Afrika - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 30 Aug 2023 19:04:36 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Afrika - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Wapinzani wa Simba AFL kujulikana Jumamosi https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/wapinzani-wa-simba-afl-kujulikana-jumamosi/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/wapinzani-wa-simba-afl-kujulikana-jumamosi/#respond Wed, 30 Aug 2023 19:04:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7594 Na mwandishi wetuSimba SC inatarajia kuwafahamu wapinzani wao Jumamosi hii kwenye michuano mipya ya African Football League (AFL) katika droo itakayochezeshwa mjini Cairo, Misri.Shirikisho la Soka Afrika (Caf) mbali na kutaja tarehe ya droo hiyo lakini pia iliweka wazi ratiba ya michuano hiyo itakayoshirikisha timu nane kabla ya msimu ujao kujumuisha timu 24 za juu […]

The post Wapinzani wa Simba AFL kujulikana Jumamosi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba SC inatarajia kuwafahamu wapinzani wao Jumamosi hii kwenye michuano mipya ya African Football League (AFL) katika droo itakayochezeshwa mjini Cairo, Misri.
Shirikisho la Soka Afrika (Caf) mbali na kutaja tarehe ya droo hiyo lakini pia iliweka wazi ratiba ya michuano hiyo itakayoshirikisha timu nane kabla ya msimu ujao kujumuisha timu 24 za juu Afrika.
Mechi za robo fainali za michuano hiyo zitaanza kuunguruma Oktoba 20 ambapo nusu fainali itachezwa Oktoba 29 na Novemba Mosi kabla ya mechi za fainali itakayopigwa Novemba 5 na 11, mwaka huu.
“Toleo hili la kihistoria la uzinduzi wa AFL litafanyika kwa muda wa wiki nne, sherehe za ufunguzi na mechi ya kwanza itafanyika Oktoba 20 jijini Dar es Salaam, Tanzania. Nusu fainali itafanyika kati ya Oktoba 29 na Novemba Mosi na fainali ambazo zitaamua mshindi wa kwanza zitafanyika Novemba 5 na 11, mwaka huu,” ilieleleza taarifa ya Caf.
Ukiachana na Simba inayoiwaikilisha Tanzania, timu nyingine zitakazoshiriki msimu huu ni Al Ahly ya Misri, Enyimba (Nigeria), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Petro Atletico (Angola), TP Mazembe (DR Congo) na Wydad AC (Morocco).

The post Wapinzani wa Simba AFL kujulikana Jumamosi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/wapinzani-wa-simba-afl-kujulikana-jumamosi/feed/ 0
Al Ahly baba wa Afrika https://www.greensports.co.tz/2023/06/12/al-ahly-baba-wa-afrika/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/12/al-ahly-baba-wa-afrika/#respond Mon, 12 Jun 2023 08:48:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6564 Casablanca , MoroccoAl Ahly ya Misri imetwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya bao 1-1 na Wydad Casablanca ya Morocco na hivyo kuweka rekodi ya kubeba mara 11 taji la michuano hiyo mikubwa ya klabu barani Afrika.Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumapili hii usiku, Ahly walipata bao la kusawazisha katika dakika ya […]

The post Al Ahly baba wa Afrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Casablanca , Morocco
Al Ahly ya Misri imetwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya bao 1-1 na Wydad Casablanca ya Morocco na hivyo kuweka rekodi ya kubeba mara 11 taji la michuano hiyo mikubwa ya klabu barani Afrika.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumapili hii usiku, Ahly walipata bao la kusawazisha katika dakika ya 78 lililofungwa kwa kichwa na Mohamed Abdelmoneim kutokana na mpira wa kona uliopigwa na Ali Maaloul.
Kwa matokeo hayo, Ahly imefanikiwa kulibeba taji hilo kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 baada ya ushindi wa mechi ya kwanza ya fainali wa mabao 2-1, mechi iliyopigwa mjini Cairo, Misri.
Ushindi umekuwa tukio kubwa la kuwafuta machozi Ahly ambao msimu uliopita walishindwa kutamba mbele ya vigogo hao wa Morocco walipolala kwa mabao 2-0 katika mechi moja ya fainali iliyopigwa mjini Casablanca.
Kabla ya Abdelmoneim kusawazishia bao, Wydad walikuwa mbele kwa bao ambalo pia lilifungwa na Yahya Attiat katika dakika ya 28, bao ambalo lingetosha kuwapa Wydad taji na kuwafanya waweke rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka Morocco kubeba taji hilo mara mbili mfululizo.
Hata hivyo mwisho wa siku walikuwa ni Ahly waliotoka uwanjani na shangwe wakineemeka na bao la Abdelmoneim na hivyo kuweka rekodi ya kulibeba taji hilo lenye hadhi barani Afrika kwa mara 11.

The post Al Ahly baba wa Afrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/12/al-ahly-baba-wa-afrika/feed/ 0
Morocco yaweka historia Afrika https://www.greensports.co.tz/2022/12/10/morocco-yaweka-historia-afrika/ https://www.greensports.co.tz/2022/12/10/morocco-yaweka-historia-afrika/#respond Sat, 10 Dec 2022 17:54:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4244 Doha, QatarMorocco, leo Jumamosi imekuwa timu ya kwanza Afrika kufikia hatua ya nusu fainali katika historia ya Kombe la Dunia baada ya kuitoa Ureno kwa bao 1-0 katika mechi ya robo fainali, matokeo yaliyotosha kumliza nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo.Baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa, Ronaldo alionekana akiingia katika vyumba vya kubadilishia nguo huku akilia […]

The post Morocco yaweka historia Afrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Doha, Qatar
Morocco, leo Jumamosi imekuwa timu ya kwanza Afrika kufikia hatua ya nusu fainali katika historia ya Kombe la Dunia baada ya kuitoa Ureno kwa bao 1-0 katika mechi ya robo fainali, matokeo yaliyotosha kumliza nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo.
Baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa, Ronaldo alionekana akiingia katika vyumba vya kubadilishia nguo huku akilia wakati mashabiki na wachezaji wa Morocco wakipagawa kwa furaha baada ya kuweka historia mpya ya fainali hizo.
Shujaa wa Morocco alikuwa ni mshambuliaji, Youssef En-Nesyri katika dakika ya 42 akiunganisha kwa kichwa krosi iliyopigwa na Yahya Attiyat-Allah. En-Nesyri alikwenda juu na kuupiga mpira uliomshinda kipa wa Ureno Diogo Costa.
Bao hilo liliamsha shangwe kwa mashabiki wa Morocco waliojazana kwenye Uwanja wa Al Thumama na kuutawala kwa namna walivyokuwa wakiishangilia timu yao mwanzo mwisho.
Nahodha wa Ureno, Bruno Fernandes nusura asawazishe bao hilo lakini shuti alilopiga liligonga mwamba na kuishia kuibua mshtuko kwa mashabiki wa Morocco.
Dakika tano baada ya mapumziko, kocha wa Ureno, Fernando Santos alimuingiza Ronaldo ambaye hata hivyo hakuweza kubadili matokeo ya mchezo huo licha ya kuisumbua safu ya ulinzi ya Morocco mara kadhaa.
Katika kipindi cha pili, Morocco walitumia muda mwingi kujihami kwa umakini wa hali ya juu na katika dakika za majeruhi, timu hiyo ilipata pigo baada ya mshambuliaji wake, Walid Cheddira kupewa kadi ya pili ya njano kwa kucheza rafu na hivyo kuwa nyekundu lakini upungufu huo wa mchezaji mmoja haukuweza kuisaidia Ureno isawazishe bao hilo.
Morocco pamoja na kutumia muda mwingi kujihami lakini haikuacha kuichachafya Ureno na kama si umakini wa safu ya ulinzi ya timu hiyo shambulizi moja la kushtukiza lingeweza kuiumiza zaidi Ureno iliyokuwa ikihaha kusaka bao la kusawazisha.
Ushindi wa Morocco unakuwa historia mpya ya fainali za Kombe la Dunia kwa Afrika ikiwa timu ya kwanza kufikia hatua ya nusu fainali, hapo kabla timu tatu za Cameroon, Senegal na Ghana zilikuwa zikishikilia rekodi ya kufikia hatua ya robo fainali.
Ushindi wa Morocco pia unakumbusha kauli iliyowahi kutolewa na kocha wa timu hiyo, Walid Regragui ambaye baada ya kufuzu hatua ya mtoano alisema kwamba si vibaya kwa timu hiyo kuota kulibeba Kombe la Dunia.
Baada ya ushindi huo wakati mashabiki wakiimba na kushangulia majukwaani, Regragui alibebwa na kurushwa juu na wachezaji wake na sasa kikosi chake kinasubiri mechi ya nusu fainali na mshindi wa mechi nyingine ya robo fainali baadaye leo kati ya Ufaransa na England.

The post Morocco yaweka historia Afrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/12/10/morocco-yaweka-historia-afrika/feed/ 0
Simba ya 11 kwa ubora Afrika https://www.greensports.co.tz/2022/10/13/simba-ya-11-kwa-ubora-afrika/ https://www.greensports.co.tz/2022/10/13/simba-ya-11-kwa-ubora-afrika/#respond Thu, 13 Oct 2022 14:19:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=3229 Na mwandishi wetuSimba imezidi kutanua makucha baada ya Shirikisho la Kimataifa la Takwimu na Historia za Soka (IFFHS) kutoa orodha ya timu 20 za Afrika zinazoongoza kwa ubora kwa kipindi cha miezi 12 iliyopita.Kwa mujibu wa takwimu hizo zilizotolewa leo, Simba inashika nafasi ya 11 Afrika na ya 131 duniani. Takwimu hizo hupangwa kulingana na […]

The post Simba ya 11 kwa ubora Afrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imezidi kutanua makucha baada ya Shirikisho la Kimataifa la Takwimu na Historia za Soka (IFFHS) kutoa orodha ya timu 20 za Afrika zinazoongoza kwa ubora kwa kipindi cha miezi 12 iliyopita.
Kwa mujibu wa takwimu hizo zilizotolewa leo, Simba inashika nafasi ya 11 Afrika na ya 131 duniani. Takwimu hizo hupangwa kulingana na matokeo ya klabu husika kwenye ligi ya ndani, makombe ya ndani na mashindano ya kimataifa.
Katika mechi za nyumbani kwa maana ya ligi Simba imekuwa katika kiwango bora kwani ni miongoni mwa timu tatu ambazo hazijapoteza mchezo wowote mpaka sasa.
Takwimu hizo zimekuja wakati Simba ikiongoza Ligi Kuu ya NBC kwa pointi 13 katika michezo mitano, ikiwa imepata sare moja na haijafungwa huku ikiwa ndiyo timu pekee iliyofungwa mabao machache, mabao mawili.
Pia, katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba imetanguliza mguu mmoja kutinga hatua ya makundi ya ligi hiyo baada ya wiki iliyopita ilipokuwa ugenini Angola kuifunga mabao 3-1 Primiero de Agosto kabla ya mechi ya marudiano itakayopigwa Jumapili hii jijini Dar es Salaam.
Katika orodha ya Afrika, Al Ahly ya Misri inaongoza kwenye 10 Bora ikifuatiwa na Wydad Casablanca, Zamalek SC, Atlético de Luanda, Mamelodi Sundowns, CR Belouizdad, Pyramids FC, RS Berkane, Raja Casablanca na ES Sétif.
Timu zinazofuatia ni Simba, JS Saoura, Orlando Pirates, Esperance, TP Mazembe, Al Masry, Al Hilal Omdurman, Al Ahli Tripoli, JS Kabylie na Red Arrows FC.

The post Simba ya 11 kwa ubora Afrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/10/13/simba-ya-11-kwa-ubora-afrika/feed/ 0