Ubaguzi wa rangi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 30 May 2023 19:50:22 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Ubaguzi wa rangi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Ubaguzi wa rangi wamuibua Pep https://www.greensports.co.tz/2023/05/30/ubaguzi-wa-rangi-wamuibua-pep/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/30/ubaguzi-wa-rangi-wamuibua-pep/#respond Tue, 30 May 2023 19:50:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6384 Manchester, EnglandKocha wa Man City, Pep Guardiola amesema hana shaka Hispania itachukua hatua sahihi kukabiliana na ubaguzi wa rangi kwenye soka.Pep ametoa kauli hiyo baada ya mshambuliaji wa Real Madrid, Vinicius Junior kukumbana na kadhia hiyo mara kwa mara hali ambayo imeibua taharuki kwa watu mbalimbali duniani kote.Vinicius amekumbana na kadhia hiyo kwa mara nyingine […]

The post Ubaguzi wa rangi wamuibua Pep first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kocha wa Man City, Pep Guardiola amesema hana shaka Hispania itachukua hatua sahihi kukabiliana na ubaguzi wa rangi kwenye soka.
Pep ametoa kauli hiyo baada ya mshambuliaji wa Real Madrid, Vinicius Junior kukumbana na kadhia hiyo mara kwa mara hali ambayo imeibua taharuki kwa watu mbalimbali duniani kote.
Vinicius amekumbana na kadhia hiyo kwa mara nyingine katika mechi na Valencia kwenye Uwanja wa Mestalla na tayari watu watatu wamekamatwa kwa kumtolea maneno na ishara za kibaguzi mchezaji huyo.
Kutokana na tukio hilo, Uwanja wa Mestalla umepewa adhabu ya kuzuia sehemu ya mashabiki kuingia uwanjani huku mamlaka za kisheria nchini Hispania zikiendelea na taratibu nyingine za kisheria dhidi ya wahusika.
Pep ambaye pia anatokea Hispania na amewahi kucheza soka katika La Liga na kuwa kocha kwenye ligi hiyo hata hivyo alisema hatarajii mambo kubadilika kwa haraka.
“Ni kweli kwamba ubaguzi wa rangi ni tatizo kila mahali, si kwa eneo fulani pekee, ni kila mahali kunakuwa na watu wanaofikiri kwamba wao ni bora kuliko jirani zao, sisi ni bora kuliko wengine,” alisema Pep.

“Tatizo ni kwamba kuna ubaguzi kila mahali, si tu wa jinsia bali pia katika rangi, hulka, tunaamini kwamba lugha yetu ni bora kuliko ya wengine, nchi yetu ni bora kuliko nyingine, ni mambo kama hayo,” alisema.


“Tunatakiwa kukubali muingiliano kama jambo zuri kwa wanaadamu,” alisema Pep kocha aliyejipatia mafanikio akiwa na klabu ya Barcelona.

The post Ubaguzi wa rangi wamuibua Pep first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/30/ubaguzi-wa-rangi-wamuibua-pep/feed/ 0
Wataka aliyembagua Vinicius afungiwe mwaka https://www.greensports.co.tz/2023/03/01/wataka-aliyembagua-vinicius-afungiwe-mwaka/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/01/wataka-aliyembagua-vinicius-afungiwe-mwaka/#respond Wed, 01 Mar 2023 11:44:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5352 Madrid, HispaniaKamati inayoendesha kampeni kupinga vurugu nchini Hispania imependekeza shabiki wa soka mbaguzi wa rangi apewe adhabu ya kutoruhusiwa kuingia kwenye viwanja vya michezo kwa mwaka mmoja.Shabiki huyo mwenye umri wa miaka 20 anatuhumiwa kumtamkia maneno ya kibaguzi mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Brazil, Vinicius JuniorKauli ya kamati hiyo imekuja wakati […]

The post Wataka aliyembagua Vinicius afungiwe mwaka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kamati inayoendesha kampeni kupinga vurugu nchini Hispania imependekeza shabiki wa soka mbaguzi wa rangi apewe adhabu ya kutoruhusiwa kuingia kwenye viwanja vya michezo kwa mwaka mmoja.
Shabiki huyo mwenye umri wa miaka 20 anatuhumiwa kumtamkia maneno ya kibaguzi mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Brazil, Vinicius Junior
Kauli ya kamati hiyo imekuja wakati ambao mashabiki wanasubiri kuona adhabu atakayopewa shabiki huyo ambaye anatuhumiwa kumtamkia Vinicius maneno hayo Februari 5 mwaka huu.
Siku ya tukio hilo, shabiki huyo anayeaminika kuwa ni wa klabu ya Real Mallorca alikuwa uwanjani wakati timu hizo zikichuana katika mechi ya Ligi Kuu Hispania maarufu La Liga.
Shabiki huyo anayedaiwa kuwa na tiketi ya msimu aligunduliwa na maofisa usalam huku ikidaiwa ndiye aliyemtamkia maneno ya kibaguzi mchezaji wa Villarreal, Samu Chukwueze ambaye kama Vinicius wote wana asili ya Afrika.
Vinicius pia alikumbana na adha ya kauli za kibaguzi mara baada ya mechi na Mallorca alipokuwa amesimama kwa ajili ya kupiga picha na mashabiki pamoja na kusaini vitabu vya kumbukumbu.
Mchezaji huyo ambaye pia amejikuta akisakamwa na mashabiki kwa kutamkiwa maneno ya kibaguzi tangu alipoanza kucheza soka Hispania takriban miaka mitano iliyopita.
Wasimamizi wa La Liga wamewahi kufikisha matukio ya kibaguzi dhidi ya Vinicius katika vyombo vya sheria lakini baadhi ya matukio hayo yamefutwa na waendesha mashitaka.

The post Wataka aliyembagua Vinicius afungiwe mwaka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/01/wataka-aliyembagua-vinicius-afungiwe-mwaka/feed/ 0
Wabaguzi wa rangi Brazil waandaliwa kibano https://www.greensports.co.tz/2023/02/16/wabaguzi-wa-rangi-waandaliwa-kibano-brazil/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/16/wabaguzi-wa-rangi-waandaliwa-kibano-brazil/#respond Thu, 16 Feb 2023 17:56:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5182 Rio de Janeiro, BrazilShirikisho la Soka Brazil (CBF) sasa litakuwa na haki ya kutoa adhabu kwa timu ambayo mwajiriwa au shabiki wake atahusika na kosa la ubahuzi wa rangi ikiwamo kuinyang’anya timu pointi.Sheria hiyo ambayo imeidhinishwa na klabu 20 za daraja la kwanza, ni sehemu ya mkakati wa CBF katika kukabiliana na dhihaka zinazoandamana na […]

The post Wabaguzi wa rangi Brazil waandaliwa kibano first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rio de Janeiro, Brazil
Shirikisho la Soka Brazil (CBF) sasa litakuwa na haki ya kutoa adhabu kwa timu ambayo mwajiriwa au shabiki wake atahusika na kosa la ubahuzi wa rangi ikiwamo kuinyang’anya timu pointi.
Sheria hiyo ambayo imeidhinishwa na klabu 20 za daraja la kwanza, ni sehemu ya mkakati wa CBF katika kukabiliana na dhihaka zinazoandamana na kauli za ubaguzi wa rangi kwenye viwanja vya soka.
Kwa mujibu wa CBF, sheria hiyo inatarajia kuanza kutumika Februari 22 wakati wa mashindano maarufu nchini Brazil ya Copa do Brazil.

“Vita dhidi ya ubaguzi wa rangi ni jambo lenye uharaka, suluhisho limekuwa mjadala kwa karne sasa lakini hakujawahi kuwa na utekelezaji, tumeamua kwenda mbele zaidi, tunaweza hata kuzinyang’anya timu pointi katika moja ya mashindano yanayoratibiwa na CBF,” alisema Rais wa CBF, Ednaldo Rodrigues.


Akiwa ndiye mtu wa kwanza mweusi mwenye asili ya Afrika kuongoza CBF katika kipindi cha zaidi ya miaka 100, Rodrigues anaichukulia vita dhidi ya ubaguzi wa rangi kwenye oka kuwa moja ya kipaumbele chake kikuu.
CBF inakuwa mamlaka ya kwanza duniani kuja na sheria ya aina hiyo kwa lengo la kukabiliana na ubaguzi wa rangi kwenye soka.
Rais wa Brazil, Lula da Silva amepitisha sheria inayolitaja kosa la dhihaka za kibaguzi kuwa ni kosa la jinai na kuongeza adhabu kosa hilo linapofanyika kwenye viwanja vya michezo au hafla za utamaduni nchini Brazil.
Tatizo la ubaguzi wa rangi hasa kwenye viwanja vya soka limekuwa kubwa zaidi barani Ulaya ambapo katika siku za karibuni mchezaji wa Brazil anayeichezea Real Madrid, Vinicius Junior amejikuta katika kadhia hiyo.
Vinicius aliwahi kusema kwamba tatizo linakuwa kubwa kwa sababu hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya wanaohusika kufanya vitendo hivyo.

The post Wabaguzi wa rangi Brazil waandaliwa kibano first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/16/wabaguzi-wa-rangi-waandaliwa-kibano-brazil/feed/ 0