Barca - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 05 Nov 2025 08:17:14 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Barca - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Real yailaza Barca, Vini Jr, Yamal wazozana https://www.greensports.co.tz/2025/10/26/real-yailaza-barca-vini-jr-yamal-wazozana/ https://www.greensports.co.tz/2025/10/26/real-yailaza-barca-vini-jr-yamal-wazozana/#respond Sun, 26 Oct 2025 19:57:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14039 Madrid, HispaniaReal Madrid imetoka kifua mbele dhidi ya mahasimu wao Barcelona kwa kuwachapa mabao 2-1, leo Jumapili Oktoba 26, 2025, mechi ambayo baada ya dakika 90 ilitawaliwa na mzozo wa wachezaji Lamine Yamal na Vinicius Junior au Vini Jr.Real Madrid wakiwa nyumbani Santiago Bernabeu, walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Kylian Mbappe kwa pasi […]

The post Real yailaza Barca, Vini Jr, Yamal wazozana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Real Madrid imetoka kifua mbele dhidi ya mahasimu wao Barcelona kwa kuwachapa mabao 2-1, leo Jumapili Oktoba 26, 2025, mechi ambayo baada ya dakika 90 ilitawaliwa na mzozo wa wachezaji Lamine Yamal na Vinicius Junior au Vini Jr.
Real Madrid wakiwa nyumbani Santiago Bernabeu, walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Kylian Mbappe kwa pasi ya Jude Bellingham ambaye aliivuruga safu ya ulinzi ya Barca kabla ya kutoa pasi iliyozaa bao hilo.
Barca walikuja juu na kusawazisha bao hilo dakika ya 38 kwa bao la Fermín López ambaye aliitumia pasi ya Marcus Rashford, mshambuliaji wa Man United anayeichezea Barca kwa mkopo.
Dakika mbili kabla ya mapumziko, Jude Bellingham aliipatia Real bao la pili na la ushindi baada ya kuinasa pasi ya Éder Milita.
Real walionesha kila dalili za kutoka na ushindi katika mechi hiyo, dakika ya pili tu ya mchezo, Vini Jr aliangushwa ndani ya eneo la penalti na mwamuzi kuipa Real penalti lakini ilifutwa baada ya mapitio ya VAR.
Picha ya VAR ilibaini kwamba kabla ya kuanguka, Vini Jr alimkwatua Lamine Yamal mgunni na hivyo maamuzi hayo kubadilishwa.
Ushindi huo ni hatua nzuri kwa Real kwani ni kama vile imefuta uteja baada ya kufungwa na Barca katika mechi zote nne za msimu uliopita.
Nje ya matokeo hayo ambayo yanaifanya Real kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa La Liga, tukio la Yamal na Vini Jr limeendelea kuteka hisia za mashabiki wa timu hizo mbili.
Tukio hilo lililotokea baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya kumaliza mchezo liliibuka kwa kinachoaminika kuwa ni vita ya maneno baina ya wachezaji hao tegemeo kwa timu zote.

Awali mzozo ulianza kati ya Yamal na Dani Carvajal kubadilishana kauli za hasira lakini wakati Yamal akielekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, Vini Jr ni kama aliuwasha moto upya kwa kumvaa Yamal kwa maneno.
Vini alianza kwa kumwambia Yamal kuwa ni mchezaji mwenye kutoa pasi za kisigino tu kabla ya kuongeza kwa kumwambia kuwa anaongea sana na kumtaka aongee baada ya matokeo hayo.
Kauli ya Vini Jr inaaminika kutokana na alichokisema Yamal kabla ya mechi hiyo kwamba Real wana tabia ya kufanya matukio ya kudanganya katika mechi zao.
Kauli za Yamal ni kama vile zilipuuzwa na wachezaji wa Real ingawa hali ilikuwa tofauti kwa mashabiki ambao kwa muda mwingi walikuwa wakimzomea mchezaji huyo.

The post Real yailaza Barca, Vini Jr, Yamal wazozana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/10/26/real-yailaza-barca-vini-jr-yamal-wazozana/feed/ 0
Dogo Barca aanza kwa neema https://www.greensports.co.tz/2023/10/23/dogo-barca-aanza-kwa-neema/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/23/dogo-barca-aanza-kwa-neema/#respond Mon, 23 Oct 2023 06:30:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8185 Barcelona, HispaniaMshambuliaji nyota mpya wa Barca, Marc Guiu ambaye ndio kwanza ana miaka 17, amecheza mechi yake ya kwanza ya La Liga na timu hiyo na kufunga bao pekee na la ushinid dhidi ya Athletic Bilbao.Giui (pichani juu) aliingia akitokea benchi katika dakika ya 79 kuchukua nafasi ya kinda mwenzake, Fermina Lopez na ilimchukua sekunde […]

The post Dogo Barca aanza kwa neema first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Mshambuliaji nyota mpya wa Barca, Marc Guiu ambaye ndio kwanza ana miaka 17, amecheza mechi yake ya kwanza ya La Liga na timu hiyo na kufunga bao pekee na la ushinid dhidi ya Athletic Bilbao.
Giui (pichani juu) aliingia akitokea benchi katika dakika ya 79 kuchukua nafasi ya kinda mwenzake, Fermina Lopez na ilimchukua sekunde 33 kuipatia timu yake bao mara baada ya kuingia uwanjani.
Kwa bao hilo, Giui anakuwa amejiwekea rekodi ya kufunga bao la haraka na la kwanza katika historia ya timu hiyo kufungwa na mchezaji ambaye ndio kwanza anacheza mechi yake ya kwanza na timu hiyo.
Ushindi huo mwembamba wa jana Jumapili umeiweka Barca katika nafasi nzuri ya kuwafukuzia vinara na mahasimu wao Real Madrid kwani kwa sasa tofauti baina yao ni pointi moja na Jumamosi ijayo wataumana nao.

“Nilimwambia kwamba atakuwa na nafasi moja nzuri, napenda kuona sura za madogo hawa, hawana woga,” alisema kocha wa Barca, Xavi.


Xavi alichukua uamuzi wa kumpandisha Giui kikosi cha kwanza kama sehemu ya mkakati wake wa kukabiliana na janga la wachezaji majeruhi linalomkabili wakiwamo Robert Lewandowski na Frenkie de Jong.
Giui alijiunga na akademi ya Barca maarufu La Masia mwaka 2013, La Masia ni kituo maarufu duniani ambapo pia alipitia nyota wa zamani wa timu hiyo, Lionel Messi ambaye kwa sasa anaichezea Inter Miami FC ya Marekani.
Mastaa wengine waliopitia La Masia na kutamba katika klabu hiyo ni kocha Xavi mwenyewe, Andres Iniesta, Carles Puyol, Gerard Pique, Jordi Alba, Sergio Busquets, Cesc Fabregas (baadaye alihamia Arsenal) na wengineo.

The post Dogo Barca aanza kwa neema first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/23/dogo-barca-aanza-kwa-neema/feed/ 0
Kashfa ya Barca kuhonga waamuzi yachukua sura mpya https://www.greensports.co.tz/2023/09/28/kashfa-ya-barca-kuhonga-waamuzi-yachukua-sura-mpya/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/28/kashfa-ya-barca-kuhonga-waamuzi-yachukua-sura-mpya/#respond Thu, 28 Sep 2023 19:51:19 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7881 Madrid, HispaniaTuhuma za klabu ya Barcelona kutoa rushwa kwa waamuzi zimechukua sura mpya baada ya polisi nchini Hispania kuvamia ofisi ya kamati ya waamuzi kama sehemu ya uchunguzi wa kashfa hiyo.Barcelona au Barca inakabiliwa na kashfa ya kutoa malipo yanayotiliwa shaka kwa makamu mwenyekiti wa zamani wa kamati ya waamuzi, Jose Maria Negreira ili kuibeba […]

The post Kashfa ya Barca kuhonga waamuzi yachukua sura mpya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Tuhuma za klabu ya Barcelona kutoa rushwa kwa waamuzi zimechukua sura mpya baada ya polisi nchini Hispania kuvamia ofisi ya kamati ya waamuzi kama sehemu ya uchunguzi wa kashfa hiyo.
Barcelona au Barca inakabiliwa na kashfa ya kutoa malipo yanayotiliwa shaka kwa makamu mwenyekiti wa zamani wa kamati ya waamuzi, Jose Maria Negreira ili kuibeba timu hiyo katika mechi zake.
Barca hata hivyo imekana kufanya kosa lolote na ingawa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa baada ya polisi kuvamia ofisi hizo zilizopo mjini Madrid, Umoja wa Vyama vya Soka Ulaya (Uefa) nao unaifanyia uchunguzi kadhia hiyo.
Awali tuhuma dhidi ya Barca ziliwalishwa na ofisi ya waendesha mashtaka ya Barcelona mwezi Machi mwaka huu na siku kadhaa baadaye, Uefa nao wakatangaza kuanza uchunguzi wao.
Katika madai hayo, Barca wanatuhumiwa kumlipa Negreira Pauni 7.4 milioni kati ya mwaka 2016 na 2018 kupitia kampuni yake ya Dasnil 95, malipo ambayo uchunguzi wa awali uliyahusisha na ukwepaji wa kodi wa kampuni hiyo inayoongozwa na Negreira.
Barca hata hivyo ilikiri kutoa malipo hayo kwenye kampuni ya Dasnil 95 lakini ilidai kwamba malipo hayo yalikuwa ni kwa ajili ya kuandika ripoti maalum ya waamuzi kwa njia ya video, ripoti ambayo iliombwa na benchi la ufundi la klabu hiyo.
Katika ufafanuzi wake klabu hiyo ilidai kwamba malipo kwa ajili ya ripoti za aina hiyo ni jambo la kawaida kufanywa na klabu profesheno.

The post Kashfa ya Barca kuhonga waamuzi yachukua sura mpya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/28/kashfa-ya-barca-kuhonga-waamuzi-yachukua-sura-mpya/feed/ 0
Barca yajitosa, yamtaka Haaland https://www.greensports.co.tz/2023/09/13/barca-yajitosa-yamtaka-haaland/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/13/barca-yajitosa-yamtaka-haaland/#respond Wed, 13 Sep 2023 06:38:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7738 Manchester, EnglandKlabu ya Barcelona ya Hispania imejitosa ikitaka kumsajili mshambuliaji wa Man City, Erling Haaland ikiamini kwamba inaweza kumpata kwa ada ya Pauni 150 milioni.Chanzo kimoja cha habari kimeripoti kuwa Barca inapiga hesabu za kumpata mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 mwaka 2025 wakiamini ataweza kupatikana kwa thamani hiyo.Barca hata hivyo ni lazima ijiandae […]

The post Barca yajitosa, yamtaka Haaland first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Klabu ya Barcelona ya Hispania imejitosa ikitaka kumsajili mshambuliaji wa Man City, Erling Haaland ikiamini kwamba inaweza kumpata kwa ada ya Pauni 150 milioni.
Chanzo kimoja cha habari kimeripoti kuwa Barca inapiga hesabu za kumpata mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 mwaka 2025 wakiamini ataweza kupatikana kwa thamani hiyo.
Barca hata hivyo ni lazima ijiandae kwa mchuano mkali kama kweli ina nia ya kumsajili mshambuliaji huyo ambaye pia amekuwa akiwindwa kwa muda mrefu na mahasimu wao wa Hispania, Real Madrid.
Real Madrid wameanza muda mrefu mbio za kumsaka Haaland hadi kuibuka habari kwamba klabu hiyo ilikuwa na makubalino maalum ambayo yangemfanya mchezaji huyo baadaye ahamia Real Madrid jambo ambalo hata hivyo kocha wa Man City, Pep Guardiola alilikanusha.
Kwa upande wa Barca, chanzo hicho hakijafafanua kwa undani nini hasa kimeifanya klabu hiyo kujiaminisha kwamba ina ubavu wa kumsajili mshambuliaji huyo ambaye mafanikio yake ya msimu uliopita wa 2022-23 yanatosha kutoa ushawishi kwa klabu yoyote duniani kuitaka saini yake.
Katika msimu huo Haaland alifunga jumla ya mabao 52 katika mechi 53 za michuano mbalimbali na kuiwezesha kwa kiasi kikubwa Man City kuweka rekodi mpya kwa kubeba kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo mataji matatu ya Ligi Kuu England, FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

The post Barca yajitosa, yamtaka Haaland first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/13/barca-yajitosa-yamtaka-haaland/feed/ 0
Barca yaichapa Real Madrid 3-0 https://www.greensports.co.tz/2023/07/31/barca-yaichapa-real-madrid-3-0/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/31/barca-yaichapa-real-madrid-3-0/#respond Mon, 31 Jul 2023 06:09:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7192 Texas, MarekaniBarcelona imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya mahasimu wao Real Madrid katika mechi ya kirafiki ya maandalizi ya msimu iliyopigwa Jumapili hii mjini Texas kwenye Uwanja wa AT&T.Mabao ya washindi katika mechi hiyo yalifungwa na Ousmane Dembele aliyefunga la kwanza yakifuatiwa na mabao mengine mawili ya Fermin Lopez na Ferran Torres.Akizungumzia matokeo […]

The post Barca yaichapa Real Madrid 3-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Texas, Marekani
Barcelona imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya mahasimu wao Real Madrid katika mechi ya kirafiki ya maandalizi ya msimu iliyopigwa Jumapili hii mjini Texas kwenye Uwanja wa AT&T.
Mabao ya washindi katika mechi hiyo yalifungwa na Ousmane Dembele aliyefunga la kwanza yakifuatiwa na mabao mengine mawili ya Fermin Lopez na Ferran Torres.
Akizungumzia matokeo hayo hata hivyo kocha wa Barca, Xavi Hernandez alisema kwa kiasi fulani ni kama yanapotosha ukweli na hivyo amewataka yasiwafanye wachezaji wake wajiamini kwa sana.
“Kwa kiasi fulani matokeo ni kama yanapotosha, hatutakiwi kuwa wenye kujiamini kwa sana, ni matokeo mazuri kwetu lakini hayana maana kwamba tulicheza kwa kiwango bora sana,” alisema Xavi.
Alifafanua zaidi kwa kusema kwamba ni aina ya mechi ambayo ina mambo yaliyokuwa sawa kwa timu zote kwani Madrid nao walitengeneza nafasi nyingi wao (Barca) wana mambo mengi ya kufanya kuboresha timu yao.
Matokeo hayo ni mwendelezo wa mechi nyingine za kirafiki zilizochezwa hapo kabla ambapo, Man United ililala kwa mabao 2-0 mbele ya Real Madrid wakati Arsenal nayo iliichapa Barca mabao 5-3.
Kwa upande wake kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti alisema matokeo ya mechi hiyo si muhimu sana na ingawa inaumiza kufungwa lakini wataendelea na mambo mazuri waliyoyafanya huko nyuma na kuisifu timu yake kwa kutengeneza nafasi nyingi.
Barca watakamilisha ziara hiyo ya mechi za kirafiki Jumanne hii kwa kucheza na AC Milan mjini Lass Vegas wakati siku inayofuata Real Madrid wao watakabiliana na Juventus mjini Orlando.

The post Barca yaichapa Real Madrid 3-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/31/barca-yaichapa-real-madrid-3-0/feed/ 0
Barca ruksa Ligi ya Mabingwa https://www.greensports.co.tz/2023/07/28/barca-ruksa-kushiriki-ligi-ya-mabingwa/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/28/barca-ruksa-kushiriki-ligi-ya-mabingwa/#respond Fri, 28 Jul 2023 05:45:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7170 Barcelona, HispaniaBarcelona hatimaye imeruhusiwa kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2023-24 baada ya kuwapo tishio la kufungiwa na Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) ikituhumiwa kumlipa fedha bosi wa waamuzi.Machi mwaka huu Uefa ilithibitisha kuanza uchunguzi wa madai ya malipo yaliyofanywa na klabu ya Barcelona yaliyohusishwa na mpango wa klabu hiyo kutaka kubebwa na waamuzi […]

The post Barca ruksa Ligi ya Mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Barcelona hatimaye imeruhusiwa kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2023-24 baada ya kuwapo tishio la kufungiwa na Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) ikituhumiwa kumlipa fedha bosi wa waamuzi.
Machi mwaka huu Uefa ilithibitisha kuanza uchunguzi wa madai ya malipo yaliyofanywa na klabu ya Barcelona yaliyohusishwa na mpango wa klabu hiyo kutaka kubebwa na waamuzi katika mechi zao.
Barcelona ambayo ilikana tuhuma hizo, sasa itashiriki michuano hiyo lakini Uefa bado wana haki ya kutoa adhabu yoyote kwa klabu hiyo wakati wowote siku zijazo kama kutakuwa na sababu ya kufanya hivyo.
Uamuzi wa Uefa kufanya uchunguzi wa sakata hilo ulikuja baada ya ofisi ya waendesha mashtaka wa mjini Barcelona kufikishiwa tuhuma hizo za jinai Machi 10 mwaka huu na kuanza kuzifanyia kazi.
Katika tuhuma hizo klabu ya Barcelona inadaiwa kumlipa Pauni 7.4 milioni makamu rais wa zamani wa Kamati ya Waamuzi, Jose Maria Negreira kupitia kampuni yake ya Dasnil 95.
Waendesha mashtaka wa Barcelona baada ya kufikishiwa tuhuma hizo walianza uchunguzi kwa kuwahusisha maofisa kadhaa wa klabu ya Barcelona kwa tuhuma za rushwa, kukosa uaminifu na kufanya biashara isiyo halali.
Katika utetezi wake Barcelona ilikiri kuilipa kampuni ya Dasnil 95 kwa ajili ya ushauri wa kitaalam na lakini si kwa lengo la kutaka kubebwa na waamuzi kama ambavyo imekuwa ikidaiwa.
Kampuni hiyo ilitakiwa kuandaa ripoti ya ufundi inayohusisha waamuzi kupitia mechi mbalimbali ili kulisaidia benchi la ufundi la timu hiyo na kwamba jambo hilo ni la kawaida kwa klabu profesheno.
Sakata hilo lilikuwa kubwa baada ya klabu 18 za La Liga kutoa taarifa zikielezea kuguswa na tuhuma hizo lakini Rais wa Barcelona, Joan Laporta amekuwa akiitetea kwa nguvu zote klabu yake akidai inachafuliwa.

The post Barca ruksa Ligi ya Mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/28/barca-ruksa-kushiriki-ligi-ya-mabingwa/feed/ 0
Dogo wa Brazil asaini Barca https://www.greensports.co.tz/2023/07/13/dogo-wa-brazil-asaini-barca/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/13/dogo-wa-brazil-asaini-barca/#respond Thu, 13 Jul 2023 07:17:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6928 Barcelona, HispaniaKlabu ya Barcelona imemsajili mshambuliaji Vitor Roque (pichani) mwenye umri wa miaka 18 kutoka klabu ya Athletico-PR ya Brazil kwa ada ya Dola 44 milioni na mkataba utakaofikia ukomo msimu wa 2030-31.Roque ambaye atajiunga na miamba hiyo ya Hispania majira ya kiangazi msimu ujao unakuwa ni usajili wa tatu katika klabu hiyo akiwa ametanguliwa […]

The post Dogo wa Brazil asaini Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Klabu ya Barcelona imemsajili mshambuliaji Vitor Roque (pichani) mwenye umri wa miaka 18 kutoka klabu ya Athletico-PR ya Brazil kwa ada ya Dola 44 milioni na mkataba utakaofikia ukomo msimu wa 2030-31.
Roque ambaye atajiunga na miamba hiyo ya Hispania majira ya kiangazi msimu ujao unakuwa ni usajili wa tatu katika klabu hiyo akiwa ametanguliwa na Ilkay Gundogan kutoka Man City na Inigo Martinez aliyekuwa Athletic Bilbao.
Inaaminika kuwa usajili wa Roque ni kama maandalizi ya kumpata msaidizi wa Robert Lewandowski ambaye Agosti atafikisha miaka 35 na hivyo lolote linaweza kumkuta kutokana na umri kuanza kumtupa mkono.
Barca baada ya kubaini kipaji cha Roque ilianza taratibu mazungumzo ya kumsajili, mazungumzo yaliyoongozwa vyema na Deco ambaye kwa sasa ndiye mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo.
Roque alionekana katika mechi kadhaa za Athletico pamoja na timu za vijana za Brazil, aliiwezesha Athletico kufikia hatua ya fainali ya michuano ya Copa Libertadores msimu uliopita na hivi karibuni aliitwa katika kikosi cha wakubwa cha timu ya Taifa ya Brazil.
Katika mechi 65 alizoichezea Athletico, Roque amefunga mabao 22 lakini la kuvutia zaidi ni mabao sita aliyoyafunga katika mechi sita zilizopita jambo ambalo limezidi kudhihirisha ubora wake katika kuzifumania nyavu.
Rais wa Barca, Joan Laporta alimpamba mchezaji huyo kutokana na namna anavyomudu kuitumia vyema miguu yote miwili jambo ambalo linamtofautisha na washambuliaji wengine wa Brazil.
“Ana staili ya kipekee, huwezi kumlinganisha na Ronaldo au Romario (washambuliaji wa zamani wa Brazil) huyu yeye ni mtu hatari kwa miguu yote anapokuwa ndani ya boksi, ni kijana, ana nguvu, na ni Mbrazil,” alisema Laporta.

The post Dogo wa Brazil asaini Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/13/dogo-wa-brazil-asaini-barca/feed/ 0
Gundogan asajiliwa Barca https://www.greensports.co.tz/2023/06/22/gundogan-asajiliwa-barca/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/22/gundogan-asajiliwa-barca/#respond Thu, 22 Jun 2023 14:44:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6678 Manchester, EnglandKlabu ya Barcelona imefikia makubaliano na Manchester City ya kumsajili kiungo Ilkay Gundogan akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake wa sasa kufikia ukomo Juni 30 mwaka huu.Gundogan, nyota wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 32, amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili na Barca ambao una kipengele kinachoiruhusu klabu hiyo kuongeza mwaka wa tatu.Hadi […]

The post Gundogan asajiliwa Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Klabu ya Barcelona imefikia makubaliano na Manchester City ya kumsajili kiungo Ilkay Gundogan akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake wa sasa kufikia ukomo Juni 30 mwaka huu.
Gundogan, nyota wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 32, amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili na Barca ambao una kipengele kinachoiruhusu klabu hiyo kuongeza mwaka wa tatu.
Hadi kukubali kujiunga na Barca, Gundogan amekataa ofa ya kuendelea kuichezea Man City akiwa tayari ameichezea timu hiyo kwa miaka saba, lakini pia amekataa ofa ya Arsenal na klabu za Saudi Arabia.
Machi mwaka huu zilikuwapo habari kwamba Barca ilianza mchakato wa kumsajili mchezaji huyo ikidaiwa kwamba kutokana na kanuni za matumizi ya fedha kuwabana, klabu hiyo imeamua kukimbilia kwa mchezaji huyo ili kumsajili akiwa huru.
Kwa upande wa Man City kulikuwa na ugumu kumruhusu kiungo huyo kuondoka ingawa ilichotaka ni kumpa mkataba wa mwaka mmoja lakini mwenyewe akaamua kuichagua Barca licha ya kocha wa Man City, Pep Guardiola kuonesha nia ya kumbakisha katika timu hiyo.
Kocha wa Barca, Xavi ndiye aliyeongoza mpango wa kumsajili Gundogan ili kuiimarisha timu hiyo hasa baada ya kumkosa Lionel Messi ambaye amejiunga na klabu ya Inter Miami ya Marekani.

The post Gundogan asajiliwa Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/22/gundogan-asajiliwa-barca/feed/ 0
Barca yatwaa taji La Liga https://www.greensports.co.tz/2023/05/15/barca-yatwaa-taji-la-liga/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/15/barca-yatwaa-taji-la-liga/#respond Mon, 15 May 2023 09:21:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6171 Barcelona, HispaniaBarcelona hatimaye imetwaa taji la La Liga msimu wa 2022/23 kwa kishindo baada ya kuichapa Espanyol mabao 4-2 ikilitwaa taji hilo mara ya pili baada ya kufanya hivyo msimu wa 2018-19.Barca imelibeba taji ikiwa na mechi nne mkononi, ina pointi 85 imewazidi mahasimu wao Real Madrid wanaoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi […]

The post Barca yatwaa taji La Liga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Barcelona hatimaye imetwaa taji la La Liga msimu wa 2022/23 kwa kishindo baada ya kuichapa Espanyol mabao 4-2 ikilitwaa taji hilo mara ya pili baada ya kufanya hivyo msimu wa 2018-19.
Barca imelibeba taji ikiwa na mechi nne mkononi, ina pointi 85 imewazidi mahasimu wao Real Madrid wanaoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi 14 ambazo hawawezi kuzifikia kwa mechi zilizobaki.
Vinara hao waliutawala vyema mchezo kuanzia kipindi cha kwanza na kupata bao la kwanza dakika ya 11 lililofungwa na Roberto Lewandowski kabla Balde hajaongeza la pili dakika ya 20.
Lewandowski ambaye amekuwa na ukame wa mabao, aliongeza bao la tatu dakika ya 40 ambalo ni bao lake la 20 na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko Barca ikiwa mbele kwa mabao 3-0.
Dakika nane baada ya kuanza kipindi cha pili, Barca iliandika bao la nne lililofungwa kwa kichwa na Jules Kounde lakini Espanyol walipambana na kupata mabao mawili ya kufutia machozi yaliyofungwa na Javier Puado dakika ya 73 na Joselu katika dakika mbili za nyongeza.
Taji hilo linakuwa la kwanza kwa kocha Xavi ambaye wakati akiichezea Barca anajivunia rekodi ya kubeba taji la La Liga mara nane katika miaka 17 aliyotamba na timu hiyo.
Kwa nahodha Sergio Busquets taji hilo ambalo ni la tisa kwake limempa jambo la kujivunia wakati akiiaga timu hiyo, akihitimisha miaka yake 18 ya mafanikio ndani ya klabu hiyo kwani tayari ametangaza kustaafu baada ya msimu huu.
Kwa upande mwingine Barca kwa sasa inajiandaa kuufanyia marekebisho uwanja wake wa Nou Campo ingawa mashabiki watapata nafasi ya kulifurahia taji hilo kwenye uwanja huo kwenye mechi mbili zilizobaki dhidi ya Real Sociedad na Real Mallorca.
Maatokeo mechi nyingine za La Liga
Espanyol 2-4 Barcelona
Celta Vigo 1-2 Valencia
Elche 1-0 Atl Madrid
Real Valladolid 0-3 Sevilla

The post Barca yatwaa taji La Liga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/15/barca-yatwaa-taji-la-liga/feed/ 0
Busquets ahitimisha miaka 18 Barca https://www.greensports.co.tz/2023/05/10/busquets-ahitimisha-miaka-18-barca/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/10/busquets-ahitimisha-miaka-18-barca/#respond Wed, 10 May 2023 19:47:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6101 Barcelona, HispaniaNahodha, Sergio Busquets hatimaye amethibitisha kuwa ataondoka Barca baada ya msimu huu na hivyo kuhitimisha safari yake ya miaka 18 akiwa na rekodi ya kuichezea timu hiyo mechi 718 hadi sasa.Busquets mwenye umri wa miaka 34 ambaye pia amewahi kutamba na timu ya Taifa ya Hispania, hadi sasa anashika nafasi ya tatu kati ya […]

The post Busquets ahitimisha miaka 18 Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Nahodha, Sergio Busquets hatimaye amethibitisha kuwa ataondoka Barca baada ya msimu huu na hivyo kuhitimisha safari yake ya miaka 18 akiwa na rekodi ya kuichezea timu hiyo mechi 718 hadi sasa.
Busquets mwenye umri wa miaka 34 ambaye pia amewahi kutamba na timu ya Taifa ya Hispania, hadi sasa anashika nafasi ya tatu kati ya wachezaji walioichezea Barca mechi nyingi.
Mchezaji huyo pia anajivunia rekodi ya kubeba mataji manane ya La Liga, saba ya Copa del Rey, saba ya Spanish Super Cup na matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
“Na ingawa haujawa uamuzi rahisi, lakini nafikiri wakati umefika, ni safari isiyosahaulika, nilikuwa wakati wote mwenye ndoto ya kucheza nikiwa na jezi ya timu hii na uwanja huu (Nou Camp), uhalisia umezidi ndoto zangu zote,” alisema Busquets.

“Imekuwa heshima kubwa, ndoto, jambo la kujifaharisha na ilimaanisha kila kitu katika kuilinda na kuiwakilisha nembo ya klabu hii kwa miaka mingi, lakini kila kitu kina mwanzo na lazima kiwe na mwisho, nataka kuwashukuru wote walionisaidia kuliwezesha hili tangu siku ya kwanza hadi ya mwisho,” alisema Busquets.


Historia ya Busquets na Barca inaanzia mwaka 2005 akiwa mchezaji wa timu ya vijana na kupiga hatua hadi Barca B kabla ya kucheza kikosi cha kwanza chini ya kocha Pep Guardiola kwa mara ya kwanza mwaka 2008 katika mechi ya ligi dhidi ya Racing Santander.
Busquets ambaye alikuwa kiungo mkabaji, Desemba mwaka jana alistaafu kuichezea timu ya Taifa ya Hispania akiwa na rekodi ya kubeba Kombe la Dunia mwaka 2010 na lile la Ulaya mwaka 2012.

The post Busquets ahitimisha miaka 18 Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/10/busquets-ahitimisha-miaka-18-barca/feed/ 0