Saka - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 01 Apr 2025 19:32:53 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Saka - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Saka yuko fiti kuikabili Fulham https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/saka-yuko-fiti-kuikabili-fulham/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/saka-yuko-fiti-kuikabili-fulham/#respond Tue, 01 Apr 2025 10:56:03 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13174 London, EnglandKocha wa Arsenal, Mikel Arteta amethibitisha kwamba nyota wake, Bukayo Saka aliyekuwa majeruhi yuko tayari kwa kazi wakati wakisubiri kuikabili Fulham Jumanne hii, Aprili Mosi 2025.Saka ambaye alipata majeraha ya misuli na kufanyiwa upasuaji Desemba mwaka jana, amekuwa nje ya kikosi cha Arsenal lakini kwa sasa yuko fiti na anatarajia kuikabili Fulham.Mshambuliaji huyo mwenye […]

The post Saka yuko fiti kuikabili Fulham first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amethibitisha kwamba nyota wake, Bukayo Saka aliyekuwa majeruhi yuko tayari kwa kazi wakati wakisubiri kuikabili Fulham Jumanne hii, Aprili Mosi 2025.
Saka ambaye alipata majeraha ya misuli na kufanyiwa upasuaji Desemba mwaka jana, amekuwa nje ya kikosi cha Arsenal lakini kwa sasa yuko fiti na anatarajia kuikabili Fulham.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, aliumia misuli ya mguu wa kulia katika kipindi cha kwanza wakati wa mechi na Crystal Palace, mechi ambayo Arsena ilitoka na ushindi wa mabao 5-1.
Kikosi cha Arsenal licha ya kuonesha makali yake msimu huu lakini kimekuwa kikiandamwa na janga la wachezaji majeruhi wakiwamo Kai Havert, Gabriel Martinelli na Gabriel Jesus ambao wamekuwa nje ya kikosi hicho kwa muda sasa.
Mchezaji mwingine ambaye naye ni majeruhi ni Riccardo Calafiori ambaye atakuwa nje kwa wiki kadhaa baada ya kuumia wakati akiiwakilishi timu ya taifa ya Italia.
Arsenal kwa sasa inapambana kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na Ligi Kuu England (EPL) ikiwa nafasi ya pili, imeachwa na vinara Liverpool kwa tofauti ya pointi 12.
Kupona kwa Saka kunakuwa faraja kubwa kwa timu hiyo kwenye EPL pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo Aprili 8 timu hiyo itaumana na Real Madrid katika mechi ya pili ya hatua ya robo fainali.

The post Saka yuko fiti kuikabili Fulham first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/saka-yuko-fiti-kuikabili-fulham/feed/ 0
Saka nje miezi mitatu https://www.greensports.co.tz/2024/12/29/saka-nje-miezi-mitatu/ https://www.greensports.co.tz/2024/12/29/saka-nje-miezi-mitatu/#respond Sun, 29 Dec 2024 08:28:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12529 London, EnglandNyota wa Arsenal, Bukayo Saka amefanyiwa upasuaji baada ya kupata majeraha ya misuli na kwa mujibu wa kocha, Mikel Arteta huenda mchezaji huyo akawa nje ya uwanja kwa takriban miezi mitatu.Arteta alithibitisa hilo hivi karibuni na kufafanua kwamba Saka aliumia misuli ya mguu wa kulia wakati wa mechi dhidi ya Crystal Palace, mechi ambayo […]

The post Saka nje miezi mitatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Nyota wa Arsenal, Bukayo Saka amefanyiwa upasuaji baada ya kupata majeraha ya misuli na kwa mujibu wa kocha, Mikel Arteta huenda mchezaji huyo akawa nje ya uwanja kwa takriban miezi mitatu.
Arteta alithibitisa hilo hivi karibuni na kufafanua kwamba Saka aliumia misuli ya mguu wa kulia wakati wa mechi dhidi ya Crystal Palace, mechi ambayo Arsenal ilishinda 5-1.
Kocha huyo alifafanua kwamba Saka alifuata taratibu za kawaida kimatibabu na kila kitu kilikwenda vizuri lakini akakikiri kwamba kwa bahati mbaya mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja kwa wiki nyingi tu.
Alipotakiwa kufafanua zaidi muda ambao Saka anatarajia kurudi dimbani Arteta alionekana hana uhakika badala yake alishikilia msimamo wake kwamba ni baada ya wiki nyingi.

“Nafikiri itakuwa zaidi ya miezi miwili, sijui kwa uhakika itachukua muda gani hasa, itategemea alipoumia na jinsi atakavyoanza kupona, wiki ya kwanza au zaidi, ngoja tuone ni vigumu kusema,” alisema Arteta.


Saka ni mmoja wa wachezaji tegemeo kwenye kikosi cha Arsenal hivyo kuumia kwake huenda kukaathiri mbio za timu hiyo katika kulisaka taji la Ligi Kuu England (EPL) msimu huu wa 2024-25.
Arsenal kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye ligi hiyo nyuma ya vinara Liverpool kwa tofauti ya pointi sita wakati Man City ambao ni washindani wengine wa taji hilo kwa miaka kadhaa sasa, hali yao msimu huu si nzuri.

The post Saka nje miezi mitatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/12/29/saka-nje-miezi-mitatu/feed/ 0
Arteta akiri kuumia Saka pigo Arsenal https://www.greensports.co.tz/2023/10/04/arteta-akiri-kuumia-saka-pigo-arsenal/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/04/arteta-akiri-kuumia-saka-pigo-arsenal/#respond Wed, 04 Oct 2023 08:26:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7940 Lens, UfaransaKocha wa Arsenal, Mikel Arteta amekiri kuumia kwa Bukayo Saka (pichani) ni jambo lililoleta hofu ingawa hajutii kumpanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana Jumanne dhidi ya Lens, mechi ambayo Arsenal ililala kwa mabao 2-1.Saka aliumia katika mechi mbili za Ligi Kuu England lakini katika hali ambayo haikutarajiwa alipangwa katika mechi ya […]

The post Arteta akiri kuumia Saka pigo Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Lens, Ufaransa
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amekiri kuumia kwa Bukayo Saka (pichani) ni jambo lililoleta hofu ingawa hajutii kumpanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana Jumanne dhidi ya Lens, mechi ambayo Arsenal ililala kwa mabao 2-1.
Saka aliumia katika mechi mbili za Ligi Kuu England lakini katika hali ambayo haikutarajiwa alipangwa katika mechi ya jana kwenye dimba la Bollaert-Delelis na kucheza kwa dakika 34 kabla ya kutolewa akiwa na maumivu ya misuli.
Mchezaji huyo ndiye aliyepika bao la kwanza la Arsenal lililofungwa na Gabriel Jesus lakini Lens walisawazisha kupitia Adrien Thomasson kabla ya kuongeza la pili lililofungwa na Elye Wahi na kuwa kipigo cha kwanza kwa Arsenal tangu kuanza kwa msimu huu.
Saka ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya England anatarajia kufanyiwa vipimo ili kujua ukubwa wa majeraha aliyonayo lakini ana uwezekano mdogo wa kucheza mechi ya Jumapili ya Ligi Kuu England (EPL) dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Man City.
“Alijaribu kupiga mpira kwa nyuma katika kipindi cha kwanza na akajikuta katika hali tofuati, ni tatizo la misuli, alijisikia vibaya na tukalazimika kumtoa nje,” alisema Arteta.

“Hatuna tunachojua zaidi ya hilo lakini ni wazi lilikuwa tatizo kubwa la kumzuia kuendelea kucheza na hilo ni dhahiri kwamba linatupa hofu, sina ninachojua kuhusu mechi ijayo, sijui,” alisema Arteta.


Alipoulizwa kama anajuta kumpanga Saka katika mechi hiyo, Arteta alisema, “hapana, ni maumivu aliyoyapata siku nyingine na akawa vizuri kabisa, ni tukio la kupiga mpira kwa nyuma ambalo linaweza kusababisha aina hii ya maumivu, ngoja tujue ukubwa wa tatizo.”
“Maumivu yaliyopita yalikuwa ya kawaida, hakukosa mechi nyingi, tulimpumzisha katika mechi na Brentford, hivyo ndivyo ilivyokuwa,” alisema Arteta.

The post Arteta akiri kuumia Saka pigo Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/04/arteta-akiri-kuumia-saka-pigo-arsenal/feed/ 0
Haaland abeba tuzo ya PFA https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/haaland-abeba-tuzo-ya-pfa/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/haaland-abeba-tuzo-ya-pfa/#respond Wed, 30 Aug 2023 08:06:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7579 London, EnglandMshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland ametwaa tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa Chama cha Wanasoka Profesheno (PFA), tuzo aliyokabidhiwa Jumanne hii usiku.Haaland alikuwa na msimu mzuri wa 2022-23 akifunga mabao 52 katika mechi 53 za mashindano tofauti na kuiwezesha City kubeba taji la Ligi Kuu England (EPL), FA na Ligi ya Mabingwa […]

The post Haaland abeba tuzo ya PFA first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland ametwaa tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa Chama cha Wanasoka Profesheno (PFA), tuzo aliyokabidhiwa Jumanne hii usiku.
Haaland alikuwa na msimu mzuri wa 2022-23 akifunga mabao 52 katika mechi 53 za mashindano tofauti na kuiwezesha City kubeba taji la Ligi Kuu England (EPL), FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 23, hadi kutwaa tuzo hiyo, amewashinda nyota wenzake wa Man City, Kevin de Bruyne na John Stones na Martin Odegaard na Bukayo Saka wa Arsenal pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Harry Kane ambaye kwa sasa anaichezea Bayern Munich.
Tuzo hiyo ni mwanzo mzuri kwa Haaland katika msimu huu wa 2023-24 akiwa ametoka kutwaa tuzo ya mwanasoka bora wa msimu wa EPL kwa wanaume, tuzo aliyopewa mwezi Mei na Chama cha Waandishi wa Soka England.
Katika tuzo ya PFA, Saka wa Arsenal yeye alitwaa tuzo ya mwaka ya Young Player ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo baada ya kuingia katika kinyang’anyiro hicho kwa mara nne mfululizo.
Kwa upande wa wanawake tuzo ya PFA imechukuliwa na mshambuliaji wa Aston Villa, Rachel Daly ambaye pia ndiye aliyemaliza msimu uliopita akiwa mfungaji bora wa ligi ya wanawake akiwa na mabao 22 wakati tuzo ya mwaka ya Young Player imechukuliwa na Lauren James wa Chelsea.

The post Haaland abeba tuzo ya PFA first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/haaland-abeba-tuzo-ya-pfa/feed/ 0
Southgate ampamba Saka https://www.greensports.co.tz/2023/03/27/southgate-ampamba-saka/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/27/southgate-ampamba-saka/#respond Mon, 27 Mar 2023 08:26:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5612 London, EnglandKocha wa England, Gareth Southgate amesema mshambuliaji wa timu hiyo, Bukayo Saka ameendelea kuwa mwenye ‘shauku ya ajabu’ ya mafanikio jambo linalosaidia kupandisha kiwango chake msimu huu.Saka ambaye pia anaichezea Arsenal, jana Jumapili aliisaidia England kupata bao la kwanza kabla ya yeye mwenyewe kufunga la pili wakati timu hiyo ikiilaza Ukraine mabao 2-0.Huo unakuwa […]

The post Southgate ampamba Saka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa England, Gareth Southgate amesema mshambuliaji wa timu hiyo, Bukayo Saka ameendelea kuwa mwenye ‘shauku ya ajabu’ ya mafanikio jambo linalosaidia kupandisha kiwango chake msimu huu.
Saka ambaye pia anaichezea Arsenal, jana Jumapili aliisaidia England kupata bao la kwanza kabla ya yeye mwenyewe kufunga la pili wakati timu hiyo ikiilaza Ukraine mabao 2-0.
Huo unakuwa ushindi wa pili mfululizo kwa England kwenye michuano ya kuwania kufuzu fainali za Euro 2024 ikiwa tayari imeanza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Italia Alhamisi iliyopita.
Katika mechi ya jana, England ilipata bao lake la kwanza kupitia kwa nahodha wa timu hiyo, Harry Kane akiitumia vizuri krosi ya Saka, hilo likiwa ni bao la 55 kwa Kane akiwa na England.
Saka alikamilisha bao la pili baada ya kuinasa pasi ya Jordan Henderson na kuonyesha uwezo binafsi kabla ya kuujaza mpira wavuni, hilo likiwa bao lake la 17 msimu huu akiwa na Arsenal na England.
“Hiyo ni ‘shauku ya ajabu’ ambayo imeongezeka katika soka lake kwa kipindi cha miezi 18 au zaidi iliyopita, kuna wakati usingekuwa na uhakika kama atafunga lakini kwa sasa ana ile hali ya kujiamini mbele ya goli,” alisema Southgate akimzungumzia Saka ambaye ndio kwanza ana miaka 21.

“Nafikiri kwa sasa anapokuwa mbele ya goli anacheza akiwa na uhakika, hilo lipo wazi katika klabu, na limeonekana katika mechi zetu, kwa sasa unamtegemea lazima afunge, na hiyo ni mabadiliko ya kifikra kuliko mbinu kwani tayari ni mchezaji mwenye mbinu,” aliongeza Southgate.


Baada ya kuiwakilisha England, Saka atarejea dimbani Jumamosi hii na jezi ya Arsenal katika Ligi Kuu England dhidi ya Leeds wakati Arsenal ikipigania pointi tatu muhimu za kujiimaisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.
Matokeo ya mechi za kufuzu Euro 2024 za jana Jumapili ni kama ifuatavyo…
Kazakhstan 3-2 Denmark
England 2-0 Ukraine
Luxembourg 0-6 Portugal
Malta 0-2 Italia
Northern Ireland 0-1 Finland
Liechtenstein 0-7 Iceland
Slovenia 2-0 San Marino
Slovakia 2-0 Bos-Herze
Mechi za kufuzu Euro 2024 zitakazochezwa leo Jumatatu ni kama ifuatavyo…
R. of Ireland v Ufaransa
Uholanzi v Gibraltar
Moldova v Jamhuri ya Czech
Poland v Albania
Austria v Estonia
Sweden v Azerbaijan
Hungary v Bulgaria
Montenegro v Serbia

The post Southgate ampamba Saka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/27/southgate-ampamba-saka/feed/ 0