Kombe la Dunia - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 15 Dec 2025 09:34:35 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Kombe la Dunia - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Wenger atetea timu 48 kombe la dunia https://www.greensports.co.tz/2025/12/10/wenger-atetea-timu-48-kombe-la-dunia/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/10/wenger-atetea-timu-48-kombe-la-dunia/#respond Wed, 10 Dec 2025 18:42:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14148 Washington, MarekaniMkurugenzi wa Maendeleo ya Soka wa Fifa, Arsene Wenger ametetea uamuzi wa ongezeko la idadi ya timu kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 kufikia 48 akisema hiyo ni idadi sahihi kwa fainali hizo.Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazofanyika katika nchi za Canada, Marekani na Mexico zitakuwa za kwanza kushirikisha timu 48 kutoka […]

The post Wenger atetea timu 48 kombe la dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Washington, Marekani
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soka wa Fifa, Arsene Wenger ametetea uamuzi wa ongezeko la idadi ya timu kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 kufikia 48 akisema hiyo ni idadi sahihi kwa fainali hizo.
Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazofanyika katika nchi za Canada, Marekani na Mexico zitakuwa za kwanza kushirikisha timu 48 kutoka michuano saba iliyopita ambayo ilishirikisha timu 32.
Uamuzi wa kuongeza timu hadi 48 umeibua hofu juu ya uwezekano wa kupoteza ushindani, ubora na hadhi ya fainali hizo lakini Wenger ambaye ni kocha wa zamani wa Arsenal ametetea ongezeko la timu.
Akizungumza mbele ya jopo la maofisa wa Fifa akiwamo kocha wa zamani wa timu ya wanawake ya Marekani, Jill Ellis, kabla ya droo ya fainali hizo, Wenger alisisitiza kuwa timu 48 ni sahihi.

“Naamini timu 48 ni sahihi, ni chini ya asilimia 25 ya nchi 211 wanachama wa Fifa, maana yake ni kwamba timu moja kati ya nne ina nafasi ya kushiriki, pia asilimia 75 ya timu hazitakuwamo,” alisema Wenger.


Kuhusu uwezekano wa ubora wa mashindano kupotea, Wenger alitolea mfano wa michuano ya hivi karibuni ya Kombe la Dunia la Vijana chini ya miaka 17, michuano ambayo pia ilishirikisha timu 48.
Wenger alisema anaamini katika ubora kwa sababu ili ufuzu ni lazima ushinde timu katika bara lako na hiyo ni ishara ya ubora, ni suala la kupata matokeo.
Alisema kwamba swali kuhusu ubora liliulizwa hata kwenye michuano ya vijana chini ya miaka 17 lakini matokeo yake ni kwamba walikutana na ubora uliowashangaza.
“Timu hazimo kwenye fainali za Kombe la Dunia kwa sababu zipo tu zimealikwa, hapana ni kwa sababu zimepata ushindi dhidi ya timu nyingine katika bara lao, suala la ubora linaonekana, angalia playoffs, aina ya wachezaji na aina ya timu zinazocheza,” alisema Wenger.

The post Wenger atetea timu 48 kombe la dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/10/wenger-atetea-timu-48-kombe-la-dunia/feed/ 0
Wazo la timu 64 Kombe la Dunia lapingwa https://www.greensports.co.tz/2025/04/15/wazo-la-timu-64-kombe-la-dunia-lapingwa/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/15/wazo-la-timu-64-kombe-la-dunia-lapingwa/#respond Tue, 15 Apr 2025 16:50:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13249 Miami, MarekaniRais wa Shirkisho la Soka Marekani Kaskazini, Kati na Carribean (Concacaf), Victor Montagliani amepinga wazo la kiongozi wa Shirikisho la Soka Marekani Kusini (CONMEBOL), Alejandro Domínguez kutaka timu shiriki kwenye fainali za Kombe la Dunia 2030 ziwe 64.Domínguez aliwasilisha rasmi wazo la kupanua mashindano hayo kwenye kikao cha Baraza la Fifa kilichoendeshwa kwa mtandao […]

The post Wazo la timu 64 Kombe la Dunia lapingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Miami, Marekani
Rais wa Shirkisho la Soka Marekani Kaskazini, Kati na Carribean (Concacaf), Victor Montagliani amepinga wazo la kiongozi wa Shirikisho la Soka Marekani Kusini (CONMEBOL), Alejandro Domínguez kutaka timu shiriki kwenye fainali za Kombe la Dunia 2030 ziwe 64.
Domínguez aliwasilisha rasmi wazo la kupanua mashindano hayo kwenye kikao cha Baraza la Fifa kilichoendeshwa kwa mtandao akisisitiza timu shiriki ziongezwe kutoka 32 za sasa hadi kufikia 64.
“Kwa upande wetu Concacaf, tumeonesha tupo wazi kwa mabadiliko kwa kuunga mkono fainali za Kombe la Dunia kwa wanawake pamoja na muendelezo wa mabadiliko wa mashirikisho yetu kwa timu za wanaume na wanawake na mashindano ya klabu,” alisema Montagliani.
“Sidhani kama kuongeza timu katika fainali za Kombe la Dunia za wanaume kufikia 64 ni hatua sahihi kwa mashindano hayo pamoja na mustakabali mpana wa soka kwa mashindano ya timu za taifa, klabu, ligi na wachezaji,” alisema Montagliani.
Fifa itaanza kufanya majaribio ya mfumo wa timu 48 kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 lakini Domínguez alisisitiza haja ya kufanya zaidi ya hilo kwa kupanua wigo wa mashindano.
Naye Rais wa Umoja wa Vyama vya Soka Ulaya (Uefa) Aleksander Čeferin pia alionesha kutounga mkono hoja ya Domínguez akisema wazo la kuongeza idadi ya timu ni baya.

“Nafikiri ni wazo baya, si wazo zuri kwa fainali zenyewe za Kombe la Dunia, na pia si wazo zuri kwa timu zinazofuzu, kwa hiyo siungi mkono wazo hili, sijui limetokea wapi lakini ni hatari kwa sababu hatukufahamu lolote kabla ya wazo hili katika Baraza la Fifa,” alisema Ceferin.


Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Soka Asia, (AFC), Sheikh Salman bin Ibrahim alisisitiza kwamba ongezeko la idadi hiyo litahamasisha na kuwa mwanzo wa mvurugano.
“Kama jambo hili litakuwa wazi kwa mabadiliko maana yake ni kwamba mlango utakuwa wazi kwa kuongeza timu 64 lakini kuna mtu pia anaweza kuja na hoja ya kutaka idadi ya timu ifikie 132, mwisho itakuwaje? Ni mvurugano,” alisema Sheikh Salman.
Katika fainali za Kombe la Dunia 2026, majaribio yatafanyika kwa timu 48 ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya fainali hizo zitakazochezwa Marekani, Mexico na Canada.

The post Wazo la timu 64 Kombe la Dunia lapingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/15/wazo-la-timu-64-kombe-la-dunia-lapingwa/feed/ 0
Beckenbauer afariki dunia https://www.greensports.co.tz/2024/01/09/beckenbauer-afariki-dunia/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/09/beckenbauer-afariki-dunia/#respond Tue, 09 Jan 2024 06:07:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9221 Berlin, UjerumaniMwanasoka na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani, Franz Beckenbauer amefariki dunia akiwa na miaka 78 akiacha rekodi ya kubeba Kombe la Dunia akiwa mchezaji mwaka 1974 na baadaye kocha mwaka 1990.Beckenbauer (pichani) ambaye alikuwa beki, mbali na timu ya taifa pia alitamba na Bayern Munich, timu ambayo aliichezea mechi 582 […]

The post Beckenbauer afariki dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Berlin, Ujerumani
Mwanasoka na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani, Franz Beckenbauer amefariki dunia akiwa na miaka 78 akiacha rekodi ya kubeba Kombe la Dunia akiwa mchezaji mwaka 1974 na baadaye kocha mwaka 1990.
Beckenbauer (pichani) ambaye alikuwa beki, mbali na timu ya taifa pia alitamba na Bayern Munich, timu ambayo aliichezea mechi 582 wakati kwenye timu ya taifa amecheza jumla ya mechi 103.
Mbali na mataji ya dunia, Beckenbauer ambaye alipewa jina la utani la ‘Der Kaiser’, pia wakati akiichezea Bayern alibeba taji la Ulaya mwaka 1972 na kushinda tuzo ya Ballon d’Or mara mbili.
Taarifa ya familia ya mchezaji huyo iliyopatikana Jumatatu usiku ilieleza kusikitishwa na msiba huo wa mume na baba wa familia.
“Kwa masikitikio makubwa tunatangaza kuwa mume wangu na baba yetu, Franz Beckenbauer amefariki kwa amani akiwa usingizini usiku wa Jumapili, tunawaomba mtupe nafasi ya kuombeleza kwa ukimya na kujiepusha na kutuuliza maswali yoyote,’ ilieleza taarifa ya familia hiyo.
Taarifa ya klabu ya Bayern ambayo aliichezea kwa mafanikio ilimpamba Beckenbauer kwa kumtaja kuwa ni mmoja wa wanasoka muhimu na mwenye mafanikio.
“Dunia ya Bayern Munich ghafla imekuwa tofauti na ilivyozoeleka, kumekuwa na kiza, ukimya na unyonge, Bayern isingeweza kuwa ilivyo sasa bila ya Beckenbauer,” ilieleza taarifa hiyo.
Beckenbauer enzi zake za soka la ushindani alikuwa akicheza nafasi ya kiungo na anakumbukwa zaidi kwa namna alivyokabana na Sir Bobby Charlton katika mechi ya fainali za Kombe la Dunia 1966, mechi ambayo England ilishinda kwa mabao 4-2 ingawa baadaye Bckenbauer alihamia nafasi ya beki.
Katika fainali za Kombe la Dunia 1966, Beckenbauer alifunga mabao manne na alishinda tuzo ya mchezaji mwenye umri mdogo aliyeshiriki fainali hizo, wakati huo alikuwa na miaka 20.
Beckenbauer ni kati ya wachezaji watatu duniani wenye rekodi ya kubeba Kombe la Dunia wakiwa wachezaji na baadaye makocha.
Katika orodha hiyo yumo Mario Zagallo wa Brazil ambaye alifariki majuzi akiwa na miaka 92 na Didier Deschamps wa Ufaransa ambaye kwa sasa ndiye mchezaji na kocha pekee mwenye rekodi hiyo aliye hai.

The post Beckenbauer afariki dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/09/beckenbauer-afariki-dunia/feed/ 0
Nani mwenyeji mechi ya fainali WC 2030? https://www.greensports.co.tz/2023/10/06/nani-mwenyeji-mechi-ya-fainali-wc-2030/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/06/nani-mwenyeji-mechi-ya-fainali-wc-2030/#respond Fri, 06 Oct 2023 07:33:12 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7969 Zurich, SwitzerlandMorocco, Hispania zimepitishwa kuwa wenyeji wa fainali za Kombe la Dunia *WC) 2030 pamoja na Ureno lakini zipo dalili za kuibuka utata baada ya nchi zote hizo kila moja kutaka uenyeji wa mechi ya fainali.Waziri wa Michezo wa Hispania, Miquel Iceta ametoa kauli inayoonesha dalili za Hispania kuwa mwenyeji wa mechi hiyo akisema hayo […]

The post Nani mwenyeji mechi ya fainali WC 2030? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Zurich, Switzerland
Morocco, Hispania zimepitishwa kuwa wenyeji wa fainali za Kombe la Dunia *WC) 2030 pamoja na Ureno lakini zipo dalili za kuibuka utata baada ya nchi zote hizo kila moja kutaka uenyeji wa mechi ya fainali.
Waziri wa Michezo wa Hispania, Miquel Iceta ametoa kauli inayoonesha dalili za Hispania kuwa mwenyeji wa mechi hiyo akisema hayo ndiyo matarajio yake ingawa alisema huwezi kutegemea kupata kifaranga kabla ya yai kutotolewa.
Kwa upande wake kiongozi wa timu ya Morocco kutoka Shirikisho la Soka Morocco, Fouzi Lekjaa alisema kwamba lengo lao ni kuona mechi ya fainali ikichezwa katika jiji la Casablanca.
Alisema ana matumaini ya kuona juhudi za nchi hiyo zikilipa kwa uwezo wa Mungu akiamini kwamba fainali ya kihistoria itachezwa katika uwanja wa mjini Casablanca.
Fifa ilitangaza juzi Jumatano kuzipa nchi za Morocco, Hispania na Ureno uenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2030 na Uruguay, Argentina na Paraguay kuwa wenyeji wa mechi tatu ambazo zitakuwa maalum kwa kumbukumbu ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa fainali za Kombe la Dunia.
Argentina nayo kwa upande wake baadhi ya maofisa wa serikali ya nchi hiyo wanadaiwa kusema kwamba nchi hiyo itaangalia uwezekano wa kuongezewa mechi nyingine badala ya mechi moja ya ufunguzi.
Lekjaa alisema kwamba nchi za Morocco, Ureno na Hispania zitakutana Oktoba 18 mjini Rabat kujadiliana kuhusu mechi za Kombe la Dunia ambapo nchini Morocco miji sita itakuwa na viwanja vya mechi hizo.

The post Nani mwenyeji mechi ya fainali WC 2030? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/06/nani-mwenyeji-mechi-ya-fainali-wc-2030/feed/ 0
Nigeria yaibana Canada Kombe la Dunia https://www.greensports.co.tz/2023/07/22/nigeria-yaibana-canada-kombe-la-dunia/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/22/nigeria-yaibana-canada-kombe-la-dunia/#respond Sat, 22 Jul 2023 07:40:12 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7060 Melbourne, AustraliaTimu ya Taifa ya Nigeria imeanza na sare ya 0-0 dhidi ya Canada katika mechi yake ya kwanza ya Kundi B ya fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake zinazoendelea New Zealand na Australia.Katika mechi hiyo, Nigeria wana kila sababu ya kujivunia matokeo hayo kwa umahiri waliouonesha ikiwamo kucheza 10 uwanjani na kipa wao, […]

The post Nigeria yaibana Canada Kombe la Dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Melbourne, Australia
Timu ya Taifa ya Nigeria imeanza na sare ya 0-0 dhidi ya Canada katika mechi yake ya kwanza ya Kundi B ya fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake zinazoendelea New Zealand na Australia.
Katika mechi hiyo, Nigeria wana kila sababu ya kujivunia matokeo hayo kwa umahiri waliouonesha ikiwamo kucheza 10 uwanjani na kipa wao, Chiamaka Nnadozie kuokoa mkwaju wa penalti.
Penalti hiyo iliyotolewa muda mfupi baada ya mapumziko ilitokana na rafu ambayo Francisca Ordega alimchezea nahodha wa Canada, Christine Sinclair ambaye ndiye aliyepiga penalti hiyo lakini Nnadozie akaokoa.
Ukiachana na penalti hiyo, Nigeria ilikutwa na majanga mengine baada ya mchezaji wake Deborah Abiodun kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Lawrance ingawa awali alipewa kadi ya njano.
Picha ya VAR ilitumika na kumfanya mwamuzi ampe mchezaji huyo kadi nyekundu hali iliyowafanya Nigeria wabaki 10 uwanjani lakini walipambana na hadi mwisho wa mchezo matokeo yakabaki 0-0 na kuwafanya Nigeria watoke uwanjani kwa furaha.
Kwa Sinclair licha ya kukosa penalti hiyo lakini anashikilia rekodi ya kuwa mmoja wa wachezaji waliofunga kwenye fainali tano za Kombe la Dunia sawa na Marta wa Brazil na Cristiano Ronaldo wa Ureno kwa upande wa wanaume.
Sinclair pia anashikilia rekodi ya kuifungia timu ya Canada mabao 190 katika mechi 324 alizoichezea hadi sasa lakini kwa kukosa penalti anakuwa ameshindwa kumfunga kipa mwenye umri wa miaka 18 ambaye ni mdogo kwake kwa miaka 22.
Matokeo Kombe la Dunia Wanawake 2023
Nigeria 0- 0 Canada
Hispania 3-0 Costa Rica
New Zealand 1-0 Norway
Australia 1-0 Jamhuri ya Ireland
Philippines 0-2 Switzerland

The post Nigeria yaibana Canada Kombe la Dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/22/nigeria-yaibana-canada-kombe-la-dunia/feed/ 0
Morocco yaweka historia Afrika https://www.greensports.co.tz/2022/12/10/morocco-yaweka-historia-afrika/ https://www.greensports.co.tz/2022/12/10/morocco-yaweka-historia-afrika/#respond Sat, 10 Dec 2022 17:54:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4244 Doha, QatarMorocco, leo Jumamosi imekuwa timu ya kwanza Afrika kufikia hatua ya nusu fainali katika historia ya Kombe la Dunia baada ya kuitoa Ureno kwa bao 1-0 katika mechi ya robo fainali, matokeo yaliyotosha kumliza nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo.Baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa, Ronaldo alionekana akiingia katika vyumba vya kubadilishia nguo huku akilia […]

The post Morocco yaweka historia Afrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Doha, Qatar
Morocco, leo Jumamosi imekuwa timu ya kwanza Afrika kufikia hatua ya nusu fainali katika historia ya Kombe la Dunia baada ya kuitoa Ureno kwa bao 1-0 katika mechi ya robo fainali, matokeo yaliyotosha kumliza nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo.
Baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa, Ronaldo alionekana akiingia katika vyumba vya kubadilishia nguo huku akilia wakati mashabiki na wachezaji wa Morocco wakipagawa kwa furaha baada ya kuweka historia mpya ya fainali hizo.
Shujaa wa Morocco alikuwa ni mshambuliaji, Youssef En-Nesyri katika dakika ya 42 akiunganisha kwa kichwa krosi iliyopigwa na Yahya Attiyat-Allah. En-Nesyri alikwenda juu na kuupiga mpira uliomshinda kipa wa Ureno Diogo Costa.
Bao hilo liliamsha shangwe kwa mashabiki wa Morocco waliojazana kwenye Uwanja wa Al Thumama na kuutawala kwa namna walivyokuwa wakiishangilia timu yao mwanzo mwisho.
Nahodha wa Ureno, Bruno Fernandes nusura asawazishe bao hilo lakini shuti alilopiga liligonga mwamba na kuishia kuibua mshtuko kwa mashabiki wa Morocco.
Dakika tano baada ya mapumziko, kocha wa Ureno, Fernando Santos alimuingiza Ronaldo ambaye hata hivyo hakuweza kubadili matokeo ya mchezo huo licha ya kuisumbua safu ya ulinzi ya Morocco mara kadhaa.
Katika kipindi cha pili, Morocco walitumia muda mwingi kujihami kwa umakini wa hali ya juu na katika dakika za majeruhi, timu hiyo ilipata pigo baada ya mshambuliaji wake, Walid Cheddira kupewa kadi ya pili ya njano kwa kucheza rafu na hivyo kuwa nyekundu lakini upungufu huo wa mchezaji mmoja haukuweza kuisaidia Ureno isawazishe bao hilo.
Morocco pamoja na kutumia muda mwingi kujihami lakini haikuacha kuichachafya Ureno na kama si umakini wa safu ya ulinzi ya timu hiyo shambulizi moja la kushtukiza lingeweza kuiumiza zaidi Ureno iliyokuwa ikihaha kusaka bao la kusawazisha.
Ushindi wa Morocco unakuwa historia mpya ya fainali za Kombe la Dunia kwa Afrika ikiwa timu ya kwanza kufikia hatua ya nusu fainali, hapo kabla timu tatu za Cameroon, Senegal na Ghana zilikuwa zikishikilia rekodi ya kufikia hatua ya robo fainali.
Ushindi wa Morocco pia unakumbusha kauli iliyowahi kutolewa na kocha wa timu hiyo, Walid Regragui ambaye baada ya kufuzu hatua ya mtoano alisema kwamba si vibaya kwa timu hiyo kuota kulibeba Kombe la Dunia.
Baada ya ushindi huo wakati mashabiki wakiimba na kushangulia majukwaani, Regragui alibebwa na kurushwa juu na wachezaji wake na sasa kikosi chake kinasubiri mechi ya nusu fainali na mshindi wa mechi nyingine ya robo fainali baadaye leo kati ya Ufaransa na England.

The post Morocco yaweka historia Afrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/12/10/morocco-yaweka-historia-afrika/feed/ 0
Ufaransa, England zatangulia Qatar mapema https://www.greensports.co.tz/2021/11/17/ufaransa-england-zatangulia-qatar/ https://www.greensports.co.tz/2021/11/17/ufaransa-england-zatangulia-qatar/#respond Wed, 17 Nov 2021 11:48:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=472 Berlin, UjerumaniMabingwa watetezi wa Kombe la Dunia, Ufaransa tayari wamefuzu kushiriki fainali hizo zinazotarajia kupigwa mwakani huko Qatar.Timu nyingine ambayo pia imefuzu kushiriki fainali hizo ni England ambao ndoto zao kulitwaa taji hilo mwaka 2018 zilizimwa na Ufaransa baada ya kushindwa kutamba katika mechi ya fainali iliyozikutanisha timu hizo.Timu nyingine ambazo tayari zimefuzu ni pamoja […]

The post Ufaransa, England zatangulia Qatar mapema first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Berlin, Ujerumani
Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia, Ufaransa tayari wamefuzu kushiriki fainali hizo zinazotarajia kupigwa mwakani huko Qatar.
Timu nyingine ambayo pia imefuzu kushiriki fainali hizo ni England ambao ndoto zao kulitwaa taji hilo mwaka 2018 zilizimwa na Ufaransa baada ya kushindwa kutamba katika mechi ya fainali iliyozikutanisha timu hizo.
Timu nyingine ambazo tayari zimefuzu ni pamoja na Denmark, Hispania, Croatia, Uswisi, Ubelgiji,
Uholanzi, Brazil, Serbia, Argentina na wenyeji Qatar.
Timu hizo zitaungana na nyingine 19 kufikisha idadi ya timu 32 zitakazopambana kulibeba taji hilo linaloshindaniwa kila baada ya miaka minne.

The post Ufaransa, England zatangulia Qatar mapema first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2021/11/17/ufaransa-england-zatangulia-qatar/feed/ 0