TFF - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 13 Jul 2026 20:05:52 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg TFF - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Dirisha la usajili ligi kuu lafunguliwa https://www.greensports.co.tz/2026/07/08/dirisha-la-usajili-ligi-kuu-lafunguliwa/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/08/dirisha-la-usajili-ligi-kuu-lafunguliwa/#respond Wed, 08 Jul 2026 20:27:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14782 Na mwandishi wetuDirisha la usajili wa wachezaji kwa ajili ya Ligi Kuu NBC msimu wa 2026-27 limefunguliwa rasmi Jumatatu Julai 6, 2026 na litafungwa Agosti 15, 2026 saa 5:59 usiku.Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyosainiwa na ofisa habari na mawasiliano wa shirikisho hilo, Cliford Ndimbo mbali na ligi kuu usajili […]

The post Dirisha la usajili ligi kuu lafunguliwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Dirisha la usajili wa wachezaji kwa ajili ya Ligi Kuu NBC msimu wa 2026-27 limefunguliwa rasmi Jumatatu Julai 6, 2026 na litafungwa Agosti 15, 2026 saa 5:59 usiku.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyosainiwa na ofisa habari na mawasiliano wa shirikisho hilo, Cliford Ndimbo mbali na ligi kuu usajili huo pia utahusisha wachezaji wa NBC Championship.
Wachezaji wengine watakaohusika katika usajili huo ni wale watakaoshiriki katika Ligi Daraja la Kwanza, Ligi ya Vijana (NBC-20) pamoja na Ligi Kuu ya Wanawake.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa mchezaji yeyote anaweza kuombewa usajili kwa njia tatu kupitia mfumo wa Fifa Connect.
Kwanza uhamisho wa jumla au wa mkopo kutoka klabu moja kwenda nyingine, pili ni kwa mchezaji anayeendelea na usajili wake kwa msimu mpya na tatu ni usajili wa mchezaji mpya kwenye mfumo.
Katika usajili huo nyaraka zinazotakiwa kuambatanishwa kwa usajili wa mchezaji mpya ambaye anaombewa usajili kwa mara ya kwanza ni hati ya kusafiria au kitambulisho cha uraia na mkataba wa ajira.
Nyaraka nyingine ni pamoja na barua ya uhamisho au kuachwa huru, cheti cha afya, picha ndogo ya mchezaji au passportsize na nakala ya malipo.
Kwa wachezaji wanaoendelea na usajili, kuhamishwa jumla au kwa mkopo wanapaswa kuambatanisha mkataba wa ajira, barua ya uhamisho au kuachwa huru, cheti cha afya, picha ya mchezaji na nakala ya malipo.
Kuhusu mchezaji anayeombewa usajili kutoka nje ya nchi anatakiwa kuambatanisha hati ya kusafiria, hati ya uhamisho wa kimataifa, mkataba wa ajira, kibali cha kuishi na kufanya kazi Tanzania, cheti cha afya, picha ya mchezaji na nakala ya malipo.
TFF imezitaka klabu kuambatanisha nyaraka sahihi na zilizokamilika na kukamilisha kila kitu kwa wakati kwa kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza.

The post Dirisha la usajili ligi kuu lafunguliwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/08/dirisha-la-usajili-ligi-kuu-lafunguliwa/feed/ 0
‘Marufuku kusambaza data mechi za TFF’ https://www.greensports.co.tz/2026/05/02/marufuku-kusambaza-data-mechi-za-tff/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/02/marufuku-kusambaza-data-mechi-za-tff/#respond Sat, 02 May 2026 11:47:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14573 Na mwandishi wetuShirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepiga marufuku kukusanya, kurekodi, kuchambua na kusambaza data za soka zinazotokana na mechi zilizo chini ya shirikisho hilo.Taarifa ya TFF iliyopatikana Alhamisi Aprili 30, 2026 ilidai kubaini baadhi ya watu na taasisi ambazo zinajihusisha na usambazaji na ukusanyaji wa data za mechi zikiwamo takwimu bila idhini.TFF imewakumbusha watu […]

The post ‘Marufuku kusambaza data mechi za TFF’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepiga marufuku kukusanya, kurekodi, kuchambua na kusambaza data za soka zinazotokana na mechi zilizo chini ya shirikisho hilo.
Taarifa ya TFF iliyopatikana Alhamisi Aprili 30, 2026 ilidai kubaini baadhi ya watu na taasisi ambazo zinajihusisha na usambazaji na ukusanyaji wa data za mechi zikiwamo takwimu bila idhini.
TFF imewakumbusha watu hao kuwa shirikisho hilo tayari lina mshirika wa data ambaye ni Kampuni ya Beta TQ ambayo ndiyo yenye haki ya kukusanya na kusambaza data hizo.
Katika taarifa hiyo TFF imemtaka mtu au taasisi yoyote inayotaka kusambaza data hizo iwasiliane na Kampuni ya Beta TQ ili kupata kibali na ruhusa ya kufanya hivyo.
TFF imetangaza kuwa itakuwa tayari kumchukulia hatua za kisheria yeyote atakayebainika kukusanya data moja kwa moja uwanjani, kutumia wafanyakazi au vifaa vya kufuatilia mechi.
Katazo hilo la TFF pia linamhusu yeyote atakayejihusisha na usambazaji, uuzaji au uchapishaji wa data zisizo rasmi atachukuliwa hatua za kisheria.

The post ‘Marufuku kusambaza data mechi za TFF’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/02/marufuku-kusambaza-data-mechi-za-tff/feed/ 0
TFF kukutana Kahama https://www.greensports.co.tz/2025/12/15/tff-kukutana-kahama/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/15/tff-kukutana-kahama/#respond Mon, 15 Dec 2025 09:30:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14177 Na mwandishi wetuShirikisho la Soka Tanzania (TFF) linatarajia kufanya mkutano mkuu wa mwaka ambao utafanyika mjini Kahama mkoani Shinyanga, Februari 21 mwakani.Taarifa ya TFF iliyopatikana Jumamosi Desemba 13, 2025 ilieleza kuwa mkutano huo wa kawaida wa 20 unafanyika kufuatia maamuzi ya kikao cha kamati ya utendaji ya shirikisho hilo kilichofanyika jijini Dar es Salaam.Kikao cha […]

The post TFF kukutana Kahama first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linatarajia kufanya mkutano mkuu wa mwaka ambao utafanyika mjini Kahama mkoani Shinyanga, Februari 21 mwakani.
Taarifa ya TFF iliyopatikana Jumamosi Desemba 13, 2025 ilieleza kuwa mkutano huo wa kawaida wa 20 unafanyika kufuatia maamuzi ya kikao cha kamati ya utendaji ya shirikisho hilo kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Kikao cha kamati ya utendaji kilichoongozwa na Rais wa TFF, Walace Karia kilipitia na kujadili mambo mbalimbali ikiwamo taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
Mkutano mkuu wa TFF utakaofanyika Kahama utakuwa wa kwanza tangu Karia achaguliwe tena kuliongoza shirikisho hilo baada ya uchaguzi uliofanyika Agosti mwaka huu na mgombea huyo kupata ushindi wa kishindo.
Uchaguzi huo hata hivyo ulipingwa na baadhi ya wadau wa soka ambao walipinga taratibu za uchaguzi na kitendo cha Karia kupitishwa kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo.
Baadhi ya wadau walipeleka suala hilo mahakamani wakidai uchaguzi huo ulikuwa batili wakitaka usitishwe na mchakato uanze upya ili watu wengine waruhusiwe kushindana na Karia kwenye sanduku la kura lakini mahakama ilizikataa hoja hizo na uchaguzi kufanyika kama kawaida.

The post TFF kukutana Kahama first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/15/tff-kukutana-kahama/feed/ 0
Karia ashinda uchaguzi TFF https://www.greensports.co.tz/2025/08/17/karia-ashinda-uchaguzi-tff/ https://www.greensports.co.tz/2025/08/17/karia-ashinda-uchaguzi-tff/#respond Sun, 17 Aug 2025 06:11:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13838 Na mwandishi wetuWallace Karia amechaguliwa kwa mara nyingine kuendelea kuliongoza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumamosi hii, Agosti 16, 2025 mkoani Tanga.Karia ameshinda nafasi hiyo kwa asilimia 100 akiwa mgombea pekee katika uchaguzi ambao ulipingwa Mahakama Kuu na jopo la mawakili lakini pingamizi hilo lilikwama na uchaguzi ukafanyika kama kawaida.Mawakili hao […]

The post Karia ashinda uchaguzi TFF first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Wallace Karia amechaguliwa kwa mara nyingine kuendelea kuliongoza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumamosi hii, Agosti 16, 2025 mkoani Tanga.
Karia ameshinda nafasi hiyo kwa asilimia 100 akiwa mgombea pekee katika uchaguzi ambao ulipingwa Mahakama Kuu na jopo la mawakili lakini pingamizi hilo lilikwama na uchaguzi ukafanyika kama kawaida.
Mawakili hao walikuwa wakipinga hatua ya Karia kupendekezwa peke yake kugombea nafasi hiyo na kutaka mchakato wa uchaguzi ufanyike upya ili kiongozi huyo apate wapinzani.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Karia alisema safari ya kuelekea katika uchaguzi huo haikuwa nyepesi na kuifananisha na kitendo cha kukiweka chuma kwenye moto ili kiwe imara.

“Changamoto tuliyokutana nayo ni kama kutukumbusha kwamba tuna kazi mbele yetu na ni lazima tukabiliane nayo,” alisema Karia ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).


Karia pia alisema kitendo cha yeye kuchaguliwa kwa mara nyingine kisionekane kama ni ushindi binafsi bali ni sawa na kupewa jukumu la kuendelea kufanya maboresho katika kusimamia soka nchini Tanzania.
Mara baada ya ushindi huo, Karia kwa mujibu wa katiba ya TFF, alimpitisha Athuman Nyamlani kuwa makamu wa rais wa shirikisho hilo, wadhifa ambao alikuwa akiushikilia.
Kwa upande wa wajumbe sita wa kamati ya utendaji ya TFF waliopita katika nafasi hizo ni Khalid Mohamed, Hosseah Lugano, Issa Bukuku, Salum Kulunge, Mohamed Aden na James Mhagama.
Hii ni mara ya tatu kwa Karia kuchaguliwa kuliongoza shirikisho hilo, mara ya kwanza aliingia madarakani mwaka 2017 kabla ya kuchaguliwa mara ya pili katika uchaguzi wa mwaka 2021.

The post Karia ashinda uchaguzi TFF first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/08/17/karia-ashinda-uchaguzi-tff/feed/ 0
TFF yaziita klabu kuomba leseni https://www.greensports.co.tz/2025/07/15/tff-yaziita-klabu-kuomba-leseni/ https://www.greensports.co.tz/2025/07/15/tff-yaziita-klabu-kuomba-leseni/#respond Tue, 15 Jul 2025 20:00:31 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13733 Na mwandishi wetuShirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kufunguliwa kwa maombi ya leseni ya klabu za ligi kuu kwa wanaume na wanawake pamoja na ligi ya Championship kwa msimu mpya wa 2025-26.Taarifa ya TFF iliyosainiwa na ofisa habari na mawasiliano wa shirikisho hilo Cliford Ndimbo ilieleza kuwa maombi hayo yatafanyika kwa njia ya mtandao kuanzia […]

The post TFF yaziita klabu kuomba leseni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kufunguliwa kwa maombi ya leseni ya klabu za ligi kuu kwa wanaume na wanawake pamoja na ligi ya Championship kwa msimu mpya wa 2025-26.
Taarifa ya TFF iliyosainiwa na ofisa habari na mawasiliano wa shirikisho hilo Cliford Ndimbo ilieleza kuwa maombi hayo yatafanyika kwa njia ya mtandao kuanzia Julai 14, 2025.
Waombaji wamekumbushwa kuwa mwisho wa kuwasilisha maombi hayo itakuwa ni Agosti 15, 2025 na yatawasilishwa kupitia mtandao https://clop.cafonline.com.
Katika taarifa hiyo, klabu zimetakiwa kuwasilisha myaraka na taarifa zote kwa wakati kwani hakutakuwa na muda wa ziada baada ya dirisha la maombi kufungwa.
TFF pia imetahadharisha kuwa klabu yoyote ambayo itakuwa inadaiwa na mchezaji haitopewa leseni ya kushiriki ligi.
Kuhusu klabu zinazoshiriki mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), TFF imefafanua kuwa kocha wa timu hiyo lazima awe na Diploma A ya CAF wakati msaidizi wake anatakiwa kuwa na Diploma B pia ya CAF.

The post TFF yaziita klabu kuomba leseni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/07/15/tff-yaziita-klabu-kuomba-leseni/feed/ 0
TFF yaruhusu Uwanja Liti kutumika https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/tff-yaruhusu-uwanja-liti-kutumika/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/tff-yaruhusu-uwanja-liti-kutumika/#respond Tue, 01 Apr 2025 19:22:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13179 Na mwandishi wetuShirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeufungulia Uwanja wa Liti mjini Singida baada ya kufanya maboresho yaliyokidhi vigezo vilivyosababisha kufungiwa kwa uwanja huo.Taarifa ya TFF iliyopatikana leo Jumanne na kusainiwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa shirikisho hilo, Clifford Ndimbo (pichani) ilizitaja sababu za kufungiwa uwanja huo kuwa ni miondombinu yake kutofaa.Uwanja huo kwa […]

The post TFF yaruhusu Uwanja Liti kutumika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeufungulia Uwanja wa Liti mjini Singida baada ya kufanya maboresho yaliyokidhi vigezo vilivyosababisha kufungiwa kwa uwanja huo.
Taarifa ya TFF iliyopatikana leo Jumanne na kusainiwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa shirikisho hilo, Clifford Ndimbo (pichani) ilizitaja sababu za kufungiwa uwanja huo kuwa ni miondombinu yake kutofaa.
Uwanja huo kwa mujibu wa TFF umekaguliwa na kuonekana umekidhi vigezo vya kikanuni baada ya marekebisho yanayodaiwa kufanywa na wamiliki wa uwanja huo.
TFF imeendelea kuzikumbusha klabu kwa kushirikiana na wamiliki wa viwanja hivyo kuhakikisha wanaboresha na kutunza miundombinu yake ili viweze kutumika kwa mechi za ligi.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF uboreshaji wa viwanja unasaidia kuongeza ushindani pamoja na thamani ya ligi.
Katika siku za hivi karibuni, TFF imekuwa ikivifungia viwanja kadhaa kutokana na mapungufu mbalimbali kwa kutokidhi vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.
Miongoni mwa viwanja vilivyofungiwa na TFF ni ule wa Jamhuri mjini Dodoma ambao pia umeshafunguliwa baada ya kufanya maboresho yaliyozingatia kanuni na sheria za mchezo wa soka.

The post TFF yaruhusu Uwanja Liti kutumika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/tff-yaruhusu-uwanja-liti-kutumika/feed/ 0
Karia awapongeza viongozi wapya Iringa https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/karia-awapongeza-viongozi-wapya-iringa/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/karia-awapongeza-viongozi-wapya-iringa/#respond Tue, 01 Apr 2025 10:52:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13172 Na mwandishi wetuRais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Walace Karia amewapongeza viongozi wapya wa Chama cha Soka Iringa (IRFA) walioachaguliwa hivi karibuni katika mkutano mkuu wa uchaguzi.Katika taarifa iliyosainiwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo imewataja viongozi hao kuwa ni Cyprian Kuyava aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti na Joel Musiba (makamu mwenyekiti).Wengine ni […]

The post Karia awapongeza viongozi wapya Iringa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Walace Karia amewapongeza viongozi wapya wa Chama cha Soka Iringa (IRFA) walioachaguliwa hivi karibuni katika mkutano mkuu wa uchaguzi.
Katika taarifa iliyosainiwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo imewataja viongozi hao kuwa ni Cyprian Kuyava aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti na Joel Musiba (makamu mwenyekiti).
Wengine ni Abousufian Sillia (mjumbe wa mkutano mkuu), Davis Wapalila, Rehema Mhehe na Victoria Mwenda ambao wamechaguliwa katika nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji.
Karia amewataka viongozi hao kusimamia maendeleo ya soka mkoani Iringa akiwataka kuwashirikisha wadau mbalimbali kwa maslahi ya soka la Iringa na Tanzania kwa ujumla.
Wakati huo huo, TFF imeufungulia Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ambao sasa utaruhusiwa kutumiwa kwa ajili ya mechi za ligi baada ya kufanya marekebisho kama ilivyotakiwa kikanuni na sheria za soka.
Uwanja huo ulifungiwa kutokana na miundombinu yake kutokidhi matakwa ya kanuni lakini baada ya kukaguliwa imebainika kuwa marekebisho yaliyofanywa yamekidhi vigezo.
TFF imewasisitiza viongozi wa klabu kuhakikisha wanaboresha mazingira ya viwanja vyao vya nyumbani kwa kushirikiana na wamiliki wa viwanja hivyo ili kukidhi vigezo vinavyotakiwa kwa mujibu wa kanuni.

The post Karia awapongeza viongozi wapya Iringa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/karia-awapongeza-viongozi-wapya-iringa/feed/ 0
TFF yawanyooshea kidole mawakala https://www.greensports.co.tz/2024/12/04/tff-yawanyooshea-kidole-mawakala/ https://www.greensports.co.tz/2024/12/04/tff-yawanyooshea-kidole-mawakala/#respond Wed, 04 Dec 2024 06:36:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12324 Na mwandishi wetuShirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa angalizo kwa mawakala wa soka nchini na kubainisha kuwa wanaotambulika ni wale tu wenye leseni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).Taarifa ya TFF iliyopatikana Jumanne hii na kusainiwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa shirikisho hilo, Cliford Ndimbo (pichani) ilitoa tahadhari kuwa mbele ya kamati zake […]

The post TFF yawanyooshea kidole mawakala first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa angalizo kwa mawakala wa soka nchini na kubainisha kuwa wanaotambulika ni wale tu wenye leseni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Taarifa ya TFF iliyopatikana Jumanne hii na kusainiwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa shirikisho hilo, Cliford Ndimbo (pichani) ilitoa tahadhari kuwa mbele ya kamati zake haitotambua uwakilishi wowote wa wakala asiye na leseni.
“TFF haitotambua uwakilishi wowote kwa mchezaji ikiwamo uhamisho na mashauri mengineyo kwa wakala ambaye hana leseni ya Fifa,” ilifafanua taarifa hiyo.
Ndimbo ameibainisha kuwa kwa mujibu wa kanuni za Fifa ni wakala wa shirikisho hilo pekee ambaye anaweza kufanya shughuli za uwakala katika mchezo wa soka.
Tarifa hiyo pia imewataka wanaotaka kufanya shughuli za uwakala kuhakikisha wanafanya mtihani wa uwakala na kufaulu ili wapewe leseni na Fifa. Mtihani wa uwakala wa Fifa hufanyika mara mbili kwa mwaka.
TFF pia imetoa onyo kwa yeyote anayefanya shughuli za uwakala katika soka bila ya kuwa na leseni kuwa shirikisho hilo halitosita kupeleka taarifa za mtu huyo Fifa ili achukuliwe hatua.
Hadi sasa Tanzania ina mawakala wa soka saba tu wanaotambuliwa na Fifa ambao ni Ismail Hassan, Nassir Mjandari, Latifa Idd Pagal, Eliya Samwel Rioba, Benjamin Masige, Erick Mavike na Hadji Shaaban Omar.

The post TFF yawanyooshea kidole mawakala first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/12/04/tff-yawanyooshea-kidole-mawakala/feed/ 0
Majaliwa: Klabu zisizo na viwanja bora zitengwe https://www.greensports.co.tz/2024/07/16/majaliwa-klabu-zisizo-na-viwanja-bora-zitengwe/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/16/majaliwa-klabu-zisizo-na-viwanja-bora-zitengwe/#respond Tue, 16 Jul 2024 07:08:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11622 Na mwandishi wetuWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameagiza klabu za soka ambazo hazina viwanja vilivyo katika ubora utakaoidhinishwa na Shirikisho la Soka Tanania (TFF) ziwekwe pembeni.Kiongozi huyo wa serikali, ametoa agizo hilo Jumatatu hii wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtambo wa Teknolojia ya VAR iliyoandaliwa na Kampuni ya Azam […]

The post Majaliwa: Klabu zisizo na viwanja bora zitengwe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameagiza klabu za soka ambazo hazina viwanja vilivyo katika ubora utakaoidhinishwa na Shirikisho la Soka Tanania (TFF) ziwekwe pembeni.
Kiongozi huyo wa serikali, ametoa agizo hilo Jumatatu hii wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtambo wa Teknolojia ya VAR iliyoandaliwa na Kampuni ya Azam Media na kufanyika katika viwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Akisitiza umuhimu wa viwanja bora, Waziri Mkuu aliwataka TFF kuwapa masharti wanachama wao wanaomiliki viwanja na atakayeshindwa kutimiza masharti hayo awekwe pembeni
Alisema kwamba Tanzania inahitaji kufika mbali kwenye viwango vya ubora Afrika na kutaka washindane na nchi za Misri na Morocco ambazo zimepiga hatua kubwa katika ubora barani Afrika.
Waziri Mkuu alisema serikali imeipa kipaumbele michezo na hilo linadhihirishwa na namna ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa mchango wake katika sekta hiyo na kuondoa ile dhana ya Tanzania kichwa cha mwendawazimu.
Akiizungumzia teknolojia ya VAR alisema kwamba itasaidia kupunguza malalamiko kwa timu pamoja na kupunguza makosa ya kibinadamu kwa waaamuzi na kuwafanya wawe makini katika kazi yao.
Teknolojia ya VAR au Video Assistance Referee hutumika kwa lengo la kumsaidia mwamuzi kujiridhisha na maamuzi hasa yale yenye utata kwa kuyarejea kupitia picha za video za mechi husika.
Teknolojia hiyo ambayo imekuwa ikitumika katika Ligi Kuu England (EPL), Kombe la Dunia 2018 na 2022 na Euro 2024 hata hivyo imekuwa ikilalamikiwa kwa kuchelewesha kutoa maamuzi na hata maamuzi yake wakati mwingine kuonekana yamejaa utata.
Ni hivi karibuni tu katika fainali za soka za Euro 2024 nchini Ujerumani, kocha wa Uholanzi, Ronald Koeman alisema kwamba VAR inaua soka.

The post Majaliwa: Klabu zisizo na viwanja bora zitengwe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/16/majaliwa-klabu-zisizo-na-viwanja-bora-zitengwe/feed/ 0
TFF yatangaza kuanza kwa usajili https://www.greensports.co.tz/2024/06/15/tff-yatangaza-kuanza-kwa-usajili/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/15/tff-yatangaza-kuanza-kwa-usajili/#respond Sat, 15 Jun 2024 08:50:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11335 Na mwandishi wetuShirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza rasmi kufunguliwa kwa dirisha la usajili kuelekea msimu ujao wa 2024-25, ambapo litafunguliwa Juni 15 Jumamosi hii na kufungwa Agosti 15, mwaka huu.Taarifa hiyo iliyotolewa Ijumaa hii na shirikisho hilo imefafanua kuwa dirisha hilo ni kwa ajili ya Ligi Kuu NBC, Ligi ya Championship, Ligi Daraja la […]

The post TFF yatangaza kuanza kwa usajili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza rasmi kufunguliwa kwa dirisha la usajili kuelekea msimu ujao wa 2024-25, ambapo litafunguliwa Juni 15 Jumamosi hii na kufungwa Agosti 15, mwaka huu.
Taarifa hiyo iliyotolewa Ijumaa hii na shirikisho hilo imefafanua kuwa dirisha hilo ni kwa ajili ya Ligi Kuu NBC, Ligi ya Championship, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Kuu ya Wanawake.
TFF pia imesisitiza kuwa hakutakuwa na muda wa ziada wa usajili baada ya kufungwa kwa dirisha hilo, hivyo imezitaka klabu zote kuzingatia muda huo.
Na pia katika taarifa hiyo, shirikisho hilo limeweka wazi kuwa dirisha dogo la usajili msimu ujao litakuwa wazi kuanzia Desemba 16, mwaka huu na kufikia ukingoni Januari 15, mwakani.
Wakati TFF ikitoa taarifa hiyo tayari klabu kongwe nchini za Simba na Yanga zimeanza kuhusishwa na wachezaji kadhaa wa kuwasajili wakiwamo wa kuwaaacha.

The post TFF yatangaza kuanza kwa usajili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/15/tff-yatangaza-kuanza-kwa-usajili/feed/ 0