Afcon - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 12 Feb 2024 07:06:33 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Afcon - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Ivory Coast yabeba taji Afcon https://www.greensports.co.tz/2024/02/12/ivory-coast-yabeba-taji-afcon/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/12/ivory-coast-yabeba-taji-afcon/#respond Mon, 12 Feb 2024 07:06:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9694 Abidjan, Ivory CoastIvory Coast hatimaye imefanikiwa kulibakisha nyumbani taji la Afcon 2023 baada ya kuichapa Nigeria mabao 2-1 katika mechi ya fainali iliyopigwa Jumapili hii usiku mjini Abidjan.Nigeria ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 38 lililofungwa na William Ekong na kuibua dalili zote za timu hiyo kubeba taji la nne la Afcon dhidi […]

The post Ivory Coast yabeba taji Afcon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Abidjan, Ivory Coast
Ivory Coast hatimaye imefanikiwa kulibakisha nyumbani taji la Afcon 2023 baada ya kuichapa Nigeria mabao 2-1 katika mechi ya fainali iliyopigwa Jumapili hii usiku mjini Abidjan.
Nigeria ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 38 lililofungwa na William Ekong na kuibua dalili zote za timu hiyo kubeba taji la nne la Afcon dhidi ya Ivory Coast waliokuwa wakisaka taji la tatu.
Hata hivyo walikuwa ni Franck Kessie aliyeisawazishia Ivory Coast bao dakika ya 62 na Sebastian Haller aliyefunga bao la ushindi dakika ya 81 na kuwafanya wenjeji kutoka katika dimba la Alassane Ouattara kwa shangwe na vigelegele.
Kwa Haller ambaye pia ni mchezaji wa Borussia Dortmund ya Ujerumani, bao hilo ni ushindi mwingine mkubwa wa pili kwake ikiwa ni takriban miezi sita imepita tangu atangaze kupona maradhi ya saratani (kansa).
Haller kwa mara ya kwanza alitangazwa kuugua kansa Julai 2022 ikiwa ni siku chache tangu aanze kufurahia maisha katika klabu ya Dortmund lakini alipata tiba sahihi na kupona na hatimaye kuendelea na soka kama kawaida.

“Tulikuwa tukiota jambo hili kwa miaka mingi, tulikuwa na matumaini ya kufikia hatua hii, na kwa mara nyingine mechi haikuwa rahisi, furaha unayoiona hapa ni kwa kile kilichotokea katika nchi hii, wana kila sababu ya kufurahi, naamini imewafanya watu wengi kuwa na furaha,” alisema Haller.


Ni Haller ambaye pia aliiwezesha Ivory Coast kufuzu hatua ya fainali baada ya kufunga bao pekee na la ushindi wakati timu hiyo ikiichapa DR Congo bao 1-0 katika mechi ya nusu fainali.
Haller ambaye ni mzaliwa wa jiji la Paris, Ufaransa lakini alichagua kuichezea nchi yake ya asili, hakutarajiwa kama angeweza kuifikisha timu hiyo hatua ya fainali hadi kubeba kombe kwa namna mwanzo ulivyokuwa mgumu.
Ivory Coast ilizianza fainali hizo vibaya ikiwamo kipigo cha mabao 4-0 mbele ya Equatorial Guinea hadi kulazimika kuchukua uamuzi mgumu wa kuachana na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Jean-Louis Gasset.
Nafasi ya Gasset alikabidhiwa kocha wa muda, Emerse Fae ambaye hatimaye alifanikiwa kubadili upepo na kulibakisha taji la Afcon Ivory Coast.

The post Ivory Coast yabeba taji Afcon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/12/ivory-coast-yabeba-taji-afcon/feed/ 0
Kocha Bafana Bafana haamini kilichotokea https://www.greensports.co.tz/2024/02/09/kocha-bafana-bafana-haamini-kilichotokea/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/09/kocha-bafana-bafana-haamini-kilichotokea/#respond Fri, 09 Feb 2024 05:54:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9645 Abidjan, Ivory CoastKocha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Hugo Broos bado (pichani) hajakubaliana na ukweli kwamba timu yake imetolewa katika Afcon 2023, badala yake anaamini timu hiyo ilicheza vizuri na ilitakiwa kushinda mechi hiyo.Afrika Kusini au Bafana Bafana ililala kwa penalti 4-2 mbele ya Nigeria jana Jumatano usiku baada ya sare ya bao […]

The post Kocha Bafana Bafana haamini kilichotokea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Abidjan, Ivory Coast
Kocha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Hugo Broos bado (pichani) hajakubaliana na ukweli kwamba timu yake imetolewa katika Afcon 2023, badala yake anaamini timu hiyo ilicheza vizuri na ilitakiwa kushinda mechi hiyo.
Afrika Kusini au Bafana Bafana ililala kwa penalti 4-2 mbele ya Nigeria jana Jumatano usiku baada ya sare ya bao 1-1 katika mechi ya nusu fainali ya Afcon.
Bafana Bafana ilipambana vizuri na kufanikiwa kusawazisha bao kwa mkwaju wa penalti katika dakika za lala salama lakini mambo yakawa magumu kwao kwenye mikwaju ya penalti.
“Soka kuna wakati ni mchezo mgumu, unapoangalia kiwango cha uchezaji cha timu yangu hii leo (jana) na baada ya hapo zinakuja penalti na unajikuta ukipoteza na haupo kwenye fainali, ni ngumu kukubali kwa sababu tulicheza vizuri,” alisema Broos.

“Nafikiri tulikuwa timu bora nusu ya kwanza, tulipata nafasi nzuri, Nigeria hawakuwa na nafasi yoyote, kipindi cha pili walipata nafasi chache zilizowapa goli na tulibadili kitu kwenye mbinu na kurudi vizuri,” alisema Broos.


Broos alisema kwamba timu yake ilitengeneza nafasi nyingi na hiyo maana yake ni kwamba kama wangefunga wao ndio wangekuwa fainali na si Nigeria.
Kocha huyo kutoka Ubelgiji hata hivyo aliipongeza timu yake kwa kucheza vizuri fainali za Afcon tangu mwanzo hadi kwenye mechi ya nusu fainali walipokwamia.
“Ni pigo kubwa kwa kila mmoja, tunaamini tulikuwa na mchezo mzuri, si leo tu lakini ni kwa kipindi chote cha fainali hizi, najivunia wachezaji wangu, maumivu yapo lakini kuna kitu cha kujivunia,” alisema Broos.
Baada ya matokeo hayo, Bafana Bafana sasa inasubiri kuumana na DR Congo keshokutwa Jumamosi katika mechi ya kuwania nafasi ya tatu.

The post Kocha Bafana Bafana haamini kilichotokea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/09/kocha-bafana-bafana-haamini-kilichotokea/feed/ 0
Fainali Afcon ni Nigeria, Ivory Coast https://www.greensports.co.tz/2024/02/08/fainali-afcon-ni-nigeria-ivory-coast/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/08/fainali-afcon-ni-nigeria-ivory-coast/#respond Thu, 08 Feb 2024 07:53:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9633 Abidjan, Ivory CoastMatumaini ya baadhi ya Watanzania kuiona DR Congo ikicheza mechi ya fainali ya Afcon 2023 yamekwama baada ya timu hiyo kulala kwa bao 1-0 mbele ya wenyeji Ivory Coast ambao ndio watakaocheza mechi ya fainali dhidi ya Nigeria.Mshambuliaji wa Borussia Dortmund ya Ujerumani, Sebastien Haller ndiye aliyefuta ndoto za DR Congo baada ya […]

The post Fainali Afcon ni Nigeria, Ivory Coast first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Abidjan, Ivory Coast
Matumaini ya baadhi ya Watanzania kuiona DR Congo ikicheza mechi ya fainali ya Afcon 2023 yamekwama baada ya timu hiyo kulala kwa bao 1-0 mbele ya wenyeji Ivory Coast ambao ndio watakaocheza mechi ya fainali dhidi ya Nigeria.
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund ya Ujerumani, Sebastien Haller ndiye aliyefuta ndoto za DR Congo baada ya kupachika bao pekee la ushindi kwa Ivory Coast katika dakika ya 65 ya mchezo huo uliopigwa usiku wa kuamkia leo Alhamisi.
Haller alifunga bao hilo kwa shuti kali akiitumia vizuri pasi ya Gradel na kupiga mpira uliomshinda kipa wa DR Congo, Lionel Mpasi na kuifanya DR Congo ishindwe kuiweka rekodi iliyokuwa ikisubiriwa na wengi.
Ushindi huo unakuwa jambo kubwa kwa wenyeji Ivory Coast ambao walilazimika kumtimua kocha wao, Jean-Louis Gasset na nafasi yake kukabidhiwa kocha wa muda, Emerse Fae ambaye hatimaye ameifikisha timu hiyo hatua ya fainali.
Fae, 40, kiungo wa zamani wa timu za Nantes na Nice za Ufaransa na Reading ya England, sasa ana mtihani mmoja wa kuiwezesha Ivory Coast kubeba taji la tatu la Afcon katika mechi ya fainali itakayopigwa Jumapili ijayo.

Ivory Coast, timu mwenyeji iliyozianza fainali za Afcon 2023 kwa kusuasua hatimaye imewapa faraja mashabiki wake ambao wanaisubiri kwa hamu Jumapili wakiamini timu yao inaweza kulibeba taji hilo baada ya kufanya hivyo mwaka 1992 na 2015.
Katika hatua nyingine wachezaji wa DR Congo na kocha wao, Sebastien Desabre walifanya mgomo wakati wa kuimba nyimbo za taifa kwa kuziba midomo wakitaka amani itafutwe mashariki mwa nchi yao.
Mechi nyingine ya nusu fainali iliyochezwa mapema jana Jumatano, Nigeria au Super Eagles ilifanikiwa kuitoa Afrika Kusini au Bafana Bafana kwa penalti 4-2 baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.
Nigeria ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na William Troost-Ekong kwa mkwaju wa penalti baada ya Victor Osimhen kuchezewa rafu ndani ya eneo la penalti na beki wa Bafana Bafana, Mothobi Mvala.
Bafana Bafana walifanikiwa kusawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penalt ya dakika ya 90 iliyofungwa na Teboho Mokoena na kuizuia Nigeria kwenda fainali moja kwa moja hadi sheria ya penalti tano tano ilipotumika na Nigeria kuibuka kinara.

The post Fainali Afcon ni Nigeria, Ivory Coast first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/08/fainali-afcon-ni-nigeria-ivory-coast/feed/ 0
Salah aahidi kurudi Afcon https://www.greensports.co.tz/2024/01/26/salah-aahidi-kurudi-afcon/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/26/salah-aahidi-kurudi-afcon/#respond Fri, 26 Jan 2024 10:49:12 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9449 Liverpool, EnglandNahodha na mshambuliaji wa timu ya Misri, Mohamed Salah ameanza tiba ya majeraha ya misuli ya nyuma ya goti huku akiahidi kufanya kila linalowezekana ili arudi Ivory Coast kuiwakilisha Misri kwenye fainali za Afcon.Salah alilazimika kurudi Liverpool Jumatano iliyopita kwa ajili ya tiba ya majeraha aliyoyapata wiki iliyopita wakati akiiwakilisha Misri dhidi ya Ghana […]

The post Salah aahidi kurudi Afcon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Liverpool, England
Nahodha na mshambuliaji wa timu ya Misri, Mohamed Salah ameanza tiba ya majeraha ya misuli ya nyuma ya goti huku akiahidi kufanya kila linalowezekana ili arudi Ivory Coast kuiwakilisha Misri kwenye fainali za Afcon.
Salah alilazimika kurudi Liverpool Jumatano iliyopita kwa ajili ya tiba ya majeraha aliyoyapata wiki iliyopita wakati akiiwakilisha Misri dhidi ya Ghana kwenye mechi ya Afcon hatua ya makundi, mechi iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2.
“Jana (juzi) nilianza utaratibu wa kupata matibabu na mazoezi ya kujiweka sawa, na nitafanya kila niwezalo ili nipone haraka iwezekanavyo na kurudi kwenye timu ya taifa kama tulivyokubaliana mwanzo,” aliandika Salah kupitia mitandao ya kijamii.
Kocha mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp pia alisema anaamini Salah atarudi kwenye fainali za Afcon kama atapona kwa wakati majeraha yanayomkabili na iwapo Misri itafikia hatua ya fainali.
Naye kocha msaidizi wa Liverpool, Pepijn Lijnders alisema Salah anatarajia kurudi uwanjani kwa kipindi cha wiki mbili au tatu kama hakutakuwa ni kitu cha kumkwaza katika tiba anayoendelea kuipata.
Kwa mujibu wa Lijnders uamuazi wa kumtaka Salah akapatiwe matibabu Liverpool haukuwa na lengo la kumuondoa kwenye timu ya Misri bali ni kuhakikisha anapata matibabu bora na sahihi.
Wakati huo huo, Klopp aliwajia juu wachambuzi na wanasoka wa zamani waliodai kwamba Salah ambaye pia ni mshambuliaji tegemeo wa Liverpool, alitakiwa kubaki Ivory Coast na kikosi cha Misri.

“Kama kuna watu wanahoji uadilifu wa Mo Salah wanatakiwa wajiulize kama uadilifu wao upo sahihi kwa sababu Mo Salah ni mchezaji muadilifu zaidi kwa timu yake ya taifa kati ya wachezaji niliowahi kukutana nao katika maisha yangu,” alisema Klopp.


Wakati mjadala wa Misri kumtumia au kutomtumia Salah kwenye Afcon ukiwa umepamba moto, Misri kwanza italazimika kufuzu mtihani wa Jumapili dhidi ya DR Congo katika mechi ya mtoano au 16 bora.

The post Salah aahidi kurudi Afcon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/26/salah-aahidi-kurudi-afcon/feed/ 0
Makocha watatu Afcon wapoteza kazi https://www.greensports.co.tz/2024/01/25/makocha-watatu-afcon-wapoteza-kazi/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/25/makocha-watatu-afcon-wapoteza-kazi/#respond Thu, 25 Jan 2024 19:24:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9443 Abdjan, Ivory CoastMatokeo mabaya kwenye fainali za Afcon yamesababisha makocha watatu kutoka nchi za Ghana, Algeria na wenyeji wa fainali hizo, Ivory Coast kupoteza kazi hadi sasa.Kocha wa wenyeji Ivory Coast, Jean-Louis Gasset ametimuliwa baada ya timu hiyo kupokea kichapo cha mabao 4-0 mbele ya Equatorial Guinea, kipigo ambacho kinatajwa kuwa ni kikubwa mno katika […]

The post Makocha watatu Afcon wapoteza kazi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Abdjan, Ivory Coast
Matokeo mabaya kwenye fainali za Afcon yamesababisha makocha watatu kutoka nchi za Ghana, Algeria na wenyeji wa fainali hizo, Ivory Coast kupoteza kazi hadi sasa.
Kocha wa wenyeji Ivory Coast, Jean-Louis Gasset ametimuliwa baada ya timu hiyo kupokea kichapo cha mabao 4-0 mbele ya Equatorial Guinea, kipigo ambacho kinatajwa kuwa ni kikubwa mno katika historia ya nchi hiyo kwenye Afcon.
Taarifa ya Shirikisho la Soka Ivory Coast ilieleza kuwa mkataba wa kocha huyo mwenye umri wa miaka 70 umesitishwa pamoja na ule wa msaidizi wake Ghislain Printant na Emerse Fae amechaguliwa kuwa kocha wa muda.
Kocha mwingine aliyejikuta akipoteza kazi ni Djamel Belmadi wa Algeria ambaye alikubali mwenyewe kusitisha mkataba wake baada ya timu hiyo kutolewa kwenye fainali za Afcon.
Belmadi aliwaambia mapema wachezaji wake kwamba atang’atuka baada ya Algeria kufungwa bao 1-0 na Mauritania.
Rais wa Shirikisho la Soka Algeria, Walid Sadi alisema kwamba alikutana na kocha huyo kwa lengo la kujadili kutolewa kwenye Afcon na mwishowe wakakubaliana kuvunja mkataba wa kocha huyo.
Belmadi alikuwa kocha wa Algeria mwaka 2019 timu hiyo ilipobeba taji la Afcon nchini Misri lakini safari hii timu yake imeishia mkiani na pia ilishindwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2022.
Chris Hughton (pichani juu) aliyekuwa na kikosi cha Ghana kwenye Afcon naye ametimuliwa baada ya Black Stars kumaliza mechi za Kundi B ikiwa na pointi mbili ikitoka sare mara mbili dhidi ya Msumbiji na Misri na kufungwa mabao 2-1 na Cape Verde.


Ghana ni kati ya timu zilizokuwa zikipewa matarajio makubwa ya kufika mbali lakini juzi Jumanne timu hiyo ilifikia mwisho na kuziaga fainali za Afcon mapema katika hatua ya makundi.
Taarifa ya Chama cha Soka Ghana (GFA) ilieleza kuwa kocha huyo ameondolewa katika majukumu yake pamoja na kuvunjwa kwa benchi zima la ufundi na siku chache zijazo GFA itatoa mwelekeo wa Black Stars na nini kitakachofanyika.
Kocha Hughton aliingia matatani hivi karibuni baada ya shabiki mmoja kumshambulia kwa maneno lakini GFA wakawa wa kwanza kumtetea kwa kudai kwamba wako pamoja na kocha huyo kwa asilimia 100 lakini hatimaye wameamua kumtimua.
Wakati huo huo hatma ya kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Adel Amrouche (pichani) ipo njia panda baada ya kusimamishwa na CAF pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Amrouche amesimamishwa mechi nane kutokana na kauli alizozitoa za kuishutumu Morocco kwa madai ya kuwa na nguvu ya maamuzi ndani ya Caf kuhusu muda wa mechi kuchezwa na uteuzi wa waamuzi.

The post Makocha watatu Afcon wapoteza kazi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/25/makocha-watatu-afcon-wapoteza-kazi/feed/ 0
Stars yaaga Afcon mapema https://www.greensports.co.tz/2024/01/25/stars-yaaga-afcon-mapema/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/25/stars-yaaga-afcon-mapema/#respond Thu, 25 Jan 2024 05:28:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9414 Abidjan, Ivory CoastTimu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeshindwa kufuzu hatua ya mtoano kwenye fainali za Afcon baada ya kukubali sare ya 0-0 mbele ya DR Congo na hivyo kuaga rasmi fainali hizo kwa kuishia hatua ya makundi.Stars katika mechi hiyo iliyopigwa Jumatano hii usiku ilihitaji ushindi wowote ili kufikisha pointi nne ambazo zingeifanya […]

The post Stars yaaga Afcon mapema first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Abidjan, Ivory Coast
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeshindwa kufuzu hatua ya mtoano kwenye fainali za Afcon baada ya kukubali sare ya 0-0 mbele ya DR Congo na hivyo kuaga rasmi fainali hizo kwa kuishia hatua ya makundi.
Stars katika mechi hiyo iliyopigwa Jumatano hii usiku ilihitaji ushindi wowote ili kufikisha pointi nne ambazo zingeifanya ifuzu hatua ya mtoano lakini sare imeifanya imalize ikiwa mkiani katika Kundi F.
Tofauti na matarajio ya wengi, Stars iliuanza mchezo huo kwa kuonesha uhai tangu mwanzo na kutoa dalili za kupata bao baada ya nahodha wake Mbwana Samatta kufika langoni mwa DR Congo katika dakika tatu za mwanzo.
Timu hiyo iliendelea kucheza kwa kujihami huku ikilisogelea lango la wapinzani wao ambao walijibu mapigo dakika ya 11 na kumlazimisha Himid Mao kucheza rafu na mwamuzi kuipa DR Congo mpira wa adhabu ambao ulipigwa na Gael Kakuta lakini haukuwa na madhara.
Dakika ya 29, Kakuta tena alimuunganishia pasi nyota wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele ambaye alipita katikati ya mabeki wa Stars, Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Bacca lakini shuti alilopiga liliokolewa na kipa wa Stars, Aishi Manula.
Stars nao walikuja juu dakika ya 48 baada ya Novatus Dismas, Samatta na Lusajo Mwaikenda kugongeana pasi wakiwa karibu na lango la DR Congo lakini mpira wa kichwa uliopigwa na Novatus ulikuwa mwepesi mno kwa kipa wa DR Congo, Mpasi.
Katika kujiimarisha DR Congo iliwatoa Silas Katompa na nafasi yake kuingia Meshack Eliya na baadaye Mayele aliyekuwa na wakati mgumu kuipenya ngome ya Stars alitoka na kuingia Bikabu.
Kwa upande wa Stars Himid Mao alitoka na nafasi yake kuingia Muzamir Yassin,
Mabadiliko hayo yalionekana kuipa uhai DR Congo na kuongeza nguvu ya kulisakama lango la Stars na katika dakika ya 77 kama si umahiri wa Manula, DR Congo wangeweza kupata bao.
Manula ambaye alitoka katika eneo lake ili kuuwahi mpira lakini aliukosa na kulazimika kurudi nyuma kwa kasi, kabla hajafika katika eneo lake, Yoane Wissa aliupiga mpira wa juu na Manula kulazimika kuruka huku akirudi nyuma, akafanikiwa kuutoa mpira huo na kuwa kona.
Stars iliendelea kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Feisal Salum ‘Fei Toto na kumuingiza Kibu Denis kabla ya kuwatoa Simon Msuva na Samatta na nafasi zao kuchukuliwa na Charles Mmombwa na Moses Abraham.
Mabadiliko hayo hata hivyo hayakuwa na tija kwa Stars kwani hadi mwisho wa mchezo matokeo yalikuwa sare ya 0-0 na kuifanya Stars iage fainali hizo mapema katika hatua ya makundi.
Katika mechi nyingine ya kundi hilo, Morocco iliichapa Zambia bao 1-0 na hivyo kumaliza mechi zake za makundi ikiwa na pointi saba ikifuatiwa na DR Congo yenye pointi nne ambazo ndizo zilizofuzu katika kundi hilo, Zambia ya tatu ikiwa na pointi mbili kama Stars iliyoishia mkiani.
Hii ni mara ya tatu katika historia ya Stars kushiriki Afcon na kuishia hatua hiyo, ilifanya hivyo kwa mara ya kwanza mwaka 1980 na baadaye mwaka 2019.

The post Stars yaaga Afcon mapema first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/25/stars-yaaga-afcon-mapema/feed/ 0
Mashabiki sita wafariki Guinea https://www.greensports.co.tz/2024/01/22/mashabiki-sita-wafariki-guinea/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/22/mashabiki-sita-wafariki-guinea/#respond Mon, 22 Jan 2024 09:07:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9377 Conakry, GuineaShirikisho la Soka Guinea (Feguifoot) limetaka kuwepo utulivu baada ya kutokea vifo vya mashabiki sita wa soka nchini humo waliokuwa wakishangilia ushindi wa kwanza wa timu yao kwenye fainali za Afcon zinazoendelea Ivory Coast.Katika mechi hiyo iliyochezwa Ijumaa iliyopita, Guinea iliichapa Gambia bao 1-0 hali iliyoibua mlipuko wa furaha miongoni mwa mashabiki ambao waliingia […]

The post Mashabiki sita wafariki Guinea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Conakry, Guinea
Shirikisho la Soka Guinea (Feguifoot) limetaka kuwepo utulivu baada ya kutokea vifo vya mashabiki sita wa soka nchini humo waliokuwa wakishangilia ushindi wa kwanza wa timu yao kwenye fainali za Afcon zinazoendelea Ivory Coast.
Katika mechi hiyo iliyochezwa Ijumaa iliyopita, Guinea iliichapa Gambia bao 1-0 hali iliyoibua mlipuko wa furaha miongoni mwa mashabiki ambao waliingia mitaani wakishangilia ushindi huo.
Kwa mujibu wa Feguifoot, vifo vya mashabiki hao vilitokea katika mji wa Conakry baada ya mashabiki baadhi yao wakiwa kwenye magari na wengine pikipiki kuingia mitaani na kushangilia ushindi huo.
Vyanzo vingi vya habari hata hivyo havijaeleza kwa undani kuhusu vifo hivyo vimesababishwa na nini hasa, umri wa waliofariki, jinsia zao pamoja na idadi ya majeruhi kama wapo.
Tukio la vifo hivyo limetokea wakati baadhi ya mashabiki wa Guinea wapo nchini Ivory Coast kwa ajili ya kuishangilia timu yao ya taifa wakati wale walio nyumbani wengi wao wanafuatilia mechi za timu hiyo kupitia televisheni.
Bao pekee lililoipa Guinea ushindi katika mechi hiyo ya Kundi C lilifungwa na Aguibou Camara katika dakika za majeruhi na kuipa timu hiyo ushindi ambao pia umeibua matumaini ya timu hiyo kusonga mbele baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Cameroon.
Guinea, ni moja ya nchi ambazo wananchi wake wana mapenzi makubwa ya soka na haikushangaza kwa wananchi kuingia barabarani kushangilia ushindi dhidi ya Gambia mara tu baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya kumaliza mchezo.

The post Mashabiki sita wafariki Guinea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/22/mashabiki-sita-wafariki-guinea/feed/ 0
Salah arudi Liverpool kufuata tiba https://www.greensports.co.tz/2024/01/22/salah-arudi-liverpool-kufuata-tiba/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/22/salah-arudi-liverpool-kufuata-tiba/#respond Mon, 22 Jan 2024 09:01:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9375 Abidjan, Ivory CoastMshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah ataondoka kwenye kambi ya timu yake ya taifa nchini Ivory Coast na kwenda Liverpool kupata tiba ya matatizo ya misuli yanayomkabili.Salah yuko Ivory Coast akiiwakilisha timu ya taifa ya Misri kwenye fainali za Afcon na leo Jumatatu timu yake itacheza na Cape […]

The post Salah arudi Liverpool kufuata tiba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Abidjan, Ivory Coast
Mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah ataondoka kwenye kambi ya timu yake ya taifa nchini Ivory Coast na kwenda Liverpool kupata tiba ya matatizo ya misuli yanayomkabili.
Salah yuko Ivory Coast akiiwakilisha timu ya taifa ya Misri kwenye fainali za Afcon na leo Jumatatu timu yake itacheza na Cape Verde na inadaiwa mchezaji huyo atakuwa jukwaani wakati wa mechi hiyo.
Chama cha Soka Misri (Efa) kimethibitisha kuwa Salah ataendelea na matibabu katika klabu yake ya Liverpool kama ilivyoshauriwa na kocha Jurgen Klopp jana Jumapili baada ya mechi ya Liverpool na Bournemouth katika Ligi Kuu England, mechi ambayo Liverpool ilishinda kwa mabao 4-0.

“Matumaini yetu ni kwamba tutakuwa naye katika hatua ya nusu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kama tutafuzu hatua hiyo,” ilieleza taarifa ya Efa.


Salah aliumia Alhamisi iliyopita katika mechi dhidi ya Ghana iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2 na hadi sasa haijawekwa wazi muda ambao majeraha yaliyompata yatapona.
Alipokutana na waandishi wa habari juzi Jumamosi, Salah hata hivyo alikwepa kuzungumzia hali ya majeraha yanayomkabili na anatarajia lini kupona.
Klopp alinukuliwa mara baada ya Salah kuumia akisema kwamba anatarajia mchezaji huyo atarudi Liverpool kwa ajili ya tiba au walau kupata wasaa wa kuwa pamoja na timu ya madaktari wa klabu hiyo.

The post Salah arudi Liverpool kufuata tiba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/22/salah-arudi-liverpool-kufuata-tiba/feed/ 0
Bosi Napoli hataki wachezaji Waafrika https://www.greensports.co.tz/2022/08/04/bosi-napoli-hataki-wachezaji-waafrika/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/04/bosi-napoli-hataki-wachezaji-waafrika/#respond Thu, 04 Aug 2022 09:56:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2119 Naples, ItaliaMmiliki na mwenyekiti wa klabu ya Napoli, Aurelio De Laurentiis amesema kwamba klabu yake haitosajili tena wachezaji wa kutoka Afrika hadi hapo wachezaji hao watakapokubali kutoshiriki michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon).Beki Msenegali, Kalidou Koulibaly ambaye kwa sasa anaichezea Chelsea na kiungo Mcameroon, Andre Zambo walikosa mechi kadhaa za Napoli wakati wakiziwakilisha nchi zao […]

The post Bosi Napoli hataki wachezaji Waafrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Naples, Italia
Mmiliki na mwenyekiti wa klabu ya Napoli, Aurelio De Laurentiis amesema kwamba klabu yake haitosajili tena wachezaji wa kutoka Afrika hadi hapo wachezaji hao watakapokubali kutoshiriki michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon).
Beki Msenegali, Kalidou Koulibaly ambaye kwa sasa anaichezea Chelsea na kiungo Mcameroon, Andre Zambo walikosa mechi kadhaa za Napoli wakati wakiziwakilisha nchi zao kwenye fainali za Afcon ambazo zilifanyika kati ya Januari na Februari mwaka huu.
“Au vinginevyo wasaini kujitoa kushiriki katika Afcon,” alisema De Laurentiis kauli ambayo Koulibaly aliijibu akionyesha kusikitishwa na msimamo wa bosi wake wa zamani.
“Ni lazima uonyeshe heshima kwa timu ya Taifa kwa sababu huwezi kuzizungumzia timu za Taifa katika namna hii,” alisema Koulibaly.
“Nikiwa ndiye nahodha wa timu ya Senegal nafikiri hiyo si namna nzuri ya kuzizungumzia timu za soka za Afrika lakini namheshimu kama anafikiri timu inaweza kucheza bila ya wachezaji wa Afrika hiyo ni juu yake, si kila mtu ana mtazamo kama wake katika klabu,” aliongeza Kaulibaly.
De Laurentiis ambaye ni mtayarishaji filamu, pia aliipinga michuano iliyotaka kuanzishwa ya European Super League ambayo ilipingwa na wengi akiitaja kuwa ni michuano ya klabu zilizoonekana kuwa na hadhi fulani kwenye soka.
“Huwezi kuanzisha ligi ya super club kwa kuhusisha wanachama wa klabu zenye hadhi ambao wanawaalika wengine, unahitaji kuwa na demokrasia na kuweka milango wazi kwa kila mmoja,” alisema.

The post Bosi Napoli hataki wachezaji Waafrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/04/bosi-napoli-hataki-wachezaji-waafrika/feed/ 0