Kimataifa - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 02 Mar 2026 08:23:13 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Kimataifa - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Yanga, Simba hakuna mbabe https://www.greensports.co.tz/2026/03/02/yanga-simba-hakuna-mbabe/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/02/yanga-simba-hakuna-mbabe/#respond Mon, 02 Mar 2026 08:22:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14389 Na mwandishi wetuVigogo wa soka la Tanzania, timu za Simba na Yanga wametoka sare ya bila kufungana katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyochezwa usiku wa Jumapili, Machi Mosi, 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.Kwa matokeo hayo, Yanga wameendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakifikisha pointi 29 na Simba kushika nafasi ya […]

The post Yanga, Simba hakuna mbabe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Vigogo wa soka la Tanzania, timu za Simba na Yanga wametoka sare ya bila kufungana katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyochezwa usiku wa Jumapili, Machi Mosi, 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.
Kwa matokeo hayo, Yanga wameendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakifikisha pointi 29 na Simba kushika nafasi ya tatu na pointi zao 24, timu zote hizo kila moja imeshacheza mechi 11.
Matokeo hayo pia yanaifanya Yanga kufikisha mechi ya saba mfululizo bila kufungwa na Simba ingawa matokeo ya sare siyo yaliyotegemewa na mashabiki walio wengi wa timu hiyo bingwa mtetezi wa ligi.
Simba waliuanza mchezo kwa kasi na katika dakika 10 za mwanzo walionesha dhamira yote ya kufuta uteja wa mechi saba zilizopita kwa kutengeneza nafasi kadhaa langoni mwa Yanga lakini hazikuzaa matunda.
Shambulizi la kwanza kabisa la kutisha la Simba langoni mwa Yanga lilifanyika dakika ya nne baada ya Jospin Loemba kuinasa pasi ya Nickson Kibabage na kufumua shuti lakini kipa Djigui Diarra alikuwa makini na kuokoa mpira huo.
Nao Yanga walijibu shambulizi hilo dakika tano baadaye, Mohamed Damaro akiwa katika nafasi nzuri aliufumania mpira na kufumua shuti ambalo hata hivyo lilitoka nje ya lango la Simba.
Katika dakika ya 70, Simba walifanya shambulizi la maana langoni mwa Yanga na kupata bao lililofungwa na Seleman Mwalimu lakini wakati mashabiki wao wakishangilia mwamuzi alipuliza filimbi kuashiria mfungaji aliotea.
Tukio hilo liliibua mzozo miongoni mwa wachezaji wa timu zote mbili na waamuzi kabla ya hali kutulia na mchezo kuendelea kama kawaida.
Wakizungumza baada ya mechi hiyo makocha wa timu hizo, Steve Barker wa Simba aliwasifia wachezaji wake licha ya kushindwa kupata ushindi wakati Pedro Concalves wa Yanga alisema mechi ilikuwa ngumu na kwamba Simba walitawala zaidi kipindi cha kwanza lakini wao Yanga walifanikiwa kuwadhibiti.
Mara ya mwisho Simba kutoka na ushindi mbele ya Yanga ilikuwa mwaka 2023 kwenye mechi ya Ngao ya Jamii, ushindi ambao ulipatikana kwa mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kutoka sare ya bila kufungana.

The post Yanga, Simba hakuna mbabe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/02/yanga-simba-hakuna-mbabe/feed/ 0
Beki Morocco astaafu timu ya taifa https://www.greensports.co.tz/2026/03/01/beki-morocco-astaafu-timu-ya-taifa/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/01/beki-morocco-astaafu-timu-ya-taifa/#respond Sun, 01 Mar 2026 20:18:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14385 Rabat, MoroccoNahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Morocco, Romain Saiss (pichani) ametangaza kujiuzulu kuichezea timu ya taifa akiwa na umri wa miaka 34, baada ya kuichezea timu hiyo kwa zaidi ya miaka 10.Saiss, beki kisiki wa kati aliyejipatia umaarufu alitangaza uamuzi huo hivi karibuni kupitia mitandao ya kijuamii akielezea kuwa wakati wake kwenye […]

The post Beki Morocco astaafu timu ya taifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rabat, Morocco
Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Morocco, Romain Saiss (pichani) ametangaza kujiuzulu kuichezea timu ya taifa akiwa na umri wa miaka 34, baada ya kuichezea timu hiyo kwa zaidi ya miaka 10.
Saiss, beki kisiki wa kati aliyejipatia umaarufu alitangaza uamuzi huo hivi karibuni kupitia mitandao ya kijuamii akielezea kuwa wakati wake kwenye timu ya taifa ya Morocco au Atlas Lion ulikuwa mzuri katika maisha yake ya soka.
Katika kipindi chote ambacho amekuwa na timu hiyo, Saiss amecheza jumla ya mechi 86 na kuwa nahodha wa timu hiyo katika kipindi cha mafanikio zaidi katika historia ya soka nchini Morocco.
Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na kufikia hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022 na kuweka rekodi ya kihistoria kwa kuwa timu ya kwanza kutoka bara la Afrika kufikia hatua hiyo.

“Leo nakamilisha ukurasa mzuri zaidi katika maisha yangu ya soka, baada ya kutafakari kwa kina, natangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa nikiwa mwenye hamasa kubwa, kuivaa jezi ya timu ya taifa ya Morocco na kuongoza timu hiyo inabaki kuwa heshima kubwa katika maisha yangu ya soka,” alisema Saiss.


Kwa kipindi chote ambacho amekuwa na timu ya taifa ya Morocco, Saiss amejijengea heshima akiwa mmoja wa mabeki imara wa kati wa timu hiyo na kiongozi aliyeheshimiwa na wachezaji wenzake.

The post Beki Morocco astaafu timu ya taifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/01/beki-morocco-astaafu-timu-ya-taifa/feed/ 0
Mashabiki watano wapigwa stop Benfica https://www.greensports.co.tz/2026/03/01/mashabiki-watano-wapigwa-stop-benfica/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/01/mashabiki-watano-wapigwa-stop-benfica/#respond Sun, 01 Mar 2026 20:14:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14382 Benfica, UrenoKlabu ya Benfica ya Ureno imewasimamisha mashabiki wake watano baada ya uchunguzi kubaini walijihusisha na vitendo vyenye viashiria vya ubaguzi wa rangi katika mechi yao dhidi ya Real Madrid hivi karibuni.Taarifa ya klabu hiyo ilieleza kuwa imechukua hatua hizo za kinidhamu dhidi ya mashabiki wake ambao huenda baadaye hatua zaidi zikachukuliwa ikiwamo uwezekano wa […]

The post Mashabiki watano wapigwa stop Benfica first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Benfica, Ureno
Klabu ya Benfica ya Ureno imewasimamisha mashabiki wake watano baada ya uchunguzi kubaini walijihusisha na vitendo vyenye viashiria vya ubaguzi wa rangi katika mechi yao dhidi ya Real Madrid hivi karibuni.
Taarifa ya klabu hiyo ilieleza kuwa imechukua hatua hizo za kinidhamu dhidi ya mashabiki wake ambao huenda baadaye hatua zaidi zikachukuliwa ikiwamo uwezekano wa mashabiki hao kufungiwa.
Katika mechi hiyo ambayo ni ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baadhi ya mashabiki wa Benfica wakiwa uwanja wao wa nyumbani walitoa dhihara ya ishara za nyani ambazo mara nyingi hufanyiwa wachezaji weusi au wenye asili ya Afrika.
Mashabiki hao ambao pia ni wanachama wa klabu hiyo wamesimamishwa uanachama baada ya kikao cha kamati ya nidhamu ambapo baadaye hatua zaidi zinatarajia kuchukuliwa kwa mujibu wa kanuni za klabu hiyo.

“Uchunguzi wa ndani uliofanywa baada ya mechi kati ya Benfica na Real Madrid iliyochezwa Februari 17 umebaini kuwapo vitendo visivyokubalika vyenye viashiria vya ubaguzi wa rangi katika majukwaa, vitendo ambavyo haviendani na miiko ya klabu,” ilieleza taarifa ya Benfica.


Benfica katika taarifa hiyo pia waliuhakikishia umma kuwa klabu yao haivumilii aina yoyote ya ubaguzi ikiwamo ubaguzi wa rangi na wataendelea kuchukua hatua kali dhidi ya tabia zozote zinazoshusha hadhi ya klabu hiyo.
Mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa kati ya timu hizo ilisimamishwa kwa dakika kadhaa mwamuzi alipoamua kutumia kanuni za kupinga ubaguzi wa rangi kwenye soka baada ya kuwapo tuhuma kwamba nyota wa Real Madrid, Vinicius Juior alifanyiwa dhihaka za kibaguzi na mshambuliaji wa Benfica, Gianluca Prestianni.
Prestianni, nyota kutoka Argentina hata hivyo alikana tuhuma hizo na hata klabu yake ilimtetea ikidai kuwa kilichopo ni sehemu ya mkakati wa kumuingiza mchezaji wao katika kesi ya udhililishaji.

The post Mashabiki watano wapigwa stop Benfica first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/01/mashabiki-watano-wapigwa-stop-benfica/feed/ 0
Pep ashtuka, ‘Real Madrid tena’ https://www.greensports.co.tz/2026/02/28/pep-ashtuka-kupangwa-na-real-madrid/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/28/pep-ashtuka-kupangwa-na-real-madrid/#respond Sat, 28 Feb 2026 08:45:00 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14376 Manchester, EnglandMan City wamepangwa kukabiliana na Real Madrid katika mechi za mtoano (16 bora) ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kitendo ambacho kidogo kinaonekana kumshangaza kama si kumshtua kocha wa Man City, Pep Guardiola.Hii inakuwa mara ya tano timu hizo kukutana katika miaka ya karibuni na jambo hilo ndilo linaloonekana kumshangaza Pep ambaye kwa sasa timu […]

The post Pep ashtuka, ‘Real Madrid tena’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Man City wamepangwa kukabiliana na Real Madrid katika mechi za mtoano (16 bora) ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kitendo ambacho kidogo kinaonekana kumshangaza kama si kumshtua kocha wa Man City, Pep Guardiola.
Hii inakuwa mara ya tano timu hizo kukutana katika miaka ya karibuni na jambo hilo ndilo linaloonekana kumshangaza Pep ambaye kwa sasa timu yake inapambana vikali kwenye mbio za taji la Ligi Kuu England.
Kwa Pep kitendo cha kupangwa tena na Real Madrid kitamfanya afikishe idadi ya mechi 15 dhidi ya timu hiyo tangu ajiunge na Man City mwaka 2016 baada ya kupitia na kujipatia mafanikio katika klabu ya Barcelona na baadaye Bayern Munich.
Pep alikiri kwamba kwa kiasi fulani jambo hilo linashangaza lakini alielezea kuwa kuna suala la mfumo wa michuano hiyo na kufafanua kwamba kwa kuwa tayari imeshapangwa hakuna namna.


Kocha huyo pia alisema kwamba kauli yake haina maana kwamba timu nyingine hazina changamoto kwa wapinzani wao kwani kuwa na imani hiyo ni kuzidharau timu hizo kwa kuona wao tu (Man City) ndio wenye wapinzani wagumu.
Pep alisema kuwa na imani kwamba wao tu ndio wenye mpinzani mgumu ni dharau ni kama vile kuona mechi kati ya Newcastle na Barcelona au Atlético Madrid na Tottenham ni rahisi wakati kiujumla Ligi ya Mabingwa ni ngumu.

“Pia sisemi Real Madrid si timu ngumu, kila mtu anafahamu ugumu wao, lakini ni hivyo hivyo kwa timu nyingine, unaweza kuzitaja, zote zipo katika hatua ngumu, unapotaka kusonga mbele katika hatua hii kwenye ligi ya mabingwa lazima ushinde dhidi ya timu bora, vinginevyo huna hadhi ya kwenda popote,” alisema Pep.


Nje ya hiyo hiyo ya Pep, kuna vita ya washambuliaji mahiri wa timu hizo mbili, Kylian Mbappe wa Real Madrid na Erling Haaland wa Man City ni yupi ambaye atafunga mabao ya kuisaidia timu yake kusonga mbele.

Mechi za kwanza katika hatua hiyo zitapigwa kati ya Machi 10 na 11 mwaka huu na marudiano Machi 17 na 18, hadi hapo kila timu itakuwa imejua hatma yake kwenye michuano hiyo mikubwa ya klabu Ulaya na duniani.
Timu pinzani 16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya
Paris St-Germain vs Chelsea
Galatasaray vs Liverpool
Real Madrid vs Manchester City
Atalanta vs Bayern Munich
Newcastle United vs Barcelona
Atletico Madrid vs Tottenham
Bodo/Glimt vs Sporting CP
Bayer Leverkusen vs Arsenal


The post Pep ashtuka, ‘Real Madrid tena’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/28/pep-ashtuka-kupangwa-na-real-madrid/feed/ 0
Ronaldo apiga bao, Al Nassr kileleni https://www.greensports.co.tz/2026/02/26/ronaldo-apiga-bao-al-nassr-kileleni/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/26/ronaldo-apiga-bao-al-nassr-kileleni/#respond Thu, 26 Feb 2026 19:11:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14370 Riyadh, Saudi ArabiaCristiano Ronaldo ametupia kambani katika ushindi wa mabao 5-0 ambao Al Nassr iliupata jana Jumatano Februari 25, 2026 dhidi ya Al Najma na kuiwezesha timu hiyo kushika usukani kwenye msimamo wa ligi.Hilo ni bao la tatu kwa Ronaldo tangu asitishe mgomo baridi na kuanza kuitumikia timu hiyo inayopambana katika mechi za Ligi Kuu […]

The post Ronaldo apiga bao, Al Nassr kileleni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabia
Cristiano Ronaldo ametupia kambani katika ushindi wa mabao 5-0 ambao Al Nassr iliupata jana Jumatano Februari 25, 2026 dhidi ya Al Najma na kuiwezesha timu hiyo kushika usukani kwenye msimamo wa ligi.
Hilo ni bao la tatu kwa Ronaldo tangu asitishe mgomo baridi na kuanza kuitumikia timu hiyo inayopambana katika mechi za Ligi Kuu Saudi Arabia maarufu Saudi Pro League.
Ronaldo ndiye aliyeanza kufungua ukurasa wa mabao baada ya kufunga kwa mkwaju wa penalti mapema dakika ya saba ya mchezo na hivyo kumfanya afikishe mabao 20 msimu huu akiwa amezidiwa katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu na Ivan Toney wa Al Ahli mwenye mabao 23.
Kasi ya Al Nassr iliendelea na kuzaa mabao mawili yaliyofungwa na Kingsley Coman na Inigo Martinez, mabao ambayo yalizifanya timu hizo ziende mapumziko Al Nassr wakiwa mbele kwa mabao 3-0.
Mabao mengine ya Al Nassr yalipachikwa wavuni na Sadio Mane mapema katika kipindi cha pili wakati ambao kocha wa timu hiyo, Jorge Jesus alianza kufanya mabadiliko kwa kuwatoa baadhi ya mastaa akiwamo Ronaldo.
Al Nassr inashika usukani wa ligi hiyo ikiwa imefikisha pointi 58 katika mechi 23 na hadi sasa imepoteza mechi moja tu na imewazidi kwa pointi mbili, Al Ahli wanaoshika nafasi ya pili.
Mapema mwezi huu Ronaldo alikosa mechi mbili za timu yake dhidi ya Al Ittihad na Al Riyadh kutokana na kilichodaiwa kuwa ni mgomo baridi aliouanzisha akipinga masuala kadhaa ya uendeshaji wa klabu na ligi ya Saudi Arabia.

The post Ronaldo apiga bao, Al Nassr kileleni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/26/ronaldo-apiga-bao-al-nassr-kileleni/feed/ 0
Messi ajuta kutojifunza Kiingereza https://www.greensports.co.tz/2026/02/26/messi-ajuta-kutojifunza-kiingereza/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/26/messi-ajuta-kutojifunza-kiingereza/#respond Thu, 26 Feb 2026 16:30:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14365 Miami, MarekaniMshambuliaji wa timu ya Inter Miami ya Marekani, Lionel Messi amesema kwamba kati ya mambo anayojutia akiwa mdogo ni kitendo cha kutojifunza lugha ya kingereza katika masomo yake wakati huo.Messi, 38, ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Argentina, amesema kuna wakati alijiona kama mjinga hasa alipokutana na watu maarufu wakati akifurahia […]

The post Messi ajuta kutojifunza Kiingereza first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Miami, Marekani
Mshambuliaji wa timu ya Inter Miami ya Marekani, Lionel Messi amesema kwamba kati ya mambo anayojutia akiwa mdogo ni kitendo cha kutojifunza lugha ya kingereza katika masomo yake wakati huo.
Messi, 38, ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Argentina, amesema kuna wakati alijiona kama mjinga hasa alipokutana na watu maarufu wakati akifurahia mafanikio katika maisha yake ya soka lakini hakuweza kuzungumza nao.
“Kuna mambo mengi ninayojuta, moja ni kutojifunza lugha ya Kiingereza wakati nikiwa kijana mdogo, nilikuwa na fursa ya kujifunza Kiingereza lakini sikufanya hivyo, najuta sana kwa hilo,” alisema Messi.
Messi alisema kwamba kuna wakati alikuwa katika mazingira ambayo alikutana na watu maarufu na wenye sifa za kipekee na ambao angeweza kuzungumza nao lakini hakuweza kufanya hivyo na mwishowe kujiona mjinga.

“Wakati wote nilikuwa nikijifikiria na kujiona mjinga, ni vipi nimepoteza muda wangu, unapokuwa mdogo huoni hilo leo ndicho kitu ninachowaambia watoto wangu, umuhimu wa elimu bora, kusoma na kujiandaa kwa lolote,” alisema Messi.


Messi alijiunga na klabu ya Barcelona akitokea kwao Argentina akiwa na miaka 13 na anakiri kwamba mwaka wake wa mwisho shuleni wakati akiwa Argentina ulikuwa wa hovyo kwani baada tu ya kumaliza shule alijiunga na akademi ya Barcelona maarufu La Masia.
Baada ya kuichezea kwa mafanikio Barcelona, Messi alijiunga na klabu ya PSG ya Ufaransa msimu wa 2020-21 na mwaka 2023 alijiunga na timu yake ya sasa ya Inter Miami inayoshiriki Ligi Kuu Marekani maarufu MLS.

The post Messi ajuta kutojifunza Kiingereza first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/26/messi-ajuta-kutojifunza-kiingereza/feed/ 0
Mechi ya Ahly, FAR Rabat yachunguzwa https://www.greensports.co.tz/2026/02/16/mechi-ya-ahly-far-rabat-kikaangoni/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/16/mechi-ya-ahly-far-rabat-kikaangoni/#respond Mon, 16 Feb 2026 15:13:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14361 Cairo, MisriShirikisho la Soka Afrika (CAF) limelaani matukio yasiyokubalika yaliyojitokeza katika mechi kati ya Al Ahly ya Misti na AS FAR Rabat ya Morocco, mechi iliyochezwa Jumapili, Februari 15, 2026 na suala hilo limefikishwa kamati ya nidhamu.Taarifa ya CAF iliyopatikana leo Jumatatu Februari 16, 2026 imeitaja mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiihusisha na […]

The post Mechi ya Ahly, FAR Rabat yachunguzwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Cairo, Misri
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limelaani matukio yasiyokubalika yaliyojitokeza katika mechi kati ya Al Ahly ya Misti na AS FAR Rabat ya Morocco, mechi iliyochezwa Jumapili, Februari 15, 2026 na suala hilo limefikishwa kamati ya nidhamu.
Taarifa ya CAF iliyopatikana leo Jumatatu Februari 16, 2026 imeitaja mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiihusisha na vitendo hivyo ingawa haikufafanua ni vitendo gani visivyokubalika vilivyojitokeza katika mechi hiyo.
Katika mechi hiyo ya Kundi B, Al Ahly wakiwa nyumbani walitoka sare ya bila kufungana na AS Rabat, mechi ambayo ilichezwa wakati Ahly wakiwa na pointi tisa na tayari walikuwa wamefuzu kucheza robo fainali.
Kwa upande wa AS Rabat ili kufuzu hatua hiyo walihitaji sare ambayo waliipata na hatimaye kufikisha pointi tisa ambazo mpinzani wao mkuu Yanga hakuweza kuzipata licha ya kupata ushindi mnono wa mabao 3-0 mbele ya JS Kablylie.
Kabla ya mechi hizo za mwisho za kundi hilo, Yanga walikuwa na pointi tano na AS Rabat pointi nane, matarajio ya Yanga yalikuwa ni Ahly ambao ni vinara wa kundi hilo wangepata ushindi na Yanga kumshinda Kabylie.
Matarajio hayo hata hivyo yalikwamishwa na matokeo ya sare ya Al Ahly na AS Rabat na kuufanya ushindi wa Yanga wa mabao 3-0 mbele ya JS Kabylie usiwe na maana yoyote kwa kuwa AS Rabat amefikisha pointi tisa.
Baadhi ya mashabiki hasa wanaoaminika kuwa wa Yanga walianza kutilia shaka mwenendo wa mechi ya AS Rabat na Ahly wengi wao wakiamini kuwa haikuwa na ushindani uliotarajiwa.
CAF katika taarifa yake ilieleza kuwa suala hilo limepelekwa kwenye kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo kwa ajili ya uchunguzi na hatua zitachukuliwa kwa wote watakaobainika kuhusika katika vitendo hivyo.

The post Mechi ya Ahly, FAR Rabat yachunguzwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/16/mechi-ya-ahly-far-rabat-kikaangoni/feed/ 0
Gamondi asaini miaka 2 Taifa Stars https://www.greensports.co.tz/2026/02/16/gamondi-asaini-miaka-2-taifa-stars/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/16/gamondi-asaini-miaka-2-taifa-stars/#respond Mon, 16 Feb 2026 14:34:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14357 Na mwandishi wetuKocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Miguel Gamondi, hatimaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu hiyo baada ya kuwa kocha wa muda kwa takriban miezi mitatu sasa.Hafla ya utiaji saini mkataba huo kati ya Gamondi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilifanyika leo Jumatatu Februari 16, 2026 jijini Dar […]

The post Gamondi asaini miaka 2 Taifa Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Miguel Gamondi, hatimaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu hiyo baada ya kuwa kocha wa muda kwa takriban miezi mitatu sasa.
Hafla ya utiaji saini mkataba huo kati ya Gamondi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilifanyika leo Jumatatu Februari 16, 2026 jijini Dar es Salaam kati ya Gamondi na Rais wa TFF, Walace Karia.
Miongoni mwa wageni waalikwa katika hafla hiyo ni Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda ambaye alithibitisha kuwa mshahara wa kocha huyo utalipwa na serikali akifafanua kuwa huo ni mojawapo ya uwekezaji wa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye michezo.
Mara baada ya kusaini mkataba huo, Gamondi akionekana mwingi wa furaha alisema kwamba mkataba huo ni heshima kwake lakini pia ni changamoto ambayo ameahidi kukabiliana nayo.
Gamondi ambaye ana uzoefu wa soka la Afrika kwa zaidi ya miaka 20 pia ahidi kutumia nguvu zake kuijenga Taifa Stars isiyoogopa na yenye uwezo wa kupambana na timu bora za Afrika.

“Hili ni jukumu kubwa lakini niko tayari kulikabili, tukiwa wamoja na tukifata ushirikiano kutoka kwa wadau wote naamini tunaweza kupata matokeo yatakayowafanya Watanzania wawe na cha kujivunia,” alisema Gamondi.


Gamondi ambaye kwa hapa Tanzania amewahi kuzinoa timu za Yanga na Singida BS pia alitumia fursa hiyo kuipongeza serikali kwa uwekezaji katika soka pamoja na TFF kwa namna inavyowajibika kusukuma mbele maendeleo ya soka.

The post Gamondi asaini miaka 2 Taifa Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/16/gamondi-asaini-miaka-2-taifa-stars/feed/ 0
Droo ligi ya mabingwa Jumanne https://www.greensports.co.tz/2026/02/16/droo-ligi-ya-mabingwa-jumanne/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/16/droo-ligi-ya-mabingwa-jumanne/#respond Mon, 16 Feb 2026 14:32:36 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14354 Cairo, MisriDroo ya timu nane zitakazocheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itafanyika kesho Jumanne Februari 17, 2026 kwenye ofisi za Chama cha Soka Misri (EFA) mjini Cairo, Misri.Droo hiyo itakayofanyika majira ya mchana itahusisha timu nane zitakazocheza hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kwa ajili ya kuzipata timu nne zitakazoumana katika hatua […]

The post Droo ligi ya mabingwa Jumanne first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Cairo, Misri
Droo ya timu nane zitakazocheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itafanyika kesho Jumanne Februari 17, 2026 kwenye ofisi za Chama cha Soka Misri (EFA) mjini Cairo, Misri.
Droo hiyo itakayofanyika majira ya mchana itahusisha timu nane zitakazocheza hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kwa ajili ya kuzipata timu nne zitakazoumana katika hatua ya nusu fainali.
Tukio hilo litarushwa moja kwa moja kwenye vyombo mbalimbali vya habari vikiwamo vile vya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuanzia YouTube Channel, CAF TV na mitandao yote ya jamii iliyo chini ya CAF.
Timu zitakazohusika katika droo hiyo ni Esperance ya Tunisia, AS FAR Rabat na RS Berkane za Morocco, Al Hilal ya Sudan, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Stade Malien ya Angola, Al Ahly na Pyramids za Misri,

The post Droo ligi ya mabingwa Jumanne first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/16/droo-ligi-ya-mabingwa-jumanne/feed/ 0
Yanga yaaga kibabe ligi ya mabingwa https://www.greensports.co.tz/2026/02/15/yanga-yaaga-ligi-ya-mabingwa-kibabe/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/15/yanga-yaaga-ligi-ya-mabingwa-kibabe/#respond Sun, 15 Feb 2026 19:45:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14347 Na mwandishi wetuYanga kama walivyo mahasimu wake Simba wote wameishia hatua ya makundi ligi ya mabingwa Afrika msimu wa 2025-26 huku Yanga ikiishia hatua hiyo kibabe kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Kabylie ya Algeria.Matokeo ya mchezo huo wa Kundi B uliopigwa leo Jumapili Februari 15, 2026 Uwanja wa Amaan, Zanzibar, bado hayakuweza […]

The post Yanga yaaga kibabe ligi ya mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga kama walivyo mahasimu wake Simba wote wameishia hatua ya makundi ligi ya mabingwa Afrika msimu wa 2025-26 huku Yanga ikiishia hatua hiyo kibabe kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Kabylie ya Algeria.
Matokeo ya mchezo huo wa Kundi B uliopigwa leo Jumapili Februari 15, 2026 Uwanja wa Amaan, Zanzibar, bado hayakuweza kuibeba Yanga kwani licha ya kufikisha pointi nane, imezidiwa pointi moja na AS FAR Rabat ya Morocco.
Rabat ambayo nayo leo ilikuwa uwanjani dhidi ya Al Ahly ya Misri imetoka sare ya bila kufungana, matokeo ambayo yametosha kuifanya Rabat iungane na Al Ahly yenye pointi 10 ambayo pia ndio kinara wa kundi hilo.
Ushindi wa Yanga ulianza kupatikana dakika ya 38 kwa bao la Depú alilofunga kwa mkwaju wa penalti ambayo ilitolewa na mwamuzi baada ya Pacome Zouzoua kuchezewa rafu.
Kipindi cha pili Yanga waliongeza kasi ya mashambulizi na kuandika bao la pili dakika ya 62 mfungaji akiwa Depu tena safari hii akiruka juu na kuuwahi mpira wa kona kabla ya kuujaza wavuni kwa kichwa.
Dakika zisizozidi tatu baada ya bao hilo, Yanga waliongeza bao la tatu na la mwisho lililofungwa na beki wa kushoto wa timu hiyo, Shadrack Boka akiitumia vizuri pasi ya Prince Dube.
Wawakilishi wengine wa Tanzania Azam FC nao wameaga rasmi michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kushindwa kutamba ugenini wakichapwa mabao 2-0 na Waydad ya Morocco.
Baada ya Azam na Yanga kukwama, Tanzania sasa inabaki bila mwakilishi katika michuano ya klabu barani Afrika kwa msimu huu wa 2025-26 na sasa timu hizo zinapaswa kuanza hesabu za msimu ujao wa 2026-27.

The post Yanga yaaga kibabe ligi ya mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/15/yanga-yaaga-ligi-ya-mabingwa-kibabe/feed/ 0