Hollywood - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 09 Oct 2023 07:46:58 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Hollywood - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Miaka 27 ya utata wa kifo cha 2Pac https://www.greensports.co.tz/2023/10/09/miaka-27-ya-utata-wa-kifo-cha-2pac/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/09/miaka-27-ya-utata-wa-kifo-cha-2pac/#respond Mon, 09 Oct 2023 07:46:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8019 New York, MarekaniWiki mbili baada ya maadhimisho ya miaka 27 ya kifo cha aliyekuwa rapa wa Marekani, Tupac Shakur ‘2Pac’, idara ya polisi nchini humo ilimkamata mtuhumiwa namba moja wa mauaji hayo, Duane ‘Keffe D’ Davis.Keffe, 60 amekamatwa na kuelezwa kuwa miongoni mwa waliopanga njama za kumuua 2Pac aliyepigwa risasi usiku wa Septemba 7 kabla […]

The post Miaka 27 ya utata wa kifo cha 2Pac first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Wiki mbili baada ya maadhimisho ya miaka 27 ya kifo cha aliyekuwa rapa wa Marekani, Tupac Shakur ‘2Pac’, idara ya polisi nchini humo ilimkamata mtuhumiwa namba moja wa mauaji hayo, Duane ‘Keffe D’ Davis.
Keffe, 60 amekamatwa na kuelezwa kuwa miongoni mwa waliopanga njama za kumuua 2Pac aliyepigwa risasi usiku wa Septemba 7 kabla ya kufariki Septemba 13, 1996 baada ya damu kuvuja ndani kwa ndani kutokana na majeraha ya risasi hizo.
Hata hivyo, wakati kesi hiyo sasa inaibuka upya, kifo cha 2Pac kimeendelea kuhusishwa na mambo mengi ikiwemo ‘bifu’ mbalimbali alizokuwa nazo enzi za uhai wake.
Mfano, Keffe amekamatwa akiunganishwa kwenye kisanga kilichomhusisha mpwa wake, Orlando ‘Baby Lane’ Anderson ambaye kamera za ukumbi wa MGM Grand, Las Vegas zilimnasa akizozana na kina 2Pac muda mchache kabla ya kifo cha rapa huyo.
2Pac aliyekuwa akifanya kazi zake California, alikwenda Las Vegas, Nevada kwenye sherehe ya mshirika wake kibiashara, Tracy Robinson sanjari na kuhudhuria pambano la swahiba wake, Mike Tyson dhidi ya Bruce Seldon.
Lakini ghafla washirika wa bosi wa 2Pac, Suge Knight walipomwona Baby Lane eneo hilo walimwambia 2Pac kuwa jamaa huyo alijaribu kuwapora mwanzoni mwa mwaka huo na ndipo mzozo ulipoanza baina yao.
Baadaye 2Pac alirudi hotelini kwake, akajiandaa na kuondoka na Suge kuelekea kwenye klabu ya usiku, lakini wakiwa wamesimama katika barabara ya East Flamingo, ikaja gari aina ya Cadillac na kusimama upande aliokuwa amekaa 2Pac na kisha kumfyatulia risasi.
Risasi nne, moja mkononi, moja kwenye paja na mbili za kifua zilimpiga 2Pac, ambaye aliwahishwa hospitali na baada ya siku sita, alitangazwa kuaga dunia akiwa na miaka 25.
Polisi inadai kuwa Keffe, alikuwemo katika Cadillac hiyo iliyotekeleza mauaji hayo yaliyoihuzunisha tasnia nzima ya muziki duniani.
P. Diddy, The Notorious B.I.G
Licha ya Baby Lane ambaye naye aliuawa mwaka 1998 akiwa na miaka 23 kutajwa mno kwenye kifo hicho, lakini chuki baina ya West Coast ya Suge na East Coast chini ya Sean Combs ‘Diddy’ ilitajwa kuwa chanzo cha mauaji ya 2Pac.
Diddy aliyekuwa akimsimamia Christopher Wallace ‘B.I.G’ kupitia Lebo ya Bad Boys walitajwa kutokana pia na ugomvi wao wa awali.
B.I.G au Biggie Smalls alikuwa rafiki wa 2Pac kabla ya baadaye kuhitilafiana. Mwaka 1995, 2Pac aliliambia Jarida la Vibe kuwa Biggie alihusika aliposhambuliwa na kupigwa risasi Novemba 1994 alipokuwa mapokezi ya studio kwa ajili ya kwenda kurekodi.
2Pac alikwenda Quad Studio (Biggie na Diddy walikuwepo ndani) kurekodi ubeti kwa maelewano ya ujira wa Dola za Marekani 7,000 na mtayarishaji James Rosemond.
Akiwa mapokezi, alivamiwa na watu asiowajua ambao walimwibia na kumtishia, alipojaribu kupambana nao aliishia kupigwa risasi takriban tano lakini aliwahishwa hospitali na baadae kupona kabisa.
Tukio hilo liliongeza chuki baina yao ambapo baada ta Biggie kusikia amehusishwa na tukio hilo, aliamua kurekodi wimbo ulioitwa Who Shot Ya?
2Pac alikasirika mno, akitasfiri wimbo huo ni kama umemdhihaki na ndipo alipotengeneza wimbo wa Hit ‘Em Up unaotajwa kuwa wimbo bora zaidi wa Hip Hop wa ‘ku-diss’, ambapo aliwataja kwa majina maadui zake akilijumuisha pia Kundi la Junior M.A.F.I.A lililokuwa likiundwa na Lil Kim na Lil Cease wakati huo.
Mpaka leo, baadhi ya wadau wanaamini kifo cha 2Pac kilitokana na bifu hilo kabla ya kugongelewa muhuri kutokana na kifo cha Biggie akiwa California kwenye gari barabarani, gari aina ya Chevrolet ilimsogelea na kumfyatulia risasi.
Licha ya juhudi za madaktari usiku wa Machi 8 kuhangaikia uhai wake lakini Machi 9, 1997 ikatangazwa kuwa Biggie ameiaga dunia akiwa na miaka 24!
Mamlaka za juu Marekani
Ingawa hakujawahi kuwa na uthibitisho wa moja kwa moja lakini wanazi wa muziki wa 2Pac kutoka Marekani wamekuwa wakizitaja mamlaka za juu za nchi hiyo kama sehemu ya kumpoteza 2Pac.
Iko hivi, mpaka leo 2Pac au Makaveli anakumbukwa kwa uanaharakati wake dhidi ya uonevu wa mamlaka kwa jamii na mambo mengi yanayokinzana na maendeleo ya binadamu wa hali ya chini.
Nyimbo zake nyingi zililenga kufundisha, kuonya na kukanya juu ya hayo. Hata alipotoa albamu yake ya kwanza ya 2Pacalypse Now, aliyekuwa Makamu wa Rais Marekani wakati huo, Dan Quayle alisema hakukuwa na sababu ya kuachiwa kwa albamu kama hiyo akidai haina nafasi katika jamii.
Lakini 2Pac hakuwahi kusikia wala kuelewa juu ya makatazo hayo na ni kwa sababu alizaliwa chini ya wanaharakati, wakati huo marehemu mama yake, Afeni Shakur alikuwa na cheo kikubwa katika Chama cha Black Panther kilichokuwa kikipigania haki za mtu mweusi.
Pia alikuzwa vyema kiunaharakati na ‘Godfather’ wake, Geronimo Pratt ambaye alifariki akiwa Arusha, Tanzania mwaka 2011.
2Pac aliwahi kuingia kwenye mgogoro wa kupigana risasi na polisi akiwa Atlanta mwaka 1993, tukio lililohusishwa na ukosoaji wake mkubwa dhidi ya serikali.
Ilielezwa kuwa, 2Pac alikorofishana na polisi wawili ndugu; Mark na Scott Whitwell walipokuwa na wake zao siku ya mapumziko wakivuka barabara.
Ingawa kila upande ulijitetea kivyake lakini mashahidi wa tukio hilo waliiambia idara ya polisi kuwa kina Whitwell ndio walioanza kuwachokoza kina 2Pac na kuwafanyia vitendo vya kibaguzi.
Na walipoanza kuzozana polisi hao ndio walioanza kurusha risasi kabla ya 2Pac kujibu mapigo na kuwajeruhi polisi hao. Japokuwa kesi hiyo ilimalizwa lakini Mark aliamua kuacha kazi miezi saba baada ya tukio hilo.
Albamu ya mwisho
The Don Killuminati: The 7 Day Theory ya Novemba, 1997 ndio ilikuwa albamu ya mwisho kutengenezwa na 2Pac akiwa hai na ndipo alipoamua pia kufanya maamuzi ya kujitambulisha rasmi kama Makaveli.
Makaveli ni jina lililotoholewa kutoka kwa mwanasiasa wa Italia, Niccolo Machiavelli ambapo 2Pac alivutiwa na falsafa za Machiavelli alipokuwa akisoma vitabu vyake wakati yupo jela.
Inaelezwa albamu hiyo iliyotungwa na kuandikwa kwa siku tatu tu kabla ya kurekodiwa ndani ya siku nne, ilikuwa na ukosoaji dhidi ya jamii za siri za dini na hilo pia linatajwa kuwa miongoni mwa chuki nyingine za kimya kimya dhidi ya 2Pac ingawa wakati inatoka rasmi 2Pac alikuwa ameshafariki.
Upande wa wanaoamini kuwa 2Pac yuko hai amejificha sehemu, wanaeleza kuwa 2Pac aliiga mtindo wa Machiavelli aliyewahi kubuni kifo chake wakati huo.
Hakuna Tupac aliyezidi miaka 45
Kama ulikuwa hufahamu, jina halisi la 2Pac ni Lesane Parish Crooks lakini alipofikisha mwaka mmoja wazazi wake rasmi wakamwita Tupac Amaru Shakur akirithi jina la Tupac Amaru II aliyekuwa mwanamapinduzi wa Peru dhidi ya watawala Uhispania.
Amaru II aliuawa mwaka 1781 akiwa na miaka 43 kama alivyouawa Mfalme wa Inca (sasa Peru), Tupac Amaru mwaka 1572 akiwa na miaka 24 tu!
Tangu kifo cha 2Pac au MC New York kama alivyokuwa akitambulika miaka ya 1989 akiwa msanii chipukizi, hajasikika Tupac Amaru mwingine maarufu mpaka sasa.

The post Miaka 27 ya utata wa kifo cha 2Pac first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/09/miaka-27-ya-utata-wa-kifo-cha-2pac/feed/ 0
Kim Kardashian: Messi, Ronaldo wote safi https://www.greensports.co.tz/2023/07/26/kim-kardashian-messi-ronaldo-wote-safi/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/26/kim-kardashian-messi-ronaldo-wote-safi/#respond Wed, 26 Jul 2023 19:19:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7132 New York, MarekaniStaa wa vipindi vya televisheni, Kim Kardashian (pichani) amejitenga na mjadala wa nani zaidi kati ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi baada ya kuwasifia wanasoka hao wawili alipoulizwa nani zaidi ya mwenzake.Katika tukio lililoonekana si la kawaida, Kim ambaye pia ni mfanyabiashara, Jumamosi iliyopita alionekana kwenye Uwanja wa DRV PNK akimshuhudia nyota mpya […]

The post Kim Kardashian: Messi, Ronaldo wote safi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Staa wa vipindi vya televisheni, Kim Kardashian (pichani) amejitenga na mjadala wa nani zaidi kati ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi baada ya kuwasifia wanasoka hao wawili alipoulizwa nani zaidi ya mwenzake.
Katika tukio lililoonekana si la kawaida, Kim ambaye pia ni mfanyabiashara, Jumamosi iliyopita alionekana kwenye Uwanja wa DRV PNK akimshuhudia nyota mpya wa Inter Miami ya Marekani, Messi akiiwakilisha timu yake dhidi ya Cruz Azul na kufunga bao katika ushindi wa 2-1.
Siku tatu baadaye, Kim alisafiri hadi Osaka, Japan kwenye Uwanja wa Yanmar kumshuhudia nyota mwingine wa soka, Ronaldo ambaye timu yake ya Al Nassr ya Saudi Arabia ilikuwa ikiumana na PSG ya Ufaransa katika mechi ya kirafiki ingawa Ronaldo hakufunga bao katika mechi hiyo.
Kabla ya kuanza kwa mechi hiyo, Kim aliulizwa swali la haraka haraka kwamba nani anamkubali zaidi kati ya Messi na Ronaldo ambapo alijibu kwa kifupi, ‘wote’ kabla ya kuanza kucheka.
Wakati akimshuhudia Messi, Kim aliambatana na mtoto wake ambaye alikuwa amevaa jezi namba 10 inayotumiwa na Messi katika klabu ya Inter Miami na baadaye alionekana akiwa ametulia na David Beckham na mkewe Victoria.
Kitendo cha Kim kuonekana uwanjani akiwashuhudia mastaa hao kimeonekana kuwavutia watu wengi hasa kwenye mitandao ya kijamii.

The post Kim Kardashian: Messi, Ronaldo wote safi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/26/kim-kardashian-messi-ronaldo-wote-safi/feed/ 0
Rapa Big Pokey afariki jukwaani https://www.greensports.co.tz/2023/06/22/rapa-big-pokey-afariki-jukwani/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/22/rapa-big-pokey-afariki-jukwani/#respond Thu, 22 Jun 2023 14:40:49 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6674 New York, MarekaniRapa Big Pokey (pichani) wa Marekani amefariki dunia jukwaani wakati akiwa kwenye onesho la muzuki katika ukumbi mmoja wa burudani Jumapili hii mjini mjini Texas.Big Pokey mwenye umri wa miaka 48 ambaye jina lake halisi ni Milton Powell mara baada ya kuzidiwa alikimbizwa hospitali kabla ya kubaika kwamba amefariki wakati juhudi za kumpatia […]

The post Rapa Big Pokey afariki jukwaani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Rapa Big Pokey (pichani) wa Marekani amefariki dunia jukwaani wakati akiwa kwenye onesho la muzuki katika ukumbi mmoja wa burudani Jumapili hii mjini mjini Texas.
Big Pokey mwenye umri wa miaka 48 ambaye jina lake halisi ni Milton Powell mara baada ya kuzidiwa alikimbizwa hospitali kabla ya kubaika kwamba amefariki wakati juhudi za kumpatia matibabu zikiendelea.
Awali Big Pokey alikuwa mmoja wa wasanii waliounda kundi la Screwed Up Click lakini alifahamika zaidi kupitia albamu yake ya kwanza ya ‘Hardest Pit in the Litter’ iliyotoka mwaka 1999.
Baada ya hapo, Big Pokey aliendelea kukimbiza kwenye gemu na kufanikiwa kutoa albamu tano ikiwamo ya hivi karibuni ya ‘Sensei’ aliyoitoa mwaka 2021.
Awali taarifa za kifo cha Big Pokey zilitolewa na rapa mwenzake Bun B ambaye alitumia mtandao wa Instagram kutoa taarifa za kifo hicho.

“Mmoja wa wasanii wenye kipaji asili mjini, asiye na makuu, mtu muungwana ambaye anakwenda na utu na heshima zake, ni mtu rahisi kumpenda na vigumu kumchukia,” alisema Bun B akimpamba Big Pokey kabla ya kuuarifu umma kwamba mtu huyo amefariki dunia.


The post Rapa Big Pokey afariki jukwaani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/22/rapa-big-pokey-afariki-jukwani/feed/ 0
Paris Hilton apata mtoto https://www.greensports.co.tz/2023/01/26/paris-hilton-apata-mtoto/ https://www.greensports.co.tz/2023/01/26/paris-hilton-apata-mtoto/#respond Thu, 26 Jan 2023 11:44:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4865 New York, MarekaniMwanamitindo na staa wa vipindi vya televisheni,, Paris Hilton kwa sasa ni mama baada ya kujifungua mtoto wa kiume ambaye anakuwa mtoto wake wa kwanza ingawa kwa mumewe, Carter Reum anakuwa mtoto wa pili.Taarifa ya Paris kupata mtoto ilipatikana kwenye mtandao wa Instagram ambapo alionyesha picha akiwa amemshika mkono mtoto huyo na kusema, […]

The post Paris Hilton apata mtoto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Mwanamitindo na staa wa vipindi vya televisheni,, Paris Hilton kwa sasa ni mama baada ya kujifungua mtoto wa kiume ambaye anakuwa mtoto wake wa kwanza ingawa kwa mumewe, Carter Reum anakuwa mtoto wa pili.
Taarifa ya Paris kupata mtoto ilipatikana kwenye mtandao wa Instagram ambapo alionyesha picha akiwa amemshika mkono mtoto huyo na kusema, “Tayari unapendwa kuliko inavyoweza kuzungumzwa.”
Bado haijajulikana ni lini mtoto huyo alizaliwa licha ya habari za awali kudai kwamba alizaliwa Jumanne na pia jina la mtoto huyo bado halijajulikana ingawa inafahamika kuwa alipata mtoto huyo kupitia kwa mwanamke mwingine (Surrogate).
Baada ya kufunga ndoa mwaka 2021, Paris Hilton na mumewe Carter waliwahi kuzungumzia nia yao ya kuwa wazazi kwa kupitia mwanamke mwingine kama ambavyo amefanya staa wa vipindi vya televisheni, Khloe Kardashian ambaye alipata mtoto wa kiume kwa utaratibu huo huo.
Paris ndio aliyekuwa akilizungumza sana jambo hilo ambapo mara ya mwisho alisema, angependa afurahie mwaka wake wa kwanza wa ndoa lakini wakati huo huo alikuwa akijiandaa kuwa mama.
“Wakati wote imekuwa ndoto yangu muwa mama na nina furaha mimi na Carter tumekutana, tuna furaha kuianza familia pamoja na mioyo yote imegubikwa upendo kwa mtoto wetu wa kiume,” alisema Paris Hilton.
Kwa miaka kadhaa, Paris Hilton alikuwa akijaribu kufuta uvumi kwamba alikuwa na tatizo la kupata mtoto, alikuwa akiupinga uvumi huo na wakati mwingine kusisitiza kuwa yeye na mumewe wanaweka mambo sawa kwa ajili ya kupata mtoto.

The post Paris Hilton apata mtoto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/01/26/paris-hilton-apata-mtoto/feed/ 0
Lisa Marie Presley afariki dunia https://www.greensports.co.tz/2023/01/14/lisa-marie-presley-afariki-dunia/ https://www.greensports.co.tz/2023/01/14/lisa-marie-presley-afariki-dunia/#respond Sat, 14 Jan 2023 12:53:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4737 California, MarekaniMwanamuziki, Lisa Marie Presley ambaye ni mtoto pekee wa mwanamuziki gwiji wa zamani Elvis Presley na mkewe Priscilla Presley, amefariki akiwa na miaka 54 baada ya kukimbizwa hospitali.Kifo cha mwanamuziki hiyo kilithibitishwa na mama yake, Priscilla mwenye umri wa miaka 77 ambaye alisema kwamba mtoto wake alifariki Alhamisi usiku baada ya kuugua. “Ni kwa […]

The post Lisa Marie Presley afariki dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

California, Marekani
Mwanamuziki, Lisa Marie Presley ambaye ni mtoto pekee wa mwanamuziki gwiji wa zamani Elvis Presley na mkewe Priscilla Presley, amefariki akiwa na miaka 54 baada ya kukimbizwa hospitali.
Kifo cha mwanamuziki hiyo kilithibitishwa na mama yake, Priscilla mwenye umri wa miaka 77 ambaye alisema kwamba mtoto wake alifariki Alhamisi usiku baada ya kuugua.

“Ni kwa masikitiko makubwa nalazimika kutoa taarifa zisizo nzuri kwamba mwanangu mpendwa Lisa Marie hatuko naye,” alisema Priscilla katika taarifa yake.


“Alikuwa mtulivu na mwenye upendo wa kipekee sijawahi kuona, tunaomba utulivu na kuwa na mambo binafsi ya ndani wakati tukikabiliana na msiba huu mkubwa, asanteni kwa upendo na maombi, kwa wakati huu hakutakuwa na maoni zaidi,” aliongeza.
Lisa alikimbizwa hospitali akitokea nyumbani kwake, Calabasas, California kwa kilichodaiwa kuwa ni matatizo ya moyo ambapo mama yake mara baada ya tukio hilo aliwaomba mashabiki kumjumuisha mtoto wake katika maombi yao.
Wakati baba yake anakufa mwaka 1977, Lisa alikuwa na miaka tisa na mwaka 1997 aliimba wimbo wa Dont Cry Daddy katika kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha baba yake na baadaye alifuata nyayo za baba yake katika muziki kwa kutoa albamu tatu akianza mwaka 2003 na albamu ya Whom It May Concern na mwaka 2005 albamu ya Now What na mwaka 2012 albamu ya Storm & Grace.
Lisa wakati wa uhai wake amefunga ndoa mara nne, aliolewa na mwanamuziki Danny Keough kati ya mwaka 1988 na 1994 na kuzaa watoto wawili, Riley Keough ambaye ni muigizaji filamu na Benjamin Keough ambaye alijiua mwaka 2020 akiwa na miaka 27.


Siku 20 baada ya kuachana na Keough, Lisa alifunga ndoa na Mfalme wa Pop, Michael Jackson (kama wanavyoonekana pichani) lakini waliachana baada ya miezi 18. Mwaka 2000 alichumbiwa na mwanamuziki John Oszajca lakini uchumba ulitoweka baada ya Lisa kukutana na Nicolas Cage na hatimaye kufunga naye ndoa Agosti 2002 lakini waliachana miezi mitatu baadaye Cage alipowasilisha maombi ya talaka.
Mwaka 2006, Lisa alifunga ndoa na mpiga gitaa wake, Michael Lockwood na kupata watoto mapacha wawili wa kike, Harper na Finley lakini baada ya miaka 10 ya ndoa, Lisa aliwasilisha maombi ya talaka.

The post Lisa Marie Presley afariki dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/01/14/lisa-marie-presley-afariki-dunia/feed/ 0
Rapa Takeoff auawa kwa risasi https://www.greensports.co.tz/2022/11/03/rapa-takeoff-auawa-kwa-risasi/ https://www.greensports.co.tz/2022/11/03/rapa-takeoff-auawa-kwa-risasi/#respond Thu, 03 Nov 2022 14:49:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=3559 Houston, MarekaniRapa Takeoff wa kundi maarufu la muziki wa rap la Migos, ameuawa kwa kupigwa risasi wakati akiwa kwenye sherehe binafsi kwenye ukumbi mmoja wa burudani mjini Houston, polisi wamethibitisha.Polisi walipokea taarifa za watu kurushiana risasi majira ya saa nane usiku wa Jumanne ambapo mbali na rapa huyo aliyeuawa watu wengine wawili, kijana miaka 24 […]

The post Rapa Takeoff auawa kwa risasi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Houston, Marekani
Rapa Takeoff wa kundi maarufu la muziki wa rap la Migos, ameuawa kwa kupigwa risasi wakati akiwa kwenye sherehe binafsi kwenye ukumbi mmoja wa burudani mjini Houston, polisi wamethibitisha.
Polisi walipokea taarifa za watu kurushiana risasi majira ya saa nane usiku wa Jumanne ambapo mbali na rapa huyo aliyeuawa watu wengine wawili, kijana miaka 24 na msichana wa miaka 23 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitali ingawa majeraha yao hayakuwa makubwa ya kutishia uhai wao.
Wafanyakazi wa kwenye ukumbi huo walidai kwamba mara baada ya sherehe kumalizika, kulitokea mzozo baina ya watu waliokuwa kwenye sherehe na baadaye kidogo ndipo milio ya risasi ilipoanza kusikika.
Taarifa ya polisi hata hivyo ilieleza kwamba wengi wa watu waliokuwa eneo la tukio walitawanyika na hawakuwapo kwa ajili ya kutoa taarifa rasmi kwa polisi.
Habari za kifo cha Takeoff ni pigo jingine kubwa kwa wapenzi wa muziki wa rap ambao wamekuwa wakituma salamu za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii kwani bado wanaugulia msiba wa rapa mwingine, PnB Rock ambaye naye aliuawa kwa risasi Septemba mwaka huu.
Kwa upande wake rapa mkongwe Ja Rule akizungumzia kifo cha Takeoff kupitia akaunti yake ya Twitter alisema, “Huu upuuzi ni lazima uachwe, pole kwa marafiki na wanafamilia.”
Takeoff alianza kujiingiza katika muziki wa rap akiimba na mjomba wake rapa Quavo kabla ya mwaka 2013 wakiwa chini na kundi la Migos kutoa kibao ‘Versace’ na mwaka 2016 wakaja na kibao kingine ‘Bad and Boujee’ walichomshirikisha Lil Uzi Vert na kuzidi kupata umaarufu.
Takeoff ambaye jina lake la kuzaliwa ni Kirshnik Khari Ball, alizaliwa Juni 18, 1994, Georgia Marekani na katika muziki alikuwa akifanya kazi na lebo za Motown, Quality Control Music na Capitol Records.

The post Rapa Takeoff auawa kwa risasi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/11/03/rapa-takeoff-auawa-kwa-risasi/feed/ 0
J.Lo, Ben Affleck katika mahaba moto moto https://www.greensports.co.tz/2022/09/11/j-lo-ben-affleck-katika-mahaba-moto-moto/ https://www.greensports.co.tz/2022/09/11/j-lo-ben-affleck-katika-mahaba-moto-moto/#respond Sun, 11 Sep 2022 14:35:18 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2779 New York, MarekaniNi mapenzi yanayonogeshwa na familia ya watu saba inayoundwa na wachumba waliofarakana na kutengana miaka 17 iliyopita lakini sasa wako katika mahaba moto moto. Ni mwanamuziki Jennifer Lopez au J.Lo na staa wa filamu Ben Affleck…Miaka 17 iliyopita moja ya habari kubwa ya kwenye vyombo iliyoteka hisia za wengi iliwahusu J.Lo na Ben […]

The post J.Lo, Ben Affleck katika mahaba moto moto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Ni mapenzi yanayonogeshwa na familia ya watu saba inayoundwa na wachumba waliofarakana na kutengana miaka 17 iliyopita lakini sasa wako katika mahaba moto moto. Ni mwanamuziki Jennifer Lopez au J.Lo na staa wa filamu Ben Affleck…
Miaka 17 iliyopita moja ya habari kubwa ya kwenye vyombo iliyoteka hisia za wengi iliwahusu J.Lo na Ben Afflek, kila walipokwenda, kila walilolifanya lilikuwa habari na hatimaye wakabatizwa jina la Super Couple.
Uchumba huo ulipambwa na tukio la mwishoni mwa mwaka 2002, Ben Affleck alipoamua kumvisha J.Lo pete ya uchumba iliyong’arishwa kwa madini ya almasi, hiyo ikiwa ni baada ya wawili kuiteka dunia wakihusishwa kuigiza pamoja filamu ya Gigli.
Baadaye katika mahojiano aliyowahi kufanya na mwandishi mmoja wa habari, J.Lo alimzungumzia Affleck akisema, “Ni mtu makini, mwenye upendo, mcheshi na anavutia, yaani navutiwa naye kwa kila namna.
Ivumayo haidumu, wakati mashabiki wao wakisubiri ndoa ya wawili hao kwa shauku kubwa, shauku iliyochangiwa na namna walivyopambwa na vyombo vya habari, ghafla wakatoa taarifa ya kufuta mpango wa ndoa iliyokuwa ifungwe Santa Barbara, California, mwishoni mwa mwaka 2003, sababu kubwa ni kero waliyokuwa wakiipata kwa kufuatiliwa kila hatua ya maisha yao na wanahabari.
Kila walipokwenda, kila hoteli waliyofikia, kila walichokula, walichokunywa, nguo walizovaa na mengineyo, vyote viligeuzwa habari, hawakuwa na muda wa kufanya mambo yao binafsi kwa uhuru, kila tukio lao liliambatana na picha na kuwa habari kubwa. Jambo hili inadaiwa liliwakera lakini zaidi lilimkera J.Lo.
Taarifa yao ilisomeka. “Kwa namna ambavyo ndoa yetu inachunguzwa na kufuatiliwa na vyombo vya habari, tumeamua kuahirisha siku ya ndoa, tukiwa katika maandalizi tumebaini kwamba kuna jambo lisilo zuri, tunaona ile fikra ya hii kuwa siku ya furaha zaidi katika maisha yetu inaweza iwe sivyo, tunaona lile jambo zuri na la kipekee linaweza kuvurugwa kwa upande wetu, familia na marafiki zetu.”

Wakati umma ukisubiri siku nyingine ya ndoa, ulijikuta ukishtukizwa na habari nyingine tofauti, J.Lo na Ben Affleck, Januari 2004 kila mmoja akatoa taarifa ya kutengana kwao rasmi na huo ukawa mwanzo na mwisho wa ndoa tarajiwa na uchumba wa Ma-Super Couple.
Taarifa ya Ben Affleck hata hivyo ilionyesha kwamba pamoja na kuachana bado kulikuwa na upendo baina yao pale aliposema, “Sitazungumza chochote kuhusu maisha yake binafsi, kila mtu anataka vita, bahati mbaya hilo kwa upande wetu halitotokea.” Na hivyo ndivyo ilivyokuwa pamoja na kuachana hakuna kati yao aliyeibuka na kuanza kuchambua hadharani maisha binafsi ya mwenzake.
Kilichofuata kila mmoja akashika lake, Ben Affleck akafunga ndoa na Jennifer Garner na kupata watoto watatu wakati J.Lo naye akafunga ndoa na mwanamuziki mwenzake Marc Anthony na kupata watoto mapacha. Wote baadaye wakajikuta wakiacha na kuachwa, Ben Affleck akaachana na Jennifer Garner na J.Lo akaachana na Marc Anthony, wote wakaingia katika mahusiano mengine tofauti tofauti.
Miaka 17 na miezi kadhaa imepita sasa, J.Lo na Ben Affleck wamerudiana, si kama wachumba tu bali wameamua kufunga ndoa ambayo iliwatia unyonge kwa kuikosa na jambo la kufurahisha ni kwamba sasa wanaunda familia ya watu saba inayounganishwa na watoto watano.
Kwa kurudiana na hatimaye kufunga ndoa, J.Lo sasa anakuwa mama wa kambo wa watoto watatu wa mumewe ambao ni Violet, Samuel na Seraphina, watoto ambao Ben Affleck amezaa na aliyekuwa mkewe ambaye pia ni mcheza filamu, Jennifer Garner.
Ben Affleck naye anakuwa baba wa kambo wa watoto wawili wa J.Lo, watoto ambao J.Lo amezaa na aliyekuwa mumewe, Marc Anthony, watoto hao mapacha ni Emme na Maximilian.

Kuna mambo mawili yanayojidhihirisha katika familia hiyo, moja ni upendo, J.Lo mara kadhaa ameonekana akiwa na mtoto wa Ben Affleck, Violet Affleck kama vile ndiye mtoto wake wa kumzaa, ni hivyo hivyo kwa Ben Affleck naye anaona ufahari kutanua na watoto wa J.Lo.
Nje ya upendo huo kuna mahaba, wanachokifanya J.Lo na Ben Affleck kwa sasa ni kama kudhihirisha kwamba kuvunjika kwa uchumba na ndoa yao ni jambo walilolikubali kwa shingo upande, mazingira yaliwafanya kufikia hatua hiyo, J.Lo kwa sasa ana miaka 53 na Ben Affleck ana miaka 50 lakini ukiwaona huwezi kuwatofautisha na ile Super Couple iliyovunjika miaka 17 iliyopita.
Popote wanapokuwa hawaoni tabu kudhihirisha mahaba yao, watashikana na kutomasana na kufanya kila wanachoona sahihi kwa kila mmoja kudhihirisha anavyompenda na kumzimia mwenzake.
Walianza kuonekana mwaka jana wakiwa Montana katika hoteli moja ya kifahari na kwa wakati wote kila mmoja alionekana kujitahidi kuonyesha namna alivyokuwa akimhitaji mwenzake, matukio ambayo yanaendelea kujidhihirisha kila wanapokuwa.

The post J.Lo, Ben Affleck katika mahaba moto moto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/09/11/j-lo-ben-affleck-katika-mahaba-moto-moto/feed/ 0
Mke wa Rambo adai talaka https://www.greensports.co.tz/2022/08/24/mke-wa-rambo-adai-talaka/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/24/mke-wa-rambo-adai-talaka/#respond Wed, 24 Aug 2022 19:40:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2547 New York, MarekaniWakati staa wa filamu, Sylvester Stallone au Rambo akifunga ndoa na mwanamitindo Jennifer Flavin mwaka 1997, Rambo alikuwa na miaka 51 na Jennifer alikuwa na miaka 22, leo hii ndoa yao ya miaka 25 au robo karne inavunjika Rambo akiwa na miaka 76 na Jennifer 54.Jennifer amewasilisha mahakamani madai ya talaka Ijumaa iliyopita, […]

The post Mke wa Rambo adai talaka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Wakati staa wa filamu, Sylvester Stallone au Rambo akifunga ndoa na mwanamitindo Jennifer Flavin mwaka 1997, Rambo alikuwa na miaka 51 na Jennifer alikuwa na miaka 22, leo hii ndoa yao ya miaka 25 au robo karne inavunjika Rambo akiwa na miaka 76 na Jennifer 54.
Jennifer amewasilisha mahakamani madai ya talaka Ijumaa iliyopita, madai ambayo pia yameambatanishwa na tuhuma dhidi ya Rambo kwamba ameanza kuhamisha mali ambazo kimsingi zinapaswa kuwa zao wakiwa mume na mke.
Katika madai yake, Jennifer anataka apewe umiliki wa mjengo wao uliopo Palm Beach kabla kesi ya madai yake ya talaka haijaanza kusikilizwa.
Jennifer ambaye mumewe amejipatia umaaufu kwa filamu mbalimbali za Hollywood zikiwamo First Blood na Rocky, katika madai yake pia ameeleza, “Kutokana na taarifa alizonazo na anachoamini, mumewe ameanza kuzihujumu, kuzipunguza au kuzifuja mali hizo jambo ambalo litakuwa na madhara kwa mali zao kiujumla.”
Kwa mantiki hiyo ametaka mahakama imzuie mumewe kuziuza, kuzipunguza, kuhamisha umiliki au kuzifanyia hujuma mali hizo wakati huu kesi ikiwa mahakamani.
Madai ya Jennifer kutaka kuachana na Rambo yamekuja wakati tayari kukiwa na uvumi kwamba ndoa hiyo ilikuwa juu ya mawe baada ya Rambo kuonekana akiwa na mchoro wa tattoo ya mbwa wake mkononi sehemu ambayo awali ilikuwa na mchoro wa tattoo ya Jennifer.
Kilichoonekana kama ni kujibu mapigo, Jennifer naye akaacha kum-follow Rambo kwenye mtandao wa Instagram na baadaye kuweka picha kwenye akaunti yake ya mtandao huo huo akiwa na watoto wao watatu wa kike na kuandika maneno yafuatayo, “Hawa wasichana ndio kila kitu kwangu, hakuna kingine ninachojali, ni sisi wanne hadi mwisho.”
Timu ya PR ya Rambo hata hivyo imekanusha wawili hao kuwa na tatizo badala yake wamesema ni tofauti za kawaida na kuhusu tattoo walidai kwamba alichotaka kufanya Rambo ni kuuboresha mchoro huo wa mkewe lakini ikashindikana na ndio akaamua kuweka mchoro wa mbwa na kwamba bado anaipenda familia yake.
Rambo na Jennifer walifunga ndoa mwaka 1997 katika jiji la London katika Hoteli ya Dorchester, mwaka huu walisherehekea miaka 25 ya ndoa hiyo ambapo Rambo alimsifia mkewe akisema ni mwanamke wa kipekee na asiye mbinafsi wakati Jennifer naye aliisifia ndoa yao akisema inakuwa bora kila mwaka na shauku yake ni kufurahia maisha yao yote wakiwa pamoja.

The post Mke wa Rambo adai talaka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/24/mke-wa-rambo-adai-talaka/feed/ 0
Britney Spears ateswa na maisha ya anasa https://www.greensports.co.tz/2022/08/24/britney-spears-ateswa-na-maisha-ya-anasa/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/24/britney-spears-ateswa-na-maisha-ya-anasa/#respond Wed, 24 Aug 2022 09:17:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2531 New York, MarekaniMsanii wa pop, Britney Spears amesema kwamba ataendelea kuteswa na matukio yake ya miaka ya nyuma ikiwamo ulevi na kila aina ya anasa na anaamini hakuna namna ya kumaliza hali hiyo labda iwe ni kwa njia ya miujiza.Britney ameendelea kufunguka kuhusu maisha yake ya nyuma ambapo kupitia akaunti yake ya Instagram, msanii huyo […]

The post Britney Spears ateswa na maisha ya anasa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Msanii wa pop, Britney Spears amesema kwamba ataendelea kuteswa na matukio yake ya miaka ya nyuma ikiwamo ulevi na kila aina ya anasa na anaamini hakuna namna ya kumaliza hali hiyo labda iwe ni kwa njia ya miujiza.
Britney ameendelea kufunguka kuhusu maisha yake ya nyuma ambapo kupitia akaunti yake ya Instagram, msanii huyo ameelezea ni kwa vipi kuna mambo ambayo hayawezi kumsahaulisha matukio yake ya miaka ya nyuma na kwa nini aliamua kutupia picha na video zake kwenye mitandao huku akidai kwamba anaamini sasa ana muonekano mzuri.
“Kila mtu maisha yake yanaonekana yako sawa, na ninapotupia picha na habari mitandaoni nafikiri kwa muda mwingi, huwa nateswa na kusumbuliwa na maisha yangu ya siku za nyuma, nani anayeweza kusahau mambo ya siku za nyuma, ndio najaribu kutupia picha zangu nikiwa katika muonekano mzuri au kile kinachoonekana kuwa ni maisha mazuri,” alisema Britney.
“Ni kweli sasa niko vizuri kifikra lakini nitaendelea kuteswa na uzoefu wa maisha yangu ya siku za nyuma, sina namna ya kutatua hilo fikra zangu zinateswa na jambo hilo, nafikiri nitahitaji miujiza ya kumaliza jambo hili,” alisema msanii huyo mwenye umri wa miaka 40 sasa na kuongeza kwamba hadi sasa huwa analia peke yake wakati akilala na huwa anakosa amani.
Britney akiwa mwenye mafanikio katika muziki hasa miaka ya 2000 mwishoni aliingia katika utumiaji madawa ya kulevya na anasa za kila aina hadi akawekewa zuio na mahakama kwa takriban miaka 13 ikiwamo kuzuiwa kulea watoto wake, kuanzisha familia mpya na kunyimwa usimamizi wa fedha zake, mmoja wa wasimamizi aliyepewa jukumu na mahakama akiwa ni baba yake, Jamie Spears.
Jamie Spears na wasimamizi wengine hata hivyo inadaiwa sasa wanachunguzwa kwa amri ya mahakama akidaiwa kukiuka taratibu za usimamizi wa msanii huyo.
Tangu mahakama ifute zuio hilo Novemba mwaka jana na Britney kupewa uhuru kujiamulia mambo yake mwenyewe, msanii huyo alifunga ndoa na rafiki yake wa zamani, Sam Asghari na pia akishirikiana na wasanii wengine anajiandaa kukipika upya kibao cha mwanamuziki Elton John cha ‘Tiny Dancer’ alichokitoa mwaka 1972 ambacho huenda Ijumaa kikatoka.

The post Britney Spears ateswa na maisha ya anasa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/24/britney-spears-ateswa-na-maisha-ya-anasa/feed/ 0
Amber Rose: Niliiona talaka kwa Kim, Kanye https://www.greensports.co.tz/2022/07/21/amber-rose-niliiona-talaka-kwa-kim-kanye/ https://www.greensports.co.tz/2022/07/21/amber-rose-niliiona-talaka-kwa-kim-kanye/#respond Thu, 21 Jul 2022 19:36:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=1785 New York, MarekaniMwanamitindo Amber Rose amesema kwamba alijua kuna talaka ilikuwa mbioni kati ya rapa, Kanye West na staa wa vipindi vya televisheni Kim Kardashian na ndio maana jambo hilo halikumshangaza hata kidogo.Rose ambaye aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Kanye kati ya mwaka 2008 hadi 2010. mahusiano ambayo yalikua maarufu lakini alisema kwamba […]

The post Amber Rose: Niliiona talaka kwa Kim, Kanye first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Mwanamitindo Amber Rose amesema kwamba alijua kuna talaka ilikuwa mbioni kati ya rapa, Kanye West na staa wa vipindi vya televisheni Kim Kardashian na ndio maana jambo hilo halikumshangaza hata kidogo.
Rose ambaye aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Kanye kati ya mwaka 2008 hadi 2010. mahusiano ambayo yalikua maarufu lakini alisema kwamba hakuwahi hata mara moja kuwaombea dua mbaya Kim na Kanye.
“Wakati wote nilikuwa nawatakia yaliyo mema, sikuwa na kinyongo chochote sikuwa kama vile nilikuwa na matumaini ya wao kuachana au wangefikia mwisho, mimi nilikuwa mwenye furaha wakati nikiwa kwenye ndoa yangu na Wiz (Khalifa),” alisema Rose.
Alipoulizwa kuhusu ukaribu wa yeye na Kim kwa sababu ya kuwa na tarehe moja ya kuzaliwa yaani Oktoba 21, Rose alisema, “Nafikiri siku yenu ya kuzaliwa inaweza kufanana lakini tumekuwa katika makuzi tofauti mimi nimekuwa katika umasikini, nililazimika kuhangaika na kupambana na yeye maisha yake yalikuwa vizuri, yenye pesa, kitu ambacho ni poa,” alisema Rose.
Kim na Kanye waliingia katika bifu baada ya kuachana ambapo, mwaka 2015, Kanye anakumbukwa kusema kwamba baada ya kuwa na Rose alilazimika kuoga mara 30 kabla ya kuanza mahusiano na Kim ambapo Rose alimjibu kwamba hakuwahi kumlaghai ila anawaachia kina Kardashian wamdhalilishe hadi watakapomaliza.

The post Amber Rose: Niliiona talaka kwa Kim, Kanye first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/07/21/amber-rose-niliiona-talaka-kwa-kim-kanye/feed/ 0