Polisi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 03 May 2023 16:46:08 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.7 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Polisi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Zahera aigeuza fainali mechi ya Polisi, Mtibwa https://www.greensports.co.tz/2023/05/03/zahera-aigeuza-fainali-mechi-ya-polisi-mtibwa/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/03/zahera-aigeuza-fainali-mechi-ya-polisi-mtibwa/#respond Wed, 03 May 2023 16:45:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5999 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Mwinyi Zahera amesema mechi yao dhidi ya Mtibwa Sugar itakuwa kama fainali kwa kuwa ndio imebeba matumaini yao ya kubaki Ligi Kuu NBC.Maafande hao watakuwa nyumbani Uwanja wa Ushirika, Moshi Mei 15, mwaka huu kucheza na Mtibwa mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na timu zote […]

The post Zahera aigeuza fainali mechi ya Polisi, Mtibwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Mwinyi Zahera amesema mechi yao dhidi ya Mtibwa Sugar itakuwa kama fainali kwa kuwa ndio imebeba matumaini yao ya kubaki Ligi Kuu NBC.
Maafande hao watakuwa nyumbani Uwanja wa Ushirika, Moshi Mei 15, mwaka huu kucheza na Mtibwa mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na timu zote mbili kuwa katika nafasi mbaya kwenye msimamo wa ligi.
Zahera ameeleza kuwa ushindi walioupata kwenye mchezo uliopita dhidi ya Ihefu umeamsha ari ya kupambana kwenye kikosi chake hivyo anaamini kwa maandalizi waliyofanya hata mchezo ujao watachukua pointi tatu.

“Ni mchezo muhimu kwetu najua utakuwa mgumu lakini naamini tutapata ushindi ambao utasaidia kujiweka angalau kwenye ‘play off’ na siyo kushuka daraja moja kwa moja,” alisema Zahera.


Kocha huyo alisema kwa nama ushindani ulivyo kwa sasa uwezekano wa kujinasua moja kwa moja na janga la kushuka daraja ni mgumu kwa hiyo wanapambana kuangukia kwenye mechi za mtoano na baada ya hapo watajipanga kucheza mechi hizo za mtoano ili kusalia Ligi Kuu.
Polisi ambayo mechi iliyopita waliifunga Ihefu mabao 2-1, ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 22 wakati Mtibwa ipo nafasi ya 12 na pointi 29 huku zikiwa zimesalia mechi tatu kumaliza msimu.

The post Zahera aigeuza fainali mechi ya Polisi, Mtibwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/03/zahera-aigeuza-fainali-mechi-ya-polisi-mtibwa/feed/ 0
Polisi wamuonya Ronaldo https://www.greensports.co.tz/2022/08/18/polisi-wamuonya-ronaldo/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/18/polisi-wamuonya-ronaldo/#respond Thu, 18 Aug 2022 20:48:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2461 Manchester, EnglandPolisi wa Manchester wamemuonya mshambuliaji wa Manchester United, Cristiano Ronaldo baada ya kudaiwa kuvunja simu ya shabiki wa soka siku ambayo timu yake ilishindwa kutamba mbele ya Everton katika mechi iliyopigwa Aprili mwaka huu.Baada ya Man Utd kulala kwa bao 1-0 kwenye dimba la Goodison Park katika mechi ya msimu uliopita, picha za vyanzo […]

The post Polisi wamuonya Ronaldo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Polisi wa Manchester wamemuonya mshambuliaji wa Manchester United, Cristiano Ronaldo baada ya kudaiwa kuvunja simu ya shabiki wa soka siku ambayo timu yake ilishindwa kutamba mbele ya Everton katika mechi iliyopigwa Aprili mwaka huu.
Baada ya Man Utd kulala kwa bao 1-0 kwenye dimba la Goodison Park katika mechi ya msimu uliopita, picha za vyanzo mbalimbali vya habari zilimuonyesha Ronaldo akiiangusha chini simu ya shabiki wakati akitoka uwanjani kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Ronaldo hata hivyo baadaye aliomba radhi kwa tukio hilo na polisi wametoa taarifa yao Jumatano hii kuhusu kilichojiri katika tukio hilo.
“Tunaweza kuthibitisha kwamba mtu mwenye umri wa miaka 37 kwa hiari yake alifika na kuhojiwa akihusishwa na tukio kushambulia na uharibifu,” ilieleza taarifa hiyo.
“Tuhuma hizo zinahusisha tukio lililojitokeza katika mechi kati ya Everton na Manchester United kwenye Uwanja wa Goodison Park, siku ya Jumamosi, Aprili 9, suala hilo limeshughulikiwa katika mazingira ya tahadhari na kufikia hitimisho.”

The post Polisi wamuonya Ronaldo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/18/polisi-wamuonya-ronaldo/feed/ 0