Kitayosce - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 17 Aug 2023 19:35:55 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Kitayosce - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 TFF yajivua lawama kwa Kitayosce https://www.greensports.co.tz/2023/08/17/tff-yajivua-lawama-kwa-kitayosce/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/17/tff-yajivua-lawama-kwa-kitayosce/#respond Thu, 17 Aug 2023 19:35:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7439 Na mwandishi wetuMtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Almasi Kasongo (pichani) amesema bodi hiyo pamoja na TFF, hawahusiki katika sakata la timu ya Kitayosce kushindwa kutumia wachezaji wake wapya iliyowasajili kwenye dirisha kubwa msimu huu bali ni uzembe wa viongozi wa timu hiyo.Jana timu hiyo ilijikuta ikicheza pungufu ikiwa na wachezaji wanane uwanjani katika […]

The post TFF yajivua lawama kwa Kitayosce first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Almasi Kasongo (pichani) amesema bodi hiyo pamoja na TFF, hawahusiki katika sakata la timu ya Kitayosce kushindwa kutumia wachezaji wake wapya iliyowasajili kwenye dirisha kubwa msimu huu bali ni uzembe wa viongozi wa timu hiyo.
Jana timu hiyo ilijikuta ikicheza pungufu ikiwa na wachezaji wanane uwanjani katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Azam FC na kufungwa mabao 4-0.
Mchezo huo hata hivyo ulivunjika baada ya wachezaji wawili wa timu hiyo akiwemo kipa kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Kasongo alisema awali timu hiyo ilifungiwa kufanya usajili na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), baada ya kupitisha siku 45 bila kumlipa mchezaji ambaye alikwenda kuwashitaki wakati wakiwa wanashiriki Ligi ya Champioship msimu uliopita.
Alisema taarifa za Kitayosce kufungiwa walipewa na Fifa siku moja kabla ya timu hiyo kupambana na Azam na walichofanya wao waliifahamisha timu hiyo na kitu kizuri viongozi wa timu hiyo walipambana na kumlipa mchezaji huyo na Fifa ikawaondolea kifungo hicho.
“Adhabu ya Fifa haihusiani na hiki ambacho viongozi wa Kitayosce wamekifanya, viongozi hao wameshindwa kuwalipia vibali vya kufanya kazi nchini wachezaji 12 wa kigeni lakini Bodi ya Ligi wala TFF hawahusiki katika hili, wazembe ni viongozi sababu sisi kama bodi tangu asubuhi ya siku ya mchezo tulikuwa tunawauliza na majibu yao yalikuwa tumekamilisha kila kitu,” alisema Kasongo.
Kauli ya Kasongo imeungwa mkono na aliyekuwa Mbunge wa Tabora Mjini na Katibu Mkuu wa FAT (sasa TFF), Ismail Aden Rage ambaye alisema viongozi wa timu hiyo wanahusika kwa kiasi kikubwa kwa uzembe walioufanya wa kushindwa kuwatafutia vibali wachezaji wao wa kigeni.
Rage alisema wamemkera sababu siku mbili nyuma kabla ya mchezo dhidi ya Azam alikuwa akiwapigia simu kuwauliza kama wana tatizo lolote lakini walijibu wako sawa.
Alisema kwamba juzi asubuhi viongozi hao walimpigia simu wakamwomba afike uwanjani kushuhudia mchezo wao lakini ameambulia fedheha kwa timu ya nyumbani kwao Tabora kucheza pungufu kwa uzembe wa viongozi.
“Sheria walizochukua waamuzi ni stahiki kabisa sababu huwezi kuendelea na mchezo ukiwa na wachezaji sita, kifupi wamenikera hawa viongozi wa hii timu sijawahi kwenda Uwanja wa Azam, ilikuwa ni mara yangu ya kwanza lakini wameniaibisha,” alisema Rage.

The post TFF yajivua lawama kwa Kitayosce first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/17/tff-yajivua-lawama-kwa-kitayosce/feed/ 0
Majanga ya Kitayosce mwanzo mwisho https://www.greensports.co.tz/2023/08/17/majanga-ya-kitayosce-mwanzo-mwisho/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/17/majanga-ya-kitayosce-mwanzo-mwisho/#respond Thu, 17 Aug 2023 19:24:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7430 Na mwandishi wetuTimu ya Kitayosce ya Tabora ni kama vile imekuwa na misukosuko mikubwa tangu imalize kampeni za kupanda Ligi Kuu NBC msimu huu, kitendo kilichopelekea matokeo mabovu na aibu katika mchezo wao wa kwanza wa ligi hiyo.Julai, mwaka huu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilitangaza timu hiyo kufungiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa […]

The post Majanga ya Kitayosce mwanzo mwisho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Kitayosce ya Tabora ni kama vile imekuwa na misukosuko mikubwa tangu imalize kampeni za kupanda Ligi Kuu NBC msimu huu, kitendo kilichopelekea matokeo mabovu na aibu katika mchezo wao wa kwanza wa ligi hiyo.
Julai, mwaka huu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilitangaza timu hiyo kufungiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kwa kilichoelezwa kutomlipa stahiki zake kocha Ahmed Soliman raia wa Misri.
Baadae ilimalizana na kocha huyo na kuachiwa huru, lakini siku mbili kabla ya mechi yao ya kwanza ya ligi dhidi ya Azam FC, TFF ikaikumbusha timu hiyo kuwasilisha majina ya usajili wa wachezaji wao katika mtandao wa Fifa.
Kama hiyo haitoshi, jana siku ya mchezo wenyewe Kitayosce ambayo imeeleza kubadili jina lake na kuitwa Tabora United, ilifungiwa kwa mara nyingine kufanya usajili kutokana na madai ya kumvunjia mkataba mchezaji wa Ghana, Rahim Osumanu na kutomlipa stahiki zake.
Lakini baadae TFF kwa mara nyingine ikaeleza kuwa Kitayosce imelimaliza suala hilo lakini ikawa na changamoto ya kutokamilisha taratibu za kuwatumia wachezaji wake katika ligi kuu na hivyo kuanza na wachezaji wanane pekee katika mechi yao hiyo iliyopigwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Benchi lao la ufundi lilikuwa na kocha msaidizi, Bernard Fabian pekee, hiyo ni kutokana na makocha wa timu hiyo akiwemo kocha mkuu kutoka Serbia, Goran Kopunovic kukosa vigezo vya kuwepo katika benchi hilo.
Katika mechi hiyo, mpaka dakika ya 13 tayari Kitayose ilishafungwa mabao manne kabla ya wachezaji wake wawili kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo na hivyo mechi hiyo kumalizwa kwa mujibu wa kanuni.
Inaruhusiwa timu kuanza mechi ikiwa na wachezaji wasiopungua saba, hivyo kutoendelea kwa wachezaji hao kulifanya wabaki sita uwanjani na hivyo mwamuzi kumaliza mechi hiyo dakika ya 15.

The post Majanga ya Kitayosce mwanzo mwisho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/17/majanga-ya-kitayosce-mwanzo-mwisho/feed/ 0
Kitayosce sasa ruksa kusajili https://www.greensports.co.tz/2023/07/14/kitayosce-sasa-ruksa-kusajili/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/14/kitayosce-sasa-ruksa-kusajili/#respond Fri, 14 Jul 2023 15:16:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6971 Na mwandishi wetuKlabu ya Kitayosce inayoshiriki Ligi Kuu NBC imeruhusiwa kuendelea na usajili wa wachezaji kama kawaida baada ya adhabu yao ya kutosajili kuondolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).Tamko hilo limetolewa leo Ijumaa ikiwa ni siku mbili pekee zimepita tangu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litangaze kufungiwa kwa timu hiyo pamoja na Fountain […]

The post Kitayosce sasa ruksa kusajili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya Kitayosce inayoshiriki Ligi Kuu NBC imeruhusiwa kuendelea na usajili wa wachezaji kama kawaida baada ya adhabu yao ya kutosajili kuondolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Tamko hilo limetolewa leo Ijumaa ikiwa ni siku mbili pekee zimepita tangu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litangaze kufungiwa kwa timu hiyo pamoja na Fountain Gate inayocheza Ligi ya Championship baada ya kocha Ahmed El Faramawy Soliman kushinda kesi za madai dhidi ya klabu hizo alizowahi kuzinoa kwa nyakati tofauti.
Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo ameeleza kwamba kilichotokea ni kwamba Kitayosce imelipa fedha zote ilizokuwa ikidaiwa na kocha huyo raia wa Misri kwa klabu hiyo kumvunjia mkataba kinyume na taratibu.
“Ni uamuzi uliotolewa na Fifa baada ya Kitayosce kulipa madai yao yote kwa kocha Ahmed Soliman. Kwa hatua hiyo sasa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania nalo limeiondolea adhabu Kitayosce ya kutofanya usajili wa ndani,” alisema Ndimbo.

The post Kitayosce sasa ruksa kusajili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/14/kitayosce-sasa-ruksa-kusajili/feed/ 0
Kitayosce sasa ni Tabora United https://www.greensports.co.tz/2023/05/16/kitayosce-sasa-ni-tabora-united/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/16/kitayosce-sasa-ni-tabora-united/#respond Tue, 16 May 2023 18:20:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6177 Na mwandishi wetuBaada ya kupanda Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza, timu ya Kitayosce imebadilishwa jina rasmi na kuwa Tabora United.Tabora United inayotumia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora imefanikiwa kupanda Ligi Kuu NBC ikiungana na mabingwa JKT Tanzania ambao wamerejea kwa mara nyingine.Katibu Mkuu wa timu hiyo, Adam Simba alisema kuwa baada […]

The post Kitayosce sasa ni Tabora United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Baada ya kupanda Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza, timu ya Kitayosce imebadilishwa jina rasmi na kuwa Tabora United.
Tabora United inayotumia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora imefanikiwa kupanda Ligi Kuu NBC ikiungana na mabingwa JKT Tanzania ambao wamerejea kwa mara nyingine.
Katibu Mkuu wa timu hiyo, Adam Simba alisema kuwa baada ya kupanda daraja sasa timu hiyo imebadilishwa jina na kuwa Tabora United na jina la Kitayosce limekufa rasmi.
“Kwa hiyo shughuli yetu kubwa na mikakati yetu endapo tutasajili vizuri na morali tuliyonayo hatuendi kushiriki ligi kuu msimu ujao bali tunaenda kupambana na kuonyesha upinzani mkubwa,” alisema Simba.

“Tunataka kusuka kikosi bora ambacho kitakuwa na mchanganyiko wa wachezaji wenye uzoefu na vijana, lengo letu ni kuurejesha mkoa wa Tabora kwenye ramani ya soka kama ilivyokuwa miaka ya nyuma,” alisema Simba.


Ni kama vile Tabora United imefuata nyayo za DTB ambayo baada ya kupanda daraja msimu wa 2021-22 ilibadili jina na kuitwa Singida Big Stars.

The post Kitayosce sasa ni Tabora United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/16/kitayosce-sasa-ni-tabora-united/feed/ 0