Luis Suarez - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 12 Sep 2025 19:32:31 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Luis Suarez - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Suarez afungiwa mechi sita https://www.greensports.co.tz/2025/09/07/suarez-afungiwa-mechi-sita/ https://www.greensports.co.tz/2025/09/07/suarez-afungiwa-mechi-sita/#respond Sun, 07 Sep 2025 09:47:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13883 Miami, MarekaniMshambuliaji wa klabu ya Inter Miami ya Marekani, Luis Suarez amefungiwa mechi sita kwa kosa la kumtemea mate mmoja wa viongozi katika benchi la ufundi la klabu ya Seattle Sounders.Tukio hilo lilitokea baada ya mechi ya Kombe la Ligi baina ya timu hizo iliyoisha kwa Sounders kutoka na ushindi wa mabao 3-0 ingawa baadaye […]

The post Suarez afungiwa mechi sita first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Miami, Marekani
Mshambuliaji wa klabu ya Inter Miami ya Marekani, Luis Suarez amefungiwa mechi sita kwa kosa la kumtemea mate mmoja wa viongozi katika benchi la ufundi la klabu ya Seattle Sounders.
Tukio hilo lilitokea baada ya mechi ya Kombe la Ligi baina ya timu hizo iliyoisha kwa Sounders kutoka na ushindi wa mabao 3-0 ingawa baadaye Suarez alijilaumu kwa kosa hilo na kuomba msamaha.
Mara baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya kumaliza mchezo, wachezaji na baadhi ya viongozi wa timu hizo mbili walianza kuzozana na kushikana na ndipo Suarez alipomtemea mate mmoja wa makocha wa timu pinzani.
Kabla ya tukio hilo, Suarez ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 38, alionekana akimkwida shingoni kiungo wa Sounders, Obed Vargas lakini wachezaji wanzake waliingilia kati.
Baada ya tukio hilo, Suarez alionekana kwa mara nyingine akizozana na mkurugenzi wa usalama wa Sounders, Gene Ramirez lakini mchezaji mwenzake Oscar Ustari alimzuia na ndipo mchezaji huyo alipoamua kumtemea mate mmoja wa makocha wa Sounders.
Kamati ya Nidhamu ya Kombe la Ligi katika taarifa yake ilifafanua kuwa adhabu ya Suarez itaanza kutumika mwakani katika michuano ya kombe hilo ingawa mamlaka za Ligi Kuu Marekani au Major League Soccer (MLS) nao wanaweza kumuongezea adhabu.
Sambamba na Suarez wachezaji wengine wa Inter Miami waliokumbana na adhabu ni Sergio Busquets aliyefungiwa mechi mbili na Tomas Aviles amefungiwa mechi tatu wakati mjumbe wa benchi la ufundi la Sounders, Steven Lenhart amefungiwa mechi tano.
Suarez, nyota wa zamani wa Liverpool na Barcelona amekuwa akiandamwa na matukio yaliyojaa utata, akiwa Liverpool alifungiwa mechi nane kwa kumfanyia dhihaka za ubaguzi wa rangi beki wa Man United Patrice Evra.
Mchezaji huyo pia amewahi kufungiwa kwa matukio matatu ya kuwang’ata wachezaji wa timu pinzani katika mechi wakati akizichezea timu za Ajax, Liverpool na timu yake ya taifa ya Uruguay.

The post Suarez afungiwa mechi sita first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/09/07/suarez-afungiwa-mechi-sita/feed/ 0
Suarez amtemea mate kocha, aomba radhi https://www.greensports.co.tz/2025/09/06/suarez-amtemea-mate-kocha-aomba-radhi/ https://www.greensports.co.tz/2025/09/06/suarez-amtemea-mate-kocha-aomba-radhi/#respond Sat, 06 Sep 2025 15:04:26 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13871 Miami, MarekaniMshambuliaji wa timu ya Inter Miami ya Marekani, Luis Suarez (pichani) ameomba radhi kwa kitendo chake cha kumtemea mate mmoja wa watu wa benchi la ufundi la timu ya Seattle Sounders.Suarez, mshambuliaji wa zamani wa timu za Barcelona na Liverpool, alifanya kitendo hicho atika mechi ya fainali ya ligi baina ya timu hizo, mechi […]

The post Suarez amtemea mate kocha, aomba radhi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Miami, Marekani
Mshambuliaji wa timu ya Inter Miami ya Marekani, Luis Suarez (pichani) ameomba radhi kwa kitendo chake cha kumtemea mate mmoja wa watu wa benchi la ufundi la timu ya Seattle Sounders.
Suarez, mshambuliaji wa zamani wa timu za Barcelona na Liverpool, alifanya kitendo hicho atika mechi ya fainali ya ligi baina ya timu hizo, mechi ambayo Miami ililala kwa mabao 3-0.
Akizungumzia tukio lilivyokuwa Suarez alisema kulikuwa na mazingira ya kuvurugwa na kuchanganyikiwa baada ya mechi na kwamba tukio walilofanyiwa halikutakiwa kufanywa.
Suarez hata hivyo alisema kwamba mazingira ya tukio hilo bado hayatoshi kuwa sababu ya kitendo alichokifanya kwani hakikuwa sahihi na anaomba radhi kwa hilo.
Tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya kumalizika kwa mechi hiyo ambapo uliibuka mzozo baina ya wachezaji wa timu hizo mbili hali iliyomtia hasira Suarez na ndipo alipofanya kosa hilo.
Katika mzozo wa wachezaji hao, Suarez alimkwida shingoni kiungo wa Sounders, Obed Vargas wakati huo huo mchezaji mwenzake Sergio Busquets naye aliingilia kati.
Muda mfupi baadaye, Suarez alianza kuzozana na makocha wa Sounders kabla ya kuzuiwa na mchezaji mwenzake, Oscar Ustari na ndipo mchezaji huyo alipomtemea mate mmoja wa makocha wa Sounders.
“Najisikia vibaya kwa kilichotokea, na sitaki kujinyima nafasi ya kukiri hilo na kuomba msamaha kwa kila mtu ambaye aliumizwa na kile nilichokifanya,” alisema Suarez.
Baada ya Suarez kuomba msamaha mjadala ulioibuka ni kuhusu adhabu atakayopewa mchezaji huyo ambaye pia aliwahi kuingia katika matatizo akihusishwa na matukio matatu ya kuwang’ata wachezaji wa timu pinzani wakati akiichezea Ajax, Liverpoo na timu yake ya taifa ya Uruguay.

The post Suarez amtemea mate kocha, aomba radhi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/09/06/suarez-amtemea-mate-kocha-aomba-radhi/feed/ 0
Luis Suarez aitwa kikosini Uruguay https://www.greensports.co.tz/2023/11/14/luis-suarez-aitwa-kikosini-uruguay/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/14/luis-suarez-aitwa-kikosini-uruguay/#respond Tue, 14 Nov 2023 06:22:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8443 Montevideo, UruguayMshambuliaji wa zamani wa Barca na Liverpool, Luis Suarez (pichani) ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uruguay kitakachoivaa Argentina keshokutwa Alhamisi katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026.Suarez mwenye umri wa miaka 36 ambaye kwa sasa anaichezea Gremio ya Brazil ndiye mfungaji bora wa ligi ya Brazil Serie A akiwa na […]

The post Luis Suarez aitwa kikosini Uruguay first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Montevideo, Uruguay
Mshambuliaji wa zamani wa Barca na Liverpool, Luis Suarez (pichani) ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uruguay kitakachoivaa Argentina keshokutwa Alhamisi katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026.
Suarez mwenye umri wa miaka 36 ambaye kwa sasa anaichezea Gremio ya Brazil ndiye mfungaji bora wa ligi ya Brazil Serie A akiwa na mabao 14 katika mechi 29 na anajiandaa kuivaa Argengtina ya Lionel Messi.
Baada ya mechi hiyo itakayopigwa mjini Buenos Aires, Suarez na timu yake ya Uruguay wataingia uwanjani tena kuivaa Bolivia siku tano baadaye.
Argentina ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia wanaongoza Kundi la Marekani Kusini katika mbio za kufuzu Kombe la Dunia wakiwa na pointi 12 katika mechi nne.
Mechi ya Argentina na Uruguay itawakutanisha Messi na Suarez ambao waliwahi kuwa pamoja katika klabu ya Barca huku Suarez akiwa njiani kuungana tena na Messi katika klabu ya Inter Miami FC ya Marekani.
Kocha wa Gremio, Renato Gaucho alithibitisha kuwa Suarez ataondoka katika klabu hiyo Desemba mwaka huu licha ya kwamba ndio kwanza yuko nusu ya mkataba wake wa miaka miwili aliousaini mwaka 2022.
Suarez amekubali kusaini mkataba wa mwaka mmoja na Inter Miami huku mkataba huo ukiwa na kipengele kinachompa fursa ya kuongeza mwaka mwingine mmoja kama atakuwa tayari kufanya hivyo.
Kikosi kamili cha Uruguay, makipa: Sergio Rochet (Internacional), Franco Israel (Sporting Lisbon), Santiago Mele (Junior Barranquilla)
Mabeki: Ronald Araujo (Barca), José María Giménez (Atletico Madrid), Sebastián Cáceres (America), Matías Viña (Sassuolo), Bruno Méndez (Corinthians), Guillermo Varela (Flamengo) na Mathías Olivera (Napoli).
Viungo: Manuel Ugarte (Paris Saint-Germain), Rodrigo Bentancur (Tottenham), Federico Valverde (Real Madrid), Felipe Carballo (Gremio), Agustín Canobbio (Athletico Paranaense), Nicolás de la Cruz (River Plate), Giorgian de Arrascaeta (Flamengo), Facundo Pellistri (Manchester United), Maximiliano Araújo (Toluca) na Facundo Torres (Orlando City)
Washambuliaji: Cristian Olivera (Los Angeles FC), Federico Viñas (Leon), Darwin Núñez (Liverpool) na mkongwe Luis Suárez (Gremio)

The post Luis Suarez aitwa kikosini Uruguay first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/14/luis-suarez-aitwa-kikosini-uruguay/feed/ 0