NIC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 05 Mar 2024 06:24:46 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg NIC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Kibabage, Pacome, Mudathir wawania tuzo Yanga https://www.greensports.co.tz/2024/03/05/kibabage-pacome-mudathir-wawania-tuzo-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/05/kibabage-pacome-mudathir-wawania-tuzo-yanga/#respond Tue, 05 Mar 2024 06:24:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10031 Na mwandishi wetuWachezaji wa Yanga; Mudathir Yahya, Pacome Zouzoua na Nickson Kibabage wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Februari wa timu hiyo.Meneja wa timu hiyo, Walter Harrison alisema Jumatatu hii sababu ya kupendekezwa wachezaji hao ni kutokana na mchango mkubwa walioutoa kwa timu yao mwezi uliopita.“Hao ndio wachezaji ambao rekodi zao […]

The post Kibabage, Pacome, Mudathir wawania tuzo Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Wachezaji wa Yanga; Mudathir Yahya, Pacome Zouzoua na Nickson Kibabage wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Februari wa timu hiyo.
Meneja wa timu hiyo, Walter Harrison alisema Jumatatu hii sababu ya kupendekezwa wachezaji hao ni kutokana na mchango mkubwa walioutoa kwa timu yao mwezi uliopita.
“Hao ndio wachezaji ambao rekodi zao zimeonesha kuibeba sana Yanga, wamefunga mabao na kutengeneza nafasi kwenye mashindano yote ndio maana tukawapendekeza kuwania tuzo hiyo ya NIC (Shirika la Bima la Taifa),” alisema Walter.
Meneja huyo alisema kazi inabaki kwa mashabiki wao kupiga kura kupitia mtandao wa klabu hiyo kuchagua mchezaji ambaye wanaamini ndiye bora ili awe mshindi wa tuzo hiyo.
Hiyo ni mara ya pili kwa Pacome kuingia kwenye kuwania tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mwezi wa Yanga. Mara ya kwanza ilikuwa Novemba, mwaka jana ambapo aliibuka mshindi dhidi ya Dickson Job na Clement Mzize.

The post Kibabage, Pacome, Mudathir wawania tuzo Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/05/kibabage-pacome-mudathir-wawania-tuzo-yanga/feed/ 0
Aziz Ki awashukuru mashabiki kwa tuzo https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/aziz-ki-awashukuru-mashabiki-kwa-tuzo/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/aziz-ki-awashukuru-mashabiki-kwa-tuzo/#respond Wed, 01 Nov 2023 06:22:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8312 Na mwandishi wetuKiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephen Aziz Ki amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa kumpigia kura zilizomwezesha kuibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba.Mchezaji huyo ameshinda tuzo hiyo ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza chini ya udhamini wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) na kujinyakulia Sh milioni 4 akiwashinda Maxi […]

The post Aziz Ki awashukuru mashabiki kwa tuzo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephen Aziz Ki amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa kumpigia kura zilizomwezesha kuibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba.
Mchezaji huyo ameshinda tuzo hiyo ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza chini ya udhamini wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) na kujinyakulia Sh milioni 4 akiwashinda Maxi Nzengeli na beki Dickson Job aliokuwa akiwania nao tuzo hiyo.
Akizungumza kupitia mtandao wa klabu hiyo leo Jumanne, mchezaji huyo alisema tuzo hiyo imempa heshima kubwa na kumwongezea ari ya kuipambania timu yake katika mashindano yote ambayo wanashiriki hivi sasa.
“Nawashukuru mashabiki wa Yanga, kwa kunipigia kura, imeonesha namna imani yao ilivyo kwangu, na mimi nitahakikisha nazidi kupambana ili kuwapa mafanikio zaidi msimu huu lakini nawashukuru wachezaji wenzangu pia kwa ushirikiano wao na benchi la ufundi kwa kunipa nafasi,” alisema Aziz Ki.
Kiungo huyo ameshinda tuzo hiyo baada ya kuifungia Yanga mabao manne mwezi Oktoba katika michuano ya Ligi Kuu NBC, ikiwemo ‘hat-trick’ aliyoifunga katika mchezo dhidi ya Azam FC wiki iliyopita.
Aziz Ki kwa msimu huu ni miongoni mwa vinara wanaoongoza kwa ufungaji kwenye Ligi Kuu NBC na timu yake akifunga mabao sita sawa na Jean Baleke wa Simba.

The post Aziz Ki awashukuru mashabiki kwa tuzo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/aziz-ki-awashukuru-mashabiki-kwa-tuzo/feed/ 0
Mchezaji bora Yanga kulamba milioni 4 https://www.greensports.co.tz/2023/10/30/mchezaji-bora-yanga-kulamba-milioni-4/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/30/mchezaji-bora-yanga-kulamba-milioni-4/#respond Mon, 30 Oct 2023 08:31:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8285 Na mwandishi wetuWadhamini wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Klabu ya Yanga, Shirika la Bima la Taifa (NIC), limeahidi kutoa Sh milioni nne kwa mchezaji atakayeshinda tuzo hiyo kuanzia mwezi huu wa Oktoba.Wachezaji ambao wameteuliwa kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho ni beki wa kati Dickson Job na viungo washambuliaji, Max Zengeli na Stephan Aziz Ki.Akizungumza kwenye […]

The post Mchezaji bora Yanga kulamba milioni 4 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Wadhamini wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Klabu ya Yanga, Shirika la Bima la Taifa (NIC), limeahidi kutoa Sh milioni nne kwa mchezaji atakayeshinda tuzo hiyo kuanzia mwezi huu wa Oktoba.
Wachezaji ambao wameteuliwa kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho ni beki wa kati Dickson Job na viungo washambuliaji, Max Zengeli na Stephan Aziz Ki.
Akizungumza kwenye hafla fupi iliyofanyika mwishoni mwa wiki ya kutangaza zawadi hizo, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema kiasi hicho cha fedha kilichowekwa na NIC kitaongeza ari ya upambanaji kwa wachezaji wao na kupata matokeo chanya katika mashindano mbalimbali yanayowakabili.
“Milioni nne si kiasi kidogo na Yanga inaweza kuwa ndio klabu ya kwanza kupata mzigo huo na hii inalirahisishia kazi hata benchi la ufundi kwani wachezaji watacheza kwa kujituma mara mbili ya inavyokuwa ili kupata pesa hiyo,” alisema Kamwe.
Alisema zoezi la kupiga kura ili kumpata mshindi linafanyika kupitia mtandao wa klabu hiyo na wahusika wakuu ni mashabiki na wanachama wa timu hiyo.
Naye Msemaji wa NIC, Karimu Meshack alisema tuzo ya mchezaji bora wa NIC Insurance imezingatia vitu vingi ikiwemo ubora wa NIC kama chapa, ubora wa Yanga kwa pamoja na uwepo wa wachezaji wazuri watakaoleta mchuano mkali.
Hii ni mara ya kwanza kwa klabu ya Yanga kupata wadhamini binafsi kwa ajili ya kutoa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi baada ya kuingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni hiyo wenye thamani ya Sh milioni 900.

The post Mchezaji bora Yanga kulamba milioni 4 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/30/mchezaji-bora-yanga-kulamba-milioni-4/feed/ 0
Yanga, NIC waingia mkataba wa milioni 900 https://www.greensports.co.tz/2023/10/09/yanga-nic-waingia-mkataba-wa-milioni-900/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/09/yanga-nic-waingia-mkataba-wa-milioni-900/#respond Mon, 09 Oct 2023 18:21:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8026 Na mwandishi wetuKlabu ya Yanga leo Jumatatu imesaini mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya shilingi milioni 900 na Kampuni ya Bima ya Taifa (NIC) kwa ajili ya kutoa tuzo za mchezaji bora wa mwezi.Akizungumza katika hafla ya makubaliano hayo jijini Dar es Salaam, Rais wa Yanga, Hersi Said alisema mkataba huo utawapa wachezaji wa […]

The post Yanga, NIC waingia mkataba wa milioni 900 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya Yanga leo Jumatatu imesaini mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya shilingi milioni 900 na Kampuni ya Bima ya Taifa (NIC) kwa ajili ya kutoa tuzo za mchezaji bora wa mwezi.
Akizungumza katika hafla ya makubaliano hayo jijini Dar es Salaam, Rais wa Yanga, Hersi Said alisema mkataba huo utawapa wachezaji wa timu yake nafasi ya kutimiza majukumu yao uwanjani pamoja na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara na NIC.
Hersi alisema kimsingi makubaliano hayo yanakwenda kunufaisha pande zote husika kwani wakati Yanga ikinufaika kwa kupata shilingi milioni 900, NIC nao wanatapa fursa ya biashara yao kutangazwa kwa ukubwa.
“Wameamua kufanya kazi na sisi kwa sababu tuna wachezaji bora ambao huwezi kuwapata kwingine, ni wachezaji wenye ushawishi ndani na nje ya uwanja jambo ambalo ni chachu ya kutangaza biashara,” alisema Hersi.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa NIC, Elihuruma Doriye alisema kwamba historia nchini imeandikwa kwa taasisi mbili kuingia makubaliano ya kibiashara kwa kipindi cha miaka mitatu.
Doriye alisema kwamba kwa Tanzania huwezi kuzungumzia bima bila ya kuitaja NIC na kwa upande wa Yanga alisema kwamba klabu hiyo ni nembo ya soka la Tanzania.

“Ni furaha kubwa kupata fursa ya kufanya biashara na taasisi kubwa kama hii, kwa upande wetu NIC tumepewa hadhi ya kuaminika,” alisema Doriye.


Naye ofisa habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema klabu yao ina furaha kwa sababu mkataba huo utaongeza ushindani kwa wachezaji wa Yanga na hamasa itazidi kuwa juu kwa upande wa mashabiki.
Simba ilikuwa klabu pekee nchini iliyokuwa ikitoa tuzo za kila mwezi kwa wachezaji wake lakini tuzo hizo zilifutwa hivi karibuni baada ya aliyekuwa mdhamini. Kampuni ya Emirates Aluminium kumaliza mkataba na klabu hiyo.

The post Yanga, NIC waingia mkataba wa milioni 900 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/09/yanga-nic-waingia-mkataba-wa-milioni-900/feed/ 0