Judo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 28 Dec 2023 14:15:28 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Judo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Judo waanza maandalizi All Africa Games https://www.greensports.co.tz/2023/12/28/judo-waanza-maandalizi-all-africa-games/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/28/judo-waanza-maandalizi-all-africa-games/#respond Thu, 28 Dec 2023 14:15:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9045 Na mwandishi wetuWachezaji 13 wa mchezo wa Judo wameanza kambi Ukonga, Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Afrika ya All African Game itakayofanyika nchini Ghana, mwakani.Katibu Mkuu wa Judo, Innocent Mallya amesema leo Alhamisi kuwa wameona waanze kujiimarisha katika kambi ya kwenda na kurudi huku wakisubiri kambi rasmi yenye maelekezo ya […]

The post Judo waanza maandalizi All Africa Games first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Wachezaji 13 wa mchezo wa Judo wameanza kambi Ukonga, Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Afrika ya All African Game itakayofanyika nchini Ghana, mwakani.
Katibu Mkuu wa Judo, Innocent Mallya amesema leo Alhamisi kuwa wameona waanze kujiimarisha katika kambi ya kwenda na kurudi huku wakisubiri kambi rasmi yenye maelekezo ya Serikali siku za usoni.
Alisema msimu huu wamedhamiria kurudi na medali ndio maana wameanza mapema maandalizi ya kujiimarisha.
“Hatutaki kwenda kushiriki bali kushindana na kurudi na medali, timu yetu imeshaanza mazoezi katika kambi iliyoko Ukonga Magereza, naamini mambo yatakwenda vizuri,” alisema Mallya.
Mallya alisema wachezaji walioingia kambini kwa sasa ni wale wenye uzoefu katika mashindano ya kimataifa na wengine wamechaguliwa kutokana na mashindano mbalimbali ya kitaifa.
Katibu huyo aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuisapoti timu hiyo ili iweze kukaa katika mazingira mazuri ya kambi na kujiandaa kwa utulivu.

The post Judo waanza maandalizi All Africa Games first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/28/judo-waanza-maandalizi-all-africa-games/feed/ 0
Dk Chana kufungua mashindano ya judo https://www.greensports.co.tz/2023/04/28/dk-chana-kufungua-mashindano-ya-judo/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/28/dk-chana-kufungua-mashindano-ya-judo/#respond Fri, 28 Apr 2023 18:43:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5964 Na mwandishi wetuWaziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Pindi Chana anatarajiwa kufungua mashindano ya Judo Afrika Mashariki yatakayoanza kesho Jumamosi kwenye viwanja vya Don Bosco, Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa Chama cha Judo Tanzania (JATA) Innocent Mallya amesema kwamba tayari timu za Uganda, Zanzibar, Rwanda na Burundi zimeshawasili nchini ambapo zitaungana na wenyeji Tanzania […]

The post Dk Chana kufungua mashindano ya judo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Pindi Chana anatarajiwa kufungua mashindano ya Judo Afrika Mashariki yatakayoanza kesho Jumamosi kwenye viwanja vya Don Bosco, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Judo Tanzania (JATA) Innocent Mallya amesema kwamba tayari timu za Uganda, Zanzibar, Rwanda na Burundi zimeshawasili nchini ambapo zitaungana na wenyeji Tanzania kufikisha jumla ya timu tano.
Kwa mujibu wa Mallya, maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika na kuwataka mashabiki na watu wote wanaopenda mchezo huo kujitokeza kushuhudia bure kwa lengo la kujifunza.
“Mambo yameshaiva, mashindano yanaanza kesho, tunawahimiza watoto, wakubwa na wadau wa michezo kwa ujumla waje washuhudie burudani, hakuna kiingilio ni sehemu ya kujifunza,”alisema.
Mallya alisema itapendeza kama mashabiki watajitokeza waione timu yao ya Taifa ikipigania ushindi ambao mara ya mwisho waliupata mwaka 2018.
Bingwa mtetezi wa mashindano hayo ni Kenya aliyeshinda mwaka jana kwenye michuano iliyofanyika Uganda wakati Tanzania ikishika nafasi ya pili na Burundi ya tatu.
Akifafanua kuhusu mashindano hayo Mallya alisema yatasaidia katika maandalizi ya timu ya Taifa kwa ajili kushriki mashindano mbalimbali ya Afrika na Dunia pamoja na kufuzu Michezo ya Olimpiki.

The post Dk Chana kufungua mashindano ya judo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/28/dk-chana-kufungua-mashindano-ya-judo/feed/ 0