Ndimbo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 14 Jul 2023 15:16:47 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Ndimbo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Kitayosce sasa ruksa kusajili https://www.greensports.co.tz/2023/07/14/kitayosce-sasa-ruksa-kusajili/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/14/kitayosce-sasa-ruksa-kusajili/#respond Fri, 14 Jul 2023 15:16:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6971 Na mwandishi wetuKlabu ya Kitayosce inayoshiriki Ligi Kuu NBC imeruhusiwa kuendelea na usajili wa wachezaji kama kawaida baada ya adhabu yao ya kutosajili kuondolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).Tamko hilo limetolewa leo Ijumaa ikiwa ni siku mbili pekee zimepita tangu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litangaze kufungiwa kwa timu hiyo pamoja na Fountain […]

The post Kitayosce sasa ruksa kusajili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya Kitayosce inayoshiriki Ligi Kuu NBC imeruhusiwa kuendelea na usajili wa wachezaji kama kawaida baada ya adhabu yao ya kutosajili kuondolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Tamko hilo limetolewa leo Ijumaa ikiwa ni siku mbili pekee zimepita tangu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litangaze kufungiwa kwa timu hiyo pamoja na Fountain Gate inayocheza Ligi ya Championship baada ya kocha Ahmed El Faramawy Soliman kushinda kesi za madai dhidi ya klabu hizo alizowahi kuzinoa kwa nyakati tofauti.
Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo ameeleza kwamba kilichotokea ni kwamba Kitayosce imelipa fedha zote ilizokuwa ikidaiwa na kocha huyo raia wa Misri kwa klabu hiyo kumvunjia mkataba kinyume na taratibu.
“Ni uamuzi uliotolewa na Fifa baada ya Kitayosce kulipa madai yao yote kwa kocha Ahmed Soliman. Kwa hatua hiyo sasa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania nalo limeiondolea adhabu Kitayosce ya kutofanya usajili wa ndani,” alisema Ndimbo.

The post Kitayosce sasa ruksa kusajili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/14/kitayosce-sasa-ruksa-kusajili/feed/ 0
Fifa yashusha rungu Kitayosce, Fountain Gate https://www.greensports.co.tz/2023/07/13/fifa-yashusha-rungu-kitayosce-fountain-gate/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/13/fifa-yashusha-rungu-kitayosce-fountain-gate/#respond Thu, 13 Jul 2023 05:47:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6923 Na mwandishi wetuKlabu za Kitayosce inayoshiriki Ligi Kuu NBC na Fountain Gate inayocheza Ligi ya Championship zimefungiwa kusajili wachezaji kwa msimu wa 2023/24.Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka (TFF), Cliford Ndimbo (Ndimbo) alisema uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) baada ya kocha Ahmed El Faramawy Yousef Mostafa Soliman kushinda […]

The post Fifa yashusha rungu Kitayosce, Fountain Gate first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu za Kitayosce inayoshiriki Ligi Kuu NBC na Fountain Gate inayocheza Ligi ya Championship zimefungiwa kusajili wachezaji kwa msimu wa 2023/24.
Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka (TFF), Cliford Ndimbo (Ndimbo) alisema uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) baada ya kocha Ahmed El Faramawy Yousef Mostafa Soliman kushinda kesi za madai yake dhidi ya klabu hizo.
“Kocha Soliman, raia wa Misri ambaye alizifundisha timu hizo kwa nyakati tofauti alifungua kesi Fifa akipinga kuvunjiwa mikataba kinyume cha taratibu. Baada ya kushinda kesi, klabu hizo zilitakiwa ziwe zimemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini hazikutekeleza hukumu hizo,” alisema Ndimbo.
Ndimbo pia alifafanua kuwa wakati Fifa imezifungia klabu hizo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, TFF yenyewe imezifungia kufanya uhamisho wa ndani.
“TFF inazikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili na iwapo klabu inataka kuvunja mkataba na mchezaji au kocha, inatakiwa kufanya hivyo kwa kuzingatia taratibu,” aliongeza Ndimbo.

The post Fifa yashusha rungu Kitayosce, Fountain Gate first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/13/fifa-yashusha-rungu-kitayosce-fountain-gate/feed/ 0