Mudathir - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 26 Mar 2024 07:39:40 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mudathir - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mudathir ‘akabidhiwa’ rasmi Mamelodi https://www.greensports.co.tz/2024/03/26/mudathir-akabidhiwa-rasmi-mamelodi/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/26/mudathir-akabidhiwa-rasmi-mamelodi/#respond Tue, 26 Mar 2024 07:39:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10370 Na mwandishi wetuUongozi wa klabu ya Yanga na benchi la ufundi la timu hiyo umemkabidhi kiungo Mudathir Yahya mchezo wao wa robo fainali wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, meneja habari na mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, alisema hiyo ni kutokana […]

The post Mudathir ‘akabidhiwa’ rasmi Mamelodi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Uongozi wa klabu ya Yanga na benchi la ufundi la timu hiyo umemkabidhi kiungo Mudathir Yahya mchezo wao wa robo fainali wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, meneja habari na mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, alisema hiyo ni kutokana na mchezaji huyo kujitoa kwake katika kuipambania timu ili kupata matokeo katika mashindano yote inayoshiriki.
“Uongozi na benchi la ufundi kwa pamoja wamekubaliana kuwa mchezo wetu dhidi ya Mamelodi, akabidhiwe kijana kutoka Kizimkazi, Mudathir Yahya, na kaulimbiu yetu kwenye mechi hii ‘Simu ziite tukutane kwa Mkapa’ alisema Kamwe.
Kamwe alisema kuwa staili ya kushangilia ya mchezaji huyo ndiyo iliyosababisha kutoa kaulimbiu hiyo wakiwataka mashabiki zao wapigiane simu ili kwenda uwanjani kuijaza Benjamin Mkapa na kuwapa sapoti ‘wanajeshi’ wao waweze kujituma na kuwapa ushindi.
Kuhusu wachezaji majeruhi kwenye kikosi chao, Kamwe alisema hadi sasa kiungo Zawadi Mauya tayari ameanza mazoezi na yupo tayari kwa mchezo, Kibwana Shomari kwa mujibu wa daktari wa timu Moses Etutu, alisema yupo katika asilimia 60 ya utimamu na bado hajaanza mazoezi.
Na Pacome Zouzoua pamoja na Khalid Aucho wao wapo zaidi ya asilimia 80 ya utimamu wao na wameanza mazoezi lakini kwa upande wa beki, Yao Kouassi bado ni asilimia 50/50 kwani bado hajawa timamu.
Yanga itacheza na Mamelodi Machi 30, mwaka huu kwenye, Uwanja wa Mkapa na timu hizo zitarudiana Aprili 5, mwaka huu nchini Afrika Kusini na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

The post Mudathir ‘akabidhiwa’ rasmi Mamelodi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/26/mudathir-akabidhiwa-rasmi-mamelodi/feed/ 0
Mudathir abeba tuzo ya NIC https://www.greensports.co.tz/2024/03/14/mudathir-abeba-tuzo-ya-nic/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/14/mudathir-abeba-tuzo-ya-nic/#respond Thu, 14 Mar 2024 19:21:36 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10194 Na mwandishi wetuKiungo mshambuliaji wa Yanga, Mudathir Yahya ameibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Februari ndani ya klabu hiyo akiwazidi Pacome Zouzoua na Nickson Kibabage.Akizungumza na GreenSports Mudathir aliye kwenye kiwango cha juu kwa sasa, aliwashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa kumpigia kura ambazo zimemfanya aibuke mshindi kwenye kinyang’anyiro hicho. “Nawashukuru mashabiki […]

The post Mudathir abeba tuzo ya NIC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mudathir Yahya ameibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Februari ndani ya klabu hiyo akiwazidi Pacome Zouzoua na Nickson Kibabage.
Akizungumza na GreenSports Mudathir aliye kwenye kiwango cha juu kwa sasa, aliwashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa kumpigia kura ambazo zimemfanya aibuke mshindi kwenye kinyang’anyiro hicho.

“Nawashukuru mashabiki na wanachama wa Yanga kwa kunipigia kura, kwangu ni kama kuniongezea ari ya kupambana nifanye vizuri zaidi ya hapa, nawashukuru sana,” alisema Mudathir.


Kiungo huyo pia aliwashukuru wachezaji wenzake na wadhamini wa tuzo hizo Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa mchango na mawazo yao ambayo kwa kiasi kikubwa yameongeza hamasa kwa wachezaji.
Kwa kushinda tuzo hiyo, Mudathir ambaye anakuwa mchezaji wa tano kubeba tuzo hiyo tangu ianzishwe Oktoba, mwaka jana, atazawadiwa kitita cha Sh milioni 4 pamoja na kombe dogo kutoka kwa wadhamini hao.

The post Mudathir abeba tuzo ya NIC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/14/mudathir-abeba-tuzo-ya-nic/feed/ 0
Mudathir akataa kupoteza mechi ya tatu kwa Simba https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/mudathir-akataa-kupoteza-mechi-ya-tatu-kwa-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/mudathir-akataa-kupoteza-mechi-ya-tatu-kwa-simba/#respond Wed, 01 Nov 2023 20:00:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8334 Na mwandishi wetuKiungo wa Yanga, Mudathir Yahya ameeleza kuwa wamejipanga kuondoka na pointi tatu dhidi ya Simba kwani hawako tayari kupoteza mchezo wa tatu mfululizo dhidi yao.Yanga imepoteza michezo miwili dhidi ya Simba kwenye mashindano tofauti, ikiwemo mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu NBC msimu uliopita kwa kichapo cha mabao 2-0 na Ngao […]

The post Mudathir akataa kupoteza mechi ya tatu kwa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya ameeleza kuwa wamejipanga kuondoka na pointi tatu dhidi ya Simba kwani hawako tayari kupoteza mchezo wa tatu mfululizo dhidi yao.
Yanga imepoteza michezo miwili dhidi ya Simba kwenye mashindano tofauti, ikiwemo mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu NBC msimu uliopita kwa kichapo cha mabao 2-0 na Ngao ya Jamii iliyofanyika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na kupoteza kwa mikwaju ya penalti 3-1.
Mudathir alisema kikosi chao kimeendelea kuimarika na kitendo cha kushinda michezo mitatu iliyopita kwenye ligi baada ya kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu kimeongeza morali kikosini mwao kuelekea mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu Afrika.
“Hii ni mechi kubwa, maandalizi yanaendelea vizuri tunahitaji kupata matokeo mazuri ya alama tatu kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo na mwisho wa msimu kutetea taji letu.

“Maandalizi yako vizuri hatutakuwa tayari kuona tunaenda kupoteza huu mchezo kwa mara nyingine, tuko imara na mashabiki wajitokeze kusapoti timu ili kuendeleza ushindani,” alisema Mudathir.


Mechi baina ya wababe hao inatarajiwa kupigwa Novemba 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam huku Yanga ikiwa inaongoza ligi kwa pointi 18, sawa na Simba ambayo imezidiwa idadi ya mabao ya kufunga huku Yanga ikiwa imecheza mechi saba, Simba imeshuka dimbani mara sita mpaka sasa.

The post Mudathir akataa kupoteza mechi ya tatu kwa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/mudathir-akataa-kupoteza-mechi-ya-tatu-kwa-simba/feed/ 0
Mudathir: Maelekezo ya Gamondi yalizaa bao https://www.greensports.co.tz/2023/09/23/mudathir-maelekezo-ya-gamondi-yalizaa-bao/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/23/mudathir-maelekezo-ya-gamondi-yalizaa-bao/#respond Sat, 23 Sep 2023 12:36:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7828 Na mwandishi wetuMfungaji wa bao pekee la Yanga katika mechi yao dhidi ya Namungo, Mudathir Yahya ameeleza kuwa kocha wake, Miguel Gamondi alimwekeleza nini cha kufanya ili wapate ushindi na alitekeleza alichoambiwa.Mudathir aliyeingia dakika ya 68 kuchukua nafasi ya Pacome Zouzoua alifunga bao dakika ya 88 katika mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Azam Complex, Dar […]

The post Mudathir: Maelekezo ya Gamondi yalizaa bao first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mfungaji wa bao pekee la Yanga katika mechi yao dhidi ya Namungo, Mudathir Yahya ameeleza kuwa kocha wake, Miguel Gamondi alimwekeleza nini cha kufanya ili wapate ushindi na alitekeleza alichoambiwa.
Mudathir aliyeingia dakika ya 68 kuchukua nafasi ya Pacome Zouzoua alifunga bao dakika ya 88 katika mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na kuipa Yanga ushindi wa bao 1-0 uliowarejesha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC.
“Mwalimu aliniambia kuwa wapinzani wamekaa nyuma kwenye lango lao hivyo ni ngumu kupata bao, akaniambia ukiona mpira umekwenda pembeni, nikimbie nyuma ya mabeki wa Namungo na kweli mpira ukapigwa krosi na Yao (Kouassi) nikafunga,” alisema Mudathir.
Kiungo huyo alifafanua kuwa kilichotokea kwenye bao hilo huwa wanajifunza kwenye uwanja wa mazoezi ndio maana walifanikiwa kupata ushindi japo si wa mabao 5-0 kama walivyofanya kwenye mechi zao mbili za awali za ligi msimu huu.

“Unajua wapinzani wakikaa nyuma mechi inakuwa ngumu sana, na nafasi tulitengeneza nyingi lakini walikuwa nyuma muda wote, endapo zile nafasi tungefunga mabao basi zingefika zile goli zetu (mabao 5-0) lakini haikuwa bahati tukafunga hilo moja,” alisema Mudathir.


The post Mudathir: Maelekezo ya Gamondi yalizaa bao first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/23/mudathir-maelekezo-ya-gamondi-yalizaa-bao/feed/ 0
Mudathir aokoa jahazi Yanga https://www.greensports.co.tz/2023/09/20/mudathir-aokoa-jahazi-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/20/mudathir-aokoa-jahazi-yanga/#respond Wed, 20 Sep 2023 19:35:31 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7813 Na mwandishi wetuMudathir Yahya leo Jumatano ameiokoa Yanga kugawana pointi na Namungo baada ya kufunga bao pekee la ushindi katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.Mudathir aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Clement Mzize alifunga bao hilo katika dakika ya 88 akimalizia pasi ya Aziz Ki […]

The post Mudathir aokoa jahazi Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mudathir Yahya leo Jumatano ameiokoa Yanga kugawana pointi na Namungo baada ya kufunga bao pekee la ushindi katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Mudathir aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Clement Mzize alifunga bao hilo katika dakika ya 88 akimalizia pasi ya Aziz Ki ambaye aliunganishiwa mpira na Kouassi Yao kutoka upande wa kulia wa Yanga.
Bao hilo lilikuja baada ya Namungo kuonesha uhai kwa muda mrefu wa mchezo kwa kujihami vizuri, kuitibulia Yanga na wakati mwingine kufanya mashambulizi yaliyoibua hofu langoni mwa wapinzani wao.
Kipindi chote cha kwanza, Namungo inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Cedric Kaze ilicheza vizuri, haikuonekana kuwa dhaifu mbele ya Yanga ambayo imetoka kushindi mabao matano kila mechi katika mechi zake mbili zilizopita za ligi hiyo.
Namungo wakati mwingine ilionekana kuwa tishio kwenye lango la Yanga kiasi cha kutoa dalili za kumaliza mchezo kwa sare au hata kuibuka na ushindi ambao ungekuwa wa kwanza dhidi ya Yanga tangu timu hiyo ipande daraja na kushiriki ligi kuu.
Dakika za 78 na 79 Namungo walifanya mashambulizi mawili ambayo yaliwaweka katika hali ya hofu mashabiki wa Yanga ambao baadhi yao walianza kupoteza matumaini ya kutoka na ushindi katika mechi hiyo.
Katika shambulizi la kwanza, winga wa zamani wa Simba, Shiza Kichuya akiwa upande wa kushoto karibu na lango la Yanga aliunasa mpira na kupiga shuti dhaifu ambalo ilikuwa kama kumpasia kipa Diarra aliyeutuliza mpira kwenye himaya yake kiurahisi.
Baada ya shambulizi hilo Namungo walirudi tena langoni mwa Yanga ambapo Buswita akiwa katika nafasi nzuri aliunasa mpira na kupiga shuti kubwa ambalo halikuwa na madhara yoyote langoni mwa Yanga.
Yanga nao walifanya mashambulizi kadhaa ikiwamo lile la dakika ya 56 baada ya Pacome Zouazoua kuinasa pasi ya Aziz Ki na kumchungulia kipa wa Namungo, Deo Munishi Dida lakini shuti la Zouazoua lilitua mikononi mwa Dida.
Dakika ya 68 kwa mara nyingine Yanga walifanya shambulizi baada ya Aziz Ki kuambaa na mpira na kuwazidi ujanja mabeki wa Namungo kabla ya kufumua shuti la chinichini lakini kwa mara nyingine Dida alionesha umahiri wake kwa kuinyima Yanga bao.
Kwa ushindi huo Yanga imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikiwa imefikisha pointi tisa na mabao 11 katika mechi tatu. Ligi hiyo itaendelea kesho Alhamisi kwa mechi kati ya Simba na Coastal Union na Azam FC dhidi ya Singida Fountain Gate au Singida Big Stars.

The post Mudathir aokoa jahazi Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/20/mudathir-aokoa-jahazi-yanga/feed/ 0
Mudathir: Nilikabidhiwa Fei Toto https://www.greensports.co.tz/2023/08/11/mudathir-nilikabidhiwa-fei-toto/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/11/mudathir-nilikabidhiwa-fei-toto/#respond Fri, 11 Aug 2023 05:05:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7327 Kiungo wa kati wa Yanga, Mudathir Yahya amesema upinzani mkubwa ulioibuka kati yake na Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam FC, ulitokana na maelekezo maalumu kutoka kwa kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi.Katika mchezo huo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii, Fei Toto, alishindwa kutamba kama yale mashuti yake aliyokuwa akiyapiga wakati akiichezea […]

The post Mudathir: Nilikabidhiwa Fei Toto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Kiungo wa kati wa Yanga, Mudathir Yahya amesema upinzani mkubwa ulioibuka kati yake na Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam FC, ulitokana na maelekezo maalumu kutoka kwa kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi.
Katika mchezo huo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii, Fei Toto, alishindwa kutamba kama yale mashuti yake aliyokuwa akiyapiga wakati akiichezea Yanga huku mara kadhaa wawili wakionekana kugongana, kukamiana na kukabana kwa nguvu.
Kiungo huyo alisema kabla ya kwenda kwenye mchezo huo walifanya kikao maalumu na kuwachambua wapinzani ikiwemo kufatilia uwezo wa mchezaji mmoja mmoja ikiwemo kubaini uwezo na madhara yao na yeye alikabidhiwa kumkaba Fei Toto.

“Kocha alinikabidhi Fei Toto akaniambia asicheze yeye wala kuichezesha timu na mimi nilitimiza jukumu alilonipa kocha wangu ndio maana Azam hawakufanya shambulizi lolote la hatari kwenye lango letu,” alisema Mudathir.


Kiungo huyo alisema anajivunia kutimiza majukumu yake vizuri kwani imemuongezea uhakika wa kupata nafasi ya kucheza chini ya kocha huyo lakini pia anaamini ameisaidia timu yake kupata ushindi katika mchezo muhimu kama huo.
Alisema mbali na yeye kufanikiwa kumdhibiti Fei lakini kilichowasaidia kushinda mchezo huo ni timu nzima kucheza kwa umakini na kufuata vyema mbinu na maelekezo waliyopewa na kocha wao.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kutinga fainali ya Ngao ya Jamii itakayochezwa Jumapili hii.

The post Mudathir: Nilikabidhiwa Fei Toto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/11/mudathir-nilikabidhiwa-fei-toto/feed/ 0
Mudathir ajiandaa kwa vita ya namba https://www.greensports.co.tz/2023/08/02/mudathir-ajiandaa-kwa-vita-ya-namba/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/02/mudathir-ajiandaa-kwa-vita-ya-namba/#respond Wed, 02 Aug 2023 11:52:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7221 Na mwandishi wetuKiungo Mudathir Yahya amesema anajipanga vya kutosha kuhakikisha anaendelea kudumu kwenye kikosi cha Yanga msimu ujao licha ya kuwa na wakati mzuri msimu uliopita.Mudathir amefafanua hayo akisema kwa sasa anajipanga vilivyo kwenye mazoezi ya kujiweka sawa kwani kuna wachezaji wapya wazuri wamesajiliwa, hivyo anahitaji kujiandaa zaidi ili kuonekana miongoni mwao.“Mazoezi ya maandalizi kwa […]

The post Mudathir ajiandaa kwa vita ya namba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo Mudathir Yahya amesema anajipanga vya kutosha kuhakikisha anaendelea kudumu kwenye kikosi cha Yanga msimu ujao licha ya kuwa na wakati mzuri msimu uliopita.
Mudathir amefafanua hayo akisema kwa sasa anajipanga vilivyo kwenye mazoezi ya kujiweka sawa kwani kuna wachezaji wapya wazuri wamesajiliwa, hivyo anahitaji kujiandaa zaidi ili kuonekana miongoni mwao.
“Mazoezi ya maandalizi kwa wakati huu ni muhimu sana, lazima upige sana kazi, ujipange maana kuna watu wengi wamekuja kufanya kazi, kwa hiyo usipofanya kazi utaishia kukaa nje na kusema sipendwi, sithaminiki lakini ukifanya kazi kila kitu kipo sawa,” alisema Mudathir aliyewahi kukipiga Azam FC.
Mchezaji huyo alisema kwa kuwa timu hiyo ina kocha mpya, Miguel Gamondi ni wazi kwamba kila kitu kinaanza upya hivyo ni lazima kujitahidi kuonesha kiwango sasa ili kuonesha ushawishi.

“Ukifanya masihara kipindi hiki, unaweza kukosa namba sababu wakati huu kocha anaangalia vitu vipya, haichezi historia eti kwa kuwa nimecheza fainali basi. Lazima ufanye kazi, kocha mpya akija hamjui yeyote yule, kwa hiyo cha msingi ni kuonesha kazi na kumskiliza kocha anasemaje,” alisema Mudathir.


Mudathir alisajiliwa Yanga kwenye dirisha dogo msimu uliopita kama mchezaji huru na kufanikiwa kucheza kwa kiwango cha juu akiwa miongoni mwa wachezaji tegemeo waliofanikisha Yanga kutwaa makombe matatu na kuingia fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza.

The post Mudathir ajiandaa kwa vita ya namba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/02/mudathir-ajiandaa-kwa-vita-ya-namba/feed/ 0
Mudathir kinara bao bora CAF https://www.greensports.co.tz/2023/04/05/mudathir-kinara-bao-bora-caf/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/05/mudathir-kinara-bao-bora-caf/#respond Wed, 05 Apr 2023 15:33:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5695 Na mwandishi wetuKiungo wa Yanga, Mudathir Yahya leo Jumatano amefanikiwa kuibuka kidedea kwa kuwa mfungaji wa bao bora la michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi msimu huu.Mudathir ameibuka mshindi akiwabwaga Aymen Mahous wa USM Alger alipoifunga FC Lupopo, Aubin Kramo wa Asec Mimosas alipoinyoosha Diables Noirs na Paul Acquah wa Rivers United […]

The post Mudathir kinara bao bora CAF first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya leo Jumatano amefanikiwa kuibuka kidedea kwa kuwa mfungaji wa bao bora la michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi msimu huu.
Mudathir ameibuka mshindi akiwabwaga Aymen Mahous wa USM Alger alipoifunga FC Lupopo, Aubin Kramo wa Asec Mimosas alipoinyoosha Diables Noirs na Paul Acquah wa Rivers United dhidi ya DC Motema Pembe.
Mchezaji huyo ameshinda kupitia bao lake alilowafunga TP Mazembe kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam katika ushindi wa mabao 3-1 walioupata Yanga katika mechi hiyo.
Kiungo huyo amewaangusha wapinzani wake kwa kura asilimia 70 dhidi ya Aymen mwenye asilimia 21, Kouame asilimia 5 na mwisho ni Acquah aliyeambualia asilimia tatu.
Kura hizo zilianza kupigwa juzi na mashabiki kupitia ukurasa wa mtandao wa Twitter wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wa michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.
Mudathir na Farid Mussa ambao wote wamewahi kukipiga Azam ndio wachezaji pekee wazawa wa Yanga waliofunga mabao katika hatua hiyo ambapo Yanga imefunga jumla ya mabao tisa na kufungwa manne.
Mabao mengine saba ya Yanga yamefungwa na Fiston Mayele, Tuisila Kisinda, Kennedy Musonda na Jesus Moloko ambao wote ni wachezaji wa kigeni.
Kwenye Ligi ya Mabingwa bao la Mahmoud Karhaba wa Al Ahly alilowafunga Al Hilal ndio limekuwa kinara dhidi ya mengine yaliyofungwa na Hamdou El Houni wa Esperance dhidi ya CR Belouizdad, Makabi Lilepo wa Al Hilal alipoichapa Coton Sport na Teboho Mokoena wa Mamelodi Sundowns walipocheza na Al Ahly.

The post Mudathir kinara bao bora CAF first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/05/mudathir-kinara-bao-bora-caf/feed/ 0
Mudathir akataa mkataba Azam https://www.greensports.co.tz/2022/08/02/mudathir-akataa-mkataba-mpya-azam/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/02/mudathir-akataa-mkataba-mpya-azam/#respond Tue, 02 Aug 2022 14:39:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2097 Na mwandishi wetuUongozi wa timu ya Azam umefunguka kuwa haikuwa matakwa yao kuachana na kiungo wao, Mudathir Yahya isipokuwa mchezaji huyo aligoma kusaini mkataba mpya na klabu hiyo.Jana Azam ilitangaza kuachana na Mudathir na kuibua hisia za kwanini wameachana na mchezaji huyo ambaye ni miongoni mwa wanaofanya vizuri kwa sasa na ndipo Azam ilipotangaza sababu […]

The post Mudathir akataa mkataba Azam first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Uongozi wa timu ya Azam umefunguka kuwa haikuwa matakwa yao kuachana na kiungo wao, Mudathir Yahya isipokuwa mchezaji huyo aligoma kusaini mkataba mpya na klabu hiyo.
Jana Azam ilitangaza kuachana na Mudathir na kuibua hisia za kwanini wameachana na mchezaji huyo ambaye ni miongoni mwa wanaofanya vizuri kwa sasa na ndipo Azam ilipotangaza sababu zake za kwanini hayo yametokea.
Ofisa Habari wa Azam, Thabiti Zakaria amefafanua kuwa walimpa mapema Mudathir ofa ya mkataba mpya baada ya mkataba wake wa awali kumalizika Juni 30 mwaka huu lakini hakusaini mkataba huo mpaka mwezi Julai unamalizika na ndipo nao walipoamua kuchukua maamuzi.
“Baada ya kutamatika kwa mkataba wake Juni 30, akawekewa mezani mkataba mpya, hakuusaini, klabu ikaendelea kumsubiri mpaka Julai imeisha, hivyo hatua ya kwanza iliyofanyika ni kuitoa namba 27 aliyokuwa akiivaa na kupewa mchezaji mwingine, Malickou Ndoye.
“Tulifanya hivyo kwa sababu mchezaji tuliyekuwa tukimsubiri (Mudathir) hivyo timu ikaamua kuendelea na maisha mengine lakini kama nilivyosema kama ilivyo kwa wengine walioondoka tunawatakia maisha mema ya mpira huko waendako, na hapa Azam ni sehemu ya maisha yao muda wowote wakitaka kurudi hapa wanakaribishwa,” alisema Zakaria.
Mudathir ameondoka Azam baada ya kuitumikia tangu mwaka 2011 akiwa timu ya vijana kabla ya baadaye kupandishwa timu kubwa na msimu wa 2017/18 kupelekwa kwa mkopo Singida United alikoonesha kiwango kikubwa na kisha kurejea Azam msimu uliofuata.
Inaelezwa kuwa Mudathir tayari amemalizana na Singida Big Stars inayonolewa na kocha wa zamani wa Singida United, Hans van Der Pluijm ikiwa ni mipango ya kuiimarisha timu hiyo kuelekea msimu ujao.

The post Mudathir akataa mkataba Azam first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/02/mudathir-akataa-mkataba-mpya-azam/feed/ 0