Lusajo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 04 Jun 2024 07:10:36 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Lusajo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mgunda, Lusajo wang’ara mwezi Mei https://www.greensports.co.tz/2024/06/04/mgunda-lusajo-wangara-mwezi-mei/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/04/mgunda-lusajo-wangara-mwezi-mei/#respond Tue, 04 Jun 2024 07:10:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11212 Na mwandishi wetuKaimu kocha mkuu Simba, Juma Mgunda ameteuliwa kuwa kocha bora wa mwezi Mei huku mshambuliaji wa Mashujaa FC, Reliant Lusajo akiteuliwa mchezaji bora, wote kwa msimu huu wa 2023-24 wa Ligi Kuu NBC.Taarifa ya Idara ya habari, mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilimtaja Lusajo kuwa mshindi akiwabwaga, Stephane Aziz Ki […]

The post Mgunda, Lusajo wang’ara mwezi Mei first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kaimu kocha mkuu Simba, Juma Mgunda ameteuliwa kuwa kocha bora wa mwezi Mei huku mshambuliaji wa Mashujaa FC, Reliant Lusajo akiteuliwa mchezaji bora, wote kwa msimu huu wa 2023-24 wa Ligi Kuu NBC.
Taarifa ya Idara ya habari, mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilimtaja Lusajo kuwa mshindi akiwabwaga, Stephane Aziz Ki wa Yanga na Feisal Salum au Fei Toto wa Azam FC.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kamati ya tuzo hizo ya TFF ilimteua Lusajo kwa kuwa alikuwa msaada mkubwa kwa timu yake katika ushindi wa mechi nne kati ya sita za timu hiyo kwa kipindi cha mwezi Mei.
Mchango wa Lusajo uliiwezesha Mashujaa kukusanya pointi 12 na hivyo kupanda kutoka nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC hadi nafasi ya nane huku Lusajo akifunga mabao matano na kuwa ‘mpishi’ wa mabao mengine mawili.
Kwa upande wa Mgunda ambaye aliteuliwa kukaimu nafasi hiyo baada ya Abdelhak Benchikha kuamua kuachia ngazi, yeye ameiwezesha Simba katika kipindi hicho kushinda mechi zake dhidi ya Tabora United, Azam, Prisons, Geita, KMC, JKT na kutoka sare ya 1-1 na Kagera Sugar.
Mgunda katika kinyang’anyiro cha kocha bora wa mwezi Mei alikuwa akishindana na Miguel Gamondi wa Yanga na Bruno Ferry wa Azam.
Kamati ya tuzo pia imemteua meneja wa Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Juma Amir kuwa meneja bora wa mwezi Mei kutokana na usimamizi mzuri wa matukio ya uwanjani pamoja na masuala yanayohusu miundombinu ya uwanja

The post Mgunda, Lusajo wang’ara mwezi Mei first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/04/mgunda-lusajo-wangara-mwezi-mei/feed/ 0
Lusajo kutupia mabao ya kutosha Mashujaa https://www.greensports.co.tz/2024/02/28/lusajo-kutupia-mabao-ya-kutosha-mashujaa/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/28/lusajo-kutupia-mabao-ya-kutosha-mashujaa/#respond Wed, 28 Feb 2024 07:07:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9910 Na mwandishi wetuMshambuliaji wa Mashujaa, Reliant Lusajo ametamba kuifungia timu hiyo mabao ya kutosha kuliko alivyokuwa Namungo FC.Akizungumza na GreenSports, mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga alisema anaamini atalitimiza hilo kutokana na uwepo wa viungo wenye uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi.“Kazi yangu ni kufunga na ninaamini nitafunga mabao mengi sana sababu tuna viungo wenye uwezo […]

The post Lusajo kutupia mabao ya kutosha Mashujaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Mashujaa, Reliant Lusajo ametamba kuifungia timu hiyo mabao ya kutosha kuliko alivyokuwa Namungo FC.
Akizungumza na GreenSports, mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga alisema anaamini atalitimiza hilo kutokana na uwepo wa viungo wenye uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi.
“Kazi yangu ni kufunga na ninaamini nitafunga mabao mengi sana sababu tuna viungo wenye uwezo wa kutoa pasi za mwisho na kufunga lakini pia nafasi ambayo kocha ananipanga inanipa urahisi wa kufanya hivyo,” alisema Lusajo.
Mchezaji huyo alisema mbali na uwepo wa viungo wengi wa kutengeneza nafasi lakini ana ushirikiano mzuri na mshambuliaji mwenzake Adam Adam hivyo hilo ni moja ya jambo ambalo linampa nguvu ya kuendeleza kile alichokifanya akiwa Namungo.
Alisema lengo lao yeye na mwenzake ni kuipigania timu hiyo kuondoka nafasi mbaya iliyopo hivi sasa na kukaa nafasi za juu ili kuendelea kushiriki Ligi Kuu NBC msimu ujao.
Lusajo aliyejiunga na timu hiyo kwenye dirisha dogo msimu huu, tayari ameifungia Mashujaa yenye maskani yake Kigoma mabao mawili katika michezo minne iliyopita.

The post Lusajo kutupia mabao ya kutosha Mashujaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/28/lusajo-kutupia-mabao-ya-kutosha-mashujaa/feed/ 0
Lusajo aondoka Namungo https://www.greensports.co.tz/2023/12/28/lusajo-aondoka-namungo/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/28/lusajo-aondoka-namungo/#respond Wed, 27 Dec 2023 21:14:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9024 Na mwandishi wetuMshambuliaji mahiri wa Namungo FC, Reliants Lusajo (pichani) ameaga kwenye timu hiyo katika dirisha hili la usajili ili kwenda kutafuta changamoto kwingine.Nyota huyo wa zamani wa Toto Africans ya Mwanza, Yanga na KMC za Dar es Salaam amewaaga mashabiki wa Namungo tayari kwa ajili ya changamoto mpya.Hadi anaondoka Namungo msimu huu Lusajo amefunga […]

The post Lusajo aondoka Namungo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji mahiri wa Namungo FC, Reliants Lusajo (pichani) ameaga kwenye timu hiyo katika dirisha hili la usajili ili kwenda kutafuta changamoto kwingine.
Nyota huyo wa zamani wa Toto Africans ya Mwanza, Yanga na KMC za Dar es Salaam amewaaga mashabiki wa Namungo tayari kwa ajili ya changamoto mpya.
Hadi anaondoka Namungo msimu huu Lusajo amefunga mabao mawili akiwa na Wauaji hao wa Kusini ambao wanashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC wakiwa na pointi 17.
Lusajo alisema kuwa baada ya kufanya kazi Namungo kwa zaidi ya misimu miwili anaamini kuwa ni wakati sahihi kwake kwenda kutafuta changamoto mpya mahala pengine bila ya kusema anakwenda kutua wapi.
“Napenda Kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi mzima wa Namungo na benchi la ufundi bila kusahau mashabiki wote wa timu ya Namungo kwa kipindi chote tulichokua pamoja.

“Ni muda wangu sasa wa kuangalia changamoto sehemu nyingine, nipende kuwatakia kila la kheri katika msimu huu wa ligi kuu, muda ukifika nitaweka wazi nitakuwa wapi,” alisema Lusajo.


The post Lusajo aondoka Namungo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/28/lusajo-aondoka-namungo/feed/ 0
Lusajo aanza mbio ufungaji bora https://www.greensports.co.tz/2022/08/16/lusajo-aanza-mbio-ufungaji-bora/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/16/lusajo-aanza-mbio-ufungaji-bora/#respond Tue, 16 Aug 2022 12:09:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2388 Na mwandishi wetuMshambuliaji wa Namungo, Reliants Lusajo ni kama vile ameanza mapema mbio za kuwania tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu wa 2022/23 baada ya kufunga mabao mawili kwenye mechi yao ya kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar.Lusajo amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao mawili kwenye mechi moja msimu huu katika […]

The post Lusajo aanza mbio ufungaji bora first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Namungo, Reliants Lusajo ni kama vile ameanza mapema mbio za kuwania tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu wa 2022/23 baada ya kufunga mabao mawili kwenye mechi yao ya kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar.
Lusajo amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao mawili kwenye mechi moja msimu huu katika sare ya mabao 2-2 kwenye mchezo huo uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Mchezaji huyo msimu uliopita alikuwa akipigana vikumbo kwenye kuwania kiatu cha ufungaji bora kilichotua kwa George Mpole wa Geita Gold aliyefunga mabao 17 dhidi ya Fiston Mayele aliyefunga mabao 16 huku Lusajo akimaliza wa tatu kwa mabao yake 10.
Pamoja ya kuanza vyema msimu huu lakini Lusajo amejiweka kando katika mbio hizo akidai jukumu lake la kwanza ni kuisaidia timu hiyo pekee hivyo hata akiwa anafunga hapigi hesabu zake binafsi zaidi ya hesabu za kuisaidia timu kwanza.
“Nashukuru Mungu kwa kufunga mabao hayo mawili lakini kwangu kikubwa ninachokiangalia zaidi ni timu yetu kufanya vizuri, siyo mimi binafsi ingawa ni muhimu lakini zaidi tunaangalia timu sio mtu mmoja mmoja.
“Ndiyo maana nasema nimejiandaa vizuri kwa ajili ya timu, ndiyo iliyotuweka hapa na ndiyo tunayoipambania, ninaamini tutaendelea kujitoa na kufanya vizuri kwa ajili ya timu kwanza,” alisema Lusajo mshambuliaji wa zamani wa Yanga.
Msimu uliopita wa 2021/22, Lusajo alionyesha matumaini katika kuwania tuzo ya mfungaji bora lakini kadri ligi ilivyokuwa ikienda kasi yake ilianza kupungua na akawaacha Mayele na Mpole wakichuana kabla ya Mpole kuibuka kinara.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa jana, Ihefu ilishindwa kutamba nyumbani baada ya kulala kwa bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting.

The post Lusajo aanza mbio ufungaji bora first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/16/lusajo-aanza-mbio-ufungaji-bora/feed/ 0