TPLB - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 18 Dec 2025 20:29:22 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.7 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg TPLB - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Sowah, Kante stop mechi tano https://www.greensports.co.tz/2025/12/17/sowah-kante-stop-mechi-tano/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/17/sowah-kante-stop-mechi-tano/#respond Wed, 17 Dec 2025 12:31:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14189 Na mwandishi wetuWachezaji wa Simba, mshambuliaji Jonathan Sowah (pichani) na kiungo, Allasante Kante wamefungiwa mechi tano kwa makosa ya utovu wa nidhamu waliyoyafanya katika mechi yao ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Azam FC.Taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) iliyopatikana Jumanne Desemba 16, 2025 ilieleza kuwa uamuzi huo umetokana na kikao cha Kamati […]

The post Sowah, Kante stop mechi tano first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Wachezaji wa Simba, mshambuliaji Jonathan Sowah (pichani) na kiungo, Allasante Kante wamefungiwa mechi tano kwa makosa ya utovu wa nidhamu waliyoyafanya katika mechi yao ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Azam FC.
Taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) iliyopatikana Jumanne Desemba 16, 2025 ilieleza kuwa uamuzi huo umetokana na kikao cha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi kilichofanyika Desemba 15, 2025 kutathmini matukio mbalimbali ya ligi hiyo.
Katika maamuzi hayo, Sowah mbali na kufungiwa mechi tano pia ametozwa faini ya Sh milioni moja, kwa kosa la kufanya kitendo kisicho cha uanamichezo kwa kumpiga kiwiko mchezaji wa Azam, Himid Mao.
Kwa upande wa Kante ambaye kama ilivyo kwa Sowah naye ametozwa faini ya Sh milioni, katika mchezo huo huo ambao Simba ililala kwa mabao 2-0, alimpiga teke kwa makusudi mchezaji wa Azam, Feisal Salum ‘Fei Toto’.
Naye mwamuzi wa kati wa mchezo huo, Abdallah Mwinyimkuu wa Singida ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi katika mizunguko mitano ya ligi hiyo kwa kushindwa kutafsiri vyema sheria za soka na kutochukua hatua dhidi ya vitendo vya ukiukwaji wa kanuni za mchezo huo.
Kamati pia imeitoza faini ya Sh milioni tano klabu ya Yanga kwa kosa la shabiki wake kutoka jukwaani na kuvuka uzio na kwenda eneo la kuchezea wakati wa mechi yao na Coastal Union kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Akiwa uwanjani shabiki huyo alifika kwenye goli la Coastal Union kabla ya kuinama kama vile alikuwa akiweka au kuokotaa kitu katika eneo hilo jambo ambalo limetajwa kuwa ni kuhatarisha usalama wa wachezaji.
Adhabu hiyo inahusisha kanuni ya ligi kuu kuhusu udhibiti kwa klabu ingawa baadhi ya mashabiki wa soka walilihusisha tukio hilo na vitendo vya ushirikina.
Naye kiungo wa Singida Black Stars, Khalid Aucho amefungiwa mechi tano na kutozwa faini ya Sh milioni moja kwa kosa la kumsukuma na kumpiga mchezaji wa TRA United, Adam Adam, katika mechi baina ya timu hizo iliyochezwa kwenye Uwanja wa KMC na TRA kutoka na ushindi wa mabao 3-1.
Mwamuzi wa mechi hiyo, Alex Pancras wa Dar es Salaam amepewa onyo kali kwa kushindwa kutafsiri vyema sheria za soka na kushindwa kuchukua hatua stahiki dhidi ya Aucho.

The post Sowah, Kante stop mechi tano first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/17/sowah-kante-stop-mechi-tano/feed/ 0
Kasongo asifu ushindani ligi kuu https://www.greensports.co.tz/2024/05/30/kasongo-asifu-ushindani-ligi-kuu-nbc/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/30/kasongo-asifu-ushindani-ligi-kuu-nbc/#respond Thu, 30 May 2024 05:54:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11170 Na mwandishi wetuMtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu (TPLB), Almasi Kasongo ameeleza kufurahishwa na namna ushindani ulivyoshamiri kwa mchezaji mmoja mmoja msimu huu kwenye Ligi Kuu NBC.Amesema ukiachilia mbali kila timu kujitafuta katika malengo yake ya msimu na kuleta presha lakini pia ushindani wa mchezaji mmoja mmoja umekuwa tija kubwa katika kuchagiza ubora wa […]

The post Kasongo asifu ushindani ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu (TPLB), Almasi Kasongo ameeleza kufurahishwa na namna ushindani ulivyoshamiri kwa mchezaji mmoja mmoja msimu huu kwenye Ligi Kuu NBC.
Amesema ukiachilia mbali kila timu kujitafuta katika malengo yake ya msimu na kuleta presha lakini pia ushindani wa mchezaji mmoja mmoja umekuwa tija kubwa katika kuchagiza ubora wa ligi ya msimu huu iliyofungwa rasmi jana Jumanne.
Akitoa mfano, Kasongo alisifia namna alivyokoshwa na ushindani wa Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam FC aliyemaliza na mabao 19 na Stephane Aziz Ki wa Yanga aliyeibuka kinara kwa mabao 21.
Kasongo pia alizungumzia ushindani wa kipa wa Coastal Union, Lqy Matampi aliyemaliza na ‘clean sheets’ 15 dhidi ya Djigui Diarra wa Yanga mwenye 14.
“Ushindani uliojitokeza ni faida kwa mpira wa miguu kiujumla, ni ushindani mzuri, kama Fei na Aziz huku Matampi na Diarra, kwetu sisi ni kitu kizuri kwa hiyo unaweza kuona kumbe unapokuwa mwisho wa mwaka wa soka kuna zoezi la kutambua mchezaji mmoja mmoja na mnakuja kugundua kwamba ni kitu ambacho kinaongeza thamani kwenye ligi kwa ujumla.

“Maana unaona kwamba kila mchezaji anapambana ili aweze kupata zawadi ya mchezaji mmoja mmoja na mchezaji anapopambana inakuwa faida kwa timu yake na kitendo cha kutambua mchango wa mchezaji mmoja mmoja inakuwa fursa, faida kwa timu na faida kwa mashabiki wanaofuatilia,” alisema Kasongo.


Ushindani wa Fei na Aziz Ki ulikwenda mpaka siku ya mwisho ambapo kila mmoja aliingia uwanjani akiwa na mabao 18 kama ilivyokuwa kwa Matampi na Diarra ambao wote waliingia dimbani wakiwa na clean sheets 14.
Mwisho wa siku matokeo ya ushindi wa 4-1 walioupata Yanga dhidi ya Tanzania Prisons na matokeo ya suluhu baina ya Coastal na KMC yalitoa majibu ya vinyang’anyiro hivyo.

The post Kasongo asifu ushindani ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/30/kasongo-asifu-ushindani-ligi-kuu-nbc/feed/ 0
TPLB waimarisha ulinzi Kwa Mkapa https://www.greensports.co.tz/2024/04/18/tplb-waimarisha-ulinzi-kwa-mkapa/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/18/tplb-waimarisha-ulinzi-kwa-mkapa/#respond Thu, 18 Apr 2024 19:26:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10657 Na mwandishi wetuKuelekea mchezo wa Watani wa Jadi, Simba na Yanga Jumamosi hii, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imeeleza kuwa ulinzi madhubuti umeanza kuimarishwa katika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam utakapopigwa mchezo huo.Hayo yameelezwa leo Alhamisi jijini Dar na Ofisa Habari wa TPLB, Karim Boimanda akifafanua kuwa tayari wamezungumza na watu wa […]

The post TPLB waimarisha ulinzi Kwa Mkapa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kuelekea mchezo wa Watani wa Jadi, Simba na Yanga Jumamosi hii, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imeeleza kuwa ulinzi madhubuti umeanza kuimarishwa katika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam utakapopigwa mchezo huo.
Hayo yameelezwa leo Alhamisi jijini Dar na Ofisa Habari wa TPLB, Karim Boimanda akifafanua kuwa tayari wamezungumza na watu wa ulinzi na usalama ili kuweka usalama kwenye mchezo huo ambao huhudhuriwa na mashabiki wengi kutoka ndani na nje ya nchi.
“Niseme tu kwamba hadi sasa tumezungumza na watu wa ulinzi juu ya kudhibiti matukio mbalimbali kwenye mchezo huo mkubwa Afrika Mashariki na Kati na mambo hayo yanakwenda vizuri kuhakikisha ulinzi madhubuti wa hadhi ya mchezo huo unakuwepo,” alisema Boimanda.
Pia, Boimanda alifafanua kuhusu utaratibu wa kuingia uwanjani, mbali na wanaokata tiketi kawaida ambapo alisema: “Kutakuwa na mialiko ya watu maalumu ambao watapewa kadi kwa mtu husika na watoto nao wataingia kwa kutumia kadi vilevile.
Boimanda hata hivyo alisema kwamba kadi hizo zitatumika kwa walengwa tu na kama mlengwa atashindwa kuhudhuria basi atoe taarifa ili utaratibu mwingine uendelee lakini kadi yake haitatumika na mtu mwingine yoyote.”
Katika mchezo huo wa 112 wa ligi kuu baina ya timu hizo, Yanga itaikaribisha Simba kwenye Uwanja wa Mkapa unaoingiza mashabiki 60,000 na kutokana na wingi wa mashabiki, ulinzi huimarishwa ili kuepuka vurugu na kuweka sawa mambo mengine ya kiusalama.

The post TPLB waimarisha ulinzi Kwa Mkapa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/18/tplb-waimarisha-ulinzi-kwa-mkapa/feed/ 0
TPLB yasifu uwekezaji Simba, Yanga https://www.greensports.co.tz/2024/03/06/tplb-yasifu-uwekezaji-simba-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/06/tplb-yasifu-uwekezaji-simba-yanga/#respond Wed, 06 Mar 2024 06:06:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10053 Na mwandishi wetuMtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Almasi Kasongo (pichani) amesema mafanikio ya klabu za Simba na Yanga kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika yametokana na uwekezaji mzuri uliofanywa na timu hizo.Miamba hiyo ya soka nchini ni miongoni mwa timu nane Afrika zilizotinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada […]

The post TPLB yasifu uwekezaji Simba, Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Almasi Kasongo (pichani) amesema mafanikio ya klabu za Simba na Yanga kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika yametokana na uwekezaji mzuri uliofanywa na timu hizo.
Miamba hiyo ya soka nchini ni miongoni mwa timu nane Afrika zilizotinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufanya vizuri kwenye mechi za hatua ya makundi.
Mtendaji huyo ameieleza GreenSports Jumanne hii kuwa uwekezaji uliofanywa na timu hizo mbili ndio msingi mkubwa wa mafanikio ya timu hizo, jambo ambalo timu nyingine zinapaswa kuiga mfano huo.

“Tunajivunia mafanikio ya Simba na Yanga, wameendelea kulitangaza soka la Tanzania lakini hiyo imetokana na uwekezaji na uaminifu wa viongozi wao ambao umeyashawishi makampuni kujitokeza kuwekeza wakiamini watapata faida,” alisema Kasongo.


Kiongozi huyo alisema mbali na hilo lakini kufanya vizuri kwa timu hizo kumethibitisha maana halisi ya kazi wanayoifanya ya kuongoza mpira wa miguu nchini pamoja na kuweka taratibu na sheria na kanuni zinazouendesha mchezo huo pendwa duniani.
Kasongo amezitaka klabu nyingine kuwa na njaa ya mafanikio kama ilivyo Simba na Yanga ili kupambana na kupata nafasi ya kushiriki mashindano hayo ya kimataifa ambayo ndani yake yana faida lukuki.

The post TPLB yasifu uwekezaji Simba, Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/06/tplb-yasifu-uwekezaji-simba-yanga/feed/ 0