Riadha - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 10 Sep 2024 19:08:00 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Riadha - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Aliyemchoma moto mwanariadha naye afariki https://www.greensports.co.tz/2024/09/10/aliyemchoma-moto-mwanariadha-naye-afariki/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/10/aliyemchoma-moto-mwanariadha-naye-afariki/#respond Tue, 10 Sep 2024 19:07:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11885 Eldoret, KenyaSiku chache baada ya mwanariadha wa Uganda, Rebecca Cheptegei (pichani) kufariki kwa kuchomwa moto wa petroli, aliyekuwa rafiki yake wa kiume, Dickson Ndiema anayedaiwa kumfanyia ukatili huo naye amefariki dunia leo Jumanne.Rebecca, 33 ambaye aliiwakilisha Uganda kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 hivi karibuni, alichomwa moto Septemba Mosi na kuungua zaidi ya asilimia […]

The post Aliyemchoma moto mwanariadha naye afariki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Eldoret, Kenya
Siku chache baada ya mwanariadha wa Uganda, Rebecca Cheptegei (pichani) kufariki kwa kuchomwa moto wa petroli, aliyekuwa rafiki yake wa kiume, Dickson Ndiema anayedaiwa kumfanyia ukatili huo naye amefariki dunia leo Jumanne.
Rebecca, 33 ambaye aliiwakilisha Uganda kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 hivi karibuni, alichomwa moto Septemba Mosi na kuungua zaidi ya asilimia 70 ya mwili wake kabla ya kufariki dunia siku nne baadaye.
Kifo cha Rebecca kilitokana na mzozo baina yake na Dickson chanzo kikidaiwa kuwa ni mgogoro baina ya wawili hao uliotokana na eneo la ardhi ambayo inadaiwa Rebecca aliinunua na kujenga nyumba.
Baada ya kifo cha Rebbeca ndugu zake na watu mbalimbali walisisitiza kutaka haki itendeke lakini kifo cha Dickson ambaye alikuwa mtuhumiwa mkuu kinazidi kuacha maswali kuhusu tukio hilo.
Wawili hao baada ya wote kuwa na majeraha ya moto walikimbizwa katika Hospitali ya Moi mjini Eldoret wakiwa na hali mbaya ingawa Rebecca ndiye aliyeungua sehemu kubwa ya mwili wake kumzidi Dickson.
Akizungumzia kifo cha Dickson, msemaji wa Hospitali ya Moi, Daniel Lang’at alisema kifo chake kilitokana na majeraha ya kuungua na moto.
Katika Michezo ya Olimpiki, Rebecca alishika nafasi ya 44 na baadhi ya makundi ya watetezi wa haki za wanawake wanahusisha kifo hicho na matukio ya unyanyasaji na unyonyaji wanaofanyiwa wanamichezo wanawake waliopata mafanikio.

The post Aliyemchoma moto mwanariadha naye afariki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/10/aliyemchoma-moto-mwanariadha-naye-afariki/feed/ 0
Mwanariadha aliyechomwa moto afariki dunia https://www.greensports.co.tz/2024/09/05/mwanariadha-wa-uganda-aliyechomwa-moto-kenya-afariki-dunia/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/05/mwanariadha-wa-uganda-aliyechomwa-moto-kenya-afariki-dunia/#respond Thu, 05 Sep 2024 13:07:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11873 Eldoret, KenyaMwanariadha wa Uganda aliyeiwakilisha nchi hiyo kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, Rebecca Cheptegei amefariki dunia siku chache baada ya kuchomwa moto na rafiki yake wa kiume.Rebecca, 33, aliungua zaidi ya asilimia 70 ya mwili wake baada ya kuchomwa moto na rafiki yake wa kiume baada ya kuibuka mzozo baina ya wawili hao.Msemaji […]

The post Mwanariadha aliyechomwa moto afariki dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Eldoret, Kenya
Mwanariadha wa Uganda aliyeiwakilisha nchi hiyo kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, Rebecca Cheptegei amefariki dunia siku chache baada ya kuchomwa moto na rafiki yake wa kiume.
Rebecca, 33, aliungua zaidi ya asilimia 70 ya mwili wake baada ya kuchomwa moto na rafiki yake wa kiume baada ya kuibuka mzozo baina ya wawili hao.
Msemaji wa Hospitali ya Moi ya mjini Eldoret, Owen Menach alithibitisha kuwa mwanariadha huyo amefariki leo Alhamisi asubuhi baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo siku chache zilizopita akiwa na hali mbaya na viungo vyake vingi kushindwa kufanya kazi.
Rebecca alishiriki vyema Michezo ya Olimpiki ya Paris akiwa mwakilishi wa Uganda na kumaliza nafasi ya 44 katika mbio za marathon kwa wanawake na umauti umemkuta akiwa hajamaliza hata mwezi mmoja tangu kuiwakilisha Uganda kwenye Olimpiki.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya hospitali hiyo, Joseph Cheptegei ambaye ni baba mzazi wa Rebecca alisema amepoteza mtoto ambaye alikuwa msaada mkubwa kwake na ana matumaini haki itatendeka.
Mapema Jumatatu taarifa ya polisi wa kaunti ya Trans-Nzoia, ilieleza kuwa rafiki wa kiume wa Rebecca alitumia galoni la petroli na kummwagia Rebecca kabla ya kumuwashia moto.
Moto huo hata hivyo uliwaunguza wote wawili na hadi sasa rafiki huyo naye amelazwa katika hospitali hiyo hiyo akiwa katika wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu.
Awali kiongozi wa eneo lililotokea tukio hilo alisema wawili hao walikuwa na mzozo ambao chanzo chake kinadaiwa ni eneo la ardhi ambalo lina nyumba inayodaiwa kujengwa na Rebecca, nyumba ambayo tukio la moto huo lilitokea.
Shirikisho la Riadha Uganda lilitoa taarifa kupitia mitandao ya kijamii kueleza kusikitishwa na kifo cha Rebecca na kumuombea marehemu apumzike kwa maani huku wakilaani tukio zima la mauaji hayo na kuomba haki itendeke.

The post Mwanariadha aliyechomwa moto afariki dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/05/mwanariadha-wa-uganda-aliyechomwa-moto-kenya-afariki-dunia/feed/ 0
Mwanariadha Uganda achomwa moto Kenya https://www.greensports.co.tz/2024/09/04/mwanariadha-wa-uganda-achomwa-moto-kenya/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/04/mwanariadha-wa-uganda-achomwa-moto-kenya/#respond Wed, 04 Sep 2024 05:58:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11860 Eldoret, KenyaMwanariadha wa Uganda aliyetoka kushiriki Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, Rebecca Cheptegei amechomwa moto na rafiki yake wa kiume nchini Kenya na kuungua zaidi ya asilimia 70 ya mwili wake.Kwa mujibu wa Polisi tukio hilo lilitokea katika jimbo la Trans-Nzoia ambapo Rebecca ambaye alishika nafasi ya 44 katika Olimpiki Paris 2024 alivamiwa Jumapili […]

The post Mwanariadha Uganda achomwa moto Kenya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Eldoret, Kenya
Mwanariadha wa Uganda aliyetoka kushiriki Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, Rebecca Cheptegei amechomwa moto na rafiki yake wa kiume nchini Kenya na kuungua zaidi ya asilimia 70 ya mwili wake.
Kwa mujibu wa Polisi tukio hilo lilitokea katika jimbo la Trans-Nzoia ambapo Rebecca ambaye alishika nafasi ya 44 katika Olimpiki Paris 2024 alivamiwa Jumapili akiwa nyumbani kwake kabla ya kukutana na kadhia hiyo.
Kamanda wa Polisi wa Trans Nzoia, Jeremiah ole Kosiom alisema rafiki wa kiume wa Rebecca akiwa na dumu la mafuta ya petroli alimmwagia na kumchoma baada ya wawili hao kutofautiana.
Katika kadhia hiyo, rafiki wa kiume wa Rebebcca naye alipatwa na majeraha ya moto na kwa sasa wote wawili wanapatiwa matibabu maalum katika hospitali ya Moi iliyopo katika jiji la Eldoret.
Wazazi wa Rebecca walinukuliwa wakisema kwamba mtoto wao alinunua kiwanja maeneo ya Trans Nzoia ili awe karibu na wanariadha wenzake kwa lengo la kurahisisha ufanyaji wa mazoezi katika kituo maalum.
Taarifa ya polisi ilimnukuu kiongozi mmoja wa eneo hilo akisema kwamba kabla ya kadhia hiyo Rebecca na rafiki yake wa kiume walikuwa na mzozo kuhusu ardhi iliyotumika kujenga nyumba hiyo na ndipo baadaye tukio la Rebecca kuchomwa moto lilipojitokeza.
Tukio la Rebecca ni mwendelezo wa matukio ya kikatili dhidi ya wanariadha wa Uganda, mwaka 2023 mwanariadha Benjamin Kiplagat alikutwa amekufa mjini Eldoret akiwa na majeraha yanayodhaniwa kuwa ni ya visu.

The post Mwanariadha Uganda achomwa moto Kenya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/04/mwanariadha-wa-uganda-achomwa-moto-kenya/feed/ 0
Viza zawakosesha mashindano wanariadha https://www.greensports.co.tz/2024/03/29/viza-zawakosesha-mashindano-wanariadha/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/29/viza-zawakosesha-mashindano-wanariadha/#respond Fri, 29 Mar 2024 15:05:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10439 Na mwandishi wetuTimu ya Taifa ya riadha ya mbio za Nyika imeshindwa kwenda Belgrade, Serbia kushiriki mashindano ya Dunia yatakayoanza leo Ijumaa baada ya baadhi ya wachezaji kukosa visa.Timu hiyo yenye wachezaji tisa, ambayo ilikuwa kambini Ngaramtoni, Arusha kuanzia Machi 22, mwaka huu ilitarajiwa kuondoka juzi Machi 27, mwaka huu lakini imeshindikana kutokana na changamoto […]

The post Viza zawakosesha mashindano wanariadha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Taifa ya riadha ya mbio za Nyika imeshindwa kwenda Belgrade, Serbia kushiriki mashindano ya Dunia yatakayoanza leo Ijumaa baada ya baadhi ya wachezaji kukosa visa.
Timu hiyo yenye wachezaji tisa, ambayo ilikuwa kambini Ngaramtoni, Arusha kuanzia Machi 22, mwaka huu ilitarajiwa kuondoka juzi Machi 27, mwaka huu lakini imeshindikana kutokana na changamoto hiyo.
Wachezaji waliotarajiwa kusafiri kwa wanaume ni Herman Sulle, Boay Dawi, Dectaforce Boniface, Mao Ako na John Nahhay na wanawake ni Hamida Nassoro, Neema Festo, Ernestina Mngolale na Anastazia Dolomongo na kocha Marcelina Gwandu.
Akizungumza leo Ijumaa, Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Silas Isangi (pichani) alikiri kuhusiana na hilo: “Wanariadha walitarajiwa kuondoka tarehe 27 lakini ililazimika kusogeza mbele safari yao hadi tarehe 28 baada ya kuchelewa kupata viza kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu.
Alisema maombi ya viza yalifanyika Machi 8, mwaka huu kwenye ubalozi wa Serbia uliopo Nairobi nchini Kenya lakini mpaka Machi 27 ni wachezaji watano tu waliofanikiwa kukamilisha upatikanaji wa nyaraka hizo.
Alisema ndege ya KLM inatarajia kuondoka kesho Jumamosi saa nne asubuhi, kutoka Tanzania kupitia Entebbe, Uganda hivyo wangechelewa kufika Amsterdam, Uholanzi kwa ajili ya kuunganisha kwenda Serbia.

The post Viza zawakosesha mashindano wanariadha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/29/viza-zawakosesha-mashindano-wanariadha/feed/ 0
Dk Ndumbaro mgeni rasmi Kili Marathon https://www.greensports.co.tz/2024/02/13/dk-ndumbaro-mgeni-rasmi-kili-marathon/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/13/dk-ndumbaro-mgeni-rasmi-kili-marathon/#respond Tue, 13 Feb 2024 19:41:49 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9718 Na mwandishi wetuWaziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio za Kilimanjaro International Marathon zitakazofanyika Moshi, Kilimanjaro Februari 25, mwaka huu.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumanne na waandaaji wa mashindano hayo, Kilimanjaro Marathon Company Limited, Dk Ndumbaro amethibitisha kushiriki na anatarajiwa kuongozana na viongozi wengine wa ngazi […]

The post Dk Ndumbaro mgeni rasmi Kili Marathon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio za Kilimanjaro International Marathon zitakazofanyika Moshi, Kilimanjaro Februari 25, mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumanne na waandaaji wa mashindano hayo, Kilimanjaro Marathon Company Limited, Dk Ndumbaro amethibitisha kushiriki na anatarajiwa kuongozana na viongozi wengine wa ngazi ya mkoa wa Kilimanjaro na wa kitaifa.
“Wakati wa hafla hiyo, Dk Ndumbaro anatarajiwa kuanzisha rasmi mbio za kilometa 42 na zile za kilometa 21 na yeye kushiriki mbio za kilometa 5 za Gee Soseji,” ilisema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo pia imeeleza namba na vifaa kwa ajili ya washiriki wa mbio hizo zinazoratibiwa na Executive Solutions Limited, vitatolewa katika viwanja vya MoCU, kuanzia Februari 22 hadi Februari 24, mwaka huu kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni.
Mashindano hayo ya riadha maarufu Kili Marathon yamekuwa yakifanyika kila mwaka na kuendelea kujipatia umaarufu yakivutia washiriki wa ndani na nje ya nchi.

The post Dk Ndumbaro mgeni rasmi Kili Marathon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/13/dk-ndumbaro-mgeni-rasmi-kili-marathon/feed/ 0
Mwanariadha Kenya afariki kwa ajali ya gari https://www.greensports.co.tz/2024/02/13/mwanariadha-kenya-afariki-kwa-ajali-ya-gari/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/13/mwanariadha-kenya-afariki-kwa-ajali-ya-gari/#respond Tue, 13 Feb 2024 06:12:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9705 Nairobi, KenyaMwanariadha wa Kenya, anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za Marathon, Kelvin Kiptum (pichani) amefariki dunia na kocha wake katika ajali ya gari iliyotokea jana Jumapili jioni.Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, Kiptum aliyekuwa akipewa nafasi kubwa kutamba kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris baadaye mwaka huu, amefariki baada ya gari alilokuwa akiendesha kuacha […]

The post Mwanariadha Kenya afariki kwa ajali ya gari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Nairobi, Kenya
Mwanariadha wa Kenya, anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za Marathon, Kelvin Kiptum (pichani) amefariki dunia na kocha wake katika ajali ya gari iliyotokea jana Jumapili jioni.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, Kiptum aliyekuwa akipewa nafasi kubwa kutamba kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris baadaye mwaka huu, amefariki baada ya gari alilokuwa akiendesha kuacha njia na kugonga mti.
Kutokana na umri wake, mdogo wa miaka 24, Kiptum alikuwa akitajwa kuwa mmoja wa wanariadha ambao walipewa nafasi kubwa ya kubeba medali katika mashindano mbalimbali makubwa duniani.
Kifo cha mwanariadha huyo pia kimemgusa Rais William Ruto wa Kenya ambaye katika taarifa yake mbali na kutuma salamu za rambirambi pia amemtaja mwanariadha huyo kuwa ni mtu wao wa baadaye akimaanisha alivyokuwa na sifa za kutamba kwenye riadha.
Kiptum akiwa na kocha wake, Gervais Hakizimana raia wa Rwanda, kwa mujibu wa polisi walipata ajali hiyo saa tano usiku karibu kabisa na mji wa Kapsabet nchini Kenya.
Mtu mwingine aliyekuwa kwenye gari hilo ni msichana wa miaka 24 ambaye kwa mujibu wa polisi aliwahishwa hospitali akiwa amejeruhiwa vibaya wakati Kiptum na Hikizimana walifariki hapo hapo.
Wanariadha na wanafamilia ya Kiptum akiwamo baba yake walifika katika chumba cha kuhifadhia maiti baada ya taarifa za vifo hivyo kusambaa kwenye vyanzo mbalimbali vya habari.
Kiptum ni mwanariadha wa kwanza kuweka rekodi ya kukimbia na kumaliza mbio za marathon kwa muda usiozidi saa mbili, rekodi aliyoiweka Oktoba mwaka jana katika Chicago Marathon na hivyo kuvunja rekodi ya Mkenya mwenzake, Eliud Kipchoge.
Katika Michezo ya Olimpiki ya Paris, Kiptum na Kipchoge ni kati ya wanariadha waliokuwa wakisubiriwa kwa hamu kuiwakilisha vyema Kenya katika michezo hiyo.
Kiptum anaingia katika orodha ya wanariadha wanne wa Kenya waliofariki dunia kwa ajali ya gari, wengine ni David Lelei aliyefariki mwaka 2010 na Francis Kiplagat na Nicholas Bett ambao walifariki mwaka 2018.

The post Mwanariadha Kenya afariki kwa ajali ya gari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/13/mwanariadha-kenya-afariki-kwa-ajali-ya-gari/feed/ 0
RT wampongeza Rais Samia https://www.greensports.co.tz/2024/01/04/rt-wampongeza-rais-samia/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/04/rt-wampongeza-rais-samia/#respond Thu, 04 Jan 2024 16:20:00 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9154 Na mwandishi wetuShirikishi la Riadha Tanzania (RT), limepongeza hotuba ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kugusa sekta ya ya michezo hususani kutambua mchango mkubwa uliotolewa na wanariadha.Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu RT, Jackson Ndaweka, hotuba ya Rais Samia, mbali ya kugusa sekta mbalimbali, hakuisahau michezo hususani riadha kwa kuchangia mafanikio na kuitangaza […]

The post RT wampongeza Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Shirikishi la Riadha Tanzania (RT), limepongeza hotuba ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kugusa sekta ya ya michezo hususani kutambua mchango mkubwa uliotolewa na wanariadha.
Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu RT, Jackson Ndaweka, hotuba ya Rais Samia, mbali ya kugusa sekta mbalimbali, hakuisahau michezo hususani riadha kwa kuchangia mafanikio na kuitangaza vema Tanzania kimataifa kwa mwaka 2023.
“Sisi kama Riadha Tanzania tumeguswa na hotuba ya mheshimiwa Rais, tumefarijika pale alipotambua mafanikio ya wanariadha wetu Magdalena Shauri na Alphonce Simbu,” alisema Ndaweka na kuongeza:
“Hii itachochea kujituma zaidi na kufanya vizuri kwa vijana wetu na sisi kama shirikisho tunaahidi kujituma na kujipanga zaidi kwa kushirikiana na Serikali hususan wizara yenye dhamana na michezo, wadhamini na wadau mbalimbali ili kuleta mafanikio makubwa zaidi katika medani ya Riadha.”
Katika hotuba yake juzi, Rais Samia akielezea mafanikio katika sekta ya michezo alisema: “Kwenye sekta ya michezo, pamoja na kuimarisha miundombinu ikiwamo ukarabati Uwanja wa Benjamin Mkapa, mwaka huu tumepata mafanikio mengi ya kujivunia ikiwemo timu ya Yanga kupata medali ya pili kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
“Pia binti wa kitanzania Magdalena Shauri kuwa mshindi wa tatu kwenye mbio za Berlin Marathon na mwanariadha Alphonce Simbu kuwa mshindi wa pili kwenye mbio za Shanghai Marathon.”

The post RT wampongeza Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/04/rt-wampongeza-rais-samia/feed/ 0
Wawili wakamatwa mauaji ya mwanariadha https://www.greensports.co.tz/2024/01/03/wawili-wakamatwa-mauaji-ya-mwanariadha/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/03/wawili-wakamatwa-mauaji-ya-mwanariadha/#respond Wed, 03 Jan 2024 07:17:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9136 Eldoret, KenyaWatu wawili wanashikiliwa na polisi wakihusishwa na mauaji ya mwanariadha wa Uganda, Benjamin Kiplagat aliyeuawa mjini Eldoret, Kenya na mwili kukutwa ndani ya gari lake ukiwa na majeraha.Kamanda wa Polisi wa kaunti ndogo ya Moiben, Stephen Okal alisema kwamba kisu kinachodaiwa kutumika kumuua Kiplagat kilikutwa kwa mmoja wa watuhumiwa.Mauji ya Kiplagat, 34, kwa mujibu […]

The post Wawili wakamatwa mauaji ya mwanariadha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Eldoret, Kenya
Watu wawili wanashikiliwa na polisi wakihusishwa na mauaji ya mwanariadha wa Uganda, Benjamin Kiplagat aliyeuawa mjini Eldoret, Kenya na mwili kukutwa ndani ya gari lake ukiwa na majeraha.
Kamanda wa Polisi wa kaunti ndogo ya Moiben, Stephen Okal alisema kwamba kisu kinachodaiwa kutumika kumuua Kiplagat kilikutwa kwa mmoja wa watuhumiwa.
Mauji ya Kiplagat, 34, kwa mujibu wa Kamanda Okal chanzo chake kinadhaniwa kuwa ni wizi uliokusudiwa kufanywa na watuhumiwa kwa kuwa simu na fedha za marehemu vyote vilichukuliwa.
Kiplagat aliiwakilisha Uganda katika Michezo ya Olimpiki mara tatu na kwenye mashindano ya dunia ya riadha aliiwakilisha nchi hiyo mara sita akishiriki mbio za mita 3,000 na katika mashindano ya Afrika mwaka 2012 alishinda medali ya shaba.
Mauaji ya Kiplagat yanakuwa ni tukio la nne kutokea kwa mwanaridha wa nchini Kenya kwa miaka ya hivi karibuni.
Mwaka 2021, bingwa mara mbili wa mashindano ya dunia ya Mbio za Nyika, Agnes Tirop aliuawa katika mji wa kwao wa Iten, mume wake hadi sasa anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji.
Mwanariadha mzaliwa wa Kenya aliyeiwakilisha Bahrain, Damaris Muthee, mwili wake ulikutwa katika nyumba ya mwanariadha mwenzake, tukio ambalo lilitokea mwaka 2022.
Katika tukio jingine mwanariadha, Rubeyita Siragi aliuawa mwezi Agosti katika tukio ambalo polisi nchini Kenya walilihusisha na ugomvi wa kugombea mwanamke.

The post Wawili wakamatwa mauaji ya mwanariadha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/03/wawili-wakamatwa-mauaji-ya-mwanariadha/feed/ 0
Mwanariadha wa Uganda auawa Kenya https://www.greensports.co.tz/2024/01/01/mwanariadha-wa-uganda-auawa-kenya/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/01/mwanariadha-wa-uganda-auawa-kenya/#respond Mon, 01 Jan 2024 20:09:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9101 Eldoret, KenyaPolisi nchini Kenya wanachunguza maauji ya mwanariadha wa Uganda, Benjamin Kiplagat (pichani) ambaye mwili wake umekutwa ndani ya gari ya kaka yake ukiwa na majeraha.Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi wa eneo hilo, Stephen Okal, Kiplagat alikuwa akiendesha gari hilo kabla ya umauti kumkuta katika mji wa Eldoret uliopo maili 160 magharibi […]

The post Mwanariadha wa Uganda auawa Kenya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Eldoret, Kenya
Polisi nchini Kenya wanachunguza maauji ya mwanariadha wa Uganda, Benjamin Kiplagat (pichani) ambaye mwili wake umekutwa ndani ya gari ya kaka yake ukiwa na majeraha.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi wa eneo hilo, Stephen Okal, Kiplagat alikuwa akiendesha gari hilo kabla ya umauti kumkuta katika mji wa Eldoret uliopo maili 160 magharibi wa jiji la Nairobi.
Mwili wa mwanariadha huyo maarufu katika nchi za Kenya na Uganda ulikutwa jana Jumapili ukiwa na majeraha katika tukio ambalo linadhaniwa kuwa ni mpango maalum ulioandaliwa kwa lengo la kumtoa uhai mwanariadha huyo.

“Haya ni mauaji lakini kwa sasa bado hatujajua nini hasa kimesababisha mauaji haya,” alisema kamanda Okal.


Kiplagat alikuwa akikimbia zaidi mbio za mita 3,000, amewahi kuiwakilisha Uganda katika mashindano ya dunia mara sita, kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Kiangazi mwaka 2008, 2012, 2016 na katika Michezo ya Olimpiki London ya 2012 alifikia hatua ya nusu fainali.
Kifo cha Kiplagat kimezua taharuki nchini Kenya na Uganda hasa kwa kuwa imekuwa vigumu kujua nini hasa sababu ya mauaji hayo ya kikatili.

The post Mwanariadha wa Uganda auawa Kenya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/01/mwanariadha-wa-uganda-auawa-kenya/feed/ 0
Bayo afariki dunia https://www.greensports.co.tz/2023/04/11/bayo-afariki-dunia/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/11/bayo-afariki-dunia/#respond Tue, 11 Apr 2023 19:16:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5762 Na mwandishi wetuAliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, John Bayo (pichani) amefariki Dunia Jijini Arusha leo Jumanne.Mtoto wa marehemu aitwaye, Gilbert Bayo, alisema kwamba baba yake alianza kusumbuliwa na figo tangu Novemba, mwaka jana ambapo alifanyiwa upasuaji kwa kutolewa moja na hapo ndipo afya yake ilipoanza kudhoofika.“Baba alikuwa akisumbuliwa na figo na […]

The post Bayo afariki dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, John Bayo (pichani) amefariki Dunia Jijini Arusha leo Jumanne.
Mtoto wa marehemu aitwaye, Gilbert Bayo, alisema kwamba baba yake alianza kusumbuliwa na figo tangu Novemba, mwaka jana ambapo alifanyiwa upasuaji kwa kutolewa moja na hapo ndipo afya yake ilipoanza kudhoofika.
“Baba alikuwa akisumbuliwa na figo na mwaka jana alifanyiwa upasuaji akarudi nyumbani. Lakini baadaye alianza kuumwa tena na mwezi mmoja uliopita tukamleta Hospitali ya Ocean Road hadi Alhamisi ya wiki iliyopita alirudi huku Arusha na leo amefariki katika Hospitali ya Mount Meru,” alisema.
Alisema msiba upo nyumbani kwa John Bayo, Majengo mkoani Arusha ambapo taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika.
Katibu wa Kamisheni ya Wanariadha Tanzania, Andrew Robhi alisema wamepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha kiongozi huyo wa zamani.
“Watu wa riadha wamesikitishwa na tukio hili, nadhani taratibu za maazishi na wapi yatafanyika tutawatangazia. Kwa sasa mwili upo Mount Meru na msiba upo nyumbani kwake Majengo Arusha,” alisema kiongozi huyo.
“Huyu Mzee alikuwa muongozaji wa mbio mbalimbali zikiwemo Kilimanjaro Marathon na nyingine na ndiye aliyekuwa mpima njia maarufu, alikuwa mtu aliyeleta mabadiliko mengi na kufanya mengi. Sisi kama wanamichezo tutamkumbuka kwa mambo aliyofanya kwa ajili ya taifa letu,” alisema.
Licha ya Bayo kuwa ndiye msimamizi wa kambi ya Olimpiki mwaka jana, pia alikuwa wa kwanza kupeleka wanariadha Ulaya kuanzia miaka ya 1980 na ameendelea kuwa nguzo kuu katika uongozi wa riadha hadi mwisho wa uhai wake.

The post Bayo afariki dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/11/bayo-afariki-dunia/feed/ 0