Ajibu - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 01 Jul 2023 19:55:37 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Ajibu - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Ajibu: Woga unawakwaza wachezaji https://www.greensports.co.tz/2023/07/01/ajibu-woga-unawakwaza-wachezaji/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/01/ajibu-woga-unawakwaza-wachezaji/#respond Sat, 01 Jul 2023 19:55:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6790 Na mwandishi wetuKiungo mshambuliaji wa Singida Fountain Gate, Ibrahim Ajibu amesema kinachowafanya wachezaji washindwe kung’ara wanaposajiliwa na timu kubwa za Simba na Yanga ni woga na kutojiamini.Ajibu ameeleza hayo ikiwa ni siku moja imepita tangu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litangaze kufunguliwa kwa dirisha la usajili kuanzia Julai Mosi mpaka Agosti 31, mwaka huu.Kiungo huyo […]

The post Ajibu: Woga unawakwaza wachezaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Singida Fountain Gate, Ibrahim Ajibu amesema kinachowafanya wachezaji washindwe kung’ara wanaposajiliwa na timu kubwa za Simba na Yanga ni woga na kutojiamini.
Ajibu ameeleza hayo ikiwa ni siku moja imepita tangu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litangaze kufunguliwa kwa dirisha la usajili kuanzia Julai Mosi mpaka Agosti 31, mwaka huu.
Kiungo huyo aliyewahi kuwika akiwa Simba na Yanga kwa nyakati tofauti, alisema kinachowavuruga wachezaji wa timu ndogo ni kukutana na wachezaji wenye uzoefu mkubwa wanapotua kwenye klabu kubwa na kongwe nchini, kitu ambacho mara nyingi humaliza ari walizonazo na kuonekana wamefeli.

“Unajua mchezaji akiwa timu ndogo au ya kawaida anaweza kuonekana lakini anapochukuliwa na kwenda timu kubwa changamoto huwa ni uzoefu wa watu anaokutana nao kikosini na kuingiwa woga, sasa kama wataacha woga na kuanza kupambana wanaweza kucheza na kuwika,” alisema Ajibu.


Alisema anafahamu kundi kubwa la wachezaji wengi wazuri wanaishia njiani wanaposajiliwa na timu kubwa lakini hiyo yote inaweza kuzuilika kama mchezaji atajiamini na kuzizingatia ndoto zake kupitia soka na kipaji alichonacho na si kingine.

The post Ajibu: Woga unawakwaza wachezaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/01/ajibu-woga-unawakwaza-wachezaji/feed/ 0
Ajibu: Singida Fountain itatamba Shirikisho https://www.greensports.co.tz/2023/06/24/ajibu-singida-fountain-itatamba-shirikisho/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/24/ajibu-singida-fountain-itatamba-shirikisho/#respond Sat, 24 Jun 2023 19:42:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6715 Na mwandishi wetuKiungo mshambuliaji wa Singida Fountain Gate, Ibrahim Ajibu amesema anaamini timu hiyo itafanya vizuri msimu ujao kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na wachezaji wengi wazoefu waliopo hapo.Akizungumza na GreenSports, Ajibu alisema ingawa timu hiyo ndiyo mara ya kwanza kushiriki michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lakini ana […]

The post Ajibu: Singida Fountain itatamba Shirikisho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Singida Fountain Gate, Ibrahim Ajibu amesema anaamini timu hiyo itafanya vizuri msimu ujao kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na wachezaji wengi wazoefu waliopo hapo.
Akizungumza na GreenSports, Ajibu alisema ingawa timu hiyo ndiyo mara ya kwanza kushiriki michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lakini ana imani watafanya vizuri kutokana na mipango ya timu ilivyo kuelekea mashindano hayo.
“Singida ni timu nzuri sababu ina wachezaji wengi wazuri na wazoefu, na mashindano yale yanahitaji sana uzoefu kwa hiyo wachezaji wengi waliopo hapa wameshacheza michuano hiyo kwa hiyo timu ndiyo itakuwa ngeni lakini wachezaji hawatakuwa wageni hivyo naamini itafanya vizuri,” alisema Ajibu.
Singida iliyoshiriki Ligi Kuu NBC kwa mara ya kwanza msimu huu, imemaliza kwenye nafasi ya nne na kukata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho msimu ujao.
Baadhi ya wachezaji waliopo Singida ambao wamewahi kushiriki michuano ya CAF ni pamoja na Meddie Kagere, Paschal Wawa, Francis Kazadi, Said Ndemla, Bruno Gomes na wengine.

The post Ajibu: Singida Fountain itatamba Shirikisho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/24/ajibu-singida-fountain-itatamba-shirikisho/feed/ 0
Ajibu akiri mambo magumu https://www.greensports.co.tz/2023/06/22/ajibu-akiri-mambo-magumu/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/22/ajibu-akiri-mambo-magumu/#respond Thu, 22 Jun 2023 16:54:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6695 Na mwandishi wetuKiungo mshambuliaji wa Singida Fountain Gate, Ibrahim Ajibu amesema msimu uliomalizika hivi karibuni wa 2022-23 haukuwa mzuri kwake kutokana na changamoto alizopitia lakini anaamini msimu ujao atakuwa vizuri zaidi.Ajibu amesema hayo akifafanua kuwa timu yake ya Singida imekuwa na wakati mzuri na kufanikiwa kumaliza nafasi ya nne lakini kwake majeraha yaliyomuweka nje ya […]

The post Ajibu akiri mambo magumu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Singida Fountain Gate, Ibrahim Ajibu amesema msimu uliomalizika hivi karibuni wa 2022-23 haukuwa mzuri kwake kutokana na changamoto alizopitia lakini anaamini msimu ujao atakuwa vizuri zaidi.
Ajibu amesema hayo akifafanua kuwa timu yake ya Singida imekuwa na wakati mzuri na kufanikiwa kumaliza nafasi ya nne lakini kwake majeraha yaliyomuweka nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili yamemkwamisha.
“Msimu kwa ujumla ulikuwa mzuri ukizungumzia kitimu, timu imefanya vizuri na kumaliza nafasi za juu lakini kwa upande wangu binafsi haukuwa mzuri, sikuwa na furaha maana nimekaa nje miezi miwili sasa kutokana na majeraha yaliyokuwa yakiniandama, ingawa sasa nimeanza kukaa vizuri,” alisema Ajibu.
Kiungo huyo alisema tayari ameanza kujifua kwenye viwanja tofauti tofauti kutafuta utimamu wa mwili kabla ya kujiunga na timu kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu NBC pamoja na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Pia, Ajibu aliyewahi kutamba na timu za Simba na Yanga kabla ya kutimkia Azam anaamini msimu ujao atafanya vizuri kwa namna anavyojipanga kwa ajili ya kuisaidia Singida kufikia malengo iliyonayo.
Aliyataja malengo hayo kuwa ni pamoja na kufanya vizuri kwenye ligi kwa msimu wa pili mfululizo tangu ilipopanda msimu uliopita na pia kufika mbali kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

The post Ajibu akiri mambo magumu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/22/ajibu-akiri-mambo-magumu/feed/ 0