Bayern Munich - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 30 Sep 2024 05:58:54 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Bayern Munich - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Majeruhi Kane hali si tete https://www.greensports.co.tz/2024/09/30/majeruhi-kane-hali-si-tete/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/30/majeruhi-kane-hali-si-tete/#respond Mon, 30 Sep 2024 05:58:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11957 Munich, UjerumaniKlabu ya Bayern Munich imemfanyia vipimo mshambuliaji wake, Harry Kane aliyeumia enka jana Jumamosi katika mechi dhidi ya Bayer Leverkusen na kubaini kuwa tatizo si kubwa.Kane, 31, ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya England alilazimika kutolewa dakika ya 86 katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Alianz Arena na kumalizika kwa […]

The post Majeruhi Kane hali si tete first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Klabu ya Bayern Munich imemfanyia vipimo mshambuliaji wake, Harry Kane aliyeumia enka jana Jumamosi katika mechi dhidi ya Bayer Leverkusen na kubaini kuwa tatizo si kubwa.
Kane, 31, ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya England alilazimika kutolewa dakika ya 86 katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Alianz Arena na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Kuumia kwa Kane kulitokana na kugongana na Amine Adli wa Leverkusen na kuibua hofu kwamba Bayern ingemkosa nyota huyo ambaye hadi sasa ana mabao 10 katika mechi saba za mashindano yote msimu huu.
Timu ya madaktari wa Bayern hata hivyo baada ya kumfanyia vipimo leo Jumapili wamebaini kwamba tatizo si kubwa na mshambuliaji huyo anaendelea vizuri.
Habari zaidi zinadai kwamba Kane mwenyewe saa kadhaa baada ya mechi hiyo alinukuliwa akisema kwamba anatarajia kuwa fiti kwa ajili ya mechi ya Jumatano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo Bayern itakuwa mgeni wa Aston Villa.
Katika mechi dhidi ya Leverkusen, Bayern ilikuwa ya kwanza kutikiswa nyavu zake na Robert Andrich kabla ya kusawazisha kwa bao lililofungwa na Aleksandar Pavlovic.
Matokeo hayo hayajaitoa Bayern kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Ujerumani au Bundsliga ikifuatiwa na RB Leipzig kwa tofauti ya pointi mbili na mabingwa watetezi Leverkusen wanashika nafasi ya tatu wakiachwa nyuma na Bayern kwa tofauti ya pointi tatu.

The post Majeruhi Kane hali si tete first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/30/majeruhi-kane-hali-si-tete/feed/ 0
Kane apagawa, mechi 43 mabao 43 https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/kane-apagawa-mechi-43-mabao-43/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/kane-apagawa-mechi-43-mabao-43/#respond Wed, 01 May 2024 20:03:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10815 Munich, UjerumaniMshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Kane amepagawa baada ya jana Jumanne kuweka rekodi ya kuifungia timu hiyo bao la 43 katika mechi ya 43 wakati wakitoka sare ya 2-2 na Real Madrid katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.Kane, pia amefunga bao lake la 11 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, rekodi ambayo ni […]

The post Kane apagawa, mechi 43 mabao 43 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Mshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Kane amepagawa baada ya jana Jumanne kuweka rekodi ya kuifungia timu hiyo bao la 43 katika mechi ya 43 wakati wakitoka sare ya 2-2 na Real Madrid katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kane, pia amefunga bao lake la 11 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, rekodi ambayo ni nzuri kwa mchezaji wa England na sasa amejawa matumaini akisubiri kwa hamu kubeba taji kubwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza.
Msimu huu wa kwanza kwa Kane mambo yangekuwa mazuri zaidi kwake binafsi baada ya kuonesha umahiri wa kuzifumania nyavu lakini tayari timu yake imeshapoteza taji la Ligi Kuu Ujeumani au Bundesliga ambalo limebebwa na Bayer Leverkusen.
Leverkusen wametibua rekodi ya Bayern ambao walikuwa wakiwania kulibeba taji hilo kwa mara ya 12 mfululizo na hivyo rekodi yao sasa inabaki ya kulibeba taji hilo mara 11 mfululizo.
“Msimu huu ni mzuri hadi sasa, kila kitu ambacho tumekuwa tukikipigania mwaka huu katika mashindano kimekuwa kigumu, sasa tunalazimika kwenda kwenye mechi ya marudiano Bernabeu tukiwa kamili wenye kujiamini,” alisema Kane.

“Niko hapa kwa miaka mingi, si mwaka mmoja na mwaka mwingine kuondoka, ni kweli mwanzoni mwa msimu matarajio yalikuwa ni kushinda mataji, Ligi ya Mabingwa ndilo taji kubwa kama tukiliweka taji hilo katika mikono yetu, hakika msimu utakuwa wa kipekee,” alisema Kane.


Sare ya Real Madrid, imempa Kane ambaye pia ni nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya England, imani kwamba Bayern inaweza kufika mbali na kulibeba taji hilo kubwa huku akisisitiza kwamba mechi kubwa kama hizo ndizo zilizomfanya aende Bayern.
“Hizi ni mechi kubwa, mazingira ya kuvutia, hii ndiyo sababu hasa nimekuja hapa, ninataka kucheza mechi hizi kubwa, kuwa katika matukio makubwa,” alisema Kane mshambuliaji wa zamani wa Tottenham.
Mechi ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya leo Jumatano
Borussia Dortmund v PSG

The post Kane apagawa, mechi 43 mabao 43 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/kane-apagawa-mechi-43-mabao-43/feed/ 0
Tuchel aifuta Bayern mbio za ubingwa https://www.greensports.co.tz/2024/03/31/tuchel-aifuta-bayern-mbio-za-ubingwa/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/31/tuchel-aifuta-bayern-mbio-za-ubingwa/#respond Sun, 31 Mar 2024 12:09:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10461 Munich, UjerumaniKocha wa Bayern Munich, Thomas Tuchel ametangaza rasmi kuitoa timu yake katika mbio za kuliwania taji la Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga msimu huu baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Borussia Dortmund.Bayern ikiwa nyumbani Munich jana Jumamosi ilikumbana na kichapo hicho matokeo ambayo yanaifanya kuwa nyuma ya vinara wa ligi hiyo, Bayern Leverkusen kwa […]

The post Tuchel aifuta Bayern mbio za ubingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Kocha wa Bayern Munich, Thomas Tuchel ametangaza rasmi kuitoa timu yake katika mbio za kuliwania taji la Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga msimu huu baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Borussia Dortmund.
Bayern ikiwa nyumbani Munich jana Jumamosi ilikumbana na kichapo hicho matokeo ambayo yanaifanya kuwa nyuma ya vinara wa ligi hiyo, Bayern Leverkusen kwa tofauti ya pointi 13.
Leverkusen inayonolewa na kocha Xabi Alonso ambaye ametangaza kuendelea kubaki na timu hiyo licha ya kutakiwa Liverpool, yenyewe ilitoka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Hoffenheim.
Alipoulizwa kama Bayern imetoka moja kwa moja katika mbio za kusaka taji hilo, Tuchel ambaye anasubiri msimu huu uishe aondoke katika nafasi hiyo alijibu, ‘ndio, hilo ni dhahiri.

“Baada ya mechi ya leo (jana Jumamosi) hakuna sababu tena ya kuhesabu pointi, ni pointi ngapi kwa sasa, hapana, hongera kwa Leverkusen,” alisema Tuchel.


Kwa Dortmund ushindi huo dhidi ya Bayern unakuwa ni wa kwanza baada ya miaka takriban 10 lakini pia umefufua matumaini ya timu hiyo kumaliza ligi ikiwa kwenye top four.
Alonso sasa anahitaji kuiwezesha Leverkusen kushinda mechi tatu kati ya saba zilizobaki kabla ya kumalizika kwa msimu huu ili timu hiyo itangazwe kinara wa taji la Bundesliga na hivyo kufuta ubabe wa Bayern iliyokuwa ikiwania kulibeba taji hilo kwa mwaka wa 12 mfululizo.
Matokeo ya mechi za Bundesliga Jumamosi…
B Leverkusen 2-1 Hoffenheim
Bayern Munich 0-2 B Dortmund
B Mgladbach 0-3 Freiburg
Frankfurt 0-0 Union Berlin
RB Leipzig 0-0 Mainz
Werder Bremen 0-2 Wolfsburg

The post Tuchel aifuta Bayern mbio za ubingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/31/tuchel-aifuta-bayern-mbio-za-ubingwa/feed/ 0
Mambo si mambo Bayern Munich https://www.greensports.co.tz/2024/02/19/mambo-si-mambo-bayern-munich/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/19/mambo-si-mambo-bayern-munich/#respond Mon, 19 Feb 2024 07:09:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9801 Munich, UjerumaniMambo si mambo katika klabu ya Bayern Munich ambayo imeendelea kuyumba katika Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga kwa kupoteza mchezo wa tatu mfululizo katika siku zisizozidi tisa.Kipigo cha jana Jumapili cha mabao 3-2 mbele ya VfL Bochum ni mwendelezo wa matokeo yasiyo ya kuridhisha kwa timu hiyo kongwe na yenye historia ya kuvutia licha […]

The post Mambo si mambo Bayern Munich first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Mambo si mambo katika klabu ya Bayern Munich ambayo imeendelea kuyumba katika Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga kwa kupoteza mchezo wa tatu mfululizo katika siku zisizozidi tisa.
Kipigo cha jana Jumapili cha mabao 3-2 mbele ya VfL Bochum ni mwendelezo wa matokeo yasiyo ya kuridhisha kwa timu hiyo kongwe na yenye historia ya kuvutia licha ya kocha Thomas Tuchel kudai kwamba wana uwezo wa kubadili mambo.
Katika mechi na Bochum, nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya England, Harry Kane ambaye nyota yake ya mabao imeendelea kuonekana katika timu hiyo, alifunga bao lakini hakuweza kuiokoa timu yake na janga la kupoteza pointi tatu.
Bayern walikuwa kwanza kupata bao lililofungwa na Jamal Musiala dakika ya 14 lakini Bochum walijibu mapigo kwa kufunga mabao mawili ya Takuma Asano na Keven Schlotterbeck katika dakika za 38 na 44.
Bochum waliongeza bao la tatu dakika ya 78 lililofungwa na Kevin Stoger kwa penalti na dakika ya 87 Kane alifunga bao la pili kwa Bayern ambalo ni bao la 25 kwake, bao ambalo liliongeza idadi ya mabao aliyofunga lakini majanga ya Bayern yaliendelea kuwa vile vile.
Mara ya mwisho Bayern kupoteza mechi tatu mfululizo ilikuwa Mei 2015 wakati timu hiyo ikinolewa na kocha wa sasa wa Man City, Pep Guardiola na sasa chini ya Thomas Tuchel (pichani juu) hali hiyo imejirudia katika namna mbaya.
Mwenendo wa timu katika mechi na Bochum haukuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo, walikosa uvumilivu na kuanza kurusha mipira ya tenisi uwanjani na wakati mwingine kumlazimisha mwamuzi asimamishe mchezo.
Bayern wamekuwa vinara wa Bundesliga kwa misimu 11 iliyopita lakini msimu huu wanaonekana kuwa na mtihani mgumu kufanikisha jambo hilo na kibaya zaidi huenda wakamaliza msimu bila taji.
Timu hiyo tayari imeharibu kwenye German Super Cup kama ilivyo kwenye German Cup na hali pia si nzuri kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, tayari imelala kwa bao 1-0 mbele ya Lazio katika mechi yake ya kwanza ya hatua ya 16 bora.
Tuchel, kocha wa zamani wa Chelsea anauona ugumu wa kubeba taji la Bundesliga msimu huu lakini hapo hapo anadai kuwa wakijiamini wanaweza kufanya kweli kama ilivyokuwa msimu uliopita juhudi zao zilivyowalipa kwa hiyo na msimu huu wataendelea kupambana.
Katika Bundesliga Bayern inashika nafasi ya pili ikiwa imeachwa kwa tofauti ya pointi nane na vinara wa ligi hiyo, Bayer Leverkusen lakini pia inafukuziwa na Stuttgart inayoshika nafasi ya tatu ikiwa imetanguliwa na Bayern kwa tofauti ya pointi nne, timu zote hizo zimecheza mechi 22.
Matokeo ya mechi za Bundesliga jana Jumapili
VfL Bochum 3-2 Bayern Munich
Freiburg 3-3 Frankfurt

The post Mambo si mambo Bayern Munich first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/19/mambo-si-mambo-bayern-munich/feed/ 0
Kane aanza kutupia Bundesliga https://www.greensports.co.tz/2023/08/19/kane-aanza-kutupia-bundesliga/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/19/kane-aanza-kutupia-bundesliga/#respond Sat, 19 Aug 2023 18:58:30 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7447 Bremen, UjerumaniNahodha wa England, Harry Kane kwa mara ya kwanza jana Ijumaa aliifungia bao timu yake mpya ya Bayern Munich iliyoipata ushindi wa 4-1 dhidi ya Werder Bremen katika mechi ya Ligi ya Bundesliga.Kane aliyejiunga na timu hiyo hivi karibuni kwa ada ya Pauni 86.4 milioni akitokea, Tottenham, alifunga bao hilo dakika ya 74 kwa […]

The post Kane aanza kutupia Bundesliga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Bremen, Ujerumani
Nahodha wa England, Harry Kane kwa mara ya kwanza jana Ijumaa aliifungia bao timu yake mpya ya Bayern Munich iliyoipata ushindi wa 4-1 dhidi ya Werder Bremen katika mechi ya Ligi ya Bundesliga.
Kane aliyejiunga na timu hiyo hivi karibuni kwa ada ya Pauni 86.4 milioni akitokea, Tottenham, alifunga bao hilo dakika ya 74 kwa shuti hafifu la mguu wa kulia la umbali wa mita 15 lililomsinda kipa wa Bremen, Jin Pavlenka.
Bao hilo la Kane lilikuwa la pili na kabla ya hapo ndiye aliyetoa pasi kwa Leroy Sane iliyozaa bao la kwanza mapema katika dakika ya nne ya mchezo.
Mabao mengine mawili ya Bayern yalipatikana katika dakika nne za nyongeza, la kwanza likifungwa na Sane kwa mara nyingine na la mwisho likifungwa na Mathys Tel.

“Nilikuwa mwenye hali ya wasiwasi na hapo hapo furaha ya kucheza mechi hii, tulianza vizuri na kupata goli katika dakika chache za awali, hakika kulikuwa na hali tete kidogo lakini wakati wote ninapokuwa uwanjani, fikra sahihi huchukua nafasi yake,” alisema Kane.


Kane alijikuta akiwa mjadala baada ya kucheza mechi yake ya kwanza na timu hiyo lakini akashindwa kuisaidia ilipokutana na kipigo cha mabao 3-0 mbele ya RB Leipzig katika mechi ya Super Cup Ujerumani.
Bayern inaamini Kane anaweza kuwa mabadala wa mpachika mabao wao mahiri, Robert Lewandowski aliyehamia Barcelona wiki kadhaa kabla ya kuanza kwa msimu uliopita wa 2022-23.

The post Kane aanza kutupia Bundesliga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/19/kane-aanza-kutupia-bundesliga/feed/ 0
Kane asubiriwa kwa hamu Bayern https://www.greensports.co.tz/2023/08/11/kane-asubiriwa-kwa-hamu-bayern/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/11/kane-asubiriwa-kwa-hamu-bayern/#respond Fri, 11 Aug 2023 06:54:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7332 Munich, UjerumaniMshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane anasuburiwa kwa hamu katika klabu ya Bayern Munich baada ya klabu hizo mbili kufikia makubaliano ya kuuziana mchezaji huyo na leo Ijumaa huenda akafanyiwa vipimo vya afya.Spurs hatimaye imekubali kumuuza mshambuliaji wao huyo tegemeo kwa ada inayodaiwa kufikia Pauni 86.4 milioni na mkataba wa miaka minne baada ya […]

The post Kane asubiriwa kwa hamu Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane anasuburiwa kwa hamu katika klabu ya Bayern Munich baada ya klabu hizo mbili kufikia makubaliano ya kuuziana mchezaji huyo na leo Ijumaa huenda akafanyiwa vipimo vya afya.
Spurs hatimaye imekubali kumuuza mshambuliaji wao huyo tegemeo kwa ada inayodaiwa kufikia Pauni 86.4 milioni na mkataba wa miaka minne baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya klabu hizo mbili.
Bayern inafurahia ujio wa Kane kwa imani kwamba atakuwa suluhisho la safu ya ushambuliaji ya timu hiyo iliyoonekana kuyumba tangu kuondoka kwa Roberto Lewandowski aliyejiunga na Barca.
Msimu uliopita wa 2022-23, Bayern bila Lewandowski ilishindwa kutamba Ulaya na inaamini inahitaji kuimarisha safu yake ya ushambuliaji huku Kane akiaminiwa kuwa ataipa nguvu safu hiyo na kuipa mafanikio Bayern hasa Ulaya.
Awali Spurs walionekana kuwa wagumu kumuachia mshambuliaji huyo wakitarajia kupiga pesa ndefu lakini Kane mwenyewe alishaweka wazi msimamo wake wa kutaka kuihama Spurs huku Bayern ikiwa chaguo lake la kwanza licha ya kuwindwa na klabu za Man United na PSG.
Wakati mjadala baina ya klabu hizo ukiendelea, kocha wa Bayern, Thomas Tuchel alimfanya Kane kuwa chaguo lake la kwanza na angejiona ameumizwa kwa kumkosa mshambuliaji huyo.
Kane ambaye amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake na Spurs, anaondoka katika timu hiyo akiwa na rekodi ya kuifungia mabao 280 katika mechi 435 na ndiye mfungaji bora wa wakati wote katika historia ya Spurs.

The post Kane asubiriwa kwa hamu Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/11/kane-asubiriwa-kwa-hamu-bayern/feed/ 0
Bayern yamkomalia Harry Kane https://www.greensports.co.tz/2023/07/04/bayern-yamkomalia-harry-kane/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/04/bayern-yamkomalia-harry-kane/#respond Tue, 04 Jul 2023 19:30:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6816 Munich, UjerumaniKlabu ya Bayern Munich imeendelea kukomaa katika mbio za kuisaka saini ya mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane baada ya kuwasilisha ofa nyingine kwa mara ya pili.Kane mwenye umri wa miaka 29 tayari amebainisha wazi kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo ili kusaka changamoto kwingineko na tayari timu nne zimeingia katika mbio za kumsaka […]

The post Bayern yamkomalia Harry Kane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Klabu ya Bayern Munich imeendelea kukomaa katika mbio za kuisaka saini ya mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane baada ya kuwasilisha ofa nyingine kwa mara ya pili.
Kane mwenye umri wa miaka 29 tayari amebainisha wazi kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo ili kusaka changamoto kwingineko na tayari timu nne zimeingia katika mbio za kumsaka mshambuliaji huyo.
Man United ilikuwa ya kwanza ingawa baadaye ilitangaza kujitoa na kuziacha timu za PSG, Real Madrid na Bayern ambayo inaonekana kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inampata Kane.
Vigogo wa klabu ya Bayern wanadaiwa kutofurahishwa na mwenendo wa timu yao msimu wa 2022-23 ulioisha hivi karibuni na wanaamini ipo haja ya kuiimarisha safu ya ushambuliaji na Kane anaonekana kuwa mtu sahihi katika eneo hilo.
Tangu Robert Lewandowski aihame Bayern na kujiunga na Barcelona, vigogo wa klabu hiyo ya nchini Ujerumani wanaamini walipoteza mtu muhimu katika safu ya ushambuliaji na sasa akili yao ipo kwa Kane lakini Spurs wanadaiwa kuwa wagumu kumuachia kirahisi mshambuliaji huyo.
Klabu za PSG na Real Madrid nazo zinadaiwa kufuatilia taratibu mbio za Bayern kabla ya kuamua nini cha kufanya kwani tangu zihusishwe na mpango wa kumtaka mshambuliaji huyo hakuna iliyotangaza kujitoa katika mbio hizo zaidi ya Man United.

The post Bayern yamkomalia Harry Kane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/04/bayern-yamkomalia-harry-kane/feed/ 0
Kane aitaka Bayern Munich https://www.greensports.co.tz/2023/06/28/kane-aitaka-bayern-munich/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/28/kane-aitaka-bayern-munich/#respond Wed, 28 Jun 2023 17:39:40 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6744 London, EnglandMshambuliaji wa Tottenham Hotspur na timu ya Taifa ya England, Harry Kane (pichani) ameamua kuweka wazi kwamba anataka kujiunga na klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani.Awali Kane alikuwa akitajwa kuwindwa na timu nne za PSG, Man United, Real Madrid pamoja na Bayern ambayo mwenyewe ametangaza kuitaka ingawa Man United imeshatangaza kutomtaka tena.Mpango wa Kane […]

The post Kane aitaka Bayern Munich first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur na timu ya Taifa ya England, Harry Kane (pichani) ameamua kuweka wazi kwamba anataka kujiunga na klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani.
Awali Kane alikuwa akitajwa kuwindwa na timu nne za PSG, Man United, Real Madrid pamoja na Bayern ambayo mwenyewe ametangaza kuitaka ingawa Man United imeshatangaza kutomtaka tena.
Mpango wa Kane kwenda Bayern hata hivyo unatatizwa na ofa ya klabu hiyo ambayo ni ndogo na huenda ikakataliwa na Spurs ambayo inataka ilipwe kuanzia Dola 100 milioni.
Habari za ndani zinadai kwamba Bayern ipo tayari kutoa Dola 70 milioni kwa ajili ya kumpata mchezaji huyo ambaye pia ni nahodha wa timu ya Taifa ya England.
Kane ambaye mkataba wake na Spurs unafikia ukomo mwishoni mwa msimu ujao, amewahi kukiri kwamba yuko tayari kuihama timu hiyo na kwenda kusaka changamoto mpya kwingineko barani Ulaya.
Na ingawa Kane ametangaza kuitaka Bayern lakini hali hiyo haiwezi kuzitoa timu za PSG na Real Madrid katika mbio za kumsaka mchezaji huyo.

The post Kane aitaka Bayern Munich first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/28/kane-aitaka-bayern-munich/feed/ 0
Bayern yabeba taji, CEO afutwa kazi https://www.greensports.co.tz/2023/05/27/bayern-yabeba-taji-ceo-afutwa-kazi/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/27/bayern-yabeba-taji-ceo-afutwa-kazi/#respond Sat, 27 May 2023 20:50:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6338 Munich, UjerumaniDakika chache baada ya Bayern Munich kutwaa taji la Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga leo Jumamosi ikiwa ni mara ya 11 mfululizo, klabu hiyo imemfuta kazi Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO). Oliver Kahn.Sambamba na Kahn ambaye ni kipa wa zamani wa Bayern aliyejipatia umaarufu na timu hiyo, kiongozi mwingine aliyefutwa kazi hapo hapo ni mkurugenzi […]

The post Bayern yabeba taji, CEO afutwa kazi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Dakika chache baada ya Bayern Munich kutwaa taji la Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga leo Jumamosi ikiwa ni mara ya 11 mfululizo, klabu hiyo imemfuta kazi Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO). Oliver Kahn.
Sambamba na Kahn ambaye ni kipa wa zamani wa Bayern aliyejipatia umaarufu na timu hiyo, kiongozi mwingine aliyefutwa kazi hapo hapo ni mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Hasan Salihamidzic.
Kahn (pichani) aliteuliwa kuwa CEO wa Bayern mwaka 2021 akichukua nafasi ya Karl-Heinz Rummenigge na baada tu ya kutimuliwa hii leo, Jan-Christian Dreesen alitangazwa hapo hapo kuwa CEO mpya. Ilieleza taarifa ya klabu hiyo.
“Ulikuwa uamuzi mgumu wa kuachana na Oliver lakini tulifikia hitimisho hilo kwa kuzingatia mpango mzima wa maendeleo na kufanya mabadiliko ya nafasi za maofisa kwenye bodi,” ilifafanua taarifa hiyo.
Bayern leo imecheza na FC Cologne na kuichapa mabao 2-1 ikiokolewa na bao la dakika ya 89 mfungaji akiwa Jamal Musiala lakini pia matokeo ya sare ya mabao 2-2 iliyoyapata Borussia Dortmund ndiyo yaliyoifanya Bayern ibebe taji kwa tofauti ya mabao.
Msimu huu haukuwa mzuri kwa Bayern ambayo imetolewa kwenye michuano ya Kombe la Ujerumani na Ligi ya Mabingwa Ulaya, yote katika hatua ya robo fainali licha ya kumtimua kocha Julian Nagelsmann na nafasi yake kuchukuliwa na Thomas Tuchel.
Akizungumzia kutimuliwa kwake Kahn alitumia mtandao wa Twitter kuipongeza timu na baada ya hapo akasema, “nilipenda kusherehekea ubingwa na wachezaji lakini bahati mbaya sijaweza, siwezi kuwa nao leo kwa sababu sikuruhusiwa.”

“Haukuwa msimu ambao tunaweza kuufurahia, haukuwa msimu ambao idadi ya pointi zimetosha kwa mahitaji yetu, ni msimu ambao kiwango cha uchezaji wetu kilitutosha sisi tu, vyovyote ilivyokuwa mwisho wa siku haukuwa msimu wa kuridhisha hata kidogo,” alisema Kahn.


The post Bayern yabeba taji, CEO afutwa kazi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/27/bayern-yabeba-taji-ceo-afutwa-kazi/feed/ 0
Sadio Mane aziingiza vitani Man Utd, Newcastle https://www.greensports.co.tz/2023/05/19/sadio-mane-aziingiza-vitani-man-utd-newcastle/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/19/sadio-mane-aziingiza-vitani-man-utd-newcastle/#respond Fri, 19 May 2023 08:08:30 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6210 London, EnglandKlabu za Newcastle na Man United zimeingia vitani kila moja ikiwania kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich, Sadio Mane (pichani) ambaye mambo yake si mazuri katika klabu hiyo.Mane mwenye umri wa miaka 31, msimu uliopita alitamba na Liverpool na ndiye aliyeiwezesha timu ya Senegal kutwaa taji la Mataifa ya Afrika, tangu atue Bayern msimu huu […]

The post Sadio Mane aziingiza vitani Man Utd, Newcastle first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Klabu za Newcastle na Man United zimeingia vitani kila moja ikiwania kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich, Sadio Mane (pichani) ambaye mambo yake si mazuri katika klabu hiyo.
Mane mwenye umri wa miaka 31, msimu uliopita alitamba na Liverpool na ndiye aliyeiwezesha timu ya Senegal kutwaa taji la Mataifa ya Afrika, tangu atue Bayern msimu huu amekuwa na wakati mgumu.
Kasi yake ya upachikaji mabao iliyozoeleka inaonekana kupotea huku akiandamwa na majanga ya hapa na pale ikiwamo tukio la hivi karibuni la kumpiga ngumi mchezaji mwenzake, Leroy Sane.
Baada ya tukio hilo lililotokea kwenye mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Man City na Bayern kulala kwa mabao 3-0, Bayern ilimsimamisha Mane na akakosa mechi moja.
Baada ya tukio hilo habari mpya zilianza kuibuka kwamba Bayern inajiandaa kumpiga bei na sasa Man United na Newcastle zimeonekana kuwa mstari wa mbele kila moja ikiitaka saini ya mchezaji huyo.
Man United na Newcastle zote zipo vizuri kwenye Ligi Kuu England (EPL) katika kupigania nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao hivyo kama kigezo cha Mane kitakuwa na michuano hiyo, atakuwa huru kuchagua mojawapo ya timu hizo.
Katika EPL, Newcastle inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 69 katika mechi 36 wakati Man United inashika nafasi ya nne baada ya kucheza mechi 35.

The post Sadio Mane aziingiza vitani Man Utd, Newcastle first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/19/sadio-mane-aziingiza-vitani-man-utd-newcastle/feed/ 0