Euro 24 - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 01 May 2024 19:16:56 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Euro 24 - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Thibaut Courtois kukosa Euro 2024 https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/thibaut-courtois-kukosa-euro-2024/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/thibaut-courtois-kukosa-euro-2024/#respond Wed, 01 May 2024 19:16:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10799 Brussels, UbelgijiKipa wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Thibaut Courtois (pichani) sasa ni rasmi kuwa hatoweza kuiwakilisha timu hiyo kwenye fainali za Euro 2024 kutokana na matatizo ya goti yanayomkabili.Habari hizo zimekuja huku kukiwa na habari nyingine zinazodai kwamba kipa huyo huenda akawa tayari kuichezea klabu yake ya Real Madrid katika mechi chache zilizobaki za […]

The post Thibaut Courtois kukosa Euro 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Brussels, Ubelgiji
Kipa wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Thibaut Courtois (pichani) sasa ni rasmi kuwa hatoweza kuiwakilisha timu hiyo kwenye fainali za Euro 2024 kutokana na matatizo ya goti yanayomkabili.
Habari hizo zimekuja huku kukiwa na habari nyingine zinazodai kwamba kipa huyo huenda akawa tayari kuichezea klabu yake ya Real Madrid katika mechi chache zilizobaki za msimu huu.
Courtois, 31, amekosekana uwanjani msimu huu wote na mwezi Machi mwaka huu, mchezaji huyo alihitaji kufanyiwa operesheni nyingine baada ya kuonekana kulikuwa na tatizo lililofanya asiweze kuwa fiti.
Akimzungumzia kipa huyo na habari za uwezekano wa kurudi kwenye kikosi cha Real Madrid kwa msimu huu, kocha wa Ubelgiji, Domenico Tedesco alimfuta moja kwa moja katika hesabu zake kwa ajili ya fainali za Euro 2024.
Desemba mwaka jana, Courtois ambaye ameichezea Ubelgiji mara 102 alisema kwamba anadhani hatokuwa amepona kwa asilimia 100 kwa ajili ya kuiwakilisha Ubelgiji kwenye fainali za Euro 2024 zitakazofanyika nchini Ujerumani kati ya mwezi Juni na Julai mwaka huu.
Kwa upande wake, Tedesco alisema kwamba suala la kipa huyo limekwisha, “kuhusu habari hiyo kila kitu kimeshasemwa, sitaki kurudiarudia, tunawaangalia wachezaji ambao wapo katika ubora.”
Naye kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amenukuliwa akisema kwamba ana matumaini ya kipa huyo kuwamo katika kikosi cha Real Madrid kitakachoumana na Cadiz Jumamosi ijayo katika mechi ya La Liga.

The post Thibaut Courtois kukosa Euro 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/thibaut-courtois-kukosa-euro-2024/feed/ 0
Ujerumani, Scotland kufungua pazia Euro 24 https://www.greensports.co.tz/2023/12/03/ujerumani-scotland-kufungua-pazia-euro-24/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/03/ujerumani-scotland-kufungua-pazia-euro-24/#respond Sun, 03 Dec 2023 10:53:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8721 UjerumaniWenyeji wa fainali za Kombe la Ulaya 2024 au Euro 24, Ujerumani wataanza mechi ya ufunguzi kwa kuumana na Scotland baada ya droo ya makundi ya fainali hizo kutangazwa Jumamosi hii na timu hizo kupangwa Kundi A.Mechi ya ufunguzi wa fainali hizo itapigwa Ijumaa ya Juni 14 kwenye dimba la Allianz Arena mjini Munich wakati […]

The post Ujerumani, Scotland kufungua pazia Euro 24 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Ujerumani
Wenyeji wa fainali za Kombe la Ulaya 2024 au Euro 24, Ujerumani wataanza mechi ya ufunguzi kwa kuumana na Scotland baada ya droo ya makundi ya fainali hizo kutangazwa Jumamosi hii na timu hizo kupangwa Kundi A.
Mechi ya ufunguzi wa fainali hizo itapigwa Ijumaa ya Juni 14 kwenye dimba la Allianz Arena mjini Munich wakati England itacheza mechi yake ya kwanza Juni 16 dhidi ya Serbia.
Timu nyingine zilizo katika Kundi A ni Hungary na Switzerland wakati England imepangwa Kundi C ambalo pia lina timu za Denmark pamoja na Slovenia.
Mabingwa watetezi wa fainali hizo, Italia wao wamepangwa Kundi B pamoja na timu za Hispania, Croatia na Albania na mechi ya fainali itakayomtangaza bingwa mpya wa michuano hiyo itapigwa Julai 14 kwenye Uwanja wa Olimpiki mjini Berlin.
Makundi ya fainali hizo ni kama ifuatavyo…
Kundi A: Ujerumani, Scotland, Hungary na Switzerland
Kundi B: Hispania, Croatia, Italia na Albania
Kund C Slovenia, Denmark, Serbia na England
Kundi D Uholanzi, Austria, Ufaransa na (mshindi play-off-A)
Kundi E: Ubelgiji, Slovakia, Romania na (mshindi play-off-B)
Kundi F: Uturuki, Ureno, Jamhuri ya Czech (mshindi play-off-C)
Play off A-Poland, Estonia, Wales, Finland, Estonia
Play off B- Israel, Bosnia-Herzegovina, Ukraine, Iceland
Play off C- Georgia, Ugiriki, Kazakhstan, Luxembourg

The post Ujerumani, Scotland kufungua pazia Euro 24 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/03/ujerumani-scotland-kufungua-pazia-euro-24/feed/ 0
England yafuzu Euro 24 https://www.greensports.co.tz/2023/10/18/england-yafuzu-euro-24/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/18/england-yafuzu-euro-24/#respond Wed, 18 Oct 2023 08:22:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8133 London, EnglandHatimaye England imefuzu fainali za Kombe la Ulaya 2024 (Euro 24) baada ya kuichapa Italia mabao 3-1 katika mechi ambayo ubora wa kiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham ulijidhihirisha kwa mara nyingine.England ilikuwa ikihitaji pointi moja ili kufuzu ingawa Italia walitaka kuvuruga sherehe baada ya kuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 15 […]

The post England yafuzu Euro 24 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Hatimaye England imefuzu fainali za Kombe la Ulaya 2024 (Euro 24) baada ya kuichapa Italia mabao 3-1 katika mechi ambayo ubora wa kiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham ulijidhihirisha kwa mara nyingine.
England ilikuwa ikihitaji pointi moja ili kufuzu ingawa Italia walitaka kuvuruga sherehe baada ya kuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 15 lililofungwa na nyota wa zamani wa West Ham, Gianluca Scamacca.
Juhudi za Bellingham hadi kuchezewa rafu na mwamuzi kutoa penalti dakika ya 32 kuliipa England bao la kusawazisha lililofungwa na Harry Kane kwa mkwaju wa penalti. Kane sasa anakuwa amefikisha mabao 60 na timu ya England.
Bellingham, 20, kwa mara nyingine alitengeneza bao la pili la England katika dakika ya 57 baada ya kumuunganishia pasi Marcus Rashford ambaye aliitumia vyema kuipatia England bao kabla Kane hajamalizia kwa bao la tatu dakika ya 77.
England kwa sasa inashika usukani Kundi C ikiwa na pointi 16 wakati Italia inashika nafasi ya tatu na itacheza mechi yake ya mwisho na Ukraine, mechi ambayo itaamua kama timu hiyo itashika nafasi ya pili na kufuzu au la.
Ushindi wa England dhidi ya Italia umedhihirisha kwa mara nyingine uwezo wa Bellingham ndani ya kikosi cha timu ya taifa baada ya kutamba katika klabu kwani alihusika na kujitoa katika kila hatua ya mechi hiyo hadi dakika ya mwisho ya mchezo.
Matokeo ya mechi za kufuzu Euro 2024…
England 3-1 Italia
Ireland Kask 0-1 Slovenia
San Marino 1-2 Denmark
Finland 1-2 Kazakhstan
Malta 1-3 Ukraine
Lithuania 2-2 Hungary
Serbia 3-1 Montenegro

The post England yafuzu Euro 24 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/18/england-yafuzu-euro-24/feed/ 0
Ufaransa, Ureno zafuzu Euro 2024 https://www.greensports.co.tz/2023/10/14/ufaransa-ureno-zafuzu-euro-2024/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/14/ufaransa-ureno-zafuzu-euro-2024/#respond Sat, 14 Oct 2023 15:06:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8103 Amsterdam, UholanziMastaa Kylian Mbappe wa Ufaransa na Cristiano Ronaldo wa Ureno wamezifungia timu zao mabao na kuziwezesha kufuzu fainali za Kombe la Ulaya 2024 au Euro 24 zitakazofanyika mwakani nchini Ujerumani.Timu nyingine iliyopata ushindi katika mechi hizo zilizochezwa jana Ijumaa na kufuzu ni Ubelgiji na kuzifanya timu hizo tatu ‘kutangulia’ nchini Ujerumani.Mabao mawili ya Mbappe […]

The post Ufaransa, Ureno zafuzu Euro 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Amsterdam, Uholanzi
Mastaa Kylian Mbappe wa Ufaransa na Cristiano Ronaldo wa Ureno wamezifungia timu zao mabao na kuziwezesha kufuzu fainali za Kombe la Ulaya 2024 au Euro 24 zitakazofanyika mwakani nchini Ujerumani.
Timu nyingine iliyopata ushindi katika mechi hizo zilizochezwa jana Ijumaa na kufuzu ni Ubelgiji na kuzifanya timu hizo tatu ‘kutangulia’ nchini Ujerumani.
Mabao mawili ya Mbappe yaliiwezesha Ufaransa kutoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji Uholanzi na huo kuwa ushindi wa sita kwa Ufaransa iliyo katika Kundi B.
Mbappe aliandika bao la kwanza dakika ya saba akiunganisha krosi ya Jonathan Clauss na kupiga shuti lililomshinda kipa wa Uholanzi, Bert Verbruggen kabla ya kufunga bao la pili dakika ya 53 akiitumia pasi ya Adrien Rabiot.
Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa na wakati mgumu katika mechi za karibuni na timu yake ya PSG, mabao yake yalimfariji kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps ambaye alisema hana cha kuhofia kwa mchezaji huyo ambaye amedhihirisha uwezo na ubora wake.
Bao pekee la Uholanzi lilipatikana dakika ya 10 kabla ya mpira kumalizika mfungaji akiwa ni kiungo wa Feyenoord, Quilindschy Hartman.
Mabao mawili ya Ronaldo yaliiwezesha Ureno kutoka na ushindi wa mabao 3-2 mbele ya Slovakia na kufuzu moja kwa moja huku Ronaldo akiimarisha rekodi yake ya mabao na timu hiyo kufikia 125 katika mechi 202.
Bao jingine la Ureno lilifungwa na Goncalo Ramos kwa kichwa wakati yale ya Slovakia yalifungwa na David Hancko na Stanislav Lobotka.
Nao Ubelgiji walipata ushindi wa mabao 3-2 mbele ya Austria mjini Vienna wakineemeka na mabao ya
Romelu Lukaku, Dodi Lukébakio aliyefunga mawili wakati mabao ya Austria yalifungwa na Konrad Laimer na Marcel Sabitzer.
Matokeo ya mechi za kufuzu Euro 24…
Iceland 1-1 Luxembourg
Liechtenstein 0-2 Bosnia-Herzegovina
Ureno 3-2 Slovakia
Uholanzi 1-2 UfaransaT
Jam Ireland 0-2 Ugiriki
Estonia 0-2 Azerbaijan
Austria 2-3 Ubelgiji
Mechi za kufuzu Euro 2024 zinazochezwa leo Jumamosi
Kask Ireland v San Marino
Ukraine v Kask Macedonia
Italia v Malta
Bulgaria v Lithuania
Hungary v Serbia
Slovenia v Finland
Denmark v Kazakhstan

The post Ufaransa, Ureno zafuzu Euro 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/14/ufaransa-ureno-zafuzu-euro-2024/feed/ 0