England - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 19 Jul 2026 14:57:26 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg England - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 England yashika nafasi ya tatu https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/england-yashika-nafasi-ya-tatu/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/england-yashika-nafasi-ya-tatu/#respond Sun, 19 Jul 2026 14:53:40 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14810 Miami, MarekaniEngland imeshika nafasi ya tatu kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 ikiilaza Ufaransa mabao 6-4 huku Jude Bellingham akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kufunga mabao saba katika moja ya Kombe la Dunia.Timu hizo ziliumana katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu Jumamosi Julai 18, 2026 huku mechi ya […]

The post England yashika nafasi ya tatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Miami, Marekani
England imeshika nafasi ya tatu kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 ikiilaza Ufaransa mabao 6-4 huku Jude Bellingham akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kufunga mabao saba katika moja ya Kombe la Dunia.
Timu hizo ziliumana katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu Jumamosi Julai 18, 2026 huku mechi ya fainali kati ya Hispania na Argentina ikisubiriwa kupigwa Jumapili Julai 19, 2026.
Bellingham ambaye pia ni kiungo wa Real Madrid, awali alifungana na nahodha na mshambuliaji wa England, Harry Kane aliyefunga mabao sita katika fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
Rekodi kama hiyo ya mabao sita kabla ya hapo ilikuwa ikishikiliwa na Garry Lineker aliyeifungia England idadi mabao kama hiyo ya mabao kwenye fainali za Kombe la Dunia 1986 nchini Mexico.
Katika mechi dhidi ya Ufaransa, Bellingham, 23, aliingizwa uwanjani dakika ya 79 na kufunga bao lililotokana na shambulizi la kushtukiza.
Dakika 12 kabla ya hapo alikuwa afunge bao kwa mkwaju wa penalti lakini akaamua kumpa nafasi hiyo Bukayo Saka ambaye hakumuangusha, aliitumia vyema penalti hiyo kuipatia England bao.
Saka hata hivyo baada ya mechi alisema kwamba ni Bellingham ndiye aliyemwambia aende akapige mpira huo wa penalti ili apate hat trick (mabao matatu).
Katika mechi hiyo mbali na Bellingham, mabao mengine ya England yalifungwa na Declan Rice dakika ya tatu, Konsa dakika ya 18 na Saka ambaye alifunga dakika za 37, 45 na 87.
Mabao ya Ufaransa yalifungwa na Kylian Mbappe aliyefunga mawili dakika za 48 na 66 wakati mengine mawili yalifungwa na Barcola dakika ya 54 na Dembele dakika ya 90.

The post England yashika nafasi ya tatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/england-yashika-nafasi-ya-tatu/feed/ 0
Tuchel ajitetea baada ya England kutolewa https://www.greensports.co.tz/2026/07/18/tuchel-ajitetea-baada-ya-england-kutolewa/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/18/tuchel-ajitetea-baada-ya-england-kutolewa/#respond Sat, 18 Jul 2026 19:34:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14802 Miami, MarekaniKocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Thomas Tuchel ametetea maamuzi yake katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Argentina licha ya timu hiyo kushindwa.Akizungumza kabla ya mechi ya kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Ufaransa, kocha huyo Mjerumani alisema kama anahitajika mtu wa kulaumiwa basi yeye yuko […]

The post Tuchel ajitetea baada ya England kutolewa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Miami, Marekani
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Thomas Tuchel ametetea maamuzi yake katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Argentina licha ya timu hiyo kushindwa.
Akizungumza kabla ya mechi ya kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Ufaransa, kocha huyo Mjerumani alisema kama anahitajika mtu wa kulaumiwa basi yeye yuko tayari kubeba zigo la lawama.
Tuchel hata hivyo alisema hana cha kujutia na kuongeza kuwa timu yake ndiyo iliyoumizwa zaidi kuliko yeyote na kwamba kilichotokea ni jeraha ambalo wanalazimika kulibeba.
Katika mechi hiyo, England walikuwa wakipambana kuweka rekodi ya kufikia hatua ya fainali ya Kombe la Dunia mara ya kwanza tangu kufanya hivyo mara ya mwisho mwaka 1966, miaka 60 iliyopita.
Kilichotokea katika mechi hiyo kiliiumiza mno England kwani baada ya kuongoza kwa bao 1-0 mambo yalibadilika mwishoni na kujikuta wakilala kwa mabao 2-1 huku wakipigwa presha na Messi.
Mabao ya Argentina yaliyopatikana dakika za 85 na 90 (+2) yaliwaumiza mno mashabiki wa England huku baadhi ya wachambuzi wakilaumu maamuzi kadhaa ya Tuchel ikiwamo kujihami zaidi badala ya kushambulia.
Alipoulizwa ni kwa nini timu yake ilicheza kwa kujihami zaidi Tuchel alisema hicho ndicho kilichotakiwa kufanywa kwa namna Argentina walivyokuwa na hajutii uamuzi wake katika hilo.

“Nilichukua maamuzi mengi, niliamini fikra zangu, uzoefu wangu, niliamini katika upambanaji wangu na nilichukua maamuzi kwa lengo la kuisaidia timu kupata matokeo lakini hatukupata matokeo,” alisema Tuchel.


England inacheza mechi ya kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Ufaransa, mechi itakayopigwa Jumamosi Julai 18, 2026 wakati mechi ya fainali kati ya Argentina na Hispania itapigwa Jumapili Julai 19, 2026.

The post Tuchel ajitetea baada ya England kutolewa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/18/tuchel-ajitetea-baada-ya-england-kutolewa/feed/ 0
Tuchel ataka England wacheze kwa raha zao https://www.greensports.co.tz/2025/06/10/tuchel-ataka-england-wacheze-kwa-raha-zao/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/10/tuchel-ataka-england-wacheze-kwa-raha-zao/#respond Tue, 10 Jun 2025 09:59:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13565 London, EnglandKocha wa England, Thomas Tuchel amewataka wachezaji kucheza kama wanapokuwa mazoezini kwa kucheza wakiwa na nyuso za furaha wakati wakijiandaa kuivaa Senegal, leo Jumanne, Juni 10, 2025.Tuchel, alionekana kutofurahia uchezaji wa timu yake licha ya ushindi wa bao 1-0 ambao timu hiyo iliupata dhidi ya Andorra katika mechi ya kufuzu fainali za Kombe la […]

The post Tuchel ataka England wacheze kwa raha zao first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
London, England
Kocha wa England, Thomas Tuchel amewataka wachezaji kucheza kama wanapokuwa mazoezini kwa kucheza wakiwa na nyuso za furaha wakati wakijiandaa kuivaa Senegal, leo Jumanne, Juni 10, 2025.
Tuchel, alionekana kutofurahia uchezaji wa timu yake licha ya ushindi wa bao 1-0 ambao timu hiyo iliupata dhidi ya Andorra katika mechi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia, Jumamosi iliyopita.
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea alisema kwamba wachezaji wake walifanya mazoezi tofauti na sasa amewataka kucheza wakiwa huru na kufuata maelekezo.
Tuchel ambaye ni Mjerumani, alianza kazi ya kuinoa England Januari mwaka huu na mechi ya leo ya kirafiki dhidi ya Senegal ni mechi yake ya nne akiwa na timu hiyo.
“Naona tunafanya mazoezi tukiwa na tabasamu lakini hatuchezi mechi tukiwa na tabasamu, kwa hakika tunahitaji kuwa bora zaidi, tunatakiwa kuchangamka katika kundi letu, naona kama tunajitenga uwanjani,” alisema Tuchel.
Tuchel aliongeza kwa kusema kwamba timu hiyo ina mambo mengi mazuri ya kuyafanya nje ya uwanja wa mazoezi ambayo amekuwa akiyaona na kinachotakiwa ni kuhakikisha yote yanahamia uwanjani wakiwa kwenye mechi.
“Jambo la muhimu ni kuweka umakini katika kanuni za mchezo, kupeana maelekezo sahihi miongoni mwa wachezaji na kile tunachokitarajia katika majukumu yao,” alisema Tuchel.

The post Tuchel ataka England wacheze kwa raha zao first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/10/tuchel-ataka-england-wacheze-kwa-raha-zao/feed/ 0
Tuchel aanza kibarua England https://www.greensports.co.tz/2025/01/01/tuchel-aanza-kibarua-england/ https://www.greensports.co.tz/2025/01/01/tuchel-aanza-kibarua-england/#respond Wed, 01 Jan 2025 20:22:00 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12555 London, EnglanedKocha wa zamani wa Chelsea na Bayern Munich, Thomas Tuchel, leo Januari Mosi, 2025 ameanza rasmi kazi yake mpya ya kuinoa timu ya taifa ya England akiwa na mkataba wa miezi 18.Tuchel ambaye Oktoba mwaka jana, alitangazwa rasmi kuchukua nafasi hiyo iliyokuwa ikishikliwa na Gareth Southgate ataiongoza timu hiyo hadi baada ya fanali za […]

The post Tuchel aanza kibarua England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, Englaned
Kocha wa zamani wa Chelsea na Bayern Munich, Thomas Tuchel, leo Januari Mosi, 2025 ameanza rasmi kazi yake mpya ya kuinoa timu ya taifa ya England akiwa na mkataba wa miezi 18.
Tuchel ambaye Oktoba mwaka jana, alitangazwa rasmi kuchukua nafasi hiyo iliyokuwa ikishikliwa na Gareth Southgate ataiongoza timu hiyo hadi baada ya fanali za Kombe la Dunia 2026.
Ikiwa na Southgate, England ilifikia hatua ya fainali ya Kombe la Ulaya 2024 au Euro 2024 nchini Ujerumani lakini licha ya matarajio makubwa timu hiyo ilishindwa kutamba mbele ya Hispania waliobeba taji hilo.
Katika kibarua hicho kipya, Tuchel atakuwa akisaidiwa na Anthony Barry ambaye pia amefanya naye kazi tangu akiwa Chelsea na baadaye Bayern Munich.
England kwenye kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia 2026 imepangwa kundi moja na timu za Serbia, Latvia, Albania na Andora.
Kati ya timu hizo, Tuchel ambaye pia amewahi kuzinoa timu za Borussia Dortmund ya Ujeruani na PSG ya Ufaransa alisema anaziheshimu Serbia na Albania ambazo alisema zina uwezo wa kuibua mshangao.
Kibarua cha kwanza kwa Tuchel na timu ya England kwenye kufuzu Kombe la Dunia 2026 kitakuwa Machi 21 mwaka huu dhidi ya Albania na siku tatu baadaye dhidi ya Latvia mechi ambazo zitapigwa kwenye dimba la Wembley.
Mara baada ya kuondoka kwa Southgate, England imekuwa chini ya kocha wa muda, Lee Carsey ambaye ana rekodi ya kushinda mechi tano kati ya sita.

The post Tuchel aanza kibarua England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/01/01/tuchel-aanza-kibarua-england/feed/ 0
Tuchel kuinoa England? https://www.greensports.co.tz/2024/10/16/tuchel-kupewa-majukumu-england/ https://www.greensports.co.tz/2024/10/16/tuchel-kupewa-majukumu-england/#respond Wed, 16 Oct 2024 06:03:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12010 London, EnglandChama cha Soka England, (FA) kinadaiwa kuanza mazungumzo na kocha wa zamani wa klabu za Chelsea na Bayen Munich, Thomas Tuchel ili akabidhiwe jukumu la kuinoa timu ya taifa ya England.Iwapo mpango huo utafanikiwa Tuchel atakuwa kocha wa tatu wa kigeni kuinoa timu hiyo baada ya Sven Goran Eriksson wa Sweden na Fabio Capelo […]

The post Tuchel kuinoa England? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Chama cha Soka England, (FA) kinadaiwa kuanza mazungumzo na kocha wa zamani wa klabu za Chelsea na Bayen Munich, Thomas Tuchel ili akabidhiwe jukumu la kuinoa timu ya taifa ya England.
Iwapo mpango huo utafanikiwa Tuchel atakuwa kocha wa tatu wa kigeni kuinoa timu hiyo baada ya Sven Goran Eriksson wa Sweden na Fabio Capelo wa Italia kuwahi kuinoa timu hiyo.
Kwa sasa timu ya England inanolewa na kocha wa muda, Lee Carsley ambaye amekuwa akiinoa timu hiyo tangu kujiuzulu kwa Gareth Southgate ambaye alidumu kwa miaka minane.
Southgate aliamua kujiuzulu baada ya tmu hiyo kufikia hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Ulaya au Euro 2024 nchini Ujerumani lakini ikashindwa kutamba mbele ya Hispania waliobeba taji.
Taarifa kuhusu mpango huo ilieleza kuwa mazungumzo ya awali na kocha huyo Mjerumani yameshafanyika huku kocha huyo akipewa nafasi kubwa ya kuchukua kibarua hicho.
Tuchel alilazimika kuachana na klabu ya Bayern Mei mwaka huu licha ya kuwa na mwaka mmoja katika mkataba wake lakini aliondoka kwa kuwa mwenendo wa timu haukuwafurahisha mabosi wake.
Kocha huyo ambaye aliiwezesha Chelsea kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, mambo yake hayakuwa mazuri Bayern baada ya timu hiyo kushindwa kubeba taji la Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga ikiwa ni mara ya kwanza tangu msimu wa 2011-12.

The post Tuchel kuinoa England? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/10/16/tuchel-kupewa-majukumu-england/feed/ 0
Ashley Cole rasmi England https://www.greensports.co.tz/2024/09/14/ashley-cole-rasmi-england/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/14/ashley-cole-rasmi-england/#respond Sat, 14 Sep 2024 15:51:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11905 London, EnglandChama cha Soka England au FA kimemkabidhi rasmi beki wa zamani wa Arsenal na Chelsea, Ashley Cole majukumu ya kocha msaidizi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya wanaume ya England.Cole ambaye amekuwa akimsaidia kocha wa muda wa timu hiyo, Lee Carsley, mbali na Arsenal na Chelsea lakini pia amewahi kuwa mchezaji tegemeo wa […]

The post Ashley Cole rasmi England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Chama cha Soka England au FA kimemkabidhi rasmi beki wa zamani wa Arsenal na Chelsea, Ashley Cole majukumu ya kocha msaidizi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya wanaume ya England.
Cole ambaye amekuwa akimsaidia kocha wa muda wa timu hiyo, Lee Carsley, mbali na Arsenal na Chelsea lakini pia amewahi kuwa mchezaji tegemeo wa timu ya England akiichezea mara 107.
Tangu mwaka 2021, Cole amekuwa akimsaidia Carsley katika timu ya vijana chini ya miaka 21 ya England ambayo waliiwezesha kubeba taji la Ulaya la vijana U-21 katika mashindano yaliyofanyika Georgia.
Mafanikio hayo bila shaka ndiyo yaliyoishawishi FA kumuamini kuwa mtu sahihi wa kusaidiana na Carsley katika timu ya England ambayo kabla ya hapo ilikuwa ikinolewa na Gareth Southgate.
Kwa mantiki hiyo beki huyo wa zamani wa kushoto sasa atakuwa na makumu mawili kwani mbali na England pia ataendelea na majukumu yake ya ukocha kwenye kikosi cha Birmingham City.
Cole akiwa mchezaji alijipatia umaarufu kwenye kikosi cha England tangu aanze kuichezea timu hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2001 amekuwa na namba ya kudumu hadi mwaka 2014.
Akiwa na timu hiyo ameshiriki mashindano matano makubwa lakini akiwa na klabu ana rekodi ya kubeba mataji ya Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2012 akiwa na Chelsea.

The post Ashley Cole rasmi England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/14/ashley-cole-rasmi-england/feed/ 0
Kocha, wachezaji England wazomewa, warushiwa makopo https://www.greensports.co.tz/2024/06/26/kocha-wachezaji-england-wazomewa-warushiwa-makopo/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/26/kocha-wachezaji-england-wazomewa-warushiwa-makopo/#respond Wed, 26 Jun 2024 05:57:00 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11440 Cologne, UjerumaniKiwango duni cha England kwenye Euro 2024 nchini Ujerumani kimewakera mashabiki wake hadi kuwazomea na kuwarushia makopo wachezaji na kocha wao jana Jumanne katika mechi yao na Slovenia iliyoisha kwa sare ya 0-0.Zomeazomea hiyo imemshangaza kocha wa timu hiyo, Gareth Southgate ambaye ametaka mashabiki kuiunga mkono timu hiyo ambayo imemaliza Kundi C ikiwa inashika […]

The post Kocha, wachezaji England wazomewa, warushiwa makopo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Cologne, Ujerumani
Kiwango duni cha England kwenye Euro 2024 nchini Ujerumani kimewakera mashabiki wake hadi kuwazomea na kuwarushia makopo wachezaji na kocha wao jana Jumanne katika mechi yao na Slovenia iliyoisha kwa sare ya 0-0.
Zomeazomea hiyo imemshangaza kocha wa timu hiyo, Gareth Southgate ambaye ametaka mashabiki kuiunga mkono timu hiyo ambayo imemaliza Kundi C ikiwa inashika usukani na kufuzu hatua ya mtoano.
Katika mechi hiyo, England ilipiga mashuti manne tu yaliyolenga goli jambo lililowakera mashabiki lakini Southgate amesisitiza kwamba mashabiki wanatakiwa kuiunga mkono timu hiyo.
Timu hiyo ilikutana na zomeazomea hiyo wakati wa mapumziko na hata baada ya mpira kumalizika Southgate alipowasogelea mashabiki na kuwaonesha ishara ya kuwashukuru wapo waliomuunga mkono na wengine kutomuunga mkono waziwazi.
Southgate hata hivyo aliwatetea wachezaji wake akitaka wasizomewe badala yake alisema kwamba anaweza kuelewa hali hiyo ikielekezwa kwake.

“Naweza kuelewa mtazamo wao kwangu na hiyo ni afadhali kuliko kuelekeza mtazamo wao kwa wachezaji inaleta mazingira tata kwenye timu, sijawahi kuona timu yoyote inafuzu na kujikuta katika hali kama hii,” alisema Southgate.


Southgate hata hivyo alisema kwamba ataendelea kuwashukuru mashabiki ambao wanakuwa watu wazuri kwake wakati wote wa mchezo.
Hatma ya Southgate kuendelea kukinoa kikosi cha England itajulikana mara baada ya fainali za Euro 2024 kumalizika ingawa mkataba wake na timu hiyo unafikia mwisho Desemba mwaka huu.

Matokeo Euro 2024 jana Jumanne
Kundi C
England 0-0 Slovenia
Denmark 0-0 Serbia
Kundi D
Uholanzi 2-3 Austria
Ufaransa 1-1 Poland

The post Kocha, wachezaji England wazomewa, warushiwa makopo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/26/kocha-wachezaji-england-wazomewa-warushiwa-makopo/feed/ 0
Kiwango England hakimvutii Southgate https://www.greensports.co.tz/2024/06/21/kiwango-england-hakimvutii-southgate/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/21/kiwango-england-hakimvutii-southgate/#respond Fri, 21 Jun 2024 08:32:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11392 Frankfurt, UjerumaniKocha wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate ameeleza kutofurahishwa na kiwango cha timu yake kwenye fainali za soka za Euro 2024 zinazoendelea Ujerumani licha ya kushinda mechi moja na kutoa sare moja.Jana Alhamisi, England ilitoa sare ya bao 1-1 na Denmark, matokeo ambayo yamewafanya washike usukani katika Kundi C na kujiweka pazuri […]

The post Kiwango England hakimvutii Southgate first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Frankfurt, Ujerumani
Kocha wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate ameeleza kutofurahishwa na kiwango cha timu yake kwenye fainali za soka za Euro 2024 zinazoendelea Ujerumani licha ya kushinda mechi moja na kutoa sare moja.
Jana Alhamisi, England ilitoa sare ya bao 1-1 na Denmark, matokeo ambayo yamewafanya washike usukani katika Kundi C na kujiweka pazuri kufuzu hatua ya mtoano inayoshirikisha timu 16.
England ambayo ilianza fainali hizo kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0 mbele ya Serbia hata hivyo, imeshindwa kuutawala vyema mchezo dhidi ya Denmark na haikuwa katika kiwango bora.
Katika mechi hiyo iliyopigwa mjini Frankfurt, England ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 18 lililofungwa na Harry Kane na Denmark walisawazisha kupitia Morten Hjulmand dakika ya 34.
“Tunaelewa kuwa watu watakuwa wamesikitishwa na kiwango na hivyo ni lazima tucheze vizuri na kuwa bora zaidi,” alisema Southgate.
Juhudi za England kusaka bao la kuongoza hazikuweza kuzaa matunda, kama wangepata bao hilo lingeweza kuwafanya wafuzu hatua inayofuata moja kwa moja wakiwa na mechi moja mkononi.

“Kwa wakati huu hatujautumia vizuri mpira kiasi cha kutosha na ni lazima tukubali kwamba kama hufanyi hivyo utaweza kukwama kama ambavyo imekuwa kwetu, tunajua kwamba kuna kiwango ambacho tunalazimika kukitafuta,” alisema Southgate.


England itakamilisha mechi yake ya hatua ya makundi dhidi ya Slovenia, katika mechi itakayopigwa Jumanne ijayo mjini Cologne.

The post Kiwango England hakimvutii Southgate first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/21/kiwango-england-hakimvutii-southgate/feed/ 0
Bellingham aokoa jahazi England https://www.greensports.co.tz/2024/06/17/bellingham-aokoa-jahazi-england/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/17/bellingham-aokoa-jahazi-england/#respond Mon, 17 Jun 2024 16:28:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11348 Munich, UjerumaniBao pekee la Jude Bellingham dhidi ya Serbia limetosha kuibeba England kwenye fainali za soka za Euro 2024 zinazoendelea nchini Ujerumani ingawa kiwango cha timu hiyo kimeanza kuibua wasiwasi.Katika mechi hiyo iliyopigwa jana Jumapili, Bellingham nyota wa Real Madrid alifunga bao hilo pekee katika dakika ya 13 kwa kichwa akiunganisha krosi iliyoanzia kwa Bukayo […]

The post Bellingham aokoa jahazi England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Bao pekee la Jude Bellingham dhidi ya Serbia limetosha kuibeba England kwenye fainali za soka za Euro 2024 zinazoendelea nchini Ujerumani ingawa kiwango cha timu hiyo kimeanza kuibua wasiwasi.
Katika mechi hiyo iliyopigwa jana Jumapili, Bellingham nyota wa Real Madrid alifunga bao hilo pekee katika dakika ya 13 kwa kichwa akiunganisha krosi iliyoanzia kwa Bukayo Saka.
Mashabiki wa England walimshangilia mara kwa mara Bellingham ambaye alionekana kuwa shujaa wao kwa kuwapa bao ambalo limewawezesha kushika usukani Kundi C ambalo pia lina timu za Denmark na Slovenia zilizotoka sare ya bao 1-1 jana hiyo hiyo.
Bellingham ndiye aliyeanzisha shambulizi lililozaa bao hilo na kwa kiasi kikubwa ndiye aliyekuwa kinara wa mashambulizi ya timu hiyo na haikushangaza kwa mashabiki kumshangilia kwa kumtaja jina lake mara kwa mara.
Pamoja na ushindi huo, bado kiwango cha England kimeacha maswali kama ni timu ambayo itaweza kufika mbali au hata kubeba taji hilo hasa kwa kuwa ilikuwa ikitajwa kati ya timu zenye uwezo huo.
Bellingham hata hivyo hakubaliani na mtazamo wa England imecheza kiwango duni badala yake anaamini timu hiyo imeonesha uwezo na ndio maana imetoka na ushindi.

“Sikubaliani na hilo, nafikiri kipindi cha kwanza tumeonesha jinsi tunavyoweza kufunga goli dhidi ya timu yoyote na kipindi cha pili tumeonesha ni kwa nini tuna uwezo wa kuzuia tusifungwe na timu yoyote,” alisema Bellingham.


Nahodha na mshambuliaji tegemeo wa England, Harry Kane alisema kwamba japo kiwango hakikuwa kizuri lakini jambo zuri ni kwamba wamepata ushindi muhimu.
“Kwa ujumla ni ushindi tuliostahili, ni suala la kupiga hatua, kuna wakati kipindi cha pili tulijikuta tukirundikana katika eneo letu na tulipata tabu kidogo kutoka, yote kwa yote huu ni ushindi muhimu,” alisema Kane.

The post Bellingham aokoa jahazi England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/17/bellingham-aokoa-jahazi-england/feed/ 0
Southgate aanza kuaga England https://www.greensports.co.tz/2024/06/12/southgate-aanza-kuaga-england/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/12/southgate-aanza-kuaga-england/#respond Wed, 12 Jun 2024 06:39:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11304 London, EnglandKocha wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate amesema kwamba fainali za Kombe la Ulaya au Euro 2024 huenda ikawa nafasi ya mwisho kwake kubeba taji akiwa kocha wa timu hiyo.Kauli ya kocha huyo imekuja huku ikifahamika kuwa mkataba wake na timu ya England unafikia ukomo Desemba mwaka huu na hivyo kutoa kila […]

The post Southgate aanza kuaga England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate amesema kwamba fainali za Kombe la Ulaya au Euro 2024 huenda ikawa nafasi ya mwisho kwake kubeba taji akiwa kocha wa timu hiyo.
Kauli ya kocha huyo imekuja huku ikifahamika kuwa mkataba wake na timu ya England unafikia ukomo Desemba mwaka huu na hivyo kutoa kila dalili kwamba haya huenda ni mashindano yake ya mwisho makubwa akiwa kocha England.
Habari nyingine hata hivyo zinadai kuwa Chama cha Soka England (FA) kinadaiwa kujipanga ili kumshawishi aendelee kuinoa timu hiyo hadi kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 ambazo zitafanyika katika nchi za Marekani, Canada na Mexico.
Pamoja na kuwapo mpango huo lakini Southgate amenukuliwa na chanzo kimoja cha habari akisema kwamba iwapo England itashindwa kubeba taji hilo nchini Ujerumani huo huenda ukawa ndio mwisho wake na timu hiyo.

“Kama hatutashinda huenda nisiwe hapa tena, hivyo hii inaweza kuwa nafasi yangu ya mwisho, kama nataka kuwa timu kubwa na nataka kuwa kocha wa hadhi ya juu hapo ni lazima kufanya makubwa katika mashindano makubwa,” alisema Southgate.


Southgate, 53 amekuwa kocha wa England tangu mwaka 2016 na anajivunia rekodi ya kuiwezesha timu hiyo kufikia hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2018, fainali Euro 2020 na robo fainali Kombe la Dunia 2022.

The post Southgate aanza kuaga England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/12/southgate-aanza-kuaga-england/feed/ 0