Serie A - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 23 Apr 2025 17:15:00 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.5 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Serie A - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Papa Francis afariki, mechi Serie A zaahirishwa https://www.greensports.co.tz/2025/04/21/papa-francis-afariki-mechi-serie-a-zaahirishwa/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/21/papa-francis-afariki-mechi-serie-a-zaahirishwa/#respond Mon, 21 Apr 2025 12:21:12 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13289 Vatican City, VaticanMechi nne za ligi kuu ya soka ya Italia maarufu, Serie A zimeahirishwa kufuatia kifo cha Papa Francis ambaye amefariki leo Jumatatu Aprili 21 akiwa na umri wa miaka 88.Taarifa ya kifo hicho imetangazwa rasmi na mamlaka za Vatican leo ikiwa ni siku kadhaa zimepita baada ya kiongozi huyo mkuu wa Kanisa Katoliki […]

The post Papa Francis afariki, mechi Serie A zaahirishwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Vatican City, Vatican
Mechi nne za ligi kuu ya soka ya Italia maarufu, Serie A zimeahirishwa kufuatia kifo cha Papa Francis ambaye amefariki leo Jumatatu Aprili 21 akiwa na umri wa miaka 88.
Taarifa ya kifo hicho imetangazwa rasmi na mamlaka za Vatican leo ikiwa ni siku kadhaa zimepita baada ya kiongozi huyo mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kutoka hospitali alikolazwa kwa takriban wiki tano.
Kifo hicho kimekuja ikiwa ni siku moja baada ya kiongozi huyo kuonekana Jumapili ya Pasaka akiwa kwenye kiti cha magurudumu na kuwabariki waumini wa kikristo.
Mechi ambazo zimeahirishwa ni kati ya Torino dhidi ya Udinese, Cagliari na Fiorentina, Genoa na Lazio na Parma dhidi ya Juventus.
Bodi inayosimamia soka la Italia imetangaza uamuzi huo na kuahidi kuzipangia siku nyingine mechi hizo badala ya leo Jumatatu ambayo kwa kawaida ni siku mapumziko nchini Italia.
Papa Francis aliteuliwa kuongoza kanisa katoliki duniani mwaka 2013 akichukua nafasi ya Papa Benedict XVI aliyeushtua ulimwengu baada ya kuamua kung’atuka katika cheo hicho.
Kihistoria Papa Francis anatokea Argentina, alifahamika kwa kipindi kirefu kuwa mpenda soka na wakati akiwa kijana mdogo alikuwa shabiki wa timu ya San Lorenzo ya Argentina
Kutokana na msiba huo mkubwa klabu kadhaa za soka nchini Italia zimetuma salamu za rambirambi mojawapo ikiwa na klabu ya Roma ambayo imeeleza kuwa jiji lote la Roma na dunia kwa ujumla imesikitishwa na msiba huo.

“Imani yake, uvumilivu, ujasiri na kujitoa kwake ni mambo yaliyogusa mioyo ya mamilioni ya watu na kumfanya awe kielelezo cha kiroho katika zama zetu,” ilieleza taarifa ya klabu ya Roma.

The post Papa Francis afariki, mechi Serie A zaahirishwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/21/papa-francis-afariki-mechi-serie-a-zaahirishwa/feed/ 0
Kocha atimuliwa kwa kumpiga kichwa mchezaji https://www.greensports.co.tz/2024/03/12/kocha-atimuliwa-kwa-kumpiga-kichwa-mchezaji/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/12/kocha-atimuliwa-kwa-kumpiga-kichwa-mchezaji/#respond Tue, 12 Mar 2024 06:36:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10146 Milan, ItaliaKlabu ya Lecce ya Italia imemfuta kazi kocha wake, Roberto D’Aversa (pichani) baada ya kocha huyo kumpiga kichwa mshambuliaji wa Verona, Thomas Henry katika mechi ya Serie A ambayo Lecce ililala kwa bao 1-0.D’Aversa, 48, na Henry kila mmoja alipewa kadi nyekundu baada ya tukio hilo ambalo lilitokana na mzozo ulioibuka mara baada ya […]

The post Kocha atimuliwa kwa kumpiga kichwa mchezaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Milan, Italia
Klabu ya Lecce ya Italia imemfuta kazi kocha wake, Roberto D’Aversa (pichani) baada ya kocha huyo kumpiga kichwa mshambuliaji wa Verona, Thomas Henry katika mechi ya Serie A ambayo Lecce ililala kwa bao 1-0.
D’Aversa, 48, na Henry kila mmoja alipewa kadi nyekundu baada ya tukio hilo ambalo lilitokana na mzozo ulioibuka mara baada ya mwamuzi kumaliza mchezo.
Akizungumza na waandishi wa habari baadaye, D’Aversa alikiri mwenyewe kwamba kosa alilolifanya halisameheki na siku moja baada ya mechi hiyo iliyochezwa Jumapili uongozi ulitangaza kumfuta kazi.
Klabu ya Lecce ilieleza kwa kifupi kuwa uamuzi wa kumfuta kazi kocha huyo ulitokana na tukio lililojitokeza baada ya mechi.
Kipigo hicho kinaifaya Lecce kushuka hadi nafasi ya 15 kwenye Ligi Kuu Italia maarufu Serie A ikiwa nafasi mbili nyuma ya Verona na hivyo kulisogelea janga la kushuka daraja.
Mambo kwa ujumla si mazuri kwa klabu ya Lecce kwenye Serie A kwa kuwa hadi sasa imeshinda mechi moja tu kati ya 12 za ligi hiyo kubwa nchini Italia ikiwa imepoteza tisa kati ya hizo na nyingine kutoa sare.
D’Aversa ambaye amewahi kuzinoa timu za Virtus Lanciano, Parma na Sampdoria alikabidhiwa jukumu la kuinoa timu hiyo majira ya kiangazi mwaka jana akichukua nafasi ya Marco Baroni.

The post Kocha atimuliwa kwa kumpiga kichwa mchezaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/12/kocha-atimuliwa-kwa-kumpiga-kichwa-mchezaji/feed/ 0
Juve yapokwa pointi 10 Serie A https://www.greensports.co.tz/2023/05/23/juve-yapokwa-pointi-10-serie-a/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/23/juve-yapokwa-pointi-10-serie-a/#respond Tue, 23 May 2023 05:41:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6253 Milan, ItaliaJuventus imenyang’anya pointi 10 katika Ligi ya Serie A kwa makosa ya kwenda kinyume na taratibu za usajili na hivyo kupoteza nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.Januari mwaka huu, klabu hiyo ilinyang’anya pointi 15 kwa kosa hilo lakini mwezi uliopita, uamuzi huo ulibatilishwa na mahakama ya juu ya michezo nchini humo […]

The post Juve yapokwa pointi 10 Serie A first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Milan, Italia
Juventus imenyang’anya pointi 10 katika Ligi ya Serie A kwa makosa ya kwenda kinyume na taratibu za usajili na hivyo kupoteza nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Januari mwaka huu, klabu hiyo ilinyang’anya pointi 15 kwa kosa hilo lakini mwezi uliopita, uamuzi huo ulibatilishwa na mahakama ya juu ya michezo nchini humo baada ya Juve kukata rufaa.
Baada ya shauri hilo kupitiwa upya hatimaye uamuzi mpya wa kuinyang’anya Juve pointi 10 ulifikiwa jana Jumatatu na mahakama hiyo saa kadhaa kabla ya timu hiyo kufungwa mabao 4-1 na Empoli.
Kwa uamuzi huo, Juve sasa inashuka hadi nafasi ya saba kwenye Serie A na kuitoa rasmi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo ni michuano mikubwa na yenye hadhi kwa ngazi ya klabu.

“Ni hali mbaya imetokea, uamuzi umekuja dakika 10 kabla ya mechi kumalizika,” alisema kocha wa Juve, Massimiliano Allegri.


Katika maombi yake ya kutaka uamuzi huo upitiwe upya, Juve pia ilitaka viongozi wake waliofungiwa wafutiwe makosa yao akiwamo aliyekuwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Pavel Nedved ambaye yeye na wenzake awali walifungiwa miezi minane kujihusisha na soka lakini sasa wamefutiwa adhabu.
Maofisa wengine wa klabu hiyo waliofutiwa adhabu ni Assia Grazioli Venier, Caitlin Mary Hughes, Paolo Garimberti, Enrico Vellano, Daniela Marilungo na Francesco Roncaglio lakini mwenyekiti wa zamani, Andrea Agnelli, ofisa mtendaji mkuu Maurizio Arrivabene pamoja na wakurugenzi wa michezo, Federico Cherubini na Fabio Paratici wataendelea kutumikia adhabu.
Baada ya adhabu ya kunyang’anywa pointi 10 kutolewa taarifa ya Juve iliyokuja baadaye ilieleza kuwa viongozi wataijadili taarifa hiyo baada ya kuisoma na kisha kuangalia taratibu za kukata rufaa.
Klabu ya Napoli tayari imetangazwa bingwa wa Serie A msimu huu wakati Juve kabla ya uamuzi wa kunya’anywa pointi 10 kufikiwa ilikuwa nafasi ya pili ikiachwa kwa tofauti ya pointi 17.
Uamuzi wa kuinyang’anya Juve pointi unatokana na uchunguzi wa sakata la miaka miwili kati ya 2019 hadi 2021 ambapo klabu hiyo inadaiwa kucheza michezo michafu katika usajili kwa kuficha baadhi ya nyaraka ikidaiwa kujipatia Euro 60 milioni.

The post Juve yapokwa pointi 10 Serie A first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/23/juve-yapokwa-pointi-10-serie-a/feed/ 0
Napoli yatwaa taji Serie A https://www.greensports.co.tz/2023/05/05/napoli-yatwaa-taji-serie-a/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/05/napoli-yatwaa-taji-serie-a/#respond Fri, 05 May 2023 08:08:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6022 Naples, ItaliaKlabu ya Napoli ya Italia hatimaye imebeba taji la Ligi Kuu Italia au Serie A ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 33 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Udinese jana Alhamisi usiku.Alikuwa ni Victor Osimhen aliyeifungia Napoli bao la kusawazisha lililoihakikishia timu hiyo pointi moja waliyohitaji ili kutangazwa mabingwa […]

The post Napoli yatwaa taji Serie A first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Naples, Italia
Klabu ya Napoli ya Italia hatimaye imebeba taji la Ligi Kuu Italia au Serie A ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 33 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Udinese jana Alhamisi usiku.
Alikuwa ni Victor Osimhen aliyeifungia Napoli bao la kusawazisha lililoihakikishia timu hiyo pointi moja waliyohitaji ili kutangazwa mabingwa wa Seria A msimu wa 2022-23 baada ya kuwa nyuma kwa bao la mapema la Udinese lililofungwa na Sandi Lovric.
Napoli sasa watacheza mechi tano zilizobaki za ligi hiyo kwa raha zao wakiwania kuboresha rekodi za ushindi kwani tayari taji la Serie A lipo kwenye himaya yao na tayari jiji la Naples limeshalipuka kwa shangwe na nderemo za mashabiki tangu jana usiku.
Mara ya mwisho Napoli ilibeba taji la Serie A mwaka 1990 ikiwa na gwiji wa soka duniani na nahodha wa zamani wa Argentina, Diego Maradona baada ya kubeba taji lao la kwanza miaka mitatu kabla.
“Kuwaona watu wa Napoli wakiwa na furaha inatosha kukupa fikra za hali waliyo nayo kwa sasa katika fikra zao,” alisema kocha wa Napoli, Luciano Spalletti.

“Hawa watu watalilikumbuka tukio hili pale maisha yanapokuwa magumu, wana kila sababu ya kushangilia jambo hili, unajiona katika hali ya utulivu kwa kuwapa tukio la furaha ya aina hii,” alisema Spalletti.


Napoli mataji yake ya mwisho yalipatikana wakati za zama za Maradona ambaye pia alikuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Argentina na ambaye uwanja wa klabu hiyo umepewe jina lake, mataji hayo yalibebwa mwaka 1987 na 1990.
Baada ya mafanikio hayo, Napoli iliangukia katika majanga ya kiuchumi ikafilisika na kushuka hadi ligi ya chini ya Serie C na ingawa waliwahi kubeba taji la Coppa Italia mara tatu, kiu ya mashabiki wa timu hiyo ilikuwa ni kubeba taji la Serie A, kiu ambayo hatimaye imekatwa rasmi jana usiku huku mashabiki zaidi ya 10,000 wakisafiri kutoka Naples ili kuishuhudia timu hiyo ikibeba taji hilo baada ya sare ya ugenini na wengine wakifurahia wakiwa nyumbani..

The post Napoli yatwaa taji Serie A first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/05/napoli-yatwaa-taji-serie-a/feed/ 0