Hispania - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 09 Aug 2026 19:15:33 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Hispania - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Hispania bingwa Kombe la Dunia 2026 https://www.greensports.co.tz/2026/07/20/hispania-bingwa-kombe-la-dunia-2026/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/20/hispania-bingwa-kombe-la-dunia-2026/#respond Sun, 19 Jul 2026 23:05:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14816 New York, MarekaniFerran Torres ameibuka shujaa baada ya kufunga bao pekee na kuiwezesha Hispania kutoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Argentina na kutwaa Kombe la Dunia 2026.Iliwachukua Hispania dakika 106 kupata bao hilo licha ya kuutawala mchezo na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Argentina lakini mashambulizi hayo hayakuweza kuzaa bao kwa dakika 90 […]

The post Hispania bingwa Kombe la Dunia 2026 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Ferran Torres ameibuka shujaa baada ya kufunga bao pekee na kuiwezesha Hispania kutoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Argentina na kutwaa Kombe la Dunia 2026.
Iliwachukua Hispania dakika 106 kupata bao hilo licha ya kuutawala mchezo na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Argentina lakini mashambulizi hayo hayakuweza kuzaa bao kwa dakika 90 za kawaida.
Kikwazo kikubwa kwa Hispania alikuwa kipa wa Argentina, Emilio Martinez ambaye aliokoa michomo kadhaa ya Hispania hadi kumaliza dakika 90 timu hizo zikiwa hazijafungana ndipo zilipoongezwa dakika 30.
Katika dakika 30 za nyongeza Hispania waliendelea kulisakama lango la Argentina huku Argentina wakitumia muda mwingi kujihami kabla hawajaadhibiwa dakika ya 106 na Torres aliyefunga bao kwa shuti kali la mguu wa kushoto.
Bao hilo lilianzia kwa mpira mrefu uliopigwa na Lamine Yamal na kumkuta Nico William ambaye alimuunganishia Torres pasi ya kichwa na Torres kufumua shuti lililomshinda Martinez.
Baada ya kuingia bao hilo, Argentina waliokuwa wamezidiwa kila idara, waliamka na kuanza mashambulizi wakiongozwa na Lionel Messi na kuibua hali ya hofu kwa Hispania.
Messi ambaye alishindwa kuonesha umahiri wake kwa kipindi kirefu, bao la Hispania ni kama lilimpa nguvu ya kuongoza mashambulizi yaliyozaa kona mbili za haraka kwenye lango la Hispania.
Ukiachana na mashambulizi hayo yaliyopamba moto baada ya Argentina kufungwa, kwa dakika zote 120, timu hiyo ilifanikiwa kupiga mashuti mawili tu ya maana langoni mwa Hispania.
Dalili za Hispania kutoka na ushindi zilianza kuonekana mapema kwa namna walivyotawala mchezo na kulisakama lango la Argentina waliokuwa na kazi ya kujihami huku wakishindwa kutengeneza mashambulizi ya maana.
Kasi ya mashambulizi ya Hispania kwenye lango la Argentina ilianza kuonekana mapema dakika za 4 na 5, Lamine Yamal alionesha umahiri lakini mashuti yake mawili yaliishia mikononi mwa kipa Martinez.
Hispania kwa mara nyingine dakika ya 38 ilifanya shambulizi langoni mwa Argentina lakini shuti la chinichini la mguu wa kushoto lililopigwa na Mikel Oyarzabal lilidakwa na kipa Martinez.
Hispania pia mara kadhaa ilifanya mashambulizi yaliyotokea upande wa kushoto kwa beki Cucurella lakini krosi za beki huyo ziliokolewa au kutoka nje ya lango.
MAmbo yalizidi kuwaharibikia Argentina baada ya nyota wao Enzo Fernandes kulimwa kadi ya pili ya njano kwa kucheza rafu na hivyo kutoka uwanjani akiwaacha wenzake 10 kupambana katika dakika 30 za nyongeza.
Hispania ambao mara ya mwisho walilibeba Kombe la Dunia mwaka 2010 katika fainali zilizofanyika nchini Afrika Kusini, pia ndio mabingwa wa Kombe la Ulaya 2024 au Euro 2024.
Fainali za Kombe la Dunia zilianza kutimua vumbi Juni 11, 2026 katika nchi za Canada, Mexico na kuhitimishwa Jumapili, Julai 19, 2026 nchini Marekani kwa mechi iliyopigwa mjini New York kwenye Uwanja wa New Jersey.

The post Hispania bingwa Kombe la Dunia 2026 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/20/hispania-bingwa-kombe-la-dunia-2026/feed/ 0
Brazil, Hispania hakuna mbabe https://www.greensports.co.tz/2024/03/27/brazil-hispania-hakuna-mbabe/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/27/brazil-hispania-hakuna-mbabe/#respond Wed, 27 Mar 2024 06:13:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10382 Madrid, HispaniaBao la penalti la dakika za lala salama la Lucas Paqueta limetosha kuifanya Brazil itoke sare ya mabao 3-3 na Hispania katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyopigwa kwenye dimba la Santiago Berbabeu.Katika mechi hiyo ya Fifa iliyochezwa jana Jumanne, Hispania ndio walioanza kupata bao dakika ya 12 lililofungwa na Rodri kwa mkwaju wa […]

The post Brazil, Hispania hakuna mbabe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Bao la penalti la dakika za lala salama la Lucas Paqueta limetosha kuifanya Brazil itoke sare ya mabao 3-3 na Hispania katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyopigwa kwenye dimba la Santiago Berbabeu.
Katika mechi hiyo ya Fifa iliyochezwa jana Jumanne, Hispania ndio walioanza kupata bao dakika ya 12 lililofungwa na Rodri kwa mkwaju wa penalti kabla Dani Olmo hajaongeza la pili dakika ya 36.
Dakika tano kabla ya mapumziko, Brazil waliandika bao lao la kwanza lililofungwa na Rodrygo na Moreira de Sousa kusawazisha dakika tano baada ya mapumziko na kufanya timu hizo ziwe sare ya mabao 2-2.
Rodri kwa mara nyingine aliifungia Hispania bao la tatu kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 86 na kufanya matokeo yawe 3-2 na hatimaye mkwaju wa penalti wa Paqueta ukatosha kuipa Brazil bao la tatu katika dakika sita za nyongeza na kufanya ubao usomeke 3-3.
England, Ubelgiji zatoka sare
Katika mechi nyingine ya kirafiki, bao la Jude Bellingham liliiwezesha England kutoka sare ya mabao 2-2 na Ubelgiji katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Wembley.
Walikuwa ni Ubelgiji walioanza kupata bao dakika ya 11 lililofungwa na Youri Tielemans lakini Ivan Toney akiichezea England kwa mara ya kwanza akasawazisha kwa mkwaju wa penalti dakika ya 17.
Ubelgiji waliendelea kupambana na kuandika bao la pili dakika ya 36 mfungaji kwa mara nyingine akiwa ni Tielemans hali iliyoiweka England katika wakati mgumu kabla Bellingham hajasawazisha katika dakika tano za nyongeza.
Matokeo ya mechi za kimataifa za kirafiki
England 2-2 Ubelgiji
Ujerumani 2-1 Uholanzi
Jamhuri ya Ireland 0-1 Uswisi
Scotland 0-1 Ireland Kask
Slovenia 2-0 Ureno
Ufaransa 3-2 Chile
Hispania 3-3 Brazil
Zambia 2-1 Malawi
Cayman Islands 0-4 Moldova
Kenya 3-1 Zimbabwe
Uganda 2-2 Ghana
Finland 2-1 Estonia

The post Brazil, Hispania hakuna mbabe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/27/brazil-hispania-hakuna-mbabe/feed/ 0
Busu lililozua taharuki https://www.greensports.co.tz/2023/09/24/busu-lililozua-taharuki/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/24/busu-lililozua-taharuki/#respond Sun, 24 Sep 2023 11:53:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7843 Na Hassan KinguUshindi wa timu ya wanawake ya Hispania kwenye Kombe la Dunia umeibua mjadala wa nje ya soka baada ya mshambuliaji wa timu hiyo, Jenni Hermoso kupigwa busu mdomoni na aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania, Luis Rubiales.Dunia ya soka ilipumzishwa kufurahia na kujadili ubingwa wa timu ya wanawake ya Hispania, ubingwa uliopatikana […]

The post Busu lililozua taharuki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Hassan Kingu
Ushindi wa timu ya wanawake ya Hispania kwenye Kombe la Dunia umeibua mjadala wa nje ya soka baada ya mshambuliaji wa timu hiyo, Jenni Hermoso kupigwa busu mdomoni na aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania, Luis Rubiales.
Dunia ya soka ilipumzishwa kufurahia na kujadili ubingwa wa timu ya wanawake ya Hispania, ubingwa uliopatikana Agosti 20, badala yake mjadala mkali uliozua taharuki ukawa ni kuhusu Luis kumpiga busu Jenni.
Ni kama ilivyokuwa mwaka 2006, timu ya wanaume ya Italia ilipobeba Kombe la Dunia, mjadala wa ushindi ulipoozeshwa na tukio la beki wa Italia, Marco Materrazi kupigwa kichwa na kiungo wa Ufaransa, Zinedine Zidane.
Tofauti ya mijadala hiyo ni kwamba Zidane au Zizou alijutia alichokifanya lakini Luis hakujutia, licha ya kusakamwa na kutakiwa ajiuzulu badala yake alisema kwamba furaha iliyopitiliza ndiyo iliyomfanya ampige Jenni busu la mdomoni.
Busu hilo likazua taharuki na kuibua shinikizo kila kona la kumtaka Luis ajiuzulu kwa kumpiga busu mwanamke ambaye huenda wapo wanaume wengine wengi waliotamani kufanya hivyo lakini hawajawahi kuipata nafasi ambayo Luis aliipata na Luis mwenyewe amegoma kujiuzulu huku hoja yake ikisimamia katika makubaliano baina yake na Jenni kwamba hakumpiga busu Jenni kwa lazima, walikubaliana.
Mjadala ukashika kasi, mashinikizo ya kumtaka Luis ajiuzulu yakaongezeka siku hadi siku, kuanzia kwa Waziri Mkuu wa Hispania, mawaziri, wanasoka wanawake na makundi mbalimbali ya wanaharakati.
Yote hayo hayakumshtua Luis, aliendelea kushikilia msimamo wa kutokuwa tayari kujiuzulu kabla ya Fifa kuingilia kati na kumsimamisha kujihusisha na masuala ya soka kwa siku 90.


Ikafuatua ofisi ya mwendesha mashtaka kutangaza kusudio la kumshitaki wakati huo huo, Jenni naye alishatangaza nia yake ya kufanya hivyo kwa alichokidai kwamba hakupenda alichofanyiwa na Luis.
Baada ya mashinikizo kuongezeka nje ya Hispania wakiwamo wachezaji wanawake kugoma kuichezea timu ya taifa kama Luis angeendelea kuwa madarakani, hatimaye Luis akakubali yaishe, akatangaza kujiuzulu.
Kujiuzulu kwa Luis hakujazuia mjadala kuendelea, bado watu wanahoji je ni kweli Luis alifanya kosa au tatizo limekuzwa bila sababu?
Watetezi wa Luis
Wanaomtetea Luis wanadai kwamba alichokifanya kilikuwa na ridhaa ya Jenni na wanatumia moja ya picha za tukio hilo kutetea hoja yao, picha inayotajwa ni ile inayoonesha mkono wa kulia wa Jenni ukimshika Luis kiunoni.
Katika picha hiyo kinachoonekana kimetafsiriwa kuwa ni Jenni kumpa ushirikiano Luis, kwa maana nyingine hakuwa na tatizo kwa alichofanyiwa na Luis.


Watetezi hao pia wanaona kama Jenni ameangukia katika shinikizo la watu ambao hawakupenda kile kilichofanywa na Luis na kwamba awali hakuliona jambo hilo kuwa ni lenye ubaya.
Hapa inajengwa hoja kwamba Luis alifurahia baada ya Hispania kubeba kombe la dunia, akafurahishwa na soka la Jenni, akaona kumkumbatia haitoshi bali busu lingeonesha alivyokuwa na furaha, na Jenni picha zinamuonesha akimpa Luis ushirikiano.
Zaidi ya yote hayo hakuna picha ya Jenni iliyomuonesha akiwa amekunja uso baada ya kupigwa busu la mdomoni hivyo hakuwa na tatizo na jambo hilo.
Mama wa Luis amekuwa mstari wa mbele kumtetea mwanaye ikiwamo kufanya mgomo wa kula na hoja yake ni moja tu kwamba mwanaye hakuwa na kosa kwani tukio zima lilifanyika kwa makubaliano baina ya Luis na Jenni.
Wanaompinga Luis
Wanaompinga Luis wanakataa kuwapo makubaliano baina yake na Jenni badala yake wanaliona tukio zima kama ni unyanyasaji na udhalilishaji mwanamke lililofanywa na kiongozi wa soka na suluhisho lake ni kumuondoa kiongozi huyo madarakani.
Hoja nyingine ya kundi hili pia inahusisha picha ile inayomuonesha Jenni akiwa ameiondoa mikono yake kwenye kiuno cha Luis, ni kama vile kwanza kukubali kukumbatiwa lakini hapo hapo kulikataa busu la mdomoni.
Kundi hili linamuweka Luis katika kundi la wanaume wanaodhalilisha wanawake na kuwakosea heshima kwa kutumia nafasi zao, ni kundi ambalo pia limekuwa likishinikiza mabadiliko ya kiungozi katika idara mbalimbali za Shirikisho la Soka Hispania.


Luis pamoja na kukubali kujiuzulu uongozi katika Shirikisho la Soka Hispania, bado ana kesi ya kujibu baada ya kushitakiwa na vyombo vya kisheria nchini Hispania.
Tumejifunza nini?
Tukio zima hili linatufundisha kuwa kuna mambo ambayo mtu hufanyiwa kwa ridhaa yake, tofauti na hivyo ni kesi kubwa. Tumefundishwa kuheshimu mipaka kati ya mwanamke na mwanaume.
Awali wengi wetu hatukutarajia kuona dunia ya soka ikijadili busu ambalo kiongozi wa soka ameamua kumpiga mchezaji wake tena baada ya kuvutiwa na soka la mchezaji huyo kwenye timu ambayo imebeba taji la dunia.

The post Busu lililozua taharuki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/24/busu-lililozua-taharuki/feed/ 0
Mama wa aliyembusu mchezaji alazwa hospitali https://www.greensports.co.tz/2023/08/31/mama-wa-aliyembusu-mchezaji-alazwa-hospitali/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/31/mama-wa-aliyembusu-mchezaji-alazwa-hospitali/#respond Thu, 31 Aug 2023 07:37:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7612 Madrid, HispaniaAngeles Bejar ambaye ni mama wa rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF) aliyesimamishwa, Luis Rubiales amekimbizwa hospitali akiwa hoi baada ya kuwa katika mgomo wa kula akishinikiza mwanaye asibughudhiwe.Mama huyo alichukua uamuzi wa kugoma kula tangu Jumatatu na kujihifadhi kanisani akifanya maombi kwa alichodai kuwa mwanaye amekuwa akisakamwa kwa madai ya kumbusu mdomoni […]

The post Mama wa aliyembusu mchezaji alazwa hospitali first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Angeles Bejar ambaye ni mama wa rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF) aliyesimamishwa, Luis Rubiales amekimbizwa hospitali akiwa hoi baada ya kuwa katika mgomo wa kula akishinikiza mwanaye asibughudhiwe.
Mama huyo alichukua uamuzi wa kugoma kula tangu Jumatatu na kujihifadhi kanisani akifanya maombi kwa alichodai kuwa mwanaye amekuwa akisakamwa kwa madai ya kumbusu mdomoni mshambuliaji wa timu ya Hispania, Jenni Hermoso.
Rubiales amejikuta akishutumiwa na kushinikizwa ajiuzulu kwa kumbusu mdomoni Jenni wakati wa shamrashamra za timu ya Hispania kubeba Kombe la Dunia baada ya timu hiyo kuichapa England bao 1-0 katika mechi ya fainali.
Katika tukio hilo lililotokea Agosti 20, awali Jenni (pichani chini) alidaiwa kumtetea Rubiales lakini baadaye alisema kwamba hakupenda alichofanyiwa na kiongozi huyo kwani hakuwa ameridhia kufanyiwa hivyo.

Akiwa kanisani mama Angeles aliahidi kuendelea na mgomo wa kula usiku na mchana bila ukomo lakini jana Jumatano hali yake ilikuwa mbaya na kulazimika kuwahishwa hospitali na hivyo kusimamisha mgomo wa kula kwa muda.

“Unyama na mashambulizi ambayo anafanyiwa mwanangu ni jambo ambalo hapaswi kukutana nalo,” alisema mama huyo.


“Amepelekwa hospitali na kulazimika kusimamisha mgomo wa kula, amekuwa si mwenye kujisikia vizuri kutokana na joto na matatizo mengineyo, miguu yake imelegea na amekuwa katika uchovu,” alisema mchungaji mmoja wa kanisa hilo aliyetajwa kwa jina moja la Antonio.
Jumamosi iliyopita, Rubiales alisimamishwa kwa siku 90 na Fifa wakati uchunguzi wa kadhia inayomkabili ukiendelea wakati baadhi ya viongozi wa soka Hispania wakimshinikiza ajiuzulu.
Wachezaji 81 wa timu ya wanawake wa Hispania wametangaza kutokuwa tayari kuichezea timu hiyo kama Rubiales ataendelea kuwa kiongozi wa REEF.
Rubiales awali alijitetea akisema kwamba alichokifanya kilitokana na furaha isiyo kifani na kutaka wenye mtazamo tofauti na tukio hilo wapuuzwe ingawa baadaye aliomba radhi lakini amekataa kujiuzulu akidai kwamba hakumbusu Jenni kwa kumlazimisha.

The post Mama wa aliyembusu mchezaji alazwa hospitali first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/31/mama-wa-aliyembusu-mchezaji-alazwa-hospitali/feed/ 0
Kocha wa Wanawake Hispania njia panda https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/kocha-wa-wanawake-hispania-njia-panda/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/kocha-wa-wanawake-hispania-njia-panda/#respond Wed, 30 Aug 2023 07:45:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7569 Madrid, HispaniaHatma ya kocha wa wanawake wa timu ya Hispania, Jorge Vilda (pichani juu) huenda akatimuliwa baada ya kuwapo habari kwamba Shirikisho la Soka Hispania (REEF) linaangalia uwezekano wa kuchukua uamuzi huo.Vilda aliyeiwezesha timu hiyo kutwaa Kombe la Dunia, ni mtu pekee kwenye benchi la ufundi la timu hiyo aliyebaki katika nafasi yake baada ya […]

The post Kocha wa Wanawake Hispania njia panda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Hatma ya kocha wa wanawake wa timu ya Hispania, Jorge Vilda (pichani juu) huenda akatimuliwa baada ya kuwapo habari kwamba Shirikisho la Soka Hispania (REEF) linaangalia uwezekano wa kuchukua uamuzi huo.
Vilda aliyeiwezesha timu hiyo kutwaa Kombe la Dunia, ni mtu pekee kwenye benchi la ufundi la timu hiyo aliyebaki katika nafasi yake baada ya wasaidizi wake wote kujiuzulu wakishinikiza kujiuzulu kwa Rais wa REEF, Luis Rubiales aliyembusu mshambuliaji wa timu hiyo, Jenni Hermoso.
Wachezaji 81 wa Hispania wakiwamo 23 walioiwezesha timu hiyo kubeba Kombe la Dunia wameahidi kutoichezea timu hiyo tena kama Rubiales ataendelea kuwa kwenye nafasi ya urais wa shirikisho hilo ingawa tayari Fifa imemsimamisha Rubiales kwa siku 90.
Vilda alionekana kwenye mkutano mkuu maalum wa REEF akimpongeza Rubiales kwa msimamo wake wa kutojiuzulu lakini baadaye alibadili msimamo na kuanza kukosoa alichokifanya Rubiales.
Mabosi ndani ya REEF wanaamini kwamba mwenendo mzima wa tukio hilo unatosha kuwa sababu ya kumtimua Vilda katika nafasi yake.


Jumatatu iliyopita, viongozi REEF walifanya mkutano mkuu maalum ulioongozwa na kaimu rais wa shirikisho hilo, Pedro Rocha na kujadili mpango wa kulifanyia maboresho shirikisho hilo kwa lengo la kuwa na mwanzo mpya.
Habari za ndani zinadai kwamba baadhi ya wajumbe wa mkutano huo hawataki kumshinikiza Rubiales ajiuzulu kwa lazima badala yake walitoa taarifa kama ya kumshauri achukua uamuzi huo jambo ambalo hadi sasa Rubiales hajakubaliana nalo.
Rubiales, 46, amejikuta akishutumiwa kila kona kwa kitendo chake cha kumbusu mdomoni Jenni baada ya Hispania kuichapa England bao 1-0 na kubeba Kombe la Dunia.
Baadaye Rubiales alisema kwamba alimpiga busu mchezaji huyo baada ya kuwa na furaha isiyo kifani na kutaka wenye tafsiri tofauti wapuuzwe lakini amejikuta akisakamwa sehemu mbalimbali duniani na alichofanya kutafsiriwa kuwa ni udhalilishaji wa kijinsia.

The post Kocha wa Wanawake Hispania njia panda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/kocha-wa-wanawake-hispania-njia-panda/feed/ 0
Aliyembusu mchezaji asimamishwa siku 90 https://www.greensports.co.tz/2023/08/27/aliyembusu-mchezaji-asimamishwa-siku-90/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/27/aliyembusu-mchezaji-asimamishwa-siku-90/#respond Sun, 27 Aug 2023 04:52:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7548 Geneva, UswisiShirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limemsimamisha kwa siku 90, Rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF), Luis Rubiales wakati kamati yake ya nidhamu ikimchunguza kwa kosa la kumbusu mdomoni mshambuliaji wa timu ya Taifa, Jenni Hermoso.Siku chache zilizopita Fifa ilitangaza kufanya uchunguzi wa kadhia ya Rubiales kumbusu mchezaji huyo mdomoni Jumapili iliyopita wakati […]

The post Aliyembusu mchezaji asimamishwa siku 90 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Geneva, Uswisi
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limemsimamisha kwa siku 90, Rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF), Luis Rubiales wakati kamati yake ya nidhamu ikimchunguza kwa kosa la kumbusu mdomoni mshambuliaji wa timu ya Taifa, Jenni Hermoso.
Siku chache zilizopita Fifa ilitangaza kufanya uchunguzi wa kadhia ya Rubiales kumbusu mchezaji huyo mdomoni Jumapili iliyopita wakati wachezaji wa Hispania wakikabidhiwa medali baada ya kuibwaga England bao 1-0 na kubeba Kombe la Dunia la Wanawake (WWC).
Uamuzi wa Fifa umekuja baada ya Rubiales kukataa kujiuzulu licha ya kuwapo malalamiko kumtaka afanya hivyo kutoka kwa watu mbalimbali wakiwamo viongozi wa Serikali ya Hispania na wanasoka wanawake wa klabu mbalimbali ndani na nje ya Hispania.
Kitendo cha Rubiales (pichani juu) kumbusu mchezaji huyo mdomoni wakati wa shamrashamra za ushindi ikiwamo kumshika shingoni licha ya kuibua mjadala lakini mwenyewe alijitetea akidai kilitokana na furaha iliyopitiliza.
Awali Jenni alionekana kumtetea Rubiales lakini baadaye akadai hakulipenda jambo hilo na kwamba halikufanyika kwa ridhaa yake na tayari wanasoka wanawake wameitisha mgomo wa kutoichezea timu ya Hispania kama kiongozi huyo ataendelea kuwa madarakani.
Taaifa ya Fifa iliyopatikana Jumamosi hii ilieleza kwa kifupi kuwa Rubiales ameondolewa madarakani kwa siku 90 ili kupisha uchunguzi ulioanza kufanywa Alhamisi iliyopita.
Fifa pia iliwataka viongozi wa REEF pamoja na Rubiales katika siku hizo 90nkutofanya mawasiliano yoyote na Jenni,


Baada ya uamuzi wa Fifa, REEF imempitisha makamu rais wake, Pedro Rocha kukaimu nafasi hiyo na kufafanua kwamba Rubiales ana imani na uchunguzi wa Fifa ambao pia utampa nafasi ya kujitetea kwa kosa analodaiwa kulifanya.
Adhabu hiyo pia unamuondoa kwa muda Rubiales katika nafasi yake ya makamu rais wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) na hatotakiwa kujihusisha na masuala ya soka kwa kipindi chote cha siku 90.
Rubiales mwenye umri wa miaka 46, iwapo atakutwa na hatia katika kadhia hiyo, anaweza kukutana na adhabu ya kuondolewa kabisa madarakani, kuonywa au kutozwa faini, kimoja kati ya hivyo au vyote kwa pamoja.
Wakati huo huo makocha wasaidizi na maofisa wa benchi la ufundi la timu ya wanawake ya Hispania iliyobeba Kombe la Dunia wote wamejiuzulu nafasi zao isipokuwa kocha mkuu Jorge Vilda, makocha hao wote wanapinga Rubiales kuongoza REEF,
Waliojiuzulu ni makocha wasaidizi, Montse Tome, Javier Lerga na Eugenio Gonzalo Martin, mwingine ni kocha wa viungo Blanca Romero Moraleda na kocha wa makipa Carlos Sanchez. Pia wamo makocha wengine sita waliokuwa na timu hiyo katika ngazi mbalimbali kuanzia timu za vijana, nao wamejiuzulu.

The post Aliyembusu mchezaji asimamishwa siku 90 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/27/aliyembusu-mchezaji-asimamishwa-siku-90/feed/ 0
Wachezaji timu ya taifa Hispania wagoma https://www.greensports.co.tz/2023/08/26/wachezaji-timu-ya-taifa-hispania-wagoma/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/26/wachezaji-timu-ya-taifa-hispania-wagoma/#respond Sat, 26 Aug 2023 17:08:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7538 Madrid, HispaniaBaada ya Rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF), Luis Rubiales kukataa kujiuzulu kwa kosa la kumpiga busu mdomoni mshambuliaji wa timu ya taifa ya wanawake, Jenni Hermoso, wachezaji 81 wanawake wa Hispania wametangaza kugoma kuichezea timu ya taifa.Katika taarifa yake hata hivyo REEF imeonya ikidai kwamba mchezaji yeyote anayechaguliwa kuiwakilisha timu ya taifa […]

The post Wachezaji timu ya taifa Hispania wagoma first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Baada ya Rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF), Luis Rubiales kukataa kujiuzulu kwa kosa la kumpiga busu mdomoni mshambuliaji wa timu ya taifa ya wanawake, Jenni Hermoso, wachezaji 81 wanawake wa Hispania wametangaza kugoma kuichezea timu ya taifa.
Katika taarifa yake hata hivyo REEF imeonya ikidai kwamba mchezaji yeyote anayechaguliwa kuiwakilisha timu ya taifa ana wajibu wa kufanya hivyo.
Mbali na Hispania, sakata la Rubiales limeanza kusambaa katika nchi nyingine likihusisha zaidi wanawake ambapo Jumamosi nchini Marekani katika mechi ya ligi ya wanawake kati ya Orlando Pride and San Diego Wave kulikuwa na matukio ya kumtetea Jenni na kadhia iliyomkuta.
Katika mechi hiyo wachezaji walivaa beji maalum za kumuunga mkono Jenni, beji hizo zilikuwa na maandishi yaliyosomeka ‘Contigo Jenni’ yaani tuko pamoja nawe Jenni.
Mmoja wa wachezaji wa Marekani aliye mstari wa mbele ni mshambuliaji Alex Morgan ambaye kabla ya hapo alinukuliwa akisema, “Nimeshtushwa na msimamo wa watu kwa alichokifanya Luis Rubiales, niko pamoja na Jenni Hermoso na wachezaji wa Hispania.
“Kushinda Kombe la Dunia inatakiwa liwe tukio bora na la kipekee katika maisha ya wachezaji hawa badala yake linafunikwa na udhalilishaji, uhuni na kushindwa kwa shirikisho la soka Hispania.
England nako timu ya wanawake ambayo ilipoteza katika mechi ya fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake (WWC) dhidi ya Hispania kwa kufungwa bao 1-0, taarifa yao imesema kwamba alichofanya Rubiales hakikubaliki.
“Tabia za watu wanaodhani kwamba wao ni imara na hawaadhibiwi, watu hawa wasivumiliwe, watu wasichukulie namna nyingine mambo wanayoyafanya ya aina yoyote ya udhalilishaji. Jenni Hermosso tunasimama pamoja nawe,” ilieleza taarifa ya timu ya wanawake ya England.
Jumapili iliyopita, Rubiales alimpiga busu la mdomoni, Jenni mara baada ya Hispania kuichapa England bao 1-0 katika mechi ya fainali dhidi ya England, kitendo hicho ambacho alikifanya wakati wachezaji wakipewa medali, kimetafsiriwa kuwa ni udhalilishaji kwa wanawake kwani mchezaji huyo hakufanyiwa jambo hilo kwa ridhaa yake.

The post Wachezaji timu ya taifa Hispania wagoma first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/26/wachezaji-timu-ya-taifa-hispania-wagoma/feed/ 0
Waziri Mkuu aingilia kati mchezaji kupigwa busu https://www.greensports.co.tz/2023/08/23/__trashed/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/23/__trashed/#respond Wed, 23 Aug 2023 05:53:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7482 Madrid, HispaniaWaziri Mkuu wa Hispania, Pedro Sanchez amekerwa na kitendo cha kiongozi wa Shirkisho la Soka Hispania (RFEF), Luis Rubiales kumpiga busu mdomoni mchezaji wa timu hiyo, Jernni Hermoso akisema kwamba msamaha alioomba kiongozi huyo hautoshi.Mara baada ya Hispania kuifunga England bao 1-0 na kubeba Kombe la Dunia la Wanawake (WWC) Jumapili iliyopita, Rubialles alimpiga […]

The post Waziri Mkuu aingilia kati mchezaji kupigwa busu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Waziri Mkuu wa Hispania, Pedro Sanchez amekerwa na kitendo cha kiongozi wa Shirkisho la Soka Hispania (RFEF), Luis Rubiales kumpiga busu mdomoni mchezaji wa timu hiyo, Jernni Hermoso akisema kwamba msamaha alioomba kiongozi huyo hautoshi.
Mara baada ya Hispania kuifunga England bao 1-0 na kubeba Kombe la Dunia la Wanawake (WWC) Jumapili iliyopita, Rubialles alimpiga Jenni busu mdomoni lakini baada ya kushutumiwa kila kona, juzi aliibuka na kuomba msamaha akidai alikosea.
Awali Rubiales aliwashangaa waliokuwa wakimshutumu akisema kuwa alichokifanya kilitokana na furaha aliyokuwa nayo na kwamba tukio hilo lilikuwa la marafiki wawili akitaka waliolipa tafsiri nyingine wapuuzwe.
“Tulichokiona ni kitu kisichokubalika, hatua ya Rubiales kuomba msamaha haitoshi na nafikiri ni kitu ambacho hakikubaliki, anatakiwa kuchukua hatua zaidi ili kuweka wazi kitu ambacho sote tulikiona,” alisema Waziri Mkuu Sanchez.
“Wachezaji walifanya kila walichoweza ili kupata ushindi lakini tabia aliyoionesha Rubiales imetoa picha ya wazi kwamba bado kuna kazi ya kufanya katika kuekelea kwenye usawa,” alisema Waziri Sanchez.


Naye Waziri Mkuu wa Pili wa Hispania, Yolanda Diaz, yeye alimtaka Rubiales ajiuzulu katika nafasi yake kwenye kuongoza RFEF.

“Msamaha anaoomba hauna maana, kikosi cha Hispania kimetuonesha mambo mengi kuhusu usawa, si katika michezo na soka tu, wametuonesha kwamba bado kuna kazi kubwa ya kufanya katika nchi yetu ili wanawake na wanaume wawe sawa,” alisema Waziri Diaz.


Awali kupitia mtandao wa Instagram, Jenni alisema hakupenda alichofanyiwa na Rubiales baada ya mechi yao ya fainali lakini taarifa iliyotolewa baadaye ilimnukuu mchezaji huo akimtetea Rubiales.
Mbali na mawaziri hao wawili, Rubiales pia ameshutumiwa na mawaziri wengine pamoja na watu mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii huku wengine wakimtaka ajiuzulu.
Katika kauli yake ya kuomba msamaha, Rubiales alisema, “Nalazimika kuomba msamaha na kujifunza kupitia jambo hili na kuelewa kwamba unapokuwa rais ni lazima kuwa makini.”

The post Waziri Mkuu aingilia kati mchezaji kupigwa busu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/23/__trashed/feed/ 0
Mfungaji bao la Hispania afiwa na baba https://www.greensports.co.tz/2023/08/22/baba-wa-mfungaji-bao-la-hispania-afariki/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/22/baba-wa-mfungaji-bao-la-hispania-afariki/#respond Tue, 22 Aug 2023 17:28:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7472 Madrid, HispaniaSaa chache baada ya Olga Carmona kufunga bao lililoiwezesha Hispania kuilaza England 1-0 na kubeba Kombe la Dunia la Wanawake (WWC), Shirikisho la Soka Hispania (RFEF) lilimuarifu mchezaji huyo kuhusu kifo cha baba yake.Olga, 23, (pichani),ambaye pia ni beki wa Real Madrid alifunga bao hilo dakika ya 29 na kuifanya timu ya wanawake ya […]

The post Mfungaji bao la Hispania afiwa na baba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Saa chache baada ya Olga Carmona kufunga bao lililoiwezesha Hispania kuilaza England 1-0 na kubeba Kombe la Dunia la Wanawake (WWC), Shirikisho la Soka Hispania (RFEF) lilimuarifu mchezaji huyo kuhusu kifo cha baba yake.
Olga, 23, (pichani),ambaye pia ni beki wa Real Madrid alifunga bao hilo dakika ya 29 na kuifanya timu ya wanawake ya Hispania iweke historia kwa kubeba taji hilo kwa mara ya kwanza.
Taarifa ya REEF ilieleza kuwa baba mzazi wa Carmona baada ya kuugua kwa muda mrefu hatimaye alifariki dunia Ijumaa wakati Hispania ilicheza na England mechi ya fainali juzi Jumapili.
“Tunasikitika kwamba tumelazimika kutangaza kifo cha baba wa Olga Carmona,” ilieleza taarifa ya RFEF ambayo pia ilichapishwa kwenye mitandao ya kijamii.
“Carmona alipata taarifa za kifo cha baba yake baada ya mechiya fainali ya Kombe la Dunia, tunatuma salamu za rambirambi kwa familia katika kipindi hiki cha huzuni. Tunakupenda Olga wewe ni sehemu ya historia ya soka la Hispania,” ilieleza taarifa hiyo ya REEF.
Mara baada ya filimbi ya kumaliza mchezo kupulizwa, wachezaji wa Hispania walianza kushangilia na kucheza uwanjani na Olga alionekana kuwa katika hali ya kawaida wakati wa makabidhiano ya kombe pamoja na medali.

Baadaye Olga alimzungumzia baba yake kupitia mitandao ya kijamii akisema kwamba hakuwa akijua kumbe kulikuwa na nyota yake iliyokuwa ikimuangazia kabla hata ya mechi kuanza.

“Najua ulinipa nguvu ya kufanikisha jambo la kipekee, najua utakuwa unaniangalia usiku huu na unajivunia mimi. Pumzika kwa amani Baba.” alisema Olga.


Klabu ya Real Madrid nayo ilituma salamu za rambirambi kwa familia ya Olga kufuatia kifo cha baba wa mchezaji huyo ambaye pia ndiye aliyefunga bao muhimu la Hispania katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Sweden katika dakika ya 89.

The post Mfungaji bao la Hispania afiwa na baba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/22/baba-wa-mfungaji-bao-la-hispania-afariki/feed/ 0
Busu lamponza bosi wa soka Hispania https://www.greensports.co.tz/2023/08/21/busu-lamponza-bosi-wa-soka-hispania/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/21/busu-lamponza-bosi-wa-soka-hispania/#respond Mon, 21 Aug 2023 18:15:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7468 Madrid, HispaniaRais wa Shirikisho la Soka Hispania, Luis Rubiales ameshutumiwa kwa kumpiga busu ‘zito’ mchezaji wa timu ya Hispania Jenni Hermoso wakati akifurahia Hispania kubeba Kombe la Dunia la Wanawake.Hispania jana Jumapili iliichapa England bao 1-0 na kubeba kombe hilo ikineemeka kwa bao hilo pekee lililofungwa na nahodha wa timu hiyo, Olga Carmona katika dakika […]

The post Busu lamponza bosi wa soka Hispania first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Rais wa Shirikisho la Soka Hispania, Luis Rubiales ameshutumiwa kwa kumpiga busu ‘zito’ mchezaji wa timu ya Hispania Jenni Hermoso wakati akifurahia Hispania kubeba Kombe la Dunia la Wanawake.
Hispania jana Jumapili iliichapa England bao 1-0 na kubeba kombe hilo ikineemeka kwa bao hilo pekee lililofungwa na nahodha wa timu hiyo, Olga Carmona katika dakika ya 29 ya mchezo huo.
Rubiales alimpiga busu Jenni katika hafla ya kukabidhiwa tuzo ya ushindi akionekana mwenye furaha lakini jinsi alivyofanya jambo hilo ni kitu kilichoibua mshangao na kiongozi huyo kujikuta akishutumiwa kila kona huku, Jenni mwenyewe akisema hakupenda alichofanyiwa.
“Sikupenda,” alisema Jenni kupitia mitandao ya kijamii lakini baadaye taarifa ya shirikisho ilimtetea rais huyo wa soka kwa alichokifanya japo viongozi kadhaa waandamizi wa serikali walimshutumu.
Waziri wa Haki na Usawa wa Hispania, Irene Montero alisema kwamba alichofanya Rubiales ni aina nyingine ya udhalilishaji kijinsia dhidi ya wanawake.
“Hii nayo ni aina ya udhalilishaji kijinsia ambayo wanawake wanakutana nayo katika maisha yao ya kila siku, ni jambo ambalo hatuwezi kulichukulia kuwa la kawaida tu,” alisema.

“Tunawajibika kutojenga dhana kwamba kumpiga mtu busu bila ridhaa yake ni jambo ambalo linatokea tu hivi hivi,” alisema.

Baadaye katika taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka, Jenni mwenye umri wa miaka 31 anadaiwa kusema kwamba busu hilo lilitokana na furaha iliyopitiliza ya kushinda Kombe la Dunia na ni jambo la kawaida kutokea.


Busu hilo limemfanya Rubiales kushutumiwa kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya waliotoa maoni hasa kupitia mtandao wa Twitter au X wakimtaka kiongozi huyo kujiuzulu.
Rubiales alizungumza na redio moja akidai kwamba busu hilo ni baina ya marafiki wawili wanaofurahia jambo fulani, na wanaoliangalia kwa namna tofauti ni watu wajinga na wa hovyo. “Tuwapuuze na tuendelee kufurahia mambo mazuri.”
Gazeti la El Pais la Hispania lilitoka na kichwa cha habari kikubwa kilichosena, ‘Jenni hakupenda busu la Rubiales, na sisi hatukupenda.”

The post Busu lamponza bosi wa soka Hispania first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/21/busu-lamponza-bosi-wa-soka-hispania/feed/ 0