Pochettino - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 12 Sep 2024 06:33:28 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Pochettino - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Pochettino kocha mkuu Marekani https://www.greensports.co.tz/2024/09/12/pochettino-kocha-mkuu-marekani/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/12/pochettino-kocha-mkuu-marekani/#respond Thu, 12 Sep 2024 06:33:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11894 New York, MarekaniAliyewahi kuwa kocha wa Tottenham Hotspur na Chelsea, Mauricio Pochettino ametangazswa kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya soka ya wanaume ya nchini Marekani.Pochettino anachukua nafasi iliyoachwa na Gregg Berhalter ambaye Julai mwaka huu alifutwa kazi baada ya Marekani ikiwa mwenyeji wa fainali za Copa America kutolewa katika hatua ya makundi.Uamuzi […]

The post Pochettino kocha mkuu Marekani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Aliyewahi kuwa kocha wa Tottenham Hotspur na Chelsea, Mauricio Pochettino ametangazswa kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya soka ya wanaume ya nchini Marekani.
Pochettino anachukua nafasi iliyoachwa na Gregg Berhalter ambaye Julai mwaka huu alifutwa kazi baada ya Marekani ikiwa mwenyeji wa fainali za Copa America kutolewa katika hatua ya makundi.
Uamuzi wa kumpa kazi Pochettino ambaye anatokea Argentina ulifikiwa kabla ya timu hiyo kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa na New Zealand ambapo kocha huyo alisema amepata fursa ambayo asingeweza kuikataa.

“Uamuzi wa kujiunga na timu Marekani kwangu si tu unahusu soka bali ni kushiriki safari ambayo nchi hii pamoja na timu zinaifanya. Nguvu, matamanio na hasira za kufanikisha mambo ni vitu vyenye historia hapa, hayo ndiyo yaliyonishawishi,” alisema Pochettino.


Alisema Marekani nchi ambayo itakuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2026, analiona kundi la wachezaji wenye vipaji na fursa tele na pamoja watatengeneza kitu cha kipekee ambacho kitaifanya nchi nzima iwe na la kujivunia.
Naye Mkurugenzi wa Soka Marekani, Matt Crocker ambaye ndiye aliyeongoza mchakato wa kumsaka kocha wa kuchukua nafasi ya Berhalter, alitumia muda mwingi akiwa Southampton wakati Pochettino akkiwa kocha.
Crocker alimtaka Pochettino kuwa ni kocha mshindi aliye na matamanio katika maendeleo ya wachezaji na amethibitisha uwezo wake wa kujenga timu imara na za ushindani.
Pochettino alijiunga na Southampton akitokea Espanyol kabla ya kujiunga na Spurs ambayo mwaka 2019 aliifikisha hatua ya fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya na baada ya hapo alizinoa PSG na Chelsea.

The post Pochettino kocha mkuu Marekani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/12/pochettino-kocha-mkuu-marekani/feed/ 0
Pochettino aondoka Chelsea, atajwa Man United https://www.greensports.co.tz/2024/05/22/pochettino-aondoka-chelsea-atajwa-man-united/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/22/pochettino-aondoka-chelsea-atajwa-man-united/#respond Wed, 22 May 2024 08:04:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11073 London, EnglandKocha Mauricio Pochettino ameachana na klabu ya Chelsea kwa makubaliano ya pande mbili na tayari zipo habari kwamba anawindwa na klabu za Man United na Bayern Munich.Pochettino amechukua uamuzi huo ikiwa imepita takriban wiki moja tangu atetewe na mwenyekiti wa klabu hiyo, Todd Boehly ambaye alisema kocha huyo anahitaji kuvumiliwa kwa kuwa mambo yameanza […]

The post Pochettino aondoka Chelsea, atajwa Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha Mauricio Pochettino ameachana na klabu ya Chelsea kwa makubaliano ya pande mbili na tayari zipo habari kwamba anawindwa na klabu za Man United na Bayern Munich.
Pochettino amechukua uamuzi huo ikiwa imepita takriban wiki moja tangu atetewe na mwenyekiti wa klabu hiyo, Todd Boehly ambaye alisema kocha huyo anahitaji kuvumiliwa kwa kuwa mambo yameanza kuwa mazuri na timu imekuwa ikiimarika.
Chelsea ilimuajiri Pochettino Julai Mosi mwaka jana kwa mkataba wa miaka miwili ambao ulikuwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja lakini ameamua kuondoka kabla ya mkataba wake kufikia ukomo.
Kwa kipindi kirefu kocha huyo kutoka Argentina amekuwa na wakati mgumu kwenye kikosi cha Chelsea lakini ushindi wa mechi tano mfululizo ulionekana kubadili upepo na alipongezwa na Boehly baada ya sare moja na kushinda mechi mbili.
Mafanikio ya hivi karibuni yameifikisha Chelsea katika nafasi ya sita kwenye Ligi Kuu England (EPL) lakini pia timu hiyo ilifikia fainali ya Carabao na nusu fainali ya Kombe la FA.

“Asante kwa wamiliki wa Chelsea na wakurugenzi wa michezo kwa fursa mliyonipa, kwa sasa klabu ipo katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye ligi kuu pamoja na Ulaya kwa miaka ijayo,” alisema Pochettino.


Kuondoka kwa Pochettino (52) kunaifanya Chelsea kuanza kusaka kocha wa kuchukua nafasi yake na tayari baadhi ya majina yameanza kutajwa akiwamo kocha wa Ipswich, Kieran McKenna, Ruben Amorin wa Sporting na Vincent Kompany wa Burnley.
Pochettino alikabidhiwa jukumu la kuinoa Chelsea baada ya kutimuliwa kwa makocha kadhaa katika kipindi kisichozidi miaka mitano wakiwamo Thomas Tuchel, Graham Potter na Frank Lampard ambaye alikuwa kocha wa muda mwishoni mwa msimu wa 2022-23.
Kuhusu uwezekano wa Pochettino kwenda Man United au Bayern ambazo zinasaka makocha wapya, habari hizo zimeandikwa na vyanzo mbalimbali vya habari barani Ulaya.

The post Pochettino aondoka Chelsea, atajwa Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/22/pochettino-aondoka-chelsea-atajwa-man-united/feed/ 0
Tajiri Chelsea amtetea Pochettino https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/tajiri-chelsea-amtetea-pochettino/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/tajiri-chelsea-amtetea-pochettino/#respond Fri, 10 May 2024 07:42:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10908 Los Angeles, MarekaniMwenyekiti na mmiliki wa klabu ya Chelsea, Todd Boehly amemtetea kocha wa timu hiyo, Mauricio Pochettino (pichani) akisema kiwango bora cha hivi karibuni ni ushahidi kuwa timu hiyo inaelekea pazuri chini ya kocha huyo.Chelsea haijapoteza mchezo hata mmoja katika mechi tatu zilizopita ikiwa imezifunga West Ham na Tottenham Hotspur baada ya kutoka sare […]

The post Tajiri Chelsea amtetea Pochettino first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Los Angeles, Marekani
Mwenyekiti na mmiliki wa klabu ya Chelsea, Todd Boehly amemtetea kocha wa timu hiyo, Mauricio Pochettino (pichani) akisema kiwango bora cha hivi karibuni ni ushahidi kuwa timu hiyo inaelekea pazuri chini ya kocha huyo.
Chelsea haijapoteza mchezo hata mmoja katika mechi tatu zilizopita ikiwa imezifunga West Ham na Tottenham Hotspur baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Aston Villa.
Matokeo hayo yameisaidia Chelsea kupanda hadi nafasi ya saba kwenye Ligi Kuu England (EPL) ikiwa imezidiwa pointi mbili na Newcastle inayoshika nafasi ya sita na ipo katika nafasi nzuri ya kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao.
Boehly amekuwa akishutumiwa kwa maneno ya kejeli na baadhi ya mashabiki hasa mwezi Machi mwaka huu lakini tajiri huyo wa nchini Marekani amesema kwamba sasa mipango ya bodi inaanza kuzaa matunda.

“Tumeona katika mechi mbili tatu zilizopita, kipindi cha pili dhidi ya Aston Villa (sare ya 2-2) na dhidi ya Tottenham (ushindi wa 2-0) na dhidi ya West Ham (ushindi wa 5-0) tulicheza soka zuri,” alisema Boehly.


Boehly aliisifia timu yake katika mechi hizo kwa namna wachezaji walivyoonekana kucheza kwa mpango, mashuti waliyoyapeleka kwenye lango la timu pinzani vyote vikionesha jinsi timu inavyokuwa vizuri.
Tajiri hiyo aliongeza kwa kusema kuwa matokeo ya mechi hizo yamebadili hata hoja za wachambuzi kuhusu timu hiyo mambo ambayo hata yeye yanamfanya kuamini kuwa Pochettino anafanya kazi nzuri.

The post Tajiri Chelsea amtetea Pochettino first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/tajiri-chelsea-amtetea-pochettino/feed/ 0
Chelsea laini yamtesa Pochettino https://www.greensports.co.tz/2024/04/24/chelsea-laini-yamtesa-pochettino/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/24/chelsea-laini-yamtesa-pochettino/#respond Wed, 24 Apr 2024 06:25:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10727 London, EnglandBaada ya kuchapwa mabao 5-0 na Arsenal kwenye Uwanja wa Emirates jana Jumanne, kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino amesema timu yake ni kama iliacha kucheza soka na ilikuwa laini.Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England (EPL), Chelsea ilikwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao 1-0 lakini kipindi cha pili ikajikuta ikichapwa mabao manne katika muda […]

The post Chelsea laini yamtesa Pochettino first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Baada ya kuchapwa mabao 5-0 na Arsenal kwenye Uwanja wa Emirates jana Jumanne, kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino amesema timu yake ni kama iliacha kucheza soka na ilikuwa laini.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England (EPL), Chelsea ilikwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao 1-0 lakini kipindi cha pili ikajikuta ikichapwa mabao manne katika muda usiozidi dakika 18.
Matokeo hayo mabaya kwa Chelsea yameweka rekodi ya kuwa kipigo kikubwa zaidi katika London Derby tangu mwaka 1986.
“Hakuna ugumu wowote wa kuelezea hali ilivyokuwa, kila mmoja aliona, hatukuwa tukipambana tangu mwanzo wa mchezo,” alisema Pochettino.
“Baada ya kufungwa goli la kwanza timu ilikuwa laini, ilinisikitisha tangu tulipoanza kwa sababu tulitakiwa kuwa na nguvu na kupambana vizuri, hatukuonesha ushindani, hatukuwa makini na mazingira ambayo ilikuwa rahisi kuyapatia suluhisho, na hiyo ndiyo sababu hasa iliyonikatisha tamaa,” alisema Pochettino
Katika mechi hiyo, Pochettino alifanya mabadiliko matatu katika safu ya ulinzi akimpumzisha Trevoh Chalobah na Thiago Silva wakati Malo Gusto alikuwa majeruhi baada ya kuumia katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Man City.
Pochettino alisema timu yake ilipambana vizuri katika mechi na Man City ambayo pia walipoteza lakini akashangaa kushindwa kufanya hivyo siku tatu baadaye na kuongeza kuwa huenda timu haikuwa ‘fresh’.

“Tulikuwa tukizungumza wakati wa mapumziko kuhusu kuanza kipindi cha pili katika namna tofauti lakini hatukufanya hivyo, tulipofungwa bao la tatu timu ni kama iliacha kucheza, hali ilikuwa ngumu,” alisema Pochettino.


Kocha huyo hata hivyo alikataa kuzungumzia wachezaji waliokosekana katika mechi hiyo kwa kile alichosema kwamba si haki kuzungumzia jambo hilo kwani tangu mwanzo wa msimu wamekuwa wakiwakosa wachezaji wengi karibu kila baada ya wiki.
Mabao ya Arsenal katika mechi hiyo yalifungwa na Trossard dakika ya nne wakati mengine yalifungwa na White dakika za 52 na 70 na Havertz dakika za 57 na 65.
Kwa ushindi huo Arsenal sasa inashika usukani EPL ikiwa imefikisha pointi 77 katika mechi 34 ikifuatiwa n Liverpool yenye pointi 74 katika mechi 33 wakati Chelsea imeshuka hadi nafasi ya tisa ikiwa na pointi 47 katika mechi 32.

The post Chelsea laini yamtesa Pochettino first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/24/chelsea-laini-yamtesa-pochettino/feed/ 0
Pochettino akana kusaka straika https://www.greensports.co.tz/2024/01/14/pochettino-akana-kusaka-straika/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/14/pochettino-akana-kusaka-straika/#respond Sun, 14 Jan 2024 19:19:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9309 London, EnglandKocha wa Man City, Mauricio Pochettino amepuuza habari kuwa Chelsea inahitaji kusajili straika katika kipindi cha usajili cha Januari na amekanusha kuiwania saini ya straika wa Brighton, Evan Ferguson.Chelsea imekuwa ikipitia kipindi kigumu katika eneo la ufungaji msimu huu na katika mechi ya jana Jumamosi dhidi ya Fulham waliyotoka na ushindi wa bao 1-0 […]

The post Pochettino akana kusaka straika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Man City, Mauricio Pochettino amepuuza habari kuwa Chelsea inahitaji kusajili straika katika kipindi cha usajili cha Januari na amekanusha kuiwania saini ya straika wa Brighton, Evan Ferguson.
Chelsea imekuwa ikipitia kipindi kigumu katika eneo la ufungaji msimu huu na katika mechi ya jana Jumamosi dhidi ya Fulham waliyotoka na ushindi wa bao 1-0 kwa mara nyingine iliwakosa, Christopher Nkunku na Nicolas Jackson.
Pochettino awali alinukuliwa akisema kwamba wanafanya mapitio ya hali ilivyo katika kikosi baada ya kukiri hofu yake kuhusu Nkunku kutokuwa fiti.
Nkunku, nyota wa zamani wa RB Leipzig ya Ujerumani aliyesajiliwa Chelsea kwa ada ya Pauni 52 milioni, hadi sasa amecheza mechi nne tu za Chelsea tangu apate tatizo ya majeraha ya goti wakati wa maandalizi ya msimu.
Awali kulikuwa na habari kwamba Chelsea pia ilikuwa ikiisaka saini ya mshambuliaji wa Napoli, Victor Osimhen na Ivan Toney wa Brentford lakini imeonekana kuna ugumu wa kuwapata wachezaji hao.
Akizungumzia habari hizo Pochettino alisema, “Hapna, nafikiri mnajua vizuri kwamba sizungumzii uvumi, siwezi katu kuwazungumzia wachezaji walio kwenye klabu nyingine, naliheshimu hilo.’
Badala yake Pochettino alisisitiza kwamba wanachofanya sasa ni mapitio ya kikosi chao na kama kuna kitakachotokea wataweka kila kitu wazi lakini kwa sasa hawajachukua uamuzi wowote.

The post Pochettino akana kusaka straika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/14/pochettino-akana-kusaka-straika/feed/ 0
Chelsea laini yamkera Pochettino https://www.greensports.co.tz/2023/11/26/chelsea-laini-yamkera-pochettino/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/26/chelsea-laini-yamkera-pochettino/#respond Sun, 26 Nov 2023 17:59:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8640 London, EnglandKocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino (pichani) amekasirishwa kwa namna ambavyo timu yake imekuwa ‘laini’ na kukubali kichapo cha mabao 4-1 mbele ya Newcastle katika mechi iliyochezwa jana Jumamosi.Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England iliyopigwa kwenye dimba la St James, hadi mapumziko, Chelsea walikuwa tayari wamesawazisha bao moja walilofungwa kabla mambo hayajaharibika kipindi cha […]

The post Chelsea laini yamkera Pochettino first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino (pichani) amekasirishwa kwa namna ambavyo timu yake imekuwa ‘laini’ na kukubali kichapo cha mabao 4-1 mbele ya Newcastle katika mechi iliyochezwa jana Jumamosi.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England iliyopigwa kwenye dimba la St James, hadi mapumziko, Chelsea walikuwa tayari wamesawazisha bao moja walilofungwa kabla mambo hayajaharibika kipindi cha pili.
Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Chelsea ambayo ilijikuta ikibaki na wachezaji 10 uwanjani baada ya nahodha wa timu hiyo Reece James kutolewa nje.
Akizungumzia matokeo hayo, Pochettino ambaye alivutiwa na kiwango cha timu yake katika mechi na Tottenham, alisema matokeo ya Newcastle yamemkatisha tamaa kwa kile alichosema timu yake ilishindwa kupambana na kuwa laini.
“Hatukuonesha kwamba tulikuwa tunacheza katika mechi muhimu, tulitakiwa kuwaonesha kwamba mechi ingekuwa ngumu kwao, kwamba isingewezekana kucheza vizuri na kutushinda,” alisema Pochettino.
“Lakini ilikuwa rahisi mno kwa namna ambavyo tulikubali kufungwa, na kwa namna tulivyokuwa laini katika kila eneo la upambanaji,” alisema Pochettino.

“Na hilo ndilo lililonifanya niwe na hasira na kuvurugwa, tunazungumzia kuhusu timu yenye vijana na ni lazima tujifunze lakini nafikiri aina hii ya mechi inanifanya niwe mwenye hasira sana kwa sababu ni suala la kuonesha ubora na upambanaji,” alisema Pochettino.


Matokeo ya mechi za Jumamosi Ligi Kuu England…
Man City 1-1 Liverpool
Burnley 1-2 West Ham
Luton Town 2-1 Crystal Palace
Newcastle 4-1 Chelsea
Nottingham Forest 2-3 Brighton
Sheffield United 1-3 Bournemouth
Brentford 0-1 Arsenal

The post Chelsea laini yamkera Pochettino first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/26/chelsea-laini-yamkera-pochettino/feed/ 0
Pochettino kocha mpya Chelsea https://www.greensports.co.tz/2023/05/14/pochettino-kocha-mpya-chelsea/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/14/pochettino-kocha-mpya-chelsea/#respond Sun, 14 May 2023 16:10:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6161 London, EnglandKlabu ya Chelsea hatimaye imefikia makubaliano na kocha wa zamani wa klabu za Tottenham Hotspur na PSG, Mauricio Pochettino ambaye sasa atakuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo.Pochettino (pichani) hivi karibuni amekuwa akitajwa kupewa jukumu la kuinoa Chelsea ambayo inanolewa na kocha wa muda Frank Lampard aliyekabidhiwa mikoba baada ya Graham Potter kutimuliwa.Kocha Pochettino […]

The post Pochettino kocha mpya Chelsea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Klabu ya Chelsea hatimaye imefikia makubaliano na kocha wa zamani wa klabu za Tottenham Hotspur na PSG, Mauricio Pochettino ambaye sasa atakuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo.
Pochettino (pichani) hivi karibuni amekuwa akitajwa kupewa jukumu la kuinoa Chelsea ambayo inanolewa na kocha wa muda Frank Lampard aliyekabidhiwa mikoba baada ya Graham Potter kutimuliwa.
Kocha Pochettino ambaye amekuwa bila ya kazi tangu majira ya kiangazi mwaka jana alipotimuliwa PSG, na nafasi yake kukabidhiwa Christophe Galtier, ataanza kazi rasmi mara baada ya msimu huu.
Pochettino mwenye umri wa miaka 51 ambaye pia amewahi kuinoa Southampton, anakuwa kocha wa sita wa Chelsea katika kipindi cha miaka mitano.
Chelsea imekuwa na msimu mbaya ikitolewa na Man City katika Kombe la FA na lile la Ligi na hivi karibuni imetolewa na Real Madrid katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kibaya zaidi ni kwamba kwa sasa inashika nafasi ya 11 kwenye Ligi Kuu England (EPL) ikiwa na rekodi ya kushinda mechi moja tu kati ya 11 zilizopita ikipoteza mechi nane na tayari imepoteza matumaini ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Machi mwaka huu baada ya Spurs kuachana na kocha Antonio Conte, Pochettino alikuwa akitajwa kurudi katika timu hiyo akikumbukwa kuiwezesha kufikia hatua ya fainali ya Kombe la Ligi mwaka 2015 na kuiwezesha kushika nafasi ya pili kwenye EPL msimu wa 2016-17.

The post Pochettino kocha mpya Chelsea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/14/pochettino-kocha-mpya-chelsea/feed/ 0