 28 Mar 2023 12:40:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5618 Na mwandishi wetuUongozi wa Yanga umemteua Fred Mbuna (pichani juu) kuwa kocha mkuu wa timu ya wanawake ya Yanga Princess na kuvunja mkataba na Sebastian Nkoma aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo.Taarifa za kuvunjwa mkataba na kocha huo iliyotolewa leo Jumanne kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo ilieleza kuwa hatua hiyo imefikiwa baada […]

The post Nkoma afutiwa mkataba Yanga Princess first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Uongozi wa Yanga umemteua Fred Mbuna (pichani juu) kuwa kocha mkuu wa timu ya wanawake ya Yanga Princess na kuvunja mkataba na Sebastian Nkoma aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo.
Taarifa za kuvunjwa mkataba na kocha huo iliyotolewa leo Jumanne kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo ilieleza kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya makubaliano ya pande zote mbili.
“Uongozi wa Yanga unamshukuru kocha Sebastian kwa kazi yake kipindi chote alichokuwa akiifundisha timu yetu ya wanawake, kwa sasa benchi la ufundi la Yanga Princess litakuwa chini ya kocha Fredy Mbuna mpaka msimu huu utakapomalizika,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Nkoma aliyetua Yanga mwanzoni mwa msimu huu baada ya kuachana na Simba Queens, anaondoka akiiacha Princess ikiwa nafasi ya nne, ikiwa imeshinda mechi sita, sare nne na kufungwa mechi mbili.
Timu hiyo imekusanya jumla ya pointi 22 wakiwa na tofauti ya pointi saba dhidi ya vinara Fountain Gate Princess wenye pointi 29.
Mbuna ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga, kabla ya hapo alikuwa ndiye msaidizi wa Nkoma katika timu hiyo.

The post Nkoma afutiwa mkataba Yanga Princess first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/28/nkoma-afutiwa-mkataba-yanga-princess/feed/ 0