Gabriel Jesus - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 09 Apr 2024 09:10:23 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Gabriel Jesus - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Jesus awaambia Bayern, Arsenal si watoto tena https://www.greensports.co.tz/2024/04/09/jesus-awaambia-bayern-arsenal-si-watoto/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/09/jesus-awaambia-bayern-arsenal-si-watoto/#respond Tue, 09 Apr 2024 08:25:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10561 London, EnglandKocha wa Bayern Munich, Thomas Tuchel amesema uzoefu wao mkubwa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya utakuwa faida kubwa katika mechi na Arsenal leo Jumanne ingawa nyota wa Arsenal, Gabriel Jesus ameionya timu hiyo akisema kwamba wao si watoto tena.Timu hizo zinaumana katika mechi ya robo fainali ya ligi hiyo huku Tuchel akisema wanajua namna […]

The post Jesus awaambia Bayern, Arsenal si watoto tena first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Bayern Munich, Thomas Tuchel amesema uzoefu wao mkubwa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya utakuwa faida kubwa katika mechi na Arsenal leo Jumanne ingawa nyota wa Arsenal, Gabriel Jesus ameionya timu hiyo akisema kwamba wao si watoto tena.
Timu hizo zinaumana katika mechi ya robo fainali ya ligi hiyo huku Tuchel akisema wanajua namna ya kuiumiza Arsenal ambayo mafanikio yao makubwa katika ligi hiyo mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2006 walipofikia hatua ya fainali.
“Tuna uzoefu zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa, ligi hii ni tofauti na Ligi Kuu England (EPL), tunataka kuitumia faida hiyo,” alisema Tuchel.
Tuchel (pichani chini) ambaye ataachana na timu hiyo baada ya msimu huu hata hivyo alisema ni sahihi kwa timu yake kukoselewa kwa kuwa imekosa matokeo bora ikiwamo kwenye Ligi Kuu Ujerumani yaani Bundesliga.
Wakati hali ikiwa hivyo kwa Bayern, Arsenal imekuwa na mwenendo mzuri na ni kati ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kulibeba taji la EPL msimu huu.
Kwa upande wake Jesus amewaonya Bayern akisema Arsenal si watoto tena na sasa wanawania kufikia hatua ya nusu fainali ambayo mara ya mwisho waliifikia mwaka 2006.
“Kama nitaona jambo naweza kuwaambia na kuwasaidia (wachezaji wenzangu) nitafanya hivyo lakini sidhani kama hapa bado kuna watoto kila mmoja ameshacheza hatua kubwa kwenye soka, Kombe la Dunia, ligi kuu na sasa ligi ya mabingwa, kwa hiyo nafikiri kila mmoja wetu yuko tayari kuisaidia Arsenal,” alisema Jesus.


Jesus alisema msimu uliopita walicheza soka la uhakika katika sehemu kubwa ya mwanzo ya msimu hadi Januari na baada ya hapo hali ikawa kidogo si nzuri, msimu huu imekuwa kinyume chake.
Bayern katika mechi ya leo itamtegemea Harry Kane kuongoza mashambulizi, mshambuliaji ambaye tayari ameonesha ubora wa kuzifumania nyavu katika msimu wake wa kwanza tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Tottenham.
Hadi sasa Kane ana mabao 38 katika mechi 37 na hivyo usajili wake ulioigharimu Bayern Dola 130 milioni umeonekana kulipa licha ya kiujumla timu hiyo kutokuwa na mwenendo mzuri.

“Kila mtu anajua ubora wa Harry Kane, kwangu mimi huyu ni mfungaji bora duniani, kwa hiyo ni jambo kubwa kucheza na timu yenye wachezaji wa aina hii lakini tunataka kumnyamazisha, na baada ya hapo tujaribu kushinda mechi,” alisema Jesus.


“Pia si Harry Kane pekee, lakini kuna wachezaji wengi kama Sane (Leroy) rafiki yangu wa zamani, Musiala (Jamal) Coman, Muller (Thomas) Gnabry, ni wengi, wana wachezaji wa hadhi ya juu,” alisema Jesus.
Mechi za leo Jumanne Ligi ya Mabingwa Ulaya
Arsenal v Bayern Munich
Real Madrid v Man City

The post Jesus awaambia Bayern, Arsenal si watoto tena first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/09/jesus-awaambia-bayern-arsenal-si-watoto/feed/ 0
Jesus: Pep alinifanya nilie Man City https://www.greensports.co.tz/2023/07/06/jesus-pep-alinifanya-nilie-man-city/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/06/jesus-pep-alinifanya-nilie-man-city/#respond Thu, 06 Jul 2023 20:55:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6838 London, EnglandMshambuliaji wa Arsenal, Gabriel Jesus amesema aliamua kuondoka Man City baada ya kocha Pep Guardiola kumfanya alie alipomtoa kwenye kikosi cha kwanza katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.Jesus alikuwa Man City chini ya Pep kwa takriban miaka mitano kabla ya kuhamia Arsenal majira ya kiangazi mwaka jana, uhamisho ambao anasema ulimfanya ajione yuko […]

The post Jesus: Pep alinifanya nilie Man City first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Mshambuliaji wa Arsenal, Gabriel Jesus amesema aliamua kuondoka Man City baada ya kocha Pep Guardiola kumfanya alie alipomtoa kwenye kikosi cha kwanza katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Jesus alikuwa Man City chini ya Pep kwa takriban miaka mitano kabla ya kuhamia Arsenal majira ya kiangazi mwaka jana, uhamisho ambao anasema ulimfanya ajione yuko huru.
Akizungumza katika mahojiano hivi karibuni, Jesus alisema mambo yake yalibadilika Man City katika mechi ya nyumbani ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2021 dhidi ya Paris Saint-Germain (PSG) alipotajwa katika orodha ya wachezaji walioanzia benchi.
“Kulikuwa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSG kwenye uwanja wa nyumbani, Pep alimpa nafasi Zinchenko acheze namba 9 feki, jambo la ajabu,” alisema Jesus.
“Siku moja kabla hakuwahi hata kumtumia Zinchenko mazoezini, alinipanga mimi katika nafasi ya ushambuliaji, Zinchenko alifikia hatua hadi ya kunidhihaki kwamba siku ile alinionea huruma,” aliongeza Jesus.
“Saa mbili kabla ya mechi kulikuwa na mazungumzo ya timu, kula pamoja, kupumzika kwa dakika 30 na kwenda kwenye mechi, na ndipo akaitaja timu, kwa kweli sikuweza kula nilikwenda moja kwa moja chumbani huku nikilia, nilimpigia simu mama na kuzungumza naye, nilimwambia nataka kuondoka, narudi nyumbani kwa sababu amempanga, Zinchenko, hakunipanga mimi, amempanga beki wa kushoto, ni ukichaa,” alisema.
Jesus baadaye aliingia kuchukua nafasi ya Zinchenko kipindi cha pili na kutoa pasi iliyozaa bao la kusawazisha kabla ya kufunga bao la ushindi na mpira kumalizika kwa City kutoka na ushindi wa 2-1.

“Sikufanya mazoezi ya kupasha misuli, nilijisikia vibaya, dakika tano baada ya Mbappe (Kylian) kufunga bao na sisi kuwa nyuma kwa bao 1-0, Pep aliniingiza, nikatoa pasi na kufunga matokeo yakawa 2-1, mechi iliyofuata dhidi ya RB Leipzig nilidhani atanipanga, hakunipanga, haikuwa rahisi nikaamua kuondoka,” alisema Jesus.


Jesus alijiunga na Man City Januari 2017 akitokea klabu ya Palmeiras ya Brazil na akiwa City ameweza kubeba mataji 11 na timu hiyo.

The post Jesus: Pep alinifanya nilie Man City first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/06/jesus-pep-alinifanya-nilie-man-city/feed/ 0
Arteta afurahia kurejea kwa Gabriel Jesus https://www.greensports.co.tz/2023/04/03/arteta-afurahia-kurejea-kwa-gabriel-jesus/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/03/arteta-afurahia-kurejea-kwa-gabriel-jesus/#respond Mon, 03 Apr 2023 08:31:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5670 London, EnglandKurejea kwa mshambuliaji, Gabriel Jesus katika kikosi cha Arsenal kumemfurahisha kocha Mikel Arteta ambaye anamuona mchezaji huyo aliyekuwa majeruhi tangu Novemba kama usajili mpya.Juzi Jumamosi, kwa mara ya kwanza tangu alipoumia wakati akiiwakilisha Brazil kwenye fainali za Kombe la Dunia, Gabriel Jesus alirejea katika kikosi cha kwanza Arsenal na kufunga mabao mawili katika ushindi […]

The post Arteta afurahia kurejea kwa Gabriel Jesus first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kurejea kwa mshambuliaji, Gabriel Jesus katika kikosi cha Arsenal kumemfurahisha kocha Mikel Arteta ambaye anamuona mchezaji huyo aliyekuwa majeruhi tangu Novemba kama usajili mpya.
Juzi Jumamosi, kwa mara ya kwanza tangu alipoumia wakati akiiwakilisha Brazil kwenye fainali za Kombe la Dunia, Gabriel Jesus alirejea katika kikosi cha kwanza Arsenal na kufunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Leeds United.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Man City, alipata maumivu ya goti na Jumamosi aliichezea Arsenal kabla ya kutolewa katika kipindi cha pili ambapo mashabiki walimpa heshima wakati akitoka uwanjani.
Mabao mawili ya mchezaji huyo yamesaidia kuimarisha mbio za Arsenal katika kulisaka taji la Ligi Kuu England ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa tofauti ya pointi nane dhidi ya Man City inayoshika nafasi ya pili.

“Tumefurahishwa naye, wote wamefurahia, sote tulimpigia makofi, amekuwa akifanya juhudi kubwa katika miezi minne au mitano iliyopita akipewa msaada mkubwa kwenye timu na maofisa,” alisema Arteta.


“Leo (Jumamosi) amekuwa na haki ya kuwa kwenye kikosi cha kwanza, amepata nafasi akiwa mwenye shauku na akapata mabao mawili,” alisema Arteta.
Matokeo ya mechi za EPL mwishoni mwa wiki…
Man City 4-1 Liverpool
Arsenal 4-1 Leeds United
Bournemouth 2-1 Fulham
Brighton 3-3 Brentford
Crystal Palace 2-1 Leicester City
Nottingham Forest 1-1 Wolverhampton
Chelsea 0-2 Aston Villa
West Ham 1-0 Southampton
Newcastle 2-0 Man United

The post Arteta afurahia kurejea kwa Gabriel Jesus first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/03/arteta-afurahia-kurejea-kwa-gabriel-jesus/feed/ 0